Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Kesi ya Wema, Kibatala nje Msando ndani

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Wakili wa msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, Peter Kibatala ameiandikia barua Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuomba kujitoa kumuwakilisha katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili.

Wakati huohuo, mahakama imepokea barua kutoka kwa Wakili Albert Msando kuomba kumuwakilisha msanii huyo, Wema, katika kesi hiyo na kuomba apewe muda wa kupitia jalada hilo kabla ya kuendelea na kesi.

Hatua hiyo imekuja baada ya Desemba 12, mwaka jana katika shauli lililopita mahakama hiyo ilielezwa kuwa wakili wa Wema  hajafika  na kushindwa kuendelea kusikiliza kesi hiyo.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema kuwa amepokea barua hizo Januari 9, mwaka huu na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 8, mwaka huu.

Mbali na Wema, washitakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa  na Matrida  Abbas.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Inadaiwa  kuwa  Februari 4, mwaka jana katika makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio,  washitakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februari Mosi, mwaka jana katika  eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam,  alitumia dawa za kulevya  aina ya bangi.

JKCI YAWAAHIDI WATANZANIA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, 
09/1/2018 Uongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) umewaahidi watanzania kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa kiwango cha kimataifa  kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. 
Ahadi hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi wakati akiongea na wakurugenzi wa Idara na vitengo vinavyojitegemea katika kikao cha kwanza cha Menejimenti  kwa mwaka 2018.
Prof. Janabi ambaye  pia ni Mwenyekiti wa kikao hicho alizitaja ahadi zingine ni pamoja na kuendeea kupunguza kupeleka wagonja nje ya nchi, kupunguza gharama za tiba, kuongeza idadi ya huduma, kuboresha usafi katika Hospitali na kuendelea  kushirikiana na wananchi.

Mwenyekiti huyo alisema kwa mwaka 2018 wamejipanga  kutoa huduma kwa wagonjwa wengi zaidi ukilinganisha na mwaka jana ambapo jumla ya wagonjwa 64,093 walitibiwa katika Taasisi hiyo kati ya hao wagonjwa wa nje walikuwa 60796  na waliolazwa 3297.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea na wakurugenzi wa Idara na vitengo vinavyojitegemea kuhusu mikakati ya utendaji kazi kwa mwaka 2018 moja ya mkakati huo ukiwa ni kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa kiwango cha kimataifa  katika kikao cha kwanza cha Menejimenti  kilichofanyika hivi karibuni. Kulia ni Mwanasheria wa Taasisi hiyo Maulid Kikondo. 
 Wakurugenzi wa Idara na vitengo vinavyojitegemea vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) alielezea kazi zilizofanyika katika Taasisi hiyo kwa mwaka 2017  katika kikao cha kwanza cha Menejimenti  kilichofanyika hivi karibuni. Jumla ya wagonjwa  1025  walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kwa mwaka 2017 na hivyo Taasisi kuokoa  zaidi ya bilioni 29 ambazo Serikali ingezilipa kama wagonjwa hawa wangefanyiwa upasuaji wa moyo nje ya nchi.
 Kikao cha kwanza cha Manejimenti  cha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mwaka  2018 kikiendelea.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akisoma  taarifa za utendaji kazi wa idara yake kwa kipindi cha miezi mitatu katika kikao cha kwanza cha Menejimenti kwa mwaka 2018 kilichofanyika hivi karibuni. Picha na JKCI

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAKAZI WA WILAYA YA BAHI MKOANI DODOMA WATAKIWA KUWARIPOTI WALE WOTE WATAKAO JIHUSISHA NA KUWAOZESHA WANFUNZI

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Dodoma 

Jamii imetakiwa kuacha kabisa tabia ya kuozesha watoto wadogo ambao awajafikia umri wa kuolewa na matokeo yake wawezeshe kupata elimu hili iweze kuwasaidia katika maisha yao ya baadae .

hayo yamesemwa na Msimamizi wa mradi wa kupinga ndoa za Utotoni na huduma ya Msichana Cafe inayoendeshwa na Tasisi ya Msichana Initiative katika Kata kumi za Wilaya ya Bahi, Francis Eugene Shao, alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Vilabu hivyo na wajumbe wa ulinzi wa Mtoto CPT wakati alipokuwa akifanya Tathmini ya mradi huo katika kata ya Kigwe.

"ifike wakati tuone umuhimu wa watoto wetu hasa wakike kuendelea na shule kuliko kuwaozesha ama kuwakimbiza mijini wakafanye kazi za ndani kwani kwa kufanya hivyo kutaweza kusaidia jamii kuwa endelevu kwa kuwa na wasomi wengi amabo wataweza kujikomboa na kukomboa jamii nzima inayowazunguka kutokana na kile walichokipata " amesea Shao.

Shao aliwasisitiza wajumbe hao wa CPT na Msichana Cafe kuwa makini na kuwaripoti wale wote watakao jiusisha na suala la kuwakatiza watoto shule na kuwapeleka mjini kufanya kazi ama kuwaozesha katika umri mdogo kwa lengo la kuweza kujipatia mali .

alitaja kuwa Msichana Initiative kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia itawachukulia hatua wale wote ambao watajihusisha na vitendo vya kuwakatiza watoto masomo kwa namna moja ama nyingine ama kuwaozesha wakiwa katika umri mdogo.
Msimamizi wa mradi wa kupinga ndoa za Utotoni na huduma ya Msichana Cafe inayoendeshwa na Tasisi ya Msichana Initiative katika Kata kumi za Wilaya ya Bahi, Francis Eugene Shao, akizungumza na moja ya wajumbe wa Msichana Cafe ya Kata ya Kigwe wilayani humo juu ya nini cha kufanya katika kuhakikisha wanaripoti kwa usahii habari za ukatili wa kijinsia na kuwafichua wale wote wanaojiusisha na kuozesha watoto katika umri mdogo hili wasendelee na shule.
Meneja Mradi wa wa Msichana Cafe unaoendeshwa na Tasisi isiyo ya Kiserikali ya Msichana Initiative, Sarah Beda akizungumza na wajumbe wa Msichana Cafe na Wajumbe wa CPT Juu ya umuhimu wa kuendelea kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia wanayofanyiwa watoto wa kike katika Kata ya Kigwe ambayo ni moja ya kata kumi zilizo katika Wilaya ya Bahi zinazonufaika na mradi wa Msichana Cafe kutoka Tasisi yake.

Msimamizi wa mradi wa kupinga ndoa za Utotoni na huduma ya Msichana Cafe inayoendeshwa na Tasisi ya Msichana Initiative katika Kata kumi za Wilaya ya Bahi, Francis Eugene Shao, akimuelekeza jambo mjumbe wa Msichana Cafe namna ya kujaza fomu ya Tathmini juu ya mradi unavyokwenda katika kata yao.
Meneja Mradi wa wa Msichana Cafe unaoendeshwa na Tasisi isiyo ya Kiserikali ya Msichana Initiative, Sarah Beda akitoa maelezo ya namna ya kujaz afomu za Tathmini ya mradi kwa wajumbe wa Msichana Cafe.
Wajumbe wa CPT wakijaza fomu za Tathmini juu ya Tasisi ya Msichana Initiative ilivyoweza kuasadia katika kufanya kazi zao za kumlinda mtoto katika kata yao na Wilaya ya Bahi.

Wajumbe wa Msichana Cafe wakisikiliza kwa Makini Maelezo yanayotolewa na Dada Sarah Beda ambaye ani meneja mradi huo (ayupo Pichani) juu ya umuhimu wa wao kuongeza juhudi ya mapambano ya ukatili wa kijinsia kwa watoto.

Msimamizi wa mradi wa kupinga ndoa za Utotoni na huduma ya Msichana Cafe inayoendeshwa na Tasisi ya Msichana Initiative katika Kata kumi za Wilaya ya Bahi, Francis Eugene Shao, akizungumza na wajumbe wa Msichana Cafe umuhimu wa kutioa taharifa za Ukatili wa kijinsia katika kituo cha Polisi kupitia Dawati la Jinsia hili waweze kupata Msaada kwa haraka.

NEC yatangaza uchaguzi mdogo wa madiwani

$
0
0
TUME ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata nyingine sita utafanyika Februari 17 mwaka huu.
Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage alisema jana kuwa uchaguzi huo unafanyika kutokana na sababu mbalibali zikiwemo kifo na baadhi ya madiwani kujiuzulu.
Alizitaja kata ambazo zitafanya uchaguzi huo mdogo kuwa ni Kata ya Buhangaza iliyoko katika Halmashauri ya wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Kata ya Kanyelele iliyoko katika halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza na kata ya Mitunduruni iliyoko katika Manispaa ya Singida.
Kata zingine ambazo zitafanya uchaguzi ni kata ya Kashashi, Gararagua na Donyomuruak ambazo madiwani wake wamejiuzulu hivi karibuni.
“Napenda kutumia nafasi hii kutoa tarifa kwa umma kuwa tume imepanga kuendesha uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hizo februari 17, 2018,”alisema Jaji Kaijage.
Uchaguzi huo unafanyika sambamba na uchaguzi mwingine mdogo wa wabunge ambao utafanyika katika majimbo mawili ya Songea Mjini ambako mbunge alifariki na Longido mbunge wake alivuliwa ubunge na mahakama.
Aliongeza kuwa kutokana na uchaguzi huo mdogo, ratiba ya uchaguzi huo itaanza tarehe 18 hadi 24 Januari ambako tume itatoa fumu za uteuzi, uteuzi wa wagombea utafanyika januari 24 na kampeni zitaanza Januari 25 hadi Februari 16 na uchaguzi wenyewe utafanyika Febuari 17.
Kaijage alitoa mwito kwa vyama vya siasa, wadau wa uchaguzi na wananchi kujitokeza kushiriki katika uchaguzi huo.
“Tume inaviasa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi kuzingatia matakwa ya katiba, sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa, kanuni za uchaguzi na serikiali za mtiaa za mwaka 2015, maadili ya uchaguzi pamoja na maelekezo yaliyotolewa na tume katika kipindi chote cha uchaguzi mdogo,”alisema Jaji Kaijange.

SMZ yaving’arisha vijiji vya Mlilile, Mbuyumaji kwa umeme

$
0
0
Kijakazi Abdalla na Mwashungi Tahir-MAELEZO
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman, amesema mapinduzi ya Zanzibar ndio yaliyowakomboa wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba kutoka kwenye makucha ya ukoloni.

Akizungumza katika ufunguzi wa mradi wa kupeleka umeme katika kijiji cha Mlilile Matemwe Wilaya ya Kaskazini A ikiwa miongoni mwa shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi.

Waziri huyo alisema si vyema kuyapuuza Mapinduzi hayo, akisisitiza wale wanaoyabeza wasipewe nafasi kwani huenda wana ajenda ya siri.

Aidha, aliwataka wananchi wa Unguja na Pemba  kuyaenzi matunda ya Mapinduzi hayo ambayo lengo lake ni kuwainua wananchi wanyonge kwa kuwaletea maendeleo yatakayoinua ustawi wa maisha yao na kuwafanya watembee kifua mbele.

Waziri Haroun alifahamisha kuwa, iko haja kwa wananchi kushirikiana kwa pamoja katika kuijenga nchi, kwa kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haimbagui mtu kwa sura yake au eneo analotoka.

Hata hivyo aliwaomba wananchi wa kijiji cha Mlilile kutumia fursa waliyoipata kwa kutumia huduma ya umeme katika kazi za ujasiriamali pamoja na miradi mingine itakayoweza kuwaingizia kipato.

Akitoa taarifa ya kitaalamu kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira, Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Ali Mbarouk, alisema serikali imelipa jukumu shirika lake kusambaza huduma ya umeme kwa wananchi hadi katikia maeneo yao popote walipo.

Alisema kazi ya usambazaji umeme vijijini itaendelea kufanywa na serikali hatua kwa hatua ili kuwawezesha wananchi wote kunufaika na huduma hiyo.

Alieleza kuwa, mradi huo katika kijiji cha Mlilile umegharimu shilingi 70,128,721.00 fedha zilizotolewa na Serikali kupitia ZECO.

Alisema utekelezaji wa mradi huo, umefanywa  kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein katika Mkoa wa Kaskazini mwezi Septemba 2017.

“Katika ziara hiyo, Dk. Shein alitoa agizo la kufikisha umeme kijijini hapa ndani ya kipindi cha miezi sita, lakini ZECO imekamilisha kazi hiyo kwa miezi mitatu tu,” alieleza Mbarouk.

Mradi mwengine kama huo, pia umezinduliwa katika kijiji cha Mbuyumaji Wilaya ya Kaskazini A na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Khalid Salum Mohammed, ambao umegharimu shilingi 79,000,000, ikiwa miongoni mwa shamrashamra hizo za Mapinduzi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haruon Ali Suleiman akibonyeza kitufe kuashiria matumizi rasmi ya  Umeme katika Kijiji cha Mlilile Wilaya ya Kaskazini A Unguja.Picha na Kijakazi Abdalla  Maelezo Zanzibar.

WATANZANIA WAHAMASISHWA KUCHANGIA DAMU SALAMA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Kutokana na ukosefu wa damu katika benki ya damu salama, Prosper Magali ameamua kuhamasisha watanzania kuchangia damu kwa ajili ya kufikia malengo ya benki ya damu kwa mwaka.

Magali amefikia hatua hiyo baada ya mwaka 2015 kutokea kwa ajali dada yake ambaye alihitaji damu ya haraka zaidi na kupatiwa damu kutoka benki ya damu ila hakuweza kukaa sana na kufatiki ndipo familia ilipoamua kuhamasisha kuchangia damu kila mwaka na 2018 ikiwa ni mara ya pili.

Meneja wa Damu salama kanda ya Mashariki Dkt Avelina Mgesa amesema kuwa kwa mwaka damu lita 450,000 inahitaji ila mwaka 2016 iliweza kupatikana lita takribani 160,000 ambapo hazitoshelezi kwa mahitaji ya kila siku.
Nesi kutoka Mpango wa  Taifa ya Benki wa damu salama Catherine Kiure akimuhudia moja ya wahamasishaji wa uchangiaji damu Prosper Magali wakati wa uchangiaji damu unaoendelea katika Enep la Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakiwa wamejitokeza kuchangia damu salama uliohamashihswa na Prosper Magali kwa ajili ya kuhakikisha bnki ya damu inakuwa na damu ya kutosha.
Mwandishi wa MMG/Kajunason Blog Cuthbert Kajuna akiwa anachangia damu leo Jijini Dar es salaam.
Muhamasishaji Prosper Magali akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea kilichompelekea kuamua kuhamasisha uchangiaji wa damu baada ya kutokea kwa ajali ya dada yake na kupelekea kuhitajika kwa damu haraka sana na kuoma kuna ulazima wa kuhamasisha wananchi waweze kuwa na utamaduni wa kuchangia damu.
Dkt Avelina Mgesa ambaye ji Meneja Damu salama kanda ya Mashariki akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea kufurahishwa na hatua aliyoamua Prosper Magali ya kuamua kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa ajili ya kuhakikisha matarajio ya kufikisha malengo ya lita 450,000 za mahitaji ya damu kwa mwaka.

DKT.KIGWANGALA AZINDUA KAMATI KUANDAA MWEZI WA URTIHI WA TAIFA LA TANZANIA

$
0
0
Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangala amekutana na Kamati ya Kitaifa ya kuratibu shughuli za maandalizi ya Mwezi Maalum wa Maadhimisho ya urithi wa Taifa la Tanzania ili kukwepo na mwezi maalum wa kusherehekea Urithi wa Taifa la Tanzania

 Pamoja na mambo mengine, Kamati hiyo ya kitaifa inategemewa kuandaa utaratibu maalam kwa Watanzania wote ndani na nje ya nchi kushiriki kikamilifu  kupitia midahalo na programu mbalimbali za kielimu; matamasha mbalimbali yakiwemo michezo ya jadi; vyakula vya asili na vazi la Kitaifa.

Dk.Kingwangala amkutana na kamati hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizundua rasmi kamati hiyo ya maandalizi ambapo pia wameamua kwa pamoja jina la maadhimisho hayo ambapo tayari wamekubaliana yatakuwa yanafanyika kila ifikapo Septemba ya kila mwaka.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea kuwa lengo la mwezi wa urithi huo wa taifa la Tanzania ni kutoa nafasi ya kuiweziwezesha jamii kuutumia urithi ambao taifa limejaliwa nao kama zao la utalii na hivyo kuchangia kiuchumi katika jamii na taifa kiujumla.

“Pia maadhmisho hayo yatatumika kuelimisha jamii kuhusu kumbukumbu tulizonazo na namna ya kuzitumia kikamilifu katika kuendeleza Taifa na kuboresha maisha yao. Kuzikumbusha jamii chimbuko la tabia, mila na desturi za watanzania

“Na kuzitambua na kuzienzi mila na desturi za makabila mbalimbali ya nchi hii pamoja na kuhakikisha kuwa matamasha yote ya utamaduni yanafanyika katika mwezi husika (mwezi wa urithi) ambao tumekubaliana iwe Septemba ya kila mwaka,”amesema Dk.Kigwangala.
 Waziri wa Maliasili na Utalii  Dkt.Hamisi Kigwangala akizungumza katika mkutano na  Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania uliofanyika leo kwenye chuo cha Utalii cha Taifa Posta jijini Dar es salaam leo kushoto ni Dkt. Aloyce Nzuki Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasoli na Utalii.


 Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mrisho Gambo  akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania katikati ni Mjumbe wa Kamati hiyo  na ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG.
 Mjumbe wa Kamati hiyo  na ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo Jokate Mwegelo.
 Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa  Simiyu Anthony Mtaka akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania wanaofuatia katika picha ni wajumbe wa kamati hiyo Mkuu wa Mkoa wa Iringa mama Amina Masenza, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Jokate Mwegelo na Imani Kajula
 Wajumbe wa kamati hiyo kutoka kulia ni Wema Sepetu na Dkt. Sebastian Ndege pamoja na wajumbe wengine.

DC SINYAMULE ALITAKA JESHI LA POLISI SAME KUONGEZA UFANISI

$
0
0
Na Mwandishi wa Globu ya Jamii, Same.
Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule amekutana na Maofisa wa jeshi la Polisi na watendaji wa jeshi hilo kuzungumzia  namna ya kuimarisha Ulinzi Na usalama wa Raia katika Mwaka  2018 sambamba  na kufanya  tathmini ya utendaji kazi  kwa mwaka 2017. 

Katika Mkutano huo DC Sinyamule alipata nafasi ya kusikiliza changamoto za jeshi la Polisi wa Wilaya hiyo na kuahidi kuzifanyia kazi katika kipindi kifupi ili waweze kuongeza ufanisi kwenye kazi zao za kila siku.

Aidha alitumia Mkutano huo kama sehemu ya kuwapongeza na  kuwashukuru kwa kazi Nzuri waliyoifanya  mwaka 2017 iliyopelekea kupungua kwa matukio ya uhalifu, kudhibiti ajali za barabarani na kupambana na  dawa za kulevya kama mirungi ambayo hapo awali ilikuwa ikipitishwa kwa wingi kupitia njia za panya katika Wilaya hiyo.

Dc Sinyamule Aliwakumbusha jeshi la Polisi kuhakikisha wananchi wanakaa kwa amani na utulivu. Kama wajibu wa kwanza kwa serikali na kuwataka kuacha kujihusisha na tamaa za upokeaji wa rushwa wa aina yoyote ile kwani kwa kufanya hivyo kutapunguza weledi wa kazi yao. 

Pia alimaliza kwa kutoa ahadi ya kuanzisha tuzo kwa kutoa lakini 5 kila miezi 3, ili askari wanaofanya vizuri wapewe na kuwanunulia tanki la Maji kwa ajili ya kituo hicho cha Polisi cha Wilaya ya Same . 

" Mh. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli anapohimiza maendeleo na watu kufanya kazi, lazima sisi tuhakikishe uwepo wa amani na utulivu ili kazi hizo ziweze kufanyika" Amesema DC Sinyamule. 
 Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule(katikati) akiandika jambo katika kikao chake na jeshi la Polisi la Wilaya hiyo juu ya kudhibiti hali ya ulinzi na Usalama .
 Baadhi ya Maofisa na Watendaji wa jeshi la Polisi waliohudhuria Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Same na Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi na Usalama
 Baadhi ya Maofisa na Watendaji wa jeshi la Polisi waliohudhuria Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Same na Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi na Usalama

RC MAKONDA AWAPIGA STOOP YONO KUWAONDOA WAFANYABIASHARA SOKO LA NDIZI MABIBO (MAHAKAMA YA NDIZI)

SERENGETI LITE YANOGESHA LIGI YA WANAWAKE,TFF,SBL WASAINI MKATABA

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo wamesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuidhamini Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) kupitia Bia ya Serengeti Lite.

Mkataba huo wa wenye thamani ya Shilingi Milioni 450 unaifanya Serengeti Lite kuwa bia ya kwanza kuidhamini Ligi ya Wanawake.Serengeti Breweries ambao pia wanaidhamini timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kupitia Bia yao ya Serengeti Premium Lager kupitia Mkurugenzi Mtendaji Hellen Weesie wanaamini udhamini huo utatoa msukumo kwa timu zote nane zilizofanikiwa kuingia hatua ya nane bora katika msimu huu wa pili wa ligi hiyo.

Weesie amesema siku zote Serengeti wanaamini katika kuendeleza vipaji hasa inapokuja katika michezo ambayo inawaleta pamoja wadau mbalimbali na wanaamini udhamini huo utawavutia mashabiki wa rika mbalimbali.
Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura akizungumzia udhamini huo amesema Serengeti Breweries wanafungua milango kwa wadhamini wengine kupitia udhamini huo wa Bia yao ya Serengeti Lite.

Amesema SBL wameangalia mbali zaidi kuingia kwenye soka la Wanawake kwakuwa hata mkutano mkubwa wa FIFA wa maendeleo ya mpira(FIFA Football Executive Summit) utakaofanyika Tanzania February 22 moja ya ajenda zake ni soka la Wanawake .

“Udhamini huu utakuwa kichocheo kwa soka la Wanawake kukua na tunaamini soka la kina mama litajulikana kama inavyojulikana bia yao na udhamini huu fedha tunayoipata tutaitumia vizuri ” Alisema Wambura.
Kwa upande wa Serikali kupitia Afisa Mkuu wa Michezo Henry Lihaya wamesema Makampuni mengine yaige mfano wa SBL kuingia kwenye michezo ambako ni chanzo cha ajira.

Naye mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wanawake Tanzania(TWFA) Amina Karuma amesema udhamini huo wanaupokea kwa furaha kubwa kwakuwa utasaidia kutimiza lengo kwa mpira wa Wanawake kuchezwa kwa ufanisi.
Ofisa mkuu wa michezo wa wizara ya habari, utamaduni,sanaa na michezo Henry Lihaya (katikati waliosimama) akishuhudia tukio la kudhaminiwa rasmi kwa ligi ya Soka la Wanawake kupitia kampuni ya Serengeti Breweries Ltd.Mkataba huo umesainiwa kati ya SBL (Mkurugenzi Mtendaji wake ni Helene Weesie) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF (,Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura).Ambapo SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne na hamsini (TZS 450) ili kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura na 

Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura na Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie wakipongezana mara baada ya tukio hilo kufanyika mbele ya Waandishi wa habari,jioni ya leo jijini Dar.

ULEGA AMEWAAGIZA WATENDAJI NGAZI YA WILAYA NA MKOA KUSIMAMIA ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO

$
0
0
Serikali imewataka  watendaji   ngazi  ya   wilaya  na  mkoa  kusimamia kwa umakini zoezi  la  upigaji  chapa   mifungo  linaloendea hapa nchini.


Agizo hilo amelitoa Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah   Ulega wakati alipokuwa anazungumza na baadhi ya watendaji  wa mkoa wa Lindi kwenye ziara  yake ya kikazi  ya siku mbili  mkoani humo.


Ulega  alisema mtendaji  yeyote  atakaye bainika kukwamishwa  zoezi hilo  hata vumiliwa  na kueleza kuwa kuna baadhi    wanaonekana kukwamisha zoezi hilo kwa madai ya kukosa  bajeti ya kuendesha zoezi.


Wapo watendaji wanaodharau zowezi hili kwa kweli serikali haita waacha salama  alisema   Ulega.Kwa upande  wake  mkuu wa mkoa wa Lindi  Godfrey Zambi  amesema kuwa kunachangamoto kadha zilizosababisha  baadahi  ya  Halmshauri kushindwa kutekeleza  jukumu  hilo  kwa wakati.

Zambi alisema   Halmshuari  ya wilaya Ruangwa ngo’mbe  268 kati  3000  wamepigwa chapa wakati wilaya   ya  Nachingwea  ngombe  328 tayari wamekamilisha zoezi  hilo.

 Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi ,Abdallah Ulega na akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Lindi mara baada ya kupokea  ripoti ya ya mkoa huo.
 Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi ,Abdallah Ulega akizindua zowezi la upigaji chapa mifugo katika mkoa wa Lindi.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii Lindi.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi ,Abdallah Ulega akizungumza na  viongozi mbalimbli,wafungaji  juu ya  kuhamasisha zowezi la ubikaji chapa mifugo mkoa wa Lindi.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Vijana uliofanyika kwenye ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani, Kikwajuni. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mhe. Maudline Cyrus Castico wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza la Vijana Zanzibar.
 Sehemu ya waliohudhuria uzinduzi wa baraza la vijana Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihamasisha vijana wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Vijana Zanzibar akiwa pamoja  na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mhe. Maudline Cyrus Castico na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Ndugu Khamis Rashid Kheri. 
 Sehemu ya wageni waalikwa mbalimbali

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni tayari wa Uzinduzi wa Baraza la Vijana Zanzibar akiongozana na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mhe. Maudline Cyrus Castico pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Ndugu Khamis Rashid Kheri. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

DKT.SHEIN AZINDUA SOKO LA KINYASINI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Mohamed Shein amefungua  Soko Jipya la Kinyasini lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) ili kutatua changamoto za kukosekana kwa soko la kisasa katika Mkoa wa Kaskazini litakalowasaidia wafanyabiashara wadogo wadogo kuendesha biashara zao.

Mhe. Rais Shein amesema soko hilo litawagusa na kuwafikia  watu wenye kipato cha chini kuinuka kiuchumi kwa kuwanufaisha   Wajasiliamali wadogo wadogo vijijini pamoja na wafanyabiashara; Asasi ndogo ndogo za kifedha zinazotoa huduma vijijini; Vyama vya Msingi vya Ushirika/ Asasi za vijijini zinazojishughulisha na usindikaji wa mazao na masoko ya mazao kwa kushirikisha wanawake katika  makundi yote.
Katika uzinduzi huo uliofanyika Januari 09, 2018 Mkoa wa Kaskazini katika eneo la Kinyasini, Mhe.Rais alisema kujengwa kwa   soko hilo kuna manufaa makubwa kwa wakulima wadogo wakiwemo wafugaji, wavuvi na wafanya kazi za mikono.
“Soko hili litakuwa lenye tija kubwa kwa wananchi wa Zanzibar bila kujali maeneo wanakotoka. Soko hili ni letu sote, lisingeweza kujengwa kila mahali, au hewani lazima lingewekwa mahali, hivyo eneo hili la Kaskazini lilipata fursa hii, hivyo niwaombe liwe la wananchi wote wa Zanzibar.”Alisema Mhe.Rais
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,  Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Soko jipya la Kinyasini lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Januari 09, 2018 eneo la Kaskazin ‘A’ Zanzibar.Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu),  Mhe.Jenista Mhagama na kushoto kwake ni Waziri wa Kilimo,Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohamed.
 Mhandisi wa Kampuni ya ZECCON Bw.Ali Mbarouk Juma akitoa maelezo ya kitaalamu kuhusu ujenzi wa Soko la kinyasini kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein wakati wa uzinduzi wa Soko hilo lililojengwa eneo la Kaskazin ‘A’ Unguja, Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia Wananchi waliohudhuria katika uzinduzi wa Soko la Kinyasini lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akitoa maelezo mafupi ya Soko la Kinyasini wakati wa uzinduzi wa Soko hilo Januari 09, 2018 Lililojengwa katika mkoa wa Kaskazin ‘A’ Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein akimpa mkono wa pongezi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama mara baada ya kuwasilisha maelezo mafupi kuhusu soko la Kinyasini lililozindulia Januari 09, 2018.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Serikali pamoja na Viongozi wa Soko jipya la Kinyasini mara baada ya Uzinduzi Januari 09, 2018. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

JK, VIONGOZI MBALIMBALI WAMFARIJI MZEE KINGUNGE NGOMALE MWIRU

$
0
0
 Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru, Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru ukiwasili nyumbani tayari kwa ibada maalum ya maombolezo, iliyofanyika jioni ya leo. Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru anatarajiwa kuzikwa kesho jioni kwenye makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akimfariji Mzee Kingunge Ngomale Mwiru kwa kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru, alipofika Nyumbani kwale Victoria, jijini Dar es salaam leo. Katikati ni Mzee Ally Mtopa.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe wakati walipokutana kwenye Msiba wa Mama Peras Ngombale Mwiru, Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru, nyumbani kwake Victoria, jijini Dar es salaam leo.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba akimfariji Mzee Kingunge Ngomale Mwiru kwa kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru, alipofika Nyumbani kwale Victoria, jijini Dar es salaam leo. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo akiwa ameambatana na viongozi Wengine wa Chama hicho waliofika nyumbani wa Mzee Kingunge Ngomale Mwiru kumfariji kwa kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru.
Sehemu ya wanafamilia wakiwa ni nwenye majonzi kwa kuondokewa na mpendwa wao.


BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO JANUARI 10, 2018


KUMBUKUMBU

SUMATRA PWANI YAKEMEA KUPANDISHWA NAULI KIHOLELA KWA MABUS YAENDAYO MIKOANI

$
0
0
 Na Mwamvua Mwinyi, Globu ya Jamii - Pwani

OFISA mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) Mkoani Pwani, Omary Ayoub amekemea tabia ya kupandishwa kwa nauli inayofanywa na baaadhi ya mabasi ya abiria yaendayo mikoani. Aidha mamlaka hiyo, imetoa wito kwa abiria kufunga mkanda pasipo kudharau kwa ajili ya usalama wao.

Ayoub aliyasema hayo, wakati wa ukaguzi wa magari ya abiria yaendayo mikoani  katika stand kuu ya Mailmoja, Kibaha, ukaguzi ambao unafanyika kwa ushirikiano kati ya Sumatra na kamati ya usalama barabarani mkoani humo. Alisema changamoto kubwa waliyonayo katika mkoa huo ni baadhi ya abiria waendao mikoani kuzidishiwa nauli tofauti na nauli halali.

Ayoub, alielezea wamepokea taarifa kutoka kwa abiria hao kuwa kuna wahusika wa mabasi ambayo yamekuwa yakipandisha nauli huku kwenye tiketi zao wakiwa wanaandikiwa nauli halali jambo ambalo linawakandamiza abiria. Alisema hawatamvumilia dereva ,kondakta wala mmiliki yoyote anayehusika kukiuka taratibu za usafirishaji. Ayoub alieleza,wanapobaini kuwa madereva au wamiliki wamekiuka taratibu zilizopo kisheria huwachukulia hatua mbalimbali ikiwemo kuwatoza faini ama kuwashtaki mahakamani.
Aliwaomba wananchi na abiria kutoa taarifa juu ya ukiukwaji wa taratibu za usafirishaji kwa wale wanaopandisha nauli na kuandika nauli zisizo sahihi kwenye tiketi zao.

“Tunaomba ushirikiano juu ya suala hili ,tunafuatilia na kusimamia ili kuwasaidia wananchi ambao hawajui haki zako na wapi waende kufikisha kero hizo"

"Msiogope kusema na kuwataja hawa wanaopandisha nauli ,;:Msilipe nauli zaidi ya iliyoandikwa kwenye tiketi " alisema Ayoub.

Akizungumzia umuhimu wa kufunga mkanda wakati wa safari ,Ayoub alisema abiria wanaona hakuna umuhimu wa kufunga mikanda lakini waelewe ni muhimu kwao. Alisema kufunga mikanda ipo kisheria ya mwaka 2007 ya Sumatra inayotakiwa abiria wafunge mikanda kwa usalama wao.

"Inastaajabisha unakuta abiria wanafunga mkanda wakiona askari wa usalama barabarani ama Sumatra wakikagua magari hayo " alisema Ayoub.

Kwa upande wake ,mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoani Pwani ,Josephine Protas aliwataka madereva na wamiliki kufuata sheria na taratibu. Aliwaasa pia madereva kuacha kuendesha kwa mwendo kasi na kutumia vileo wakati wakiendesha. Josephine alisema ,kuendesha pasipo kuwa makini na tahadhari ukiwa barabarani kunasabababisha ajali zembe na kuhatarisha maisha ya watu wasio na hatia. Aliyataka magari madogo ya abiria yanayofanya safari zake Mbezi-Mlandizi-Chalinze kutoa tiketi kwa abiria ili kuondoa usumbufu kwa abiria 

WANANCHI WASHAURIWA KUTOISUBIRI SERIKALI KUWAFANYIA KILA KITU

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akitengeneza tofali kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Kata ya Kakese iliyopo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi katika ziara yake ya siku mbili kuamsha ari ya wananchi katika kujitolea kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amewashauri wananchi wa Kata ya Kakese Wilayani Mpanda Mkoani Katavi kutoisubiri Serikali kuwafanyia kila kitu wakati wanana uwezo wa kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili katika maeneo yao. Ameyasema hayo wakati wa ziara yake mkoani Katavi yenye lengo la kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Ameongeza kuwa lengo la ziara hiyo ni kufuatilia namna ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii ambayo inasisitiza ushirikishwaji wa jamii katika maamuzi, kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli au miradi ya maendeleo ikiwemo upanuzi na uendelezaji wa miundo mbinu mijini na vijijini kama Shule, Barabara, Zahanati na Maghala kwa kutumia rasilimali zilizopo.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Lilian Matinga akitengeneza tofali kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Kata ya Kakese iliyopo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi katika ziara ya siku mbili ya Naibu Wazriri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile kuamsha ari ya wananchi katika kujitolea kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Wizara yake imeamua kufuatilia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi za Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kushiriki kwa vitendo kwa kufanya kazi na jamii kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu  ya Elimu, Afya, Kilimo, Barabara na Viwanda.

“Hakikisheni mnafanya kazi kwa bidii inayotoa matokeo yenye mashiko na tija katika jamii. Tumieni stadi na mbinu shirikishi kuwezesha maendeleo jumuishi ambapo makundi yote katika jamii yanashiriki katika maendeleo yao alisistiza Mhe. Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile ameeleza  kuwa pamoja na msisitizo uliotolewa na Sera kuwa wananchi ni kitovu cha maendeleo, taarifa kutoka kwa wadau mbali mbali wanaofanya kazi na jamii zinaonesha kuwa ari ya wananchi kushiriki katika kazi za maendeleo imeshuka kwa kiasi kikubwa ila kwa sasa wamejipanga kuirudisha ari ya wananchi kujitolea.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kulia) akikabidhi moja ya mifuko 42 ya saruji kwa uongozi wa Kata ya Kakese Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi katika kuunga mkono juhudi za wananchi katika kujiletea maendeleo yao.

“Hali hii ya wananchi kutojitolea na kushiriki katika shughuli za maendeleo inapelekea kutokamilika na kukosekana kwa uendelevu wa miradi mingi ya maendeleo ambayo inahitaji nguvu ya wananchi alisema Mhe. Dkt Ndugulile

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Lilian Matinga amempongeza  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile kwa kuamua kushirikiana na wananchi na viongozi kufanya kazi katika kuamsha ari ya wananchi kujitolea katika shughuli za maendeleo katika kujenga shule ya Sekondari ambayo itasaidia watoto kupata elimu jirani na makazi yao.

Mmoja ya wananchi wa Kata ya Kakese Bw. Fedrick Kanangu ameishukuru Serikali kwa kuunga mkono jitihada zao na kuwashauri wananchi wenzake kuendelea kujitolea katika kufanya kazi za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akizungumza na wananchi wa Kata ya Kakese Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi na kuwashauri kutoisubiri Serikali kuwafanyia kila kitu hata yale ambayo wanaweza kuyafanya kwa nguvu zao katika ziara yake ya kuamsha ari ya wananchi katika kujitolea kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

“Ushiriki wa jamii katika kutekeleza kazi na miradi ya maendeleo huharakisha kufikiwa kwa malengo mbalimbali ngazi ya jamii na taifa kwa ujumla” alisema Bw. Kanangu.

Wote kwa pamoja tuendelee kushirikiana na kusukuma gurudumu la maendeleo mbele kwa kuweka uzalendo mbele na kuchapa kazi kwa bidii na kwa kuwaunga mkono kwa kazi za maendeleo wanazofanya wananchi wa Kata ya Kakese Naibu Waziriwa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alichangia  mifuko 42 ya saruji.
Baaadhi ya wananchi wa Kata ya kaseke wakimsikiliza Naibu Wazriri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile mara baada ya kushirikiana naye kufyatua tofali kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kakese iliyopo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi. Picha Zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.

Herry James asifu ushirikiano wa wananchi Mkoani Arusha

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Herry James akisalimiana na baadhi ya viongozi wa UVCCM Mkoa wa Arusha mara baada ya kuwasili Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha Na Mathias Canal

Na Mathias Canal, Arusha

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Herry James amesifu ushirikiano wa wananchi Mkoani Arusha kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli katika kusimamia rasilimali za Taifa.

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM ameeleza hayo Mara baada ya kuwasilia Mkoani Arusha leo 10 Januari 2018 katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine atashiriki kampeni za kumnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Longido katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Akizungumza na Vijana wa Chama Cha Mapinduzi waliozuru kumlaki katika Mtaa wa Tengeru, Wilaya ya Meru, Herry aliwasisitiza Vijana hao kuendeleza mahusiano mazuri kwa Chama na serikali ili kuwa na jamii yenye nidhamu, weledi na mtazamo chanya katika utendaji.

Alisema pia mahusiano mazuri ndio msingi wa ushindi wa ngazi mbalimbali ikiwemo uchaguzi mdogo wa udiwani uliomalizika hivi karibuni na CCM kuibuka kidedea kwa zaidi ya asilimia 97%.

Aidha, Herry amewafikishia vijana hao salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa kuwa amemuelekeza kushiriki kampeni za Uchaguzi mdogo ambapo pamoja na mambo mengine Rais Magufuli anatarajia matokeo ya ushindi wa kishindo katika chaguzi zote za marudio nchini.

Aliongeza kuwa katika kipindi kirefu Mkoa wa Arusha umekuwa na viongozi wasiokuwa na maamuzi lakini kupitia serikali ya awamu ya Tano viongozi wengi wamekuwa na maamuzi muhimu na mazuri kwa wakati sahihi huku akisifu uwajibikaji wa Kamishna wa CCM Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Mhe Mrisho Gambo.

Sambamba na hayo pia amewasihi Vijana wote nchini kusimamia kile wanachokiamini kwa maslahi ya wengi na kuwa na maamuzi yakinifu kwa wakati sahihi. 

JIJI LA DAR LASHINDA TUZO YA KWANZA BARANI AFRIKA YA HUDUMA BORA YA USAFIRI ENDELEVU MWAKA 2018 JIJINI WASHINGTON, D.C., MAREKANI

$
0
0
Balozi wa Tanzania katika nchi za Marekani na Mexico, Mhe. Wilson M. Masilingi, alipokea Tuzo ya Huduma Bora ya Usafiri Endelevu Mwaka 2018 (Sustainable Transport Award) kwa Jiji la Dar es Salaam kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 09 Januari, 2018. Balozi Wilson M. Masilingi aliambatana na Naibu Katibu Mkuu (E) kutoka OR - TAMISEMI Bw. Tixon Nzunda, Mwenyekiti wa Bodi ya DART, Profesa David Mfinanga pamoja na Mtendaji Mkuu wa DART Mhandisi Ronald Lwakatare. 

Sehemu ya Hotuba ya Mhe. Balozi Masilingi inasema:


"On behalf of my Government and people of the United Republic of Tanzania, I would like to take this opportunity to express my sincere gratitude to the Respected Jury members for selecting Dar es Salaam City and honouring us with this prestigious “Sustainable Transport” Award. I also thank the Institute of Transportation and Development Policy (ITDP) for inviting us to this historical event, Sustainable Transport Award Ceremony 2018, in Washington D.C. in this great Country the United States of America.

I bring to this "Sustainable Transport Award 2018" Ceremony warm greetings and best wishes for this New Year from His Excellency Dr. John Pombe Joseph Magufuli, the President of the United Republic of Tanzania. The Government and people of the United Republic of Tanzania are greatly honoured to receive this prestigious Sustainable Transport Award 2018 given to the City of Dar es Salaam, Tanzania. We humbly and happily accept the Award as the first City in Africa to receive such an honour. Thanks to the Visionary and decisive leadership of our past President’s and the current President of our country H.E. Dr. John Pombe Joseph Magufuli. The Exemplary take off of our six phased Dar es Salaam Bus Rapid Transit Project (DART System) is due to their good leadership. We also sincerely thank our partners the World Bank and the Institute for Transportation and Development Policy (ITDP) for the cooperation and support in raising the required finances and technical guidance to achieve sustainable transportation."
Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi akitoa hotuba ya shukurani, kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu (E) kutoka OR - TAMISEMI Bw. Tixon Nzunda
Mhe. Balozi Wilson Masilingi akishika tuzo pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya DART, Profesa David Mfinanga na Mtendaji Mkuu wa DART Mhandisi Ronald Lwakatare.
Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiwa na viongozi wa ITDP (The Institute for Transportation and Development Policy) na washindi wa Tuzo wa miaka iliyopita.
Mhe. Balozi Wilson Masilingi, Bw. Tixon Nzunda, Mhandisi Ronald Lwakatare, Profesa David Mfinanga pamoja na Watanzania walioshiriki waishio Marekani katika hafla ya kupokea tuzo.
Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiwa katika katika picha ya pamoja na Wasimamizi wa Taasisi ya kutoa Tuzo "Institute for Transport and Development Policy (ITDP)".
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images