Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

ASKOFU MPYA WA JIMBO LA BUKOBA

0
0
 Na Mwandishi Maalumu
Waamini na wapenzi wa Bukoba na Kagera wamefurahi sana kumpata Baba Askofu Desiderius Rwoma (pichani juu) kama askofu wa Jimbo la Bukoba kumrithi askofu Nestor Timanywa ambaye amestaafu kufuatana na sheria za kanisa.

Askofu Desiderius Rwoma alizaliwa mwaka 1947 katika parokia ya Rutabo, Kamachumu jimbo Katoliki la Bukoba. Parokia moja na Mwadhama Laurean Kardinali Rugambwa. Alipata upadrisho kwa mikono ya Baba Askofu Nestor Timaywa, mwaka 1974 pale Rutabo.

·        Akiwa jimboni Bukoba aliwahi kuwa gambera (Mkuu wa shule) ya seminari ya Rubya kwa miaka mingi. Wakati wake shule ya Rubya mara kadhaa ilikuwa ya kwanza kitaifa katika mitihani na karibu mara zote ilikuwa kila mara kati ya shule 10 bora taifani. Mapadre wengi vijana jimboni Bukoba walipitia mikono yake hivyo anawajua vizuri na wanampenda.
·        Vile vile alikuwa mlezi wa kiroho wa shirika la masista wa Mtakatifu Terezia wa Mtoto Yesu, shirika la jimbo na hivyo analifahamu vizuri na kila mara amekuwa  karibu nao.
·        Kabla ya kuteuliwa kuwa askofu wa Singida alikuwa makamu wa askofu wa Bukoba na hivyo kulijua jimbo la Bukoba na uongozi wake. Alifanya kazi hii vizuri sana na hivyo kuteuliwa kuwa askofu wa Singida.
·        Akiwa askofu wa Singida (1999 – 2013) ameonyesha karama zake za uongozi. Ameweza kuleta maendeleo ya kichungaji na kibinadamu katika jimbo. Ameonnyesha uelewano wake kwa kuwaalika mashirika mengi ya kitawa ambayo kila moja limeleta karama yake ya maendeleo, uchungaji, shule, vituo vya afya, maendeleo ya akina mama na vijana nk.
·        Katika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania anasimamia idara kubwa ya Utume wa Walei

Askofu Desiderius Rwoma ni mpole, mnyenyekevu, msikivu, muwazi na mpenda maendeleo. Ana uhusinao mzuri na kila mtu bila kujali hali, jinsia, kabila, taifa au dini.

WANABUKOBA NA WANAKAGERA WANAKUKARIBISHA KWA FURAHA NA SHANGWE, KARIBU NYUMBANI
 Bishop D. Rwoma na Bishop Nestor Timanywa katika basi na mabishop wengine
 Bishop Rwoma akiwa na baadhi ya Mabishop wazawa wa  Bukoba 
 Bishop Rwoma na Bishop Dallu wa Geita
 Bishop Rwoma na Bishop Kilaini wakiwa Singida
 Bishop Rwoma akiwa na waseminari wa  Singida
Bishop Rwoma baada ya kumuweka wakfu mchungaji mpya Singida

a word from Miriam Lulu Chemmoss

0
0

Click Display Images To Show The Picture

Hello Friends,
It is now 3 weeks into the year and if you are like me, you must be wondering what 2013 has in store for you. While I stay optimistic for a great year filled with many wonderful things, I also acknowledge that life has its ups and down. There will be joy and laughter....but there will also be sadness and tears.

As I look back into my own life and reflect on past disappointments and failures, I recognize on a deep level
that sometimes disappointments can lead us to a better place. As the wise saying goes, 'When one door closes,
another one opens".

And so I have come to accept that life is simple, yet sometimes it can get complicated. I’ve always wanted to write a song about life as it really is; the good, the bad and the ugly.

   Could there be life without death?
   Are there times when right is wrong?
   Do all endings lead to new beginnings?

Life's Duality is a song I wrote about the seasonal nature of life. Things are born and things also die. Things get
stronger while other things weaken. Sometimes it rains and sometimes it’s clear. You too, have seasons and that’s ok.

During good times, I relish and enjoy every moment and during tough times, it helps to know that 'this too shall
pass'. Whatever season you are in, whether a beginning or an ending, I hope this song speaks to you. Click here to watch the lyric video.

Blessings!
~~~
Miriam Lulu Chemmoss

P.S
Thank you for all your wonderful comments on the new album. It's available on iTunes & other stores or you can buy it from www.miriamchemmoss.com for exclusive bonuses.

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

0
0
Ngoma ya 'Shingo La Upanga' ya Jamhuri Jazz Band ilikuwa moto enzi hizo

ngoma azipendazo ankal - kizazi kipya

0
0
Ngoma ya 'Chanzo mwanaume' Mapacha watatu wakiwa na Khadija kopa si mchezo wallahi...

FAMILY DAY YA TANAPA YAFANA JIJINI ARUSHA

0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la hifadhi za taifa (TANAPA) wakiwa na familia zao kwenye sherehe ya familia waliyokuwa wameiandaa hivi karibuni iliyofanyika kwenye bustani ya Triple A iliyoko sakina nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Baadhi ya watoto wa Wafanyakazi wa  shirika la hifadhi za taifa (TANAPA) wakicheza moja ya michezo iliyokuwepo kwenye hafla hiyo hivi karibuni.

Article 16

DStv TO SCREEN OPRAH INTERVIEW WITH LANCE ARMSTRONG

0
0

DStv will broadcast the first ever no-holds-barred interview with world-renowned sporting personality, cyclist Lance Armstrong when he sits down with the queen of talk Oprah on Discovery TLC (Channel 172) on Friday 18 January at 19:30 CAT.

In this exclusive interview, which will be screened 24-hours after it airs in America; Armstrong addresses the alleged doping scandal, years of accusations of cheating and charges of lying about the use of performance-enhancing drugs throughout his storied cycling career.  

This is his only interview since the seven-time Tour de France winner was stripped of his titles and dropped from millions of dollars in endorsement deals. This, after the U.S. Anti-Doping Agency released an extensive report accusing the renowned cyclist of doping throughout his career.  Armstrong was given a lifetime ban on competing professionally.

Late last year, Armstrong resigned as chairman of the foundation he created, Livestrong, which has raised hundreds of millions of dollars in the fight against cancer.

Make sure to catch this sure-to-be-riveting interview! Repeats of the interview will be screened on Saturday 19 January at 12:50 CAT, Sunday 20 January at 17:50 CAT and Monday 21 January at 1:35 CAT.  

For more information log on to www.dstv.com

African Development Bank Approves US $24 Million Equity Investment to Boost East African Development Bank’s Balance Sheet

0
0
This week the Board of Directors of the African Development Bank (AfDB) approved an equity investment of US $24 million in the East African Development Bank (EADB) to strengthen its balance sheet and contribute to improve its international credit rating. In particular, US $10 million will be “paid in” with the balance in the form of callable capital.

The project will help EADB consolidate the gains of its successful restructuring program. It will assist the current business strategy of the bank by strengthening its capital base. This is a crucial condition for mobilizing financial resources from capital markets at more affordable terms and meeting the growing demand for investment in the East African Community (EAC).

In particular, in addition to providing fresh resources to EADB, the project is expected to contribute to improve the quality of the callable capital of the bank, which is a major factor driving its credit rating. A technical assistance package, financed by the Fund for African Private Sector Assistance (FAPA), to reinforce institutional capacity at EADB would complement the proposed equity investment. 

 By partnering with EADB, AfDB will exploit synergies stemming from complementary sources of comparative advantage. EADB, with its field presence and local knowledge of the EAC market, provides a logical conduit for AfDB to reach out to end-customers, including Small and Medium Enterprises (SMEs), by efficiently leveraging its scale.

From this perspective, the project is aligned with AfDB’s East African Integration Strategy, with its focus on sub-regional development finance institutions, as well as with the key pillars of AfDB’s forthcoming Long-Term Strategy, particularly private sector development and regional integration.

HAKUNA ATAKAYE KUFA WAKATI AKILETA KIUMBE DUNIANI - MAMA SALMA KIKWETE

0
0
Mahmoud Ahmad - Globu ya Jamii,Arusha

Kauli mbiu ya kongamano la ulimwengu la Afya ya uzazi linaloendelea jijini hapa imepewa msisitizo na kuwa hakuna mama atakayekufa wakati akileta kiumbe duniani na pia Afya ya mama na mtoto ipewe kipaumbele.

Kauli hiyo imeendelea kutolewa na mke wa raisi mama Salma Kikwete wakati akiwasilisha na kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo jijini hapa na kuwataka watafiti na wataalamu hao kuja na majibu yatakayosaidia kupunguza vifo vya wamama wakati wa kujifungua.

Mama kikwete alisema kuwa takwimu zinaonyesha kupungua kwa kiasi kidogo tatizo la kujifungua na kupoteza maisha hapa nchini na kuwataka wataalamu humu nchini kuchukuwa uzoefu walioupata kuchangia kupunguza vifo vya wamama wakati wa kujifungua sanjari na watoto huku wajawazito zaidi ya 459 hufa kila mwaka wakati wakijifungua.

“Asilimia 90% ya nchi zilizoendelea wanaweza kupunguza ama kuokoa maisha ya kinamama na watoto huku hapa nchini wakiandaa mpango endelevu wa kuokoa maisha ya wamamawajawazito wakati wa kijifungua na kutoa rai kuwa wamama wasife kwa magonjwa ambayo yanaweza kupatiwa tiba”alisema mama Salma.

Mama Salma alisema kuwa suala la afya ya uzazi liwe mpango endelevu kwa serekali na asasi mbali mbali na kuitaka serekali kulipa kipaumbele suala la afya ya mama na mtoto licha ya majukumu mbali mbali iliyonayo.

Nae naibu waziri wa Afya na maendeleo ya jamii hapa nchini Seif Raishid alisema kuwa serekali kupitia wizara hiyo wameweka kipaumbele suala la mama afya ya uzazi na kuwa hakuna mama atakaeyekufa wakati akiwa analeta kiumbe duniani sanjari na watoto na wamejipanga kuongeza wigo wa kuwafikia wakinamama kwa kuongeza zahanati kuwa karibu na usafiri sanjari na huduma muhimu.

Rashid akwataka watanzania walioshiriki kongamano hilo kutoa uzoefu walioupata kutatua tatizo la afya ya mama na watoto ilikupunguza vifo ambvyo vinawezekana kuepukika kutokana na kukosa eidha huduma muhimu wakati wakujifungua.

Kwa upande wake mkurugenzi wa afya dkt dumilia chalamila alisema kuwa mkutano huo umewashirikisha zaidi ya wataalam na watoa maamuzi zaidi ya 800 kutoka mataifa mbali mbali ulimwenguni wakichangia uzoefu katika kulipatia ufumbuzi suala la afya ya uzazi.

kichaka barabara ya sam nujoma rodi

0
0
Habari Michuzi Team,
Naomba muipost hiyo picha hii ili wahusika waweze kufyeka hivyo vichaka. Hili ni eneo la njia panda ya chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) karibu na daraja la Ubungo barabara ya Sam Nujoma. 

 Unapotoka Mlimani City ukifika njia panda hiyo kwenye mataa karibu na daraja, unapokata kwenda UDSM huwezi kuona vizuri magari yatokayo Ubungo mataa na hivyo ni rahisi kutokea ajali na hasa ukizingatia kuwa magari mengi huja kwa kasi eneo hilo. 

Naomba wahusika mlifanyie kazi swala hili.

MAJIBU YA HOJA YA Gesi: Tunagombania Bakuli za Supu, Ng’ombe Hajachinjwa!

Dkt. Shein akutana na Viongozi wa Jumuiya mbali mbali za CCM Zanzibar leo

0
0
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Viongozi wa Tawi la CCM Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui,wakiwemo Viongozi wa Jumuiya mbali mbali za Chama hicho katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo,MakamuMwenyekiti alifanya ziara maalum ya kusalimana na Viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuimarisha Chama cha Mapinduzi,(CCM) (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,na (kushoto) Mwenyekiti wa Tawi Nadra Juma Mohamed.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wapili kulia) akizungumza na Viongozi wa Tawi la CCM Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui,wakiwemo Viongozi wa Jumuiya mbali mbali za Chama hicho katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo,Makamu Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya kusalimana na Viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuimarisha Chama cha Mapinduzi,(CCM) (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

ZAIDI YA MILLION 31.9 ZAGHARAMIA VIFAA LIGI YA MOHAMMED DEWJI, SINGIDA

0
0

Mwenyekiti wa CCM jimbo la Singida mjini, Hamisi Nguli (kushoto) akikabidhi vifaa vya michezo kwa kiongozi wa tawi la Mitunduruni.

Foleni ya viongozi wa matawi katika jimbo la Singida mjini wakikabidhiwa vifaa vya michezo kwa ajili ya timu zao kushiriki kombe la MO inayotarajiwa kuanza Januari 20 mwaka huu.
Baadhi ya msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji kwa ajili ya kuendeleza mchezo wa soka jimboni kwake. (Picha zote na Nathaniel Limu).

Mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji,ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 31.9 vitakavyotumika kwenye ligi ya kombe lake, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi januari 20 mwaka huu.

Vifaa hivyo ni pamoja na jezi pea 854,mipira 122,soksi pea 854 na cloves za magolikipa 61.Vifaa hivyo ni kwa ajili ya timu zitakazoshiriki ligi ngazi ya kitongoji katika jimbo la Singida mjini.Baada ya ligi hiyo,itafuatwa na ligi ngazi ya kata ambayo atakuwa na vifaa vyake pia.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo,mwenyekiti wa CCM jimbo la Singida mjini, Hamisi Nguli amepongeza mbunge Dewji kwa kuendelea kutoa misaada mikubwa mbalimbali katika jimbo lake kwa lengo la kuendeleza wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla.

“Dewji toka awe mbunge wa jimbo la Singida mjini,siku zote yupo karibu zaidi na vijana. Amewasaidia mambo mengi makubwa ikiwemo kuwaendeleza kimichezo na pia ametoa pikipiki kwa ajili ya vijana wa bodaboda watakaojiunga katika vikundi”,alisema.

Awali msaidizi wa mbunge Dewji, Duda Mughenyi,amesema msaada huyo wa vifaa,ni mwendelezo wa Dewji kuhakikisha vijana wanatumia michezo kujiendeleza kimaisha.

TAARIFA KWA WATANZANIA WAISHIO KATIKAMAENEO YA UWAKILISHI WA UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINIAFRIKA KUSINI

Push Mobile, Channel Ten kutoa zawadi ya gari Valentine Day

0
0
Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa shindano la kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanao ‘ Valentine Day’ iliyoandaliwa kwa kushirikiana na Kampuni ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM. Kushoto ni AFISA Masoko na Mauzo wa AMG, Prosper Vedasto.

Na Mwandishi wetu

KAMPUNI ya Push Media Mobile itatoa zawadi ya gari aina ya Vitz lenye thamani ya shs milioni 8 kwa mshindi wa kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanoa “Valentine Day” ikayoa adhimishwa Februari 14.

Hayo yalisemwa na Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo katika uzinduzi wa kampeni hiyi pamoja na Kampuni ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM.

Rugambo alisema kuwa wameamua kutoa zawadi kubwa hiyo ili kuwafanya wapendanao wegi kushiriki na kupata nafasi ya kushinda. Alisema kuwa ili kuingia katika droo ya shindano hilo, unatakiwa kutuma neno “Penzi” kwenda namba 15678 na kujibu maswali mbali mbali yahusiyo masuala ya mapenzi na siku ya Valentine.

“Hii ni promosheni ya kwanza kubwa hapa nchini na mshindi kujishindia gari, lengo kubwa ni kutoa ufahamu kuhusiana na sikukuu ya wapendanao na vile vile kuwazawadia wadau waokwa kushiriki katika shughuli zao za ujenzi wa taifa,” alisema Rugambo.

Alisema kuwa mbali ya zawadi hizo, washiriki wa promosheni hiyo pia watapata nafasi ya kujisha kompyuta (Laptop) aina ya HP yenye thamani ya shs milioni 1.5, simu aina ya Blackberry Curve yenye thamani ya shs 500,000 na Home theatre ya thamani ya shs 400,000 na Ipad.

Kwa mujibu wa Rugambo, lengo lao kubwa ni kuifanya sikukuu ya wapendanao kuwa kubwa kama nyingine kwani mapenzi ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila siku.

Alisema kuwa mipango yao ni kuwekeza katika sikukuu hiyo ambayo jamii imeanza kuitilia mkazo japo si siku ya mapumziko kama sikukuu nyingine. Alisema kuwa kwa mwaka huu, wameweka bajeti ya shs milioni 30 ili kufanikisha zaoezi hilo.

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere hakuna kiyoyozi abiria walia kwa Joto

0
0
 Abiria wakiwa kwenye foleni ya kuboard kwa ajili ya safari ya kwenda sehemu mbali mbali duniani hivi sasa ,ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,wakiwa na vitambaa vyao vya kufutia jasho huku wengine wakionekana kulowa jasho kwenye mashati yao baada ya kiyoyozi cha uwanjani hapo kutofanya kazi na haijulikani ni kwanini. sasa pata picha hapa ndani jinsi palivyo halafu watu wapo kwenye foleni namna hii na kiyoyozi ndio hivyo kimegoma,unafikiri inakuwaje??

BREKING NYUUUUUZ: BRITISH AIRWAYS YAFUNGA VIRAGO TANZANIA

0
0
BAADA YA KUWA TANZANIA KWA KIPINDI CHA MIAKA 82, TOKA ENZI ZA BOAC, SHIRIKA LA NDEGE LA UINGEREZA YAANI BRITISH AIRWAYS LIMEAMUA KUITOSA RASMI TANZANIA,GLOBU YA JAMII INAWEZA KUTHIBITISHA!

HABARI ZA UHAKIKA TOKA JIKONI ZINASEMA NDEGE YA MWISHO YA BRITISH AIRWAYS KUTUA TANZANIA ITAKUWA MACHI 29, 2013 WAKATI BOEING 767 YA SHIRIKA HILO AMBAYO NI KIJEBA (ZINAZOKUJA HUKU ZINA UMRI ZAIDI YA MIAKA 20) ITATUA KWA MARA YA MWISHO.

NA KWA HUZUNI KUBWA KWA WADAU WAKE, OFISI ZA BRITISH AIRWAYS PALE SERENA INN JIJINI DAR ES SALAAM ZITAPIGWA KUFULI RASMI MACHI 31, 2013

MZEE MALECELA, WAZIRI MKUU MSTAAFU SUMAYE NA JAJI MKUU MSTAAFU SAMATTA WATOA MAONI KATIBA MPYA LEO

0
0
Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliokutana nao leo kutoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Mjumbe wa Tume Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim (katikati).
Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliokutana nao leo kutoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba.
Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela akipata maelezo kuhusu Kitengo cha Utafiti cha Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoka kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume Bw. Mohammed Hamad leo mara baada ya kutoa maoni yake kuhusu katiba Mpya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba.
Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliokutana nao leo kutoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Mjumbe wa Tume Prof. Mwesiga Baregu.
Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela akitoka nje ya ukumbi wa mikutano wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo mara baada ya kutoa maoni yake kuhusu katiba Mpya. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na kulia ni Mjumbe wa Tume Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim.

TANGAZO

0
0

Mpenzi msomaji, wa Gazeti la HABARILEO, tuletee picha za harusi, Kumuaga Bi Harusi, Uchumba, Ubatizo, Kipa imara, na nyinginezo, nasi tutazichapisha bureee katika Ukurasa huu.



Unaweza kutuletea moja kwa moja katika Ofisi zetu Zilizoko Jengo la Daily News Makao Makuu, Barabara ya Mandela Tazara (Tunatazamana na Ofisi za TAZARA), Dar es Salaam au kupitia anuani ya barua pepe habarizapicha@gmail.com–MHARIRI. 

PIA waweza kuzituma kwa barua pepe:- mrokim@gmail.comKWA MAELEZO ZAIDI PIGA +255 755 373999 AU +255 717 002303.

Mama Salma Kikwete afunga kongamano la Kimataifa la afya ya uzazi jijini Arusha leo

0
0

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete akizungumza wakato akifunga kongamano la Kimataifa la Afya ya Uzazi la siku 3 Katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC mjini Arusha leo, Kongamano hilo lilewashirikisha wataalamu wa masuala ya afya ya uzazi wapatao 800 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni.
Pichani toka kulia ni Naibu Wazirii wa Afya,Dkt. Seif Rashid (Kulia) ,Waziri wa Afya Zanzibar,Dkt. Juma Haji Duni (kati) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh. Magesa Mulongo wakifuatilia Kongamano hilo.
Baadhi ya wataalamu wa kongamano la Kimataifa la afya ya uzazi wakimsikiliza Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete (hayupo pichani wakati wa kufunga kongamano hilo leo jijini Arusha, ambapo wataalamu wa masuala ya afya ya uzazi zaidi ya 800 kutoka ndani na nje ya nchi wamehudhuria.
Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar,Dkt. Juma Haji Duni akiongea katika kongamano hilo leo mjini Arusha.kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh. Magesa Mulongo
Mke wa Rais na Mwenyikiti wa Taasisis ya WAMA ,Mama salma Kikwete (alievaa kitenge) akiogozana na watendaji wakuu wakielekea kwenye Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha leo.
Mama Salma Kikwete akifurahia ngoma ya msanja ya kikundi cha akina mama huko Arusha.
Picha ya pamoja na watendaji wakuu wa kongamano la Kimataifa la Afya ya Uzazi.Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images