Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109974 articles
Browse latest View live

DKT.NDUGULILE AWATUNUKU VYETI WATOA HUDUMA WA KUJITOLEA WA MASHAURI YA WATOTO MKOANI KATAV


NAIBU WAZIRI WA MAJI AWAHAKIKISHIA HUDUMA YA MAJI YA UHAKIKA WAKAZI WA KISHAPU

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameendelea na ziara yake mkoani Shinyanga kwa kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa upande wa Sekta ya Maji katika Wilaya ya Kishapu.
Akihutubia katika mkutano wake kwa wakazi wa Kishapu, Aweso amewahakikishia wananchi hao kuwa Serikali yao itafanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha inamaliza kero ya maji na hakuna kijiji hata kimoja ambacho kitapitwa na huduma ya majisafi.
Naibu Waziri Aweso ametoa rai kwa wananchi wote kutoa ushirikiano wa dhati kwa Serikali na viongozi wa ngazi zote, pamoja na kuunga mkono juhudi inazozifanya kwa lengo la kutimiza upatikanaji wa maji ya uhakika, salama na ya kutosheleza kwa maendeleo ya Tanzania.
Kwa upande wao wananchi waliohudhuria mkutano huo wamemshukuru Naibu Waziri wa Maji kwa kazi kubwa anayoifanya na jinsi anavyojitoa kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma ya maji. Pia, wamemtaka afikishe salamu zao za pongezi kwa Rais Magufuli kwa nia yake thabiti ya kuliletea taifa maendeleo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akimtambulisha Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (katikati) kwa wananchi (hawamo pichani), alipofika wilayani hapo kukagua maendeleo ya huduma ya maji.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa amebeba ndoo ya maji na akina mama wa Kijiji cha Bubiki ikiwa ni ishara ya nia ya Serikali kumuondolea mwanamke adha ya kero ya maji wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga alipokuwa akikagua maendeleo ya huduma ya maji.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Bubiki, wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, alipokuwa akikagua maendeleo ya huduma ya maji.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 12.01.2018

bandari ya Dar es salaam yatangazwa kwenye muungano wa falme za kiarabu

$
0
0
Ujumbe wa chama cha wamiliki wa magari ya mizigo pamoja na chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) upo Dubai katika ziara ya kuitangaza bandari ya Dar es salaam kwenye falme za kiarabu (UAE).
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) Bw. Tony Swai nia ya ziara hiyo ni kuipromote Bandari ya Dar es Salaam pamoja na  kukutana na wateja ambao wana-export na ku-import mizigo yao kuja na kutoka Kampala, Uganda.
Mwenyekiti wa wamiliki wa Magari yabebayo Mizigo kutoka Bandari ya Dar Es Salaam Bi. Angelina Ngalula akisalimiana na Balozi Nimisha Madhavan Balozi wa Uganda katika muungano wa  Falme za Kiarabu (UAE) mjini Dubai jana. Kushoto ni Katibu Mkuu chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) Bw. Tony Swai pamoja na Bw. Ordreck Rwabogo mwakilishi wa Mamlaka ya Bandari Uganda na Jimmy Kutosi Mwakilishi wa Uganda Board of Exporters
 Mwenyekiti wa wamiliki wa Magari yabebayo Mizigo kutoka Bandari ya Dar es ealaam Bi. Angelina Ngalula akiongea  na Balozi Nimisha Madhavan Balozi wa Uganda katika Falme za Kiarabu (UAE) mjini Dubai jana. Kushoto ni Katibu Mkuu chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) Bw. Tony Swai pamoja na Bw. Ordreck Rwabogo mwakilishi wa Mamlaka ya Bandari Uganda na Jimmy Kutosi Mwakilishi wa Uganda Board of Exporters

QUICK ROCKA AMKANA MPENZI WAKE HADHARANI, ALIKIBA NA ABDUKIBA BADO BILABILA..

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AKABIDHI JESHI LA POLISI MKOA WA KILIMANJARO MSAADA WA VIFAA VYA MAWASILIANO YA KOMPYUTA

$
0
0

Afisa Mnadhimu wa jeshi la Polisi daraja la kwanza ,Kamishna Mwandamizi Msaidizi ,Koka Moita akizungumza wakati wa ukaribisho wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro katika uwanja 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi,Hamis Issah akitoa neno la shukrani la utangulizi kwa msaada wa vifaa vya Mawasiliano ya Kompyuta ambazo zitagawiwa katika vituo vya Polisi vya wilaya za mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akimkabidhi Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah vifaa vya Mawasiliano ya Kompyuta kwa ajili ya ofisi za jeshi hilo mkoa wa Kilimanjaro. 

CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAMILIKI WA VIWANDA VYA MAZAO YA MISITU NCHINI KUTATULIWA

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewahakikishia wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu   nchini kuwapa ushirikiano wa kutosha pale inapohitajika kwa kuzishughulikia  changamoto mbalimbali zinazowakabili  ili kwenda sambamba na azma ya serikali ya awamu ya tano  ya Tanzania ya viwanda.
Amesema   Wizara ya Maliasili na Utalii  imedhamiria   kutatua changamoto zinazowakabili  ili kuwawezesha  wamiliki wa viwanda hivyo hasa  wazawa  kutoa  ajira nyingi kwa wananchi.
Amesema  Wizara hiyo haiwezi kufanya kazi pekee yake pasipo  kushirikiana  na sekta binafsi kwani  wao ndo wamiliki wa viwanda vinavyotoa ajira kwa wananchi ambao ndio walinzi wakubwa   misitu nchini.
Akizungumza kwenye kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, kati ya  viongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na  Wawakilishi wa Wamiliki wa Viwanda vya mazao ya misitu nchini,  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga aliwataka wadau hao  wasisite kuwasiliana nae pale wanapokuwa na jambo lolote linalohusu maendeleo ya viwanda vyao
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na  Rais wa Shirikisho la viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus  (kulia) wakati Rais  huyo  alipokuwa  akiwasilisha  taarifa  ya  wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu  wakati wa kikao   kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa  Wizara kukutana na wadau wa Wizara  kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa  ( Picha na Lusungu Helela-MNRT) 
 Rais wa Shirikisho la viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus  akiwasilisha  taarifa  ya  wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga  wakati wa kikao   kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa  Wizara kukutana na wadau wa Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili. 
 Baadhi ya  wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu  wakimsikiliza  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Japhet Hasunga  kwenye  kikao    kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa  Wizara kukutana na wadau wa Wizara  kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza  kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga  kufungua  kikao cha  wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu  kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa  Wizara kukutana na wadau wa Wizara  kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili.  
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu  mara baada   kufungua kikao    kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa  Wizara kukutana na wadau wa Wizara  kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU WAZIRI WA MAJI AWAHAKIKISHIA HUDUMA YA MAJI YA UHAKIKA WAKAZI WA KISHAPU

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameendelea na ziara yake mkoani Shinyanga kwa kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa upande wa Sekta ya Maji katika Wilaya ya Kishapu.  
Akihutubia katika mkutano wake kwa wakazi wa Kishapu, Aweso amewahakikishia wananchi hao kuwa Serikali yao itafanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha inamaliza kero ya maji na hakuna kijiji hata kimoja ambacho kitapitwa na huduma ya majisafi.
Naibu Waziri Aweso ametoa rai kwa wananchi wote kutoa ushirikiano wa dhati kwa Serikali na viongozi wa ngazi zote, pamoja na kuunga mkono juhudi inazozifanya kwa lengo la kutimiza upatikanaji wa maji ya uhakika, salama na ya kutosheleza kwa maendeleo ya Tanzania.
Kwa upande wao wananchi waliohudhuria mkutano huo wamemshukuru Naibu Waziri wa Maji kwa kazi kubwa anayoifanya na jinsi anavyojitoa kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma ya maji. Pia, wamemtaka afikishe salamu zao za pongezi kwa Rais Magufuli kwa nia yake thabiti ya kuliletea taifa maendeleo.

 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akimtambulisha Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (katikati) kwa wananchi (hawamo pichani), alipofika wilayani hapo kukagua maendeleo ya huduma ya maji.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa amebeba ndoo ya maji na akina mama wa Kijiji cha Bubiki ikiwa ni ishara ya nia ya Serikali kumuondolea mwanamke adha ya kero ya maji wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga alipokuwa akikagua maendeleo ya huduma ya maji.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Bubiki, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga alipokuwa akikagua maendeleo ya huduma ya maji.


“ASIYETAKA KWENDA NA KASI YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO ATAKIWA KUACHIA NGAZI” - RC TABORA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imetaka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ambao wamechoshwa na ufanyaji kazi kwa kuzingatia kasi ya Awamu ya Tano ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametakiwa kuandika barua za kuacha kazi ili kuwapisha ambao wataweza kuendana na kasi hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kufuatia baadhi yao kutoroka zoezi la upandaji miti na wengine kushindwa kutekeleza majukumu yao katika zoezi hilo.

Alisema kuwa wapo watu wengi ambao wanahitaji kufanyakazi lakini hawana fursa hiyo, kama mtu anaona kazi zinazotolewa na viongozi ni bughuza kwake ni vema akajiondoa kwa hiari yake kabla hajachukuliwa hatu ikiwemo kuondolewa.

Mwanri alisema kuwa haiwezekani mtumishi wa umma akachagua kazi za kufanya na kutofanya kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha maelekezo ya barua yake ya ajira.

“Mlipopata barua zenu za ajira zilikuwa zinaeleza kuwa zinaorosha kazi ambazo mtafanya na kumalizia kuwa na kazi nyingine ambazo utapangiwa na viongozi wao, na kazi hizo ni pamoja na kupanda miti” alisema Mwanri.

Alisema kuwa haiwezekani Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaagiza kila Mkoa na kila Wilaya na kila kijiji kipande miti kisha wanatokea watumishi wanakaidi kwa kudai kuwa sio sehemu ya majukumu.

Mwanri alisema kuwa kama Mtumishi wa Umma anaona kuwa upandaji miti kwake sio jukumu lake ni vema akaandika barua na akaondoka kwa amani ili aende kwa mwajiri mwingine anayeona anamfaa.

Alisema kuwa suala la kupanda miti ni kila mkazi wa Tabora wakiwemo watumishi wa umma na wananchi.

Mwanri alisema kuwa miti si mali ya Mkuu wa Mkoa , wala Mkuu wa Wilaya bali ni kwa ajili ya faida ya wakazi wote wa Tabora.

Alisema kuwa kukitokea jangwa hakutamuathiri Mkuu wa Mkoa au viongozi pekee hata wale wanaojifanya hawataki kupanda miti.

"NISHATI JIRIDHISHENI NA UBORA WA VIFAA" -MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Nishati ijiridhishe na ubora wa vifaa vinavyotumiwa na wakandarasi katika miradi ya umeme.

Pia iwasimamie wakandarasi hao kwa ukaribu ili kuhakikisha thamani ya miradi inayotekelezwa inalingana na kiasi cha fedhawanacholipwa wakandarasi hao.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Januari 13, 2018) wakati akizungumza katika kikao cha maendeleo ya usambazaji umeme kilichofanyika , Ofisini kwake, Dodoma.
Waziri Mkuu amesema wakati huu ambao Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakiendelea na miradi ya usambazaji umeme, ni vema wizara hiyo ikajiridhisha na ubora wa vifaa.
“Wasimamieni wakandarasi kikamilifu na kama hamjaridhishwa na kazi wanayofanya msisite kuwachukulia hatua, tunataka  wananchi wapate umeme.”
Amesema Rais Dkt. John Magufuli amedhamilia kuona umeme unasambazwa kwenye vijiji vyote nchini kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi.
Hivyo, Waziri Mkuu amesisiza kwamba ni lazima wakandarasi waliopewa jukumu hilo wasimamiwe kikamilifu ili mradi hiyo iweze kuwa na ubora unaostahili.
Kwa upande wake Waziri wa Nishati, Dkt.  Medard Kalemani amesema tayari wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA namba tatu wameshaanza kazi.
Amesema kwa wakandarasi ambao bado hawajaanza wamekubaliana kwamba wataanza wakati wowote na wa mwisho ataanza Machi 2, 2018.
Dkt. Kalemani amesema wizara yake itahakikisha miradi yote ya kusambaza umeme inasimamiwa kikamilifu na inakamilika kwa wakati na katika ubora unaostahili.
Kikao hicho kilihudhuliwa na Waziri wa Nishati Dkt.Kalemani, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa Nishati Bibi Subira Mgalu, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bibi Maimuna Tarishi.
Wengine ni pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Mtendaji Mkuu wa REA, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Kamishna Msaidizi-Bajeti.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAMOSI, JANUARI 13, 2017.

BALOZI MTEULE WA AUSTRALIA AWASILISHA NAKALA ZA HATI ZA UTANBULISHO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Australia nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Mhe. WANG Ke kabla ya kwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho. 
Balozi Mteule wa Australia nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Mhe. WANG Ke akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga leo jijini Dar es Salaam . 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi Mteule wa Australia nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Mhe. WANG Ke mara baada ya zoezi la kwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kukamilika. 
Mazungumzo yanaendelea. 

DKT. MAHIGA AKUTANA NA TIMU YA KUCHUNGUZA MAUAJI YA ASKARI NCHINI DRC

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa katika mazungumzo na Bw. Domitry Titov, Kiongozi wa Timu ya Umoja wa Mataifa inayochunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC wakifuatilia mazungumzo. 
Ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukifuatilia mazungumzo hayo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na Msemaji wa Wizara na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Mindi Kasiga. 
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakinukuu mambo muhimu ya mazungumzo. 
Wajumbe wa pande mbili wakiwa katika mazungumzo. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga mstari wa mbele katikati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WATANZANIA WANAOISHI SAUDI ARABIA WASHEREHEKEA SIKUKUU YA MAPINDUZI

$
0
0
Baadhi ya Watanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mgaza katikati mwenye suti.

Na mwandishi maalum, Riyadh - Saudi Arabia
Wanadiaspora na Watanzania waishio Riyadh nchini Saudi Arabia walisherehekea na kuandhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar siku ya ijumaa tarehe 12 Januari, 2018 katika ukumbi wa Riyadh Palace Hotel.

Sherehe hizo zilindaliwa na jumuiya ya Watanzania 'Tanzania Walfare Society' ambapo waalikwa mbalimbali kutoka miji ya Riyadh, Qasim na maeneo ya karibu walihudhuria. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe.

Hemedi Mgaza. Miongoni mwa walihudhuria sherehe hizo pia walikuwa wanafunzi wa vyuo vikuu, wafanyakazi wapya wa kampuni ya ufugaji ng'ombe wa Maziwa ya Al Marai na wengine kutoka kampuni ya ufugaji kuku ya Al Watania. Kwa picha na habari zaidi angalia kupitia you tube 'Prince eddycool'

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania ya Riyadh, Bw. Fuad Mabruk akitoa hotuba mbele ya Watanzania na wanadiaspora wa mji wa Riyadh huku nyuma yake walioketi kwenye meza kuu kuanzia kulia ni Makamu wa Mwenyekiti wa Jumuiya Dkt. Mahmoud Tuli, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza, Afisa Mkuu wa Utawala wa Ubalozi Bw. Ahmada Sufiani, Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Bw. Saeed Al Jabry na wa kwanza kushoto ni Mweka Hazina wa Jumuiya Bw. Mohamed Saeed.

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, akizungumza na Watanzania.
Baadhi ya Watanzania na wanadiaspora wakisikiliza hotuba zilizokuwa zikitolewa na baadaye walipata fursa ya kuuliza maswali na kutoa maoni.

CUBA YAKUBALI KUSOMESHA MADAKTARI KUTOKA ZANZIBAR

$
0
0
Serikali ya Jamuhuri ya Cuba imetiliana Saini Mkataba na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Usomeshwaji wa Madaktari Wazalendo 15 wa Zanzibar Nchini Cuba katika Fani ya Shahada ya Uzamili ya Udaktari.


Madaktari hao 15 ambao Wanane wa Mwanzo wataanza Mafunzo yao Mwezi ujao wakifuatiwa na wengine 7 wa awamu ya Pili ni Miongoni mwa Wanafunzi waliomaliza masomo yao kupitia mpango wa masomo ulioasisiwa kati ya Serikali ya Cuba na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Saini ya Mkataba huo kwa Serikali ya Cuba imewekwa na Balozi wa Nchi hiyo Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo Hernades na kwa upande wa Zanzibar Saini ikatiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bibi Halima Maulid Salum.

Hafla hiyo fupi ya Kihistoria imeshuhudiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyejumuika pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Wizara husika, Watendaji wa Wizara hizo na kufanyika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo Kushoto na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bibi Halima Maulid Salum wakisaini Mkataba wa Usomeshwaji wa Madaktari Wazalendo 15 wa Zanzibar Nchini Cuba katika Fani ya Shahada ya Uzamili ya Udaktari.Nyuma yao ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na aliye simama mbele yao ni msaidizi wa Balozi wa Cuba Meylin Suarez.
Profesa Lucas Domingo Kushoto na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bibi Halima Maulid Salum wakibadilishana nyaraka za Mikataba mara baada ya kusaini.
Balozi Lucas Domingo akizungumza kabla ya utiaji saini kwenye Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyopo Vuga Mjini Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Waziri wa Afya Zanzibar Mheshimwa Mahmoud Thabit Kombo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar na ule wa Ubalozi wa Cuba Nchini Tanzania. Kulia ya Balozi Seif ni Balozi wa Cuba Prifesa Lucas Domingo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moha’d Aboud Moha’d, Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Afya Mh. Mahmoud Thabit Kombo na Msidizi wa Balozi Cuba Nchini Tanzania Bibi Meylin Suarez.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA 

WAZIRI UMMY ASHUHUDIA COASTAL UNION IKIILAZA KURUGENZI YA MUFINDI MABAO 3-0 DAKIKA 45 ZA KIPINDI CHA KWANZA LEO

$
0
0
 Sehemu ya mashabiki wa soka mkoa wa Tanga wakiojitokeza kufuatilia mchezo huo
 Wachezaji wa timu ya Coastal Union wakishangilia moja ya bao nne ambazo walifunga wakati wa kipindi cha dakika 45 za kwanza kabla ya kuanza kipindi cha piliambapo Coastal Union ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-0
 Mchezaji wa timu ya Coastal Union Raizani Hafidhi kushoto akijaribu kumtoka wa timu ya Kurugenzi FC ya Mufindi Nickraus Mwansumbule wakati wa mchezo wa Ligi Daraja la kwanza uliochezwa leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga ambapo mpaka dakika 45 Coastal Union walikuwa wakiongoza kwa mabao 3-0

ASILIMIA 80 YA WANAOHITAJI DAMU NCHINI NI WANAWAKE.

$
0
0

NA WAMJW-DAR ES SALAAM

ASILIMIA 80 ya wanaohitaji damu nchini ni wanawake kwa sababu mbalimbali ikiwemo uzazi salama wakati wa kujifungua kwa njia ya kawaida na njia ya upasuaji. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu ambayo inafanywa na Chama cha wanawake wa Tasnia ya Filamu nchini leo jijini Dar es salaam. 

“Napenda kusisitiza Damu haiuzwi na kwa mgonjwa yeyote atakayeuziwa damu kwenye kituo chochote cha afya cha Serikali atoe taarifa kwenye idara husika na atachukuliwa hatua” alisisitiza Waziri Ummy Mwalimu. 

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Uongozi wa Hospitali au kituo cha Afya cha Serikali wahakikishe kuwa wanaweka matangazo yanayoelimisha wananchi kuwa damu haiuzwi bali inatolewa bila ya malipo na matangazo yaelekeze wananchi sehemu ya kutoa malalamiko. 
Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyesimama akiongea na wananchi hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chama cha wanawake cha Tasania ya Filamu nchini leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyesimama kushoto akimsalimia mwananchi anayepata huduma katika moja ya banda lililokuwa likitoa huduma za afya katika viwanja vya Biafra wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chama cha wanawake cha Tasania ya Filamu nchini leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa kike wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chama cha wanawake cha Tasania ya Filamu nchini leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wasanii wakiwa wanasubiri huduma ya kuchangia damu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chama cha wanawake cha Tasania ya Filamu nchini leo jijini Dar es salaam.

DC ALI HAPI AZIPONGEZA DAWASA NA DAWASCO KWA USIMAMIZI MZURI UTEKELEZAJI WA UJENZI WA MIRADI YA UBORESHAJI MAJI

$
0
0

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mhe., Ali Hapi, (katikati), akiteremka kutoka juu ya tenki kubwa la kuhifadhia maji linalojengwa huko Mabwepande nje kidogo ya jiji, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya maji wilayani kwake Januari 13, 2018.
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said


MKUU wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Ali Hapi, amewataka wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji wilayani kwake kuongeza kasi ya kukamilisha mradi huo kama ambavyo mkataba unaelekeza.
Mhe. Hapi aliyasema hayo leo Januari 13, 2018 mwishoni mwa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundomnbinu hiyo inayohusisha matenki makubwa manne na vituo vinne vya kusukuma maji (Booster Stations) ikiwa ni pamoja na utandikaji  wa mabomba ya kusafirisha maji.
Mradi huo ambao unatekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam, (DAWASA), ni sehemu ya mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Pwani,  Dar es Salaam, sehemu ya mikoa ya Morogoro na Tanga na ulianza kutekelezwa mwezi Machi 2016.
“Mradi huu ulipaswa kuwa umekamilika Novemba mwaka jana, lakini hatua waliyofikia baadhi ya maeneo wako asilimia 80, mengine asilimia 75 na mengine asilimia 50, ahadi yao ni kwamba ndani ya kipindi kifupi kijacho wataweza kukamilisha mradi huu.” AlisemaMhe. Hapi, akimsikiliza Mkandarasi,   Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, alipotembelea sehemu ya ujenzi wa mtambo wa kusukuma maji huko Salasala jijini Dar es Salaam.
 Mhe. Hapi, akimsikiliza Mkandarasi,   Mhandisi P.G. Rajani(kulia) wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, alipotembelea sehemu ya ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhia maji huko Salasala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Modester Mushi kaimu mkurugenzi wa ufundi DAWASA.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI WA MAJI AWAAGIZA WAKANDARASI WA MAJI KUMALIZA MAPEMA MIRADI HIYO

$
0
0

Na,Joel Maduka,Geita.

Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi ,Isack Kamwelwe amewataka wakandarasi wa miradi mbalimbali ya maji kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ili kuwaondolea wananchi changamoto ya ukosekanaji maji ambayo imeendelea kuwakabili kwa muda mrefu .

Mhandisi Kamwelwe ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani Chato Mkoani Geita iliyokuwa na lengo la kukagua miradi ya maji inayotekelezwa wilayani humo.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Katoro na Buseresere amesema matatizo ya maji katika miji ya Muganza, Buzirayombo na Buseresere yataanza kufanyiwa kazi na pindi tu usanifu wa mradi huu utakapokuwa tayari miradi hiyo itaanza kutekelezwa ili kumaliza kero kubwa ya maji.

Isack Saimon ambaye ni mkazi wa Buseresere amemuomba waziri kuharakisha zaidi mradi huo ambao ametoa ahadi kwa wananchi hao kwani kwasasa wameendelea kupata shida kubwa ya kupata maji na kwamba wamekuwa wakinunua ndoo ya maji kwa shilingi elfu moja hali ambayo inasababisha wasio na uwezo kushindwa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Gabriel Luhumbi amewasisitiza wakandarasi wote wa miradi ya maji kutumia vibarua kwa wananchi wa maeneo husika ambapo miradi hiyo inatekelezwa.Katika Wilaya ya Chato jumla ya wananchi ambao wamekuwa wakuipata maji safi na salama ni ni asilimia 41.
Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi ,Isack Kamwelwe akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Katoro pamoja na Buseresere wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi kwenye Wilaya ya Chato Mkoani Geita. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akimuomba Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi ,Isack Kamwelwe kutatua changamoto ambayo imeendelea kuwepo kwenye baadhi ya maeneo katika Mkoa huo. 
Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi ,Isack Kamwelwe akikagua baadhi ya miradi ya maji kwenye kijiji cha imalabupina wilayani chato. 


WAZIRI UMMY AIKABIDHI TIMU YA COASTAL UNION MILIONI 2 BAADA YA KUIFUNGA KURUGENZI MUFINDI MABAO 3-0 LEO

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa pili kutoka kulia Ummy Mwalimu akimkabidhi kitita cha sh.milioni mbili nahodha wa timu ya Coastal Hussein Shariff maarufu Casilas mara baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga leo kulia ni Mwandishi wa TBC Tanga Bertha Mwambela akishuhudia
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa pili kutoka kulia Ummy Mwalimu akimkabidhi kitita cha sh.milioni mbili nahodha wa timu ya Coastal Hussein Sharifu maarufu Casilasi mara baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa ligi daraja la kwanza dhidi ya Kurugenzi wa Mufindi uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga leo
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa pili kutoka kulia Ummy Mwalimu akicheza ngoma ya kiisifu Coastal Union wakati alipokuwa akihamasisha ushindi wa timu hiyo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani leo ambapo Coastal Union iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kurugenzi wa Mufundi 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa pili kutoka kulia Ummy Mwalimu akicheza ngoma ya kiisifu Coastal Union wakati alipokuwa akihamasisha ushindi wa timu hiyo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani leo ambapo Coastal Union iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kurugenzi wa Mufundi 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa pili kutoka kulia Ummy Mwalimu akicheza ngoma ya kiisifu Coastal Union wakati alipokuwa akihamasisha ushindi wa timu hiyo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani leo ambapo Coastal Union iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kurugenzi wa Mufundi(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

TANGAZO KWA ABIRIA WA TRENI ZA KWENDA BARA.

$
0
0
KAMPUNI YA RELI TANZANIA

TANGAZO KWA ABIRIA WA TRENI ZA KWENDA BARA.

KAMPUNI YA RELI TANZANIA INASIKITIKA KUTANGAZA KWAMBA KUTOKANA NA MVUA KUBWA ZINAZOENDELEA KUNYESHA SEHEMU MBALIMBALI NCHINI  MIUNDOMBINU YA RELI YETU KATI YA KILOSA NA GULWE IMEHARIBIKA. 

KUTOKANA NA UHARIBIFU HUO UMESABABISHA HUDUMA YA USAFIRI WA TRENI KUSITISHWA KWA MUDA KUTOKEA DAR ES SALAAM KWENDA DODOMA ILI KUWEZESHA UKARABATI WA MIUNDOMBINU HIYO KUFANYIKA KWA HARAKA.

KAMPUNI INAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAOJITOKEZA KATIKA KIPINDI AMBACHO HUDUMA HII YA USAFIRI HAITAKUWEPO MPAKA HAPO  ITAKAPO REJESHWA TENA NA WANANCHI WATAFAHAMISHWA  RASMI KUPITIA VYOMBO VYA HABARI.

HATA HIVYO HUDUMA YA USAFIRI WA TRENI YA ABIRIA NA MIZIGO KWA TRENI YA KUTOKA DODOMA KWENDA TABORA - MWANZA - KIGOMA NA MPANDA ITAENDELEA KAMA KAWAIDA.

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO KWA NIABA YA
MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL 
ND MASANJA KADOGOSA
MAKAO MAKUU YA TRL
DAR ES SALAAM
JANUARI 13, 2018


Viewing all 109974 articles
Browse latest View live




Latest Images