Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

KOCHA MPYA WA SIMBA KUSHUHUDIA MTANANGE WA LEO

0
0
Klabu ya Simba inayo furaha kubwa kuwajulisha Wanachama na washabiki wake kwamba imempata kocha wake mkuu mpya, Mfaransa Pierre Lechantre.

Kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo

Kocha Lichantre keshawahi kufundisha vilabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroun kilichotwaa ubingwa wa Africa 2000.
Kocha huyo pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na pia barani Asia mwaka 2012.

Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi

Na leo jioni kocha Lechantre ataishuhudia Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa.

IMETOLEWA NA 
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI SIMBA SC 
SIMBA SC NGUVU MOJA

BEI YA MATUNDA SOKO LA MABIBO

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii

WAFANYABIASHARA wa matunda katika Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam wamelezea bei mbalimbali za matunda wanayouza kwa wateja wao sokoni hapo.

Wakizungumza na Michuzi Blog jijini Dar es Salaam wafanyabiashara hao wametaja bei ya kila tunda na wanalouza.Bei hizo ni kama zinavyoonesha hapa. 
Bei ya Nanasi katika Soko la Mabibo linauzwa kati shilingi. 500 hadi shilingi 2000/=
Bei ya Embe sokoni hapo ni kati ya Shilingi 400 hadi Shilingi 600. 
Bei ya Embe ndogo ni Shilingi 300 hadi Shilingi 400 katika soko hilo. 
Bei ya Ndizi sokoni hapo inauzwa kati ya Shilingi 20,000 hadi Shilingi 35,000 kwa mkungu mmoja.
Bei ya Tikitikiti maji ni kati ya Shilingi 700 hadi Shilingi 2500. 
Bei ya Parachichi ni kati ya Shilingi 400 hadi Shilingi 1000.
Bei ya Ndizi Mbivu inauzwa kati ya Shilingi 150 hadi Shilingi 160 kwa bei ya jumla na rejareja. 
Bei ya Boga linauzwa kati ya Shilingi 1500 hadi shilingi 3500 kwa bei ya jumla na rejareja.

KWANDIKWA AAGIZA DARAJA LA RUHUHU KUKAMILIKA

0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, amemtaka mkandarasi anayejenga daraja la Ruhuhu wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha anamaliza daraja hilo kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Agizo hilo amelitoa leo Wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma alipokuwa akikagua ujenzi wa daraja hilo ambapo ameusisitiza Uongozi wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Makao makuu kuhakikisha kuwa utaratibu wa zoezi zima la ununuzi wa vyuma vitakavyowekwa juu ya daraja hilo linaenda sambamba na makadirio ya muda wa mradi ili kupelekea kazi hiyo kukamilika kwa muda uliopangwa.

"Nafikiri sasa jipangeni vizuri ili masika yakiiisha mhakikishe mnafanya kazi kwa bidii ya hali ya juu, nataka kufikia mwezi Juni daraja liwe limekamilika, pia TANROADS Makao makuu hakikisheni mchakato wa manunuzi ya vyuma vya daraja mnauanza mapema ili kuweza kukamilika mapema, msisubiri hadi daraja hili kukamilika", amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Ameongeza kuwa daraja hilo likikamilika litakuwa ni kiungo kwa watu wa Nyasa mkoani Ruvuma na Ludewa mkoani Njombe kwani wamekuwa wakilisubiri daraja hilo kwa ajili ya kujiendeleza katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.Aidha, amemwagiza Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), mkoani humo, Mhandisi Elisha Mgira, kuhakikisha anarekebisha kasoro zilizopo kwenye kivuko cha Ruhuhu ili kuweza kufanya kazi katika kipindi hiki ambacho wananchi wanasubiri ujenzi wa daraja kukamilika.

Kwa upande wake, Mhandisi Mkazi wa daraja hilo, Mhandisi Napegwa Kiseko, amesema kuwa Ujenzi wa mradi huo umefika asilimia 50 ambapo kazi zinazofanyika sasa ni kujaza matabaka ya barabara zinazoingia darajani hapo ili kunyanyua tuta la barabara.

Amefafanua kuwa kazi hiyo inaendelea pande zote mbili yaani mkoa wa Ruvuma na Njombe ingawa kwa kipindi hiki cha mvua kazi hiyo imekuwa na vikwazo vingi."Ujenzi wa misingi ya daraja kwa upande wa mkoa wa Ruvuma upo kwenye hatua za mwisho na kwa upande wa Njombe ujenzi wa misingi ulianza mwishoni mwa mwezi Disemba na unaendelea", amesisitiza Mhandisi Kiseko.

Mradi wa ujenzi wa daraja la mto Ruhuhu ambao upo mpakani mwa mkoa wa Ruvuma na Njombe unatarajiwa kugharimu takribani kiasi cha shilingi Bilioni 6 ambazo ni fedha za Serikali kwa asilimia mia moja na unatarajiwa kukamilka mwezi Juni mwaka huu.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Mhandisi Mkazi anayesimamia ujenzi wa Daraja la Ruhuhu, Mhandisi Napegwa Kiseko, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo linalounganisha Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe na wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa daraja hilo kwa upande wa mkoa wa Ruvuma.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Lazeck Alinanuswe (katikati), akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa Daraja la Ruhuhu lililopo wilayani Nyasa, mkoani humo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, wakati alipokagua daraja hilo kuona maendeleo ya ujenzi wake.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Lazeck Alinanuswe (katikati), wakati alipokagua ujenzi wa Daraja la Ruhuhu linalojengwa wilayani Nyasa na mkandarasi wa kampuni ya Lukolo kwa gharama ya shilingi bilioni 6.
Muonekano wa Daraja la Ruhuhu linalojengwa wilayani Nyasa na mkandarasi wa kampuni ya Lukolo kwa gharama ya shilingi bilioni 6. Daraja hilo litaunganisha Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukifanyia ukarabati kivuko cha MV Ruhuhu kinachotoa huduma kati ya wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe ili kiweze kutoa huduma kipindi chote wakati ujenzi wa Daraja la Ruhuhu ukiendelea.
Muonekano wa Kivuko cha MV. Ruhuhu kinachotoa huduma kati ya wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe. Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba magari 6 na watu 100.
Muonekano wa barabara ya Kitai-Lituhi yenye urefu wa KM 89 inayojengwa kwa kiwango cha changarawe mkoani Ruvuma.

UN yapitisha kikombe baada ya marekani kupunguza misaada Palestina

SERIKALI YAJA NA MUONGOZO WA KUPAMBANA NA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA.

0
0

NA WAMJW-DAR ES SALAAM


SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeandaa Muongozo wa matibabu nchini na orodha ya dawa zote muhimu ili kuepukana na tatizo la usugu wa vimelea vya dawa. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa Muongozo wa matibabu na orodha ya dawa zote muhimu uliofanyika leo jijini Dar es salaam. 

Ni muhimu kila kituo cha afya kuwa na dawa za kutosha, vifaa na vifaa tiba lakini ni lazima tuzingatie muongozo wa matibabu na orodha ya dawa kulingana na ugonjwa fulani ili kuepuka tatizo hili" alisema Waziri Ummy,

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Muongozo huo umezingatia vigezo vyote vya kuweka dawa ambazo zilikuwa hazipo katika ngazi ya zahanati na vituo vya afya ambazo zimepata uthibitisho kutoka Shirika la Afya la Dunia (WHO). 

Aidha Waziri Ummy amewapiga marufuku Bohari Kuu ya dawa ya Taifa MSD na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) kuagiza na kuandika dawa zilizo nje ya muongozo uliozinduliwa leo ili kuondoa matumizi ya dawa yasiyo sahihi. Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa kila kituo cha afya ni lazima kiongozwe na Tabibu na sio vinginevyo ili kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana katika kituo cha afya husika. 

Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa itafika kipindi vituo vya afya ambavyo havikizi vigezo vitafungiwa ili kuepuka usababishwaji wa vifo visivyo vya lazima kwa watanzania. Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi amesema kuwa muongozo wa kutibu magonjwa mbambali umezingatia Orodha ya dawa ambazo zitakuwa zinatumika nchini kwetu kama dawa muhimu za kutibu magonjwa hayo. 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Muongozo wa Matibabu na Orodha ya dawa muhimu wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali prof. Mohammed Bakari Kambi na kushoto ni Mwakilishi wa WHO.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Muongozo wa Matibabu na Orodha ya dawa muhimu wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali prof. Mohammed Bakari Kambi na kushoto ni Mwakilishi wa WHO.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa Muongozo wa matibabu na orodha ya dawa zote muhimu leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto mwenye kilemba akiwakabidhi baadhi ya wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Afya nchini Muongozo wa Matibabu na orodha ya dawa wakati wa uzinduzi wa Muongozo huo leo jijini Dar es salaam.

WAZIRI MWIGULU AKUTANA NA VIONGOZI KUJADILI MASUALA YA JESHI LA MAGEREZA

0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba, akizungumza wakati wa kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya Jeshi la Magereza baada ya kukutana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira (kushoto) na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk . Juma Malewa.Kikao hicho kimefanyika leo ofisi ya wizara,jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira (kushoto) na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa(kulia), wakimsikiliza Waziri wa wizara hiyo,Dk. Mwigulu Nchemba walipokutana kujadili masuala  ya jeshi hilo. Kikao hicho kimefanyika leo ofisi ya wizara,jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira, akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa (kulia), wakati wa kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya jeshi hilo.Kikao hicho kimefanyika leo ofisi ya wizara,jijini Dar es Salaam.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

WADAU WAJADILI MTAALA WA MAFUNZO KWA VYUO VYA USTAWI

0
0
Kamishna Msaidizi Ustawi wa Jamii (Mafunzo) kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Bw. Simon Panga amesema utengenezaji mitaala ya taaluma ya Ustawi wa Jamii katika ngazi ya cheti na astashahada itasaidia kuboresha elimu ya ustawi wa jamii nchini.

Panga alisema hayo leo wakati akifungua mkutano wa siku moja wa wadau wa Ustawi wa Jamii kutengeneza mtaala wa Ustawi wa jamii kwa vyuo vinavyofundisha masuala ya Ustawi katika ngazi ya Cheti na astashahada leo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi Ustawi wa Jamii (Mafunzo), mtaala utakaopendekezwa na wadau utatumika na vyuo vyote Nchini tofauti na sasa ambapo kila chuo kinajitengenezea mtaala na utakuwa umepunguza majukumu na gharama kwa vyuo katika kutengeneza na kuandaa mitaala yao.
Kamishna Msaidizi Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawke na Watoto Simon Panga akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku moja wa wadau wa Ustawi wa Jamii kutengeneza mtaala wa Ustawi wa jamii kwa vyuo vinavyofundisha masuala ya Ustawi katika ngazi ya Cheti na Diploma jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Paulo Mwangozi akitoa ufafanuzi wakati wa wa mkutano wa siku moja wa wadau wa Ustawi wa Jamii kutengeneza mtaala wa Ustawi wa jamii kwa vyuo vinavyofundisha masuala ya Ustawi katika ngazi ya Cheti na Diploma jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa wadau wa Ustawi wa Jamii kutengeneza mtaala wa Ustawi wa jamii kwa vyuo vinavyofundisha masuala ya Ustawi katika ngazi ya Cheti na Diploma jijini Dar es Salaam.

KAMISHNA GASTON SANGA AMWAKILISHA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA KUFUNGUA MAFUNZO YA MAAFISA VIUNGANISHI WA UTUNZAJI WA TAKWIMU

0
0
Afisa Mradi wa Envirocare , ndugu Antony Mlelwa (Mwenye shati jeupe) akifungua na kumkabidhi kompyuta Afande Kamishna Gaston Sanga huku Mkurugenzi na Meneja Mradi wakishuhudia. Kompyuta hizo zitatumika kuhifadhia Taarifa na Takwimu kwa wataalam wapya wa katika Mradi wa Msaada wa Kisheria Magerezani.
Mkurugenzi wa Envirocare Bi Loyce Lema akitoa maelezo mafupi ya historia ya Envirocare kabla ya kumkaribisha Afande Kamishna Gaston Sanga kutoa hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza na kufungua rasmi mafunzo ya siku tatu kwa wataalamu wapya wa Utunzaji wa Takwimu katika Mradi wa Msaada wa Kisheria Magerezani
Kamishna Sanga akitoa Nasaha za Kamishna Jenerali wa Magereza kabla ya kufungua rasmi mafunzo ya wataalam wapya Utunzaji wa Takwimu ambayo yanafanyika Makongo juu jijini Dar es Salaam kwenye ofisi Envirocare
Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza Afande Gaston Sanga( wa pili kulia), Mkurugenzi wa Envirocare Bi Loyce Lema (wa pili kushoto) ,Meneja Mradi Bi Catherine Jerome( wa kwanza kulia) na Mwanasheria wa Jeshi la Magereza Makao Makuu, Mkaguzi Msaidizi Hobokela Mwansumbule(wa kwanza kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya Utunzaji wa Taarifa na Takwimu.
Picha zote na Makao Makuu ya Magereza kitengo cha Habari.


Wateja sita wa Benki ya NBC wajinyakulia Suzuki Carry ‘kirikuu’ kampeni ya Malengo

0
0

WATEJA sita wa Benki ya NBC wameibuka kidedea baada ya kila mmoja kujishindia gari jipya aina ya Suzuki Carry maarufu kama ‘Kirikuu’ katika droo kubwa ya Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Kampeni hiyo iliyodumu kwa miezi mitatu imeshuhudia wateja hao kutoka katika maeneo yaliyogawanywa katika kanda sita nchini wakitangazwa washindi wa magari hayo yenye thamani ya shs millioni 30 kila moja jumla yakiwa na thamani ya shs milino 180.

Akizungumza wakati wa droo hiyo, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi alisema kampeni hiyo iliyovutia waterja wengi wapya kujiunga ilishuhudia washindi wengine 24 kupatikana katika droo mbili zilizofanyika katika miezi miwili ya nyuma ambapo kila mmoja alijishindia zawadi ya pesa taslimu shs milioni 1. “Kampeni hii ya Akaunti ya Malengo ya NBC imekuwa na mafanikio makubwa kwani tumeshuhudia zaidi ya akaunti mpya 6000 ziikifunguliwa na wateja wetu wakihamasika kujiwekea akiba kwa malengo yao ya baadae”, alisema.

Alisema kampeni hiyo ilizinduliwa mwaka jana kipindi ambacho NBC ilikuwa ikiadhimisha miaka 50 ya huduma bora kwa wateja tokea kuanzishwa kwake. Katika droo hiyo zawadi hizo za Suzuki Carry sita ‘kirikuu’ zilikwenda kwa Fatuma Ramadhani kutoka kanda ya Dar es Salaam, Saidi Chiwini wa Pwani, Lucina Massawe wa kanda ya kaskazini, Kelvin Machage wa kanda ya ziwa, Patrick Mgimwa wa kanda ya kati na Fridino Benito kutoka kanda ya kusini.

Hii ni mara ya tatu Benki ya NBC kuendesha kampeni ya akaunti ya Malengo mara hii ikitoa zawadi zenye thamani ya zaidi ya shs milioni 204 ambapo mwaka 2016 wateja wawili Aldo Nsuha mkazi wa Tabata Dar es Salaam na Lawrence Njozi kutoka Masasi mkoani Mtwara wakijishindia magari mapya aina ya Toyota Hilux double cabin. 

Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Fi​l​bert Mponzi (katikati), akizungumza wakati wa droo kubwa ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Kampeni, Mtenya Cheya na kulia ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid. Washindi sita walijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry maarufu kama ‘Kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi hao ni Fatuma Ramadhani kutoka kanda ya Dar es Salaam, Saidi Chiwini wa Pwani, Lucina Massawe wa kanda ya kaskazini, Kelvin Machage wa kanda ya ziwa, Patrick Mgimwa wa kanda ya kati na Fridino Benito kutoka kanda ya kusini. Katika kampeni hiyo iliyochukua muda wa miezi mitatu washindi wengine 24 walijishinda zawadi ya pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja.
Meneja wa Amana za Wateja wa Benki ya NBC, Dorothea Mabonye (wa pili kushoto), akichezesha droo kubwa ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Washindi sita walijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry maarufu kama ‘Kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi hao ni Fatuma Ramadhani kutoka kanda ya Dar es Salaam, Saidi Chiwini wa Pwani, Lucina Massawe wa kanda ya kaskazini, Kelvin Machage wa kanda ya ziwa, Patrick Mgimwa wa kanda ya kati na Fridino Benito kutoka kanda ya kusini. Katika kampeni hiyo iliyochukua muda wa miezi mitatu washindi wengine 24 walijishinda zawadi ya pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja. Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bakari Maggid, Meneja Kampeni ya Malengo, Mtenya Cheya na Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi.

Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Fi​l​bert Mponzi (​wa pili kulia ), akizungumza wakati wa droo kubwa ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC jijini Dar es Salaam leo ​ ambapo NBC imetoa zawadi zawadi ya gari aina  ya Suzuki Carry 'Kirikuu' kama inavyoonekana moja ya gari hilo (kushoto) likionyeshwa kwa waandishi wa habari wakati wa droo hiyo. ​

RC NDIKILO AWAPA ONYO WARATIBU WA ELIMU KATA /AWATAKA KUJIKITA KWENYE AJIRA YAO ILI KUINUA TAALUMA MKOANI PWANI

0
0

Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze

MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,amewaasa waratibu wa elimu kata,kusimamia masuala ya elimu ili kuinua kiwango cha taaluma,na atakaebainika kwenda kinyume na majukumu yake ajihesabu amejifukuzisha kazi.

Aidha hajafurahishwa na hali ya mahudhurio ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu ambapo mahudhurio yapo chini ya asilimia 50 kimkoa.Pamoja na hayo,ametoa rai kukamatwa na kufikishwa mahakamani , wazazi na walezi wote ambao watashindwa kuwapeleka watoto wao kuripoti shule kwa wakati.

Ndikilo,aliyasema hayo ,wakati akizungumza na baadhi ya waratibu wa kata, maafisa elimu wa Chalinze na Bagamoyo,walimu na wajumbe wa bodi ya shule ya sekondari Mboga,iliyopo Chalinze .Alisema mratibu wa elimu kata atakayefanya uzembe na kubainika kujishughulisha na masuala tofauti na kazi yake atamvua kazi.

Ndikilo ,aliwapa siku saba kuhakikisha hali ya mahudhurio ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mashuleni inakuwa nzuri tofauti na sasa.Alisema hali ya mahudhurio hairidhishi ,kwani wanafunzi waliotakiwa kuripoti shule ya sekondari Mboga hadi sasa ni asilimia 51 pekee.
Kaimu afisa elimu sekondari halmashauri ya Chalinze ,Irene Lubega akimkabidhi ripoti ya taarifa ya mahudhurio ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mashuleni hadi sasa ,mkuu Wa Mkoa Wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,ambapo mahudhurio hayaridhishi kimkoa bado yakiwa chini ya asilimia 50
Kaimu afisa elimu sekondari halmashauri ya Bagamoyo ,Juma Yusuph akisoma ripoti ya taarifa ya mahudhurio ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mashuleni hadi sasa mbele ya mkuu Wa Mkoa Wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,ambapo mahudhurio hayaridhishi kimkoa bado yakiwa chini ya asilimia 50
Mbunge wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete akizungumzia masuala ya kielimu mara baada ya mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,kupitia shule ya sekondari Mboga ,Chalinze kuzungumzia hali ya mahudhurio ya wanafunzi wanaotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu ambapo hali ya mahudhurio mashuleni hayaridhishi kimkoa bado yakiwa chini ya asilimia 50
Mkuu Wa Mkoa Wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo(aliyesimama) akizungumzia masuala ya kielimu mara baada ya kupitia shule ya sekondari Mboga ,Chalinze kuzungumzia hali ya mahudhurio ya wanafunzi wanaotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu ambapo hali ya mahudhurio mashuleni hayaridhishi kimkoa bado yakiwa chini ya asilimia 50.Picha na Mwamvua Mwinyi


MAAZIMIO YA MKUTANO KATI YA SMZ NA SMT KUSHUGHULIKIA MELI ZINAZOPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA KWA TUHUMA ZA KUSAFIRISHA SILAHA NA MADAWA YA KULEVYA

0
0
Meli hizo ni: Kaluba yenye usajili namba IMO 6828753 iliyokamatwa tarehe 27 Desemba 2017 ikiwa na wastani wa kilo 1,600 za dawa za kulevya huko katika maeneo ya Jamhuri ya Dominican Republic; na 

Andromeda yenye namba za usajili IMO 7614666 iliyokamatwa kwa kusafirisha silaha kinyume na Sheria za kimataifa. Meli zote mbili zimesajiliwa Tanzania kupitia taasisi yetu ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar ambayo ndiyo imepewa mamlaka ya kusajili meli za nje.

Hapa kwetu Tanzania tuna aina mbili za kusajili Meli; usajili wa Meli zenye asili ya Tanzania na zile zenye asili ya Nje. kwa kuzingatia kuwa Tanzania ni nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa na mashirika yake mbalimbali, siku zote tumekuwa tunaheshimu na kutekeleza kikamilifu majukumu yetu ya kimataifa yaliyowekwa kupitia mikataba na maazimio mbalimbali ya vyombo hivyo

Ndugu Waandishi wa Habari, kwa mujibu wa mkataba wa UNCLOS 1982 kila nchi imepewa haki ya kufanya usajili wa meli kwa kuzingatia mikataba ya kimataifa na sheria za nchi husika.Kwa upande wa Tanzania, usajili wa meli za kimataifa unasimamiwa na Sheria Na 5 ya mwaka 2006,


(Kwa upande wa SUMATRA ina Merchant Shipping Act ya mwaka 2003. Sheria hi inaruhusu usajili wa meli inayomilikiwa na Mtanzania, au meli inayomilikiwa kwa ubia kati ya Mtanzania na raia wa nchi nyingine. Kwa sheria hii ili meli ipate usajili wa SUMATRA na kuruhusiwa kupeperusha bendera ya Tanzania ni lazima umiliki wa meli uhusishwe na raia wa Tanzania kwa umiliki wote au kwa ubia lakini ni lazima Mtanzania awe na hisa nyingi. 

Vilevile kampuni hiyo ya umiliki lazima iwe ya Kitanzania kwa maana ya kusajiliwa na kujiendesha kutokea Tanzania hata kama kampuni hiyo inamilikiwa na watu wasio Watanzania. Na kwa upande wa Zanzibar kupitia ZMA wana Maritime Transport Act ya mwaka 2006).
Ndugu Waandishi wa Habari, nimewaita hapa kuzungumza nanyi na kupitia kwenu kuzungumza na wananchi wenzangu kuhusu taaarifa ya kukamatwa kwa meli zilizokuwa zimepakia shehena za dawa za kulevya na silaha zikiwa zinapeperusha bendera ya nchi yetu.


WATOTO WENYE SHIDA WAFAIDIKA NA BIMA YA AFYA

0
0
Na Anthony Ishengoma.

Watoto wanaoishi katika Makao ya Taifa ya Watoto Kurasini wamefaidika na huduma ya Bima ya Afya kwa ajili ya matibabu yao baada ya shirika la Abbot Tanzania kuwezesha ufadhili wa huduma hiyo muhimu pamoja kuwafungulia akaunti za benki ili waweze kumudu kulipia upya wakati bima zao zinapofikia mwisho wa muda wake.

Shirika hili limekuwa mfadhili mkuu wa Makao ya Taifa ya watoto tangu mwaka 2001na limewezasha watoto wa kituo hiki kuhakikisha wanapata huduma mbalimbali ikiwemo ustawi wa watoto kiafya na huduma nyinginezo kama vyeti vya kuzaliwa, ujenzi wa mabweni pamoja na huduma za miundombinu ya kituo hicho.
Makao ya Taifa ya watoto wenye shida Kurasini yametembelewa na ujumbe maalum katoka Shirika linalofadhili kituo hiki la Abbot Tanzania ili kujionea Maendeleo ya shughuli za kituo hicho zinazofadhiliwa na shirika hilo.
Akiongea wakati wa kuwakaribisha wageni hao kituoni hapo, Kaimu  Kamishina wa Ustawi wa Jamii Simon Panga amesema Shirika la Abbot Tanzania limekuwa likitoa ifadhili wake kwa kituo hiki tangu mwaka 2001 na kufanikiwa kuleta mageuzi makubwa kwa Maendeleo ya kituo hiki.
 Wageni wa Makao ya Taifa ya Watoto Kurasini wakiangalia moja ya mradi wa ufugaji unaofadhiliwa na na Mfuko wa Abbot Tanzania katika Makao ya Taifa Dar es Salaam  aliye katikati ni Makamu wa Rais wa Mfuko wa Abbot  Bi. Jenna Daugherty.
 Baadhi ya watoto wa Makao ya Taifa ya Watoto wakiimba mbele ya wageni kutoka wafadhili wa Makao yao Abbot Tanzania pamoja na uongozi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto jijini Dar es Salaam.
Mlezi wa Makao ya Taifa ya Watoto Bi. Beatrice Mugubilo akiongoza wageni wa Makao yake kuangalia maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Abbot Tanzania.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Profesa Mbarawa awataka TPA kukamilisha na kuhamia jengo jipya

0
0
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), kuhakikisha kazi ya kukamilisha ujenzi wa jengo jipya 'One Stop Centre' inakamilika haraka na kuanza kutoa huduma kwa mamlaka hiyo na wadau wake wote.

Akizungumza mara baada ya kukagua jengo hilo leo jijini Dar es Salaam, Prof. Mbarawa  amesema ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam utafikiwa pale wadau wote wa bandari hiyo watakapofanya kazi saa 24 na katika eneo moja ili kumrahisishia mteja kupata huduma kwa haraka na katika kiwango kinachokubalika kimataifa.

"Natoa miezi sita kuanzia leo kwa TPA msimamieni mkandarasi  kikamilifu ili ikifika Juni muwe mmehamia ninyi na wadau wenu wote katika jengo hili," alisititiza Prof. Mbarawa katika ziara hiyo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa katika kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati tayari yeye amehamia kwenye jengo hilo, ili kuongeza hamasa kwa mkandarasi kukamilisha ujenzi wake.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko (kulia)akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Mbarawa (kushoto) alipokagua jengo jipya 'One Stop Centre' la TPA leo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) akitoa maelekezo katika ziara ya kukagua ujenzi wa jengo jipya 'One Stop Centre' la Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) lililopo bandarini leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko na Naibu Mkurugenzi wa TPA (Miundombinu), Eng. Karim Mattaka wakimsikiliza.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) akimsikiliza kwa makini mmoja wa abiria wa Kivuko cha Magogoni alipofanya ukaguzi wa kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) akiwa na baadhi ya abiria wa Kivuko cha Magogoni mara baada ya ukaguzi wa kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo katika ziara ya kukagua ujenzi wa jengo jipya 'One Stop Centre' la Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) lililopo bandarini leo jijini Dar es Salaam. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI KUMALIZA MGOGORO WA NYAMONGO-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza mgogoro ulipo kati ya wananchi wa Kata ya Nyamongo na muwekezaji wa mgodi wa North Mara.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi pamoja na mwekezaji wa mgodi huo wanaishi na kuendesha shughuli zao za kimaendeleo kwa kufuata sheria za nchi.Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Januari 18, 2018) wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kata ya Nyamongo, wilayani Tarime.

Waziri Mkuu amesema Serikali haiwezi kuvumilia kuona wananchi na wawekezaji wakigombana, inataka kumaliza mgogoro huo ili pande zote zifanye kazi zake kwa amani.Katika kuhakikisha mgogoro huo unakuwa historia Waziri Mkuu ameitisha kikao kitakachowakutanisha wawakilishi wa wananchi , viongozi wa mgodi na mbunge wa jimbo la Tarime Bw. John Heche.

Amesema katika hicho kitakachofanyika Januari 28, 2018 Ofisini kwa Waziri Mkuu mjini Dodoma, ambapo aliwakikishia wananchi hao kwamba Serikali italinda maslahi yao.Awali, Waziri Mkuu alitembelea kata ya Nyamwaga na kukagua kituo cha afya cha Nyamwaga, ambapo amesema kinatosha kupandishwa hadhi na kuwa hospitali ya wilaya.

Hivyo amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dkt. Francis Mwanisi aanze mchakato wa kupeleka vifaa katika kituo hicho ili wananchi wa Halmashauri ya Tarime waanze kutibiwa.Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. John Magufuli ameongeza bajeti ya ununuzi wa dawa na kufikia sh. bilioni 269 ili kuhakikisha hakuna mgonjwa anayekwenda hospitali na kukosa dawa.

Amesema mbali na kuongeza bajeti katika ununuzi wa dawa, pia ameziagiza halmashauri zote kuhakikisha suala la utoaji wa vitambulisho kwa wazee ili watibiwe bure linatekelezwa

ZIARA YA DK SHEIN ENEO LA UJENZI WA MATANKI YA MAFUTA MWANGAPWANI ZANZIBAR

0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Ardhi Zanzibar  Ahmeid Rashid akitowa maelezo ya ujenzi wa Matenki ya kuhifadhia mafuta katika eneo la Mangwa pwani Zanzibar (Picha na Ikulu).


KAKOLANYA KUMALIZANA NA YANGA MWISHO WA MWEZI HUU

0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

BAADA ya kutokuwepo katika kikosi cha Yanga kwa muda mrefu, Mlinda mlango wa timu hiyo Beno Kakolanya ameweka wazi kuwa sasa amerejea baada ya kumalizana na uongozi kuhusu stahiki zake za fedha za usajili.

Kakolanya ambaye alijiunga na Yanga msimu wa 2016/17 kutokea Tanzania Prisons ya Mbeya baada ya kufanya vizuri kwenye msimu mzuri uliopita na kusaini kandarasi ya miaka miwili.

Takribani mwezi mmoja sasa Kakolanya amekuwa nje ya kikosi cha Yanga kukiwa na taarifa kuwa ana madai yake ya fedha za usajili na kushindwa kuungana na wenzake.

Akizungumza na Globu ya Michuzi, Kakolanya amesema kuwa  tayari uongozi umemuhakikishia mwishoni mwa mwezi huu watamalizana nae fedha za usajili zilizosalia ila tayari ameanza kujumuika kwenye mazoezi na wenzake.

" Uongozi umeniambia kuwa mwishoni mwa mwezi huu watanipatia stahiki zangu kwahiyo kwa sasa naendelea na mazoezi kama kawaida nikiwa tayari nimeshaungana na wenzangu toka walivyorejea kutoka Zanzibar kwenye michuano ya Mapinduzi,"amesema Kakolanya.

Awali Kakolanya aliweka shinikizo la kutokuwepo katika kikosi cha Yanga hadi hapo atakapokamilishiwa fedha zake usajili ambazo alikuwa bado hajamaliziwa na uongozi wa klabu hiyo.

DK. MAHIGA AHIMIZA MAZINGIRA MAZURI KUVUTIA WAWEKEZAJI

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk.Augustine Mahiga amesema kuwa ili kufikia uchumi wa viwanda ni muhimu kutengeneza mazingira mazuri ya kuwavutia wawekezaji katika sekta mbalimbali zikiwamo za sheria, kodi, ajira,vvivutio vya uwekezaji na kilimo.

Dk.Mahiga, ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kuzindua kongamano la siku mbili lililoandaliwa na Ubalozi wa India nchini Tanzania kwa kushirikisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Lengo la kongamano hilo pamoja na mambo mengine washiriki wamezungumzia namna ya ushiriki wa sasa na siku zijazo unavyoweza kuleta amani katika nchi wanachama wa jumuiya hizo.Kauli mbiu ya kongamano katika kongamano hilo inasema "Amani, utulivu na maendeleo".

Dk. Mahiga amefafanua jambo hilo si jipya kuzungumzwa isipokuwa bado halijaeleweka na hivyo linatakiwa kuzunguzwa Tanzania pamoja EAC.

“Tunamkakati madhubuti wa kujenga viwanda katika EAC na SADC. Sasa kusema nataka viwanda ni kingine, kuvuta viwanda ni kingine, kufanya viwanda vizalishe na vistawi ni jambo lingine.

"Na ukisema unataka viwanda mazingira yapo?  unataka kufanikisha viwanda je  utaalam upo? hapo sasa kupitia mambo hayo matatu unaweza kuendesha viwanda,” amesema Dk.Mahiga.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwenye Kongamano la siku mbili lililoandaliwa na Ubalozi wa India nchini Tanzania kwa kushirikisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk.Augustine Mahiga akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua rasmi Kongamano la siku mbili ambalo limeandaliwa na Ubalozi wa India nchini Tanzania.Kauli mbiu ya kongamano hilo ni Amani, Utulivu na Maendeleo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WATEJA AIRTEL MONEY WAPATA GAWIO LA BILIONI 1.7/-

0
0

Na Agness Francis, Globu ya Jamii

KAMPUNI ya simu za mkononi Airtel imetangaza rasmi kugawa gawio la Sh.bilioni 1.7 kwa kila robo ya mwaka kwa wateja wake wote wanaotumia Airtel Money  ikiwa ni mara ya tano kufanyika tangu ianzishwe huduma hiyo mwaka 2015.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Masomo Airtel  Money Isack Nchunda, amesema kuwa leo wametoa rasmi Sh, bilioni 1.7 ambayo ni riba ya robo ya mwaka iliyopita  ikiwa zoezi hilo litakuwa endelevu badala ya ule utaratibu wa mwanzowa kila  miezi sita ambapo gawio hilo la faida litawafikia moja kwa moja  walengwa ambao ni wateja pamoja na mawakala wote wanaotumia huduma hiyo ya Airtel Money hapa nchini. 

Amefafanua Nchunda amesema Mr. Money atarudisha gawio kulingana na salio linalosalia katika akaunti kila siku kwa anayetumia huduma hiyo ambayo mteja atakuwa huru kufanya matumizi yake binafsi kama kununua bando, luku, na mahitaji mengine kupitia riba hiyo bila kupangiwa na Mr. Money  huyo.

Kwa upande wake Meneja wa Huduma za Airtel Money Ibrahim Malando, amewataka mawakala hao kuendelea kufanya huduma bora kwa wateja wao kwani ni hatua nzuri ya kujiongezea zaidi faida kwa gawio lijalo.
Mkurugenzi wa masomo Airtel Tanzania Isack Nchunda akiongea Jijini Dar es Salaam leo wakati wa gawio kwa wateja na mawakala wa Airtel money ambapo jumla Sh bilioni 1.7 zitatolewa kwa robo ya mwaka iliyoisha Disemba 2017.kushoto ni Meneja huduma za Airtel money  Ibrahim Malando na Meneja uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando.

 Meneja huduma za Airtel money Ibrahim Malando akiongea Jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza gawio kwa wateja na mawakala wa Airtel money ambapo jumla y sh bilioni 1.7 zitatilewa kwa robo ya mwaka iliyoisha Disemba 2017 katika ni Mkurugenzi wa masoko Airtel money Tanzania Isack Nchunda  na Meneja  uhusiano wa Airtel  Tanzania Jackson  Mmbando

OKWI NA UFUNGAJI BORA WA VPL

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Ikiwa ni katika kuhakikisha anabeba kiatu cha ufungaji bora msimu wa 2017/18 mshambuliaji wa Simba , Emmanuel Okwi leo ameweza kuifungia timu yake magoli 2 na kujiweka juu ya msimamo.

Okwi aliyefikisha magoli 10 ikiwa ni muda mrefu toka awe na ukame wa magoli huku na kuamsha mbio za ufungaji bora.

Katika mechi dhidi ya Singida, Okwi aliyeingua katika dakika ya 65 akichukua nafasi ya Mzamiru Yassin aliweza kuandika goli la 3 kwa timu yake kwenye dakika ya 75 akipokea pasi ya Kichuya.

Dakika ya 81, Okwi anaandika goli la 4 na la 10 kwa upande wake akipokea pasi ya Said Ndemla na kuzidi kudidimiza matumaini ya Singida United.

Awali Okwi alikwama akiwa na mabao nane kwa kipindi kirefu hadi mshambuliaji wa Mbao FC, Habibu Kiyombo akafikisha mabao 7.

Simba imeweza kuimaliza Singida United kwa mabao 4-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam goli la kwanza likifungwa dakika ya 3 na Shiza Kichuya na la pili dakika ya 25 na Asante Kwasi na kuendelea kusalia kileleni kwa alama 29 akifuatiwa na Azam yenye alama 27.

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA DARAJA MTO MARA

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la mto Mara linalounganisha wilaya za Tarime na Serengeti akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara Januari 18, 2018. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kuweka jiwe la msingi la daraja la mto Mara linalounganisha wilaya za Serengeti na Tarime Januari 18, 2018. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege , Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mara, Samweli Kiboyi, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwagilia mti alioupanda baada ya kuweka jiwe la musing la ujenzi wa daraja la mto Mara linalounganisha wilaya za Tarime na Serengeti akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara, Januari 18, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizunguma na wananchi wa Kijiji cha Nyamwaga wilayani Tarime akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara , Januari 18, 2018. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images