Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live

WAKULIMA WA USAGALI AMCOS WILAYANI NZEGA WAMUOMBA MKUU WA MKOA KUWASAIDIA ILI WALIPWE DENI LAO LA MILIONI 193

$
0
0
RS TABORA

WAKULIMA wa Tumbaku wa Chama cha Msingi cha Ushirika Usagali (AMCOS) wilayani Nzega wameiomba Serikali ya Mkoa wa Tabora kuwasaidia kusimamia madai yao ya fedha zao kiasi cha shilingi milioni 193 za mauzo ya tumbaku kwa msimu 2015/2016 ambayo watuhumu kuchukuliwa na viongozi waliokuwa madarakani wakati huo.

Wakulima hao walitoa kilio hicho jana katika Kijiji cha Usagali wilayani Nzega wakati Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey akiwa katika ziara ya kutembelea Vyama vya Ushirika kuhimiza upandaji miti kupitia ushirika kwa ajili ya kurudisha uoto wa asili na kukifanya kilimo cha tumambaku kiwe rafiki kwa mazingira.

Mmoja wa wakulima Peter Mashoto alisema kuwa waliokuwa Viongozi wa Usagali na wajumbe wa Bodi wanatuhumiwa kulipwa fedha na Kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco Company (TLTC) lakini wao walishindwa kuwalipa wakulima waliouza tumbaku yao na kuzichua wao kwa ajili ya matumizi binafsi.

Aliongeza kuwa wakulima waliodhulumiwa fedha hizo wameendelea kuishi maisha ya dhiki wakati watuhumiwa wanaendelea kuishi maisha mazuri na kujiendeleza wao binafsi huku wao wakishinda hata kuwaeneleza watoto wao kielimu.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa sasa wa Usagali AMCOS Alphonce Sylvester aliomba Mrajisi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuwasaidia kusimamia madai ya wakulima ili waweze kulipa fedha zao na kuwarudishia matumini.
Alisema kuwa baadhi ya wakulima wanaolima zao hilo yamekata tamaa baada ya kuona fedha za msimu msimu 2015/2016 hawajalipwa na kuona kuwa vitendo vya namna hiyo vinaweza kuendelea.

Sylvester aliongeza kuwa ili kurudisha matumaini kwa wakulima ni vema Serikali isaidie kusimamia ili haki itoewe na wakulima waweze kupata fedha zao.Kufuatia kilio hicho cha wakulima hao, Mkuu wa Tabora Mwanri aliwaagiza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega kwa kushirikiana na Ofisi ya Mrajisiri Mkoa kufuatilia suala hilo na kuoana limekwamia wapi ili wakulima waweze kupatiwa haki yao kama madai yao ni halali.

Aliongeza kuwa ni jukumu lao kuhakikisha wanawashika mkono wakulima walidhulumiwa ili hatua dhidi wahusika zichukuliwe kwa ajili ya kuhakikisha haki inatendeka.Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Jacob Ntalitinya aliahaidi kushirikiana na viongozi wa Ushirika kushughulikia tatizo hilo lilikwamia wapi ili wakulima wapate fedha zao na wahusika wachukuliwe hatua zinazostahili.

KESI YA UHUJUMU UCHUMI YA VIGOGO WATATU WA SIX TELECOMS YAPIGWA KALENDA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeipiga kalenda kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wa Kampuni ya mawasiliano ya Six Telecoms, akiwemo Wakili Dk Ringo Tenga na wenzake kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.

Mbali na Dk. Tenga, washitakiwa wengine ni Mfanyabiashara Peter Noni, Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Hafidhi Shamte, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo, Noel Odeny Chacha na Kampuni ya Six Telecoms Limited.

Wakili wa Serikali, Leonard Challo alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi bado unaendelea.

Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 26, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.Katika kesi hiyo namba 73 ya 2017, inadaiwa kati ya January 1, 2014 na January 14,2016 Dar es Salaam washitakiwa, walitoza malipo ya simu za kimataifa kwa kiwango cha dola 0.25 kwa dakika kwa lengo la kujipatia faida.

Pia washtakiwa hao wanadaiwa katika tarehe hizo, washtakiwa waliisababishia TCRA hasara ya Dola za Marekani 3,736,861, sawa na Sh bilioni nane
Pichani ni Watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo hao Watatu wa Kampuni ya mawasiliano ya Six Telecoms, akiwemo Wakili Dk Ringo Tenga na wenzake wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema leo .

WANANCHI NJOMBE WAKIRI KUKWAMA KATIKA BAADHI YA HUDUMA KWA KUKOSA VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
Wananchi wa mkoa wa Njombe wameonyesha mwamko mkubwa kujitikoza kwa wingi kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa wakielezea namna wanavyotegemea kuvitumia katika kupata huduma mbalimbali za kijamii.

Wilaya ya Njombe Halmashauri ya Mji wa Makambako, ambako zoezi la usajili linaendelea hivi sasa, wananchi wengi wamekiri kupoteza muda wao mwingi kufuatilia kupata vitambulisho vya Taifa kutokana na Umuhimu mkubwa wa Vitambulisho hivyo katika huduma mbalimbali za kijamii.

Bwana Alphonce Mtengela mkazi wa Njombe akiwa anasubiri kupata huduma amesema “Sasa hivi kila mahali wanahitaji Kitambulisho cha Taifa ili waweze kukuhudumia, nimekwama kuchukua Mkopo baada ya kutokuwa na Kitambulisho cha Taifa hivyo kuna haja ya kuwa nacho ili iwe rahisi kutambulika katika huduma za Kijamii”

Wananchi wa Mkoa wa Njombe katika Wilaya za Njombe, Ludewa, Wanging’ombe, Makete na Makambako wanaendelea na zoezi la Usajili utakaomalizika mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.
Ndugu Nicholaus Lugandu mkazi wa Kijiji cha Ikelu Kata ya Ikelu Wilaya Njombe akichukuliwa alama za Vidole wakati akipatiwa huduma ya usajili na Utambuzi uliohusisha uchukuaji wa alama za Kibaiologia, saini ya Kielektroniki pamoja na Picha, zoezi linaloendelea hivi sasa katika Wilaya ya Njombe Halmashauri ya Mji wa Makambako.
Wakazi wa Kijiji cha Lyamkena Halmashauri ya Mji Makambako wakiwa nje ya Moja ya kituo cha Usajili wilayani Njombe wakisubiri kupatiwa huduma ya Usajili na Utambuzi ili kupatiwa Vitambulisho vya Taifa.
Bwana Alphonce Mtengela wa Kijiji cha Lyamkena Kata ya Lyamkena Wilaya Njombe akichukuliwa alama za Vidole wakati akipatiwa huduma ya usajili na Utambuzi uliohusisha uchukuaji wa alama za Kibaiologia, saini ya Kielektroniki pamoja na Picha, zoezi linaloendelea hivi sasa katika Wilaya ya Njombe Halmashauri ya Mji wa Makambako.
Bi. Anusiata Mwakalebela mwananchi mkazi wa wa Kijiji cha Lyamkena Kata ya Lyamkena Wilaya Njombe akichukuliwa alama za Vidole wakati akipatiwa huduma ya usajili na Utambuzi uliohusisha uchukuaji wa alama za Kibaiologia, saini ya Kielektroniki pamoja na Picha, zoezi linaloendelea hivi sasa katika Wilaya ya Njombe Halmashauri ya Mji wa Makambako.


KILIMANJARO MARATHON 2018 YAZINDULIWA RASMI MOSHI

$
0
0
Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 ambayo ni ya 16 tangu kuanzishwa kwake, imezinduliwa rasmi Kibo Palace Homes kwa kushirikisha wadhamini, Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro (KAAA) na waandaaji wa mbio hizo.
Akizindua mbio hizo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira aliwapongeza wadhamnini na waandaaji wakiongozwa na Kilimanjaro Premium Lager 42km, Tigo-21km Grand Malt 5km na wadhamini wengine wa meza za maji kwa kazi nzuri kwani wamezifanya mbio hizi ziwe maarufu kabisa tangu kuanishwa kwake miaka 16 iliyopita na hivi kufanya Moshi na Kilimanjaro kwa ujumla ifahamike na watu kutaka kupatembelea. 
Mkuu wa Mkoa huyo alitoa wito kwa wafanya biashara kutumia fursa hii vizurikwani wakati huu wa Kilimanjaro Marathon ndio muda wa kufanya biashara tofauti tofauti kutokana na wingi wa watu huku pia akiwataka washiriki hasa wanaotokea Kilimanjaro kuonesha mfanomzurikwa kushinda zawadi nyingi iwezekanavyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira akizindua Kili Marathon 2018 Kibo Palace Homes Moshi huku akiwa na viongozi na wadhamini wa mbio hizo.

“Ofisi yangu iko tayari kabisa kushirikiana na nyinyi na kuwa mwenyeji wa tukio hili muhimu kwani tutahakikisha kuna usalama wa kutosha ili washiriki wawe salama na amani wakati wote wa mashindano,” alisema huku pia akitoa raikwa washiriki kuhakikisha wanatembelea vivutio mbalimbali vya utalii ndani na nje ya Kilimanjaro baada yam bio hizo. 
Alipongeza wadhamini wengine wakiwemo First National Bank, Kilimanjaro Water, Diamond Motors Ltd, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Simba Cement, KNAUF Gypsum, AAR ambao ndio wabia rasmi wa matibabu, Kibo Palace Hotel iliyodhamini uzinduzi huo na waandaaji Wild Frontiers, Deep Blue Media na Executive Solutions ambao ni waratibu wa kitaifa. Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja Masoko, Udhamini, Habari na Promosheni wa TBL Group (Afrika Mashariki, George Kavishe alisema Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kudhamini mbio hizo kwa miaka 16 sasa kutokana na weledi na uzoefu mkubwa wa waandaaji ambao wamefanya mbio hizoziwe maarufu sana na moja ya matokeo makubwa nchini. Meneja Masoko, Udhamini, Habari na Promosheni wa TBL Group (Afrika Mashariki, George Kavishe akizungumza katika uzinduzi huo.
Alisema kwa mwaka huu, Kilimanjaro Premium Lager imejiandaa vizuri kwani itatoa zawadi zenye thamani ya Tsh milioni 20 ambapo mshindi wa kwanza wa mbio za kilometa 42 kwa upande wa mshiriki mwanaume na mwanamke watapata tsh milioni 4 kila mmoja. Alisema mbio maarufu zakilometa 5 maarufu kama Fun Run, zinazodhaminiwa na Grand Malt pia zitafanyika ambapo watu wa rika zote wanaruhusiwa kushiriki. 
“Hizi ni mbio za kujifurahisha kwa hivyo watu wa rika zote wanakaribishwa kushiriki ili pia iwe kama sehemmu ya mazoezi huku wakipata kinywaji chao cha Grand malt chenye afya tele,” alisema. Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo akizungumza kwenye uzinduzi wa hafla hiyo.
Kaimu Mkurueni wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo alisema wamejiandaa vizuri kwa kilometa 21 na kuwataka washiriki wajiandikishe kwa wakati kwani mbio hizo zimekuwa maarufu sana na hii imewapasababu zaidi ya kuendelea kudhamini mbio hizo. 
Alisema katika mwaka wake wan ne wa udhamini, Tigo itatoa zawadi zenye thamani ya Tsh Milioni 11 ambapo washindi wa kwanza hadi 10 watapata zawadi huku wa kwanza kwa upande wa wanaume na wanawake akipata Milioni 2 kila mmoja na kuongeza kuwa washiriki wote watakaomaliza mbio hizo watapata medali.  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira akiwa na wadhamini wa Kilimanjaro Marathon 2018.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wild Frontiers ambaye pia ni Muandaaji wa mbio hizo, John Addison alisema maandalizi yote yamekamilika na mbio za mwaka huu zitafanyika katika Machi 4 katika Chuo Cha Ushirika Moshi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi ambapo mbio za kilometa 42 zinatarajiwa kuanza. “Tunawashukuru mno wadhamini wetu kwa kutuunga mkono kwani tunatarajia kuwa mashindano ya mwaka huu yatakuwa makubwa na ya kusisimua zaidi,” alisema.

TANROADS WAAGIZWA KULETA MZANI MAKAMBAKO

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa ameuagiza uongozi  Wakala wa Barabara (TANROADS), Makao makuu kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja  wanaweka mzani mwingine wa kuhamishika katika eneo la mzani wa Makambako ili kuweza kutatua  changamoto ya msongamano wa magari katika eneo hilo.
Naibu Waziri huyo ametoa agizo hilo mkoani Njombe, mara baada ya kufika katika mzani huo ambapo amejionea changamoto zake na kusisitiza kuwa,  kuongeza mzani wa kuhamishika katika eneo hilo kutasaidia kupunguza kero hiyo ya msongammano wakati Serikali ikitafuta ufumbuzi wa kudumu wa kujenga mzani mwengine katika eneo hilo.
"Naagiza TANROADS Makao makuu mfanye kila linalowezekana  ndani ya mwezi mmoja mlete mzani wa  kuhamishika hapa Makambako,  tunataka tutoe huduma ya haraka kwa madereva  ili  pasiwe na  msongamano katika eneo hili", amesema Naibu Waziri Kwandikwa.
Amewaonya wale madereva wote wanaotumia kisingizio cha uwepo wa foleni  katika mzani  huo kwa kufanya mambo yao binafsi kuacha mara moja tabia hiyo, kwani ikibainika kwa dereva yeyote ambae ameshapatiwa huduma lakini bado ameegesha gari lake katika eneo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria dhidi yake.
Ameagiza Taasisi zote zinazotoa huduma katika mzani huo kushirikiana na kuandaa maoni yao kuhusu namna ya kupunguza msongamano katika mzani huo na kuyawasilisha Wizarani ili yaweze kufanyiwa kazi.
Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Njombe, Mhandisi, Yusuph Mazana, ametaja baadhi ya changamoto zilizopo katika Mzani huo kuwa ni kuharibika kwa mzani mara kwa mara kutokana na mzani huo kuwa ni wa siku nyingi na kuwepo na muingiliano wa huduma kutoka Taasisi mbalimbali za serikali kama  Uhamiaji, Polisi na TRA.
Ameongeza kuwa changamoto nyingine ni baadhi ya magari kuegeshwa nje ya maeneo ya mzani baada ya kupima na hivyo kusababisha msongamano wa magari yanayotakiwa kuingia ndani ya eneo la mzani kwa ajili ya kupata huduma ya upimaji au kufanya taratibu nyingine.
Naibu Waziri Kwandikwa amemaliza ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ambapo alipata fursa ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali   inayotekelezwa na Sekta yake.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akizungumza na wafanyakazi wa mzani wa Makambako, wakati alipotembelea mzani huo kufahamu changamoto wanazozipata katika utendaji wao wa kazi, Mkoani Njombe. 
Muonekano wa mzani wa Makambako, mkoani Njombe, wenye uwezo wa kudhibiti uzito wa magari makubwa yanayozidi 3500kg (tani 3.50). 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

MTANDAO WA KIJAMII WAJITOLEA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Globu ya jamii
MTANDAO wa kijamii wa kuutangaza utalii wa Deiplaces umesema umejipanga vema kutoa taarifa sahihi za vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Deiplaces Dk.Paul Bamutaze amesema kwa kutumia mtandao huo watakuwa wakitoa taarifa mbalimbali zinazohusu utalii wa Tanzania ambapo taarifa hizo zitasomwa na watu wa mataifa mbalimbali duniani.

Amesema wanatambua juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuutangaza utalii pamoja na vivutio vilivyopo lakini nao wameona ipo haja ya kusaidia kutangaza utalii uliopo nchini Tanzania.

"Tumekuja Tanzania kwa ajili ya kuanzisha mtandao wa kijamii ambao utakuwa ukihusika na utoaji taarifa sahihi zinazohusu utalii na vivutio vilivyopo. Lengo letu ni kufanikisha kila anayetaka kufahamu kuhusu Tanzania na vivutio vyake vya utalii basi apate kutoka kwetu.

"Pia mtandao huu utakuwa sehemu sahihi ya hata vyombo vya habari ambavyo vinataka kupata habari sahihi zinazohusu utalii basi watazikuta kwetu.

"Hakutakuwa na gharama yoyote unapotaka kupitia taarifa za utalii ambazo tunakuwa tunaziweka,"amesema. Dk.Bamutaze amefafanua unapotaka kuzungumzia Mlima wa Kilimanjaro hakuna ambaye hajui historia yake, na hivyo wao watakapoamua kutoa habari za mlima huo watajikita kuelezea maisha ya watu wanaouzunguka mlima huo pamoja na mazingira yake.

Amesema unapotaka kuizingumzia mbuga ya Serengeti ambayo ina kila aina ya vivutio vya utalii basi lazima taarifa ziwe zenye ukweli na si za kupotosha. Amefafanua wamekuwa wakitangaza utalii wa nchi mbalimbali za Afrika na sasa wanataka kujikita Tanzania.
Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa deiplaces Dk.Paul Bamutaze akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kutoa taarifa sahihi za vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania.

WATOA HUDUMA ZA MAWASILIANO ZINGATIENI SHERIA- NDITIYE

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amesema watoa huduma za mawasiliano nchini lazima wafuate sheria zilizowekwa ili kutoa huduma bora za mawasiliano kwa walaji.

Mhandisi Nditiye ameyasema hayo katika uzinduzi wa mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bdhaa za mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)wakati wa mkutano wa wadau jijini Dar es Salaam.

Amesema TCRA isiache kuwachukulia hatua watoa huduma wanaokwenda kinyume na sheria za leseni ya utoaji wa huduma za mawasiliano nchini. Amefanunua kitabu cha mwongozo kinatoa elimu kuhusu kutatua cha changamoto za mawasiliano na njia za kufuata pale wanapoona taarifa tofauti katika matumizi ya mawasiliano.

Kwa upande wa Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo na Sanaa, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuingia kwa teknolojia kumefanya kwenda kisasa tofauti na miaka ya nyuma .

Amesema katika tekonolojia ya Tehama wajasiriamali wengi wanaitumia katika kujiingizia kipato ambapo lazima watoe maudhui yanayoendana katika sheria zilizowekwa. MKurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema mwongozo uliopo katika kitabu hicho utasaidia kutatua changamoto za mawasiliano kwa watumiaji kujua njia za kufuata pindi wanapoona taarifa tofauti.
 Naibu Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza katika uzinduzi wa mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Dk.Harrison Mwakyembe akizungumza katika uzinduzi wa mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kuhusu sekta ya utangazaji , leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba akitoa taarifa za uandaji wa kitabu cha mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano na sekta ya utangazaji , leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa,Dk. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandisi Atashasta Nditiye wakiwa wameshika vitabu kuashiria uzinduzi wa kitabu cha mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano, jijini Dar es Salaam.
 Msanii Mrisho Mpoto maarufu Mjomba akitumbuiza kwenye uzinduzi wa kitabu cha mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano , leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa  kitabu cha mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano , leo jijini Dar es Salaam.

MTANDAO WA KIJAMII WAJITOLEA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA

$
0
0
MTANDAO wa kijamii wa kuutangaza utalii wa deiplaces umesema wamejipanga vema kutoa taarifa sahihi za vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania. 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam,Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa deiplaces Dk.Paul Bamutaze amesema kwa kutu mia mtandao huo watakuwa wakitoa taarifa mbalimbali zinazohusu utalii wa Tanzania ambapo taarifa hizo zitasomwa na watu wa mataifa mbalimbali duniani.

Amesema wanatambua juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuutangaza utalii pamoja na vivutio  vilivyopo lakini nao wameona ipo haja ya kusaidia kutangaza utalii uliopo nchini Tanzania.

"Tumekuja Tanzania kwa ajili ya kuanzisha mtandao wa kijamii ambao utakuwa ukihusika na utoaji taarifa sahihi zinazohusu utalii na vivutio vilivyopo.Lengo letu ni kufanikisha kila anayetaka kufahamu kuhusu

Tanzania na vivutio vyake vya utalii basi apate kutoka kwetu. "Pia mtandao huu utakuwa sehemu sahihi ya hata vyombo vya habari ambavyo vinataka kupata habari sahihi zinazohusu utalii basi watazikuta kwetu.

"Hakutakuwa na gharama yoyote unapotaka kupitia taarifa za utalii ambazo tunakuwa tunaziweka,"amesema. Dk.Bamutaze amefafanua unapotaka kuzungumzia Mlima wa Kilimanjaro hakuna ambaye hajui historia yake ,na hivyo wao watakapoamua kutoa habari za mlima huo watajikita kuelezea maisha ya watu wanaouzunguka mlima huo pamoja na mazingira yake.

Amesema unapotaka kuizingumzia mbuga ya Serengeti ambayo ina kila aina ya vivutio vya utalii basi lazima  taarifa ziwe zenye ukweli na si za kupotosha. Amefafanua wamekuwa wakitangaza utalii wa nchi mbalimbali za Afrika na sasa wanataka kujikita Tanzania.
.Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa deiplaces Dk.Paul Bamutaze akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kutoa taarifa sahihi za vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania.

WATOA HUDUMA ZA MAWASILIANO ZINGATIENI SHERIA- NDITIYE

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

NAIBU Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amesema watoa huduma za mawasiliano nchini lazima wafuate sheria zilizowekwa ili kutoa huduma bora za mawasiliano kwa walaji.

Mhandisi Nditiye ameyasema hayo katika uzinduzi wa mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bdhaa za mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)wakati wa mkutano wa wadau jijini Dar es Salaam.

Amesema TCRA isiache kuwachukulia hatua watoa huduma wanaokwenda kinyume na sheria za leseni ya utoaji wa huduma za mawasiliano nchini. Amefanunua kitabu cha mwongozo kinatoa elimu kuhusu kutatua cha changamoto za mawasiliano na njia za kufuata pale wanapoona taarifa tofauti katika matumizi ya mawasiliano.

Kwa upande wa Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo na Sanaa, Dk.Harrison Mwakyembe amesema kuingia kwa teknolojia kumefanya kwenda kisasa tofauti na miaka ya nyuma .

Amesema katika tekonolojia ya Tehama wajasiriamali wengi wanaitumia katika kujiingizia kipato ambapo lazima watoe maudhui yanayoendana katika sheria zilizowekwa. MKurugenzi Mkuu wa TCRA,Mhandisi James Malaba amesema mwongozo uliopo katika kitabu hicho utasaidia kutatua changamoto za mawasiliano kwa watumiaji kujua njia za kufuata pindi wanapoona taarifa tofauti.
 Naibu Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza katika uzinduzi wa mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Dk.Harrison Mwakyembe akizungumza katika uzinduzi wa mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kuhusu sekta ya utangazaji , leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa TCRA,Mhandisi James Malaba akitoa taarifa za uandaji wa kitabu cha mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano na sekta ya utangazaji , leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa,Dk. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandisi Atashasta Nditiye wakiwa wameshika vitabu kuashiria uzinduzi wa kitabu cha mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano, jijini Dar es Salaam.
 Msanii Mrisho Mpoto maarufu Mjomba akitumbuiza kwenye uzinduzi wa kitabu cha mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano , leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa  kitabu cha mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano , leo jijini Dar es Salaam.

Waafrika wazidi kuteswa Libya

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 19, 2018. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga, na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Zanzibar Balozi Ali Karume,
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisikiliza hoja zikitolewa na Balozi Celestine Mushi wakati alipoongea na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 19, 2018. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 19, 2018. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji  wa Zanzibar Balozi Ali Karume, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi Muombwa, Mkurugenzi wa Idara ya Usalama a Taifa Dkt. Modestus Kipilimba na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisikiliza hoja wakati alipoongea na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 19, 2018. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Zanzibar Balozi Ali Karume, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi Muombwa, Mkurugenzi wa Idara ya Usalama a Taifa Dkt. Modestus Kipilimba na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James wakati alipoongea na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 19, 2018. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Zanzibar Balozi Ali Karume, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi Muombwa, Mkurugenzi wa Idara ya Usalama a Taifa Dkt. Modestus Kipilimba.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga wakifurahia jambo baada ya Mhe. Rais kuongea na watumishi wa Wizara hiyo kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 19, 2018. Picha na IKULU

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA SERENGETI NA BUNDA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti cha shukurani, Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengti, Bw. William Mwakileme kutokana na mchango mkubwa wa hifadhi hiyo katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Robada wilayani Serengeti. Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika ziara ya mkoa wa Mara Januari 19, 2017. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara, Samweli Kiboyi.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha  Hunyari baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa wodi ya wazazi katika zahanati  hiyo wilayani Bunda Januari 19, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. akikagua mashine za kusukuma maji wakati  alipoembelea mradi wa chanzo cha maji Bunda akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara, Januari 18, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizindua ushirika wa Igembe Sabo wilayani Bunda akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara, Januari 19, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfereji wa maji wakati alipozindua chama cha ushirika cha Igembe Sabo kinachojishughulisha na kilimo cha mpunga  wilayani Bunda Januari 19, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwakabidhi  hati ya usajili wa chama viongozi  wa chama cha ushirika cha Igembe Sabo cha Bunda , Malongo Mashimo ambaye ni Katibu (kulia) na Maria Nengwa ambaye ni Mwenyekiti wa Ujenzi baada ya  kuzindua ushirika huo akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara, Januari 19, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KIWANDA CHA DANGOTE CHAAGIZWA KUWALIPA KWA WAKATI WACHIMBAJI WA JASI

$
0
0
Kampuni ya Saruji ya Dangote imetakiwa kuwalipa kwa wakati Wachimbaji wa Madini ya Jasi ili kuwawezesha kulipa kodi zao kwa Serikali kulingana na taratibu zilizopo.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko alipotembelea kiwandani hapo wakati wa ziara yake ya kutembelea Mikoa ya Lindi na Mtwara.Naibu Waziri amesema kuwa, lazima Wachimbaji Wadogo wapate malipo yao kwa wakati baada ya kuuza madini ili kuwawezesha kulipa kodi za Serikali pamoja na kurejesha mikopo yao kwa wakati katika Benki walizokopa.

Pia, Naibu Waziri Biteko ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kuandaa rasimu ya Mkataba ndani ya kipindi cha wiki mbili na kueleza kuwa, kuwepo kwa mkataba huo ambao kutawawezesha Wachimbaji wadogo wa madini ya Jasi kutatua changamoto zilizopo baina yao na Kiwanda husika.

“Andaeni rasimu ya mkataba ili kila moja auze madini yake kwa bei inayoeleweka bila kuoneana na kila moja apate faida anayostahili,” amesema Biteko.Ameongeza kuwa zipo changamoto za Wachimbaji wadogo kutokuwa na umoja na hivyo kuwataka kuwa na umoja ili waweze kufanikiwa katika shughuli zao ikiwemo kuwepo na bei moja ya madini yao.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa pili kushoto) akisaini kitabu cha wageni katika ukumbi wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote wakati alipofanya ziara yake kiwandani hao. Wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Mayigi Makolobela. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtwara Vijijini, na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mitambo ya Uzalishaji Kiwanda cha Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha.
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Mayigi Makolobela akimweleza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa nne kulia) katika eneo la uzalishaji la Block 1 la Kiwanda cha Saruji cha Dangote. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mitambo ya Uzalishaji, Hemendra Raithatha (mwenye suti nyeusi). Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo wa Jasi, Peter Ludvick, Wafanyakazi wa Wizara ya Madini, Wafanyakazi wa Kiwanda cha Dangote na Uongozi wa Wachimbaji Wadogo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (mbele) akiongoza kikao baina yake na Uongozi na Wafanyakazi wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote, Wafanyakazi wa Wizara ya Madini, pamoja na Uongozi wa Wachimbaji wa Madini ya Jasi.

INTRODUCING: CHIBWA & TANAH TANCHY - ALONE (OFFICIAL VIDEO)

UTEUZI WA KATIBU MTENDAJI TCU


MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WADAU WA MAZINGIRA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameongoza kikao cha Wadau wa Mazingira kuhusu Changamoto ya Mafuriko na Hifadhi ya Mazingira katika mkoa wa Dar es Salaam, kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliopo kwenye ofisi ya Makamu wa Rais mtaa wa Luthuli.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam kuchukua hatua za haraka katika kukabiliana na mafuriko katika jiji la Dar es Salaam.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa mkutano na Wadau wa Mazingira kuhusu changamoto ya mafuriko na hifadhi ya mazingira katika mkoa wa Dar es Salaam.

Makamu wa Rais alisema kulikosekana umakini katika kusimamia mazingira na miundo mbinu katika jiji la Dar es Salaam.

Makamu wa Rais alizungumzia changamoto za kuwepo kwa taka ngumu ambazo zingeweza kuzalisha umeme na gesi, “kuna miradi watu wanaomba kuzalisha umeme kwa taka, anazungushwa mtu miaka mitano, sita , saba, haambiwi ndio wala haambiwi hapana “

Makamu wa Rais amesema kuna uhitaji sana wa elimu ya mazingira kwa jamii na kupeana taarifa mbali mbali zinazohusiana na mazingira .

Makamu wa Rais alisema moja ya tatizo kubwa ni kuchukua nyezo za uthibiti kufanya nyenzo za mapato “Vibali, leseni hivi ni vitu vinavyotolewa kwa ajili ya uthibiti lakini tumevigeuza kuwa vyombo vya mapato” kutokana na hali hiyo vibali vimeendelea kutolewa hovyo bila kuzingatia taratibu.

Makamu wa Rais alitoa maagizo ya kuundwa kwa Kamati ya Mazingira ya mkoa wa Dar es Salaam ambayo itaundwa na  Waziri wa Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na kuratibiwa  na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda.

Makamu wa Rais aliwashukuru wadau wa maendeleo wakiongozwa na Benki ya Dunia katika kusaidia kupambana na tatizo la uharibifu wa mazingira na mafuriko jijini Dar es Salaam.

Awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba alisema ni wakati wa kutafakari na kupata jawabu la kudumu la suala la mafuriko yanayotokea katika jiji la Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Wadau wa Mazingira kuhusu Changamoto ya Mafuriko na Hifadhi ya Mazingira katika mkoa wa Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


PROF. CHARLES KIHAMPA APPOINTED EXECUTIVE SECRETARY OF THE TCU

SERIKALI YAKATAZA KULIMA PAMBA KWA MKATABA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imekataza kilimo cha pamba cha mkataba kwa sababu kinawanyonya wakulima.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Januari 19, 2018) wakati akizungumza na wananchi baada ya kukagua zahanati ya Hunyari wilayani Bunda, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mara.

“Ni marufuku kwa wanunuzi wa pamba kulima pamoja na wakulima kwa sababu wakulima wanakosa uamuzi wa kupanga bei. Kuanzia sasa zao hilo litauzwa kwa njia ya mnada.”Amesema Serikali imeweka mkakati wa kuimarisha mazao makuu ya biashara ambayo uzalishaji wake umeanza kupungua likiwemo na zao la pamba.Waziri Mkuu amesema Serikali imeamua kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa kilimo cha zao la pamba kuanzia hatua za maandalizi ya shamba, pembejeo hadi masoko.

Pia Waziri Mkuu amewaagiza Maofisa Kilimo katika wilaya hiyo wawafuate wakulima vijijini kwa ajili ya kutoa elimu itakayowawezesha wakulima kulima kwa kufuata njia bora za kisasa.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wafugaji kuhakikisha wanakuwa na idadi ya mifugo kulingana na uwezo wa eneo lao.“Marufuku kulisha mifugo katika mashamba ya watu.”

Amesema Serikali itachukua hatua kali za kisheria kwa mfugaji yeyote atakayelisha mifugo yake katika mashamba ya wakulima kwani tabia hiyo huchangia migogo baina yao.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
IJUMAA, JANUARI 19, 2018.

Ajipanga Kutembea Hadi Magogoni Kuunga Mkono Juhudi za Rais Magufuli

$
0
0

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Kijana mzalendo, Omary Kombe amejipanga kutembea kutoka Kimara hadi Kivukoni siku ya Jumamosi, Januari 20, 2018 ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika kuliletea Taifa maendeleo.

Kombe ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya nia ya matembezi yake pamoja na mpango wake wa kutoa tuzo kwa Rais Magufuli itakayojulikana kama ‘Tuzo ya Kiongozi Mzalendo’.

Kombe amesema kuwa Rais Magufuli amekuwa ni kiongozi makini, mwenye uthubutu, mwenye msimamo thabiti na mzalendo wa kweli kwani amefanya mambo mbalimbali yakiwemo ya kuimarisha mfumo wa ulipaji kodi, kubadilisha sheri kandamizi za madini, kukomesha vitendo vya ujangili katika mbuga za wanyama, rushwa na dawa za kulevya pia kurejesha nidhamu kwa watumishi wa umma.

“Kubwa kuliko yote, Serikali ya Awamu wa Tano kwa ujumla imekuwa ikihamasisha kwa vitendo kuhusu ujenzi wa Tanzania ya Viwanda na kupelekea nchi kuwa na uchumi wa kati hivyo kwa niaba ya vijana wazalendo napenda kumpongeza kwa kufanya matembezi, kumpa tuzo ya kiongozi mzalendo pamoja na kutoa msaada katika hospitali ya Ocean Road iliyopo jijini hapa,” alieleza Kombe.
Kijana Mzarendo,Omary Kombe akizungumzana na waandishi wa hawapo pichani juu ya kutembea kutoka Kimara hadi Kivukoni siku ya Jumamosi, Januari 20,mwaka huu ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika kuliletea Taifa maendeleo, Mwenyekiti Mwenza Kamati ya Kutoa Elimu ya Unyonyaji kwa Watu Wenye Ualbino, Maiko Lugendo.
Mwenyekiti Mwenza Kamati ya Kutoa Elimu ya Unyonyaji kwa Watu Wenye Ualbino,Maiko Lugendo akimkabdhi Kijana Mzarendo,Omary Kombe t-shirt atakayo vaakesho kwaajili ya matembezi hayo.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.


SABABU ILIYOMUWEKA PEMBENI KWA MUDA MSANII NURU THE LIGHT

Viewing all 110129 articles
Browse latest View live




Latest Images