Na Fredy Mgunda,Mufindi.
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini amewataka viongozi wa vijiji na kata kuwachukulia hatua za kisheria wazazi wote ambao hawataki kuwapele shule watoto wao wakifaulu mitihani ya shule ya msingi kwenda shule ya sekondari.
Akizungumza na blog hii mbunge Mahamuod Mgimwa alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo baadae.
“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa jimbo la Mufindi Kaskazini sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Mgimwa
Mgimwa alisema kuwa wazazi wa jimbo la Mufindi la Mufinda watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani pindi wamalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza maendeleo yao.
“Haiwezekani mwanafunzi amefaulu halafu mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi kukubali hata kidogo maana nimegundugua wazazi wengi hawapendi watoto wao waendelee kusoma badala yake wanataka wakafanye kazi za ndani narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa shule nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi” alisema Mgimwa.
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa akizungumza na viongozi wa kata ya Kibengu kuhusu maswala mbalimbali ya kimaendeleo sambamba na kutoa maagizo mbalimbali ambayo yatasaidia kuchochea maendeleo ya kata ya hiyo na jimbo hilo kwa ujumla
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa na viongozi wengine wakisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya kata ya Kibengu
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa akiangalia moja ya mradi wa ujenzi wa vyoo
Diwani wa kata ya Kibengu Zakayo Kilyenyi akiwa na viongozi wa kata ya hiyo mara baada ya kutoka kwenye kikao na mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini.