Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109583 articles
Browse latest View live

MAOFISA WA BUNGE WATOA ELIMU KWA WANAFUNZI WA NYAMIONGO, MWISENGE

0
0
 Mkurugenzi Msaidizi na Mratibu wa Dawati la Bunge la Afrika kutoka Ofisi ya Bunge, Ndg. Lawrence Makigi, akizungumza  jambo wakati akitoa Elimu kwa Shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Bunge la Tanzania kwa Shule za Sekondari za Nyamiongo, Mwisenge na Mokoko ikiwa ni mwendelezo wa utoaji wa elimu kwa Shule za sekondari zilizopo Manispaa ya Musoma, katika tukio lililofanyika leo katika Shule ya Sekondari Mwisenge iliyopo Manispaa ya Musoma.
Afisa wa Bunge, kutoka Ofisi ya Bunge Dodoma Ndg. Bakari kishoma akizungumza  wakati akitoa Elimu kwa Shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Bunge la Tanzania kwa Shule za Sekondari za Nyamiongo, Mwisenge na Mokoko ikiwa ni mwendelezo wa utoaji wa elimu kwa Shule za sekondari zilizopo Manispaa ya Musoma, katika tukio lililofanyika leo katika Shule ya Sekondari Mwisenge iliyopo Manispaa ya Musoma.
 Wanafunzi wa Shule za Sekondari za Nyamiongo, Mwisenge na Mokoko zilizopo Manispaa ya Musoma wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi na Mratibu wa Dawati la Bunge la Afrika kutoka Ofisi ya Bunge, Ndg. Lawrence Makigi akizungumza  wakati akitoa Elimu kwa Shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Bunge la Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa utoaji wa Elimu kwa Shule za Sekondari zilizopo Manispaa ya Musoma, katika tukio lililofanyika leo katika Shule ya Sekondari Mwisenge iliyopo Manispaa ya Musoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

RC MARA TOKOMEZA UVUVI HARAMU ZIWA VICTORIA-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza  Mkuu wa Mkoa wa Mara, Bw. Adam Malima kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa  wahakikisha wanatokomeza uvuvi haramu katika ziwa Victoria.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumapili, Januari 21, 2018) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa huo katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi  mkoani Mara.

“Kuna tatizo kubwa la uvuvi haramu katika Ziwa Viktoria. Fanyeni doria za mara kwa mara na watakaobainika hatua stahiki za kisheria zichukuliwe dhidi yao.”

Alisema viongozi hao wanatakiwa wahakikishe wanatokomeza  uvuvi haramu haraka iwezekanavyo na pia wasimamie ulinzi wa rasilimali za ziwa Victoria ili ziweze kuwanufaisha wananchi wa mkoa huo na Taifa kwa ujumla.

Waziri Mkuu alisema baadhi ya wavuvi wamekua wakivua kwa kutumia nyavu zilizopigwa marufuku, kokoro pamoja na mabomu jambo ambalo haliwezi kuvumilika kwa sababu zana hizo zinaharibu uhai wa viumbe hai ndani ya ziwa Victoria.

Alisena ni vema mkoa huo ukaanzisha operesheni za mara kwa mara  katika ziwa Victoria kwa lengo la kuwasaka watu wote wanaojihusisha na vitendo vya uvuvi haramu na kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa wote watakaokamatwa.

Awali, Waziri Mkuu alizindua jengo la mama na mtoto pamoja na nyumba za watumishi katika kituo cha afya cha Murangi kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Musoma Vijijini.

Pia Waziri Mkuu akiambatana na Mkewe Mama Mary Majaliwa walitembelea nyumba ya kihistoria ambayo Baba wa Taifa marehemu Mwalimu Julius Nyerere alifikia akiwa katika harakati za kutafuta Uhuru, 1954. Nyumba hiyo ipo kata ya Murangi.

Akizungumzia kuhusu nyumba hiyo ambayo baadae ilitumika kama ofisi ya chama cha TANU kwa upande wa Majita, alisema ni lazima eneo hilo liendelee kudumishwa kwa sababu linabeba historia muhimu kwa Taifa.

Baada ya kutembelea nyumba hiyo, Waziri Mkuu aliwahutubia wakazi wa Halmashauri hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Murangi,  ambapo alitumia fursa hiyo kueleza juhudi mbalimbali za kuwaletea maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATATU, JANUARI 22, 2018.

WADAU WA SEKTA YA UJENZI WAJADILI RASIMU YA SERA MPYA

0
0
 Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),  Elizabeth Tagora akifungua mkutano wa wadau kuhusu mapitio ya Sera ya Ujenzi ya mwaka 2003 na uwasilishwaji wa rasimu ya Sera ya Ujenzi na Mkakati wa Utekelezaji 2018/19- 2029/30 jijini Dar es Salaam.
 Mwezeshaji wa majadiliano kuhusu rasimu ya Mkakati wa Utekelezaji wa sera ya Ujenzi ya mwaka 2018/19- 2029/30, Cyril Batalia akiwasilisha mada kwa wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu mapitio ya sera mpya ya ujenzi kwenye mkutano wa wadau wa ujenzi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wadau wa sekta ya ujenzi wakijadili rasimu kuhusu mapitio ya sera mpya ya ujenzi na mkakati wa utekelezaji wake 2018/19- 2029/30 leo jijini Dar es Salaam.
Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao cha mapitio ya sera mpya ya ujenzi na mkakati wa utekelezaji wake 2018/19- 2029/30 leo jijini Dar es Salaam(.picha na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii)

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI SITA, IKULU JIJINI DAR

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 22 Januari, 2018 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi sita walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha hati zao ni Mhe. Konstantinos Moatsos – Balozi wa Ugiriki hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Mhe. Fafre Camara – Balozi wa Mali hapa nchini mwenye makazi yake Addis Ababa nchini Ethiopia na Mhe. Dina Mufti Sid – Balozi wa Ethiopia hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya.

Wengine ni Mhe. Elizabeth Taylor – Balozi wa Colombia hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Mhe. Martin Gomez Bustillo – Balozi wa Argentina hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya na Mhe. Uriel Norman R. Garibay – Balozi wa Ufilipino mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya.

Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Mabalozi wote kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na ameahidi kuwapa ushirikiano utakaowezesha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi zao kukua zaidi.

Mhe. Rais Magufuli amewahakikishia kuwa Tanzania inatambua uwepo wa fursa mbalimbali za kibiashara na kiuchumi katika nchi hizo pamoja na ujuzi na uzoefu katika nyanja mbalimbali, na kwamba ni matarajio yake kuwa ujio wao utasaidia kuongeza manufaa ya kiuchumi na kubadilishana uzoefu.

Pia Mhe. Rais Magufuli amewaomba Mabalozi hao kufikisha salamu zake kwa viongozi wa nchi zao na amewakaribisha kutembelea Tanzania.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
22 Januari, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Balozi mteule wa Ugiriki hapa nchini Konstantinos Moatsos wakati alipokuwa akijitambulisha kabla ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Mali hapa nchini Fafre Camara Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwa Balozi wa Ethiopia hapa nchini Dina Mufti Said Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Colombia hapa nchini Elizabeth Taylor mara baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Argentina hapa nchini Martin Gomez Bustillo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Ufilipino hapa nchini Uriel Norman Garibay Ikulu jijini Dar es Salaam.

KIWANDA CHA SUNFLAG CHA ARUSHA CHAPIGWA FAINI KUFADHILI UVUVI HARAMU

0
0
Na John Mapepele

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amekitoza faini ya Shilingi milioni mia moja Kiwanda cha Sunflag Tanzania Limited cha jijini Arusha baada ya kukutwa na makosa mawili ambayo ni kuzalisha na kuuza nyavu bila kuwa na leseni kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kuzalisha na kuuza nyavu ambazo ziko kinyume na matakwa ya Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2009.

Kulingana na maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ajay Shah, kiwanda kimekuwa kikitengeneza vyavu hizo haramu kwa miaka mitatu mfululizo sasa ambapo inakadiliwa kuwa tayari kimeshatengeneza tani 1296 nyavu hizo zenye thamani ya shilingi bilioni nne.

Akitoa taarifa kwa Waziri Mpina, Kiongozi wa kikosi kazi cha kutokomeza uvuvi haramu katika kanda ya Ziwa Victoria, West Mbembati amesema kuwa tarehe 17/1/2018 walifika kwenye kiwanda hicho na kukamata marobota 584 yenye thamani ya milioni mia kufuatia maelekezo ya Waziri Mpina yaliyotolewa Mjini mwanza hivi karibuni baada ya mfanyabiashara Dastan Venanti kukamatwa na nyavu hizo zenye thamani ya milioni sitini na tano ambazo nyaraka zilionyesha alinunua katika kiwanda hicho.

Akipokea taarifa hiyo Waziri Mpina alisema mkakati uliopo kwa sasa ni kuwabaini watengenezaji na wasambazaji wote wa zana haribifu za uvuvi ikiwa ni pamoja na vyavu zisizoruhusiwa kisheria ambapo amesema hatua za kali za kisheria dhidi yao zitatumika ili kudhibiti uvuvi haramu kwenye maji(mito,maziwa na bahari) ya nchi yetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sunflag cha mjini Arusha, Ajay Shah, akiongoza zoezi la kuchoma nyavu haramu za dagaa zilizo chini ya sentimita 8 (marobota 584) zenye jumla ya shilingi milioni mia moja zilizokamatwa kwenye Kiwanda chake na Kikosi Kazi Maalum cha Kutokomeza Uvuvi Haramu nchini kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina kwenye dampo la takataka nje kidogo ya jiji la Arusha leo.(Na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (mwenye kofia) akikagua chumba cha baridi cha kuhifadhia samaki (Cold room) cha kampuni ya Alpha Choice mjini Arusha leo akiwa katika operesheni maalumu ya kudhibiti uvuvi haramu kulia ni mmliki wa kampuni hiyo Yussuf Khatry. 
Marobota 584 ya nyavu haramu yaliyotengenezwa na Kiwanda cha Sunflag cha mjini Arusha yenye thamani ya shilingi milioni 100 wakitekea kwenye dampo nje ya jiji la Arusha leo. Marobota hayo alikamatwa na Kikosi Kazi Maalum cha Kutokomeza Uvuvi Haramu nchini kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina ambapo uteketezaji huo uliongozwa na mmliki wa kiwanda hicho Ajey Shah.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (mwenye kofia) akisikiliza taarifa ya ukamataji wa marobota 584 ya nyavu haramu yaliyotengenezwa na Kiwanda cha Sunflag cha mjini Arusha yenye thamani ya shilingi milioni 100 kutoka kwa kiongozi wa Kikosi Kazi Maalum cha Kutokomeza Uvuvi Haramu nchini West Mbembati aliye kulia, kushoto mwakilishi wa Afisa Tawala wa Mkoa wa Arusha David Lyamongi.


JUKWAA LA USIMAMIZI WA MAAFA LAHITAJI UTASHI KISIASA,KISHERIA -PROF KAMUZORA

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu),Profesa Faustine Kamuzora amesema jukwaa la usimamizi wa maafa la Taifa linahitaji utashi wa kisiasa,uwajibikaji kisheria ,uelewa wa umma ,elimu ya kisayansi  na mipango makini ya maendeleo ili kutekeleza majukumu yake.

Profesa Kamuzora amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua jukwaa la Usimamizi wa Maafa la Taifa lililofanyika kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam.

“Jukwaa hili ni chombo cha kisheria hapa nchini kwa ajili ya kutathmini na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Serikali kuhusu majanga ya aina zote, hivyo linaundwa kwa kuzingatia kifungu cha 40 cha Sheria ya Usimamizi wa maafa namba 7 ya mwaka 2015,” amesema Profesa Kamuzora.

Amesema jukwaa hilo linakutana kwa mara ya kwanza toka sharia hiyo ianze kutumika hapa nchini, hivyo jukwaa linatoa fursa ya utaratibu wa usimamizi wa maafa kwa ushirikiano wa wataalam wa fani mbalimbali kwa kujumuisha sekta ya umma na sekta binafsi, mashirika ya kimataifa na Umoja wa Mataifa.

Ameongeza jukwaa linawajibu wa kushughulikia changamoto za kijamii ,kiuchumi na mazingira ya kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufanikisha kujumuisha upunguzaji wa madhara ya maafa katika mipango na sera za maendeleo ya Taifa na katika misaada ya kibinadamu.

TANZIA: BIBI LULU AKIDA SILVESTER AFARIKI DUNIA

0
0
TANZIA: Familia ya Bwana Sylvester Manase Matunda Lema, wa Sinza mkabala na kituo cha daladala Simu 2000 jijini Dar es Salaam, inasikitika kutangaza kifo cha mama yao, Bibi.Lulu Sylvester kilichotokea katika Hospitali ya Agha Khan tarehe 20/01/ 2018 majira ya saa 10;30 alfajiri.

Maandalizi ya mazishi yanafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza mkabala na kituo cha daladala Simu 2000. Mwili utaagwa Jumatano Januari 24, 2018 kuanzia saa 8 mchana Kanisani KKKT Usharika wa Sinza -Kumekucha. 

Mwili wa marehemu utasafirishwa siku ya Alhamisi tarehe 25/01/2018 kuelekea Kijiji cha Nronga-Machame, wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro.

Waziri Makamba akutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira. Kikao hicho kimejumuisha pia wajumbe kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambapo Mhe. Makamba amewasilisha taarifa ya Utekelezaji wa agizo la kutotumia mifuko ya plastiki nchini.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Kulia) akifuatilia hoja za wabunge  katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira hii leo mjini Dodoma. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo na Naibu Katibu Mkuu Bi. Butamo Phillip.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira hii leo mjini Dodoma.
 Sehemu ya waheshimiwa wabunge, Mhe. Mussa Ramadhani Sima na Mhe. Anatropia Lwehikila Theonest wakifuatilia mawasilisho juu ya Utekelezaji wa agizo la kutotumia mifuko ya plastiki nchini, katika kikao cha Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira. Kikao hicho kimejumuisha pia wajumbe kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambapo Mhe. Makamba amewasilisha taarifa ya Utekelezaji wa agizo la kutotumia mifuko ya plastiki nchini.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Kulia) akifuatilia hoja za wabunge  katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira hii leo mjini Dodoma. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo na Naibu Katibu Mkuu Bi. Butamo Phillip.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira hii leo mjini Dodoma.
 Sehemu ya waheshimiwa wabunge, Mhe. Mussa Ramadhani Sima na Mhe. Anatropia Lwehikila Theonest wakifuatilia mawasilisho juu ya Utekelezaji wa agizo la kutotumia mifuko ya plastiki nchini, katika kikao cha Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira mjini Dodoma.

MV Njombe yafungua fursa za biashara Tanzania, Malawi na Msumbiji

0
0
Kuanza safari kwa Meli za kisasa za mizigo za MV Njombe na MV Ruvuma ambazo zina uwezo wa kubeba uzito wa tani 1,000 kumefungua fursa za kibiashara kati ya Tanzania, Malawi na Msumbiji.

Meli ya Mv Njombe ambayo imefanya safari yake kwa mara ya kwanza nchini Malawi imefika salama na kutia nanga katika bandari za Nkhata Bay. Meli ya Mv Ruvuma inayopakia shehena ya Clinker inatarajiwa kutia nanga katika Bandari ya Monkey Bay nchini Malawi siku mbili zijazo.MV Njombe ambayo ilibeba takribani tani 800 ya shehena ya saruji kutoka bandari ya Kiwira nchini Tanzania hadi bandari ya Nkhata Bay nchini Malawi imetia nanga salama na imetumia muda mfupi zaidi kufika Malawi.

MV Ruvuma ambayo ni pacha wa MV Njombe nayo imepakia takribani tani 800 za shehena ya ‘Clinker’ katika bandari ya Kiwira nchini Tanzania kuelekea bandari ya Monkey bay nchini Malawi.Akizungumzia ujio wa shehena hizo za Saruji na ‘Clinker’, Balozi wa Tanzania nchini Malawi ambaye pia alikuja kushuhudia tukio hilo, Mheshimiwa Benedicto Mashiba amesema kwamba kuanza kwa safari hizo ni habari njema kwa wafanyabiashara wa Tanzania na Malawi .

Balozi Mashiba amesema kwamba, ujio wa meli hizo ni ufunguo wa biashara kati ya Tanzania na Malawi kwani kusafirisha bidhaa kwa njia ya maji ni nafuu na salama zaidi ukilinganisha na barabara.

“Usafiri huu ni mkombozi kwa wananchi na wafanyabiashara wa nchi hizi mbili (Malawi na Tanzania) kwani utawezesha usafirishaji wa mizigo kwa wingi ukilinganisha na njia nyingine kama barabara,” amesema Balozi Mashiba.Mashiba amesema kwamba kuna biashara kubwa ya kusafirisha mizigo kati ya Tanzania, Malawi na Msumbiji kupitia Ziwa Nyasa hivyo kuanza safari kwa meli hizo kutasaidia kuongeza zaidi ukubwa wa shehena katika ya nchi hizo.
 Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Balozi Benedicto Mashiba kushoto, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nkhata Bay nchini Malawi Alex Mdooa mara baada ya meli kuwasili bandarini hapo
 Mkuu wa bandari za Ziwa Nyasa, Ajuaye Msese kushoto, akitoa maelezo kwa Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Balozi Benedicto Mashiba kulia, katikati kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkhata Bay nchini Malawi Alex Mdooa
 MV Njombe ilipowasili bandari ya Nkhata Bay nchini Malawi
MV Njombe mara baada ya kutia nanga bandari ya Nkhata Bay nchini Malawi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MIFUKO 3000 SARUJI YACHANGWA KUKAMILISHA USHINDI SEMINARI

0
0
NA TIGANYA VINCENT

VIONGOZI  mbalimbali wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) na Serikali Mkoani Tabora wameahidi kutoa mifuko 3000 ya saruji kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Shule ya Seminari ya Ushindi inayojengwa katika eneo la Kipalapala kwenye Manispaa ya Tabora.

Akizungumza jana mjini Tabora kabla ya zoezi hilo la harambee kuanza Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzanaia Askofu Dkt Barnabas Mtokambali alisema kuwa Kanisa limeamua kujenga Shule mbalimbali ili kutoa mchango katika kupiga vita umaskini , maradhi na ujinga.

Alisema kuwa Kanisa linachukua hatua hiyo kwa kutambua kuwa silaha kubwa ya kupambana na maadui hao watatu ni elimu ndio maana pamoja na kutoa huduma nyingine katika jamii kama vile afya na maji pia wawekeza katika kujenga kujenga ili kuelimisha jamii.

Askofu Mkuu wa TAG Askofu Dkt.Mtokambali alisema kuwa Viongozi wa Kanisa na watu wengine kama wazazi wanalojukumu la kuwasaidia watoto kuwapata elimu bora na yenye maadili itakayowasaidia kupiga vita umaskini, ujunga na maradhi.

Alisema kuwa elimu bora na yenye maadili itamwezesha mtoto kuweza kutawala mazingira yake ambayo yatamasaidia kuondoa maadui hao watatu.Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salamu za Mkoa wakati wa zoezi hilo , alisema kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa madhehebu yote na wadau mbalimbali wanaungana na Serikali katika kutoa huduma mbalimbali ikiwemo elimu na afya.

Alisema kuwa atahakikisha kuwa vikwazo vyote ambavyo vichelewesha upatikanaji wa huduma hizo kwa jamii vinaondolewa haraka ili wananchi waweze kunufaika haraka na huduma zilizopangwa kutolewa.Awali Mkurugenzi wa akielezea maendeleo ya ujenzi wa Seminari ya Ushindi alimuomba Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha anawasaidia kuwatambulisha kwa uongozi wa elimu mkoani humo ili waweze kufanyakazi kwa karibu zaidi.

Alisema kuwa  Idara ya Elimu ya TAG mkoani Tabora imekuwa haifanyi vizuri katika baadhi ya shule kwa sababu ya kukosa ushirikiano kwa watendaji wa sekta ya elimu.

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Barala la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 22, 2018. PICHA NA IKULU

MALI ZA CHAMA CHA USHIRIKA MARA KUKAGULIWA-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itatuma wakaguzi ili wakague mali za Chama cha Ushirika cha mkoa wa Mara.

Amesema Serikali imeanza kufuatilia mali za vyama vya Ushirika nchini zikiwemo za chama cha Ushirika mkoa wa Mara.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumapili, Januari 21, 2018) katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Mara.

Alisema ukaguzi huo utakwenda sambamba na kufuatilia fedha wanazodai waliokuwa watumishi wa chama hicho.

“Kumekuwepo na matatizo makubwa ndani ya vyama vya ushirika kiasi cha kudumaza maendeleo ya wananchi.”

Pia Waziri Mkuu aliitaka mikoa yote ikomeshe matumizi ya vipimo visivyo rasmi kama butura na kangomba ili mkulima wapate tija.

“Vipimo hivyo ni vya kinyonyaji na vinamwibia mkulima na kuwanufaisha wafanyabiashara jambo ambalo si sahihi.”

Pia Waziri Mkuu aliziagiza Halmashauri zipunguze watumishi walio kwenye Makao Makuu ya Halmashauri na kuwapeleka maeneo ya vijijini ili wakawahudumie wananchi.

Alisema watumishi watakaobaki Makao makuu ya Halmashauri wanatakiwa nao waweke utaratibu wa usafiri ili kwenda vijijini kutatua kero za wananchi.

Kwa upande wa kilimo, aliagiza Maafisa Kilimo wote wapelekwe vijijini kuwahudumia wananchi na watakaobakia Ofisini ni Mkuu wa Idara, Afisa Bustani na Afisa Utafiti tu.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATATU, JANUARI 22, 2018.

USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA WAENDELEA BUTIAMA MKOANI MARA

0
0
Wananchi katika Wilaya ya Butiama mkoani Mara wameendelea kujitokeza kwa mamia kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa pamoja na changamoto ya umeme iliyopo kwa sasa katika kijiji cha Rwamkoma ambacho kwa sasa kinaendelea na hatua za Usajili.

Aidha wamepongeza Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kwa kuwajali na kuwasogezea huduma kwenye maeneo wanakoishi.Akizungumzia mwenendo wa zoezi hilo Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bw. Musa Luseke, amesema kuwa zoezi linakwenda vizuri na wananchi katika kijiji hicho kuendelea kujitokeza kwa wingi kusajiliwa na kutambulika. 

Kwa upande wake Afisa Usajili wa wilaya hiyo Bw. Paul Meela amesema kuwa zoezi la usajili kwa wilaya yake linatazamiwa kumalizika ifikapo katikati ya mwezi huu; na kuwataka wananchi katika Kata zote ambao bado kusajiliwa kujitokeza kwa wingi ili kumaliza zoezi kwa wakati.

Amewataka wananchi katika Kata ambazo Usajili umemamalizi kujitokeka kwa wingi kwenye zoezi la uhakiki wa taarifa na mapingamizi kwa wale ambao siyo Raia ili zoezi la kuandaa vitambulisho liweze kwenda kasi ili kuruhusu kuanza kwa matumizi ya Vitambulisho.
Baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Rwamkoma wakiwa katika kituo cha uandikishaji Vitambuisho vya Taifa wakishubiri kukamilisha zoezi la usajili.
Bw. Ezekiel Midamo (mwenye koti jeupe) mzazi wa Bw. Jared Ezekiel (anayejaza fomu) wakazi wa kijiji cha Rwamkoma, akimuelekeza kijana wake namna ya kujaza fomu wakati wa zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa katika Kata ya Butiama wilayani Butiama.
Baadhi ya akinamama wakazi wa kijiji cha Rwamkoma wakielekezana namna ya ujazaji wa fomu wakati wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa.
Bi. Dotto Wambura mkazi wa kijiji cha Rwamkoma akiwa katika hatua za kukamilisha zoezi la usajili kwa kuweka saini yake ya kielekroniki wakati wa zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa.
Afisa Usajili wilayani Butiama Bw. Paul Meena (katikati) akielekezana jambo na wasimamizi wa kituo cha kijiji cha Rwamkoma katika Kata ya Butiama. Kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha Rwankoma na kulia ni Afisa Mtendani wa kijiji cha Rwamkoma Bw. Musa Luseke.

HANANASIFU JOGGING WATOA MSAADA KWA YATIMA DAR

0
0

Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa wa Kawawa Kata ya Hananasifu Elizabeth Masao akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, katika hafla ya kukabidhi vya kula kwa watoto yatima wa Kituo cha Maunga Centre vilivyotolewa na kikundi cha Hananasifu Jogging Club Kinondoni.
Mwenyekiti wa Jogging Club Kinondoni Majani Mrope akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, katika hafla ya kukabidhi vya kula kwa watoto yatima wa Kituo cha Maunga Centre.
Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa wa Kawawa Kata ya Hananasifu Kinondoni Elizabeth Masao, akikabidhi baadhi ya vitu kwa mtoto anaelelewa na kituo cha yatima cha Maunga Centre Thabiti Amili, vilivyotolewa na kikunda cha Hananasifu Jogging Club Kinondoni.
Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa wa Kawawa Kata ya Hananasifu Kinondoni Elizabeth Masao, akikabidhi baadhi ya vitu kwa mtoto anaelelewa na kituo cha yatima cha Maunga Centre Thabiti Amili, vilivyotolewa na kikunda cha Hananasifu Jogging Club Kinondoni.
Baadhi ya wana kikundi cha Hananasifu Jogging Club Kinondoni, wakimkabidhi vitu.

DHAMANA KESI YA UHUJUMU UCHUMI KUJULIKANA FEBRUARI 5 MWAKA HUU

0
0
*Ni inayomhusu bosi meli ya Huihang 68 inayotuhumiwa kupeperusha bendera ya Tanzania bila kibali

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imesema Februari 5, mwaka huu, itatoa uamuzi dhidi ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabiki Mkurugenzi wa Kampuni ya Lucky Shipping Co.Ltd , Issa Haji( 39) na wenzake Abdallah Issa Hanga( 73), kama watapata dhamana au la.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa, amesema hayo leo baada ya upande wa utetezi kuwasilisha maombi mahakamani hapo wakitaka washtakiwa hao kupewa dhamana.Wakili wa utetezi, Dismas Raphael amewasilisha maombi hayo akipinga hati ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), aliyewasilisha hati ya kuzuia ya dhamana ya washtakiwa akidai hati hiyo ya haijafafanua ni kwa namna gani usalama na maslahi ya Taifa yatazurika endapo washtakiwa watapewa dhamana, hivyo wanahoji uhalali wa DPP kumnyima mtu dhamana bila kufafanua misingi yake.

Awali, wakili wa Serikali Simon Wankyo alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa wakipewa dhamana, wataingilia maslahi ya Taifa na kuiomba Mahakama ijielekeze katika suala hilo.Wakili Wankyo aliiomba Mahakama itupilie mbali hoja za upande wa utetezi kwa sababu hazina msingi.

Baada ya mabishano ya kisheria ya pande zote mbili, kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 5 Mwaka huu, kwa ajili ya uamuzi kama washtakiwa watapata dhamana au la.Washtakiwa wanadaiwa kujihusisha na mtandao wa uhalifu kinyume na sheria.

Katika hati ya mashtaka ilidaiwa, kati ya Julai 19,mwaka 2017 na Januari 16, mwaka 2018 jijini Dar es Salaam, walitoa ushauri, msaada na maelekezo katika kutenda kosa la jinai la mtandao wa uhalifu ambalo ni kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye meli iitwayo Huihang 68 zamani ilijulikana kama Greko 02, bila kuwa na hati ya usajili kutoka kwa msajili wa meli nchini kwa lengo la kujipatia faida kutoka katika shughuli za uvuvi haramu.

Pia kati ya Julai 19, mwaka jana na Januari 16, mwaka huu, washitakiwa hao huku wakifahamu kuwa ni kosa kisheria waliruhusu upeperushwaji wa bendera katika meli hiyo bila kuwa na leseni kutoka kwa msajili wa meli kwa lengo la kuifanya ionekane kuwa ya Tanzania wakati si kweli.

ISRAEL KUJENGA KITENGO CHA DHARULA NA TIBA YA MIFUPA MKOANI DODOMA

0
0

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

SERIKALI ya Tanzania imesaini makubaliano na Serikali ya Israel ya ujenzi wa kitengo cha dharula na tiba ya mifupo katika hospitali ya Benjamini mkoani Dodoma.

Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk.Otilia Gowelle amesema kuwa ujenzi wa kitengo hicho utasaidia katika utoaji wa huduma za afya zilizo bora.

Amesema kitengo hicho kitajengwa na Serikali ya Israel ikiwa ni pamoja na madaktari nchini kujengewa uwezo katika utoaji wa huduma katika kitengo hicho.Dk. Gowelle amesema kuwa ushirikiano uliopo kati ya Israel na Tanzania ni uhusiano imara katika kusaidia utoaji huduma katika sekta ya afya.
.Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Otilia Gowelle akisaini makubaliano na Naibu Balozi wa Israel Nchini, Michael Baror ya ujenzi wa kitengo cha dharula na tiba ya mifupa katika Hospitali ya Benjamini mkoani Dodoma, leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Otilia Gowelle akibadilishana hati ya makubaliano na Naibu Balozi wa Israel Nchini, ,Michael Baror ya ujenzi wa kitengo cha dharula na tiba ya mifupa katika Hospitali ya Benjamini mkoani Dodoma, leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Otilia Gowelle na Naibu Balozi wa Israel Nchini,Michael Baror pamoja na watendaji mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini makubaliano ya ujenzi wa kitengo cha dharula na tiba ya mifupa katika Hospitali ya Benjamini mkoani Dodoma, leo jijini Dar es Salaam.

NIDA YAFANIKISHA SHEREHE ZA MAULID,MWINYI AWATAKA WAISLAMU KUFUATA MAAGIZO YA MTUME

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Waumini wa dini ya kiislamu Tanzania wametakiwa kufuata mafunzo na maagizo ya Mtume ili kuweza kupata dhawabu mbele za Mwenyezi Mungu.

Hayo yamesemwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuber alipokuwa katika hafla ya Maulidi iliyoandaliwa na Kiwanda cha NIDA textile Mills|(T) ltd NAMERA GROUP OF INDUSTIES. amabapo amewataka Waumini wa dini hiyo kusikiliza na kufuata  maamulisho ya Mwenzi Mungu.
Amesema kufanya matendo mema ikiwa na kufanya maulid kunamfanya mwanadamu kupanda daraja kwa kile ambacho anakitoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Aidha amesema waislam wameasewa kufanya matendo mema ikiwa katika biashara kutoa katika kutafuta nafasi ya daraja kwa Mwenyezi Mungu.

Nae  Shekh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi pamoja na uongozi mzima wa kiwanda cha NIDA amesema hafla hiyo inafanyika kila mwaka na kwamba katika kufanya hivi kunasaidia amani ya nchi kuendelea kupatikana kwani katika kuadhimisha Maulidi hayo wanafanya maombi hasa ya kuombea taifa.

Aidha amewashukuru uongozi wa NIDA pamoja na kuwapongeza kuweza kuaanda Maulidi hayo kwani kwa kufanya hivyo wanawakumbusha waumini pamoja na watu wa dini zote kutenda mambo yatakayoleta Dhawabu  mbele za Mwenyezi Mungu.

Hafla hiyo imehudhuriwa na wageni mbalimbali Mgeni rasmi akiwa ni Mh. Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, alieambatana na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohammed Gharib Bilali , Waziri Ulinzi ,Dk. Hussein Mwinyi  pamoja Viongozi mbalimbali wa dini ya Kiislam.

Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuber akizungumza na waandishi habari katika mauli iliyoandaliwa na NIDA  Jijini Dar es Salaam.
"Nitoe wito kwa Waumini wa dini ya Kiislamu kufuata na kusikiliza kile anachokisema Mtume kwa sababu Mtume amefundisha mambo mbalimbali ambayo yana Maslaha kwa binadamu name ulimwengu wao hivyo yawapasa kuangalia Mtume amewafundisha nini Alisema
 Shekh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akizungumza katika maulid iliyoandaliwa na NIDA.
Mh. Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohammed Gharib Bilali na Viongozi mbalimbali wa dini ya Kiislam katika picha wakifurahia jambo .
Mkurugenzi wa Kiwanda cha NIDA Hamza Rafiq (KUSHOTO)akizungumza jambo na Meneja Mkuu wa NIDA , Muhammad Waseem.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha NIDA Hamza Rafiq akitoa Zawadi kwa Wageni mbalimbali.

UNNewsKiswahili:Watu 6 wauawa wakati wa maandamano DRC Congo

MAGAZETI YA JUMANNE LEO JANUARY 23,2017

UVCCM SIMANJIRO WAJINYANYUA KIUCHUMI

0
0
VIJANA wajasiriamali wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamefanikiwa kujinyanyua kiuchumi kwa kukusanya sh40 milioni, kupitia kikundi cha kuweka na kukopa (SACCOS) waliyoianzisha kwa vikundi 68 kujiunga nayo, kati ya vikundi 97 vya ujasiriamali vilivyosajiwa. 

Kati ya vikundi hivyo 68, vilivyojiunga na SACCOS, hadi sasa vikundi 12 vimepata mikopo, ambapo kila kikundi kina wanachama 30 sawa na watu 360 wameanza kunufaika kupitia sh40 milioni kwenye mikopo wanayokopeshana. 

Katibu wa UVCCM wilayani Simanjiro, Bakari Mwacha aliyasema hayo wakati akisoma taarifa ya wilaya hiyo kwa Mwenyekiti wa UVCCM wa mkoa wa Manyara Mosses Komba alipofanya ziara ya siku moja. Mwacha alisema kupitia SACCOS hiyo vijana hao wanachukua mikopo na kurudisha kwa wakati na uaminifu kupitia shughuli za ujasiriamali wanazozifanya. 

Alisema wanatoa ombi kwa halmashauri ya wilaya hiyo kutoa kipaumbele kwa vijana hao kuwapatia ile mikopo ya asilimia 5 ya mapato ya ndani kwani wataweza kuirejesha kwa wakati tofauti na vijana wengine. "Hawa wana uzoefu hata wakipewa mikopo inakuwa kwenye mikono salama tofauti na wengine ambao wakipewa wanasuasua kurejesha ila vijana wetu watakuwa na uhakika kwani wana SACCOS yao," alisema Mwacha 

Alisema vijana wengi wanajiunga na uanachama kwenye jumuiya hiyo ambapo hadi sasa wapo 9,205 na wengine wapya 139 wamejiunga mji mdogo wa Mirerani. Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Manyara, Mosses Komba aliupongeza uongozi wa UVCCM wilaya ya Simanjiro, kwa kusimamia ipasavyo vikundi hivyo hadi kupatikana kwa fedha hizo na kujinufaisha kiuchumi. 

"Mmekuwa mfano bora kwa vijana wa mkoa wa Manyara, kwani wilaya nyingine zinapaswa kuiga mfano wenu wa kuchangamkia fursa za kuongeza kipato," alisema Komba. Alisema baada ya kuwa na vikundi hivyo suala la kupatiwa mikopo na halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, litakuwa rahisi kwani ninyi mtakuwa na uzoefu wa kufanya ujasiriamali. 

Mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya ya Simanjiro, Thomas Mollel alisema atahakikisha anapigania upatikanaji wa asilimia tano ya mikopo kwenye halmashauri ya wilaya ili vijana wapate mikopo. Mollel alisema vijana wa Simanjiro wanapaswa kushirikiana kwa pamoja ili kujijenga kiuchumi na kujitolea nguvu kazi ili kutekeleza ilani ya CCM. 
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Manyara Mosses Komba akipokewa na wanachama wa CCM wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro alipoanza ziara yake ya siku moja. 
Viewing all 109583 articles
Browse latest View live




Latest Images