Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110102 articles
Browse latest View live

Ratiba ya Kuaga na Mazishi ya Paul Beda Moshi (Mzee Nuru) wa NURU Funeral Services

$
0
0


Leo Jumapili  tarehe 7 January, 2018 kutakuwepo na shughuli ya kumuaga Mpendwa wetu Marehemu Mzee Paul Beda Mosh,Kuanzia Saa nne asubuhi mpaka saa saba Mchana .

Ndugu, jamaa na marafiki watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu. 

Saa 07:00(Saba) Ibada itaanza ambayo itafanyikia nyumbani kwa Marehemu.

Baada ya Ibada, safari ya kuelekea Rombo kwa Mazishi itaanza.

Kwa hapa Dar es Salaam msiba upo maeneo ya Kawe Tripple Seven - 777, Kuelekea Lugalo Golf club.

Baada ya hapo Safari ya kuelekea Tarekea, Rombo itaanza. 

*Jumatatu 8.1.2017*

Kutakuwa na ibada ya mazishi huko Tarakea, Rombo, Kilimanjaro.

MBUNGE UNGANDO KUTATUA KERO YA KITANDA CHA KUJIFUNGULIA HUKO MUYUYU

$
0
0

Na Mwamvua Mwinyi,Kibiti

MBUNGE wa jimbo la Kibiti ,mkoani Pwani ,Ally Ungando ameahidi kuitatua kero ya kitanda cha kujifungulia akinamama wa kijiji cha Muyuyu kata ya Mtunda,kero ambayo imedumu kwa muda mrefu sasa.

Pamoja na hilo amesema atatoa fedha kiasi cha sh.mil.nne ambapo mil.mbili itakuwa kwa ajili ya kujenga choo kwenye nyumba ya mganga wa zahanati ya Muyuyu na milioni mbili nyingine kwa lengo la kumalizia choo katika shule ya msingi Muyuyu.

Ungando alibaini kero hiyo wakati akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya siku 21 jimboni humo .Hata hivyo Ungando ,alisema ataendelea kwenda sambamba na kauli mbiu yake yake ya mwendo kasi katika maendeleo ya Kibiti .

Alieleza ,jukumu lake kubwa ni kushirikiana na wananchi kutatua kero mbalimbali zinazowakabili ,kuzisimamia kwenye idara husika na kufuatilia yale yanayoendelea kufanyiwa kazi .Ungando ,aliwataka wananchi wa Kibiti kushirikiana nae kuchangia pia shughuli za kimaendeleo badala ya kuisubiria serikali pekee ama wafadhili suala ambalo litawachelewesha kupiga hatua na kutoka walipo sasa .

"Ninafanya ziara hii ,sio kujua changamoto zilizojitokeza na kuwaeleza nilipofikia kwenye ufuatiliaji kwa zile nilizoanza nazo " serikali inafanya yale ambayo yapo kwenye taratibu zake hivyo na sie jamii tuiungr mkono kwa kuendeleza yale ambayo yapo kwenye uwezo wetu "alisema Ungando.

Mbunge huyo ,alipokuwa kata ya Kiongoroni alitembelea visiwa vya Pombwe,Jaja,Kiongoroni na Ruma aliwaasa wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule na kuacha tabia ya kuwaacha majumbani jambo ambalo linawakosesha haki ya kielimu.

Ungando alitaka wananchi wa visiwa hivyo ,kuwachunguza watu ambao wana mashaka nao kwakuwa wahalifu wakitokea Gongoni wanaweza kukimbilia visiwani.Alisema ulinzi na usalama upo mikononi mwa kila mmoja hivyo wachunguzane wao kwa wao kwani wanajuana.

Akiwa visiwani hapo,alipokea changamoto za uchache wa watumishi wa idara ya afya,elimu ikiwemo upungufu wa nyumba za walimu na miundo mbinu ya barabara na kuahidi atazisimamia .Wananchi wa vijiji hivyo walimshukuru Mbunge wao Kwa juhudi anazozionyesha kwa kuwatumikia na walimuomba akafanyie kazi changamoto walizomueleza ili kuondokana na adha walizonazo.

Katika ziara hiyo ,Ungando alitoa mifuko ya saruji 100 kwenye kata alizopitia ili kusaidia masuala ya maendeleo ambapo ameshatembelea kata ya Mtunda,Mtawanya,Ruaruke na Kiongoroni.
Mbunge wa jimbo la Kibiti, mkoani Pwani Ally Seif Ungando ,wa kwanza kulia akisafiri na msafara wake ,kwa kutumia njia ya majini kuelekea kwenye visiwa vilivyopo kata ya Kiongoroni, kwenye muendelezo wa ziara yake jimboni humo .(picha na Mwamvua Mwinyi)

MDAU AUNDA GARI LAKE JIJINI MBEYA

OHOOO..!

KAMANDA WA POLISI TANGA ATOA UFAFANUZI WA BASI LA SIMBA COACH KUCHOMWA MOTO

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii

JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga limetoa ufafanuzi kuhusu tukio la kuchomwa moto kwa basi la Simba Coach.

Kwa mujibu wa taarifa zinaeleza basi hilo limechomwa leo na wananchi wenye hasira kali baada ya dereva wake kumgonga dereva wa bodaboda.

Akizungumza na Michuzi Globu kwa njia ya simu muda huu, Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Tanga Edward Bukombe amefafanua ni kweli amesikia taarifa za kuchomwa moto basi hilo lakini halijachomwa mkoani Tanga kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.

Amesema baada ya kuona taarifa za kuchomwa basi la Simba Coach waliamua kufuatilia lakini wamejiridhisha haikutokea kwenye mkoa wao ila  basi hilo limechomwa nchini Kenya.

Kamanda Bukombe ameiambia Michuzi Globu kuwa basi hiyo ilikuwa inatoka Mombasa nchini Kenya na taarifa walizonazo limechomwa huko huko nchini Kenya kwani lilikuwa halijaingia kwenye mipaka ya nchi yetu ya Tanzania na hasa mkoani Tanga.

Alipoulizwa iwapo anafahamu namba za basi hilo linalodaiwa kuchomwa moto na dereva aliyekuwa analiendesha ,amejibu wanaendelea kufuatilia kwa polisi wa nchini Kenya na kisha atatoa taarifa kuufahamisha umma.

"Tunaendelea kukusanya taarifa na kwa kuwa limechomwa huko Kenya tunawasiliana na polisi wa huko ili tuwe na uhakika wa taarifa Kamili za tukio hilo.Hatujapata namba za basi.Wananchi wasubiri tutaeleza kwa usahihi tutakapokamilisha kupata ukweli zinazohusu tukio hilo, "amesema Kamanda Bukombe.

TAARIFA KUCHOMWA MOTO SIMBA MTOTO

Mapema asubuhi ya leo katika mitandao ya kijamii zilianza kuzagaa picha zinazoesha basi linaungua moto, na vyanzo vya moto huo ikawa inaelezwa ni wananchi wenye hasira wamechoma moto basi la Simba Coach.

Taarifa hizo zikawa zinadai tukio hilo limetokea Mkoa wa Tanga lakini haikuwa inaonesha ni wananchi wa eneo gani walioamua kuchoma basi hilo.

Pia taarifa hiyo imedai basi limochomwa moto kutokana na dereva wake kugonga dereva wa pikipiki na hivyo wananchi wakaonesha hasira zao kwa kulichoma moto basi hilo. 

 

DKT.MARIA MASHINGO AWATAKA WAFUGAJI KUHAKIKISHA IFIKAPO JANUARI 31 MIFUGO YOTE NCHINI IWE IMEPIGWA CHAPA

$
0
0

Na Kumbuka Ndatta, WMUV

KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dk. Maria Mashingo amewataka wafugaji kuhakikisha wamekamilisha zoezi la upigaji chapa mifugo yao kabla ya muda ulioongezwa na Serikali wa hadi Januari 31 mwaka huu kwani baada muda huo kupita haijulikani Serikali itaamua nini kuhusu mifugo itakayokuwa haijapigwa chapa.

Akizungumza wakati akishiriki zoezi la upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Igalula Kata ya Mpanda ndogo Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, Dk. Mashingo alisema zoezi hilo la upigaji chapa linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya utambuzi ,usajili na ufuatiliaji wa mifugo Na. 12 ya Mwaka 2010 .

Dk. Mashingo alisema upigaji chapa umelenga kudhibiti magonjwa ya mifugo,wizi wa mifugo, uimarishaji usalama wa afya na mazao ya mifugo sambamba na kudhibiti usafirishaji na uhamaji wa mifugo kiholela na kuimarisha biashara ya mifugo na mazao yake kitaifa na kimataifa.

"Wafugaji hakikisheni mifugo yenu yote inapigwa chapa kwani baada ya Januari 31 mwaka huu hatujui Serikali itaamua nini kwa mifugo itakayokuwa haijapigwa chapa "alisema.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Maria Mashingo akipiga chapa  ng’ombe katika Kijiji cha Igalula Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi leo alipokwenda kuhamasisha zoezi la upigaji na kuwataka wafugaji kuhakikisha mifugo yote inapigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo) Dk. Maria Mashingo akiwaonesha wafugaji sehemu sahihi ambayo ng’ombe anatakiwa kupigwa chapa ili kuepuka kuiraribu ngozi baada ya kushiriki zoezi la upigaji chapa katika Kijiji cha Igalula wilayani Tanganyika mkoani Katavi leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Maria Mashingo akipiga chapa  ng’ombe katika Kijiji cha Igalula Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi mapema leo alipokwenda kuhamasisha zoezi la upigaji na kuwataka wafugaji kuhakikisha mifugo yote inapigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.

KAULI YA MBUNGE YADAIWA KUCHOCHEA WANANCHI KUUA TEMBO

$
0
0

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

KAULI za baadhi ya wanasiasa za kuhamasisha wananchi kuua tembo katika Jimbo la Serengeti mkoani Mara zinadaiwa zimeanza kuleta athari baada ya watu wanne kukamatwa na Polisi kwa tuhuma za kuua tembo.

Baadhi ya wananchi ambao wameomba majina yao kutoandikwa kwenye habari hii, wameiambia Michuzi Globu kwa njia ya simu kuwa kuna mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Chacha(Chadema) akiwa kwenye msiba wa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 32 aliyeuliwa na tembo katika kijiji cha Kenoku kwa Mfano aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali imeshindwa kuweka uzio ili tembo wasilete madhara, hivyo nao wawaue tembo tu.

Kwa mujibu wa watoa taarifa hizi wamedai baada ya kauli hiyo imeonekana kuchochea watu kufanya ujangiri kwa kuua tembo na Jumatano ya wiki hii kuna watu wanne katika kijiji cha Robanda wamekamatwa kwa tuhuma za kuua tembo.

"Ni vema Mbunge akawa makini na kauli zake kwani baada ya kuwaambia wananchi waue tembo wanapokuja kijijini, tayari kuna watu wanne wamekamatwa kwa tuhuma za kuua tembo eneo la kijiji cha Robanda jimboni Serengeti."Hili si la kulifumbia macho kwa mbunge wetu amekuwa na utamaduni wa kutoa kauli ambazo zinachangia wananchi kuua tembo"amedai moja ya watoa taarifa hizi.

MBUNGE AFAFANUA

Akizungumza na Michuzi Globu, Mbunge wa Serengeti Chacha Marwa amesema madai ya wananchi hao ambao wametoa taarifa hizo hayana ukweli wowote.

Kwani amesema hakuna mahali ambako amewaambia wananchi waue tembo na badala yake amekuwa akiiomba Serikali kufanya jitihada za kuweka uzio ili tembo wasiingie vijijini kwa wananchi kwani watu wanakufa na mazao yanaharibiwa kila kukicha.Marwa amesema amefuatilia suala hilo muda mrefu Wizara ya Maliasili na Utalii tangu Waziri akiwa Profesa Jumanne Maghembe lakini hakuna uzio hadi leo hii.

Ameongeza amewahi kuandika barua kwa Spika wa Bunge ya kulalamikia tembo kuingia maeneo ya wananchi na kuleta madhara hakuna ambacho kimefanyika."Nikweli nilienda kushiriki kwenye msiba wa kijana mmoja aliyeuliwa na tembo siku za karibuni, ila sijahamasisha wananchi kuua tembo na siwezi kufanya hivyo.

"Kwanza kijiji ambacho msiba umetokea ni kilometa 50 na kijiji cha Robanda, sasa kwanini wanizushie hayo maneno.Hayo ni mambo tu ya siasa za huku kwetu."Pia tuseme ukweli, wananchi wamekuwa wakiteseka sana kutokana na tembo kuja kwenye makazi ya watu na kuleta madhara, kila siku wananchi wanalia na ipo siku watachoka kweli.

"Hivyo niiombe Serikali itusaidie kuondoa tatizo hili huku kwetu kwa kulinda usalama wa wananchi wake,"amesema Marwa.

POLISI YATAJA WANAOSHIKILIWA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara limekiri kukamatwa kwa watu hao baada ya kupatikana kwa taarifa za kuua tembo hao ambapo kwa sasa jeshi hilo linawashikilia. 

Limewataja watuhumiwa wanaoshikiliwa kwa kutuhuma hizo za kuua tembo na kukutwa wakiwa na meno yake ni Kirihena Bwanana(34),mkazi wa Bwitenga.Wengine ni Kasimu Mussa(40),mkazi wa Robanda, Hamisi Gamuhu(37),mkazi wa Robanda na Hamisi Mabula(52) mkazi wa Kitembele.
 Watuhumiwa wa pembe za ndovu wakiwa wamewekwa chini ya ulinzi mara baada ya kunaswa wakituhumiwa kuua tembo.
 Mtuhumiwa wa pembe za ndovu akiwa amewekwa chini ya Ulinzi na Askari Wanyama Pori  

Mtuhumiwa wa pembe za ndovu akiwa amewekwa chini ya Ulinzi na Askari Wanyama Pori  

WAZIRI MKUU AAGIZA VIONGOZI NCHINI WATOE TAARIFA

$
0
0
*Ni kuanzia Mawaziri hadi Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Mawaziri wote, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya na Wakurugenzi watoe taarifa za fedha za miradi ya maendeleo kwa wananchi badala ya kusubiri ziara za viongozi wakuu.

Ametoa agizo hilo jana (Jumamosi, Januari 6, 2018) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwenye kikao kilichofanyika hoteli ya Mt. Vicent, mjini Mbamba Bay, wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.

“Kuanzia sasa ninaagiza, viongozi wote wa ngazi za juu wakiwemo Mawaziri hadi Wakurugenzi na hata ninyi wakuu wa idara mnawajibika kutoa taarifa za fedha tunazopeleka kwenye miradi kwa sababu wananchi wana haki ya kujua utekelezaji wa ahadi za Serikali,” alisema.

Alisema kila wanapoenda kwenye ziara ya kikazi vijijini, waelezee thamani za kazi zilizofanyika na waeleze ni lini miradi hiyo itakamilika.

“Mnapopata fursa ya kupanda jukwaani, tumieni wasaa huo kueleza kazi kubwa ambazo zimefanywa na Serikali. Elezeni Serikali imeleta fedha kiasi gani, kwa ajili ya kitu gani na kwa kufanya hivyo, mtasaidia kutoa taarifa za utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa kampeni,” alisema.

Alisema wananchi wana haki ya kupatiwa taarifa za utendaji wa Serikali yao na akawataka viongozi hao wasisubiri ziara za viongozi wa kitaifa. “Nendeni mkaongee na wananchi, msiwaachie Wakuu wa Wilaya au Wabunge peke yao ndiyo waseme na wananchi,” alisema.

Waziri Mkuu leo anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma kwa kukagua kituo cha kufua umeme kilichopo Unangwa, kuweka jiwe la msingi la ofisi ya TANESCO, kuzungumza na wananchi na kisha kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Songea.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMAPILI, JANUARI 7, 2018.

WAZIRI MKUU AAGIZA VIONGOZI NCHINI WATOE TAARIFA

$
0
0
*Ni kuanzia Mawaziri hadi Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Mawaziri wote, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya na Wakurugenzi watoe taarifa za fedha za miradi ya maendeleo kwa wananchi badala ya kusubiri ziara za viongozi wakuu.

Ametoa agizo hilo jana (Jumamosi, Januari 6, 2018) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwenye kikao kilichofanyika hoteli ya Mt. Vicent, mjini Mbamba Bay, wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.

“Kuanzia sasa ninaagiza, viongozi wote wa ngazi za juu wakiwemo Mawaziri hadi Wakurugenzi na hata ninyi wakuu wa idara mnawajibika kutoa taarifa za fedha tunazopeleka kwenye miradi kwa sababu wananchi wana haki ya kujua utekelezaji wa ahadi za Serikali,” alisema.

Alisema kila wanapoenda kwenye ziara ya kikazi vijijini, waelezee thamani za kazi zilizofanyika na waeleze ni lini miradi hiyo itakamilika.

“Mnapopata fursa ya kupanda jukwaani, tumieni wasaa huo kueleza kazi kubwa ambazo zimefanywa na Serikali. Elezeni Serikali imeleta fedha kiasi gani, kwa ajili ya kitu gani na kwa kufanya hivyo, mtasaidia kutoa taarifa za utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa kampeni,” alisema.

Alisema wananchi wana haki ya kupatiwa taarifa za utendaji wa Serikali yao na akawataka viongozi hao wasisubiri ziara za viongozi wa kitaifa. “Nendeni mkaongee na wananchi, msiwaachie Wakuu wa Wilaya au Wabunge peke yao ndiyo waseme na wananchi,” alisema.

Waziri Mkuu leo anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma kwa kukagua kituo cha kufua umeme kilichopo Unangwa, kuweka jiwe la msingi la ofisi ya TANESCO, kuzungumza na wananchi na kisha kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Songea.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMAPILI, JANUARI 7, 2018.

BABU SEYA NA PAPII KOCHA WAAHIDI KUUKOMBOA MUZIKI WA DANSI

Msanii Pretty Kind afungiwa kujihusisha na kazi za Sanaa kwa muda wa Miezi Sita, Giggy Money aitwa kujieleza

$
0
0
Na Anitha Jonas – WHUSM ,Dar es Salaam

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amemfungia Msanii Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind kujihusisha na shughuli za Sanaa kwa muda wa miezi sita.
Naibu Waziri Shonza amechukua hatua hiyo leo jijini Dar es Salaam kutokana na msanii huyo Kutoa wimbo usiyo na maadili wenye jina la ‘’Viduduwasha’’, Kufanya kazi ya Sanaa bila kusajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa, pamoja na kuweka mtandaoni picha ya nusu utupu kinyume na maadili ya Kitanzania.
‘’Kumekuwa na wimbi kubwa la wasanii sasa hivi kutoa nyimbo zenye maneno ya matusi na zisizo na maadili pamoja na wasanii hasa wanawake kupiga picha wakiwa wamevaa nusu utupu na kuweka picha hizo katika mitandao,nataka kuwapa angalizo wasanii wenye tabia hizi kuwa Serikali inawafuatilia kwa karibu na mwaka huu tumeanza na huyu na wengine wanafuata kama msanii Gift Stanford maarufu kama Gigy Money na Jane Rimoy maarufu kama Sanchi,’’ alisema Mhe.Shonza.
Mhe.Shonza alitoa msisitizo wa kumtaka msanii Gigy Money kufika ofisini kwake haraka, kutokana kuwa hivi karibuni alimtumia ujumbe wakumtaka afike ofisini kwake lakini bado hajafika mpaka sasa hivyo amemwambia kuwa atambue hawezi kushindana na Serikali.
Kwa upande wa Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza katika mkutano huo alieleza kuwa kwa mujibu wa Kanuni 31 (1) ya Baraza ya mwaka 2005,inaeleza kuwa msanii kufanya kazi bila kusajiliwa ni kosa na anaweza kufungiwa, na pia kwa upande wa mavazi zinasema msanii anatakiwa kuvaa mavazi yenye stara yasiyomdhalilisha wala kudhalilisha watazamaji wake.

‘’Napenda kuwasisitiwa wasanii wote ambao wanajijua kuwa hawajasajiliwa BASATA kuja kujisajili haraka na kwa wale waandaji wa kazi za Sanaa kama waongozaji wa (Directors),Waandaaji (Producers) na wamiliki wa Studio za kurekodi kazi za Sanaa ambao hawajasajiliwa nao waje kujisajili haraka ’’ alisema Bw.Mungereza.
Pamoja na hayo naye Msanii Suzan Michael Maarufu kama Pretty Kind aliomba radhi mashabiki wake kwa kufanya makosa hayo pamoja na watanzania wote kwa ujumla na kuaahidi kujirekebisha na kuto kurudia tena makosa hayo.
Halikadhalika Naibu Waziri Shonza ametoa rai kwa wamiliki wa vyombo vya Habari kutokubali kupiga nyimbo au video za nimbo zisizo na maadili kwani wanakuwa ni sehemu ya kutangaza vitendo hivyo vilivyo kinyume na maadili kwani itafika mahali serikali itachukulia hatua hata vyombo vinavyopiga nyimbo zisizo na maadili.


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu kumfungia kujihusisha na kazi za Sanaa kwa muda wa Miezi Sita Msanii Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind, kutokana na kuimba wimbo usiyo na maadili wenye jina la Viduduwasha,Kufanya kazi za Kisanii bila kusajiliwa na Baraza la Sanaa (BASATA) pamoja na kuweka mtandaoni picha aliyokuwa amevaa nusu utupu. Kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa Godfrey Mngereza na kulia ni Msanii aliyefungiwa Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind.
Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa Godfrey Mngereza akitoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu sheria iliyotumika kumfungia Msanii Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind kwa mujibu wa BASATA (kushoto),kulia kwake ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza.
Msanii Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind akimwaga machozi mara baada ya kuelezwa adhabu anayopewa ya kufungiwa kujihusisha na kazi za Sanaa kwa muda wa miezi Sit+*+99a na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (hayupo pichani) kutokana na kufanya kazi ya Sanaa pasipo kusajiliwa,kukiuka maadili ikiwepo kuweka picha ya utupu mtandaoni leo jijini Dar es Salaam.

RATIBA RASMI YA MAZISHI YA MKE WA MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU

DKT. MWAKYEMBE AOMBOLEZA KIFO CHA MCHORA KATUNI MASHUHURI THADDEI THOMAS MAREALLE

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mchora Katuni mashuhuri Ndg. Thaddei Thomas Marealle kilichotokea asubuhi ya tarehe 05 Januari, 2018 katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam. 
Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa kifo chake Ndg. Thaddei kimeinyang’anya fani ya uchoraji na kwa ujumla tasnia nzima ya Sanaa za Ufundi mmoja wa Wasanii mahiri waliokuwa tegemeo kubwa la Maendeleo ya tasnia hiyo nchini. 
Dkt. Mwakyembe ametoa pole kwa familia, uongozi wa kampuni ya WAMASA Puplications Ltd, ndugu, jamaa, marafiki na wanasanaa wote nchini na kuwaombea Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha msiba. 
Kipindi cha uhai wake marehemu Ndg. Thaddei alifanya kazi na kampuni ya WAMASA Publications Ltd inayo chapishaji gazeti la Sani.  Marehemu Thaddei atakumbukwa sana kwa katuni yake maarufu ya Sokomoko iliyokuwa ikichapishwa na gazeti la Sani.                         
Imetolewa na:
   
Octavian F. Kimario
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
07/01/2018.


RAIS MSTAAFU WA ZANZIBAR DKT. AMANI ABEID KARUME AZINDUA UKUTA WA BAHARINI FORODHANI.

$
0
0
 Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt,Aman Abeid Karume alipokata utepe kuashiria Uzinduzi wa  Ukuta wa Baharini Mizingani Mjini Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia  Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.kulia yake ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt,Khalid Salum Mohammed na kushoto ni Mwakilishi wa Benki ya Dunia Andre Bald.
 Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt,Aman Abeid Karume akiangalia Ramani na kupata maelezo kutoka kwa  Mratibu wa Mradi wa Huduma za Jamii Mijini(ZUSP)Makame Ali Makame kuhusiana na Ujenzi wa Ukuta wa Baharini katika uzinduzi wa ukuta huo Mizingani Mjini Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia  Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt,Aman Abeid Karume  akikunjuwa Kitambaa kuashiria Uzinduzi wa  Ukuta wa Baharini Mizingani Mjini Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia  Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt,Aman Abeid Karume  katikati akitembea kwa miguu baada ya uzinduzi wa  Ukuta wa Baharini Mizingani kuelekea katika Bustani ya Forodhani  Mjini Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia  Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi wa  Ukuta wa Baharini Mizingani sherehe zilizofanyika katika Bustani ya Forodhani  Mjini Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia  Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Mwakilishi wa Benki ya Dunia Andre Bald akitoa maelezo kuhusiana na ujenzi wa  Ukuta wa Baharini Mizingani sherehe zilizofanyika katika Bustani ya Forodhani  Mjini Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia  Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt,Khalid Salum Mohammed akitoa hotuba khusiana na Ujenzi wa Ukuta wa Baharini Mizingani pamoja na miradi mbalimbali ya serikali katika katika uzinduzi wa  Ukuta wa Baharini Mizingani sherehe zilizofanyika katika Bustani ya Forodhani  Mjini Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia  Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt,Aman Abeid Karume akisisitiza jambo alipotoa hotuba ya Uzinduzi wa Ukuta wa Baharini Mizingani sherehe zilizofanyika katika Bustani ya Forodhani  Mjini Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia  Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.kushoto yake ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt,Khalid Salum Mohammed na kulia ni Mwakilishi wa Benki ya Dunia Andre Bald.
PICHA NA YUSSUF SIMAI - MAELEZO ZANZIBAR.

Azam TV - MAPINDUZI CUP, FULL HIGHLIGHTS: SIMBA 0-1 AZAM FC


2nd Karata Tournament Winners from Tanzania!

$
0
0

Congratulations Benson Akwilini and Saidy Suleiman!
Benson was the Best Player and Saidy was the Leaderboard Winner! They will both receive a Lifestyle Action Camera!
 Benson Akwilini is  a Senior Graduate Engineer from Tegeta (Dar-es-Salaam) in Tanzania. He has two brothers and his hobbies are football​, poker games, surfing, and working on personal projects.
His experience in playing Albastini since he was in Secondary school is what helped him to become the Best Player in the tournament (Benson only lost 2 games in the entire tournament earning him an 85% winning ratio).
Benson will enjoy taking pictures/videos on his new Action Camera to share on his Facebook & Instagram page.

Saidy Suleiman is from Tanga, Tanzania, and he has three brothers. His Hobbies are playing football, reading story books, and playing challenging online games like Albastini and Pro Evolution Soccer. 
Saidy learned how to play the game from community elders many years ago.
He advises other players to never give up until the end of the game because anything is possible.
We are looking forward to seeing all the exciting new videos/pictures that Saidy will take on his brand new Lifestyle Action Camara to share on his Facebook & Instagram page. 

NEC yavitaka vyama vya siasa vitumie Sheria na Kanuni kuwasilisha malalamiko ya uchaguzi

$
0
0
Na Hussein Makame
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka vyama vya siasa vitumie utaratibu uliopo wa kisheria na kikanuni kuwasilisha malalamiko juu ya mambo yanayojitokeza wakati wa uchaguzi badala ya kuitaka Tume ishughulikie malalamiko ambayo haina mamlaka nayo.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa NEC Jaji (R) Semistocles Kaijage wakati akifungua mkutano wa Tume na viongozi wa vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Alisema kuwa uzoefu wa chaguzi zilizopita umeonyesha kuwa viongozi wa vyama vya siasa wamekuwa wakifuata vyema taratibu zilizowekwa chini ya Sheria za Uchaguzi katika hatua ya uteuzi wa wagombea katika chaguzi.  
Hata hivyo, alibainisha kuwa katika hatua za kampeni hadi kutangaza matokeo, baadhi ya vyama vya siasa na wagombea wao mara kadhaa wameshindwa kufuata taratibu zilizoainishwa katika Sheria za Uchaguzi na Maadili ya Uchaguzi hasa pale ambapo viongozi hao wagombea wanaona haja ya kuchukuliwa hatua dhidi ya uvunjwaji wa Sheria, Kanuni au Maadili ya Uchaguzi na au taratibu za Uchaguzi.
“Tume inachukua fursa hii kuwakumbusha viongozi wa vyama vya siasa kuwa kwenye Maadili ya Uchaguzi, Sheria za Uchaguzi na kwenye Sheria nyingine za Nchi umewekwa utaratibu fasaha wa jinsi na namna ya kushughulikia malalamiko yanayohusu na kugusa ukiukwaji wa Sheria, taratibu na Maadili ya Uchaguzi” alisema Jaji Kaijage.
Alifafanua kuwa miongozo hiyo imetaja na kuainisha adhabu na hatua mbalimbali za kisheria na kikanuni dhidi ya mgombea yeyote, chama chochote, Afisa wa Uchaguzi yeyote na hata kwa mwananchi yeyote anayekiuka Sheria za Nchi au Maadili ya Uchaguzi.
Aliongeza kuwa Sheria na Kanuni za Uchaguzi zimeweka mamlaka na taratibu za kushughulikia malalamiko ya ukiukwaji wa Sheria, taratibu na Maadili ya Uchaguzi.  
“Kwa kuzingatia ukweli huu, Tume inaviasa vyama vyote vya siasa na wafuasi wao kutopendelea utaratibu wa kutafuta ufumbuzi wa kiutawala kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika mambo au masuala ambayo Tume haina mamlaka nayo na ambayo utatuzi wake unahitaji kufuata taratibu za Kisheria na Kikanuni.” Alisema.
Alisema utaratibu huo umewekwa bayana kwenye kipengele cha 2.3(e) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 ambacho pamoja na mambo mengine kinasisitiza malalamiko yeyote yafikishwe kwenye mamlaka inayohusika kwa utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria.
“Tume ya Uchaguzi inashauri kwa mara nyingine kuwa ni vyema vyama vya siasa, kwa kadri inavyowezekana, vitumie utaratibu uliopo wa Kisheria na Kikanuni kuwasilisha malalamiko yanapojitokeza wakati wa Kampeni, kabla na baada ya kuhesabu  kura na baada ya matokeo ya kura kutangazwa.” alisisitiza Jaji Kaijage.
Naye Mkurugenzi wa Uchauzi Kailima Ramadhani alisema kuwa maandalizi ya uchaguzi mdogo katika majimbo matatu na kata sita yamekamilika kwa asilimia kubwa huku vifaa vyote vinavyohitajika kwa ajili ya uchaguzi huo vimeshasafirishwa kwenye halmashauri zote zinazoshiriki uchaguzi huo ikiwemo karatasi za kura.
Alisema wapiga kura 278,137 wanategemewa kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa Ubunge majimbo matatu na 324,435 katika uchaguzi mdogo wa Madiwani katika kata sita wakati katika uchaguzi mdogo wa Februari 17, 2018 wa majimbo mawili ya Siha na Kinondoni, wapiga kura 319,482 wanategemewa kupiga kura na 27,120 katika uchaguzi mdogo wa Madiwani katika Kata nne.
Katika mkutano huo ulioshirikisha Tume, viongozi wa vyama vya siasa, mwakilishi wa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mkuu wa Jeshi la Polisi na Serikali, viongozi wa vyama vya siasa waliwasilisha malalamiko yao na kupatiwa majibu kutoka Tume na Jeshi la Polisi.
Mkutano huo wa Tume na viongozi wa vyama vya siasa umejumuisha maandalizi ya uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Longido, Singida Kaskazini na Songea Mjini na Kata 6 unaotarajia kufanyika Januari 13, 2018 na ule wa majimbo 2 na kata 4 utakaofanyika tarehe 17 Februari mwaka 2017.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi baada ya kumalizika kwa mkutano wa Tume na viongozi wa vyama vya siasa kuelekea Uchaguzi Mdogo wa Januari 13, 2018.Katikati ni Mwakilishi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Stephen Kazidi.
 Mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kailima Ramdhani akifuarahia jambo na mmoja wa viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage akizungumza na waandishi wa habari nje ya mkutano wa Tume na viongozi wa vyama vya siasa.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja viongozi kutoka vyama vyama vya siasa 19 vilivyoshiriki mkutano huo.Kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mst. (Znz) Hamid Mahmoud Hamid na kushoto ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani na Mjumbe wa Tume Jaji Mst. Mary Longway (wa pili kushoto na viongozi wengine waalikwa katika mkutano huo. Picha na Hussein Makame-NEC

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA KATIKA ZIARA YA MKOA WA RUVUMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi katika Mradi wa Kituo cha kupoozea umeme, eneo la Unanga, katika Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Januari 7, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mradi wa Kituo cha kupoozea umeme, katika eneo la Unanga, Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, kushoto ni Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani. Januari 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe, wakati akizindua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tanesco Mkoa wa Ruvuma, lililopo katika Wilaya ya Songea Mjini, Mkoani Ruvuma. Januari 7, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na wananchi, baada ya akizindua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tanesco Mkoa wa Ruvuma, lililopo katika Wilaya ya Songea Mjini, Mkoani Ruvuma. Januari 7, 2018. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

MAGAZETI YA JUMATATU LEO JANUARY 8,2018

DC GAIRO AAMURU KUKAMATWA VIONGOZI WALIOKULA FEDHA ZA UJENZI WA SEKONDARI YA KATA IDIBO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe ameagiza kukamatwa kwa viongozi wote waliofuja shilingi milioni 32 za ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata ya Idibo. Kauli hiyo ameitoa leo wakati alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa shule hiyo lililokwenda sambamba na ugawaji wa mabati na vifaa mbali mbali kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Kituo cha Polisi Idibo. 
Mhe. Mchembe aliwaomba TAKUKURU kuwakamata viongozi wote wanaosimamia ujenzi wa shule ili waweze kuhojiwa matumizi ya pesa na wizi uliotokea tokea kuanza kwa ujenzi huo. 
"Nimepokea taarifa ya Kamati ya Ujenzi ambayo imebaini wizi wa shilingi milioni 12 na matumizi ya utata yenye thamani ya shilingi milioni 20, hivyo ninawaagiza TAKUKURU na OCD ndani ya siku saba kuwakamata wale wote wanaohusika na sheria ichukue mkondo wake," alisema Mhe. Mchembe. 
Aidha mpaka sasa japo kuna dosari Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata Idibo umemaliza madarasa 3, vyoo na jengo la utawala. Wakati huo huo Mhe. Mchembe alikabidhi msaada wa mabati 120 na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kupanua kituo cha Polisi Idibo kilichojengwa kwa nguvu za wananchi. 
Katika hafla hiyo, Mhe. Mchembe aliyepokelewa na mwenyeji wake OCD - Gairo, Mratibu Mwandamizi Jeshi la Polisi, Ramadhani Kitantu, alitoa pongezi kwa Diwani Kata ya Idibo Mhe. Rajabu Mguhi na viongozi wake wote na wananchi wa Idibo kwa michango yao hadi boma kukamilika. 
Mhe. Mchenbe aliwaomba wananchi washiriki kuchangia awamu ya pili ya umaliziaji bila kusahau nyumba za Polisi. Pia anakaribisha Wadau wengine wa maendeleo wenye Mapenzi mema na Gairo TUSHIRIKIANE. 
Katibu Tawala Wilaya Bw. Adam John wakati wa ziara hizo alisisitiza wananchi kushirikiana na Serikali ili kujiletea Maendeleo yao. Pale ambapo kuna matatizo atahakikisha anayashughulikia ipasavyo kwa mujibu wa Sheria, Taratibu na Kanuni (STK). 
Ndani ya mwaka mmoja tumefanikiwa kufungua Sekondari za Kata mbili ambazo ni Chagongwe na Chanjale. Kote huko watoto walikuwa wanatembea zaidi ya km 20 kwenda shule na maabara sita. Miradi yote ni nguvu za wananchi kwa zaidi ya asilimia 45 na fedha kutoka Serikali. 
Pongezi kwa Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwajali watoto wa masikini huku pembezoni vijijini kabisa ambapo nao wanajisikia vizuri na wanajenga Uzalendo wa kuipenda nchi yao tangu wadogo. 
Gairo ina kituo kimoja tu cha Polisi hivyo hiki kitakuwa cha pili. Kituo hiki kitahudumia Kata tano za Gairo na Kata jirani zaidi ya sita kutoka Wilaya ya Kilindi, Kiteto na Mvomero kwani kipo mpakani mwa Wilaya hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe (kushoto) akizungumza  na OCD - Gairo, Mrakibu Mwandamizi Jeshi la Polisi, Ramadhani Kitantu (kulia) wakati alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi Idibo, shule ya sekondari ya kata ya Idibo sambamba na ugawaji wa mabati na vifaa mbali mbali kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Kituo cha Polisi Idibo.
Ukaguzi wa Ujenzi shule ya Sekondari Kata ya Idibo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe (wa kwanza kulia) akabidhi msaada wa mabati 120 na vifaa mbalimbali kwa Jeshi la Polisi na uongozi wa kata ya Idibo kwa ajili ya kupaua kituo cha Polisi Idibo kilichojengwa kwa nguvu za wananchi.
Wananchi na Wazee Maarufu wakifuatilia mkutano na makabidhiano. 
Viewing all 110102 articles
Browse latest View live




Latest Images