Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live

SETHI ASUBIRI MADAKTARI KUTOKA AFRIKA KUSINI KWA UPASUAJI, RUGEMALIRA HANA KANSA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MMILIKI wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habinder Sethi na Mfanyabiashara, James Rugemarila wameomba madaktari wao kutoka India na Afrika kusini kuwepo wakati wakifanyiwa uchunguzi wa afya zao.

Maombi ya mshtakiwa, Harbinder Seth yamewasilishwa na Wakili wake, Alex Balomi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya kupata taarifa kutoka upande wa mashtaka.

Akitoa taarifa hiyo mapema leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai amedai kuwa alikwenda magereza kufuatilia hali za washitakiwa hao kama mahakama ilivyoagiza.

Swai amedai kuwa washitakiwa hao wameomba magereza wakati wanapofanyiwa uchunguzi kiafya madaktari wao kutoka nje ya nchi wawepo. 

Amesema, mshtakiwa Sethi ambaye anaishi na puto tumboni ambalo kwa uchunguzi aliofanyiwa na daktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Desemba mwaka jana linatakiwa litolewe na, mshitakiwa alishirikishwa katika hatua hiyo lakini akaomba daktari wake kutoka Afrika Kusini awepo wakati wa kufanyiwa upasuaji.

Aisha amedai mshtakiwa huyo ameomba muda Wa kuwasiliana na daktari wake

Aidha amedai kuwa madaktari wa hapa nchini wamekubaliana na ombi la mshtakiwa ila wamesema kama afya ya mshitakiwa itaendelea kuathirika wataliondoa hilo puto.

Aliendelea kudai, kuhusu afya ya mshtakiwa Rugemalira, yeye anatibiwa na magereza pamoja na daktari wake anayeitwa Fred kutoka Hospitali ya Sanitas ambaye anachukua vipimo na kupeleka hospitalini kwake kisha kurudisha majibu magereza.

Alidai katika majibu hayo yanaonesha kuwa hana saratani kama alivyodai na kwamba serikali inafuatilia afya zao kwani hakuna jambo nyeti litakaloweza kuhatarisha maisha yao.
Wakili Balomi, akipinga hayo amedai, Hospitali ya Muhimbili wamethibitisha kuwa hawana uwezo wa kumfanyia upasuaji wa ama kuondoa au kuweka hilo puto na kusisitiza kwamba umuhimu wa daktari wake kutoka Afrika Kusini ni la kutiliwa mkazo kwani wamepokea maoni kutoka kwa madaktari hao Ka kusisitiza lazima wawepo wakati wa upasuaji.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Article 6

MUONEKANO WA SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO

$
0
0
Wachuuzi wa Samaki wakisubiri kununua kitoweo katika Soko la samaki la Wilaya ya Bagamoyo, Bei ya samaki katika soko hilo imeongezeka kutokana kupatikana na shida kutokana na mabadiliko ya hali y Hewa.
Mvuvi akiwauzia wachuuzi samaki katika soko la samaki la wilaya ya Bagamoyo.
Mwananchi akiwa amepumzika kando ya soko la samaki la wilaya ya bagamaoyo. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

MICHUZI BEAT: ENOCK BELLA AZUNGUMZIA UJIO WAKE MPYA..

MICHUZI TV: SERIKALI YAKATAZA KULIMA PAMBA KWA MKATABA

Athman Kambi aomba Radhi Wadau wa Soka-Mtwara.

$
0
0
Kutokana  na Kamati ya Maadili Kuwakuta na Hatia Viongozi wawili Wa Shirikisho la Soka TFF akiwemo Msimamizi wa  Mchezo Mkoa wa Mtwara Dastan Mkundi pamoja na katibu Mku wa Chama Hicho Mkoa wa Mtwara Kizito Mbano Mwenyekiti wa soko Mkoa wa Mtwara Athman Kambi amewaomba radhi Mashabiki wa soka Mkoa wa Mtwara kwa Kashfa Hiyo.

Kwa Mujibu wa kamati ya Maadili Aliyekuwa Msimamizi wa Mchezo wa Ndanda FC dhidi ya Simba  tarehe 30 amehukumiwa  kifungo cha  Maisha Kutojihusisha na Soka kutoka na kosa LA Kughushi na Udanganyifu wa Mapato ya Mchezo huo ikiwa ni kinyume cha Kanuni ya Kifungu 32(2) na ile ya 32(4) pamoja na Katibu mkuu wa chama hicho Mkoa wa Mtwara  Kizito Mbano kwa Mujibu wa Kanuni za Maadili za TFF kifungu 73( 7) na amehukumiwa Miaka mitano Kutojihusisha na Soka huku Suleiman Kachele Kupewa Onyo

Akiongea mara baada ya Taarifa hizo Athman Kambi amesema swala la soka linahitaji uaminifu ili kuweza kusaidiwa na wadau wa soka.Lakini nao baadhi ya wadau wa soka wamesema bado kuna mapato yanapotea hasa katika mechi kubwa ambazo zinachezwa Mkoa wa Mtwara.

 Kwa mujibu wa kanuni za Chama cha Soka Nchini TFF Baada ya kamati ya Maadili kutoa Hukumu watuhumiwa wanaweza kukata Rufaa katika kamati ya Rufaa ya maadili na wanaweza wakasikilizwa Upya.
 

SHONZA:HATUTA MUANGALIA USONI MTU YEYOTE ATAKAYE KIUKA MAADILI YA MTANZANIA

JKCI yakabidhiwa wodi ndani ya jengo la wodi ya watoto

$
0
0
 
 Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH) ) Agnes Mtawa akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya funguzo za baadhi ya wodi zilizopo ndani ya  jengo la wodi ya watoto  ambazo Hospitali hiyo imezitoa kwa JKCI ili wazitumie kutokana na   uhaba wa wodi ya watoto walionao.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH) ) Agnes Mtawa akitoa maelezo kwa viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kuhusu wodi zilizopo ndani ya jengo la watoto ambazo  Hospitali hiyo imezitoa kwa Taasisi hiyo  ili wazitumie kutokana na uhaba wa wodi ya watoto walionao.
 Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH) ) Agnes Mtawa kuangalia wodi zilizopo ndani ya jengo la wodi ya watoto ambazo  Hospitali hiyo imezitoa kwa Taasisi hiyo  ili waweze kuzitumia kutokana na uhaba wa wodi ya watoto walionao.
 Wodi zilizopo ndani ya jengo la wodi za watoto ambazo  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imezitoa kwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  ili wazitumie kutokana na uhaba wa wodi ya watoto walionao.

Picha na JKCI


USAJILI NDANI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU

$
0
0
Usajili katika kata za Uhuru, Ayamohe, Ayamami, Imboru, Silaloda umemalizika wilayani Mbulu huku wananchi wakimininika kuendelea na Usajili kwenye Kata za Daudi, Marang, Gidamba, Gehandu na Titiwi huhu vijana wakijitokeza kwa wingi baada ya kutambua umuhimu wake katika masuala ya Elimu.

Ndg. Prosper Alfred Marmo mkazi wa Kata ya Daudi Kijiji cha Moringa, Kitongoji cha Magasi amesema ameona ni vyema akatii agizo la Serikali ili apate Kitambulisho kitakachomtambulisha kupata huduma mbalimbali ikiwemo mikopo ya elimu ya juu pindi wakati utakapofika.

Akizungumzia zoezi la Usajili linaloendelea kwa sasa Wilayani Mbulu; Afisa Usajili Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bi. Amina Farijala amesema pamoja na kwamba msimu huu ni wakilimo na wananchi wengi wako kwenye shughuli za kilimo mwitikio wao umekuwa mkubwa hasa nyakati za mchana na hivyo kuwaasa kupanga vizuri shughuli zao ili kujitokeza kwa wingi nakwa wakati kusajiliwa.“ Mwitiko hawa wa kundi la wazee umekuwa mkubwa na kutumia moyo hasa tunapoona wazee wanafika kwenye vituo kusajiliwa” alisema

Kwa sasa NIDA inandelea na zoezi la Usajili kwa mikao 19 ya Tanzania Ikiwemo Manyara na inakusudia kufikia Desemba 2018 zoezi hili kuwa limemalizika nchi nzima na wananchi kuanza kutumia Utambulisho wao kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi na kimaendeleo.
Afisa Msajili Halmashauri ya Mji wa Mbulu Ndg. Amina Farijala akitoa maelekezo

Wananchi Kijiji cha Moringa Halmashauri ya Mji ya Mbulu wajitokeza Kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa.
Wananchi Kata ya Daudi Halmashauri ya Mji ya Mbulu wakiwa wamepanga foleni tayari kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa.
Ndg. Emmanuel Safari Amnaay mkazi wa Kitongoji cha Malasi (kulia) akiwa na Ndg. Josephati Faustini Masay mkazi wa Malasi kwa pamoja wakijaza fomu ya maombi ya Kitambulisho cha Taifa wakati wa zoezi la Usajili linaloendelea.

Zuriel’s 3 Country Film Class Ends in Abidjan, After Accra & Lagos Stops

$
0
0
The UN’s 17 Sustainable Development Goals towards a better world by 2030 wraps around a myriad of action areas, including Girls/Gender Development & Quality Education, areas 4 & 5. 

Believing that Education is more than what is learned in school, Zuriel Oduwole then 13 years old, launched her basic “Film Making 101 Class” for 25 Girls in Namibia, back in February 2016. It was one of several initiatives over a 4 year period that got her honored by the US Secretary of State in January 2017 in Washington DC. 

The film making program with the support of Sahara Group, has just completed across 3 ECOWAS countries of GhanaNigeria and Cote D’Ivoire While the classes in Nigeria and Ghana featured traditional and vocational School Girls aged between 15 and 19, the class in Abidjan – Cote D’Ivoire was delivered for women between the ages of 19 and 38 – most with social, economic, domestic, cultural and environmental challenges, who were looking for a second chance in life, and hopefully, participate in the New Digital Economy.

Introducing "UTATULIA" by Lavalava

BENKI YA DUNIA YATOA UFADHILI WA SHILINGI BIL. 47 KUHIFADHI RASILIMALI YA BONDE LA MTO WAMI - RUVU.

$
0
0
 Na. Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Benki ya Dunia imetoa ufadhili wa shilingi Bilioni 47 kutekeleza mradi wa uhifadhi wa rasilimali za maji awamu ya pili katika bonde la mto Wami.

Akizindua mradi huo mapema leo, Mjini Dodoma Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa Tanzania ina jumla ya mabonde tisa ya maji lakini mabonde hayo yameathiriwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za kibinadamu na kiuchumi zinazosababisha kupungua kwa maji katika mabonde hayo.

"Fedha hizi zilizotolewa na Benki ya Dunia zitaenda kutoa elimu kuanzia ngazi ya juu mpaka mwananchi wa kawaida juu ya njia za kutumika kutunza rasimalimali za maji ndani ya hifadhi ya bonde la mto Wami," alisema Mhandisi Kamwelwe. 

Aidha Mhandisi Kamwelwe amewataka wananchi na viongozi watakaopata elimu hiyo kutunza   rasilimali hiyo wao wenyewe kwa kutofanya shughuli za kibinadamu na za kiuchumi ndani ya hifadhi la bonde hilo.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Benki ya Dunia Alex William amesema kuwa jukumu la utunzaji wa rasilimali za maji ni za kila mwananchi, kiongozi pamoja na taasisi za umma na binafsiHivyo amewata Watanzania kupitia mradi huo kutunza rasilimali hiyo ili kuongeza kiwango cha maji ndani ya bonde hilo ambayo yatatumika katika shughuli za nyumbani, viwandani, mashambani  katika shughuli za uvuvi pamoja na utalii.

Naye, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Nazifa Kemikimba amesema mradi huo utasaidia upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es Salaam na mikoa ya karibu ukiwemo mkoa wa Morogoro.

WAZIRI MKUCHIKA AWAFUNDA WALENGWA WA TASAF

$
0
0
NA ESTOM SANGA-MBEYA

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa George Mkuchika amewatembelea Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF katika halmashauri ya Jiji la Mbeya na kuwataka kuongeza jitihada zaidi za kujitegemea kwa kutumia ruzuku wanayoipata kwa kuanzisha miradi ya uzalishaji mali ili kukuza kipato chao.


Mheshimiwa Mkuchika amesema jitihada za serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF za kuhamasisha wananchi kuuchukia umasikini haziwezi kuwa endelevu ikiwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini hawatatumia fedha wanazozipata kubuni miradi ya uzalishaji mali.


“hiki mnachokipata kutoka serikalini kupitia TASAF kiwe chachu ya kuanzisha miradi ya uzalishaji mali ili hatimaye muweze kujitegemea” amesisitiza Waziri Mkuchika.Akiwa katika eneo la Shule ya Sekondari ya Lupeta katika jiji la Mbeya , shule ambayo TASAF imejenga jengo la Utawala na Maabara,Waziri Mkuchika ameeleza kuridhishwa na matokeo ya ujenzi wa majengo hayo na kupunguza kero iliyokuwa inawakabili walimu na wanafunzi shuleni hapo.

Aidha Mheshimiwa Mkuchika amekutana na vikundi vya uzalishaji mali vilivyoanzishwa na Walengwa wa TASAF kwa kutumia ruzuku ya fedha kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambapo walengwa hao wamekuwa wakikopeshana fedha zinazotokana na uzalishaji wa bidhaa zikiwemo mikeka,na hivyo kuwaongezea uwezo wa kuhudumia kaya zao.


Hata hivyo Waziri huyo ametoa maagizo kwa uongozi wa mkoa wa  Mbeya kuhakikisha kuwa watu wanaonufaika na fedha za ruzuku kutoka TASAF ni wale wanaokidhi vigezo vya umasikini na kutaka fedha zilizolipwa kwa watu wasiostahiki zirejeshwe mara moja.


“rejesheni fedha za serikali ili ziwanufaishe walengwa wanaostahiki kupata ruzuku hiyo kama ilivyokusudiwa na serikali” ameonya Waziri Mkuchika.Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bi. Mercy Mandawa ameishukuru serikali kwa kuendelea kuusimamia kikamilifu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF ili uendelee kusaidia jitihada za kuwaondolea wananchi kero ya umaskini.

Amesema tangu kuanzishwa kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ,kumekuwa na mwitikio chanya kwa walengwa kutumia ruzuku hiyo kuboresha maisha yao huku mkazo ukiwekwa katika kuboresha elimu,afya na lishe kwa watoto wanaotoka  kwenye kaya za walengwa huku akisisitiza juu ya matumizi sahihi ya ruzuku inayotolewa kila baada ya miezi miwili.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Mhe. George Mkuchika (aliyevaa suti nyeusi) akikagua bidhaa zilizotengenezwa na Walengwa wa TASAFkatika mtgaa wa Inyala katika jiji la Mbeya  kama njia mojawapo ya kujiongezea  kipato. 

 Waziri Mkuchika (aliyevaa tai) akimsikiliza mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lupeta katika jiji la Mbeya alipotoa maelezo ya maabara iliyojengwa na TASAF shuleni hapo.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika akikagua jengo la maabara lililojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF katika shule ya Sekondari ya Lupeta katika halmashauri ya jiji la Mbeya.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, DK. HAMISI KIGWANGALLA ATEUA WAJUMBE WAPYA WA BODI YA MAMLAKA YA HIFADHI YA ENEO LA NGORONGORO

KUMBILAMOTO APOKEA MIFUKO 90 YA VIROBA VYA NILU KUTOKA TOL

$
0
0

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kupokea Mifuko 90 ya Nilu kutoka kiwanda cha Tanzania Oxygen Limited ambapo Nilu hiyo itatumika kwa ajili ya kupaka katika shule mbalimbali zinazojengwa ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akipokea viroba vya Nilu ambavyo vitatumika kupaka shule zilizopo katika Manispaa ya Ilala.
Karani kutoka kampuni ya Tanzania Oxygen Limited (TOL),Dorothy Katala akimuonesha Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto, Idadi ya Viroba vya Nilu anavyotakiwa kuchukua .
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto, akisimamia upakiaji wa Viroba vya Nilu kwenye gari hili iweze kufika panapo husika.

BBC DIRA YA DUNIA 19.01.2018

VOA SWAHILI: Duniani Leo Januaryi 19, 2018

INTRODUCING "NAMPA" BY PZONE FEAT MR.BLUE

UNNewsKiswahili: Hofu yaongezeka kwa wanawake na watoto wanaokimbia vita

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 20, 2018

Viewing all 110031 articles
Browse latest View live




Latest Images