Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110079 articles
Browse latest View live

Kamal Group brings New-Year smiles to hundreds in artificial limb project

$
0
0
Dar es Salaam. Over 100 people, who lost their limbs in various accidents, will now be able to walk again, thanks to a multi-million shilling initiative by the Dar es Salaam-based Kamal Group guided by India’s Bharat Vikas Parishad.

Through their Peoples’ Empowerment Foundation (PEF), institutions donated 108 artificial limbs to some Dar es Salaam residents at the weekend during a brief event that was graced by the Deputy Minister of State in the Prime Minister’s Office (Policy, Parliamentary Affairs, Labour, Employment and Youth and the Disabled), Mr Anthony Mavunde.

“I don’t have anything to give back to Kamal Group but allow me to say, I am extremely delighted because after nine years, I will now be able to walk again,” said Ms Mwanaisha Mohammed.

Speaking during the event, the Kamal Group chairman, Mr Gagan Gupta said it was basing on its philosophy of growing with the community that the company launched the initiative of helping the people with disabilities three years ago.

“We have set up a special unit that manufactures these artificial limbs at Kamal Steel as a way of cutting costs associated with the making of the products….We are doing this for the third year and we will continue doing so,” he said, thanking the Dar es Salaam Regional Commissioner, Mr Paul Makonda for bringing the disabled people together so they could get the limbs

In his remarks, Mr Mavunde acknowledged the wonderful contribution of PEF and Kamal Group to Tanzania’s social economic development and urged other companies to emulate.

“Through this Kamal Group is showing us that it is a good corporate citizen. If every company can emulate this, we in government will be happy with them. This will then give us an impetus to further improve the business climate,” he said.

He said the government will meet with Kamal Group officials with a view to designing the best way to ensure that the artificial limb project reaches all the needy Tanzanians across the country. Available data (help me with the source in line with your video clip) at least 3.6 million Tanzanians have various forms of disabilities. Out of the number, some 1.7 million have disabled parts, including limbs and arms among others.

Howver, data from the Tanzania Association of the Disabled, show that it is only about 20 per cent who can actually get access artificial body parts such as limbs. To access an artificial limb in a hospitals, one needs up to Sh3 million.
Some of the disabled people celebrate after they received artificial limbs from the Dar es Salaam-based Kamal Group during a brief event that was held at the weekend. The Deputy Minister of State in the Prime Minister’s Office (Policy, Parliamentary Affairs, Labour, Employment and Youth and the Disabled), Mr Anthony Mavunde (not in the picture) graced the event.
The Deputy Minister of State in the Prime Minister’s Office (Policy, Parliamentary Affairs, Labour, Employment and Youth and the Disabled), Mr Anthony Mavunde (centre) presents an artificial limb to Ms Mwanaisha Mohammed during an event where the Dar es Salaam-based Kamal Group donated a total of 108 artificial limbs to the disabled people in the city at the weekend. From left is: a lecturer from Mzumbe University Dar es Salaam Campus, Dr Coretha Komba, a Kamal Group director, Mr Satyam Gupta, Kamal Group founder, Mr Santosh Gupta, Kamal Group chairman, Mr Gagan Gupta and director, Mr Sameer Gupta.
A cross section of people with disabilities try their artificial limbs shortly after they were donated to them by the Dar es Salaam-based Kamal Group during a brief event that was graced by the Deputy Minister of State in the Prime Minister’s Office (Policy, Parliamentary Affairs, Labour, Employment and Youth and the Disabled), Mr Anthony Mavunde (not in the picture) during the weekend.

MICHUZI TV: RC MAKONDA KUKUTANA NA WANANCHI WA DAR

MICHUZI TV: EXCLUSIVE INTERVIEW NA RAYVANNY...

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 22, 2018

BABU SEYA NA PAPII KOCHA WAANZA MAANDALIZI YA UJIO WAO MPYA

$
0
0
​Muimbaji nguli wa muziki wa dance, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya pamoja na mwanae, Papii Kocha wameanza maandalizi ya ujio wao mpya, ikiwa ni takriban miaka 14 tangu waachie kibao kipya.

Wawili hao walipewa msamaha na Rais Dkt John Magufuli kwenye maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru. Serikali imeonesha nia ya kuwasaidia waimbaji hao wanaopendwa sana kurejea tena kwenye muziki kwa kishindo.

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Bi. Juliana Shonza aliwakutanisha na uongozi wa Wanene Studios waliokubali kuchukua jukumu la kuwarudisha tena kwenye muziki. Tayari wameanza kuingia studio kuandaa kazi mpya katika studio hizo kubwa na bora zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Wameanza kwa kufanya photoshoot, kitu ambacho wamekiri kuwa ni kigeni mno kwao kutokana na kuwa gerezani kwa miaka 14 na wametoka katika nyakati ambazo muziki wa Tanzania umepiga hatua kubwa ukilinganisha na zamani.

“Miaka 14 si mchezo, mambo kama haya si unayaona mwenyewe, niliyamiss, nimemiss vitu vingi, picha za ukweli, mambo haya kule tulipotoka hamna. Lazima uelewe hii ni dunia nyingine,” alisema Papii Kocha wakati wa photoshoot.

Kwa kujiamini, Papii amesema kuwa kazi zao mpya zitakuwa kali zaidi ya zile za zamani. “Kwasababu tumejipanga vizuri na kazi zinazokuja zitakuwa nzuri zaidi ya zile tulizofanya mwanzo,” amesisitiza Papii.

Kwenye photoshoot hiyo iliyofanywa na mpiga picha mahiri Eric Luga, Babu Seya na Papii Kocha walivalishwa na mbunifu wa mavazi, Mtani Nyamakababi.

Unaweza kufuatilia kila hatua ya safari yao kuelekea kuachia kazi mpya kwa kulike ukurasa wao rasmi wa Instagram@babanamwana, Facebook: baba na mwana. Pia subscribe kwenye channel yao ya Youtube iitwayo Baba na Mwana kuona video mbalimbali za behind the scenes.
​​​​​​​​​​​​​​​
Unaweza kuangalia video ya behind the scenes ya upigaji picha kwa kufuata link hii >> https://youtu.be/h-Kdp87now4

Rais Dk. Shein Awasili Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu Kuanza Ziara Yake

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Kiongozi wa Ngazi za Juu wa nchi za Umoja wa nchi za Falme za Kiarabu( UAE) Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai, kuanza ziara yake ya wiki moja kulia ni Balozi wa Tanzania Katika Nchi za Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Kiongozi wa Ngazi za Juu wa nchi za Umoja wa nchi za Falme za Kiarabu( UAE) Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai kuanza ziara yake ya Wiki moja.(Picha na Ikulu)MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Mke wa Balozi wa Tanzania katika Nchi za Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Kiongozi wa ngazi za Juu wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi,alipowasili katika Uwanja waNdege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai kuaza ziara yake ya Kiserikali ya Wiki moja. kushoto Balozi wa Tanzania katika Nchi za Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu (UAE) Mbarouk Nassor Mbarouk(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Kiongozi wa Juu wa Umoja wa Nchi za Falme za Nchi za Kiarabu (UAE) Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi, alipowaili katka Uwanja waNdege wa Kimataifa wa Al Maljis Dubai kuaza ziara yake ya Wiki moja, kushoto Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohammed.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Juu wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai.

RC LUHUMBI ATANGAZA KIAMA KWA WAZAZI NA WALEZI WALIOGOMA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE

$
0
0
Na,Joel Maduka,Geita

Serikali mkoani Geita imetangaza oparesheni ya kuwafuatilia wazazi na walezi ambao watoto wao walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na kwamba hadi sasa bado awajawapelekwa shuleni na pindi watakapobainika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria .

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Geita Robert Gabriel wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa kwa seekondari hali sio nzuri ya wanafunzi ambao wametakiwa kuingia kidato cha kwanza kwani hadi sasa asilimia 46 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza hawajaripoti shuleni. 

Luhumbi ameongezea kwamba suala la elimu ni haki ya mtoto na hayupo tayari kuona wazazi wanawaozesha ama kuwaajiri kwenye shughuli za migodi na biashara ndogondogo watoto ambao wanaumri wa kwenda shule na wamefaulu mtihani wa darasa la saba.

Ameendelea kusema anafuatilia taarifa ya walimu ambao wameonekana kuwa ni kikwaza kwa kuchangisha fedha na kwamba endapo wakibaini hatua kali zitachukuliwa na kwamba amesikia kuna baadhi ya shule walimu wameendelea kuwatoza fedha wanafunzi kinyume na sheria.katika mtihani wa darasa la saba mwaka jana wanafunzi 32,110 walifaulu na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu lakini hadi kufikia tarehe 18 janaury mwaka huu wameripoti wanafunzi 17,202 sawa na asilimia 54 .

Kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na idara ya elimu mkoa inaonyesha wilaya ya Bukombe walichaguliwa wanafunzi 3,985 na hadi sasa wameripoti 1,620 sawa na asilimia 41,Chato walichaguliwa 6,449 walioripoti ni 3,691 sawa na asilimia 57,Geita mji walichaguliwa 4,286 walioripoti ni 2,751,sawa na asilimia 64 huku Mbogwe waliochaguliwa ni 3,029 walioripoti ni 1,924 sawa na asilimia 64.

Halmashauri ya Geita vijijini wanafunzi 11,760 walichaguliwa kujiunga kidato cha kwanza lakini hadi sasa wameripoti wanafunzi 5,872 ambayo ni sawa na asilimia 50,wilaya ya Nyanghwale 2,601 walioripoti ni 1,344 sawa na asilimia 52.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akizungumza na waandishi wa habari na baaadhi ya wakuu wa idara mbali mbali pamoja na kati ya ulinzi na usalama ya Mkoa huo wakati alipokuwa akielezea mikakati ya Mkoa huo na shughuli ambazo zimefanyiika. 
Baadhi ya wakuu wa idara pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wakati alipokuwa akizungumza na kuelezea mikakati iliyopo mkoani humo. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiwashukuru wananchi ambao wamekuwa wakijitoa kuunga juhudi za serikali za kuhakikisha kila eneo linatatuliwa changamoto zake. 


TAMASHA LA BUSARA KUENZI SANAA NA UTAMADUNI WA MWAFRIKA

$
0
0
. Watanzania wametakiwa kuenzi sanaa na utamaduni waliona kwa ajili ya kizazi kijacho ili kukijendea uzalendo wa kupenda nchi yao. 

Hayo yamesema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud wakati akielezea ujio wa Tamasha la 15 linalotarajiwa kufanyika Ngome Kongwe, Unguja - Zanzibar kwa kushirikisha wanamuziki na vikundi mbali mbali vya sanaa kutoka pande zote za bara la Afrika na Ulaya.

 “Katika Tamasha hili, ni sehemu ambapo watu wenye weledi wa sanaa mbalimbali hukutana, kuanzia kwa wakurugenzi wa matamasha mpaka kwa wazalishaji wa muziki, mameneja wa wanamuziki, wasambazaji wa muziki, wote hawa huja hapa Zanzibar mwezi Februari kuja kushuhudia utamu wa midundo ya muziki wa Ukanda wa Afrika Mashariki,” anasema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud.

Anaongeza kuwa, “Hili siyo tu tukio ambalo watumbuizaji wa Tamasha pekee huhudhuria, bali hata baadhi ya wanamuziki ambao hawapo katika orodha ya kutumbuiza huja kwa minajili ya kujifunza kutoka kwa wale wanaofanya maonesho mbalimbali, na pia hupata fursa ya kufahamiana na wadau muhimu wa tasnia yao na kutengeneza mahusiano ya kikazi kwa miezi ijayo, hata zaidi ya hapo baada ya tamasha kuisha.” Likisifika kuwa miongoni mwa matamasha yanayoheshimika, Sauti za Busara likiwa na kauli mbiu ya “Kuunganishwa na Muziki” kwa mwaka huu, linawakutanisha pamoja zaidi ya wanamuziki 460 katika visiwa vya Zanzibar.

Likiwa ni tamasha ambalo limeshuhudia ukuaji mkubwa katika uadhimishwaji wake na mwaka huu ukiwa wa 15, Tamasha hili linavutia wataalamu wa habari na muziki kutoka katika kila pembe ya Afrika, Ulaya na mahali pengine, ambapo hutoa jukwaa la kipekee kwa wanamuziki wa Afrika Mashariki kuutanganza muziki wao duniani.


WANACHAMA 139 WA CHADEMA SIMANJIRO WAJIUNGA NA CCM

$
0
0
WANACHAMA 139 wa Chadema wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, wamejiunga na CCM na kupokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM wa Mkoa wa Manyara Mosses Komba. 

Akizungumza wakati wa kuwapokea na kuwakabidhi kadi za CCM wanachama hao wapya, Komba alisema wamefanya uamuzi sahihi kwa wakati sahihi. Komba alisema hawatajuta kujiunga na CCM kwani hivi sasa chama hicho kinachoongozwa na Mwenyekiti wake Rais John Magufuli kinawatumikia wananchi kwa kutatua kero na kuufanikisha maendeleo. 

Alisema wanakaribishwa CCM kwa moyo mmoja hivyo washirikiane na wanachama wengine ili kuhakikisha wanalirudisha jimbo hilo na kata sita zinazotawaliwa na Chadema. "Kati ya makosa tuliyofanya kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ni kuachia jimbo la Simanjiro liende Chadema na kata za Mirerani, Naberera, Loiborsiret, Ruvu Remit, Loiborsoit na Endiamtu zichukuliwe na wapinzani," alisema Komba. 

Alisema ushabiki wa kufuata mkumbo ndiyo uliowagharimu wananchi wa wilaya hiyo na kata hizo, hadi kusababisha wakapatikana madiwani na mbunge wa kutoka upinzani badala ya CCM."Nakuagiza Mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya ya Simanjiro, Thomas Mollel na wenyeviti UVCCM wa kata husika ambazo madiwani wao ni wapinzani, mkishindwa tena 2020 mjiuzulu," alisema Komba. 

Serikali yatoa Msimamo wake kwa Klabu ya Simba kuhusu suala la uwekezaji

$
0
0
Na Anitha Jonas – WHUSM

Serikali imetoa msisitizo kwa Klabu ya Mchezo ya Simba kuzingatia sheria na kanuni zinayosimamia suala la uwekezaji kwa Klabu zilizoanzishwa na wanachama ambapo wanachama wanachukua 51% na mwekezaji anachukua 49%.

Msisitizo huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokutana na uongozi wa Klabu ya Simba na kuzungumza nao kufuatia kutoa asilimia 50% kwa mwekezaji wa klabu hiyo Bw.Mohamed Dewji waliyemtanganza hivi karibuni ambapo ni kinyume na sheria.

“Kanuni zinazosimamia masuala ya udhamini kwa vilabu zilifanyiwa marekebisho Novemba 2017 kwa ambapo ilioneka ni vyema klabu za michezo zilizoanzishwa na wanachama wanapopata muwekezaji basi mwekezaji achukue 49% na wanachama kutoka na mchango wao kwa mkubwa kwa klabu hiyo basi wapewe 51% lengo ikiwa ni mwanachama aweze kunufaika vizuri,”Dkt.Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari Mheshimiwa Mwakyembe alisema kuwa serikali ya awamu ya tano hajaja kuuwa michezo bali lengo lake ni kuboresha michezo na kuifanya kuwa na tija zaidi pamoja na kuleta maendeleo endelevu katika sekta hiyo.

Naye Katibu wa Baraza la Michezo Taifa Bw.Mohamed Kiganga alieleza kuwa ofisi yake ipo katika maandalizi ya kuwaandikia barua Klabu ya Simba ya wapamsisitizo wa Serikali katika kuzingatia sheria katika suala la udhamini na barua hiyo itawafikia wiki ijayo.

Kwa Upande wa Kaimu Rais wa Klabu ya Simba Bw.Salim Abdallah alieleza vyombo vya habari kuwa wanashukuru serikali kwa kuwaeleza kuwa milango iko wazi pale watakapo kuwa na tatizo au watakapo hitaji ushauri wanaweza kuonana na watendaji wake.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akieleza waandishi wa habari (hawapo pichani) msimamo wa serikali kwa Klabu ya Michezo ya Simba kuhusu suala la uwekezaji kwa vyama vya michezo vilivyoanzishwa na wanachama kwa kuzingatia wa sheria kuwa ni 49% kwa mwekezaji na 51% kwa wanachama kufuatia kutangaza kumpa mwekezaji wao 50% hivi karibuni kinyume na kanuni jana jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Kaimu Rais wa Klabu ya Michezo ya Simba Bw.Salim Abdallah na Katikati ni Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja.
Kaimu Rais wa Klabu ya Michezo ya Simba Bw. Salim Abdallah akieleza waandishi habari (hawapo pichani) kuwa msimamo wa serikali wameuelewa na watakwenda kuzungumza na mwekezaji wao Mohamed Dewji kuhusu kumpunguzia 1% na kumpa 49% badala ya 50% waliyokuwa wametangaza hivi karibuni kumpa jana jijini Dar es Salaam,pembeni yake ni Mwanasheria wa Klabu ya Michezo ya Simba Bw.Evodius Mtawala.

SIMANJIRO YAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BILIONI 25.3

$
0
0
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamepitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya shilingi bilioni 25.3 kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019. 

Akizungumza baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Jackson Sipitieck alisema vipaumbele vya bajeti hiyo ni elimu, afya, maji na viwanda. 

Sipitieck alisema suala la kupitishwa kwa bajeti ni jambo moja na utekelezaji ni jambo lingine, hivyo kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake ipasavyo wakiwemo madiwani na watumishi, ili kufanikisha hilo. Alisema kila mmoja kwa nafasi yake akisimama kwa nguvu zote, wilaya ya Simanjiro itapiga hatua kubwa ya maendeleo na wananchi wake watakuwa wanapata huduma zao za kijamii kwa ufanisi mkubwa zaidi. 

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi alisema bajeti hiyo ni kwa ajili ya matumizi mbalimbali, ikiwemo miradi ya maendeleo, ruzuku ya uendeshaji ofisi na mishahara. Myenzi alisema wilaya hiyo imeweka mikakati ya kuhakikisha wanaboresha vipaumbele vyao vya elimu, afya, maji na viwanda. Alisema mazao ya mifugo, ikiwemo maziwa, ngozi na nyama inapaswa kuboreshwa ili iwe chachu ya vichocheo vya uchumi. 

Katibu Tawala wa wilaya ya Simanjiro Zuwena Omary aliwapongeza madiwani wa halmashauri hiyo kwa kupitisha mpango huo wa bajeti ya mwaka 2018/2019 kwa manufaa ya wananchi. "Pamoja na hayo tunapaswa kuhakikisha tunatekeleza agizo la kila mkoa kuwa na viwanda 100 kwa sisi Simanjiro kuanzisha viwanda 15 ambayo vitasambazwa kwenye kata zetu na vijiji," alisema Omary. 

Hata hivyo, Diwani wa Kata ya Komolo, Michael Haiyo aliipongeza bajeti hiyo na kusisitiza ikamilishwe kwa vitendo. Haiyo alisema bajeti hiyo imegawanywa bila upendeleo kwani kata zote zimepatiwa miradi ila umuhimu wake utaoneka endapo itatekelezwa kwa vitendo. Diwani wa kata ya Naisinyai, Kilempu Ole Kinoka alisema bajeti hiyo inapaswa kujali suala zima la uboreshaji wa mifugo kwani asilimia kubwa ya wananchi wa eneo hilo ni wafugaji. 

"Sisi kwetu kahawa ya Simanjiro ni mifugo ambayo ni roho ya uchumi, hivyo tunapaswa kulizingatia hilo kwenye utekelezaji wa bajeti yetu," alisema Ole Kinoka.
Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Leskar Sipitieck akizungumza kwenye kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo baada ya kupitisha mpango wa bajeti ya shilingi bilioni 25.3 kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 kushoto ni Makamu Mwenyekiti Albert Msole na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Zuwena Omary na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Yefred Myenzi. 

WAZIRI ULEGA AONGOZA KUTEKETEZA NYAVU HARAMU ZA MAMILIONI MWALO WA IGOMBE MKOANI MWANZA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla Hamisi Ulega jana ameongoza shughuli ya kuziteketeza nyavu haramu zenye thamani ya jumla ya shilingi Milioni 400 katika Mwalo wa Igombe,mkoani Mwanza.

Akihutubia umati mkubwa wa wakazi waliohudhuria katika shughuli hiyo ya uchomaji nyavu hizo,Mhe.Ulega alsema kuwa rasilimali za uvuvi ni muhimu zitunzwe, Ili ziweze kulisaidia Taifa na wala sio kukineemesha/nufaisha kikundi cha watu wachache.

Ameutaka uongozi wa Manispaa kutumia BMUs katika kukusanya maduhuri yatokanayo na samaki na Mazao yake.Aidha Mhe.Ulega ameutaka uongozi wa manispaa kuhakikisha hawawi sehemu ya Uvuvi uharamu.


"Viongozi wa Serikali za mitaa wapo hapa,kwa nini hamzuii Uvuvi haramu,au na ninyi ni sehemu ya uvuvi haramu?inamaana hamuoni haya mpaka Rais anatutuma sisi tuje hapa".alihoji Ulega.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega (wa kwanza kulia) akiongoza shughuli ya kuteketeza nyavu haramu zenye thamani ya jumla ya shilingi Milioni 400 zilizo salimishwa na wavuvi wa mwalo wa Igombe mkoa wa Mwanza.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega akizungumza na wanachi wa mwalo wa Igombe mkoa wa Mwanza kabla ya kuteketeza  nyavu haramu zenye thamani ya jumla ya shilingi Milioni  400 zilizo salimishwa na wavuvi.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega akiwa ameongonzana na watumishi wa mkoa wa Mwanza wakiwasili katika kiwanda cha Tanzania Fish Processors (TFP) mkoa wa Mwanza.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega akipima urefu samaki kwa kutumia kipimo cha kisasa chenye urefu wa sentimita 50-85 kilicho ruhusiwa kisheria




WAZIRI MKUCHIKA AFURAHISHWA NA MAENDELEO YA TPSC TAWI LA MBEYA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika (katikati) akipatiwa maelezo juu maendeleo ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Mbeya kutoka kwa Mkurugenzi wa tawi hilo Dkt. Heriel Nguvava ,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika.Waziri alitembelea tawi hilo mwishoni mwa wiki ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kuyatembelea matawi ya TPSC.TPSC ina matawi sita.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi wa tawi la Mbeya wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt Heriel Nguvava (kulia) wakati Waziri alipotembelea tawi hilo mwishoni mwa wiki ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kuyatembelea matawi ya TPSC, TPSC ina matawi sita, kushoto ni Mkuu wa TPSC Dkt. Henry Mambo 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika kulia akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa tawi la Mbeya wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt Heriel Nguvava wakati Waziri huyo alipotembelea tawi hilo mwishoni mwa wiki ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kuyatembelea matawi ya TPSC, TPSC ina matawi sita 
Mfanyakazi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Mbeya Nuhuman Iddy akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika wakati Waziri huyo alipotembelea tawi hilo mwishoni mwa wiki ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kuyatembelea matawi ya TPSC, TPSC ina matawi sita 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika (katikati aliyekaa mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Mbeya, kulia kwake ni Mkuu wa TPSC Dkt. Henry Mambo , wengine ni viongozi waandamizi wa mkoa wa Mbeya 

Makete: Diwani apanga kwenda kwa Waziri Lukuvi

$
0
0

Diwani wa kata ya Mbalatse Wilayani Makete Mkoani Njombe (CHADEMA) Edson Msigwa amesema wanampango wa kwenda kumuona Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi awasaidie kutatua matatizo ya ardhi yaliyopo katika Kata hiyo

Katika Mahojiano Maalum na Eddy Blog, Diwani huyo ameelezea mengi, mtazame kwenye hiyo video kwa kubonyeza play hapo chini

MBUNGE WA CHALINZE MH. RIDHIWANI KIKWETE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI KWAKE

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Shedeli Mikole Mwenyekiti wa CCM kata ya Vigwaza wakati akiwa katika ziara ya kikazi kukagua huduma za maendeleo na miradi mbalimbali inayotekelezwa jimboni humo, Mh. Ridhiwan Kikwete ametembelea kata na vijiji vya Visezi, Buyuni , kata ya Vigwaza. na Magulumatari, Kisanga Kata ya Talawanda, Bago na Msinune kata ya Kiwangwa.
Sehemu ya Bidhaa zinazotengenezwa na vikundi vya Kimaendeleo. Kikundi cha Jipe Moyo ambacho ni moja kati ya vikundi vilivyofaidika na fursa za Mitaji Katika Halmashauri na Mfuko wa Jimbo ambao upo chini ya Mbunge wa Chalinze wakionyesha kazi zinazotokana na Mikono yao mbele ya Mbunge.
Mmoja wa wananchi akizungumza mbele ya Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze .
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikagua Nguzo za umeme zipatazo 60 katika Kijiji cha Visezi. ambazo zipo hapo toka mwaka 2015 sasa ni miaka miwili toka Zilipoletwa hadi leo hazijaunganishwa. Serikali kupitia mradi wa Peri-Urban Enlightment Initiative watakuja waunganishia wananchi wa Visezi.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano wa Mh. Ridhiwani Kikwete Mbunge wa jimbo la Chalinze.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AHITIMISHA ZIARA YA MKOA WA MARA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua mabweni mawili ya Magufuli na Majaliwa katika Shule ya Sekondari ya Bumagi wilayani Butiama Januari 20, 2018. Watatu kulia ni mkewe Mary.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi baada ya kuzindua mabweni mawili yaliyopewa majina ya Magufuli na Majaliwa katika shule ya Secondari ya Bumagi wilayani Butiama Januari 20, 2018. Wapili kushoto ni mkewe Mary.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mbuge wa Butiama, Nimrod Mkono cheti cha shukurani kilichotolewa na wilaya ya Butiama ili kuthami mchango wake mkubwa wa kujenga na kuchangia maendeleo ya elimu wilayani humo. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Chuo Kikuu cha Julius Kambarage Nyerere kilichojengwa na mbunge huyo kikiwa na sekonda na kutokana na ubora wake kilibadilishwa kuwa Chuo Kikuu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhungo katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye kijiji cha Muragi Januari 21, 2018.

Timu mbili zaidi zaongezeka kuwania taji la Taifa la mashindano ya kuogelea ya yoso

$
0
0
Timu mbili zaidi zimethibisha zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya taifa ya kuogelea kwa vijana wa umri  kuanzia miaka  saba mpaka 14 yaliyopangwa kuanza Ijumaa (Januari 26) na kumalizikia Jumamosi (Januari 27).


Timu hizo ni Mwanza Swim Club na Isamilo kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa klabu ya Dar Swim Club (DSC), Inviolata Itatiro. Klabu hizo zinaungana na Bluefins, Arusha Swim Club, Shule ya Kimataifa ya Moshi, na Champion Rise.


Vilabu vingine kwa mujibu wa Inviolata ni Taliss, Hopac, Wahoo ya Zanzibar, Kennedy House, Shule ya Kimataifa ya Morogoro na wenyeji, DSC. Inviolata alisema kuwa,  Kisima Water, Knight Support,    Coca-Cola,  Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), Label Promotions, Print Galore Ltd na kituo cha televisheni cha ITV wamejitokeza kudhamini mashindano hayo.
Alisema kuwa bado wanaendelea kutafuta wadhamini ili kufanikisha mashindano hayo yenye lengo la kuendeleza mchezo wa kuogelea nchini na hasa waogeleaji chipukizi ambao ni nguzo ya nchi katika mashindano yajayo ya kimataifa.


“Maandalizi yanaendelea na kwa sasa tunaomba wadhamini watusaidie kufanikisha mashindano haya, ni mashindano ya vijana wadogo ambao wanahitaji kuona kila kitu kinakuwa sawa, ni muhimu kupata msaada kutoka kwa wadau na makampuni,” alisema Inviolata.



Alisema kuwa klabu yake inaandaa mashindano hayo kwa mara ya pili na mafanikio yameanza kuonekana kwani kuna waogeleaji wengi chipukizi wameanza kuwa tishio katika mashindano ya Taifa. Alifafanua kuwa wamepewa kibali na Chama Cha Kuogelea Nchini (TSA) kufanya mashindano hayo  ambayo awali yalikuwa ya ngazi ya vilabu kabla ya kupasishwa kuwa ya kitaifa.
waogeleaji chipukizi wakijifua

Airtel FURSA: zaidi ya vijana 10,000 wajiandikisha kusoma kupitia VSOMO

$
0
0
Meneja Miradi Airtel Tanzania Jane Matinde akizungumza wakati wa semina kwa vijana kuhusu umuhimu wa kusoma kwa kutumia mtandao kupitia aplikesheni ya VISOMO inayotumiwa na VETA kwa kushirikiana na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel katika makao makuu ya kampuni hiyo Morocco, Dar es Salaam.
Takribani wanafunzi 10,000 tayari wameshajiandikisha na masomo ya ufundi ya VETA kupitia application ya VSOMO  ili kusoma kozi mbalimbali za ufundi nchini. Mafunzo hayo ya ufundi ya VSOMO yanapatikana kupitia simu za mkononi kwa ushirikiano kati ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na mamlaka ya mafunzo ya ufundi stadi (VETA)  yamekuwa nikichocheo kikubwa katika upatikanaji wa elimu kwa njia ya mtandao na kuongeza idadi ya wanafunzi wanataraji na wanaosoma masomo ya ufundi katika nyanja mbalimbali nchini.

 Akiongea jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu program hiyo, Kaimu Mkuu wa chuo cha ufundi cha VETA kipawa, BwanaHarold Mganga alisema “ mafunzo ya ufundi ya muda mfupi yamekuwa yakitolewa na katika vyuo cha VETA kwa miaka mingi na hivyo idadi ya wanafunzi kuongezeka kila mwaka,  kwa kuliona hilo VETA tukaona ni vyema kutanua wigo kwa kushirikiana na Airtel ili kutoa mafunzo haya kwa njia ya mtandao ili kuwawezesha vijana katika maeneo mbalimbali hususani maeneo ya pembezo au walio katika shughuli zao za kazi  kupata nafasi ya kusoma masomo ya nadharia kupitia simu zao mahali popote wakati wotote kisha kufanya mafunzo ya vitendo katika vyuo vyetu vya VETA mara baada ya kafaulu mitihani yao.  Najisikia fahari kusema kuwa ushirikiano wetu na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel umekuwa na tija kubwa katika kuwafikishia watanzania wote mafunzo haya kwa urahisi na ufanisi mahali popote nchini.

 Mpaka sasa wanafunzi 9975 wamejiandikisha kupata mafunzo haya na Zaidi ya watanzania elfu 33 wameshapakuwa application ya VSOMO kupitia simu zao za mkononi. Kwetu sisi haya ni mafanikio makubwa na tuaamini kuwa mapinduzi haya ya elimu kupitia mtandao ndio yatakayoleta tija na kutuwezesha kuwa na nguvukazi yenye uledi ili kwenda sambamba na mahitaji ya nchi katika kufikia uchumi wa viwanda kwani nguvukazi ni moja kati ya nguzo muhimu katika kuendesha viwanda hivyo.

 Kwa upande wake Meneja Mradi wa VSOMO Airtel, Bi Jane Matinde alisema “ Tunayo mikakati mingi mwaka huu itakayowezesha watanzania wengi hususani vijana kuvutiwa na kujiunga na masomo haya ikiwemo kuongeza idadi ya kozi, kutoa elimu kwa uma juu ya upatikanaji wamasomo haya, kuboresha namba yetu ya kituo cha simu cha VSOMO ya 0699859573 na0699859572  na masaa ya kupata huduma na vilevile  kutanua wigo wa upatikanaji wa huduma hii na kuboresha malipo ya ada pamoja na mikakati mingi zaidi.

 Lakini  pia mkakati tulionao mpaka kufikia mwezi wa februari mwisho mwaka huu  tutazindua kozi tano mpya  ambazo ni pamoja na kozi ya usafi, kutengeneza Keki,  kuoka mikate, ufugaji wa kuku pamoja na upambaji wamaua. Mpaka sasa tunazo kozi kumi na moja ambazo tayari tumeshazizindua na zinapatikana katika application hiyo ya VSOMO ambazo ni pamoja na kozi ya Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta,umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani, Umeme wa magari, kutengeneza na kupamba keki, ufundi wa simu, ufundi pikipiki, Utaalamu saluni na urembo, ufuni wa kuchomelea pamoja na ufundi wa Aluminium.. 

Tunaamini upatikanaji wa kozi mbalimbali kutawezesha watanzania wengi kujiunga na kusoma masomo haya na kutanua wigo wa wanafunzi wengi zaidi kusoma na kupata vyeti kila mwaka. Tunatoa wito kwa vijana , wazazi na walezi kutumia mfumo huu kujiendeleza nakupata ujuzi zaidi aliongeza Matinde

 Mpaka sasa mikoa minayoongeza kwa kuwa na mwitikio mkubwa wa wanafunzi kujiandikisha ni pamoja na Dar es saalam, Mwanza , Arusha, Morogoro na Dodoma huku vijana toka mikoa 26 nchini wamejiandikisha na mafunzo haya.

WAJASILIAMALI WATAKIWA KUTUMIA MAFUNZO YA SIDO KIKAMILIFU

$
0
0
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Lyana akiongea na wajasiliamali mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akifunga mafunzo yaliyokuwa yameandaliwa na SIDO jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuwajengea uwezo na kuzipa thamani bidhaa wanazozitengeza. Pembeni yake ni Meneja wa SIDO Dar es Salaam, McDonald Maganga. Picha na Cathbert Kajuna -KAJUNASON/MMG.
Meneja wa SIDO Dar es Salaam, McDonald Maganga akitolea ufafanuzi mafunzo hayo ambayo wamekuwa wakiyatoa kwa wajasiliamali mbali mbali ili kuwajengea uwezo wa kuzipa thamani bidhaa zao wanazozitengeneza. Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Lyana (wa nne kutoka kushoto) na Meneja wa SIDO Dar es Salaam, McDonald Maganga anayemfuatia wakifurahia jambo na wajasiliamali mara baada ya kuhudhuria sherehe ya kufunga kwa mafunzo yao.

BREAKING: Salum Njwete "Scorpion" atupwa gerezani miaka Saba na kutakiwa kumlipa aliyemjeruhi fidia ya Sh. milioni 30

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii
Mahakama ya wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imemuhukumu Mwalimu wa Sanaa ya kujihami, 'Martial arts' Salum Njwete maarufu kama Scorpion, kutumikia kifungo cha miaka saba gerezani na fidia ya sh. Milioni thelathini ambayo anatakiwa haraka iwekenavyo.
Hukumu hiyo imesomwa baada ya Scorpion kupatikana na hatia katika kesi ya kujeruhi ikiwemo kumtoboa macho kinyozi Said Mrisho na kuachiwa huru kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.
Hukumu dhidi ya Njwete ambaye pia ni msanii wa filamu za kibongo na mshindi wa shindano la Dume Challenge ambapo alijinyakulia kitita cha milioni 20 imesomwa na Hakimu Mkazi Wa mahakama hiyo Flora Haule.
Salum Njwete maarufu kama "Scorpion"  akitolewa mahakamani leo mara baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya kujeruhi ikiwemo kumtoboa macho kinyozi Said Mrisho leo kwenye mahakama ya Ilala jijini Dar es Salaam. Picha na Mudy wa Blogu ya Jamii
 Said Mrisho(aliyevaa miwani) akitoka mahakamani leo mara baada ya hukumu kutolewa leo.

Viewing all 110079 articles
Browse latest View live




Latest Images