Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

WATANZANIA TISA KUCHEZESHA NA KUSIMAMIA LIGI YAMABINGWA NA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRICA

0
0
Waamuzi nane kutoka Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF kuchezesha mechi za Ligi ya Mabingwa Africa na Kombe la Shirikisho.

Waamuzi wanne wameteuliwa kuchezesha mchezo wa Ligi ya mabingwa kati ya Lydia Ludic Burundi Academic ya Burundi na Rayon Sports ya Rwanda.

Mwamuzi Mfaume Ali Nassoro atakuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Frank John Komba wakati mwamuzi msaidizi namba mbili atakuwa Soud Idd Lila na mwamuzi wa akiba Israel Omusingi Njunwa Mujuni huku kamishna wa mechi hiyo akitokea nchini Zimbabwe Gladmore Muzambi.

Mchezo huo utachezwa kati ya Februari 20 na 21, 2018 nchini Burundi.Waamuzi wengine wanne wa Tanzania watachezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Masters Security Services FC ya Malawi dhidi ya Atletico Petroleos de Luanda ya Angola nutakaochezwa kati ya Febriari 20 na 21,2018 nchini Malawi.

Elly Ally Sasii atakuwa mwamuzi wa katikati kwenye mchezo huo akisaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba moja Salim Mkono Mohamed na mwamuzi msaidizi namba mbili Ferdinand Chacha na mwamuzi wa akiba Alphonce Mwandembwa Emmanuel wakati kamishna wa mchezo huo atatokea Ethiopia Luleseged Gegashaw Asfaw.

Wakati huo huo Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF limemteua Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Ndugu Michael Richard Wambura kuwa Kamishna wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Africa kati ya Bidvest Wits ya Africa Kusini na Pamplemousses SC ya Mauritius utakaochezwa Februari 10, 2018 kwenye uwanja wa Johannesburg-Bidvest.

Wambura atasimamia mchezo huo utakaochezeshwa na waamuzi kutokea Seychelles.Mwamuzi wa kati Nelson Emile Fred akisaidiwa na Hensley Danny Petrousse na James Fedrick Emile wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Allister Barra.Huu unakuwa ni muendelezo kwa CAF kuteua viongozi mbalimbali wa Tanzania kuwa makamishna wa mechi zinazoandaliwa na Shirikisho hilo.

Tayari Rais wa TFF Ndugu Wallace Karia licha ya kuteuliwa kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya fainali za Africa kwa wachezaji wanaocheza ndani CHAN pia ameteuliwa mara mbili kuwa Kamishna wa mechi ya ufunguzi ya CHAN wenyeji Morocco walipocheza dhidi ya Mauritania Februari 13, 2018 na mchezo mwingine uliowakutanisha Namibia na Zambia uliochezwa Februari 22, 2018.

Aidha mjumbe mwingine wa kamati ya utendaji Ahmed Iddi Mgoyi naye ameteuliwa na CAF kuwa kamishna wa mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya AFC Leopards ya Kenya dhidi ya Fosa Juniors ya Madagascar mchezo utakaochezwa kati ya Februari 9,10 na 11,2018 nchini Kenya.

WADADISI WATAKIWA KUZINGATIA MAJUKUMU YAO WAKATI WA UKUSANYAJI WA TAKWIMU

WADAU WA SEKTA BINAFSI WAKUTANA KUJADILI NAMNA YA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kifo cha Jaji Mstaafu Robert Kisanga

0
0
Jaji Mstaafu Robert Kisanga enzi za uhai wake.


TRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA KODI KWA WADAU MBALIMBALI

0
0

Na: Veronica Kazimoto.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imepongezwa kwa kuendelea kutoa elimu ya kodi kwa wadau mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wa ofisi za Serikali na Asasi za Kiraia kwa ajili ya kuongeza ufahamu na kuwa mabalozi wa masuala yanayohusu kodi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya elimu ya kodi kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) yaliyofanyika leo ofisini hapo,  Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Bw. Edwin Rutageruka amesema TRA inastahili kupongezwa kwa kazi inayoifanya ambayo imepelekea kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato.
"Ni dhahiri kwamba, sasa hivi  TRA inafanya kazi kubwa ya ukusanyaji wa mapato na kutoa elimu ya kodi kwa vikundi na taasisi mbalimbali, hivyo, fursa hii tuliyoipata tuitumie vizuri ili kuongeza uelewa wa kutosha kuhusu kodi ili tuwe  mabalozi wazuri kwa wengine", amesema Rutageruka.
Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania  Bi. Rose Mahendeka, akiwasilisha mada ya Kodi na Mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2017 amesema,  kila mwananchi anajukumu la kudai risiti kila anaponunua bidhaa na kila mfanyabiashara anatakiwa kutoa risti kila anapofanya mauzo.
 Afisa Muelimishaji Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Rose Mahendeka akiwaelimisha Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuhusu Kodi na Mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya Mwaka 2017/18 katika ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo 24 Januari, 2018.
 Msaidizi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Chama Siriwa akiwasilisha mada mbele ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuhusu Kodi ya Majengo, katika ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo 24 Januari, 2018.
Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Valentine Baltazar akiwasilisha mada mbele ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuhusu Taratibu za Kiforodha, katika ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo 24 Januari, 2018. (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

CAF YATAJA WAAMUZI WATAKAOCHEZESHA MECHI YA YANGA NA SAINT LOUIS FC LIGI YA MABINGWA

0
0
Shirikisho la Mpira wa miguu Barani Africa CAF limetaja waamuzi watakaochezesha mchezo wa kwanza na mchezo wa pili wa Ligi ya mabingwa Africa kati ya Yanga ya Tanzania dhidi ya Saint Louis FC ya Seychelles.

Mchezo wa kwanza utachezwa Februari 10, 2018 uwanja wa Taifa na utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia na Kamishna wa mchezo akitokea nchini Namibia.

Mwamuzi wa kati atakuwa Belay Tadesse Asserese akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Tigle Gizaw Belachew na mwamuzi msaidizi namba mbili Kinfe Yilma Kinfe wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Amanuel Heleselass Worku na Kamishna Frans Vatileni Mbidi.

Mechi ya pili itakayochezwa Seychelles kati ya Februari 20 na 21,2018 itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar na kamishna atatoka Mauritius.

Mwamuzi wa kati atakuwa Andofetra Avombitana Rakotojaona akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Lionel Hasinjarasoa Andrianantenaina na mwamuzi msaidizi namba mbili Pierre Jean Eric Andrivoavonjy na mwamuzi wa akiba Hamada el Moussa Nampiandraza,kamishna wa mchezo huo Ahmad Nazeer Hossen Bowud.

WANANCHI WAVUTIWA NA HUDUMA KATIKA BANDA LA MAONYESHO LA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA) ZANZIBAR

0
0
Mamia ya wananchi wa Tanzania Zanzibar wameendelea kufurika katika viwanja vya Maisara Zanzibar kunakofanyika Tamasha la Nne la Maonyesho ya Biashara la Zanzibar; yakiwa ni sehemuu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.

Katika maonyesho hayo pamoja na mambo Mengine Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa inatoa huduma ya ugawaji Vitambulisho vya Taifa, kusajiliwa kwa wale ambao hawakuwahi kusajiliwa pamoja na kupatiwa maelezo yanayohusu huduma zinazotolewa na Mamlaka.

Miongoni mwa Shehia ambazo Vitambulisho vinatolewa ni Mkunazini, Kiponda, Shangani,Kikwajuni juu, Kikwajuni Bondeni,Kisima Majongoo,Kiswandui, Malindi, Mchangani,Mwembe Tanga, Kilimani, Urusi, na Jang’ombe,.

Akizungummzia huduma zinazotolewa kwenye Banda hilo Meneja wa Mifumo wa Komputa ndugu Abdallah Mmanga amesema Wananchi waliofika kwenye Banda la NIDA kusajiliwa wanatakiwa kufika na nakala ya Cheti cha kuzaliwa, Vyeti  vya shule kuanzia na  Cheti cha kuhitimu Elimu ya Msingi, Pasi ya kusafiria (Pasport),Kadi ya Kupigia kura, Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, Leseni ya Udereva, Kadi ya Bima ya Afya, Kadi ya mfuko wa Jamii (NSSF,ZSSF,PPF,GEPF nk)

Pindi maonyesho hayo yatakapomalizika; wananchi ambao watakosa fursa wameshauriwa kufika kwenye ofisi za NIDA zilizopo kwenye kila Wilaya kwa Unguja na Pemba; ili kusajiliwa pamoja na kuendelea kuchukua Vitambulisho vyao kwa wale ambao wamekamilisha taratibu za Usajili.

Kwasasa Zanzibar imekamilisha Usajili wananchi Vitambulisho vya Taifa kwa asilimia 99 na mipango ya kuanza rasmi kwa matumizi ya Vitambulisho vya Taifa inaendelea kupitia wadau mbalimbali ili wananchi kuanza kunufaika.
  Afisa Uhamiaji Ndg. Ali S. Nasor Mkuu wa Utawala na Fedha (DCI) Makao Makuu ya Ofisi ya Uhamiji ZanzIbar akiweka saini kwenye kitabu cha wageni alipotembelea banda la maonyesho la Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) viwanja vya Maisara -  Unguja.

Wananchi waliotembelea Banda la Maonesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakifuatilia Vitambulisho vyao kutoka Shehia mbali mbali za Mjini Unguja, wakati zoezi la Ugawaji Vitambulisho likiendelea. 

HALMASHAURI ISIYOPANDA MITI MILIONI 1.5 MWAKA HUU ITATOZWA FAINI- RC WANGABO

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameziagiza Halmashauri nne za Mkoa wa Rukwa kuhakikisha zinafikia lengo la kupanda miti milioni 1.5 kila moja hadi kufikia mwisho wa mwaka wa 2017/2018 ili kufikia lengo la Mkoa la kupanda miti milioni 6 katika kutekeleza sera ya kupanda miti kitaifa.

Amesema kuwa Halmashauri itakayoshindwa kufikia lengo itatakiwa kulipa faini ya shilingi Milioni 1 kuilipa Halmashauri itakayofika lengo ambapo Halmashauri Mshindi inategemewa kupata shilingi Milioni 3 na fedha hizo itapewa taasisi itakayopanda miti mingi kuliko taasisi nyingine ya serikali ndani ya Halmashauri iliyoshinda hasa mashule ili kuwafundisha wanafunzi umuhimu wa kupanda miti.

“Halmashauri ambayo haikufikia lengo imuume kutoa shilingi Milioni 1 kumlipa mwenzake, katika hizo Halmashauri 4, kwa maana mshindi atapata shilingi Milioni 3, lakini endapo Halmashauri zote zitafikia malengo nitazipa Halmashauri Shilingi Milioni 1, na hiyo fedha itakwenda kwenye taasisi iliyopanda miti mingi kuliko taasisi nyingine hasa mashule,” Mh. Wangabo alibainisha.

Ameongeza kuwa mwaka ujao wa 2018/2019 halmashauri itakayoshindwa kufikia lengo la kupanda miti Milioni 1.5 italipa faini ya shilingi Milioni 5 ili kila halmashauri iweze kufikia lengo na kutimiza maelekezo ya serikali na kuwaonya wote wenye tabia ya kuchoma misitu jambo linalokwamisha jitihada za kutunza mazingira.

Mwenyekiti wa Taasisi ya REYO Abdallah Rubega (Flana Nyeupe) akitoa maelezo juu ya aina ya miti itakayopandwa katika msitu wa Wangabo kwa heshima ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mazingira huku ameshikilia bango la kuhamasisha wananchi kuacha kuchoma moto misitu na kuendelea kutunza vyanzo vya maji. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akipanda mti ishara ya kufungua upandaji miti Mkoani Rukwa iuli kufikia lengo la mkoa la kupanda miti milioni 6, Maadhimisho yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Matai, Wilayani kalambo.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule (kulia) akisaidiana na baadhi ya wananfunzi wa Shule ya Sekondari Matai kupanda miti ikiwa ni juhudi za kuwaelimisha wananfunzi umuhimu wa kupanda miti.
Wanafunzi mbalimbali wakiendelea kupanda miti  katika eneo lililoandaliwa maalum kwa kupanda miti katika shule hiyo. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
  ​

WADAU WA SEKTA BINAFSI WAKUTANA KUJADILI NAMNA YA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

CAF YATAJA WAAMUZI SIMBA, GENDARMERIE KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

0
0
Waamuzi kutoka Sudan Kusini wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF kuchezesha mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Simba ya Tanzania na Gendarmerie Tnale ya Djobouti itakayochezwa Februari 21, 2018 Uwanja wa Taifa.

Mwamuzi wa kati atakuwa Alier Michael James akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Abdallah Suleiman Gassim ,mwamuzi msaidizi namba mbili Gasim Madir Dehiya wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Kalisto Gumesi Simon Samson na Kamishna wa mchezo huo kutoka Botswana ni Mmonwagotlhe Edwin Senai.

Mchezo wa marudiano utakaochezwa Djibouti kati ya Februari 20 na 21,2018 wenyewe utachezeshwa na waamuzi kutoka Burundi na Kamishna wa mchezo atatokea nchini Rwanda.

Mwamuzi wa kati ni Eric Manirakiza akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Pascal Ndimunzigo,mwamuzi msaidizi namba mbili Willy Habimana,mwamuzi wa akiba Pacifique Ndabihawenimana na kamishna Gaspard Kayijuka.

SIMBA SC WAJINOA UWANJA WA BANDARI

0
0
 Kocha  mkuu wa Simba SC, Pierre  Lechantre  katikati na kushoto ni kocha Msaidizi  Masoud Djuma wakipeana maelekezo katika mazoezi  hayo kulia ni Meneja wa Simba SC, Robert Richard Uwanja wa Bandari Temeke Jijini Dar es Salaam.
 Wachezaji SimbaSc wakiwa kwenye mazoezi ya kujifua kukabiliana na mchezo wao wa raundi ya 16 dhidi ya Wanalizombe MajimajiFc utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili hii majira ya Saa 10 jioni.
Mchezaji wa Simba SC, Shomari Kapombe akifanya mazoezi ya kujifua kwa akili ya mchezo wao wa raundi ya 16 dhidi ya MajimajiFc yenye makzi yake Mkoani Ruvuma leo katika Uwanja wa Bandari uliopo Jijini Dar es Salaam.

Michuzi TV: JKCI YAISHUKURU REDIO TIMES KWA KUTAMBUA MCHANGO TAASISI HIYO

Mrisho Mpoto atoa msaada kwa yatima, awapa msingi wa maisha

0
0
Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto kwa kushirikiana na team yake ya Mpoto Foundation alitembelea kituo cha watoto yatima cha  Mwandaliwa na madrasa ya Tidaiya iliyopo Tandale jijini Dar es salaam leo.

Akizungumza  akikabidhi zawadi hizo, Mpoto alisema lengo kubwa la kutoa zawadi hizo ni kusaidia malezi ya watoto katika vituo hivyo ili wakue wakiwa katika maadili mazuri.
“Nimeamua kugawana na watoto kidogo nilichojaliwa nacho ili waweze kufurahi lakini pia kuwasaidia katika makuzi hasa kwenye suala zima la kidini na maadili.” alisema Mpoto.
Aidha Mpoto aliongeza kuwa kutokana na mambo mengi yanayoendelea kwa sasa nchini na duniani kote, kuna uwezekano kwa watoto kukua bila misingi mizuri ya dini, heshima na uzalendo kama wasipoandaliwa mazingira mazuri.
Ili kuhakikisha hilo halitokei, Mpoto amesema imekuwa sababu kubwa iliyompelekea kujitolea zawadi hizo ambapo kwa yeye ni kuufungua mwaka 2018 akiwa na thawabu kutoka kwa watoto.
 Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto akigawa misaada kwa kituo cha watoto yatima cha  Mwandaliwa na madrasa ya Tidaiya iliyopo Tandale jijini Dar es salaam leo.
 Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto akipata picha ya kumbukumbu katika  kituo cha watoto yatima cha  Mwandaliwa na madrasa ya Tidaiya iliyopo Tandale jijini Dar es salaam leo.
  Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto akigawa misaada kwa kituo cha watoto yatima cha  Mwandaliwa na madrasa ya Tidaiya iliyopo Tandale jijini Dar es salaam leo.

VOA Swahili: Duniani Leo 24th January 2018

MICHUZI TV 1 TO 1 GOSSIP: MTOTO WA RAY KIGOSI UTATA MTANDAONI, NABII TITO NI MZOZO..


MAGAZETI YA ALHAMIS LEO JANUARY 25,2018

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LAKABIDHI NYUMBA ZA MAKAZI 63 ZA IYUMBU SATELLITE CENTER KWA UHAMIAJI

0
0

Meneja wa Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Itandula Gambalagi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa na Kamishna wa Fedha, Ndugu Peter Chogero kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wakikabidhiana hati ya makabidhiano ya nyumba baada ya kukabidhi nyumba 63 kwa Jeshi la Uhamiaji.
Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Nyumba na Uhamiaji baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Nyumba na Uhamiaji baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
Wafanyakazi na uongozi wa Jeshi la Uhamiaji wakiwa wameshika mfano wa ufunguo baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.

Mradi huu ambao ujenzi wake ulianza Desemba 2016 una ukubwa wa ekari 234 na ni moja ya sehemu ya mji uliopangiliwa kitaalamu kwa kuzingatia sheria na kanuni za mipango miji na utajengwa katika awamu tatu. Nyumba hizi 63 ambazo zimeshakamilika na kuanza kukaliwa zinakabidhiwa leo kwa Idara ya Uhamiaji.

Makabidhiano haya yamefanywa na Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Ndugu Itandula Gambalagi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC na Kamishna wa Fedha, Ndugu Peter Chogero kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.

Makabidhiano haya yanafanyika baada ya ahadi ya Shirika la Nyumba kwa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ya kujenga nyumba makao makuu ya nchi Dodoma.Katika uzinduzi wa nyumba hizi, Mkurugenzi Mkuu wa NHC alimhakikishia Mh. Rais kwamba nyumba hizi zimekamilika na ziko tayari kwa kukaliwa.

Leo ni siku ya furaha kuona kwamba NHC inakabidhi nyumba kwa Uhamiaji ambaye ni mmoja wa wanunuzi wakubwa wa nyumba katika mradi huu.Nyumba hizi ni bora kabisa zimejengwa kwa ustadi mkubwa. Ni wito wetu kwamba nyumba hizi watazitunza ikiwa na mazingira yake.

Mradi huu wa nyumba 300 ikiwa 150 zimekamilika ni kati ya miradi mingi ambayo NHC inatekeleza.

KILA MWAKA WATANZANIA 50,000 HUPATA SARATANI

0
0
*Yaelezwa saratani ya shingo ya kizazi ndiyo inayoongoza 
*Wanafunzi wa kike kuanzia darasa la nne kupewa chanjo

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

TAASISI ya Saratani ya Ocean Road imesema imekuwa ikipokea wagonjwa wapya wa saratani 50,000 kila mwaka huku ikielezwa saratani ya shingo ya kizazi ndio inayoonekana kuongeza.

Pamoja na hali hiyo, imeelezwa jitihada mbalimbali zinafanywa na Serikali kwa kushirikiana na taasisi hiyo ambapo wameweka mkakati wa kuhakikisha wanafunzi wa kike waliopo kuanzia dasara la nne nchi kote watapatiwa chanjo itayakayosaidia kuwakinga na aina hiyo ya saratani.

Hayo yamesemwa leo (jana)  jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Kinga katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk.Chrispin Kahesa wakati wa semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini.

Lengo la semina hiyo ilikuwa ni kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa satarani, hali ilivyo kwa sasa nchini, sababu zinazosababisha ugonjwa huo na pamoja na jitihada zinazochukuliwa kupunguza kasi ya saratani nchini.

WATANZANIA 50,000 KILA MWAKA HUPATA SARATANI

Akizungumzia ugonjwa huo ,Dk.Kahesa amesema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani(HWO), Tanzania kila mwaka kunakuwa na wagonjwa wapya 50,000 wa saratani na hivyo unaweza kuona ukubwa wa ugonjwa huo nchini kwetu.

"Kila mwaka Tanzani wagonjwa wapya wa saratani ni 50,000.Ni idadi kubwa ambayo lazima tuweke mikakati ya pamoja kuhakiksha tunapunguza idadi hiyo na ukweli tunaweza."Ni suala la kuamua tu kuanzia mtu mmoja mmoja, familia na Watanzania kwa ujumla kwani baadhi ya sababu zinazosababisha ugonjwa huu tunaweza kuzikwepa.

"Baadhi ya sababu zinazosababisha saratani ni uvutaji sigara, pombe, vyakula vyenye mafuta mengi, kutofanya mazoezi ya mwili,unene na  taka sumu.Hivyo ukiangalia hizo sababu unaweza kuziepuka na ukishindwa zote basi chagua hata sababu mbili zieupuke,"amesema.

Amefafanua zipo saratani ambayo hutokana na kirusi ambacho hubebwa na mwanaume na kisha kukiacha kwa mwanamke kupita tendo la ndoa na aina hiyo ya kirusi ndicho kinachosababisha saratani ya shingo ya kizazi.



WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA WILAYA MKOA WA MARA WAIMWAGIA SIFA AGPAHI

0
0
Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya mkoa wa Mara wamelipongeza Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) kwa kutekeleza kikamilifu mradi wa “Boresha” unaotoa huduma za kinga, tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU na Ukimwi mkoani humo.

Pongezi hizo zimetolewa Januari 23,2018 na Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya mkoa wa Mara, Charles Kitamuru Chacha ambaye ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Rorya wakati akifunga mafunzo kuhusu taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za wafadhili ‘Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC)’.

Mafunzo hayo ya siku mbili kuhusu taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za wafadhili yaliyoanza Januari 22,2018 hadi Januari 23,2018 yalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwembeni na kuhudhuriwa na wakurugenzi na viongozi wa timu za afya za mikoa na wilaya.

Mwenyekiti huyo wa wakurugenzi alisema shirika la AGPAHI limekuwa msaada mkubwa katika sekta ya afya kwenye halmashauri za wilaya mkoani humo hususani katika miradi yake ya Ukimwi na kusisitiza kuwa halmashauri zote zitaendelea kuunga mkono shughuli zinazofanywa na AGPAHI.

“Kwa niaba ya wakurugenzi wenzangu nikiwa kama mwenyekiti wa wakurugenzi wa halmashauri za wilaya mkoani hapa, natoa shukrani za pekee kwa wadau wetu AGPAHI na Watu wa Marekani kupitia CDC kwa shughuli mnazofanya kufanikisha huduma za kinga, tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU na Ukimwi”, alieleza Chacha.
Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya 9 za mkoa wa Mara, Charles Kitamuru Chacha akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kuhusu taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za wafadhili "Watu wa Marekani kupitia CDC" katika ukumbi wa Mwembeni uliopo katika manispaa ya Musoma.
Chacha akiwasisitiza washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia mambo waliyojifunza ili kuboresha utendaji kazi kwenye maeneo yao.
Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mara, Dk. Oning'o Felix akilishukuru shirika la AGPAHI kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kuboresha huduma katika vituo vya afya.
Afisa Ruzuku Mwandamizi wa shirika la AGPAHI, Leticia Gilba akiwapongeza washiriki wa mafunzo hayo kwa kuwa wasikivu katika mada zote zilizotolewa kwa muda wa siku mbili.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images