Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

AZAM YAMINYWA NA MAJIMAJI, YAKUBALI SARE YA 1-1

$
0
0
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Majimaji katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliofanyika leo mchana kwenye Uwanja wa Majimaji, mjini Songea mkoani Ruvuma.

Sare hiyo inaifanya Azam FC kufikisha pointi 27 na kuwa katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi baada ya   Simba kupata ushindi dhidi ya Singida na kukaa  kileleni kwa pointi 29.

Azam FC ndiyo iliyoanza kuliona lango la Majimaji dakika ya 30 kupitia bao safi la winga Joseph Mahundi, aliyeunganisha kiustadi pasi safi ya mshambuliaji Yahya Zayd, bao lililodumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

Kipindi cha pili Azam FC iliwaingiza nyota kadhaa kwenye dakika tofauti wakiingia viungo Frank Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na mshambuliaji Shaaban Idd, ikiwatoa Bernard Arthur, Salmin Hoza na Idd Kipagwile, mabadiliko ambayo yaliongeza kasi ya mashambulizi wakati timu hiyo ilipokuwa ikishambulia.

Dakika ya 73 Majimaji iliweza kusawazisha bao hilo kupitia kwa Marcel Boniventure, aliyepiga mpira wa moja kwa moja wa kona uliojaa wavuni na kufanya matokeo kuisha kwa sare hiyo.

Kama Azam FC ingekuwa makini ingeweza kujipatia mabao mengine kupitia nafasi walizopoteza kwenye mchezo huo, kipindi cha kwanza kupitia kwa Bernard Arthur, kipindi cha pili ikipoteza nyingine kwa washambuliaji wake Yahya Zayd, Shaaban Idd na beki Yakubu Mohammed.

Mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Azam FC kinatarajia kuelekea mkoani Mbeya kesho Ijumaa asubuhi tayari kabisa kwenda kucheza na Tanzania Prisons, mchezo utakaofanyika Uwanja wa Sokoine Jumapili hii.

VIGOGO WIZARA MALIASILI, UTALII KORTINI KWA TUHUMA ZA KUSABABISHA HASARA DOLA 32,599

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii

WAFANYAKAZI watatu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka sita likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya dola 32,599.

Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini(Takukuru) Leonard Swai, amewataja washtakiwa hao ni, Ofisa Muhifadhi anayehusika na uwindaji wa matumizi endelevu ya wanyamapori Rajabu Hochi, Ofisa wa Muhifadhi mwenye wajibu wa kukusanya wa mapato ya uwindaji , Mohamed Madehele na Isaac Maji.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri imedaiwa kuwa, washtakiwa wakiwa watumishi kitengo cha Wanyamapori, walitenda makosa hayo katika makao makuu ya wizara hiyo.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali Pendo Temu amedai,kati ya Januari 12 na Desemba 31, mwaka 2008, makao makuu ya wizara hiyo, Hochi na Madehele wakiwa watumishi wa wizara hiyo, wakiwa na wajibu wa kukusanya mapato yanayotokana na uwindaji walitumia madaraka yao vibaya kwa kuzidisha wanyama pori kwa Kampuni ya Uwindaji ya Northern Hunting Enterprises (Tanzania) kinyume cha sheria na hivyo kuiwezesha kampuni hiyo kupata faida ya USD 250 isivyo halali.

Pia Hochi na Madehele, wanadaiwa kati ya Agosti 11 na Desemba 31, mwaka 2011, makao makuu ya wizara hiyo,waliiwezesha kampuni hiyo kujipatia dola za Marekani 250 isivyo halali.Aidha, Hochi na Madehele, wanadaiwa, kati ya Septemba 5 na Desemba 31,mwaka 2010, walishindwa kukusanya faini ya dola za Marekani 15,630 kutoka katika kampuni hiyo.

Pia washtakiwa Hochi na Madehele,wanadaiwa kushindwa kukusanya faini ya dola za Marekani 250 kutoka kampuni ya uwindaji ya Hunting Enterprises (Tanzania), kinyume cha sheria.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 18.01.2018

New full-length live video from Mzungu Kichaa's 2017 tour

SHUKURANI toka kwa familia ya MAREHEMU BADRIYA RAMADHAN KIONDO

$
0
0
Sisi, Familia ya Mrs Bdariya Ramadhan Kiondo (Aliekuwa Afisa waMambo ya Nje Mkuu na Mkuu wa Utawala na Fedha katika Ubalozi wa Tanzania New Delhi, India, tunamshukuru Mungu kwa zawadi aliotupa kwetu kama Mke,Mama,Bibi, Shangazi ,Ndugu na kwa mwili wa kumcha Mungu.
Tunashukuru kwa upendo mkuu,kwa kushiriki nasi katika kumsindikiza mpendwa wetu katika nyumba yake ya milele tarehe 15 Desemba  2017.Tunapenda kuwashukuru marafiki,ndugu, Wafanyakazi wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Watumishi wenzake katika Ubalozi wa Tanzania Nchini New Delhi,India, marafiki na Ndugu wote kutoka Nchi mbali  mbali Duniani,(hasa India,,Uingereza, Uholanzi, Canada, Oman UAE na USA).
Shukran za pekee pia ziwafikie Madaktari wake wote katika Hospitali ya Apollo New Delhi,Mwambata Tiba katika Ubalozi wetu New Delhi kwa juhudi kubwa waliofanya katika matibabu yake, Viongozi Wakuu mbali mbali Serikalini,Balozi na Wafanyakazi wa Ubalozi wetu New Delhi India,Uongozi na wafanyakazi wa Wizara ya mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika mashariki,Majirani wa Kiondoni Ada Estate flats, ndugu na jamaa wote kutoka Zanzibar,Tanga na Msikiti wa Al Maamur ,Upanga Dar es salaam. Asanteni Sana.
Kisomo cha 40 ya Marehemu kitakuwa  tarehe 27 January 2018 huko Mkwajuni, Kivunge Kijijini, kwa Foum Kimara, Zanzibar baada ya Swala ya Adhuhuri (Saa saba mchana). Wote mnakaribishwa kushiriki nasi.
Ni vigumu kumshukuru kila mmoja kwa majina tunaomba mlioshiriki kwa namna moja au nyingine mpokee shukrani  zetu hizi za upendo kwa kuwa nasi katika kipindi hiki kigumu.
Tunaendelea kuomba Roho ya mpendwa wetu “B”ipumzike kwa Amani na utakuwa nasi daima milele Amen.

Pumzika kwa Amanai Mpendwa wetu.                                    
Innalilah wainailah rajiun.

WAJUMBE BARAZA VYAMA VYA SIASA WAJADILI MAPENDEKEZO YA KUTUNGWA SHERIA MPYA

$
0
0
Na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

BARAZA la Vyama vya Siasa nchini limekutana na wajumbe wanaounda baraza hilo kwa lengo la kujadili mapendekezo  ya kutungwa kwa ya sheria mpya ya vyama vya siasa.

Akizungumza jana  jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa baraza hilo, John Shibuda amesema katika kujadili mapendekezo mjadala utaanzia katika kamati ya Baraza vyama vya siasa ‘Kamati ya sheria na Utawala Bora’ inaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Hassan Almas na Makamu Mwenyekiti, Sudd Said Sudd.

Alifafanua kuwa Kamati ya Sheria na utawala bora itapokea  mpango kitita katoka katika mawazo ya wanachama wa baraza hilo na kuongeza kuwa mchakato wa kutungwa kwa sheria mpya ya vyama vya siasa haujatendeka pamoja mchakato wa mapendekezo  ya sheria usajili wa vyama vya siasa.

Shibuda amesema baraza hilo liko huru bila kusukwa na mtu yeoyote.Amesema ndani ya wiki mbili inatakiwa kamati ya sheria na utawala bora iwe imekamilisha na baada ya hapo wiki mbili zingine iwe ni kwenda kamati ya baraza la vyama siasa inayoongozwa na Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa.
 Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini, John Shibuda (pili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao cho cha baraza la vyama vya siasa leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara), Philip Mangula akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao cha vyama vya siasa kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

 Sehemu ya viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wakifatilia ajenda katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii

DAWASCO YAGHARAMIA MATIBABU YA WALIOJERUHIWA KWA MOTO BUGURUNI

$
0
0
Na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii .


SHIRIKA la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam(DAWASCO), limeamua kugharamia matibabu kwa wananchi ambao wamepata majeraha mwilini kutokana na mlipuko wa moto ambao umetokana na kutoboka kwa bomba la gesi uliotokea maeneo ya Buguruni jijini Dar es Salaam, ambapo kwa sasa majeruhi hao wanaendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili. 

Akizungumza akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,Ofisa Habari wa Dawasco Everlasting Lyaro amesema wameamua kugharamia matibabu ya majeruhi hao baada ya kujiridhisha ni kweli wamepata majeraha kutokana na mlipuko wa moto ambao ulitokana na kutobolewa kwa bomba la gesi.

Amesema kuwa wafanyakazi wa Dawasco wakiwa katika eneo hilo la Buguruni wakiendelea na shughuli zao za kuziba bomba la maji la nchi 10, kwa bahati mbaya wakatoboa bomba la gesi na kusababisha moto kuanza kuwaka na kuleta madhara kwa baadhi ya wananchi waliokuwa eneo hilo. 

"Watu ambao wamepata majeraha kutokona na mlipuko huo wa moto uliotokea Buguruni ni watatu.Hivyo tumefika Hospitali ya Taifa Muhimbil kwa ajili ya kuwasalimia na kuwapa pole na kubwa zaidi ni kugharamia matibabu yao wakiwa hospitalini hapo,"amesema.

Mmoja wa wakazi wa eneo la Buguruni jijini Mariam Rubaa ambaye watoto wake wawili wamepata majeraha kutokana na kuungua moto amesema anaishukuru Dawasco kwa msaada huo wa matibabu kwa waliojeruhiwa na kuongeza kilichotokea ni ajali kwani hakuna aliyetarajia kama moto ungetokea eneo hilo na kusababisha madhara kwa wananchi. 
 Mmoja wa wahanga wa mlipuko wa moto ambao ulitokana na kutobolewa kwa bomba la gesi akiwa kwenye gari la wagonjwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tayari kwa kupatiwa matibabu

Mmoja wa wahanga wa mlipuko wa moto ambao ulitokana na kutobolewa kwa bomba la gesi akishushwa kwenye gari la wagonjwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tayari kwa kupatiwa matibabu. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

WIZARA YA ARDHI YADHAMIRIA MIJI MIKUU NCHINI KUWA KWENYE MPANGILIO MZURI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI wa Mipango Miji Mijini na Vijijini kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa John Lupala amesema Serikali imejipanga vema kuhakikisha miji mikuu nchini inakuwa katika mpangilio unaotakiwa huku akifafanua ipo haja ya kushirikisha sekta binafsi katika kufanikisha mkakati huo.

Prof.Lupala ametoa kauli hiyo jana  jijini Dar es Salaam alipokutana na wadau mbalimbali katika mkutano wa majadiliano wa namna inayoweza kufanikisha mkakati wa Serikali kupitia Wizara hiyo kufanikisha kupangilia miji mikuu yote nchini huku akielezea pia mkakati wa miaka 10 uliopo ambao utahusisha kupima , kupanga na kumilikisha.

Akizungumza zaidi kuhusu ambavyo wamejipanga kuhakikisha miji mikuu inakuwa katika mpangilio unaotakiwa amesema kuna mikakati mbalimbali ya kufanikisha mchakato huo ambapo upo wa miaka mitano na ule wa miaka 10.

Amesema kwa kushirikiana na wadau ambao wanahusika na masuala ya mipango miji wanaamini wataharakisha kuweka mpangilio mzuri wa miji ili wananchi sasa waweze kufuata, tofauti na siku za nyuma ambapo wananchi walikuwa wanatangulia kuanzisha mji halafu namna ya kuupangilia mji 
unachelewa.

Amesema mkakati wa kufanikisha mpangilio wa miji ni wa kitaifa ingawa kuna baadhi ya maeneo tayari wamekamilisha kupanga mji na kuongeza wataendelea kufanya hivyo katika maeneo yote.Profesa Lupala amesema anatambua kuna changamoto ya wananchi kutokuwa na uwezo wa kujenga kulingana na namna ambavyo wizara inataka lakini ifahamike kuwa wamejipana vema kuhakikisha kunakuwa na miji ambayo itakuwa imepangika.

"Niseme tu kama wizara tumejipanga vilivyo na katika kipindi hiki cha miaka mitano lazima tuwe na Master plan' ambayo sasa itatuongoza na ukishakuwa nayo inakuwa rahisi kushirikisha wadau kuangalia namna ya kuiharakisha."Kuna kampuni zaidi ya 60 za upimaji na upangaji na tunaamini tukiwashirikisha tutakwenda kwa kasi zaidi.Ifahamike Master Plan haindaliwi na Wizara bali ni kazi ya halmashauri ni kazi yetu ni kuratibu,"amesema.

Amesema programu ambazo zinaandaliwa ni za muda mrefu na lengo lake ni kuona miji mikuu yote ya mikoa inakuwa na master plan na inapokuwepo ni rahisi kuandaa michoro.Alipoulizwa ni miji gani ambayo haipo kwenye mpangilio mzuri, Profesa Lupala amejibu kuwa ipo miji mingi tu ambayo haiko kwenye mpangilio na miongoni mwao lipo Jiji la Dar es Salaam ambalo linaongoza kwa kutokuwa kwenye mpangilio mzuri na kuongeza pia Mwanza,Dodoma na Arusha.

Hivyo wanaendelea na kazi ya kuweka miji hiyo kwenye mpangilio unaoeleweka na kufafanua katika mpango wa miaka 10 wa kupanga, kupima na kumilikisha wananchi watakuwa wakichangia gharama za upimaji maeneo yao.

Vyombo vya Habari Vyaaswa Kuwa na Watumishi Wa kutosha Mkoani Dodoma

$
0
0

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Dkt. Hassan Abbas ametoa wito kwa vyombo vyote vya habari mkoani Dodoma na kwingine nchini kuhakikisha wanakuwa na wafanyakazi wa kutosha watakaokidhi mahitaji kutokana na Serikali kuhamia Dodoma.
Dkt. Abbas ametoa wito huo mjini Dodoma wakati wa muendelezo wa ziara yake kutembelea vyombo vya habari mkoani humo ambapo leo ametembelea ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Uhuru Redio pamoja na Uhuru gazeti.
“Lengo la ziara yangu ni kuona na kujua changamoto za kiutendaji mnazao kutana nazo pamoja na jinsi gani mmejipanga juu ya ujio wa Serikali kuhamia Dodoma kwani matukio mengi ya kiserikali yatafanyika Mkoani hapa” ameongeza Dkt. Abbas.Aidha, Dkt. Abbas amevitaka vyombo vya Habari kufanya kazi kwa bidii, ushirikiano, ubunifu na kufuata maadili katika utendaji kazi hasa katika wakati huu wa mageuzi makubwa nchini.

“Katika mabadiliko au mageuzi yeyote hasa yanayoendelea sasa nchini kila mtu anapaswa kutimiza wajibu wake mahali pake pa kazi ili katika Tanzania ijayo ajivunie si kwa kuwa mlalamishi tu bali ajivunie kuwa naye alishiriki ipasavyo katika safari hii ya mabadiliko” amesisitiza Dkt. Abbas.

Dkt. Abbas ameongeza kuwa “Kwa upande wa habari mimi nimepewa jukumu la kusimamia maadili katika vyombo vya habari hivyo nasimamia na kufuata sheria na busara katika kila jambo linalohusu sekta ya habari ndio maana hatuchukui hatua tu bali tunashauriana na kuonyana kwanza pale wachache wanapokengeuka”.

Mbali na hayo Dkt. Abbas amesema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli anapambana na azma ya kupigania nchi kujitegemea na si kutegemea nchi za nje kwa maisha yetu yote hivyo vyombo vya habari vinajukumu la kupongeza pale Serikali inapotimiza kazi vyema na kukosoa pale ambapo Serikali inakosea lakini si kwa kukejeli, kutusi au chombo cha habari kuonekana kinafanya inda.

Ziara hiyo itaendelea kesho mkoani humo ambapo Dkt. Abbas atatembelea vituo vya Redio Alternative Fm (AFm) na Redio Nyemo Fm.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Kanda ya Kati Dodoma wakati wa ziara ya kutembelea vyombo vya Habari Mkoani Dodoma mapema leo.kulia ni Mkuu wa TBC Kanda ya Kati Bw. Bakari Msulwa.
Mmoja wa Mafundi Mitambo wa TBC Kanda ya Kati Bw. Mbijimi Mzungu akitoa maelezo kwa. Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi kuhusu namna mitambo ya Shirika hilo inavyofanya kazi wakati wa ziara yake katika Ofisi za Shirika hilo mapema leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akikagua vifaa vilivyopo ndani ya moja ya Studio za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Kanda ya Kati Dodoma wakati wa ziara yake mapema leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Kanda ya Kati Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na watumishi wa redio na gazeti la Uhuru Mkoani Dodoma mapema leo wakati wa ziara ya kutembelea vyombo vya Habari.

WANAOISHI MAENEO HATARISHI KUHAMISHWA CHEMBA

$
0
0
SERIKALI wilayani Chemba mkoani Dodoma imesema kuwa imepanga kuwahamisha watu wanaoishi maeneo hatarishi ya kupata mafuriko kutokana zaidi ya kaya 2,000 zimezungukwa na maji katika kata ya Mrijo hadi hivi sasa.

Akiongea wakati akitoa taarifa kwa waratibu wa maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu waliokwenda kufanya tathimini ya maafa yaliyotokana na mafuriko ya mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo, mkuu wa wilaya ya Chemba, Simon Odunga alibainisha kuwa mkakati wa muda mrefu walionao ni kuwatafutia wakazi hao maeneo salama. 

Odunga Alisema kuwa kwa sasa kamati za maafa zimechukua hatua ya kukabili maafa ya mafuriko kutokana na idadi ya nyumba zilizozungukwa na maji imekuwa ikiongezeka siku hadi siku kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivyo wameanzisha kambi maalum kwa watu ambao nyumba zao zimeanguka kutokana na maafa hayo.

Aliongeza kuwa msaada wa haraka unahitajika kutokana na waathirika hao wa mafuriko kutumia baadhi ya majengo ya madarasa ambayo yanapaswa kutumiwa na wanafunzi ambao wanajiunga na masomo mwaka huu.

“kwa sasa tunahitaji sana mahema, mataulo, mashuka , chakula pamoja na madawa kwajili ya kuwahudumia hawa watu ambao tunao hapa na tukipata vifaa hivyo basi tutaondoka hapa na kwenda kutengeza kambi sehemu nyingine ambayo tumeiandaa maaluum kwajili ya kuwahifadhi hawa watu na kuacha haya madarasa kwajili ya matumizi ya wanafunzi” alisema Odunga.

Mkuu huyo wa wilaya aliongeza kuwa tayari wilaya imeshaunda kamati mbalimbali ambazo zinahusika katika kusaidia wahanga hao kuwa salama kiafya kwa kuchukua tahadhari zinazoweza kuibuka kwa magonjwa ya mlipuko.

Naye mratibu wa maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu Ally Mwatima, alisema kuwa mahitaji yote ambayo yameanishwa na mkuu huyo wa wilaya wameyachukua na watayawasilisha ili hatua ziweze kuchukuliwa mapema iwezekanavyo.

“Kwanza niwapongeze kwa kukabili maafa kwa mujibuwa sheria,kanuni namiongozo ya menejimentiya maafa, hali hii imesaidia kuokoa maisha ya hawa wenzetu na mahitaji yote mliyobainisha ni ya msingi sana hivyo tutakwenda kuonana pia na kamati ya maafa mkoa ili kuweza kuona na sisi tunaongeza nguvu katika vitu gani vya msingi ambavyo vitawasadia hawa wenzetu”alisema Mwatima.
Mkuu wa wilaya ya Chemba ,Simon Odunga akifafanuajamba wakati kamati ya maafa ya wilaya nakata ya Mrijo walipokutana na wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajiliya tahmini ya athari zamaafa ya mafuriko katika katika wilaya hiyo.
Muonekano wa sehemu ya soko wilayani Chemba ambapo ni eneo mabalo wilaya hiyo imepanga kuweka kambi ya waathirika wa maafa ya mafuriko wakati wanapanga mikakati ya kuwapangia makazi salama waathirika hao.
Baadhi ya nyumba ambazo zimezungukwa na maji katika kata ya Mrijo wilayani Chemba kutokana na maafa ya mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo.
Baadhi ya waathirika wa maafa ya mafuriko wakiwa katika kambi ya muda iliyo andaliwa na kamati ya maafaya wilaya ya Chemba kutokana na thari za maafa ya mafuriko wilayani humo.
Mratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (shati jeupe), Eward Boniphace, akifuatilia majadiliano wakati kamati ya maafa ya wilaya na kata ya Mrijo walipokutana na wataalamu kutoka Ofisi hiyo kwa ajili ya tahmini ya athari za maafa ya mafuriko wilayani Chemba mkoani Dodoma.

INTRODUCING New Single By SG-SHINE

KILWA YAJIPANGA KUBORESHA MIUNDOMBINI YA AFYA

$
0
0

Angela Msimbira- OR TAMISEMI KILWA


Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Dr. Khalfanis Mbukwa amesema kituo cha afya cha Kilwa Msoko ni miongoni mwa vituo 44 vya afya vilivyopatiwa shilingi milioni 500 kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) kwa ufadhili wa watu wa CANADA kwa ajili uanzishwaji wa huduma za upasuaji wa dharura kwa akina mama.

Akitoa taarifa kwa Wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwenye zoezi la ufuatiliaji wa utekelezaji wa ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya nchini katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi Dr. Khalfanis Mbukwa amesema majengo yaliyojengwa ni chumba cha kuhifadhia maiti, nyumba ya Mtumishi, maabara, wodi ya akina mama, wodi ya watoto,, jengo la upasuaji na kichomea taka.

Dr.Mbukwa amesema jumla ya shilingi 356,988,598 zilikadiriwa kutumika katika ujenzi huo na mpaka sasa zimetumika shilingi 351,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti, nyumba ya mtumishi, maabara, wodi ya akina mama, wodi ya watoto na jengo la upasuaji.

Amesema ujenzi huu utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ya miundombinu ya afya kwa jamii kwa kuwa awali katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko hakukuwa na Majengo ya Upasuaji, Wodi ya akinamama, wodi ya watoto, maabara na jengo la kuifadhia Maiti kuwa chakavu .

Amesema kuwa Kamati ya Manunuzi, Kamati ya mapokezi ya vifaa na kamati ya ujenzi imejipanga vyema kuendelea kusimamia kwa makini ili kuhakikisha dhamani fedha zilizotolewa na serikali zinaenda sambamba na ujenzi uliokubalika.Aidha ameongeza kuwa kiasi cha fedha kitakachobaki kitatumika kwa ajili ya ujenzi wa uzio,ukarabati wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), ukarabati wa nyumba za watumishi na ujenzi wa jengo la kiliniki ya Mama, Baba na Mtoto.
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Dr. Khalfanis Mbukwa akitoa taarifa kwa wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhusu maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya katika Wilaya hiyo.
Moja ya jengo la Wodi ya akinamama lililojengwa katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi.
Moja ya jengo la upasuaji lililojengwa katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi
Baadhi ya Watumishi wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Masoko wakimsikiliza Mkuu wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Mathew Mganga(Hayupo pichani) kwenye ufuatiliaji wa Ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya nchini katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi



SIKILIZA WIMBO MPYA WA MSANII VICTOR MKWANZANIA UITWAO MAARIFA.

Mtwarefa yatoa Tamko-Mtwara

$
0
0
Siku chahche baada ya Sekretarieti ya Shirikisho la Soka Nchini TFF kutoa taarifa ya kuwafikisha katika kamati ya maadili Viongozi wanne wa Soka Wakiwamo Msimamizi wa Kituo cha Mtwara Dastan Mkundi 

Katibu Mkuu wa Mkoa wa Mtwarefa Kizito Mbano,katibu Msaidizi wa Timu ya Ndanda FC Seleman Kachele na Mhasibu Msaidizi wa Club ya simba Sluiman Kahumbu  kwa Tuhuma za Kughushi Nyaraka,Chama Cha Soka mkoa wa Mtwara Kimeibuka na Kutoa Tamko.

Mwenyekiti wa Chamacha Soka Mkoa wa Mtwara MTWAREFA Athman Kambi amesema Chama Chake Kinatambua FORM  Inayoonesha mapato ya shilingi Million 37.7yaliyopatikana katika Mchezo Ndanda FC dhidi ya Simba FC Uliochezwa desemba 30 katika uwanja wa Umoja nangwanda sijaona Mkoani mtwara.

Aidha kambi amekiri kuwa Licha ya kuwa bado haijathibitishwa lakini Tuhuma Hizo zimeonesha Taswira Mbaya katika soko la Mkoa wa Mtwara

Kwa mujibu ya Kauni za Shirikisho ya Chama cha Mpira wa Miguu Nchini TFF mapato yanayopatikana baada ya Mechi  Asilimia 40 yanakwenda kwa timu mwenyeji,asilimia20 kwa timu inayocheza Ugenini,uwanja asilimia 15 na TFF wanapata asilimia5.

MWANAMITINDO WA KIMATAIFA FLAVIANA MATATA AZINDUA JENGO LA MADARASA MAWILI ALIYOYAJENGA YA SHULE YA MSINGI MKOANI PWANI

$
0
0
Na Evance Ng’ingo

MWANAMITINDO wa kimataifa afanyaye shughuli zake nchini Marekani, Flaviana Matata madarasa mawili ya shule za msingi iliyopo katika kijiji cha Msinune kilichopo kata ya Kiwangwa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Flaviana alipewa jukumu la ulezi wa shule hiyo na wanakijiji wa Msinune mwaka 2014 wakati alipoenda kuwasaidia wanafunzi mabegi ya shule, walimpatia jukumu la kuwatengenezea vyoo, ofisi na nyumba za walimu pamoja na kumalizia ujenzi wa darasa.

Tangia alipopewa majukumu hayo alianza kwa ujenzi wa vyoo vya walimu na wanafunzi, na juzi alienda kukabidhi jengo la madarasa, darasa la saba na la sita pamoja na ofisi ya Mkuu wa Shule.Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Flaviana alisema, tangia alipopewa jukumu la ulezi wa shule hiyo amekuwa akihangaika huku na kule kupata fedha za kutatua kero za shule hiyo.

Alisema, kwa kufanikiwa kukabidhi jengo hio la madarasa anaona kuwa ameshiriki kikamilifu katika kutekeleza jukumu lake kama mwanajamii la kusaidia maendeleo ya elimu kwa jamii iliyokuwa na uhitaji mkubwa.

Alisema” sisi kama vijana kama watanzania tunalo jukumu la kujitokeza na kusaidia maendeleo ya elimu na sekta nyingine muhimu nchini kwa kuwa hili sio jukumu la serikali peke yake, sasa nimeshatengeneza vyoo vya walimu na wanafunzi na leo nakabidhi darasa”

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Alex Lugaigalila alisema ujenzi wa darasa huo utawaongezea ufanisi wanafunzi katika masomo yao huku akibainisha wazi ushiriki wa Flaviana kwenye maendeleo ya shule hiyo umeongeza hamasa ya wanafunzi kusoma.

Kwa upande wake Afisa wa elimu wa Kata hiyo,Blasius Alphonce alisema kwa ujenzi wa jengo hilo, Flaviana amesaidia jitihada za serikali katika kuendeleza elimu kwenye kata hiyo yenye vijiji vitano.

Jengo hilo la darasa lililojengwa lina vyumba viwili vikubwa vilivyoezekwa kwa bati huku likuwa na madirisha makubwa yanayowezesha kupitisha hewa na chumba cha mwalimu mkuu.
Mwanamitindo wa Kimataifa afanyae kazi zake nchini Marekani, Flaviana Matata (wa tatu kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo alilojenga la madarasa mawili na ofisi ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi kwa shule ya msingi Msinune, iliyopo kata ya Kiwangwa wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani jana.
Mwanamitindo wa Kimataifa afanyae kazi zake nchini Marekani, Flaviana Matata kushoto akikabidhi mipira kwa wanaafunzi wa shule hiyo, Flaviana ni mlezi wa shule hiyo.
Mwanamitindo Flaviana akionesha cheti cha heshima alichotunukiwa na uongozi wa kata ya Chiwangwa baada ya kuwajengea majengo ya shule.
Flaviana akipokea zawadi ya mbuzi kutokea kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Msinune, Ramadhan Mtokeni (kushoto) huku Diwana wa kata ya Chiwangwa (kulia) Malota Kwagga na Afisa elimu wa kata hiyo Blasius Alphonce kulia kwa diwani na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Msinune, Alex Lugaigalila wakiangalia.


MAKAMU WA RAIS AKAGUA MIFEREJI YA MAJI KATIKA ENEO LA BUGURUNI MIVINJENI NA MTONI KWA AZIZI ALI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wanaoishi kwenye mpaka kati ya Buguruni Mivinjeni na Sharifu Shamba pamoja na Mtoni kwa Azizi Ali kuwa watunzaji wazuri wa mitaro ya maji kwani ni mali yao wenyewe na si ya serikali.

Makamu wa Rais aliyasema hayo wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku mbili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kuta za bahari na mitaro ya maji jijini Dar es Salaam.Makamu wa Rais aliwaeleza wananchi hao kuwa mabadiliko ya tabia nchi yameathiri shughuli za kiuchumi , kijamii na kimazingira.

Makamu wa Rais Makamu wa Rais alisema kila mmoja anapaswa kujishughulisha katika suala la kusafisha na kuhifadhi mazingira .“ubaya wa mazingira ukiyaharibu yanakuadhibu” alisisitiza Makamu wa Rais.Mtaro wa Buguruni Mivinjeni una urefu wa mita 475 na ule wa kwa Azizi Ali una urefu wa mita 550.

Makamu wa Rais alisema nchi inapozungumzia uchumi wa viwanda ni mazingira “tukiharibu mazingira hamna uchumi wa viwanda” hata viwanda vitakavyojengwa vinahitaji kutunza mazingira, visafishe maji yake kabla ya kutiririsha.

Makamu wa Rais alitoa rai kwa yeyote atakayebainika kuharibu miundo mbinu wanachukuliwa hatua za haraka.Makamu wa Rais alimalizia kwa kusema kuwa Usalama wa Nchi, Amani, afya, mazingira bora hayana chama hivyo ni jukumu la kila mmoja kuwajibika ili maendeleo yaweze kupatikana.

Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema kuongezeka kwa watu katika jiji la Dar es Salaam na mabadiliko ya tabia nchi kutaendelea kutoa changamoto za miundo mbinu hivyo Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kujenga miundo mbinu itakayowezesha wananchi kuendelea na shughuli zao kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua kuelekea Baharini katika maeneo ya Ilala Bungoni na Temeke kwa Aziz Ally Jijini Dar es Salaam leo. Mifereji hiyo inajengwa ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo lengo ni kunusuru hali ya mafuriko katika maeneo hayo. Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando..
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelekezo kutoka kwa mmoja wa mafundi wa wanaojenga mfereji wa maji taka eneo la Ilala Bungoni alipotembelea mradi huo leo Jijini Dar es Salaam
Sehemu ya mfereji unaojengwa katika eneo la Ilala Bungoni kwa ajili ya kupeleka maji hadi katika bonde la mto msimbazi ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo mafuriko.
Sehemu ya mfereji unaojengwa katika eneo la Temeke kwa Aziz Ally kwa ajili ya kusafirisha maji ya ikiwa ni njia ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo mafuriko.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiulizia jambo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa mfereji wa maji katika eneo la Ilala Bungoni leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando, Mbunge wa Segerea Bonnah Kaluwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiulizia jambo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa mfereji wa maji kuelekea baharini katika eneo la Temeke kwa Aziz Ally leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba.Picha na: Frank Shija – MAELEZO

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 19, 2018

WAZIRI MKUU AKABIDHI KADI ZA MATIBABU KWA WAZEE 280

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amegawa kadi za matibabu kwa wazee 280 wa wilaya ya Serengeti mkoani Mara, kadi hizo zitawawezesha wazee hao kutibiwa bure.

Amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa matibabu bure kwa wazee walio na umri wa kuanzia miaka 60.

Waziri Mkuu alikabidhi kadi hizo jana (Alhamisi, Januari 18, 2018) alipotembelea mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Serengeti, inayojengwa katika mji wa Mugumu.Alisema Serikali kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Serengeti itakamilisha ujenzi wa hospitali hiyo, itakayokuwa na uwezo wa kuwahudumia wakazi wa wilaya hiyo na wageni.

Waziri Mkuu alisema ujenzi wa hospitali hiyo ni muhimu kwa kuwa mbali na kuwanufaisha wananchi, pia watalii wanaotembelea mbuga ya Serengeti nao wataweza kutibiwa hapo.Awali, Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Nurdin Babu alisema tangu mwaka 1974 wilaya hiyo ilipoanzishwa hadi sasa haina hospitali ya wilaya na wakazi wake wanatibiwa katika hospitali teule ya Nyerere inayomilikiwa na kanisa la Mennonite Tanzania.

Alisema kutokana na kuongeka kwa idadi ya wakazi hao pamoja na idadi kubwa ya wageni wanaotembelea Serengeti, hususan watalii hospitali hiyo haina tena uwezo wa kutoa huduma kwa kiwango kinachostahili.Bw. Babu alisema mara nyingi wageni wanaotembelea mbuga ya Serengeti hulazimika kufuata huduma za afya mjini Arusha au Nairobi nchini Kenya pale wanapougua au kupata ajali katika shughuli zao za kitalii.

Alisema kwa upande wa wakazi wa wilaya ya Serengeti wao hulazimika kufuata huduma za afya katika hospitali ya Mkoa au hospitali ya Rufaa ya Bugando, hivyo kukamilika kwa mradi huo wa ujenzi wa hospitali utawapunguzia kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo.

Pia Mkuu huyo wa wilaya alisema alianzisha kampeni ya changia sh. 1,000 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya, kwa lengo la kuwafanya wakazi hao wajisikie kuwa wameshiriki katika ujenzi huo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
IJUMAA, JANUARI 19, 2018.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kadi ya matibabu ya bure kwa wazee, Johaness Chacha, moja wa wazee 280waliopatiwa vitambulishbo hivyo vitakavyowawezesha kutibiwa bure popote wilayani Serengeti katika makabidhiano yaliyofanyika kwenye viwanja vya hospitali ya wilaya ya Mugumu Januari 18, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Serikali haijapiga marufuku biashara na matumizi ya mkaa

$
0
0
Wakala unapenda kuujulisha umma kuwa Serikali ya Tanzania haijapiga marufuku biashara na matumizi ya mkaa, isipokuwa inachotaka ni kuona uvunaji misitu unafanywa kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizotungwa. Serikali inataka watu wafanye biashara hiyo kwa njia halali na walipe ushuru na kodi kwa mujibu wa sheria.

Wafanyabiashara wa mazao ya misitu wanatakiwa kutimiza masharti yafuatayo:
(i) Awe na hati ya usajili;
(ii) Awe na hati ya usafirishaji wa mazao ya misitu (Transit Pass);
(iii) Awe na leseni ya kuvuna mazao ya misitu;
(iv) Awe na leseni ya biashara ikiwa ni pamoja na TIN namba;
(v) Alipie ushuru wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kama ilivyobainishwa kisheria;
(vi) Awe na daftari la kumbukumbu ya kupokea na kuuza mazao ya misitu.
Kutokana na Kanuni za usafirishaji wa mazao ya misitu za mwaka 1999 hairuhusiwi mtu yeyote kusafirisha mazao ya misitu (kwa njia ya barabara au maji) kati ya saa kumi na mbili jioni na saa kumi na mbili asubuhi.
Atakayevunja masharti hayo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Mkaa.
Hairuhusiwi mtu yeyote kusafirisha mkaa hadi atimize masharti yaliyoko hapo juuu. Vilevile, mkaa, hata kama ni mfuko mmoja kwa ajili ya biashara au matumizi ya nyumbani, sharti ulipiwe.Pamoja na kutimiza masharti yaliyoorodheshwa hapo juu, wafanyabiashara wa mkaa wanatakiwa kutimiza masharti yafuatayo:-


(i) Awe na leseni itakayotolewa na Afisa Misitu wa Wilaya au Wakala wa Huduma za Misitu;
(ii) Awe na hati ya kusafirisha mkaa (Transit Pass), ambayo itagongwa muhuri katika kila kituo cha ukaguzi wa mazao ya misitu.
(iii) Mkaa usafirishwe kupitia njia zilizoruhusiwa na Ofisi za Misitu.
(iv) Atatakiwa alipie ushuru wa Serikali kwa kila kilogramu moja Sh 250 au kilogramu 50 kwa Sh 12500.
Kwa mtu yeyote atakayesafirisha mkaa bila kutimiza masharti yaliyotajwa hapo juu, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Maelezo zaidi yanapatikana katika ofisi za Misitu za Wilaya na TFS.

Haya sio matenga ya samaki la hasa ni mbinu mpya iliyobuniwa na wahalifu  wanaosafirisha mkaa kinyume na taratibu kama yalivyokutwa na maafisa Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Kanda ya Mashariki walipokuwa wakifanya doria eneo la Dumila barabara ya Domoma - Morogoro jana.
 
kulia ni Herman Awet Afisa Misitu kanda ya mashariki akiwa na  henry malya ambaye anasimamia safu ya Dumila wakimueleza Mama mfanya biashara (aligoma kutaja jina lake) taratibu za bishara na usafirishaji wa mkaa mara baada ya kumkamata kwa kosa la kukiuka taratibu za usafirishaji mkaa kwa kuweka mkaa huo kwenye matenga na kusafirisha kama matenga ya samaki ili kukwepa maduhuli ya Serikali. Mama huyo alikamatwa Barabara ya Dumila.

watatu walamba mamilioni ya tatumzuka jumapili Jackpot

$
0
0
 Meneja Mawasiliano wa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) hivi karibuni wakati wa kuwatambulisha na  kuwakabidhi hundi zao washindi watatu wa TatuMzuka (Jumapili Jackpot),mchezo huo ulifanyika mwishoni mwa wiki.Maganga amewaomba Watanzania kuendelea kujitokeza kwa wingi kuendelea kucheza mchezo huo,kwani umekuwa ukiwakwamua wengi waliobahatika na kuwa wafanyabiashara/wajasiliamali wazuri na vipato vyao vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku.
Pichani kati ni Lucas Swebe akitoa ushuhuda wa namna alivyojishindia fedha taslimi Milioni tano katika  mchezo wa TatuMzuka (Jumapili Jackpot),Pichani kulia ni mshindi mwingine aitwaye Mrisho Maganga aliyejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 22 pamoja nae (kutosho) ni Daniel Mwachali ambaye naye alijinyakulia kitita cha shilingi Milioni 22.
 Meneja Mawasiliano wa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi ya Milioni 22,Danie Mwachali aliyojishindia kwenye mchezo wa TatuMzuka (Jumapili Jackpot) uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images