Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

Sekta Ya Habari Ina Wajibu Wa Kupongeza Mafanikio Ya Serikali: Dkt. Abbas

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA

Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO Dkt. Hassan Abbas amesema Sekta ya habari inawajibu wa kupongeza mafanikio ya Serikali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa, elimu bila malipo, ununuzi wa dawa pamoja na ununuzi wa ndege kubwa za kisasa.

Dkt. Abbas ameyasema hayo leo Mjini Dodoma wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari vilivyopo Dodoma ambapo leo ametembelea Redio A.FM na Nyemo FM kwa lengo la kuona na kujua changamoto za kiutendaji wanazokutana nazo pamoja na jinsi gani wamejipanga juu ya ujio wa Serikali kuhamia Dodoma kutokana na matukio mengi ya Serikali kufanyika Mkoani humo.

“Serikali inapaswa kuungwa mkono, yapo mambo mengi ya kimaendeleo ambayo yanatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika sekta mbalimbali ila vyombo vyetu vya habari havitekelezi wajibu wake”

“Sisi kama vyombo vya habari tunawajibu wa kupongeza kwenye mafanikio, kama kuna watendaji wa Serikali wanakosea basi wakosolewe kwa kusema ukweli, hakina staha pale penye mapungufu na sio kwa kukejeli” amesisitiza Dkt. Abbas.

Aidha, Dkt. Abbas amevitaka vyombo vya habari mkoani humo kubadilika katika uandaaji wa vipindi wanavyo virusha kwa kuanza kuandaa vipindi vitakavyogusa mikoa yote na si Dodoma peke yake.“Dodoma sasa inawageni ambao ni watumishi wa Serikali zaidi ya 3000 kwa hiyo na wao wangependa kusikia habari na nyimbo za makabila yao kutoka kwenye redio zenu hivyo yawapasa kubadili utendaji kazi wenu” ameongeza Dkt. Abbas.

Vilevile amevitaka vyombo hivyo kuandaa vipindi vinavyohamasisha wananchi kufanya kazi, kulipa kodi pamoja na kuwaeleza wana thamani gani katika nchi.Kwa upande wake Meneja wa redio A.FM Tatenda Nyawo amesema kuwa redio Afm ipo katika harakati za kuongeza masafa ya redio hiyo kwa lengo la kupanua wigo wa matangazo yao kitaifa ili mikoa mingine iweze kupata habari mbalimbali kutoka Makao Makuu ya Nchi.

Mhariri wa A-fm Regina Mndeme ameongeza, “redio Afm tumejipanga vizuri kuhusu ujio wa Serikali kuhamia Dodoma kwa kufanya kazi kwa weledi na kutangaza rasimali zilizopo mkoani hapa”.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifanya mahojiano katika Kituo cha redio A Fm cha mjini Dodoma wakati wa ziara yake yakutembelea vyombo vya Habari Mkoani humo .
Meneja wa Kituo cha redio cha A Fm cha mjini Dodoma Bw. Tatenda Nyawo (kushoto) akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa ziara yake katika Ofisi za Kituo hicho mapema leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifurahia jambo nammoja wa wamiliki wa Kituo cha redio cha A fm Bw. Emmanuel Rutagonya wakati wa ziara yake katika Ofisi za Kituo hicho mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Kituo cha redio Afm cha mjini Dodoma mara baada ya ziara yake katika kituo hicho.
Meneja wa Kituo cha redio Nyemo Bw. Hezron Mwandambo (kushoto) ya mjini Dodoma akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa ziara yake katika kituo hicho mapema leo.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Dkt. Hassan Abbasi akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Kituo cha redio Nyemo ya mijini Dodoma.(Picha zote na Frank Mvungi

KATIBU MKUU WA CCM KINANA AKUTANA NA BALOZI WA CHINA HAPA NCHINI TANZANIA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Komredi Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
Katibu Mkuu wa CCM Komredi Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
 Mazungumzo yakiendelea
 Katibu Mkuu wa CCM Komredi Abdulrahman Kinana akimsindikiza mgeni wake, Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke baada ya mazungumzo yao, ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. kushoto ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
 Katibu Mkuu wa CCM Komredi Abdulrahman Kinana akiagana na Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke baada ya mazungumzo yao, ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
 "Byeee" Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke, akimuaga Katibu Mkuu wa CCM Komredi Kinana wakati akiwa tayari kuondoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Saslaam, leo. Kulia ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.

INTRODUCING "ULINGO" BY ENGINE

One on ONe Gossip

Mkoa wa Mtwara waanza Uhamasishaji kutokomeza mimba za Utotoni/Utoro

$
0
0
Mkoa wa Mtwara Umeanza Kufanya Uhamasishaji wa Kuondoa Mimba za Utotoni na Wanafunzi wanaoacha Shule kutokana na Sababu Mbalimbali zinazowakumba Wanafunzi wa Kike kwa Njia ya Sanaa ya Maigizo.

Kupitia kituo cha Sports Development Aid (SDA) tayari kimefanya Mafunzo ya Sanaa ya Maigizo kwa Kuwatumia Waigizaji wenye Mafanikio kwa lengo la kutoa elimu kwa Wanafunzi wa Jinsia zote katika Shule ya Sekondari ya Shangani.

Kituo cha SDA tayari kimeanza Kutoa Mafunzo ya Elimu ya Jinsia kwa shule za Mtwara mjini na Vijijini kwa Kutumia njia ya Michezo, ambapo imekuwa ikigawa Vifaa vya Michezo pamoja na Kukarabati Viwanja Michezo vya Shule.
 Msanii wa Maigizo Yvone Sherry (Monalisa)Akiongea na Wanafunzi wa Shangani Sekondari mkoani Mtwara pamoja kusimamia Igizo La Elim ya Jinsia kwa njia ya Maigizo.
 Viongozi wa Kituo cha Sports Development Aid (SDA) ambao ndio waandaaji wa Mafunzo hayo wakiongea na Wanafunzi wa Sekondari ya Shangani Iliyopo mkoani Mtwara.
 Pichani ni Afisa taalum wa Mkoa wa Mtwara Masalanga akiongea na Wanafunzi wa Sekondari ya Shangani katika Mafunzo kupitia Sanaa ya Maigizo.

ZAIDI YA WALEMAVU IO8 WALIOMKIMBILIA KWA RC MAKONDA WANEEMEKA

$
0
0
Zoezi la ugawaji wa Miguu ya kisasa ya bandia kwa watu wenye ulemavu wa Miguu awamu ya pili limeanza jana, ikiwa ni Kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kuwapatia Miguu ya kisasa inayowawezesha kufanya shughuli za uzalishaji Mali Kama awali ambapo imejidhihirisha kuwa RC Makonda akiahidi jambo analitimiza kwa vitendo na sio Siasa.

Katika awamu ya pili iliyoanza jana zaidi ya Walemavu 108 wamepatiwa Miguu ya kisasa ya Bandia ambayo inakadiriwa Mguu mmoja unagharimu kiasi cha shilling million 2 hadi 3 ambapo yote kwa pamoja ni Shilling Million 324,000,000 lakini kwa jitiada za RC Makonda wamepatiwa Miguu hiyo Bure.

Katika awamu ya Kwanza jumla ya Wagonjwa 35 wa kisukari walipatiwa miguu ya kisasa ya bandia yenye thamani ya Shilling million 157 kutoka CCBRT na kufanya jumla ya walemavu waliopatiwa miguu hiyo kufikia 143 yenye thamani ya Million 481 Bure.

Baadhi ya Walemavu waliopatiwa Miguu hiyo wamemshukuru RC Makonda kwa moyo wa pekee wa kuwajali wananchi wake kwa kuzingatia makundi yote kwenye jamii ambapo wamesema kwa sasa wataenda kufanya kazi na kuachana na utegemezi.

Aidha wameishukuru kampuni ya Kamal Group kwa kumuunga mkono RC Makonda kutimiza maono yake ya kuwawezesha walemavu kupata miguu ya kisasa inayowawezesha kufanya shughuli za kujiingizia kipato.
 Baadhi ya Walemavu 108 wamepatiwa Miguu ya kisasa ya Bandia ambayo inakadiriwa kuwa Mguu mmoja unagharimu kiasi cha shilling million 2 hadi 3 ambapo yote kwa pamoja ni Shilling Million 324,000,000 lakini kwa jitihada za RC Makonda wamepatiwa Miguu hiyo Bure.
 Iliuwa ni furaha kwa Walemavu hao kupatiwa miguu ya bandia bure
  Miguu ya kisasa ya Bandia ikiwa tayari kugaiwa kwa walengwa

WAZIRI MKUU AMKABIDHI MKURUGENZI WA MUWASA KWA TAKUKURU

WIZARA HAINA MPANGO WA KUONGEZA TENA MUDA WA KUPIGA CHAPA MIFUGO-MPINA

$
0
0
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema wizara yake haina mpango wa kuongeza tena muda zoezi la utambuzi wa mifugo na kuwataka wafugaji popote walipo nchini kupaza sauti zao ili kuhakikisha kuwa ng’ombe na punda wote wamepigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.

Pia Waziri Mpina amechukizwa na tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali kuwakatalia wafugaji kupiga chapa mifugo yao kwa kisingizio kuwa sio wakazi halali wa maeneo husika jambo ambalo amesema halikubaliki na kusisitiza kuwa zoezi lisihusishwe na migogoro ya muda mrefu ya matumizi ya ardhi na hivyo kuagiza kuwa ng’ombe na punda wote nchini wapigwe chapa isipokuwa ya kutoka nchi jirani.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu tathmini ya utekelezaji wa zoezi upigaji chapa mifugo, Mpina alisema hadi kufikia Januari 16 mwaka huu jumla ya ng’ombe 10,306,359 sawa na asilimia 59.3 ya lengo wameshapigwa chapa ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 ya tathmini ya awali.

Aidha amesema wafugaji wote nchini wataoshindwa kupiga chapa mifugo yao ndani ya muda uliowekwa hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Namba 12 ya mwaka 2010 ibara ya 4 kifungu cha 26 huku akizionya halmashauri ambazo zitashindwa kutekeleza kikamilifu hatua kali zitachukuliwa dhidi ya viongozi wake.

Alisema hadi sasa halmashauri 100 zimepiga chapa zaidi ya asilimia 50, halmashauri 54 zimepiga kati ya asilimia 10 hadi 50, halmashauri 14 zimepiga chini ya asilimia 10 huku halmashauri 9 zikiwa bado hazijaanza kabisa zoezi hilo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Joelson Mpina akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari katika ukumbi wa Ofisi ya Wizara hiyo mjini Dodoma leo. Kushoto ni Naibu Waziri wake Mhe.Abdalah Ulega na mwishoni ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo. Mkutano huo ulikuwa kwa ajili yakutoa tathimini ya zoezi la upigaji chapa mifugo baada ya kumalizika kwa siku 15 za awali baada ya muda wa nyongeza wa siku 30 uliotolewa na Waziri Mpina.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Joelson Mpina akijibu maswali ya Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Ofisi ya Wizara hiyo Mjini Dodoma leo. Mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya kutoa tathimini ya zoezi la upigaji chapa mifugo baada ya kumalizika kwa siku 15 za awali baada ya muda wa nyongeza wa siku 30 uliotolewa na Waziri Mpina.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Joelson Mpina akijibu maswali ya Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Ofisi ya Wizara hiyo Mjini Dodoma leo. Mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya kutoa tathimini ya zoezi la upigaji chapa mifugo baada ya kumalizika kwa siku 15 za awali baada ya muda wa nyongeza wa siku 30 uliotolewa na Waziri Mpina. Kulia ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji, Mashimba Ndaki. 



TAG KUFUNGA NA KUOMBA KWA SIKU 21 KUMWOMBEA JPM NA SERIKALI

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT,RS-TABORA

KANISA la Tanzania Assemblies of God (TAG) linatarajia kufunga na kuomba kwa muda wa siku 21 nchini kote kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mihili mitatu ya Serikali kuanzia Jumatatu ijayo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzanaia Askofu Dkt Barnabas Mtokambali wakati wa uzinduzi wa Chuo cha Biblia (Western Bible College) kilichojengwa Wilayani Uyui na Uzinduzi wa Shule ya Seminari ya Ushindi inayojengwa katika Manispaa ya Tabora.

Alisema kuwa kuanzia Jumatatu (22 January 2018) kitakuwa ni kipindi cha kuanza kufunga na maombi ya katika Makanisa ya TAG nchi nzima waumini wake watafunga na kuomba katika maombi yatakayojulikana kama maombi ya Daniel.

Askofu Mkuu wa TAG Askofu Dkt .Mtokambali alisema kuwa katika maombi hayo mojawapo ya ajenda ni kumwombea Rais Magufuli na Mihimili yote ya serikali ikiwa ni Serikali, Mahakama na Bunge ili aendelee kuwatumikia Watanzania vizuri kama alivyoanza.

“Mkuu wa Mkoa umeleta ombi lako wakati muafaka la kutaka Kanisa limuombee Rais katika kazi nzuri anazowafanyia Watanzania…Majenerali wa Bwana Yesu wa Kanisa letu wapo hapa kuanzia Jumatau ya tarehe 22 Januari 2018, Makanisa yetu yote tutakusanyika makanisani kwa ajili ya kufunga na kuomba” alisema Askofu Mkuu huyo wa TAG.

Rais Dkt Shein aenda Ziara Falme za Kiarabu

$
0
0







RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi,kabla ya kuaza ziara yake katika Nchi za Falme za Kiarabu wakiwa katika chumba cha VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaan Karume Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na UsaIama Zanzibar wakati wa kuondoa Zanzibar kuaza ziara yake ya Kiserikali katika Nchi za Falme za Nchi za Kiarabu.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Wazee wa CCM Zanzibar katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kuaza ziara yake ya Wiki moja katika Nchi za Falma za Kiarab.

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanziba

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuaza ziara yake ya Kiserikali katika Nchi za Falme za Kiarabu.

Picha na Ikulu

RC NDIKILO AAGIZA KUFUTWA KWA LESENI YA KITALU CHA MAWE

$
0
0

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

SERIKALI mkoani Pwani ,imemuagiza kamishna wa madini wa kanda ya mashariki ,kufuta leseni ya kitalu cha mawe ya kampuni ya Global Mining Company katika eneo la Kinzagu,Lugoba wilayani Bagamoyo kutokana na kushindwa kukiendeleza miaka 17 iliyopita.

Aidha ameagiza kufutwa kwa leseni iliyohodhi eneo la ofisi ya serikali ya kijiji cha Kinzagu na mhusika ananganywe mara moja.

Pamoja na hayo,ametoa wiki mbili kwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,kumpelekea orodha ya leseni za vitalu vya mawe ambavyo vina mali za serikali .Mkuu wa mkoa wa Pwani,Evarist Ndikilo,alitoa maagizo hayo ,wakati alipokwenda kuingilia kati mgogoro baina ya mwekezaji Global co.ltd ,mwekezaji Gulf na wananchi katika kijiji cha Kinzagu. 

Alisema pia atawashughulikia wale wawekezaji wote ambao walikubaliana na serikali za vijiji lakini utekeleza baadhi ya mambo ambaoyo kwasasa wamekana makubaliano hayo.Ndikilo alisema ,kuanzia sasa eneo hilo liachiwe kampuni ya Gulf ambayo imeonyesha nia ya kuliendeleza eneo hilo na kulipa fidia wananchi 80 kwa fidia ya mil.540.2##

"Angalizo inawezekana Global Co.isiridhike hivyo ni haki yake kwenda kwenye vyombo vya sheria," Huku akae akijua mimi napeleka orodha ya wawekezaji wasioendeleza maeneo yao kipindi kirefu kwa waziri mwenye mamlaka husika.

"Tusibembelezane ,mkoa wa Pwani,sio shamba la bibi njooni mfanye maendeleo lakini msije na ghiliba ,mtu anachukua aneo anakaa nalo kama anatamia mayai????" alifafanua Ndikilo.Ndikilo alitaka orodha ya wawekezaji wanaohitaji kuendeleza maeneo ipelekwe ofisini kwake ili apeleke wizara ya madini na kupewa ridhaa ya kufanya maendeleo na sio ubabaishaji.

Nae mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,alhaj Majid Mwanga alisema wameshughulikia mgogoro huo lakini kumekuwa na ugumu hali ambayo ilisababisha migogoro na kukandamiza maendeleo ya wananchi.Alizitaka serikali za vijiji kuandaa taarifa za wawekezaji waliokwapua ardhi za watu bila makubaliano na kupata ridhaa ya mkutano mkuu wa vijiji.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete ,aliwataka wataalamu wa madini kusimamia haki za wananchi badala ya kunufaisha wawekezaji wasioitakia mema jamii.Alisema ,migogoro kati ya wawekezaji kwa wawekezaji inaumiza wananchi wasio husika.

Ridhiwani,aliipongeza serikali ya Mkoa huo kwa kufanya maamuzi hayo na kuchukua hatua yenye tija kwa wakazi wa Kinzagu.Kwa upande wake,Kamishna wa Madini wa Kanda ya Mashariki ,Julius Salota alisema atashughulikia maagizo hayo haraka iwezekanavyo.

Alisema watazungumza na kampuni ya Global ili kuangalia namna mbadala ya kumpatia eneo jingine .

Mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,(pichani)alipokuwa akizungumzia mgogoro wa wawekezaji baina ya Global co.mining ltd na Gulf.Conc na wananchi wa kijiji cha Kinzagu kata ya Lugoba,Chalinze

Mwekezaji wa kampuni ya Gulf.Conc.Khaled Mohammed ,alipokuwa akizungumza mara baada ya mkutano wa kijiji Kinzagu kata ya Lugoba na mkuu wa mkoa wa Pwani,ambae ameingilia kati mgogoro huo ,na kutoa maelekezo na agizo kampuni ya Gulf. conc iendelee kuendeleza eneo lililokuwa na mgogoro na kulipa wananchi fidia ya mil.540 .2 ili kupisha eneo hill. (picha na Mwamvua Mwinyi).

WATAALAMU WA MAJI NCHINI WAAGIZWA KUWASIMAMIA WAKANDARASI WA MIRADI YA MAJI

$
0
0
Na Jumbe Ismailly -SINGIDA.

NAIBU Waziri wa maji,Juma Aweso amewaagiza wataalamu wa maji nchini kuwasimia kwa karibu wakandarasi waliopewa kazi za miradi ya maji katika suala zima la utekelezaji wa miradi hiyo na kuwaahidi kwamba wizara hiyo haitaweza kuwa kikwazo katika kuhakikisha wakandarsi hao wanalipwa fedha zao kwa wakati ili miradi hiyo isikwame.

Naibu Waziri huyo alitoa agizo hilo mjini Singida wakati wa ziara yake ya siku moja Mkoani Singida kutembelea na kukagua baadhi ya miradi ya maji iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida.

Aidha Aweso alisisitiza kwamba katika ziara zake anazoendelea kufanya amebaini kwamba matatizo ya upatikanajai wa huduma ya maji safi na salama haiwezi kupatikana kwa wataalamu wa wizara hiyo kukaa ofisini kwa kuchezea kompyuta,bali maji yanapatikana kwa wananchi kutokana na kuwatembelea wananchi na kubaini kero zao.

“Na tunafanya ziara tukitambua kabisa maji hayapatikani kwa kukaa ofisini kwa kuccheze kompyuta,maji yanapatikana kwa wananchi kwa sababu anayelala na mgonjwa ndiye anayejua mihemo ya mgonjwa.”alifafanua Naibu Waziri huyo.

Hata hivyo Aweso aliweka bayana kwamba akiwakatika ziara yake ya wiki moja Mkoani Shinyanga alibaini baadhi ya miradid iliyokuwa ikisuasua lakini baada ya kuisukuma imeanza kwenda vizuri na hivyo kutumia fursa hiyo kuwaahidi wananchi wa Mkoa wa Singida kwamba anatarajia kurudi Mkoani hapa kufanya ziara katika Halmashauri zote za Mkoa wa Singida.
Naibu waziri wa maji,Bwana Juma Aweso akiteta jambo na katibu wake mara baada ya kupokea taarifa ya Halmashauri ya wilaya ya Singida inayohusu sekta ya maji.
kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida,Faustine Kiyui akisoma taarifa ya sekta ya maji ya Manispaa ya Singida kwa Naibu waziri wa maji,Bwana Juma Aweso.
Naibu wazziri wa maji,Bwana Juma Awesso akiongozaa kikao cha watendaji wa Halmashauri ya wilaya na Manispaa ya Singida baada ya kupokea taarifa za Halmashauri hizo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Ni baadhi ya watendaji wa serikali wa wilaya ya Singida wakiwa katika kikao cha pamoja na Naibu waziri wa maji,Bwana Juma Aweso kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Singida. 

MWAKYEMBE ATEMBELEA KAMBI YA SERENGETI BOYS LEO JIJINI DAR

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Dr. Harrison Mwakyembe, Leo Jumamosi Januari 20, 2018 ameitembelea timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 16 Serengeti Boys iliyopo kambini kwenye hostel za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF na kuwaachia ujumbe wa Serikali. 

Dr. Mwakyembe akitoa salamu za Serikali amewaambia Vijana wanaounda timu hiyo kuwa serikali inawaamini na wanalo jukumu la kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania. 

Amewataka kupambana kwa ajili ya Tanzania na kuhakikisha wanafanya vyema kwenye kila mashindano huku akiwataka makocha wa kikosi hicho kuwapa mafunzo mazuri kwa ustawi wa Vijana hao. 

Aidha Dr. Mwakyembe amesema anaamini Vijana hao watakuwa bora chini ya TFF iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais Ndugu Wallace Karia. "Naamini mtaimarika na kuwa bora maana hata TFF hii sasa ina ari na morali kubwa".Alisema Dr. Mwakyembe. 

Katika ziara yake hiyo Dr. Mwakyembe alipata nafasi ya kutazama mchezo wa kirafiki kati ya Serengeti Boys na Makongo Sekondari iliyomalizika kwa Serengeti Boys kupata ushindi wa mabao 4-1.

Kabla ya mchezo huo Serengeti Boys walicheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Kituo cha Bombom iliyomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

TFF:KAMATI YA MAADILI YAPITIA SHAURI LA WATUHUMIWA WA KUGHUSHI NA UDANGANYIFU WA MAPATO.

$
0
0
Kamati ya Maadili iliyokutana Januari 18, 2018 imepitia shauri lililowasilishwa na Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF wakiwatuhumu viongozi wanne kwa makosa ya kughushi na udanganyifu wa mapato kwenye mchezo namba 94 kati ya Ndanda FC na Simba uliochezwa Disemba 30,2017.

Shauri la kwanza lililomuhusu Katibu msaidizi wa Ndanda Ndugu Selemani Kachele,Kamati imegundua kuwa mtuhumiwa aliitwa wakati wa kuhesabu mapato kuthibitisha deni dhidi ya Ndanda lenye thamani ya Shilingi Milioni mbili laki mbili na elfu hamsini(2,250,000),deni ambalo TFF waliagiza wakatwe kwenye mapato ya mechi hiyo,Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mtwara alithibitisha kuwa alimuita kuthibitisha uhalali wa deni hilo baada ya Muhasibu wa Ndanda kugoma kulipa deni hilo ambalo linahusu pango la Ndanda kwa Mama mwenye Nyumba.

Hata hivyo Kamati ilimuhoji zaidi na akashindwa kutoa uthibitisho wa kulipwa kwa deni hilo na hakuna kumbukumbu zozote zinazoonyesha kuwa deni hilo limelipwa.Kamati imempa onyo kwa mujibu wa kifungu cha 6(1)(a) kanuni za maadili ya TFF toleo la 2013 na imeiomba Sekretarieti ya TFF ifuatilie kama deni hilo limeshalipwa ili kuepusha ulipaji wa Zaidi ya mara moja.

Shauri la Pili lilimuhusu Muhasibu msaidizi wa Simba Ndugu Suleiman Kahumbu.Kamati haikuendelea na tuhuma dhidi yake baada ya Sekretarieti ya TFF kuamua kuondoa shauri dhidi yake kwa kuwa alitoa ushirikiano na kutosheka kuwa hana hatia na badala yake alitumika kama shahidi wa upande wa washtaki.

Shauri la tatu lilimuhusu Katibu mkuu wa Chama cha soka Mtwara Ndugu Kizito Mbano.Kamati ilimuhoji mtuhumiwa na alikiri kuwepo kwa mawasiliano na msimamizi wa kituo Ndugu Dunstan Mkundi kuhusu nia ya kughushi fomu ya marejesho ya mapato ya mchezo kati ya Ndanda FC na Simba SC.

Ndugu Kizito Mbano hakutoa taarifa yoyote ile wala kuonyesha ushirikiano kwa Sekretarieti ya TFF na Bodi ya Ligi wakati yeye akiwa msimamizi msaidizi wa kituo na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka cha Mkoa wa Mtwara,hivyo Kamati imemkuta na hatia na imemuhukumu kutojihusisha na shughuli za Mpira wa Miguu kwa kipindi cha miaka Mitano(5) kwa mujibu wa kifungu cha 73(7) cha kanuni za maadili TFF toleo la 2013.

WAZIRI MKUU AMKABIDHI MKURUGENZI WA MUWASA KWA TAKUKURU

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameamuru Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mara kumkamata na kumuhoji Mkurugenzi Mtendani wa Mamlaka ya Maji Musoma (MUWASA) Mhandisi Gantala Said kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mradi wa maji Bunda.

Mbali na Mkurugenzi huyo pia TAKUKURU inawashikilia wakandarasi wanaojenga mradi huo ambao ni Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Nyakirang'anyi Bw Mauza Mmangi ambaye ndiye mkandarasi anajenga mradi huo unaotoa maji kutoka Ziwa Victoria kwenye eneo la Nyabehu hadi Bunda mjini.

Wengine waliokamatwa ni pamoja na Mhasibu wa Kampuni ya Ujenzi ya Nyakirang'anyi Bw. Amon Gideon pamoja na viongozi wa kampuni nyingine ya ujenzi ya Fortrss Bw. Juvenari Chirianga na Ephraim Mpeko ambao nao walishiriki katika ujenzi wa mradi huo.

Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo jana jioni (Ijumaa, Januari 19, 2018) baada ya Mkurugenzi huyo kushindwa kueleza sababu zilizosababisha mradi wa maji Bunda kutokamilika pamoja na Serikali kutoa fedha nyingi.

Akizungumza katika kikao maalumu cha kujadili changamoto za utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Mara, alichokiitisha mjini Bunda, Waziri Mkuu alisema alimua kuitisha kikao hicho baada ya kutoridhishwa na utekelezwaji wa miradi hiyo hususan inayosimamiwa na MUWASA .

Alisema kwa sasa Serikali inatekeleza Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani. Kampeni hiyo inayolenga kuwaondolea wananchi tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, hivyo itawachukulia hatua wote watakaokwamisha miradi ya maji.

Waziri Mkuu amesema malengo ya kampeni hiyo ni kuwafikishia wananchi huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Pia Waziri Mkuu aliagiza kupitiwa upya kwa mradi huo kwa sababu hafurahishwi na ujenzi wake.” Kama Mkurugenzi wa MUWASA anasema mradi umekamilika kwa asilimia 98 sasa kwa nini wananchi walalamikie kukosa huduma hiyo.”

Alisema Mkurugenzi huyo amekuwa akimlipa mkandarasi fedha kabla ya kufanya kazi ambapo hadi sasa tayari mkandarasi anayenga mradi huo ameshalipwa zaidi ya sh. bilioni saba na mradi haujakamilika na wananchi wanaendelea kutumia maji ambayo siyo salama.

Waziri Mkuu alisema viongozi hao wahojiwe na wakibainika kuhusika na ubadhilifuu wa fedha za mradi huo, wachukuliwe hatua kali za kisheria.”Serikali imedhamiria kuimarisha huduma za maji, hivyo hatuhitaji mtu atakayeenda kinyume na mpango huo.”

Mradi wa kupeleka maji kwenye mji wa Bunda maji kutoka ziwa Victoria katika eneo la Nyabeho ulisanifiwa mwaka 2006 na ulikuwa unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha za maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw. Adam Malima aliagiza kufungwa na ofisi za MUWASA na kuwataka wafanyakazi wa mamlaka hiyo kutoruhusiwa kuingia ofisini hadi hapo uchungi utakapokamilika.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAMOSI, JANUARI 20, 2018.


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamalaka ya Maji Musoma, Mhandisi Said Gantala (kushoto) akitoka kwenye ukumbi wa Balili Rock Resort mjini Bunda baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuamuru kuwa akamatwe na ahojiwe na TAKUKURU Januari 19, 2018.Kulia ni Kamanda wa TAKUKURU wa mkoa wa Mara, Alex Kuhanda.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

DC LYANIVA AWAASA WATAALAMU WA MANUNUZI KUWA WAZALENDO

$
0
0
 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amewaasa Wanafunzi wanaosoma masuala ya Ununuzi na Ugavi katika chuo cha Uhasibu TIA  Kuwa Wazalendo pindi wanapofika katika maeneo yao ya kazi ili wawe mfano bora kwa Taifa.

Dc Lyaniva ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua mafunzo ya Masuala ya ununuzi na Ugavi,yaliyoandaliwa na Bodi ya PSPTB kwa wanafunzi wa Chuo cha TIA ambao wanasoma masuala ya manunuzi.

"Msiwe na mawazo ya kufikiria kupata pesa za haraka haraka pindi mnapopata kazi,kwani mkiwa na moyo huo mtaangukia katika makosa ya uhujumu Uchumi ,jambo ambalo watu wengi wa taaluma yenu mwisho wa siku wamekuwa wakiangukia Polisi"amesema Dc Lyaniva.

Ameaongeza kwa kusema kuwa anapenda kuwambia kwamba Maadili yenye Uzalendo ndio nguzo ya Msingi  katika kufanya kazi, ndio Maana Rais wetu Dk John Magufuli amefanikiwa kubadilisha mambo mengi katika nchi kutokana na uzalendo wake.
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu cha TIA Kampasi ya Dar es Salaam, wanaosoma Masuala ya Manunuzi wakati wa Semina Maalum iliyoandaliwa na bodi ya Wataalam wa Manunuzi PSPTB
 Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Wataalam wa Manunuzi nchini, Godfred Mbanyi akizungumza na Wanafunzi wa Chuo cha uhasibu cha TIA ambao walikuwa wanapata Semina Maalum juu ya masuala ya Manunuzi.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu TIA, Mugisha Kamala akizungumza kwa ajili ya kuwakaribisha wageni na Mkuu wa Wilaya ya Temeke katika Semina hiyo ya masuala ya Ununuzi na Ugavi
Sehemu ya Wanafunzi waliohudhuria Mafunzo ya masuala ya Ununuzi na Ugavi kutoka PSPTB yaliyoendeshwa katika Chuo cha uhasibu TIA.

KWANDIKWA: BARABARA ZA MCHEPUO KUPUNGUZA MSONGAMANO DODOMA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, amesema kuwa ujenzi wa barabara ya Mbande – Kongwa (Km 11.7) na Chimwaga – Ihumwa (Km 10) utasaidia kupunguza msongamano kwa magari yanayoingia Dodoma mjini.

Naibu Waziri huyo ameyasema hayo wakati akikagua barabara hizo na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wake ambapo amesisitiza kwa makandarasi wanaojenga barabara hizo kuhakikisha wanamaliza kazi hizo kwa muda uliopangwa na kwa viwango vilivyo kwenye mkataba.

“Tutaendelea kujenga na kuboresha barabara hizi za mchepuo lengo ni kupunguza foleni katikati ya mji kwani Dodoma sasa inakua kutokana na uwepo wa watumishi wengi wa Serikali na ongezeko la magari, kwa hiyo sisi kama Serikali hatuna budi kuangalia namna ya kuboresha miundombinu yetu ili ikidhi haja ya ongezeko hili”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Aidha, amefafanua kuwa barabara hizo zikikamilika zitakuwa ni njia mbadala kwa watumiaji kwani sio lazima kwa magari yote kupita mjini na badala yake yatatumia njia nyingine za mchepuo kuendelea na safari zake.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kwandikwa amekagua athari za mvua katika barabara za mji wa Dodoma na kuwataka wananchi na madereva kuchukua tahadhari ili kuepusha hatari zinazoweza kuwakabili wakati wakivuka ama kupitisha magari yao katika kipindi hiki ambacho baadhi ya sehemu za barabara zinajaa maji kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha. 
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu, akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, sehemu ya ujenzi wa barabara ya mchepuo kutoka Chimwaga-Ihumwa yenye urefu wa KM 10 inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa ajili ya kupunguza msongamano wa magari yanayoingia mkoani humo.Mhandisi Mkazi anayesimamia ujenzi wa barabara ya Chimwaga-Ihumwa KM 10 kwa kiwango cha lami, Mhandisi Nicholaus Mzeru, akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi kwa waandishi wa habari ambapo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 92.4 na KM 8 zimeshakamilika kujengwa, mkoani DodomaMeneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu, akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, athari za mvua eneo la katondo katika barabara za mji huo.Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akiongozana na Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu, wakikagua athari za mvua eneo la Kibaigwa, katika barabara ya Dodoma-Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

CUF WAJIGAMBA UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI MCHAGUZI MDOGO

$
0
0
Na Ripota , Globu ya jamii .

CHAMA cha Wananchi(CUF) kimesema kimejipanga vema kuhakikisha wanashinda uchaguzi mdogo jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam, huku kikionesha kutokuwa na wasiswasi na mgombea wa Chadema Salum Mwalimu ambaye amejitosa kwenye uchaguzi huo. 

Kauli ya CUF inakuja siku moja tu baada ya Mwalimu ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema upande wa Zanzibar kuchukua fomu ya kugombea ubunge Kinondoni. 

Akizungumza na Michuzi Blogu leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF , Abdallah Kambaya amesema wao walishajipanga na kuweka mikakati ya kushinda uchaguzi huo kupitia Salim Jumaa . 

Amefafanua tangu mwanzo walishasema wataingia kwenye uchaguzi huo kwani wanajua jimbo la Kinondoni ni ngome ya CUF na hivyo hakuna wa kuwasumbua. 

"Tumejipanga mapema na tumeona Salum Mwalimu amechukua fomu ya kugombea ubunge na tayari kairudisha huku akisindikizwa na safu ya viongozi wake. Tulitarajia Mwalimu atachukua fomu na ndicho alichofanya. 

"Kwetu sisi wala hakuna ambacho tuna hofu.Hawatumiizi kichwa,"amesema Kambaya na kuongeza CUF imekamilisha kila idara kuhakikisha wanashinda.

MAJALIWA ATEMBELEA SHAMBA LA JKT RWAMKOMA WILAYANI BUTIAMA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua shamba la uzalishaji wa mbegu bora za mihogo aina ya mkombozi linalomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha Rwamkoma wilayani Butiama.

Amekagua shamba hilo linalomilikiwa na Kikosi cha JKT Rwamkoma leo (Jumamosi, Januari 20, 2018) alipowasili wilayani Butiama akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mara. Kikosi hicho kimewezeshwa na Halmashauri ya Butihama.

Waziri Mkuu amewakipongeza kikosi cha JKT Rwamkoma kwa uamuzi huo wa kuzalisha mbegu bora za mihogo ambazo baadae zitasambazwa kwa wakulima wa zao hilo wilayani hapa.Pia amewataka wakazi wanaoishi karibu na shamba la kikosi hicho hilo kulitumia kama shamba darasa kwa ajili ya kujifunza namna bora ya kulima zao hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi hicho Luteni Kanali David Msakulo alisema shamba hilo linaukubwa wa ekari 60, na mbegu zitakazozalishwa zitatosha kupanda ekari 900.Mkuu huyo wa kikosi hicho aliongeza kuwa mbegu hizo zinazozalishwa katika shamba hilo zitagawanywa kwa wakulima katika kata zote 18 za wilaya ya Butihama.

Alisema mbali ya kuzalisha mbegu pia wanatarajia kuanzisha kiwanda cha kuchakata zao la mihogo ili kuweza kuliongezea thamani.Mbali na shamba la mbegu bora za mihogo pia kikosi hicho kina shamba lingine la pamba lenye ukubwa wa ekari 57, ambapo wanatarajia kuvuna tani 57 za pamba. Mwakani wanatarajia kuongeza ukubwa wa shamba na kufikia ekari 300.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea shamba darasa la mkoa wa Mara la zao la pamba lililopo Kisangwa wilayani Bunda akiwa njiani kuelekea wilayani Butihama, kuendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Mara.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Bw. Adam Malima alisema shamba darasa hilo ni moja ya jitihada za Mkoa wa Mara kuelimisha wakulima wa zao hilo mbinu bora za uzalishaji ili kuongeza tija katika uzalishaji.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima wakati alipotembelea shamba la kuzalisha mbegu bora ya mhogo  aina ya mkombozi katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ya Rwmkoma wilayani Butiama, Januari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama  shamba la Pamba wakati alipotembelea shamba la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lililopo Rwamkoma wilayani Butiama Januari 20, 2018. Shamba hilo  pia linazalisha mbegu bora za mhogo aina ya mkombozi.

SHIMIWI kutekeleza agizo la Makamu wa Rais

$
0
0
SHIRIKISHO la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), litatekeleza agizo la Makamu wa Rais wa Tanzania Bara, Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na mabonanza kila mwisho wa mwezi yatakayohusisha wachezajiw a michezo mbalimbali.

Moshi Makuka, Katibu Mkuu wa SHIMIWI, alisema wamekubaliana katika kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika hivi karibu, ambapo wataanza na bonanza kubwa litakalofanyika Februari mwaka huu mkoani Dodoma, ambapo sasa Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali zimeshahamia mkoani hapo.

“Hili bonanza litakuwa kubwa sana kwani ukiangalia tayari wizara, taasisi na Idara za serikali kwa asilimia kubwa zimeshahamia Dodoma, hivyo timu zianze kujiandaa na baada ya kukamilisha hili baadaye katika tarehe zitakazotangazwa tutafanya tena Jijini Dar es Salaam,” alisema Makuka.

Makamu wa Rais, mwaka jana alitoa agizo kufanyike mazoezi ya kila mwezi kwa kuhusisha wafanyakazi ili kujijengea afya zao. Michezo inayochezwa SHIMIWI ni pamoja na soka, netiboli, kuvuta kamba, baiskeli, karata, bao na draft (wanawake na wanaume).

Mbali na kuanza kwa mabonanza, pia Kamati hiyo ya Utendaji imeunda Kamati mbalimbali ikiwemo ya Habari na Mawasiliano ambayo itaongozwa na Itika Mwankenja (Mwenyekiti), Elias Malima (Katibu), huku wajumbe ni Bahati Mollel, Jane John, James Katubuka, David Kitila na Jessey John; kamati ya utendaji na nafasi zao ni Daniel Mwalusamba (Mwenyekiti), Ally Katembo (Makamu Mwenyekiti), Makuka (Katibu Mkuu), Alex Temba (Katibu Msaidizi), William Mkombozi (Mweka hazina), Frank Kibona (mweka hazina msaidizi) na wajumbe ni Appolo Kayungi, Damian Manembe, Seleman Kifyoga, Assumpta Mwilanga na Aloyce Ngonyani, huku wajumbe wa viti maalum ni Mariam Kihange na Mwajuma Kisengo.
Uongozi mpya wa Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) mara baada ya kutangazwa na msimamizi wa uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kwenye hoteli ya Mount Uluguru mkoani Morogoro.

Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images