Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

DC MLOZI AHIMIZA WATENDAJI,MADIWANI WA MANISPAA YA TABORA KUZINGATIA MUDA

$
0
0
Na Tiganya Vincent

MKUU wa Wilaya ya Tabora Queen Mlozi amewataka Madiwani na Watumishi wa Manispaa ya Tabora kuzingatia muda wanapokuwa katika shughuli mbalimbali kama wanataka kupata maendeleo ya haraka.

Queen alitoa hiyo jana mjini hapa baada ya kukwera baadhi ya watumishi na Madiwani wa Manispaa ya Tabora kuchelewa kuingia katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza Maalumu la Madiwani lilikuwa likipitia rasmu ya mpango wa bajeti ya mwaka ujao.

Alisema kuwa hatua hiyo baadhi ya watumishi na madiwani kuchelewa kulisababisha Kikao hicho kichelewe kuanza na hivyo kukwamisha shughuli nyingine za maendeleo kwa ajili ya wananchi.Queen alisema kuwa wakiendelea na mwendeo huo watasababisha Manispaa hiyo kupitia na Halmashauri nyingine kimaendeleo na hawataweza kwenda na kasi ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Naomba nieleze kusikitishwa kwangu kwa ucheleweji huo wa kuanza vikao…nimefika hapa saa 3.00 asubuhi nikitarajia ndio muda wa kikao kuanza lakini hadi hivi sasa saa 5.00 asubuhi ndio tunaanza kikao…kwa kasi hiyo hatuwezi kuendelea ni lazima tubadilike” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.Mkuu huyo wa Wilaya alielezea masikitiko yake kwa kitendo cha madiwani na watumishi wengine kuendelea kuchelewa licha ya kufanya ziara ya mafunzo na kujionea Halmashauri nyingine zilivyopiga hatua kwa sababu ya kuzingatia muda.

Alisema kuwa ni vema Madiwani na Watumishi watambue kuwa muda ni uchumi na pia ni vema na watambue kuwa kila dakika wanayopoteza wajiletea hasara.Naye Diwani wa Kata ya Ng’ambo George Mpepo aliwaomba Madiwani wenzake kuufanyia kazi ushauri wa Mkuu huyo wa Wilaya kwa sababu utawasaidia kuongeza makusanyo na kuwa na fedha kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wakazi wa Manisapaa ya Tabora.

Kamishna Nsekela: Zingatieni mgongano wa Maslahi mnapojadili rasimu ya kanuni

$
0
0
Kamishna wa Maadili Jaji (Mst) Harold Nsekela amewataka wadau wa maadili kuzingatia suala la mgongano wa maslahi wanapojadili rasimu ya kanuni za maadili ili kupata kanuni sahihi zitakazosaidia kutekeleza Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na 13 ya mwaka 1995.

Kamishna Nsekela alisema hayo mwishoni mwa wiki mjini Dodoma wakati akifungua warsha ya wadau kujadili kanuni za Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.“Ndugu washiriki wa warsha hii tuweke msisitizo katika sualal la mgongano wa maslahi na kutoa mapendekezo kwani suala lhili ni gumu sio tu kwa Tanzania bali pia nchi nyingine zinazoendelea,” alisema.

Kamishna Nsekela aliwataka washiriki hao kujadili kanuni kwa kujenga msingi thabiti utakaosaidia kuongeza uadilifu miongozi mwa viongozi wa umma ili kuepuka udanganyifu hasa katika kutoa Tamko la Rasilimali na Madeni.

“Tunapojadili kanuni hizi, naomba tujadili kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya nchi na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995 ili kupata kanuni sahihi za utekelezaji wa Sheria,” aliongeza.Mjadala wa kujadili rasimu ya kanuni za maadili unatokana na ukosefu wa kanuni zilizopitishwa kutafsiri Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma tangu ilipotungwa mwaka 1995.

Uwepo wa kanuni za maadili utatoa fursa kwa wananchi kupata ufafanuzi juu ya tabia, mienendo ya viongozi na matumizi mabaya ya madaraka katika utendaji wao wa kazi.Baadhi ya wadau walioudhuria warsha hiyo iliyofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ni viongozi wa dini, vyama vya siasa, wawakilishi kutoka asasi za kiraia na wabunge.

SERIKALI YAUZA MENO YA VIBOKO KWA SH.30,900,000/= KATIKA MNADA WA HADHARA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imefanya mnada wa hadhara wa kuuza meno ya viboko vipande 12,467 yenye uzito wa kilo 3,580.29 katika ofisi zake ndogo katika Jengo la Mpingo, jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya makampuni 19 yenye leseni daraja la kwanza yameshiriki katika mnada huo.

Mnada huo umefanyika chini ya usimamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango ambapo kampuni ya On Tours Tanzania Limited imeibuka mshindi kwa kwa kununua meno hayo kwa jumla ya shilingi 30,900,000/= 

Awali akizungumza katika mnada huo, Mwenyekiti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Karerema Kwaleh aliwataka wafanyabiashara kuzingatia masharti mnada huo.

Ambapo Karerema alimtaka mfanyabiashara yeyote atakeibuka mshindi kulipia asilimia ishirini na tano (25%) ya bei papo hapo na asilimia sabini na tano (75%) italipwa yote katika muda wa siku kumi na nne (14) baada ya mnada.

Kufuatia sharti hilo baada ya kutangazwa kwa mshindi, Mwakilishi kutoka Kampuni hiyo, Grey Kilas aliweza kulipia asilimia kiasi hicho cha asilimia ishirini na tano (25%) papo hapo na asilimia sabini na tano (75%) atailipia ifikapo Februari 11, 2018.


 Baadhi ya  meno ya viboko vipande  12,467 yenye uzito wa kilo 3,580.29 ambayo yameuzwa kwa njia ya mnada wa hadhara  leo   jijini Dar es Salaam kwa Kampuni ya On Tours Tanzania Limited kwa kiasi cha shilingi 30,900,000/= (Picha na Lusungu Helela-MNRT).

Rais Shein Afungua Warsha ya Uelewa Mamlaka ya Viwanda Vidog Vidogo Zanzibar.( SMID )

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia na kulifungua Kongamano la Warsha ya Uelewa Juu ya Mamlaka Itakayosimamia Viwanda Vidogo vidogona Vya Kati (SMIDA) hafla hiyo imewashirikisha Wajasiriamali mbalimbali wa Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la Wawakilishi kikwajuni Zanzibar.(Pcha na Ikulu)
KATIBU Mkuu Wizara ya Viwanda na Masoko Zanzibar Juma Ali Juma akizungumza kitaalamu juu ya Uelewa Juu ya Mamlaka ya Itakayosimamia Viwanda Vidogo vidogo Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza kikwajuni Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Tanzania Profesa Sylvester M Mpanduji, akitowa maelezo juu ya umuhimu wa uaznzishaji wa Viwanda Vidogo vidogo kwa wajasiriamali wakatikwa warsha hiyo ilioandaliwa na Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi Kikwajuni.
WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali, akitowa maelezo ya hafla hiyo kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kulifungua Kongamano hilo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid, Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, na kulia Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud wakiwa katika picha ya pamoja na Wajasiriamali.Picha na Ikulu).



BALOZI SIMBA AKUTANA NA UGENI KUTOKA NCHINI MAREKANI

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia) akimkaribisha katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, Afisa wa Masuala ya Siasa kutoka Ubalozi wa Marekani nchini, Daniel Daley, kabla ya kuanza mazungumzo kwa ajili ya ugeni kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo. Katikati ni Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Rendi Mccoy aliyetembelea Wizara hiyo kwa ajili ya kuona Serikali ya Tanzania inavyotekeleza vita dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu pamoja na kuangalia ni jinsi gani Marekani inaweza ikasaidia katika kukabiliana na vita hiyo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati) akiwafafanulia jambo, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Rendi Mccoy (wapili kushoto), na Afisa wa Masuala ya Siasa kutoka Ubalozi wa Marekani nchini, Daniel Daley (kushoto), wakati wa mazungumzo na maafisa hao yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Maafisa hao kutoka Marekani wamefika wizarani hapo kwa ajili ya kuona jinsi Serikali ya Tanzania inavyotekeleza vita dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu pamoja na kuangalia ni jinsi gani Marekani inaweza ikasaidia katika kukabiliana na vita hiyo. Kulia ni Selectine Makoba, Afisa kutoka Ofisi ya Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia) akimsikiliza Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Rendi Mccoy (katikati), wakati alipokua anafafanua jambo baada ya kupewa taarifa ya jinsi Serikali ya Tanzania inavyotekeleza vita dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu. Ugeni huo kutoka Marekani pia uliangalia jinsi gani nchi hiyo inaweza ikaisaidia Tanzania katika kukabiliana na vita hiyo. Kushoto ni Afisa wa Masuala ya Siasa kutoka Ubalozi wa Marekani nchini, Daniel Daley. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

YANGA KUKWEA PIPA ALFAJIRI KESHO KUWAHI MECHI SAA 10 JIONI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KIKOSI cha Yanga kesho kinatarajia kukwea pipa alfajiri na mapema ili kuwahi mechi yao  dhidi ya Ihefu ikiwa ni mchezo wa kombe la Azam Sports HD  utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine  Jijini Mbeya majira ya saa 10 jioni siku hiyo hiyo.

Timu ya Ihefu inayoshiriki ligi darala la pili ilifanikiwa kuwaondoa timu ya Mbeya City katika mchezo wao wa kwanza huku Yanga wakiwaondoka timu ya Reha na kufanikiwa kuingia hatua ya pili ya kombe la Shirikisho FA .

Yanga itakayoshuka dimbani kesho kuvaana na Ihefu, kikosi chao kinatarajiwab kuondoka alfajiri ya kesho ili kuwahi mchezo utakaochezwa majira ya saa 10 alasiri huku wakilalamikia ratiba kutokuwa rafiki kwa upande wao.

Akizungumza na Globu ya Jamii, Meneja wa timu ya Yanga amesema kuwa kikosi kitaondoka na wachezaji wao wote isipokuwa wale waliokuwa majeruhi ambapo bado hawajaungana na wenzao kikamilifu.

"wachezaji watakaokosekana katika mchezo wa kesho ni saba ambao bado hawajaanza kuungana na wenzao katika mazoezi ya jumla ila wachezaji wengine wote wako katika hali nzuri," amesema Hafidh.

BFB WAANDAA MASHINDANO YA KUJIMA NGUVU KUELEKEA JUMUIYA YA MADOLA

$
0
0
Na Agness Francis Globu ya Jamii. 

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Ngumi Tanzania(BFT) Makore Mashaga amesema katika kujiandaa na michuano kuelekea Jumuiya ya Madola watakwenda Mjini Dodoma kwa ajili ya kufanya mashindano yenye lengo la kupima uwezo wa mabondioa wao 13.

Mashanga amesema hayo leo akiwa Ofisini zao Temeke jijini Dar es Salaam na kufafanua licha ya kujianda vema katika michuano hiyo wameona ni vizuri kufanya shindano la kujipima nguvu ili kubaini viwango vya mabondioa wao na kutambua nini kifanyike katika kuwaimarisha zaidi.

"Nia yetu ni kuona viwango vya mabondia hao ili kujua wamefikia kiwango gani na makocha waweze kurekebisha makosa kabla ya kwenda kwenye michuano hiyo ya Jumuiya ya madola,"amesema. Amesema mazoezi yalianza Aprili mwaka 2017 wakiwa na mabondia 30 ikiwa mpaka sasa wamebaki 13 kutokana na mchujo mara baada ya kumaliza mazoezi. 

Ameongeza katika mashindano hayo wamealika wageni kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo mikoa yote nchini, Afrika Mashariki na nje ya Bara la Afrika.Mashindano hayo yatafanyika Februari 25 mpaka Machi 2 mwaka huu."Kati ya mabondia13 watachaguliwa 5 ikiwa mataifa mengine wanapeleka washiriki 10 ila tunaomba angalau tupeleke mabondia 8 na tunataka angalau kufikia uwiano wa nchi nyingine,"amesema Mashaga. 

Kwa upande wa Kocha wa BFT David Yombayomba amesema mandalizi ni mazuri wachezaji wote wamekamilika kila idara na wananguvu za kutosha na wanaamini watafanya vema katika mazoezi ya kuelekea michuano ya Jumuiya ya Madola.
Karibu Mkuu BFT Makore Mashaga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi yanayoendelea kuelekea Michuano ya Jumiya ya Madola leo katika ofisi zao Temeke Jijini Dar es salaam.
Kocha BFT Davidi YombaYomba akizungumza na waandishi wa habari huku akijiitapa kuwa vijana wake wapo vizuri kabisa tayari kwa mpambano leo katika ofisi zao Temeke Jijini Dar es Salaam

NAIBU SPIKA AONGOZA KIKAO KAMATI YA UONGOZI MJINI DODOMA.

$
0
0
 Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha kamati ya uongozi kilichokuwa kinalenga kupokea na kujadili Shughuli za Mkutano wa kumi wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano huo, kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
Mjumbe wa kamati ya uongozi, Mheshimiwa Mwanne Mchemba akizungumza wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichokuwa kinalenga kupokea na kujadili Shughuli za Mkutano wa kumi wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano huo. kulia ni Mjumbe Mheshimiwa Naghenjwa kaboyoka na kushoto ni Mjumbe pia Mheshimiwa Najma Giga, ​​katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
Wajumbe wa kamati ya uongozi wakimsikiliza Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson wakati wa kikao cha kamati ya uongozi kilichokuwa kinalenga kupokea na kujadili Shughuli za Mkutano wa kumi wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano huo, kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

BASI LA TAHMEED LATETEKEA KWA MOTO KABUKU WILAYANI HANDENI

$
0
0

Basi la kampuni ya Tahmeed lenye namba za usajili T483 BFL limeungua moto katika Kijiji cha Kabuku wilayani Handeni. 

Kwamujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, SACP Edward Bukombe alisema basi hilo ambalo lilikuwa na abiria 9 tu kutoka Dar es salam liliungua moto kutokana na hitilafu za umeme. 

Alisema Dereva wa bus hilo Bakari Said (34) alihisi halipo vizuri katika mfumo wa engine akasimamisha gari kisha kuwaomba abiria washuke.

Hata hivyo hakukuwa na mtu aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo. Hii ni mara ya pili kwa basi la kampuni hiyo kupata hitilafu Kwenye mfumo wa injini na kuungua moto.

ASKARI 16 WA JESHI LA POLISI WATUNUKIWA VYETI

$
0
0
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa RUVUMA Gemini mushi amewatunuku vyeti askari 16 kikosi cha usalama barabarani kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kipindi cha mwaka 2016 na 2017.

KIPINDI MAALUM CHA RAIS DKT. MAGUFULI KUKUTANA NA MAAFISA WA JWTZ WANAOTARAJIWA KUSTAAFU, KUKUTANA MA BALOZI MTEULE DKT. SLAA

SHERIA YA TAKWIMU MWAKA 2015 HAIJAZUIA TAFITI ELIMU YA JUU

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MKURUGENZI wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Albina Chuwa amesema sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, hazigusi tafiti zinazofanywa na Vyuo Vikuu nchini kutokana na taratibu wanazozifanya zinakidhi maadili ya kufanya tafiti hizo katika masomo mbalimbali ya wanafunzi wa elimu ya juu. 

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anafungua mkutano wa uelimishaji umma kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 na kueleza NBS haijazuia vyuo kufanya tafiti zake katika masomo.Dk.Chuwa ameongeza sheria hiyo imekuwa ikileta changamoto kwa baadhi ya taasisi vikiwemo vyuo vikuu katika uandaji wa tafiti za kimasomo kwa wanafunzi.

Dk.Chuwa amesema sheria ya takwimu ya mwaka 2015 haijazuia mtu au taasisi yoyote kutoa takwimu badala yake sheria hiyo imetoa wigo na kuweka misingi ya njia  bora  zinazotakiwa kufuatwa na wadau wa takwimu katika mchakato wa uzalishaji takwimu rasimi.

Amefafanua NBS haiwezi kutoa takwimu rasmi yenyewe bila kushirikiana na wadau ambao ndio watumiaji katika kuharakisha maendeleo ya nchi."Takwimu rasmi zina kanuni na miongozo yake ya kutumia hadi kutumika kupanga sera bora za kuleta maendeleo kwa wananchi,"amesema Dk.Chuwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Albina Chuwa akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau kuhusiana na Uelimishaji Umma kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Waratibu wa Jukwaa la Maendeleo Endelevu –Tanzania, Stephen Chacha akizungumza katika mkutano kuhusu namna ya kushirikiana na NBS leo jijjini Dar es Salaam.
Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Oscar Mangula akizungumza katika mkutano wa wadau kuhusiana na sheria ya Taifa ya Takwimu leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau katika mkutano wa wadau wa Takwimu

MGOMBEA TLP AOMBA WANANCHI KUENDELEA KUWAAMINI WAPINZANI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
MGOMBEA ubunge Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam kupitia Tanzania Labour Party(TLP), Dk. Godfrey Malisa ameomba wananchi wa jimbo hilo kuendelea kuamini kuwa upinzani bado uko imara na kuwataka kujitokeza kwa  wingi na kumpigia kura  ili kuhakikisha jimbo hilo linabaki katika mikono ya upinzani kama walivyokuwa wameaminiwa hapo awali.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Dk.Malisa amesema TLP iko imara na kitahakikisha kinatatua kero zote za jimbo la Kinondoni na kuwaomba wananchi kurudisha imani yao kwao licha ya kuonesha kukerwa kwao na kitendo cha Mbunge wa CUF Maulid Mtulia ambaye wapinzani walimchagua kwa nguvu zote katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 kuhamia Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Amesema, katika kipindi cha siku saba ambacho wanaendelea na kampeni zao, wananchi wamekuwa wakimlalamikia  na kumueleza kuwa wamekerwa na kitendo cha Mbunge wa CUF kuhamia CCM na hata kufukia kumuuliza  iwapo watamchagua nae si anaweza kwenda huko huko kama hao wanaosikia wanahama kila siku.

Aidha amesema, Chadema siku za nyuma walishasema hawatasimamisha mgombea kwenye chaguzi ndogo kutokana na kutokuwa na imani na Serikali lakini cha kushangaza safari hii wameamua kusimamia mgombea kwenye jimbo hilo.

Ameeleza kitendo cha Chadema kumsimamisha mgombea Salum Mwalimu kimewaathiri na zaidi kimeonesha kutokuwa na misimamo kwenye mambo wanayowaambia wananchi.

“Kurudi kwao kunatuathiri sana kwani watanzania watakuwa hawatuamini, yaani wapiga kura wataona sisi wapinzani hatuaminiki, hatueleweki kwani tunapoongea inaonekana tunaongea uongo,"amesema Dk.Malisa.

Ameongeza akichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Kinondoni kipaumbele chake cha kwanza ni  la vijana na ujasiriamali kwani ni eneo lenye changamoto nyingi na kusisitiza atatumia nafasi yake kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kupitia chama cha TLP, Dk. Godfrey Malisa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam .

Bodi ya Filamu Yamaliza Mzozo Malipo Filamu ya Utu Wangu

$
0
0
Na: Mwandishi Wetu
Hatimaye Bodi ya Filamu nchini imerejesha furaha kwa msanii na mtayarishaji wa filamu ya Utu Wangu kufuatia kuongoza kikao cha usuluhishi kilichofikia muafaka kwa msanii huyo kulipwa stahiki zake.
Hayo yamejitokeza leo wakati wa kikao cha usuluhishi wa madai ya Msanii Sikujua Mbwembe mtayarishaji wa Filamu ya Utu Wangu dhidi ya Kampuni ya Steps Entertainment kilichofanyika katika ofisi za Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
“Nitumie fursa hii kumshukuru Dilesh Mkurugenzi wa Steps kwa kukubali wito lakini pia kukiri kuwa msanii huyu haja;ipwa stahiki zake na kuamua kumaliza suala hili kwa kumlipa kwa jasho lake Bibi. Sikujua” alisema Mama Fissoo.
Mama Fissoo ameishukuru Kampuni ya Steps kwa hatua ilizochukua na kusema kuwa huo ni muendelezo way ale ambayo walikubaliana huko awali ikiwemo kuwalipa wale wote wanaoidai Kampuni hiyo jambo ambalo wameanza kulitekeleza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Steps Entertainment Dilesh Solanki amesema kuwa wao kama kampuni inayojihusisha na mambo mbalimbali ikiwemo usambazaji wa filamu hawafurahishi na kuona wana ingia migogoro na wasanii kwa hao ndio wateja wao muhimu.
Aidha amesema kuwa shida ambayo ilipelekea kutoka kwa tatizo la malipo kwa msanii huyo ni kitendo cha kuwepo kwa mtu wa kati ambaye kwa kiasi kikubwa bndiye amekuwa akifanya mawasiliano nao tofauti na mhusika mkuu.
Kwa upande wake Msanii Sikujua Mbwembwe ameishukuru Serikali kupitia Bodi ya Filamu kwa kusema kuwa ameamini kweli kwamba Awamu ya Tani ni Serikali ya kutetea wanyonge ndiyo maana leo hii haki yake anaenda kuipata kwani ameangahika kwa muda mrefu sana.
“Binafsi nipende kuchukua fursa hii kuishukuru sana Serikali kupitia Ofisi yetu ya Bodi ya Filamu Tanzania, nimeleta malalamiko yangu tumekaa vikao vitatu haki yangu imepatikana keli Mungu ni mwema sana” alisema Bi. Sikujua.
Sikujua Mbwembe ni msaani mwenye ulemavu wa miguu ambaye alitayarisha filamu yake ya Utu Wangu na kuingia mkataba na Kampuni ya Steps Entertainment na kukutana na misukosuko katika malipo yake hata hivyo hii inaonyesha alipita katika njia zisizo sahihi, pamoja na yote hayo baada ya kuwasilisha madai yake katika mamlaka husika suala lake limeshughulikiwa na sasa anataraji kulipwa fedha zake na kunufaika na jasho lake mwenyewe.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF) Bibi. Joyce Fissoo akipitia nyaraka za makubaliano ya mauziano ya Filamu ya Utu Wangu baina ya Mtayarishaji wa Filamu hiyo Bi. Sikujua Mbwembwe (hayupo pichani) na Kampuni ya Steps Entertainment wakati wa kikao cha usuluhishi leo jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Bodi ya Filamu kufuatia mlalamikaji ambaye ni mtayarishaji wa filamu hiyo kufikisha malalamiko ya kutolipwa haki yake tangu mwaka 2015.

Mwenyekiti wa Kikao cha usuluhishi wa madai ya msanii wa filamu na mtayarishaji wa Filamu ya Mtu Wangu, Bw. Andrew Makungu ambaye pia ni mwakilishi kutoka Jeshi la Polisi Makao Makuu akielezea jambo mbele ya wajumbe wa kikao hicho kilichohudhuriwa na uongozi wa Kampuni ya Steps Entertainment pamoja na upande wa mdai ambaye ni Bi. Sikujua Mbwembwe (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Steps  Entertainment Dilesh Solanki akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa kikao cha usuluhishi wa madai ya msanii wa filamu na mtayarishaji wa filamu ya Utu Wangu Bi. Sikujua Mbwembe leo jijini Dar es Salaam. Madai hayo yanahusi kutolipwa kwa haki za mauziano ya filamu hiyo waliyokubaliana tangu mwaka 2015, hata hivyo suala hilo limepatiwa ufumbuzi baada ya Steps kuamua kulipa deni hilo. Kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Steps ambaye ni mtumishi wa zamani wa Cosota Bw. Yustus Mkinga na kulia ni Mtayarishaji wa Filamu John Lister.
Mwanasheria wa Kampuni ya Steps  Entertainment inayojishughulisha na usambazaji wa Filamu Bw. Yustus Mkinga akifafanua jambo wakati wa kikao cha usuluhishi usuluhishi wa madai ya msanii wa filamu na mtayarishaji wa filamu ya Utu Wangu Bi. Sikujua Mbwembe leo jijini Dar es Salaam. Mwaka 2015 Kampuni ya Steps iliingia mkataba wa kumiliki filamu hiyo kwa makubaliano ya kulipa sh. 7.5 milioni ambazo mpaka leo hawajalipa hali iliyopelekea madai hayo kufikishwa katika Ofisi za Bodi ya Filamu kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi. Kutoka kulia ni Watayarishaji wa Filamu Suleiman Omary (Suleshi) na John Lister, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Steps Entertainments Dilesh Solanki. Mtayarishaji wa Filamu ya Utu Wangu Bi. Sikujua Mbwembwe akiwa ndani ya Ofisi ya Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (hayupo pichani) alipohudhuria kikao cha usuluhishi wa madai yake dhidi ya Kampuni ya Steps Entertainment leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Steps Entertainment Dilesh Solanki akibadilishani mihutasari ya kikao cha usuluhi wa madai ya msanii wa filamu Bi. Sikujua Mbwembwe ambaye aliilalamikia Steps kutomlipa stahiki yake kufuatia kuwauzia kazi yake ya filamu ya Utu Wangu mara baada ya kumaliza kikao na kufikia muafaka wa Steps kumlipa msanii huyo pesa zake kuanzia tarehe 5 Februari 2018. Kulia anayeshuhudia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo. 

UZINDUZI WA KAMPENI ZA UBUNGE ZA CCM WILAYA YA KINONDONI


Kuanza Kwa Mkutano Wa Kumi Wa Bunge mjini DODOMA Jumanne Januari 20, 2018

Introducing "WATAKUBALI" by Mbosso

INTRODUCING "TUNAPENDANA" BY KAREN

Introducing "Nang'ang'ania" by Atan

MKOA WA PWANI WAZINDUA MSIMU MPYA WA KILIMO IKIWEMO MPUNGA 2018/2019

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,amekiagiza Chama Cha Ushirika cha Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU), kumnyang'anya mwekezaji wa Kichina M/S Guoming Tang ,hekari 300 kati ya 380 alizozihodhi,ili zitumiwe na wakulima msimu mpya wa kilimo.
Aidha ameuagiza ushirika huo, halmashauri ya Chalinze na serikali ya wilaya ya Bagamoyo kukakikisha hekta 1,800 kati ya 3,209 zilizopo kwenye shamba hilo ,zinatumika kupandwa mikorosho ya kisasa.
Ndikilo aliyatoa maagizo hayo wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa kilimo ikiwemo mpunga msimu wa 2018/2019.
Alisema ,mwekezaji huyo anapaswa kubakia na eneo atakaloweza kulifanyia kazi kuliko kuchukua eneo kubwa ambalo analikodisha na kujinufaisha nalo.
"Tena asisuesue ,nashukuru uongozi wa CHAURU uliopo umefanyia kazi maelekezo   aliyoyatoa Naibu Waziri kilimo, uvuvi na mifugo, William Ole Nasha na mie naagiza ,maelekezo hayo yafanyiwe kazi;"
"Msikubali kuwa watumwa kwenye ardhi na nchi yenu ,nasikia ameanza kutoa baadhi ya vitu vyake hivyo anyanganywe eneo hilo ,na nitakuja tena hapa kuona kama eneo hilo amenyang'anywa" alisisitiza.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani ,alikemea tabia inayofanywa pia na baadhi ya watu ya kuchukua maeneo makubwa kwenye shamba hilo na kuyakodisha.
Ndikilo ,alieleza ni marufuku kuwa madalali kwa kukodisha maeneo badala ya kulima wenyewe.
Pamoja na hayo ,alisema CHAURU ina eneo lenye hekta 3,209 ,ambapo zinazotumika katika Kilimo cha umwagiliaji ni 720 ,hivyo alielekeza hekta 1,800 zitumiwe kwenye kilimo kingine cha korosho .
"Leo hii mnaweza mkadharau lakini niwahakikishie miaka ijayo ,wakati mkifanikiwa katika kilimo hiki cha korosho ,mtanikumbuka ," alisema Ndikilo.
Akizungumzia msimu mpya wa kilimo ,Ndikilo aliwataka wakulima mkoani Pwani kulima kilimo cha kisasa kwa kujipanga kutumia zana za kisasa.
Alikemea kulea migogoro na uchochezi inayofanywa na baadhi ya wanachama na kusema atakaejihusisha na vitendo hivyo achukuliwe hatua hata kufukuzwa uanachama.
 Mkuu Wa Mkoa Wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,akizindua msimu Mpya Wa Kilimo 2018/2019,ikiwemo mpunga, Mkoani hapo ,kwa kulima kisasa kwa kutumia  trekta 
Mkuu Wa Mkoa Wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo akikagua mchele unaolimwa kupitia chama cha ushirika cha wakulima wa umwagiliaji Ruvu (CHAURU )wilayani Bagamoyo
Mkuu Wa Mkoa Wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, akizungumza jambo kabla ya kuzindua msimu mpya wa Kilimo 2018/2019 katika mashamba ya Ushirika wa CHAURU ,huko Ruvu,Bagamoyo mkoani Pwani.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images