Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110148 articles
Browse latest View live

DALADALA ZA KIMARA MATOSA ZATISHIA KUGOMA SIKU YA JUMATANO WIKI HII


MAGAZETI YA JUMANNE LEO JANUARY 30,2018

WAZIRI MKUU NA MATUKIO KATIKA PICHA ETHIOPIA ADIS ABABA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe Naimi Aziz, nje ya ukumbi wa Nelson Mandela mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, wakati alipo mtembelea kwenye Hoteli ya Radisson Blue, mjini Addis Ababa Ethiopia. Januari 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

GLOBAL FUND YAIPA SERIKALI TRILIONI 1.155/- KUPAMBANA NA UKIMWI, TB, MALARIA

$
0
0

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 

SERIKALI ya Tanzania na Global Fund wamewekeana saini mkataba wa Dola za Marekani milioni 525 sawa na Sh.Trilioni 1.155 kwa lengo la kufadhili shughuli za kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu,Maralia na uimarishaji wa mifumo ya afya nchini. 

Imeelezwa ushirikiano huo wa Global Fund ambao ndio waliotoa fedha hizo kwa Serikali ya Tanzania unategemewa kuongeza kuongeza idadi ya Watanzania wanaonufaika na huduma za afya Katina magonjwa hayo. 

Wakati wa utiwaji saini wa mikataba ya fedha hizo, wadau mbalimbali walihudhuria ambao ni viongozi wa Serikali, mabalozi, asasi za kiraia za ndani na za kimataifa.Pia wajumbe wa bodi ya uratibu ya Global Fund nchini pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo ndiyo iliyoandaa shughuli hiyo. 

Akizungumza mapema jana jijini Dar es Salaam baada ya utiwaji saini wa mikataba ya fedha hizo, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Global Fund wamekuwa wachingiaji muhimu katika sekta ya afya.

Amefafanua wamekuwa wachangiaji wakubwa katika kuzuia na kupambana na magonjwa hayo matatu tangu kuanzishwa kwa mfuko huo mwaka 2001."Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania napenda kutoa shukrani za dhati kwa Global Fund kwa ushirikiano wao ambao umewezesha nchi kuboresha afya za wananchi wetu pamoja na kuboresha mifumo ya afya, "amesema Mwalim. 

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora (kulia), na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban, wakisaini hati za makabidhiano ya sh.  trioni moja zilizotolewa na Shirika la Global Fund kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia mapambano ya Ukimwi, TB na Malaria katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo. Wengine waliosimama katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na viongozi wengine kutoka Global Fund.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Mpoki Ulisubisya, akizungumza katika hafla hiyo.
Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania, Frederic Clavier, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban (kulia), akimkabidhi hati ya makabidhiano Mwakilishi wa Global Fund Tanzania, Linden Morrison.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora, akizungumza.
Taswira ya ukumbi wa mkutano katika uzinduzi huo.



MAWAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO WA TANZANIA NA RWANDA WAKUTANA KUJADILI MRADI WA UJENZI WA RELI YA ISAKA- KIGALI

$
0
0

Benny Mwaipaja, WFM

Mawaziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania na Rwanda wamekutana Jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kupata fedha za Ujenzi wa Reli yenye Kiwango cha Kimataifa (SGR) kutoka Isaka Shinyanga hadi Kigali Rwanda ikiwa ni mwendelezo wa mikutano kuhusu suala hilo iliyoanza kuanzia Januari 20, 2018.

Katika Mkutano huo wamejadili kuhusu njia ambayo inaweza kuwa rahisi kupata fedha ikiwemo ya kutumia Sekta binafsi, Serikali kukopa au kumweka mwekezaji ambapo wamekubaliana kupitia upya taarifa zilizo wasilishwa mezani za pande hizo mbili na kufanya maboresho na pia kuzungumza na Benki ya Dunia (WB), Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa pamoja ili wakati wa kikao kijacho waweze kujadili suala hilo kwa kuangalia vigezo na masharti ya kupata fedha.

Kikao hicho ambacho ni cha watalamu kimewakutanisha Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri kutoka Rwanda Mhe. Gatete Claver pamoja na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura na Makatibu wakuu wa wizara hizo na wajumbe wengine.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James na mwenzake wa Rwanda Bw. Caleb Rwaungaza, wamesaini maagizo hayo ya Mawaziri kwa ajili ya utekelezaji. Ikumbukwe kuwa mapema mwezi huu Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Rwanda Paul Kagame walikubaliana kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa Reli kutoka Isaka Shinyanga hadi Kigali Rwanda na wakatoa maagizo ya kuanza utekelezaji kwa kuangalia namna ya kupata fedha za mradi huo.

Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (wa pili kushoto) na Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (wa pili kulia) ukiendelea kuhusu upatikanaji  wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (kushoto) na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (kulia) wakiondoka baada ya kumalizika kwa mkutano kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda Jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James (kulia) na mwenzake wa Rwanda Bw. Caleb Rwaunganza wakisaini maagizo kutoka kwa Mawaziri wa Wizara hizo mbili kuhusu hatua za upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda Jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James (kulia) na mwenzake wa Rwanda Bw. Caleb Rwaunganza wakibadilishana taarifa walizosaini za maagizo kutoka kwa Mawaziri wa Wizara hizo mbili kuhusu hatua za upatikanaji wa Fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Zawadi kem kem promosheni ya Jero Yako ya Zantel.

$
0
0
 Meneja Masojo wa Zantel, Bi.  Rukia Mtingwa (kulia) akikabidhi zawadi ya simu ya kisasa aina ya Moto C 4G toka Zantel kwa Bwana Moiz Johar Hussein Hassanali  mmoja wa washindi wa wiki wa promosheni ya ‘Jero yako tu’ ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam ambayo mteja wa Zantel  akiongeza muda wa maongezi kuanzia shs mia tano hujipatia nafasi kushiriki. Zawadi za pikipiki, baiskeli, simu na pesa taslimu hutolewa kila wiki.
 Meneja Masoko wa Zantel, Bi. Rukia Mtingwa akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mshindi huyo Bwana Moiz Johar Hussein Hassanali .
 Meneja Masoko wa Zantel, Bi. Rukia Mtingwa (kulia) akipiga simu kwa  kwa simu na mmoja wa washindi wa promosheni ya Jero yako ya Zantel huku mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kuabahatisha Jehud Ngolo (kushoto) akisikiliza pamoja na mfanyakazi mwingine wa Zantel katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Zantel mjini Zanzibar, Mohammed Mussa Baucha (kulia), akikabidhi zawadi ya simu kwa Taimur Mohamed Hussein  mmoja wa washindi wa promosheni ya Jero yako, kisiwani humo juzi. 

AFRIKA YAAZIMIA KUZALISHA UMEME WA KUTOSHA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassima Majaliwa amesema nchi za Bara la Afrika zimeazimia kujiimarisha katika uzalishaji wa umeme hadi vijijini ili uweze kuleta maendeleo.

Aliyasema hayo jana (Jumatatu Januari 29, 2018) alipozungumza baada ya mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.Katika Mkutano huo ambao Waziri Mkuu alimuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, alisema nchi za Afrika zimejipanga kuzalisha umeme wa kutosha mijini na vijijini.

Waziri Mkuu alisema nchi hizo zimeazimia kuzalisha umeme mwingi kwa lengo la kuinua kiwango cha maisha ya wananchi wake na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.

Alisema nchi za Afrika zinatakiwa zijitegemee kiuchumi, ambapo nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya nyingine za Afrika zimefikia amapendekezo ya kuimarisha uzalishaji wa umeme. “Tanzania iko vizuri kwa sababu ina vyanzo vingi vya kuzalisha umene na sasa inamikakati ya kuzalisha umeme wa kutosha kuendesha viwanda vikubwa na kukaribisha wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema maelengo ya mkutamo huo yalikuwa ni kupokea taarifa za tume mbalimbali zilizoundwa katika kikao kilichopita.Alisema miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na ya tume iliyokuwa inashughulikia masuala ya usalama na amani katika Bara la Afrika.

“Tume nyingine ilihusika na mapitio ya namna kuhamasisha nchi za Afrika kufikia kwenye maendeleo na nyingine ilikuwa inahamasisha mahusiano ya nchi kupitia kwenye Jumuia zilizopo ndani ya Bara la Afrika kama SADC.”

Pia Waziri Mkuu alisema mkutano huo ulifanya mapitio ya mapendekezo ya namna nchi za Afrika zinavyoweza kupata mitaji kupitia michango ya nchi mbalimbali, ambapo kanuni ziliandaliwa ili kuwezesha kila nchi kuchangia katika mfuko mkuu wa Umoja wa Afrika.

Alisema Tanzania ilihusika kutoa mchango juu suala la amani na usalama katika nchi za Afrika. ambapo kila nchi inawajibika kujilinda yenyewe na kulinda nchi jirani pamoja na Jumuia zake.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMANNE, JANUARI 30, 2018.

Wajasiliamaji watakiwa kuendelea kutengeneza bidhaa bora kujenga uchumi wa Tanzania

$
0
0
. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji NSSF, Bathow Mmuni wakati akifunga mfunzo ya Sido yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam ambapo aliwataka wajasiliamali kuendelea kuwa wabunifu kwa kutenegeza bidhaa zenye ubora.

 "Nawaomba wajasiliamali mtengeneze bidhaa zenye ubora na nzuri zitakazowavutia wateja ili mtakapoziuza zitachangia pato la taifa kukua zaidi," alisema Mmuni. Aliongeza kuwa kwa sasa NSSF wamejipanga kurudi kuanza kuwasaidia wajasiliamali ili kukuza kipato chao ili waweze kuendeleza uchumi wa viwanda. Kwa upande wa Mkurugenzi wa Sido- Dar es Salaam, MacDonald Maganga aliwaomba wajasiliamali wote walipo mtaani kuchangamkia mafunzo ya Sido ili yaweze kuwaongezea ujuzi na kuzifanya bidhaa zao zikawa na thamani zaidi.

"Wajasiliamali jitokezeni kokote pale mlipo mchangamkie mafunzo tunayoyatoa maana yamekuwa yakiwajenga zaidi kwa kuongeza ubora wa bidhaa mnazozitengeneza, ukiangalia katika kundi lenu hili kuwa watu wameshaanza kutengeneza bidhaa ila wamekuja kujiongezea ujuzi zaidi jambo ambao ni jema zaidi maana unapopata cheti cha Sido kitakusaidia kuweza kupenya katika soko," alisema Maganga.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni ambaye alikuwa mgeni rasmi akifunga mfunzo ya wajasiliamali yaliyoendeshwa na Sido mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi wa Sido Dar es Salaam, MacDonald Maganga. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akionyeshwa nguo ya batiki iliyotengenezwa na wajasiliamali waliokuwa waliopata mafunzo ya Sido-Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akionyeswa mafuta na sabuni walizotengeneza wajasiliamali waliopata mafunzo ya Sido-Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi wa Sido Dar es Salaam, MacDonald Maganga.  
Wajasiliamali wakiwa katika picha ya pamoja.


SEHEMU YA BAADHI MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017/2018

SERIKALI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WA AFYA NCHINI

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeahidi kuendelea kutatua changamoto za zinazowakabili watumishi wa Kada ya Afya nchini ikiwemo kuboresha miundombinu inayowazunguka.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) mapema leo wakati akizindua Baraza la Wauguzi na Wakunga katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.

“Asilimia 80% ya Kazi zote za kutoa huduma za Afya, zinafanywa na Wauguzi na Wakunga, kwaiyo wakati tunazungumzia kuboresha huduma za, Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuzifanyika kazi changamoto hizo ikiwemo suala la watumishi” alisema Mh. Ummy Mwalimu.

Mh. Ummy aliendelea kusema kwamba, sambamba na changamoto Wauguzi na Wakunga wanazoendelea kukumbana nazo Serikali itaendelea kutimiza wajibu wake wa kutatua changamoto hizo katika kuboresha Huduma za Afya.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.
Watumishi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga pamoja na Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (Hayupo kwenye Picha) wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga.
Afisa Uuguzi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Jane Mazigo akitoa maelezo mbele ya Mgeni rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga.
Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga aliyemaliza muda wake Stuart Mbelwa akipokea Cheti kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa Baraza la Uuguzi na Wakunga, Kulia ni Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Lena Mfalila
Mwenyekiti aliyeingia kuliongoza Baraza la Uuguzi na Ukunga Abner Mathube akiahidi kuchapa kazi mbele ya mgeni rasmi ambae ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga.
Picha ya Pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati akizindua Baraza la Uuguzi na Ukunga katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.


NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017/18, ST. FRANCIS YASHIKA NAFASI YA KWANZA

$
0
0
*Philison Mdee aongoza kwa wavulana,  Ellizabeth  Mangu aongoza wasichana

*Wengine 265 matokeo yafutwa, yumo aliyeandika matusi kwenye majibu


 Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SHULE ya Sekondari ya St.Francis Girls imeongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2017.

Akitangaza  sekondari ambazo zimeshika nafasi za juu kwenye matokeo hayo, leo jijijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk.Charles Msonde amesema nafasi ya pili imechukuliwa na sekondari ya Feza Boys na nafasi ya tatu sekondari ya Kemebos.

Wakati nafasi ya nne imeshikiliwa na sekondari ya  Bethel Saabs Girls, nafasi ya tano sekondari ya Anuarite, nafasi ya sita sekondari ya  Marian Gilrs huku nafasi ya saba ikishikiliwa na sekondari ya Canossa, wakati nafasi ya nane imechukuliwa na sekondari ya Feza Girls, nafasi ya tisa sekondari ya Marian Boys na nafasi ya 10 sekondari ya Shamsiye Boys

WALIOONGOZA 10 BORA KITAIFA
Kwa upande wa wanafunzi ambao wameshika nafasi ya kwanza hadi ya kumi kitaifa kwenye matokeo hayo, Dk.Msonde alisema nafasi ya  kwanza imeshikwa na mwanafunzi Philison Mdee(Marian Boys), wakati nafasi ya pili imeshikwa na Eliza Mangu(Marian Girls), nafasi ya tatu
Ana Mshana(Marian Girls)

Ametaja nafasi ya nne imeshikwa na Emanuel Makoye(Ilboru), nafasi ya tano Lukelo Luoga(Ilboru), nafasi ya sita Fuad Thabit(Feza Boys), nafasi ya saba Godfrey Mwakatage(Uwata), nafasi ya nane Baraka Mohamed(Angeles), nafasi ya tisa Lilian Moses(Marian Girls) na nafasi ya kumi kitaifa imechukuliwa na Everine Mlowe(St. Francis Gr)

WAVULANA 10 BORA KITAIFA 
Akitangaza walioshika nafasi ya kwanza hadi ya 10 kitaifa kwa mujibu wa Dk.Msonde ni Philison Mdee(Marian Boys), nafasi ya pili Lameck Makoye(Ilboru), nafasi ya tatu Tadei Luoga(Ilboru), nafasi ya nne Fuad Thabit (Feza Boys).

Wakati nafasi ya tano ni  Godfrey Mwakatage(Uwata),nafasi ya sita  Baraka Mohamed(Angeles),nafasi ya saba  Noel Shimba(Marian Boys), nafasi ya nane ni Patrick Robert(Mzumbe), nafasi ya tisa Robison Eliona(ILboru) na nafasi ya 10 bora kitaifa imechukuliwa na mwanafunzi Harrison Simkoko (Mzumbe)


KUPASUKA KWA BOMBA LA MAJI LAZUA TAHARUKI KWA WAKAZI WA TABATA

$
0
0
 Wakazi wa Tabata Chang'ombe wakiwa wanashangaa bomba la maji lililopasuka kutokana na ukarabati unaoendelea katika barabara hizo ambazo zinajengwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini(Tarura), ukarabati wa barabara hizo utasaidi kuwaunganisha wakazi wa Tabata Chang'ombe na Kisukulu bila kuzunguka njia ya Bima.
 Sehemu ya Barabara ya inayokarabatiwa na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini(Tarura) eneo la Tabatra Chang'ombe .

YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Ackson akisoma dua ya kuliombea Bunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.
 Mbunge wa Namtumbo, Eng.Edwin Ngonyani akiuliza swali wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,  Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt.Suzan  Kolimba na Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula  wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma. Picha na Daudi Manongi,MAELEZO.

WAZIRI MKUU AREJEA NCHINI AKITOKEA ETHIOPIA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, kwenye Hoteli ya Radisson Blue, mjini Addis Ababa, wakati akiondoka kurejea Dar es salaam, kushoto ni Mke wa Salim Ahmed salim, Amne Salim.Waziri Mkuu alikua Ethiopia kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiagana na Rais wa Comoros, Azali Assoumani, ndani ya ndege ya shirika la Ethiopian Airline, wakiwa wanarejea kutoka kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja AU, Januari 30, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, nje ya ndege ya shirika la Ethiopian Airline, wakati akiwasili kutoka kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja AU, Januari 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JPM Kuzindua Pasipoti ya Kielektroniki

$
0
0
Jonas Kamaleki- MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli kesho atazindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo utafanyika Jumatano, Januari 31, 2018 kuanzia saa moja na nusu asubuhi, Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na Mrakibu wa Uhamiaji ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ali Mtanda katika mahojiano maalum na Idara ya Habari (MAELEZO).Mtanda amesema kuwa Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki ni sehemu ya Mfumo wa Uhamiaji Mtandao ambao utakuwa na visa, vibali mbali mbali na manejimenti mipakani.

Kwa kuwa teknolojia inazidi kukua, Tanzania haiwezi kubaki nyuma ndiyo maana imeamua kuingia katika masuala ya digiti. Uzinduzi huu utahudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein.Marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, waheshimiwa, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wa Serikali wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo kwa mujibu wa Mtanda.

Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika kutoa huduma zake kwa wananchi kwa njia ya mtandao. Ikumbukwe kuwa usajili wa makampuni chini ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wamezindua usajili wa makampuni kwa njia ya mtandao, miamala ya pesa inafanyika kwa kiwango kikubwa kwa njia ya mtandao na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi ikiwepo kulipa kodi mbali mbali.

WABUNGE WATEULE WALA VIAPO BUNGENI LEO

$
0
0
  Mbunge wa Songea Mjini (CCM) Mhe.Dkt.Damas Daniel Ndumbaro akila kiapo cha uaminifu mbele ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Ackson (hayupo pichani)  wakati wa kikao cha kwanza cha mkutano wa kumi ulionza leo Mkoani Dodoma. 
 Mbunge wa  Singida  Kaskazini Mhe.Monko Justine Joseph  akila kiapo cha uaminifu mbele ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe.Dkt.Tulia Ackson wakati wa kikao cha kwanza cha mkutano wa kumi ulionza leo Mkoani Dodoma. 
Mbunge wa Longido Mhe.Dkt.Stephano Lemomo Kiruswa akila kiapo cha uaminifu mbele ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Ackson wakati wa kikao cha kwanza cha mkutano wa kumi ulioanza leo Mkoani Dodoma.

Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO

St Anne Maria yazawadia walioipaisha kitaifa

$
0
0
SHULE ya St Anne Maria ya Mbezi jijini Dar es Salaam imewazawadia wanafunzi wake waliofanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la nne na kidato cha pili yaliyotangazwa hivi karibuni na kuipaisha kitaifa.

Akizungumza na wakati wa hafla hiyo shuleni hapo, Mkuu wa Shule hiyo, Gladius Ndyetabura, alisema shule yake imeweka utaratibu wa kuwazawadia wanafunzi hao vitu mbalimbali kama vitabu na madaftari kama motisha wa kuendelea kufanya vizuri kwenye masomo.

Alisema wanafunzi wa darasa la nne wamefanikiwa kuitoa kimasomaso shule hiyo kwa kuiwezesha kuwa ya pili kiwilaya kati ya shule 90 na ya pili Mkoa wa Dar es Salaam kati ya shule 497.Alisema mbali na kuiwezesha shule hiyo kupata mafanikio hayo kiwilaya na kimkoa pia wanafunzi wote wa darasa la nne wamefanikiwa kupata wastani wa wa ufaulu wa alama A mtihani wa kitaifa.

“Mafanikio yameanzia msingi hadi sekondari maana kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka 2017 shule ilikuwa ya kwanza kwa Wilaya ya Ubungo na ya  tano Mkoa wa Dar es Salaam tulitoa daraja la kwanza wanafunzi 15, daraja la pili 48, daraja la tatu 23 na daraja la nne mmoja tu na hatuna aliyepata 0,” alisema

Alisema hivi karibuni Mkoa wa Dar es Salaam uliipatia Ngao Maalum shule hiyo kama sehemu ya kutambua mchango wake katika kuinua elimu hapa nchini na kuwa miongoni mwa shule zinazofanya vizuri kitaaluma.

Alisema shule yake ilipewa ngao inayoonyesha kuwa ni miongoni mwa shule zilizofanya vizuri zaidi kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka 2016, Best Performing Primary School in Tanzania.Alisema ngao hiyo imewapa changamoto ya kuendelea kufundisha kwa bidii ili hatimaye wapate matokeo mazuri zaidi ya mwaka huu.

Alisema ingawa shule yake imefanikiwa kuingia kumi bora kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu, lakini hawajabweteka na badala yake wanafanya jitihada za kuwa namba moja.“Kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu tumefanikiwa kuwa wa kwanza Wilaya ya Ubungo, tumekuwa wa pili Mkoa wa Dar es Salaam na tumekuwa wanane kitaifa sasa hii haitufanyi tubweteke tutapambana kupata nafasi za juu zaidi,” alisema 
 Mwalimu Mkuu wa shule ya St Anne Maria Academy ya Mbezi, Gladius Ndyetabura, akimkabidhi zawadi mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi kwenye mtihani wa darasa la nne mwaka 2017 Charles Lusato, ambaye alipata alama A kwenye masomo yote na kuwezesha shule hiyo kuwa ya pili Wilaya ya Ubungo kati ya shule 90 na ya pili pia kwa Mkoa wa Dar es Salaam kati ya shule 497.
Mwalimu Mkuu wa shule ya St Anne Maria ya Mbezi, Gladius Ndyetabura akiwasomea matokeo ya kidato cha pili wanafunzi wa shule hiyo ambayo yanaonyesha wanafunzi 48 kupata daraja la kwanza, 31 daraja la pili, 27 daraja la tatu na 13 daraja la nne na hakuna aliyepata 0.

SERIKALI YASISITIZA UWAZI SHUGHULI ZA MADINI

$
0
0
Kampuni za Madini nchini zimetakiwa kufanya shughuli zake kwa uwazi sambamba na kufuata Sheria za nchi ili kuepuka migongano.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam Januari 29, 2018 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila kwenye mkutano na Balozi wa Canada nchini, Ian Myles aliyeambatana na Mshauri masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey Davidson.

Ujumbe huo ulimtembelea Katibu Mkuu Msanjila kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali kwenye Sekta ya Madini ikiwemo suala la Sheria ya Madini, masuala ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) yanayofanywa na kampuni mbalimbali zikiwemo za kutoka nchini Canada na matarajio ya Serikali kwa kampuni (wawekezaji).

Profesa Msanjila alisisitiza kuwa kampuni zinazofanya shughuli zake nchini zinalazimika kufuata taratibu na sheria za nchi ili kujijengea mazingira rafiki ya utekelezaji wa shughuli husika.Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha Sekta ya Madini inanufaisha Taifa kwa ujumla sambamba na wawekezaji na alibainisha kwamba lengo hilo litafikiwa ikiwa kampuni husika zitatekeleza wajibu wake kwa uwazi kulingana na matakwa ya sheria.

“Kampuni zinazojihusisha na shuguli za madini zinapaswa kufanya shughuli zake kwa usahihi na uwazi,” alisisitiza Profesa Msanjila.Aidha, Profesa Msanjila alisisitiza kuwa kampuni zinazojihusisha na shughuli za madini nchini, zinapaswa kupata taarifa sahihi kutoka kwa Wataalam waliopo Serikalini ili kupata mwelekeo sahihi wa dhamira ya Serikali.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (katikati) akizungumza jambo wakati wa mkutano na Balozi wa Canada nchini, Ian Myles (kulia) na Mshauri masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey Davidson (kushoto).
 Watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Madini na Ubalozi wa Canada nchini Tanzania wakifuatilia majadiliano kwenye mkutano wa Katibu Mkuu Madini na Balozi wa Canada (hawapo pichani). Kushoto ni Kamishna wa Madini ambaye pia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Madini, Profesa Shukrani Manya na kulia ni Kamishna wa Biashara Ubalozi wa Canada nchini, Anita Kundy. Wengine ni Maafisa kutoa Wizara ya Madini.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (kulia) akimsikiliza Mshauri masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey Davidson (katikati). Kushoto ni Balozi wa Canada nchini, Ian Myles (kulia). 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (wa pili kulia) mara baada ya kumalizika kwa mkutano na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Ian Myles (katikati). Kulia ni Kamishna wa Madini ambaye pia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Madini, Profesa Shukrani Manya. Kutoka kushoto ni Mshauri masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey Davidson na Kamishna wa Biashara Ubalozi wa Canada nchini, Anita Kundy.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

BEI ZA MATUNDA SOKO LA MABIBO KWA SIKU YA LEO

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii

WAFANYABIASHARA wa matunda Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam wameeleza kuwa kwa sasa matunda yameongezeka, huku wakibainisha wazi bei ambazo wanauza kwa wateja wao. 

Wakizungumza leo na Michuzi Blog jijini Dar es Salaam wafanyabiashara  hao kuhusu bei ya matunda sokoni hapo. Bei hizo ni kama ilivyo hapo chini.
Bei ya tikitiki maji ni kati ya Sh.1000 hadi Sh. 3500.
Bei ya Parachichi ni kati ya Sh.500 hadi Sh.1000.
 Bei ya Ndizi Mbivu inauzwa kati ya Sh. 100 hadi Sh. 160.
 Bei ya Embe sokoni hapo ni kati ya Sh.400 hadi Sh.700.Bei hiyo hiyo kwa wanaonunua kwa rejareja.
Bei ya Tango  katika Soko la Mabibo yanauzwa kwa fungu moja lenye matango matano kwash.1000.
Bei ya Ndizi inauzwa katika sokoni hapo inauzwa kati ya Sh.20000 hadi Sh.30000 kwa mkungu mmoja.
Bei ya viazi vitamu Sh.1000 kwa fungu katika soko la Mabibo jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wanunuzi na wauzaji katika soko hilo wakiwa katika pilikapilika.

REPOA YAONGOZA MKUTANO WA WHY THINKS MATTER NCHINI

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Tasisi ya Utafiti nchini Repoa leo imeongoza watafiti mbalimbali nchini katika Mkutano wa Watafiti Duniani ujulikanao kama "WHY THINKS MATTER"  Ambao umefanywa na watafiti wote Duniani kuanzia Saa tatu mpaka Saa tano.

Dr Mmari amesema kuwa Mkutano huo unafanyika na nchi 170 Duniani amabpo mwaka huu wanazungumzia Umuhimu wa Tasisi za Utafiti wa Duniani ambapo  kwa sasa kumekuwa na Changamoto ya ukuwaji wa teknolojia na watu kupotosha tafiti kutoka na hali ya kisiasa.

"siku hizi kuna changamoto ya mitandao ya kijamii taharifa zinasambaa haraka  na taharifa zingine azina ukweli wowote na kusababisha viongozi wakaziamini na kuzitumia katika utungaji wa sera na kuendesha shughuli mbalimbali za Serikali , hivyo ikaonekana kuwa ni muhimu mwaka huu wakazungumzia tafiti ambazo zimefanyiwa kazi kisayansi" Amesema Dr Mmari.

amesema umuhimu wa Watafiti umeweza kusaidia katika kufanya Maendeleo ya kweli hivyo nashawishi Watanzania waweze kuendelea kufanya tafiti ambazo zinaweza zitatumika kwa ajili ya mipango ya Maendeleo ya Serikali na Wadau Mbalimbali.

Amemaliza kwa kusema kuwa si vyema watafaiti wakafanya tafiti ambazo zinawekwa  tu kwenye makabati pasipo kuwa na Matokeo yoyote kwa Taifa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Utafiti Nchini,REPOA, Dr Donald Mmari  akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Tafiti Duniani ambao kwa Tanzania ulifanyika katika Ofisi za Repoa na kuitwa jina la Umuhimu wa Tafiti Duniani
 Balozi wa Swideni Nchini, Katarina Rangnitt akizungumza wakati wa Mkutano wa Watafiti Duniani(WHY THINK TANKS MATTER) uliofanyika katika Taasisi ya utafiti ya Repoa kwa hapa nchini.
 Mtafiti Kutoka Tasisi ya Utafiti ya Repoa,  Dr Blandina Kilama akizungumza wakati wa mkutano huo wa watafiti Duniani.
 Baadhi ya Maprofesa walioshiriki Mkutano huo wakiongozwa na Profesa Mwesigwa Baregu wa kwanza kulia Pichani.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano huo wakisikiliza Mada Mbalimbali kutoka kwa watafiti  na Wadau mbalimbali.
Viewing all 110148 articles
Browse latest View live




Latest Images