Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

WALIOPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA BILA KIBALI WAPANDISHWA KIZIMBANI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Mkurugenzi wa Saha Limited  na mwingine wa Lucky Shipping Co.Ltd, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka mawili ya uhujumu uchumi ikiwemo kupeperusha bendera ya Tanzania bila kibali kwa nia ovu.

Mwendesha Wakili wa Serikali, Wankyo Saimon amewataja washtakiwa hao kuwa ni Issa Haji au Salum (39) ambaye ni baharia na Mkurugenzi wa Kampuni ya Lucky Shipping pamoja na Abdullah Hanga (73) mfanyabiashara na Mkurugenzi wa Kampuni ya Saha ambaye ni mkazi wa Mbezi Beach.

Washitakiwa hao wanadaiwa kujihusisha na mtandao wa uhalifu kinyume sheria inayohusiana na vyombo vya baharini na Sheria ya Uhujumu uchumi.

Akisoma hati ya mashtaka wakili Simon amedai katika tarehe tofauti tofauti, kati ya Julai 19, mwaka jana na Januari 16, mwaka huu jijini Dar es Salaam,washtakiwa hao, walitoa ushauri, msaada na maelekezo katika kutenda kosa la jinai la mtandao wa uhalifu.

Amedai, kosa hilo ni kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye meli iitwayo ‘Huihang 68’ ambayo zamani ilijulikana kama Greko 02, bila kuwa na hati ya usajili kutoka kwa msajili wa meli nchini kwa lengo la kujipatia faida kutoka katika shughuli za uvuvi haramu.

Pia imedaiwa kuwa Julai 19, mwaka jana na Januari 16, mwaka huu ndani ya jiji la Dar es Salaam washitakiwa hao huku wakifahamu kuwa ni kosa kisheria waliruhusu upeperushwaji wa bendera katika meli hiyo bila kuwa na leseni kutoka kwa msajili wa meli kwa lengo la kuifanya ionekane kuwa ya Tanzania wakati sio kweli.

Hata hivyo, washitakiwa hawakutakiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.Hata hivyo, Saimon alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuieleza mahakama taarifa za upelelezi huo umefikia wapi.

Aidha upande wa mashtaka ulidai Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), amewasilisha hati ya kuzuia dhamana kwa washitakiwa hao kwani wakipewa dhamana wataingilia maslahi ya Taifa hivyo mahakama ijielekeze katika suala hilo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 22, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na upande wa utetezi kuwasilisha hoja zao kuhusu mapingamizi ya  hati ya DPP washitakiwa wamerudishwa rumande.
Watuhumiwa ambao ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lucky Shipping,   Issa Haji au Salum(kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Saha, Abdullah Hanga (Kushoto)  wanaodaiwa kujihusisha na uhujumu uchumi ikiwemo kupeperusha bendera ya Tanzania bila kibali kwa nia ovu wakiwa mahakamani wakisubilia kusomewa mashtaka yanayowakabili.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI AMTAKA MKANDARASI KUMALIZA DARAJA KWA WAKATI

$
0
0
Naibu waziri wa ujenzi ELIAS KWANDIKWA amemwagiza mkandarasi anayejenga daraja la RUHUHU liliopo lituhi wilayani nyasa mkaoni ruvuma ambalo pia linganisha mkoa wa LUDEWA kukamilisha kwa wakati ili kupisha shughuli za maendeleo zinazofanywa na wananchi katika maneneo hayo. Naibu waziri kwandikwa amesema hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa daraja hilo na kuridhishwa na hali ya ujenzi unaofanya na kampuni ya lukolo HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE

KAMATI YA RAIS YA KUCHUNGUZA BIASHARA YA MADINI YA TANZANITE YAANZA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI YA TANZANITE ONE

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuchunguza biashara ya madini ya Tanzanite ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi   akisalimiana  jijini Dar es salaam leo Januari 17, 2018   na wawakilishi wa kampuni ya Tanzanite One kabla ya kuanza na mazungumzo ambayo yanalenga kuhakikisha Tanzania inanufaika ipasavyo na rasilimali ya madini hayo ambayo yanachimbwa nchini Tanzania pekee. Picha na IKULU

WATEJA SOKO LA KUKU SHEKILANGO WAPUNGUA

$
0
0
Na Agness Francis, Globu ya Jamii 

WAFANYABIASHARA wa kuku katika soko la Kuku lililopo Shekilango jijini Dar es Salaam wamesema kwa sasa soko limekuwa gumu kidogo kutokana na kupungua kwa wateja tofauti na siku za nyuma.

Wakizungumza na Michuzi Blog, leo sokoni hapo ,wafanyabishara hao wamesema hali hiyo imewafanya wawe katika wakati mgumu kurudisha faida.

Mmoja wa wafanyabishara wa kuku sokoni hapo Mussa Shaaban amesema changamoto ya wateja wa kuku kupungua imekuwa kubwa na hivyo kijikuta wakiwa na hali ngumu kiuchumi kwani kuku hao kabla ya kununuliwa wanahitaji kuhudumiwa na hiyo nayo inahitaji gharama yake.

Pia amesema changamoto nyingine kwenye biashara hiyo ni baadhi ya kuku kufia njiani kutokana na umbali mrefu wanaotumia wakati wa kuwasafirisha hadi kufika sokoni hapo kwani wanawanunua mikoani.

Kuhusu bei, amesema wao wananunua kuku wa kienyeji kwa Sh 13,500 hadi Sh 14, 000 na kisha wao huuza kuku mmoja kwa Sh 18,000 hadi Sh.20,000. Pia amesema kwa kuku wa kisasa wamekuwa wakiwauza kwa Sh 6,300.

Pia imeelezwa na wafanyabishara hao kuku wa mayai wao wananunua kuku mmoja kwa Sh 8,000 hadi Sh 8,500 na kisha wanawauza kwa reja reja kwa Sh10,000 na kwa jumla wanauza Sh 9000 hadi Sh.9500.

SERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 24.4 KUJENGA NA KUKARABATI MELI

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa shilingi bilioni 24.496 kwa ajili ya kujenga meli mpya mbili na kukarabati meli tano ili ziweze kutoa huduma ya uchukuzi wa kusafirisha abiria na mizigo katika maziwa makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa. 

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu ujenzi wa meli katika maziwa makuu kwenye kikao kilichofanyika bungeni mjini Dodoma. 

Mhe. Nditiye aliongeza kuwa fedha hizo tayari zimeshatolewa na Serikali na kupatiwa Kampuni ya MSCL kwa ajili ya kuanza ujenzi wa meli 2 mpya za kubeba abiria na mizigo katika ziwa Tanganyika na Victoria na kukarabati meli 5 ambazo ni MV. Victoria, MV. Butiama, MV. Liemba, MV. Umoja na MV. Serengeti. 

Mhandisi Nditiye aliongeza kuwa lengo la Serikali la kutoa fedha hizo ni kuboresha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo katika maziwa makuu ili wananchi waweze kupata huduma za usafiri wa uhakika; kwa wakati na zinazozingatia usalama wa abiria na mizigo yao; kuiwezesha Serikali kupata mapato na kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla; na kwa kutambua fursa ya biashara iliyopo kwenye maziwa hayo kwa kuzingatia kuwa meli hizo ni kiungo kikubwa baina ya nchi yetu na nchi za jirani za Uganda, Kenya, Zambia, Malawi na DRC Congo kwa kuwa zinatumia meli zetu kusafirisha abiria na mizigo yao kupitia maziwa hayo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akipata maelezo kutoka kwa Kapteni Desiderius Chuwa wa Meli ya MV. Clarias kuhusu usalama wa chombo hicho na abiria wake kabla ya kuanza safari ya kutoka Mwanza kwenda Kisiwa cha Ukerewe wakati wa ziara yake mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa maelekezo kuhusu usalama wa abiria na matumizi ya vifaa vya uokoaji majini kwa watendaji na abiria wa meli ya MV. Clarias kabla ya kuanza safari ya kutoka Mwanza kwenda Kisiwa cha Ukerewe wakati wa ziara yake mkoani humo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akipatiwa maelezo kuhusu matengenezo ya yaliyofanyika ya mfumo wa mafuta wa meli ya MV. Clarias inayosafirisha abiria kutoka Mwanza kwenda Kisiwa cha Ukerewe wakati wa ziara yake mkoani humo. Wa kwanza kulia ni Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSL) Bwana Eric Hamissi.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) akikagua meli ya MV. Clarias inayosafirisha abiria kutoka Mwanza kwenda kisiwa cha Ukerewe wakati wa ziara yake mkoani humo. Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSL) Bwana Eric Hamissi (kushoto) akitoa maelezo kuhusu meli hiyo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) alipokagua meli ya MV. Clarias inayomilikiwa na Kampuni ya Huduma za Meli (MSL) ikiwa tayari kusafirisha abiria kutoka Mwanza kwenda kisiwa cha Ukerewe wakati wa ziara yake mkoani humo. 

ZANTEL YAZINDUA KAMPENI YA ‘JERO YAKO TU' KUWAZAWADIA WATEJA WAKE

$
0
0
Kampuni ya Mawasiliano ya ZANTEL, leo imezindua kampeni yake kabambe inayoitwa 'JERO YAKO TU', promosheni ambayo imelenga kuwashukuru wateja kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu.

Kampeni hiyo ambayo imeanza rasmi siku ya leo, itadumu kwa muda wa miezi mitatu huku takribani washindi 235 wakitarajiwa kuibuka na zawadi kabambe kutoka Zantel.

Zawadi kubwa katika promosheni hii itakuwa ni pamoja na magari matatu aina ya Suzuki Carry kwa washindi watatu, ambazo zitakabidhiwa mwishoni mwa kampeni hii mwezi Machi.Zawadi za kila wiki ni pamoja na pikipiki 1, na baiskeli 4 huku zawadi za kila siku zikiwa ni simu aina ya smartphone 4G pamoja na fedha taslimu kiasi cha Sh. 50,000/= kila siku.

Kwa mujibu wa Zantel, Promosheni ya ‘JERO YAKO TU' ni mahususi kwa ajili ya kuwazawadia wateja na kuthamini uvumilivu wao wakati ambapo mtandao huo ulikuwa kwenye hatua za maboresho na hatimaye kuzindua mfumo wa 4G katika mikoa 22 nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mjini Zanzibar, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Sherrif El- Barbary alisema, "Sisi Zantel tunathamini mchango wa wateja wetu ambao wametuonyesha kwa miaka mingi, na wanastahili kupongezwa kwa kuendelea kuwa nasi hususani kutufanya kuendeliea kuwa mtandao wa simu unaoongoza Zanzibar pamoja na kuongoza kwenye utoaji wa huduma ya data nchini Tanzania.

Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Baucha) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘JERO YAKO TU’ iliyozinduliwa na Zantel jana mjini Zanzibar. Kampeni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Sherif El-Barbary na kushoto ni Mkurugenzi wa kitengo cha Biashara Zantel, Wane Ngambi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Sherif El Barbary akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘JERO YAKO TU’ iliyozinduliwa na Zantel jana mjini Zanzibar. Kampeni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa kitengo cha Biashara Zantel, Wane Ngambi (kushoto) na Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Baucha) (kulia).
Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Sherif El-Barbary akijaribu moja ya Pikipiki ambazo zitakazoshindaniwa kila wiki kwenye Kampeni ya ‘JERO YAKO TU’ iliyozinduliwa na Zantel jana mjini Zanzibar. Kampeni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu. Pamoja nae ni Mkuu wa Zantel, Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Baucha). 


MAKAMU WA RAIS ATAKA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUHARIBU MAZINGIRA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka  Watanzania kuchana na  vitendo vya uharibifu wa mazingira kwa lengo la kujiepusha  na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

Mama Samia amesema hayo leo jijijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya ujenzi wa kuta za kingo katika Bahari ya Hindi eneo la Ocean Road na Kigamboni.

Amesema kuwa Tanzania imeharibu mazingira yake kwa kiasi kikubwa hali inayofanya sehemu kubwa ya maeneo yote kuwa na hali tofauti na tulivyotegemea.Ametoa mfano Mji wa Dodoma ambao watu wamekata miti yote na hivyo kusababisha eneo hilo kuwa jangwa kiasi cha kusababisha maafa pindi mvua zinaponyesha.

Ametaja kuwa  mikoa mingi ambayo iliyokuwa na baridi sasa hivi imekuwa ikiongoza kwa joto sawasawa na mikoa iliyopo Pwani kwa mfano mikoa ya Kilimanjaro kila ukiangalia utabiri wa hali ya hewa unaambiwa ina nyuzi joto 32 hadi 33, kiasi ambacho awali haikuwahi kufikia hapo. Amesema adhabu yote hiyo na  athari zinazoonekana sasa inatokana na uharibifu huo mkubwa wa mazingira unaofanywa na baadhi ya wanachi kwenye maeneo mbalimbali nchini .

“Napenda kutumia mfano anaotumia Papa Francis kuwa ukimkosea mwanadamu utakwenda kulia kanisani au Msikitini utasamehewa lakini ukiyakosea mazingira hayana Msikiti wala Kanisa yatakuadhibu mpaka utakaporudi kuwa rafiki tena,"amesema Makamu wa Rais .

Ameongeza kuwa "Nasi tumeharibu mazingira kwa kukata miti, kuchimba mchanga katika fukwe na matokeo yake bahari imepata nguvu ya kula ardhi yetu,hivyo turekebishe tulipoharibu ili kurudisha urafiki huu".Amesema kwa Mkoa wa Dar es Salaam wakazi wake wamekuwa wakitupa taka katika mitaro na ikiziba inaleta madhara ya mafuriko, hivyo hiyo ni hasara kwa Taifa kwa kuwa tunatumia muda mwingi kutoa pole na anayepewa pole hutegemea uende na chochote umsaidie kama mahindi na fedha. 

UPELELEZI KESI YA KUISABABISHIA HASARA SERIKALI BILIONI 2.4/- MBIONI KUKAMILIKA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

UPELELEZI katika kesi  ya uhujumu uchumi na kuisababishia hasara Serikali ya Shilingi bilioni 2.4 inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini ya Madini, Archard Kalugendo na mwenzake upo hatua za mwisho kukamilika.

Mbali ya Kalugendo, mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Mthamini wa Madini ya Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu.

Wakili wa Serikali,  Ester Martin amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi  Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuongeza kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi bado haujakamilika na kwamba wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuja kieleza hatua ya upelelezi.

Katika tarehe ya kutajwa iliyopita, upande wa mashitaka ulidai kuna baadhi ya vitu vinapaswa kukamilishwa katika kesi hiyo ikiwemo kusubiri uamuzi kama ikasikilizwe Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi  'Mafisadi' ama lah.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 31, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.Kwa pamoja washitakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababisha Serikali hasara ya zaidi ya Sh.bilioni 2.4.

Inadaiwa kuwa kati ya August 25 na 31 mwaka  2017 katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga, kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathamini walioajiriwa na Wizara ya Nishati na Madini waliisababisha serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha.


OPERESHENI YA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YASHIKA KASI KWA WANUFAIKA WA MIKOPO

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB) imesema kuwa kwa kipindi cha miezi mitatu ya operesheni ya kudai mikopo kwa wanufaika hao watafikiwa katika ofisi zao kutokana na tangazo waliotoa hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari katika operesheni, Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji wa Bodi ya Mikopo, Phidelis Joseph amesema kuwa utaratibu umewekwa kwa watu kulipa bila kujalisha mtu alimeajiliwa au amejiajiri.Katika operesheni hiyo wametembelea kampuni mbili ambazo zinadawa zaidi ya milioni tisa zinazotokana na faini ya kuchelewesha mikopo.

Kampuni hizo ni Hegy Engeenering(T) Limeted pamoja na Sincro Sitewatch ambapo zinadaiwa kuchelewesha malipo katika bodi ya mikopo hali ambayo inachelewesha watu wengine wasinufaike.Kampuni ya Sincro Sitewatch inadaiwa shilingi 7.6 milioni ambazo ni faini inayotokana na kuchelewesha kulipa mikopo kwa wakati uliowekwa kisheria.

Joseph amesema katika operesheni hiyo wamekuwa na changamoto zinazotokana na baadhi ya wahusika kushindwa kutoa ushirikiano pale wanapowatembelea.Aidha amesema kuwa kwa wale ambao watashindwa kulipa fedha kwa kipindi kilichowekwa bodi itawafungulia mashitaka kwa mujibu wa sheria zilizowekwa.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Hegy Engeneering (T) Limited, Benedict Mushi amesema kuwa bodi inafanya utaratibu mzuri kwa kuwa kama mamlaka ya mapato nchini (TRA) kupitia wadai wake.

Amesema kuwa fedha wanazodaiwa watalipa kwa wakati kwa kutambua umuhimu fedha hiyo katika kusomesha watanzania wenye mahitaji ya mkopo wa kuweza kupata elimu kwa maendeleo ya taifa.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu , Phidelis Joseph akizungumza katika kampuni ya Hegy Engeneering (T) Limited kuhusiana na urejeshaji mikopo kwa wanufaika walioajiliwa katika kampuni hiyo ikiwa ni operesheni ya bodi ya mikopo kufatilia wanufaika, jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Hegy Engeneering (T) Limited, Benedict Mushi akizungumza na maofisa wa Bodi ya Mikopo jinsi watavyotekeleza kulipa fedha katika bodi kwa muda uliopangwa, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Phidelis Joseph akizungumza na waandishi habari kuhusiana na operesheni katika kampuni mbili ambazo wanadai zaidi ya milioni tisa, jijini Dar es Salaam.

MPINA AKAMATA MAROBOTA 1152 YA NYAVU HARAMU MWANZA NA SINGIDA ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 894.

$
0
0

Na John Mapepele

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Joelson Mpina amekamata marobota 1152 ya aina mbalimbali za nyavu haramu zisizoruhusiwa kisheria kutumika kuvulia samaki zenye thamani ya shilingi milioni 894 jijini Mwanza na Singida ambapo baadhi ya nyavu hizo zimetaifishwa na nyingine kuteketezwa na wamiliki wakitakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 120 ndani ya masaa 24 kwa makosa ya kufanya biashara ya nyavu hizo kinyume cha sheria.

Akiongea na Vyombo vya Habari jijini Mwanza katika ghala la nyavu la Meshack Chacha mara baada ya kukamata shehena ya marobota 600 ya nyavu haramu kwenye ghala lake, Mhe. Mpina alisema nyavu haramu 294 kati ya 894 zilikamatwa na kikosi kazi maalum cha kudhibiti uvuvi haramu katika kanda ya Ziwa Victoria alichokiunda hivi karibuni wakati mmoja wa wafanyabiashara hao Masagati Majani alijaribu kutorosha vyavu hizo kwa kutumia gari aina ya Scania lenye namba za usajili T.452 BBS kutoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam.

Gari hilo lipo katika kituo cha polisi cha Singida kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria ambapo kulingana na sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003, imetoa mamlaka kwa watendaji wa Serikali kutaifisha mali zote zilitumika katika uvuvi haramu kupitia kifungu cha 37(a) (ii) na (iii)

Aliwataja wamiliki wengine ambao walikamatwa kutokana na kujihusisha na biashara haramu ya uagizaji na uuzaji wa vyavu zisizoruhusiwa kisheria kuwa ni Josia Jonam Obielo, Jeremiah Asam na Dastun Venant ambapo alisema Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba wafanyabiashara wote wanao agiza na kuuza zana haramu za uvuvi wanakamatwa na sheria kali zinachukuliwa ili kudhibiti uvuvi haramu nchini.

“Niliapa kusimamia ulinzi wa raslimali za uvuvi nchini hivyo nitahakikisha operesheni hii inakuwa ya kudumu katika kupambana na uvuvi haramu hadi uvuvi haramu utakapokwisha” alisisitiza Mpina

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina(mwenye kofia) akiwa na Kiongozi wa Operesheni ya maalum ya kudhibiti uvuvi haramu katika ukanda wa Ziwa Victoria, Shafii Ramadhani Kiteri wakikagua shehena ya marobota 600 ya nyavu haramu zenye thamani ya shilingi milioni mia tano inayomilikiwa na Meshaki Chacha jijini Mwanza leo. Nyavu hizo zimetaifishwa na nyingine kuteketezwa na mmliki akitakiwa kulipa faini ya shilingi milioni hamsini ndani ya masaa 24.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani na kofia )akisikiliza jambo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ukerewe, Frank Bahati (kushoto) wakiwa kwenye boti ya doria kutoka katika kijiji Kakukuru wakielekea kwenye kambi ya uvuvi ya Kisiwa cha Galinzila ambapo Mhe.Waziri alifanya mkutano na wavuvi . Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estomiah Chang’a. (Na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani)akikagua nyavu haramu za kuvulia samaki katika kijiji cha Kakukuru wilayani Ukerewe ambapo alichoma moto nyavu haramu za zenye thamani ya shilingi bilioni mbili. Kulia ni Lameki Mongo, Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kushoto ni Abbakary Murshidi, Afisa Uvuvi wa Wilaya ya  Ukerewe (Na John Mapepele) Aapa kutokomeza uvuvi haramu nchini
Asema imebaki 3% tu ya Sangara wanaokubalika kuvuliwa katika ziwa Victoria .

Dkt. Abbas Atembelea Vyombo vya Habari Mkoani Dodoma

$
0
0
​Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA

Mkurugenzi wa Idara Habari( MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi ameanza ziara ya kutembelea vyombo vya habari Mkoani Dodoma kwa lengo la kuona na kujua changamoto za kiutendaji pamoja na jinsi gani wamejipanga juu ya Serikali kuhamia Dodoma.

Akiwa katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Abbasi amevitaka vyombo vya habari vya Dodoma kuwa tayari na ujio wa Serikali kuhamia Dodona kwani matukio mengi ya kiserikali yatafanyika Mkoani humo.

"Kwa baadhi ya matukio yaliyofanyika hapa Dodoma nimeona uzubaifu kwa baadhi ya waandishi wa habari hivyo wanahabari wenzangu tuchangamke kwani matukio mengi ya Serikali yatafanyika hapa" amefafanua Dkt. Abbasi.Aidha, Dkt. Abbasi ameutaka uongozi wa TSN kufuata maadili katika utendaji kazi kwani wananchi hutazama kampuni hiyo kwa jicho la utofauti kama chombo cha Serikali.

“Mkiwa kama Kampuni ya Magazeti ya Serikali mnatakiwa kuibeba agenda kuu ya Serikali ya Awamu ya Tano kufikia uchumi wa kati kupitia Viwanda" ameongeza Dkt.Abbasi.

Akiwa katika Ofisi za Mwananchi Communications Ltd mkoani humo, Dkt Abbasi amesema kuwa asilimia 99 ya waandishi wamejikita katika masuala ya kisiasa kuliko masuala ya maendeleo ya nchi au bajeti mbalimbali zinazohusu serikali hivyo ameshauri vyombo vya habari kujikita katika zaidi katika masuala ya maendeleo kwa manufaa ya jamii.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwaeleza watumishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) umuhimu wa kubeba  ajenda ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda wakati wa ziara yakutembelea vyombo vya habari Mkoani Dodoma  iliyoanza mapema leo.

 Muwakilishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali Mkoani Dodoma Bw.Felix Mushi akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi katika Ofisi za Kampuni hiyo Mkoani Dodoma.
 Watumishi wa Gazeti la Mwananchi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi  wakati wa ziara yake yakutembelea vyombo vya Habari Mkoani Dodoma iliyoanza Januari 17, 2017.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi  akiagana na Meneja Masoko wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd Mkoani Dodoma mara baada  ya kutembelea Ofisi za Kampuni hiyo  na kuzungumza na wafanyakazi, kushoto ni Mkuu wa Kanda wa Gazeti la Mwananchi.(Picha zote na Frank Mvungi- Maelezo Dodoma)

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MBUNGE NJALU AFANYA HARAMBEE YA UJENZI WA SHULE SIMIYU

$
0
0

Na Mwandishi wa Globu, Simiyu.



Mbunge wa jimbo la Itilima Mkoani Simiyu Njalu Daudi Silanga ameshiriki ibaada katika kanisa la SDA liliopo Kijiji cha Itubilo na kufanya harambee ya uchangiaji wa ujenzi ya shule ya  Itubilo Pre & Primary Medium School  na kuhamasisha wananchi kujitokeza na kusaidia kwenye ujenzi huo.

Njalu ambaye alikuwa mgeni ramsi kwenye harambee hiyo, aliweza kuzungumza na wanakijiji wa Itubilo na kuwataka wafahamu kuwa msingi mkubwa wa urithi kwa mtoto ni elimu na zaidi wanakijiji washirikiane kwa pamoja kuhakikisha wanafanikisha ujenzi wa shule hiyo itakayokuja kuwa na manufaa kwa vizazi vya baadae.

Wakati wa uendeshaji wa jarambee hiyo, Njalu aliweza kuchangia kiasi cha fedha shillingi milioni moja na laki tano (1,500,000) pamoja na mifuko ya saruji 170 ili kuongeza nguvu ya ujenzi wa kanisa hilo.

Wazee wa Kanisa kwa pamoja waliweza kumshukuru Mbunge wao Njalu kwa hatua kubwa aliyofanya ya kuwapatia mifuko ya saruji ambapo wanaamini kuwa wataitumia kuendeleza ujenzi wa shule hiyo itakayokuwa ni kuanzia elimu ya  awali na Msingi. 

Mbunge wa jimbo la Itilima Mkoani Simiyu Njalu Daudi Silanga akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa shule ya ITUBILO PRE &APRIMARY MEDIUM SCHOOL lililojengwa kwa mfuko wa kanisa mmara baada ya kumaliza ibda ya pamoja na waumini wa kanisa hilo, Pembeni ni Mchungaji wa kanisa la SDA Itubilo Michael Phabian.

Mbunge wa jimbo la Itilima Mkoani Simiyu Njalu Daudi Silanga akizungumza na waumini wa Kanisa la SDA Itubilo pamoja na wanakijiji baada ya kumaliza ibada ya pamoja na kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Itubilo Pre & Primary Medium School na kuchangia kiasi cha shillingi milioni moja na laki tano (1,500,000) na mifuko ya saruji 170 kwa ajili ya ujenzi wa shule.


Mbunge wa jimbo la Itilima Mkoani Simiyu Njalu Daudi Silanga akifuatilia jambo sambamba na wanakijiji wa Itubilo wakati wa harambee ya uchangiaji ya ujenzi wa shule ya Itubilo Pre & Primary Medium School na kuchangia kiasi cha shillingi milioni moja na laki tano (1, 500,000) na mifuko ya saruji 170 kwa ajili ya ujenzi wa shule.

HABARI ZAIDI BOFYA HABA





SIJARIDHISHWA NA UJENZI WA KITUO CHA SIRARI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na ubora wa ujenzi wa kituo cha forodha cha Sirari kilichopo kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.

Kufuatia hali hiyo amemtaka Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) afike ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma akiwa na mkandarasi aliyejenga kituo hicho.“Serikali haiwezi kuvumilia ujenzi wa hovyo kiasi hiki, namtaka Kamishna wa TRA aje ofisini kwangu Januari 25, 2018 pamoja na mkandarasi aliyejenga kituo hiki akiwa na nyaraka zote za ujenzi wa jengo hilo.”

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Januari 17, 2018) mara baada ya kumaliza kukagua kituo hicho kilichopo wilayani Tarime, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mara.Waziri Mkuu amesema hajaridhishwa na ujenzi huo kwa kuwa upo chini ya kiwango. Kituo hicho kilianza kujengwa mwaka 2011 na kukamilika mwaka 2014.

Waziri Mkuu amejionea mwenyewe kuta za jengo hilo zikiwa na nyufa nyingi kuanzia ukutani hadi sakafuni na pia rangi za baadhi ya kuta zikiwa zimebanduka.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wananchi wa wilaya hiyo kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa kuzingatia sheria na wajiepusha na biashara za magendo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimu wagonjwa wakati alipotembela  hospitali ya wilaya ya Tarime akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara, Januari 17, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adm Malima. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kukagua jengo la Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Sirari na kueleza kutorihishwa kwake na viwango vya ujenzi wa jengo hilo (pichani) ambalo limeanza kuharibika Januari 17, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adama Malima. (Picha na Ofisi  Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kukagua jengo la Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Sirari na kueleza kutorihishwa kwake na viwango vya ujenzi wa jengo hilo (pichani) ambalo limeanza kuharibika Januari 17, 2018. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Sirari wilayani Tarime Januari 17, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Boreha wilayani Tarime, Januari 17, 2018. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

HII NDIO ASILI YA JINA LA MKOA WA MBEYA

$
0
0
 Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya Mikoa 32 ya Tanzania, unapatikana nyanda za juu kusini mwa nchi yetu hii. jina la mkoa wa Mbeya ni neno la kiasili la kabila la Kisafwa lilikuwa likitamkwa ‘Ibheya’ likiwa na maana chumvi. Inaelezwa kuwa wafanyabiashara wengi walikuwa wakifika eneo hilo kwa biashara ya kubadilishana chumvi na mazao yao.

Inaelezwa kuwa mji wa sasa wa Mbeya ulianzishwa na wakoloni Waingereza mnamo mwaka 1927 kufuatia kushamiri kwa upatikanaji wa dhahabu kwenye milima ya Loleza na mkondo wake uliokwenda mpaka kufika mji wa Chunya.

Wakazi wenyeji wa mkoa wa Mbeya ni wa kabila la Wasafwa ambao wamekuwa wakihamia milimani kupisha wageni. Kukua kwa kasi kwa jiji la Mbeya kumepelekea wenyeji hao kuuza maeneo yao na wao kurudi maeneo ya milimani wakiendelea kujishughulisha na kilimo pamoja na ufugaji kidogo. 
 Mkoa wa Mbeya kwa sasa una wilaya nne, hii ni baada ya kugawanywa kwa mkoa huo na Mkoa wa Songwe ambao nao pia umebakiwa na wilaya nne ambazo ni Ileje, Chunya, Mbozi na Momba. 

Leo hii eneo la wilaya ya Mbeya ambako ndipo jiji lilipo limetawaliwa zaidi na Wanyakyusa na Wakinga wakiwa ndiyo wafanyabiashara wakubwa na Wahindi pia.

Wenyeji wengine wa Mbeya ni watu wa kabila la Wamalila, Wenyeji wa wilaya za Rungwe na Kyela ni Wanyakyusa Wenyeji wa wilaya ya Mbarali ni Wasangu, Wawanji, Wabena na Wakinga.

Wenyeji wa wilaya ya Ileje ni Wandali, Wenyeji wa wilaya ya Chunya ni Wabungu ingawa watu waishio huko zaidi ni Wanyiha. Wenyeji wa wilaya ya Mbozi ni Wanyiha na Wanyamwanga, lakini mji wa Tunduma umetawaliwa zaidi na Wakinga ambao ndiyo wafanyabiashara wenye kumiliki uchumi wa mji huo mdogo.

SERIKALI YATOA TAMKO SAFARI YA SIMBU, YAWAONYA TFF

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

SERIKALI imetoa tamko kuhusu ushiriki wa mwanariadha Alphonce Simbu katika mashindani ya Jumuiya ya Madola yanayotarajiwa kufanyika April mwaka huu.

Mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika Gold Coast nchini Australia, ambapo Serikali na Kamati ya Olimpiki Taifa (TOC) walipokea barua kutoka kwa Simbu ya kuomba ashiriki mashindano ya London Marathon ambayo ni makubwa zaidi kuliko ya Jumuiya ya Madola.
 
Simbu ambaye ni mshindi wa tatu wa London Marathon 2017, Serikali kwa kushirikiana na Chama cha Riadha (RT) na kamati ya Olimpiki (TOC) walikaa katika kikao cha pamoja Januari 13 mwaka huu na waliridhia ombi la Simbu kuweza kushiriki huko na pia aweze kupata muda wa kujiandaa zaidi ili kuiwakilisha vyema Taifa katika mashindano hayo.

Akitolea ufafanuzi huo, Ofisa habari wa Baraza la Michezo Taifa (BMT) Najaha Bakari amesema kuwa Watanzania wasiwe na hofu kwani wameshafanya uchaguzi wa wawakilishi wa kwenda kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola na wanaamini kuwa watafanya vizuri zaidi na kurudisha medali nyumbani.

Mbali na hilo, Najaha amesema kuwa vyama vyote vya michezo nchini vilivyopo chini ya BMT wanatakiwa kuwasilisha kalenda za mwaka kabla ya Februari 10 mwaka huu na kwa chama chochote ambapo hakitafanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

"Kuna vyama kila mwaka vinakuwa haviwasilishi kalenda yao ya mwaka ambapo mfano wake ni Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) ambao wao wanaona ni chama kikubwa sana ila wanatakiwa wajue kuwa wote ni wadogo na wanatakiwa wawasilishe kalenda yao BMT,"amesema Najaha.

Najaha amesisitiza kuwasilishwa kwa kalenda hizo kutasaidia katika kuandaa miundombinu ya viwanja kwani kumekuwa na muingiliano wa baadhi ya matukio ya michezo kutokana na kutokuwa na kalenda za vyama vyao.


MAKALA YA SHERIA:JE ALIYETEULIWA NA MAREHEMU KWENYE WOSIA KUSIMAMIA MIRATHI ANAHITAJI KUTHIBITISHWA NA MAHAKAMA ?.

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.


 Wako  wasimamizi  wa  mirathi  wa  aina  mbili. Kwanza ni  yule  ambaye  marehemu  mwenyewe  amemteua  kabla  ya  kufa  kwake  na  akaandika/kusema  kwenye  wosia  kuwa  fulani  ndiye  atasimamia  mirathi  yangu  baada  ya  kuondoka.


Pili,  ni  yule  ambaye  hakuteuliwa  na  marehemu  mwenyewe  bali   ameteuliwa  na  wanafamilia  kwenye  kikao  cha  familia. Kwa  walio  wengi  huyu  ndiye  tunamjua  kuwa  ni  lazima  jina  lake  lipelekwe  mahakamani  kwa  ajili  ya  kuthibitishwa  ili  aweze kuwa  msimamizi  kamili.  Makala yatapitia Sheria  ya  Usimamizi  wa Mirathi, Sura ya 352  na kanuni zake.


1.      HAKI  NA  WAJIBU  WA  WASIMAMIZI  WA  MIRATHI.


Haki  na  wajibu  wa  msimamia  mirathi  aliyeteuliwa  na  marehemu kabla ya kifo na  ambaye  hakuteuliwa na marehemu ni  sawa. Awe  aliteuliwa  na  marehemu  mwenyewe  au  aliteuliwa  na  wanafamilia  bado  haki  na wajibu  alionao  ni  uleule. 


Wajibu  mkuu  wa  msimamia  mirathi  ni  kuwa  mwadilifu, na  kuenenda  kwa  mujibu  wa  sheria  katika  kila  hatua  anayopiga katika  kusimamia  kwake  mirathi.



2.    SIO  LAZIMA  MSIMAMIZI  WA MIRATHI  AWE  NDUGU/MWANAFAMILIA.


Hili ni  muhimu  zaidi  kulieleza.  Sio  kweli  kuwa  msimamizi  wa  mirathi  lazima awe  mtoto  wa  marehemu, shangazi, baba  mdogo/mkubwa,  mjomba kaka,dada nk.  Bali  msimamizi  wa  mirathi  anaweza  kuwa yeyote.  Suala  la  msingi  ni  atimize  sifa  za  kuwa  msimamizi  wa  mirathi. Na katika sifa hamna udugu.


Hakuna  haja  ya  kuwa  na  ugomvi  kuwa  msimamizi  wa  mirathi  lazima  atoke  katika  familia. Hakuna  ulazima  huo  ikiwa  mmeshindwa  kuaminiana  kwenye  familia. Mnaweza  kumteua  hata  kiongozi  wa  dini au  mtu  mwingine  yeyote  muadilifu  ambaye  mnadhani  ataweza  kutenda  haki  katika usimamizi.


Jambo  jingine  msimamizi  wa  mirathi  sio  lazima  awe  mmoja. Ikiwa  kuna  pande mbili  zinazozana  basi  sheria  inaruhusu  kila  upande  kutoa  msimamizi  wa  mirathi  ili  alinde  maslahi  ya  upande  wake.  Kwahiyo  wasimamizi  watakuwa  wawili   na  sheria  haikatazi.


Nyongeza ya  hapo ni kuwa hata kampuni  au taasisi  inaweza kuteuliwa kusimamia mirathi.



                   KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

ELIMU BURE KWA WOTE: TULIAHIDI TUMETEKELEZA

$
0
0
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg. John Lipesi Kayombo akiwaonyesha utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2015 - 2020 wajumbe wa Kamati ya siasa Wilaya ya Ubungo inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo Ndg. Lucas Mgonja.

Mkurugenzi Kayombo kwa kushirikiana na watumishi wa Manispaa hiyo ameweza kujenga ukuta (fensi), vyoo na vyumba nane vya madarasa katika shule ya msingi Ubungo Plaza.

Kabla ya hapo shule hiyo ilikuwa haina uzio,hali ambayo ilikuwa ni hatarishi kwa wanafunzi wa jinsia zote.

Pia kulikuwa na uhaba wa vyoo, ambapo kilikuwa ni chanzo kikubwa cha magonjwa.Sambamba na hilo wanafunzi walikuwa wanasoma katika majengo chakavu hali iliyokuwa ikihatarisha maisha yao.

Habari njema ni kuwa Mkurugenzi Kayombo ameahidi kujenga shule ya Sekondari ya A - level katika eneo hilo.Jambo ambalo litakuwa ni Mara ya kwa Manispaa hiyo tangu ianzishwe.

Hongera Mkurugenzi Kayombo kwa kuendelea kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2015 - 2020 kwa vitendo.
vyumba nane vya madarasa vikiwa katika hatua ya mwisho kabisa,katika shule ya msingi Ubungo Plaza.
 Ukuta wa shule hiyo 
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg. John Lipesi Kayombo akiwaonyesha utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2015 - 2020 wajumbe wa Kamati ya siasa Wilaya ya Ubungo inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo Ndg. Lucas Mgonja.
 Vyoo vya shule hiyo vikiwa tayari kuanza kutumika.

ALICHOKIZUNGUMZA DKT NDUGULILE KWA WANAWAKE WAJASILIAMALI WA MKOA WA MBEYA

MWENYEKITI WA UVCCM KHERI JAMES AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI MBALI MBALI WA UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM.

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Cha Mapinduzi Ndugu Kheri Denis James (MCC) jana amekutana na kufanya mazungumzo na kamati ya Utekelezaji ya Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wajumbe wa Baraza la Vijana (UVCCM) Wilaya ya Kinondoni kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi wa marudio utakaofanyika tarehe 17 Februari, 2018.

Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti amesisitiza kuwa  nguvu ya Vijana wa CCM itumike vizuri katika kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo Uchanguzi huo.  ''Suala la ushindi wa CCM katika uchaguzi huu wa marudio halina mjadala tutashinda kwa heshima, Amani na  demokrasia vijana wa CCM tumejipanga vyema kufanikisha hilo ngazi zote"Alisisitiza  Mwenyekiti Kheri

Wakati huo amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Viongozi wa Matawi yote ya Vyuo na Vyuo Vikuu vilivyopo Mkoa wa Dar es Salaam. 

''Tunatambua na kuthamini mchango wa Vijana wenzetu wote katika jamii mkiwemo ninyi wa Vyuo na Vyuo Vikuu tunawategemea sana hivyo tutaendelea kufanya kazi nanyi katika maeneo yote katika kutimiza wajibu wetu wa msingi” Alibainisha Mwenyekiti Kheir.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Mussa Kilakala, Mwenyekiti wa Seneti Mkoa wa Dar es Salaam Asha Feruzi pamoja na Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Alex Gwantwa.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza  kwa Msisistizo wakati wa kikao na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya mkoa wa dar esa salaam pamoja na Baraza kuu la Vijana Wilaya ya Kinondoni, kulia ni Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar Es Salaam Mussa Kilakala,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza wakati wa kikao na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya mkoa wa dar esa salaam pamoja na Baraza kuu la Vijana Wilaya ya Kinondoni ,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.
Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza wakati wa kikao na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya mkoa wa dar esa salaam pamoja na Baraza kuu la Vijana Wilaya ya Kinondoni ,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.
 Sehemu ya Wajumbe wa Vyuo na Vyuo Vikuu wakifurahia jambo(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images