Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109975 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 10, 2018


Waziri Profesa Mbarawa avamia bandarini Dar es salaam Usiku, abaini madudu...

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akifanya mahojiano na mmoja wa maofisa wa Bandari ya Dar es Salaam baada ya kukagua kama huduma zinatolewa saa 24 kama Serikali ilivyoelekeza.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza kwa simu na mmoja wa maofisa wa Bandari ya Dar es Salaam baada ya kutembelea ofisini kwake na kumkuta hayupo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiondoka katika eneo linalotolewa huduma za kibenki bandarini jana usiku mara baada ya kukagua kama huduma zinatolewa saa 24 kama Serikali ilivyoelekeza.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), Giliadi Ngewe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), wakishuhudia moja ya wakala wa meli akiwa amefunga ofisi kinyume cha maelekezo ya Serikali ya kufanya kazi saa 24.

RC RUVUMA AWAONYA WAFANYABIASHARA WA MBOLEA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma B CHRISTINA MNDEME amefanya ziara ya kushitukiza katika maghala ya SONAMCU ya kuhifadhia mbolea huku akikuta uchache wa mbolea katika maghala hayo habari kamili hii hapa video yake.

Wanafunzi 26 wa IFM wala nondozzzz ya uzamili ya Teknolojia ya Habari na Uongozi

$
0
0
 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WANAFUNZI 26 wamehitimu shahada ya uzamili ya Teknolojia ya habari  na Uongozi  wa katika chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Profesa Thadeo Satta amesema shahada ya uzamili  ya Teknolojia ya habari  na Uongozi inatolewa kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Avinashillingam  cha  nchini India.
Amesema kuwa  tangu shahada hiyo imeanza kutolewa kumekuwa na mwitikio mkubwa kutokana na mabadiliko ya dunia ya teknolojia ya habarai.
Satta amesema kuwa kuanzishwa kwa shahada hiyo nchini kwa ushirikiano chuo kikuu cha nchini o India kumewapunguzia gharama wahitaji wa shahada hiyo ambapo walitakiwa wakasome nchini India lakini wanapata kupitia Chuo cha IFM.
Aidha amesema kuwa kuwa wanashirikiana na vyuo mbalimbali katika kutoa kozi nchini kupitia chuo cha IFM.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Avinashillingam  cha  nchini India.Dk. Premavathy Vijayan akizungumza katika mahafali ya 11 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jana  jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Profesa Thadeo Satta akizungumza katika mahafali ya 11 ya shahada ya uzamili  ya Teknolojia ya Habari na Uongozi  jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi 26 wakitunukiwa shahada ya uzamili  ya Teknolojia ya Habari na Uongozi katika mahafali ya 11 Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM),  jijini Dar es Salaam.
 Mhitimu wa shahada ya uzamili  ya Teknolojia ya Habari na Uongozi,     Edwin Owawa akitunukiwa cheti  katika mahafali ya 11 Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Avinashillingam  cha  nchini India.Dk. Premavathy Vijayan akiwa katika picha ya pamoja ya Watendaji wa IFM na Wahitimu 26 katika mahafali ya 11 ya Chuo cha IFM  jijini Dar es Salaam.

OHOOOOO: MATUNDA SAFI NA SALAMA YAPATATIKANA HAPA....

Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba asimamia zoezi la kusafirisha mbolea

$
0
0
 Gari iliyopakiwa mbolea ikiondoka kwenye kwenye ghala la kuhifadhia mbolea la Kampuni ya Mohammed Enterprises lililopo eneo la Mbagala  Jijini Dar es Salaam jana kuelekea mikoa ya Mbeya na Rukwa
ambapo tani 600 ilitegemewa kusafirishwa jana.
 Mbolea tani elfu tatu (3,0000 ikiwa kwenye ghala la kuhifadhia mbolea la Kampuni ya Mohammed Enterprises lililopo eneo la Mbagala ikisubiri kusafirishwa  Jijini Dar es Salaam jana. Tani 600 ilitegemewa kusafirishwa jana.
Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba akifanya mawasiliano ya moja kwa moja na mawakala wa mbolea katika mikoa ya Rukwa na Mbeya kupata uhakika wa kuwasili kwa shehena ya mbolea alipokuwa kwenye ghala la kuhifadhia mbolea la Kampuni ya Mohammed Enterprises lililopo eneo la Mbagala, Jijini Dar es Salaam jana.

UTARATIBU WA KUSAJILI CHAMA CHA SIASA HUU HAPA.

$
0
0

Na  Bashir  Yakub.

Haki ya  kusajili  na  kuwa  na  chama  cha  siasa  ipo  kwa kila  mtanzania.  Hata  wewe  unaweza  kuwa  na  chama  cha  siasa  ikiwa  utataka  kufanya  hivyo.  Wako  wanaofikiri  kusajili  chama  siasa  ni  jambo  kubwa  mno. Laa  hasha  ni  jambo  la  kawaida    na  utaratibu  wa  usajili  si  mgumu  kama  wengi  wanavyodhani.

Tutaona  hapa  utaratibu  wa  kusajili  chama  cha  siasa.  Sheria  namba  5 ya  1992  Sheria ya  Vyama  vya  Siasa  na  kanuni  zake  za  mwaka  1992 ndizo  zinazoeleza  utaratibu utakaoelezwa  hapa  chini.

USAJILI  HUPITIA  HATUA  KUU  MBILI.

Kwa  mujibu  wa  kifungu  cha8( 1 ) cha  sheria  ya  vyama  vya  siasa  usajili  hupitia  katika  hatua  kuu  mbili.

Kwanza  usajili  wa  muda  na  pili  usajili  wa  kudumu.  Kwahiyo  ili  usajili  chama  cha  siasa  yakupasa  kupitia  hatua  hizi  mbili.

1.      USAJILI  WA  MUDA(PROVISIONAL REGISTRATION).

Usajili  wa  muda  umeelezwa  katika kifungu  cha  9  cha  sheria  hiyo.  Usajili  wa  muda  maana  yake  chama  kitasajiliwa   na  kitaruhusiwa  kufanya  baadhi  ya  kazi  ila  usajili  huo  utakuwa  haujakamilika  mpaka  baada  ya  kutimiza  masharti, sifa  na  viwango  vilivyowekwa  na  sheria   ndani  ya  muda  maalum  ulioainishwa na sheria.  Usajili wa muda ndio  unaoanza  na  utaratibu  wake  ni huu ;

( a ) Andaa  katiba  ya  chama na  hakikisha  unakuwa  nayo. Mnajua  kila  chama  cha  siasa  huwa  na  katiba  yake, basi  hiyo  ndiyo  inayotakiwa hapa.

( b ) Hakikisha  mko  waanzilishi  wasiopungua  wawili.

( c ) Andaa  kanuni  za  chama. Kanuni  na  katiba  ni  tofauti. Kanuni  ndizo  zinazotafsiri  katiba kwa hiyo  kanuni  hutokana  na  katiba.



COASTAL UNION WAKATAA UFADHILI WA WAZIRI JANUARY MAKAMBA

$
0
0
Uongozi wa timu ya Coastal Union ya Tanga(al maarufu Wagosi wa Kaya) umekataa ufadhili waliotafutiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira na Muungano, January Makamba kwa madai kwamba kampuni aliyoitafuta kwa ajili ya ufadhili inajishughulisha na masuala ya Kamari.


Waziri Makamba alitafuta Ufadhili kutoka kampuni ya BIKO inayojihusisha na michezo ya kubahatisha ambayo ilikubali kuifadhili timu ya Coastal kwa kuingia nayo mkataba ambao utawezesha kulipa mishahara ya wachezaji pamoja na mahitaji mengine kwa kipindi cha mwaka mmoja. 

 Makamba alisema lengo la yeye kukubali kuwatafutia ufadhili ilikuwa ni kutaka kuinua kiwango cha soka pamoja na kuipa nguvu ili iweze kupanda daraja timu hiyo iliyoporomoka kisoka. 

 Akizungumza kwa simu na mwandishi wa habari hii, Waziri Makamba alikiri kuitafutia ufadhili timu hiyo ambao ungewawezesha kulipwa mishahara na mahitaji mengine kwa kipindi cha mwaka mzima. imefahamika kuwa uongozi wa Coastal Union umekataa ufadhili huo licha ya kufanyika mazungumzo ya awali kwa ajili ya kuingia mkataba. 
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa BIKO, Charles Mgeta alisema kuwa taratibu za ufadhili zilikuwa zimekamilika na walipeleka fedha za awali zipatazo sh.15m/= kwa klabu hiyo kati ya fedha sh.50m/= zilizokubaliwa kwa matumizi ya mwaka mzima. 
 Mgeta alisema kwamba licha ya kupeleka fedha za awali pia walipeleka jezi 30 kwa ajili ya timu hiyo na kuahidi kutengeneza jezi 30 nyingine. 
 Ofisa Mkuu huyo alisema baada ya kutokea sintofahamu juu ya ufadhili huo kutoka CoastalUnion, kampuni ya BIKO imewataka viongozi wa klabu hiyo kurudisha fedha walizopokea kutoka kwao. Hata hivyo, uongozi wa Coastal Union umethibitisha kupokea fedha zipatazo shs.15m= kutoka BIKO na kwamba wanachofahamu ni kwamba wanaendelea na mazungumzo na kampuni hiyo ili waweze kupata suluhu, ingawa hakufafanua zaidi. 
 Mwenyekiti wa Coastal Union, Stephen Mgutto alisema kwamba klabu yake ilipendekeza ipewe ufadhili wa shs. 50m/= badala ya shs. 30m/= ambazo walitajiwa. Alieleza kuwa kushindwa kufikiwa muafaka wa shs.50m/= ulifanya uongozi wa klabu hiyo kutotaka kuendelea na mkataba na kampuni hiyo. 
 Katibu wa Kamati Maalum ya mashindano na Usajili, Salim Bawazir alisema kuwa Waziri Makamba amekuwa mfadhili wa timu hiyo kwa muda mrefu na alitaja baadhi ya misaada iliyotolewa naWaziri Makamba kwa Coastal Union kuwa ni pamoja na kugharamia kambi ya timu hiyo wakati wakijinoa kwa muda wa majuma mawili kwa kutoa shs.2m/=. “Mheshimiwa, ametugharamia kuweka kambi ambayo ilihusisha chakula na vitu vingine, ambapo Mohamed Enterprises naye aliisaidia timu kwa kutoa vyakula vyenye thamani ya shs.2m/=”. Alisema Bawazir. 
 Makamba alisema kuwa ametumia karibu shs.6m/= kuisaidia timu hiyo kwa matumizi yao kuanzia mwaka jana. “Nimewalipia mara kadhaa mahitaji yao yanayofikia shs.6m/=”, alisema Waziri huyo. Alisema amesikia tetesi za mtafaruku baina ya viongozi kuhusu upokeaji wa msaada huo na kueleza kuwa amesikitika sana. 
"Iwapo msaada huo hauhitajiki, tutawapa wengine wanaohitaji”, alisema Makamba na kuongeza amekuwa akisaidia michezo kwa muda mrefu na mwaka jana alipewa ngao ya shukurani na timu ya Majimaji ya Songea kwa sababu aliwasaidia na wakafanikiwa. 
 "Viongozi hao wanajua kabisa kwamba mara kadhaa nimelipia mahitaji mbalimbali ya klabu ingawa kipato changu ni kidogo. Nimeenda kambini na kufanya mkutano na wachezaji kuhusu hali zao. Nikihesabu tangu mwaka jana ni fedha nyingi," alisema. 
Alieleza kuwa kuna kipindi timu ilipitia Iringa na akalazimika kuwaomba marafiki zake wa Iringa wawapokee, kuweka mafuta na kuwapa chakula na malazi. Alisema anatumaini kuwa mzozo huo utamalizwa kwa ustawi wa soka la Tanga.

NAIBU WAZIRI AWESO AZIAGIZA HALMASHAURI KUTOWAPA KAZI WAKANDARASI WASIOJALI MASLAHI YA TAIFA

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso, ameziagiza halmashauri zote nchini kutowapa kazi za utekelezaji wa miradi ya maji wakandarasi wasiojali maslahi ya taifa na kusisitiza kuwa Serikali haitavumilia wakandarasi wazembe, ambao wanapewa kazi lakini wanashindwa kuzimaliza kwa muda uliopangwa.

Aweso alitoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Shinyanga na wakazi wa Kijiji cha Mendo, mkoani Shinyanga na  kusikitishwa na mwenendo wa utekelezaji usioridhisha wa mradi wa maji kijijini hapo.

‘‘Nikuombe sana Mkurugenzi wa Halmashauri, hakikisha mnawapa kazi wakandarasi watakaohaikisha miradi inakamilika kulingana na mikataba yao, miradi mingi ya Serikali imekua haina manufaa kwa wananchi na kukosa tija kwa taifa kwa sababu tunawapa wakandarasi wazembe, wanaokosa uzalendo na kutokujali maslahi ya taifa.’’

‘‘Mfano mzuri ni mradi huu wa Mendo ulioanza kutekelezwa tangu Aprili 2014 na ulitakiwa kukamilika Disemba 2017, lakini bado haujakamilika wakati Serikali imeshaingia gharama ya zaidi ya Sh. mil 300. Jambo ambalo si sahihi, hivyo naagiza ifikapo mwisho wa mwezi huu uwe umeshakamilika na wananchi wapatao 2199 waanze kupata maji,’’ aliagiza Naibu Waziri Aweso.

Naibu Waziri Aweso ameanza ziara ya siku 5 mkoani Sinyanga inayolenga kukagua maendeleo ya miradi ya maji na kuweka msukumo katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa nia ya kuhakikisha inakamilika kwa wakati na wananchi wa  mkoa huo wanapata huduma ya maji  ya uhakika kulingana na Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akitembelea Kijiji cha Mendo, mkoani Shinyanga 
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiongea na wananchi wa Kijiji cha Mendo, mkoani Shinyanga 

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akikagua mtambo wa maji Kijiji cha Mendo, mkoani Shinyanga.

TANZIA: MPIGANAJI WA Radio Free Africa Zuberi Msabaha katutoka

$
0
0
Aliyekuwa mtangazaji wa muda mrefu wa Radio Free Africa, Zuberi Msabaha amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatano Januari 10, 2018,  huko jijini Mwanza.

Zuberi Msabaha alikuwa ameugua kwa muda mrefu huku akipatiwa matibabu yake sehemu tofauti tofauti hapa nchini. Msiba wake upo Mabatini jijini Mwanza na mazishi yatafanyika Jumatano ya leo. 
Marehemu Zuberi Msabaha alijijengea umaarufu mkubwa kupitia kipindi chake cha Bolingo Time kinachorushwa hewani na kituo cha Radio cha RFA.
Zuberi Msabaha alikuwa mchambuzi mzuri sana wa muziki wa Dansi hasa muziki wa Kongo ambao mara nyingi unaimbwa kwa lugha ya Kilingala, Kikongo, kikasai, na Kifaransa.

Mungu ailaze Mahali Pema Peponi Roho 
ya mpendwa wetu Papa Zuberi Msabaha.
#darmpya

WANANCHI WA LIWALE NA NACHINGWEA WALILIA BARABARA

$
0
0
Wananchi wa wilaya ya Liwale na Nachingwea mkoani Lindi wameiomba Serikali kuhakikisha inaanza ujenzi wa barabara ya Liwale - Nachingwea (Km 129) kwa kiwango cha lami ili kutatua changamoto za usafirishaji wa abiria na mazao katika wilaya hizo. 

Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, Mkuu wa wilaya ya Liwale Bi. Sarah Chiwamba amesema kuwa wanachi wake wanaamini kuwa Liwale itafunguka kibiashara na kiuchumi endapo itakuwa imeimarishwa katika mtandao wa barabara ambazo zitaiunganisha wilaya hiyo na wilaya jirani pamoja na nchi kwa ujumla.

"Naamini barabara hizi zikikamilika wilaya hii na mkoa wetu utaendelea kiuchumi kwani suala la miundombinu ya barabara imekuwa ni kilio cha muda mrefu katika wilaya yetu", amesema Mkuu wa Wilaya.
Aidha, Bi. Sarah amefafanua kuwa wananchi wengi katika wilaya hiyo ni wakulima, hivyo wamekuwa wakitumia miundombinu ya barabara kusafirisha mazao ya korosho na ufuta yanayozalishwa kwa wingi kuelekea maeneo mbalimbali ya nchi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri huyo anayeshughulikia masuala ya Ujenzi, amewataka wataalamu wote wa masuala ya ujenzi nchini kupitia Sera ya Ujenzi ya mwaka 2003 ambayo itawasaidia kuwapa mwongozo katika utekelezaji wa majukumu yao katika kutoa huduma bora kwa jamii.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akionesha Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa watendaji wa Wilaya ya Liwale (hawapo pichani), ambapo utekelezaji wa miradi yote ya barabara hapa nchini umeanishwa humo wakati alipowatembelea kuona hali ya mtandao wa barabara katika wilaya hiyo, mkoani Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Sara Chiwamba.
 Mkuu wa Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, Bi. Sara Chiwamba akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, kuhusu hali ya mtandao wa barabara wilayani humo katika ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo, mkoani humo kukagua miundombinu hiyo.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Bi. Rukia Muwango kuhusu nia ya Serikali ya kuhakikisha inafungua wilaya hiyo na wilaya jirani ya Liwale kwa kuwajengea barabara kwa kiwango cha lami, mkoani Lindi.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akisisitiza jambo kwa uongozi wa Wilaya ya Ruangwa wakati alipofanya kikao nao wilayani hapo. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Joseph Mkirikiti.
 Muonekano wa sehemu ya barabara ya Ruangwa- Namichiga KM 22 ambapo Wakala wa Barabara mkoa wa Lindi wamepewa jukumu la kuhakikisha inapitika wakati wote.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi Mzawa kutoka Kampuni ya Southern Link, Mhandisi Felix Aminieli, anayejenga Daraja la Nandanga lenye urefu wa mita 30 ambalo lipo katika mto wa Lukuledi, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw.Joseph Mkirikiti.
 Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Lindi, Mhandisi Isaack Mwanawima akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua za ujenzi wa daraja la Nandanga lenye urefu wa mita 30 ambalo lipo katika mto wa Lukuledi, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.

Muonekano wa daraja la Nandanga ambalo lipo katika barabara ya Wilaya ya Luchelegwa-Ndanda inayounganisha wilaya za Ruangwa mkoa wa Lindi na Masasi mkoani Mtwara. Daraja hilo linatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS SHEIN AMETEMBELEA STUDIO ZA ZBC RADIO RAHALEO MJINI UNGUJA.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Ali Mohammed Shein akisalimiana na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Habari la Zanzibar ZBC, Bi Nasra Mohammed mara baada ya kuwasili katika Jumba la Studio za ZBC radio Rahaleo mjini Unguja kwa ajili ya kuangalia Mitambo na Vifaa mbalimbali vya kurushia matangazo.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Ali Mohammed Shein wapili kulia akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Habari la ZBC, Aiman Duwe mara baada ya kuingia katika Jumba la Studio za ZBC radio Rahaleo mjini Unguja kwa ajili ya kuangalia Mitambo na Vifaa mbalimbali vya kurushia matangazo. Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohammed Shein kushoto akipata maelezo kutoka kwa Msaidizi Fundi Mkuu Radio Lazaro Joseph wakati alipotembelea moja katika Studio za ZBC radio Rahaleo mjini Unguja kwa ajili ya kuangalia Mitambo na Vifaa mbalimbali vya kurushia matangazo.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohammed Shein wapili kushoto akisikiliza  maelezo kutoka kwa  Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma wakati alipotembelea moja katika Studio za ZBC radio Rahaleo mjini Unguja kwa ajili ya kuangalia Mitambo na Vifaa mbalimbali vya kurushia matangazo.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohammed Shein akitembelea sehemu mbalimbali za Jumba la Studio za ZBC radio Rahaleo mjini Unguja kwa ajili ya kuangalia Mitambo na Vifaa mbalimbali vya kurushia matangazo.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohammed Shein wapili kushoto akitembelea sehemu mbalimbali za Jumba la Studio za ZBC radio Rahaleo mjini Unguja kwa ajili ya kuangalia Mitambo na Vifaa mbalimbali vya kurushia matangazo.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

WAZIRI MWAKYEMBE AMLILIA MTANGAZAJI WA RADIO FREE AFRICA ALIEFARIKI LEO JIJINI MWANZA

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA USAFIRISHWAJI WA MBOLEA

$
0
0
*Aitaka TFC kuwa na mikakati madhubuti.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na usafirishaji wa mbolea kutoka wa wasambazaji wa pembejeo nchini kwenda kwa wakulima. Pia ameitaka Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kuwa na mikakati madhubuti itakayowezesha upatikanaji wa mbolea kwa wakati wote nchini.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Januari 10, 2018) wakati akikagua usafirishaji wa mbolea kwenye maghala makubwa matatu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu amesema Serikali inahitaji kuona wakulima wote nchini wanapata pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea kwa wakati ili kilimo kiweze kuwaletea tija.

Amesema TFC inatakiwa ianze maandalizi ya usambazaji wa mbolea mapema kwani Serikali inataka wakulima wapate pembejeo miezi miwili kabla ya kuanza kwa msimu.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amemtaka Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba akutane na wadau na kufanya mapitio ya gharama za usafirishaji wa mbolea.

Amesema lengo la mapitio hayo ni kuhakikisha mkulima aliyeko kijijini anapata  mbolea hiyo kwa gharama nafuu bila ya kumuathiri mfanyabiashara.
Pia amemtakaDkt. Tezeba ashirikiane na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba ili kuhakikisha malori yanayobeba mbolea yanafika katika mikoa husika kwa wakati.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Kilimo awasiliane na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbawala ili malori yanayobeba mbolea yakifika kwenye vituo vya mizani yapewe kipaumbele.

“Si kwamba yaongeze uzito hapana, bali yapewe kipaumbele cha kupima haraka ili yaweze kuwahisha mbolea kwa wakulima kwani tayari msimu umeshaanza.”

Naye Waziri wa Kilimo, Dkt. Tizeba alisema watahakikisha mbolea ya kutosha inakuwepo nchini na kwamba wakulima wote wanaipata kwa wakati na kwa gharama nafuu.

Maghala aliyoyakagua Waziri Mkuu ni ghala la Mohammed Enterprises lililoko Mbagala, ghala la  Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) lililoko Kurasini na ghala la Premium lililoko Vingunguti ambako kote amekuta malori yakipakia mbolea kwa ajili ya uisafirisha katika mikoa mbalimbali nchini.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATANO, JANUARI 10, 2018.
 Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa katikati amekagua shughuli ya usafirishaji wa Mbolea  kwenda mikoani kutoka katika ghala la Mohamed Interprises lilipo Mbagala.kushoto kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Kilimo  Dkt. Charles Tizeba. nG1`a kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mohamed Interprises. Bwana Mohamed Dewji .Waziri Mkuu amefanya ukaguzi huo  leo Mkoani Dar es salaam   Januari 10/2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.  kushoto akiongea na Waziri wa Viwanda na  Biashara  (kulia).Bwana Charles Mwijage na  Waziri wa Kilimo (katikati) Dkt. Charles Tizeba pamoja na Maofisa wa JWTZ wakati alipo tembelea Kikosi cha 95KJ kinacho Safirisha Mbolea kwenda Mikoani. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

ALICHOKISEMA RC GAMBO LEO BAADA YA LOWASSA KWENDA IKULU NA KUONANA NA RAIS DKT MAGUFULI


MASAUNI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA KUWAIT NCHINI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Mohammad Alamiri(kulia) kuhusu ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na Kuwait katika masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama kwa raia wa nchi hizo mbili. Mazungumzo hayo yamefanyika leo ofisi za wizara,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Balozi wa Kuwait nchini, Mohammad Alamiri, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,(kushoto) kuhusu ushirikiano baina ya nchi ya Kuwait na Tanzania katika masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama kwa raia wa nchi hizo mbili. Mazungumzo hayo yamefanyika leo ofisi za wizara,jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea zawadi kwa niaba ya wizara kutoka kwa Balozi wa Kuwait nchini, Mohammad Alamiri(kulia), baada ya kumaliza mazungumzo  kuhusu ushirikiano baina ya nchi za Tanzania na Kuwait katika masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama kwa raia wa nchi hizo mbili.Mazungumzo hayo yamefanyika leo ofisi za wizara,jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini, Mohammad Alamiri, akipeaa mikono  na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto) wakati akimkabidhi zawadi baada ya mazungumzo kuhusu ushirikiano baina ya nchi za Tanzania na Kuwait katika masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama kwa raia wa nchi hizo mbili.Mazungumzo hayo yamefanyika leo ofisi za wizara,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

WAZIRI AFUNGUA KITUO CHA AFYA TUMBATU

$
0
0
Na Mwashungi Tahir, Maelezo Zanzibar.
WAZIRI Wa Nchi, Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa , Serikali za Mitaa na Idara Maalum  za SMZ Haji Omar Kheir alisema kabla ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar Kisiwa cha Tumbatu kulikuwa hakuna huduma yoyote ya maendeleo ikiwemo ya afya.

Akizungumza hayo Waziri huyo kwa niaba yaWaziri wa Nchi  Ofisi ya Rais  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Issa Haji Gavu  wakati wa ufunguzi ya wodi ya wazazi Tumbatu Gomani ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea miaka  54  ya Mapinduzi Matukufu.

Alisema huduma ya Afya kabla ya Mapinduzi ilikuwa adimu sana na kupatikana kwake ilikuwa lazima uifate Mkokotoni au kila alkhamis wanakuja madaktari kwa kutoa huduma ya afya kwa wananchi wa kisiwa hichi.

Hivyo Baada ya Mapinduzi Matukufu Marehemu Mzee Karume  akatoa ahadi ya kujenga kituo cha afya  kisiwani humo na huduma zikaanza kutolewa bila ya ubaguzi  na wananchi wote wakaanza kufaidika na huduma hiyo.

Aliwaomba kuitumia fursa hii akina mama  kwa kujifunguliya katika kituo hicho ambacho kina vifaa vyote vya huduma ya uzazi , na kuacha kujifunguliya majumbani kwani kunaweza kuhatarish afya ya mama na mtoto.

Aidha alisema hii ni ahadi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh Ali Mohammed Shein katika kutimiza ahadi zake za kuwapelekea wananchi wake huduma zilizo muhimu ikiwemo ya Afya katika maeneo ya mjini na vijijini ikiwa ni sera na ilani ya Chama cha Mapinduzi .

“Tuyatunze, tuyaenzi na tuyadumishe Mapinduzi yetu matukufu 1964  kwani ndio yaliyotukomboa katika madhila mbali mbali hadi kufikia hapa tulipo”.Alisema Waziri huyo.

Pia Waziri huyo aliahidi kuongeza vitanda 10 vya kujifunguliya pamoja na magodoro ili lengo kuiboresha Zaidi huduma hiyo.

Nae Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo alisema haya yote ni Matunda ya Mapinduzi Matukufu na jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya awamu ya saba ya  Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein kwa kuwajali wananchi wake kwa kuwasogezea huduma  mbali mbali za maendeleo  ikiwemo hii ya afya bora.

Waziri Kombo na Wizara yake,  amewaahidi kuwapelekea huduma zote kila panapostahiki ikiwemo dawa kwa wakati , na pia kuwanasihi wafanyakazi wa kituo hicho kuwa na maneno mazuri katika kuwahudumia wagonjwa pale wanapofika katika kituo hicho.

“Maneno mazuri  peke yake ni lugha ya faraja kwa mgonjwa, tayari unamjenga matumaini   na inampa amani na kuwa ni nusu ya tiba kwa upande wake mgonjwa huyo”. Alisema Waziri huyo.

Wakisoma risala yao  wananchi wa kisiwa cha Tumbatu  Gomani wamesema wanamshukuru Mh. Rais  wa  Zanzibar Dkt Ali Mohammed Shein kwa kuwapelekea mandeleo katika kisiwa hicho  ikiwemo huduma za afya bora na wanaahidi watakitunza na kukienzi na kuthamini juhudi zake za kuwajali wananchi wake.

Wakitoa changamoto wameiomba wizara ya Afya kuwapatia  madaktari kwa vituo vyote viwili vilivyopo Tumbatu Gomani na Jongowe, kupatiwa boti ya kisasa ya kusafirisha wagonjwa na wafanyakazi iwapo ikitokea dharurua, na kuwekewe vifaa vya kisasa vinavyoendana na uzuri wa jengo lenyewe. Jumla ya shilingi 221, 119 zimetumika kwa gharama za ujenzi pamoja na vifaa.        
Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheir kwa niaba ya Waziri wa Nchi ya  Ofisi na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.  Issa Haji Gavu  akifungua pazia akiashiria kufungua Wodi ya Wazazi Kituo cha Afya Tumbatu Gomani (Picha na Kijakazi Abdalla Maelezo )

RAIS WA TFF WALLACE KARIA AOMBOLEZA KIFO CHA OMARY KAPERA:

$
0
0

Kufuatia kifo cha beki wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Omary Kapera (wa tatu toka kulia) ,Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kifo cha beki huyo wa zamani. 
Rais Karia akitoa salamu za rambirambi amesema ni masikitiko makubwa kumpoteza mmoja wa wachezaji wa zamani aliyeitumikia pia timu ya taifa. 
"Nimeshtushwa na taarifa hizo za kifo cha Kapera hasa ikichukuliwa bado tupo kwenye majonzi ya kumpoteza mchezaji mwingine wa zamani Athuman Juma Chama,kwa niaba ya Shirikisho natoa pole kwa wote walioguswa na msiba huo kuanzia kwa familia,ndugu,jamaa na marafiki.”Alisema Rais Karia. 
Wakati wa uhai wake akicheza mpira amecheza katika klabu za Pan Africans na Yanga huku akipata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” 
Kufuatia msiba huo TFF itatoa rambirambi kwa familia ya Kapera.
  

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

IDARA YA MAGONJWA YA NDANI HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI KUHAMIA MLOGANZILA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUATILIA KWA KARIBU USAFIRISHAJI WA MBOLEA

Viewing all 109975 articles
Browse latest View live




Latest Images