Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

TPA yanunua vifaa vya kisasa Bandari ya Mtwara

0
0
Na Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imenunua vitendea kazi vipya na vya kisasa kwa ajili ya bandari ya Mtwara ili kuongeza ufanisi.
Vifaa hivyo ambavyo tayari baadhi vimeshawasili bandarini hapo ni pamoja na mzani wa kisasa ‘Movable Weigh Bridge’ wenye uwezo wa kupima hadi tani 100 ambao tayari unatumika.
Vifaa vingine vilivyonunuliwa na vinavyotarajiwa kuwasili kuanzia mwezi Januari, 2018 ni pamoja na ‘Reach Stalker’ mbili mpya zenye uwezo wa kubeba tani 40 kwa wakati mmoja.
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko ameyasema hayo wakati wa majumuisho ya ziara za Kamati za Bodi za Wakurugenzi wa TPA zinazoshughulikia TEHAMA na Utelekezaji na ile ya Uwekezaji na Maendeleo ya Biashara.
Wakurugenzi wa Bodi za Kamati hizo ambazo ziliongozwa na Mwenyekiti, Dkt. Jabiri K. Bakari, ni pamoja na Jayne K. Nyimbo, Renatus Mkinga, Aziz M. Kilonge na Jaffer S. Machano.
Kamati hizo zilitembelea miradi mbalimbali iliyopo Bandari za Mtwara na Lindi na kutoa maelekezo kadhaa ambayo ni muhimu katika kuendeleza bandari hizo ili kuongeza huduma zake.
Akizungumzia vifaa vipya vilivyowasili na vinavyotarajiwa kuwasili hivi karibuni, Mhandisi Kakoko amesema ununuzi wa vifaa hivyo ni utekelezaji wa mipango ya kuifanya bandari hiyo kuwa ya kisasa zaidi.
“Ununuzi wa vifaa tunaofanya sasahivi utasaidia kuboresha na kuimarisha zaidi utendaji kazi wa bandari ya Mtwara na kuongeza ufanisi zaidi,” amesema Mhandisi Kakoko.
 Mkuu wa bandari ya Mtwara, Nelson Mlali (Kulia) akitoa maelezo kwa Wakurugenzi wa Bodi wa TPA wa Kamati za TEHAMA na Utekelezaji pamoja na ya Uwekezaji na Maendeleo ya Biashara mara baada ya wajumbe wa kamati hizo kufanya ziara ya kikazi banddari ya Mtwara hivi karibuni.
Mkuu wa bandari ya Mtwara, Nelson Mlali (Kulia) akitoa maelezo kwa Wakurugenzi wa Bodi wa TPA wa Kamati za TEHAMA na Utekelezaji pamoja na ya Uwekezaji na Maendeleo ya Biashara mara baada ya wajumbe wa kamati hizo kufanya ziara ya kikazi banddari ya Mtwara hivi karibuni.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AFUNGUZI JENGO LA MTAKIMWI MKUU WA SEREKALI MAZIZINI ZANZIBAR

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohammed Shein akikunjuwa kitambaa kuashiria Uzinduzi wa Jengo jipya la Mtakwimu Mkuu wa Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar Mazizini Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DSC_0133
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohammed Shein akifukia mche wa Mnazi baada ya kuupanda katika Uzinduzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mazizini Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DSC_0235
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohammed Shein akisisitiza jambo alipotoa hotuba ya Uzinduzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mazizini Wilaya ya Magharibi B Unguja  .Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar. kulia yake ni Makamo wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Idi
DSC_0156
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika Uzinduzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mazizini Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DSC_0177
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bi,Mayasa Mahfoudh Mwinyi akisoma Risala  katika Uzinduzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mazizini Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DSC_0186
Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia  Ms,Bella Bird akitoa maelezo mafupi katika Uzinduzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mazizini Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DSC_0213
Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt,Khalid Salum Mohammed akitoa maelezo kuhusiana na utekelezaji wa maazimio yaliotolewa wakati wasemina ya watendaji wakuu kuhusu umuhimu wa Takwimu  katika Uzinduzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mazizini Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar. .PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

DC MVOMERO ATOA SIKU NNE KWA WAFUGAJI KUONDOKA MAENEO YALIYOTENGWA KWA SHUGHULI ZA KILIMO

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh muhamed Utaly ametoa siku kumi na nne kwa wafugaji waliovamia maeneo yaliyotengwa kwaajili ya shughuli za kilimo katika kata ya Melela,kuondoka mara moja katika maeneo hayo na kupisha shughuli zilizo kusudiwa .

Tamko hilo la mkuu wa Wilaya linafuatia hivi karibuni baada ya ofisi yake kupokea barua ya malalamiko kutoka kwa wafugaji, wakiilalamikia serikali ya kijiji cha melela kuwa wamevamia katika eneo lao wanaloishi na sasa wanataka kuligawa kwa wakulima kwa shughuli za kilimo ,jambo ambalo lilimlazimu mkuu huyo wa Wilaya kwenda kukutana na pande hizo mbili ili kupata muafaka.

Awali akitoa maelezo kwa niaba ya serikali ya kijiji mwenyekiti wa kijiji hicho Said Membe amesema kuwa eneo hilo linalolalamikiwa na  wafugaji lilitengwa maalum  kwa shughuli za kilimo na kufuata taratibu zote za kisheria .

Bw membe amesema wao kama serikali ya kijiji wapo kwaajili ya kufuata na kusimamia taratibu za kisheria na kwakutambua hilo ofisi yake imeanzisha mchakato wa kukusanya maombi kutoka kwa wananchi wanaohitiji maeneo ya kulima na mchakato utakapo kamilika basi watayarudisha kwa wananchi wenyewe ilizoezi lakugawa mashamba hayo ufanyike kwa kufuata taratibu zote za kisheria.

Naye bwana wecha kwaniaba ya wafugaji waliopeleka malalamiko hayo kwa Mkuu wa Wilaya amethibitisha kuwa nikweli wamekuwa wakiishi katika maeneo hayo bila kuwa na utamburisho rasmi  wa kisheria unaowapa uhalali wa kumiliki maeneo hayo ukiacha mfugaji mmoja ambaye ndiye anayetambulika kisheria na serikali ya kijiji

TATIZO LA MAJI MKURANGA KUWA HISTORIA- NAIBU WAZIRI ULEGA

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema suala la maji Mkuranga ni tatizo la muda lakini sasa matumaini yameanza kuonekana baada ya  benki ya Dunia kuleta  mradi wa maji wa visima 29 utakaokuwa na thamani ya zaidi ya bilioni mbili.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwanambaya, amesema kuwa mradi wa maji utakuwa historia kutokana na hatua zinazochukuliwa na serikali. Amesema katika ziara zake amekuwa akikutana na changamoto za maji lakini hatua zimeanza kuchukuliwa kwa kiangazi cha mwaka huu maji yatakuwa tayari.

Katika Mkutano huyo amehidi kutoa bati 100 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili ya shule ya Msingi Mwanambaya.

Naibu Waziri huyo ameiomba kamati ya kijiji kukutana na mganga Mkuu ili waweze kuipandisha dispensari hiyo kwenda kituo cha afya.

Mbali na hilo wananchi wa kijiji cha Mwanambaya  wamemuomba mbunge Ulega kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo kulipwa stahiki zao za kupitiwa  na mradi wa mabomba ya gesi ya  Kilwa Energy.
Sehemu ya wananchi wa mwanambaya katika Mkutano. picha ,Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.


 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi  wa Kijiji cha  Mwanambaya wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani wakati wa ziara yake ndani ya Jimbo la Mkuranga.

DROO RAUNDI YA TATU KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM KUCHEZESHWA KESHO

0
0


Droo ya raundi ya tatu(3) ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) inachezeshwa kesho Januari 5, 2018 ikishirikisha timu 32.

Raundi hiyo ya Tatu itahusisha timu nne(4) za mabingwa wa mikoa timu tatu(3) za Ligi Daraja la Pili,timu Kumi na Mbili (12) za Ligi Daraja la Kwanza na timu 13 za Ligi Kuu.

Hatua hiyo ya raundi ya tatu inabakiza timu Kumi na Sita(16) zitakazopambana kwenye hatua inayofuata.

Timu zitakazochezeshwa kwenye Droo ya hapo kesho ambayo itarushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Azam ni pamoja na Buseresere ya Geita,Majimaji Rangers ya Lindi,Shupavu FC ya Morogoro na KariakooFC ya Lindi zote kutoka Ligi ya Mabingwa wa mikoa.

Nyingine zinazotoka Ligi Daraja la Pili ni Green Warriors ya Dar es Salaam,Ihefu FC ya Mbeya na Burkina FC ya Morogoro.

Zilizofanikiwa kuingia hatua hiyo kutoka Ligi Daraja la Kwanza ni Toto Africans ya Mwanza,KMC ya Dar es Salaam,Friends Rangers ya Dar es Salaam,Biashara ya Mara,Polisi Dar ya Dar es Salaam,Polisi Tanzania ya Kilimanjaro,,Rhino Rangers ya Tabora,JKT Oljoro ya Arusha,Pamba FC ya Mwanza na Dodoma FC ya Dodoma.

Timu za Ligi Kuu zilioingia hatua hiyo ya raundi ya tatu ni Azam FC,Yanga(Dar es Salaam),Mtibwa Sugar ya Morogoro,Mbao FC ya Mwanza,Majimaji ya Songea,Kagera Sugar ya Kagera,Mwadui,Stand United (Shinyanga),Ruvu Shooting ya Pwani,Njombe Mji ya Njombe,Singida United ya Singida,Ndanda ya Mtwara na Tanzania Prisons ya Mbeya.


korosho zikiandaliwa vizuri tayari kwa kuhifadhiwa kwenye la Mkuranga

0
0
Watalaam wa zao la korosho  wakiangalia ubora wa korosho  na kuziweka katika madaraja ili kuingia  katika ghala la Mkuranga baada ya kuchambuliwa na kuandaliwa.
 Akina mama wa Wilaya ya Mkuranga wakichambua na kuandaa  Korosho ili ziweze kuwa na ubora kwa ajili ya kwenda kuzihifadhi katika ghala la Mkuranga. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

KAMATI YA MASHINDANO TFF YAIPA USHIND PRISONS NA JKT RUVU KOMBE LA FA

0
0
Kikao cha kamati ya Mashindano kilichokutana Desemba 29, 2017 kwenye makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kujadili mchezo namba 31 na 32 uliohusisha timu za Abajalo FC dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya na ule kati ya Mvuvumwa na JKT Ruvu katika Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) iliyokuwa ifanyike Desemba 20, 2017 kwenye Uwanja wa Uhuru na Chamazi.


Kamati ilikaa na kupitia taarifa mbalimbali za michezo hiyo.

Kamati kupitia kanuni ya 24 kifungu cha (1) katika mchezo kati ya Abajalo FC na Tanzania Prisons imeipa ushindi timu ya Tanzania Prisons baada ya kubaini Abajalo kukiuka kanuni hiyo.

Kwenye mchezo mwingine kati ya Mvuvumwa na JKT Ruvu Kamati baada ya kupitia na kujiridhisha imeipa ushindi timu ya JKT Ruvu baada ya Mvuvumwa pia kukiuka kanuni ya 24 kifungu (1).

Kwa maamuzi hayo timu za Tanzania Prisons na JKT Ruvu zinafuzu kwenda kwenye hatua ya tatu(3) ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

ALIYEKUWA MPIGAPICHA TSN, ATHUMAN HAMISI MSINGI KUZIKWA KESHO

0
0
Mwili wa Mpendwa wetu Athumani Hamisi Msengi unatarajia kuzikwa hapo kesho Januari 5, 2018 baada ya Swala ya Ijumaa na Maziko yatafanyika katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Mipango ya Mazishi inafanyika Nyumbani kwa Marehemu Sinza Madukani  Mtaa wa Weruweru (Njia ya Namnani Hotel Nyumba na 26).

Marehemu Athumani Hamisi amefariki asubuhi ya leo Januari 4,2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikofikishwa kwa matibabu baada ya kuzidiwa ghafla usiku akiwa nyumbani kwake.

TUNATOA POLE KWA WOTE MLIOFIKWA NA MSIBA HUU.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa aliyekuwa mpigapicha wa magazeti Habari Leo, marehemu Athumani Hamisi nyumbani kwake Sinza jijini.
 Baadhi ya ndugu wakiwa msibani.
Waombolezaji.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARY 5, 2018

JK AMLILIA MAREHEMU ATHUMAN HAMISI,KUZIKWA LEO MAKABURI YA KISUTU

0
0
1
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Dkt . Ibrahim Msengi Ndugu wa Marehemu Athman Khamis Nyumbani kwake Sinza kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba, Marehemu amefariki ghafla usiku wa kuamkia jana kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua ghafla na kulazwa hospitalini hapo kwa matibabu.Marehemu Athuman Hamisi alikuwa mfanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali TSN,anatarajiwa kuzikwa leo makaburi ya Kisutu .
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali TSN Dkt. Jimmy Yonaz nyumbani kwa Marehemu Athuman Hamisi  Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba.
3
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi. Tuma Abdallah Naibu Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali TSN Nyumbani kwa Marehemu Athman Khamis Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba.
4
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na watoto wa Marehemu Athman Khamis Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba.
5
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na watoto wa Marehemu Athuman Hamisi, Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba.
6
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na na Dkt.. Jimmy Yonaz Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali TSN na ndugu wa marehemu Dkt Ibrahim Msengi Nyumbani kwa Marehemu Athumani Hamisi, Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba.
7
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Ankal  Issa Michuzi nyumbani kwa Marehemu Athuman Hamisi,Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba.
8
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na ndugu , na jamaa na marehemu wa Marehemu Athman Khamis Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba.
9
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiafamilia ndugu , na jamaa na marehemu wa Marehemu Athman Khamis Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba.

MAAMUZI YA KAMATI YA NIDHAMU YA TFF

0
0
Kamati ya nidhamu iliyokutana Januari 1, 2018 ilipitia ripoti mbalimbali za mchezo kati ya Kagera Sugar na Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Kaitaba Novemba 2, 2017 na ule kati ya Azam Fc na Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Chamazi Oktoba 27, 2017.


Kwenye mchezo kati ya Kagera Sugar na Tanzania Prisons,Meneja wa timu ya Tanzania Prisons Erasto Ntabahani alipelekwa kwenye kamati hiyo ya nidhamu kwa kosa la kumshambulia muamuzi wa akiba,kamati imejiridhisha kuwa Ntabahani alimshambulia kwa maneno muamuzi huyo wa akiba na hivyo imemfungia miezi miwili(2) na kulipa faini kwa mujibu wa kanuni ya 40(2) ya udhibiti wa viongozi.

Kamati pia ilipitia suala la golikipa wa Mbeya City Owen Chaima kudaiwa kumpiga mshambuliaji wa Azam FC Yahya Mohamed.

Chaima alikiri kumpiga Yahya na Kamati kupitia kanuni ya 35(7b) ya udhibiti wa wachezaji imemfungia kucheza mechi 4 na faini.

WAZIRI MPINA ATOZA FAINI YA MILIONI 180 VIWANDA VYA KUCHAKATA MINOFU YA SAMAKI

0
0

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewaamuru wamiliki wa viwanda vitano vya kuchakata minofu ya samaki vilivyoko jijini Mwanza kulipa faini ya shilingi milioni 180 ndani ya saa 24 baada ya kubainika kupokea na kuchakata samaki wasioruhusiwa kwa kukiuka Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009 sambamba na Sheria ya usimamizi wa Mazingira namba 20 ya mwaka 2004

Pia Waziri Mpina amechukizwa na kitendo cha viwanda hivyo kufadhili uvuvi haramu na kueleza kuwa ni bora kutokuwa na kiwanda hata kimoja cha samaki kuliko kuendelea kuwa na viwanda vinavyofadhili uvuvi haramu na kutishia kuvifunga viwanda vyote sambamba na kutaifisha samaki, magari na boti zinazobeba samaki wasioruhusiwa.

Waziri Mpina amesema hayo leo kwa nyakati tofauti wakati alipofanya ziara kutembelea viwanda vinavyochakata samaki jijini Mwanza ambapo pia amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Yohana Budeba kuwasimamisha kazi maofisa watatu wa Kitengo cha Udhibiti wa Usalama na Ubora wa Mazao ya Uvuvi Kituo cha Mwanza kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kulisababishia Taifa hasara kubwa.

Maofisa hao ambao Waziri Mpina ameagiza wasimamishwe kazi na kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ni pamoja na Philemon Mugabo,Dorina Mlenge na John Bosco Rubajuna


Meneja uchakataji wa Kiwanda cha kuchakata samaki Victoria cha jijini Mwanza, Endwin Okwong’o (aliyeshika kofia) akimuelezea Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani), namna ambavyo wanapokea samaki kutoka kwa mawakala na kuwachambua kabla ya hatua ya kuchakata kiwandani hapo kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina(mwenye kofia), akimpima urefu samaki aina ya Sangara kwenye rula maalum ili kubaini kama ana urefu unaotakiwa kisheria kwenye kiwanda cha Nile Perch Limited jijini Mwanza, kushoto Dkt. Yohana Budeba Katibu Mkuu Uvuvi na kulia ni Bwana Gabriel Mageni Afisa Mvuvi Mkuu. Samaki chini ya sentimita 50 na mwenye zaidi ya sentimita 85 hawaruhusiwi kisheria kuvuliwa.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akimbeba samaki aina ya sangara aliyevuliwa kinyume na taratibu alipokuwa katika ukaguzi wa mazao ya uvuvi katika Kiwanda cha Nature Fisheries Limited Jijini Mwanza, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Yohana Budeba na kulia ni Afisa Uvuvi Mkuu Bw. Boniface Shatila.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (Mwenye Kofia) akitoa tamko la Serikali la kuwataka wenye viwanda vya samaki kutofadhili uvuvi haramu alipotembelea katika gati la Kiwanda cha samaki cha Tanzania Fish Processing (TFP) jijini Mwanza leo, kulia ni Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba.

Samaki mzazi aina ya Sangara aliyevuliwa kinyume na taratibu(alikuwa na urefu wa sentimita 120), samaki ambaye akiachwa ziwani kwa muda wa miezi mitatu ana uwezo wa kuzaa samaki milioni tatu, na kuongeza idadi kubwa ya jamii hiyo ya samaki katika ziwa Victoria.

WAFANYAKAZI WAPYA WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) WAPIGWA MSASA

0
0
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kufanya kazi zao kwa kufuata maadili ya utumishi wa umma na kuepuka vitendo vya rushwa.

Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Prof. Mohamed Janabi, wakati alipokuwa akuzungumza na wafanyakazi wapya 57 wa kada mbalimbali walioajiriwa hivi karibuni.Alisema miongoni mwa wafanyakazi hao, wapo madaktari, maafisa uuguzi, wahasibu, maafisa Tehama, wahudumu wa afya, wataalam wa maabara na maafisa ustawi wa jamii.

“Mtumishi wa umma lazima ufanye kazi kwa kuzingatia maadili na sheria za kazi ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa ufanisi, weledi na kuzingatia maadili ya taaluma yako.“Humu ndani ya taasisi kazi yetu inahitaji nidhamu ya hali ya juu kwa sababu tukikosea hata kidogo maana yake tunapoteza maisha ya mtu.

“Ukipangiwa zamu zingatia, msipokee rushwa, kwani ni kitu hatari sana ukimuona mwenzio anajihusisha na vitendo hivyo hatua ya kwanza ni kumkemea na kumshauri kuacha mara moja,” amesisitiza.Amewataka wafanyakazi hao kuzingatia kuvaa mavazi yenye staha wakati wote hususan wale ambao watakuwa hawavai sare maalum za kazi.

“Hakikisheni mnawahi kazini, kama unaishi mbali jitahidi kuwahi mapema kutekeleza majukumu yenu,” amewasihi.Prof Janabi hakusita kuwaeleza wafanyakazi hao baadhi ya changamoto zinazoikabili taasisi hiyo ikiwamo ufinyu wa nafasi.“Ofisi tulizonazo ni chache, kwa kuanzia tutashirikiana hivyo hivyo hasa wale ambao si wataalamu wa afya,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu wa Taasisi hiyo, Ghati Chacha alisema kati ya wafanyakazi walioajiriwa 23 ni wanaume na 29 ni wanawake.“Wameajiriwa JKCI baada ya kupatiwa kibali na Serikali kulikuwa na nafasi 57 zilizojazwa ni 56 na hadi sasa walioripoti kazini ni 52, wanne wameomba udhuru kwani wana dharura na hadi kufikia wiki ijayo tunatarajia nao watakuwa wameripoti kazini,” amesema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza leo na wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa katika Taasisi hiyo kuhusu umuhimu kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma.
Baadhi ya Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na vitengo vya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi (hayupi pichani) wakati akinzungumza na wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa katika Taasisi hiyo.
Afisa Tawala wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joachim Asenga akiwaelekeza jinsi ya kujaza fomu watumishi wapya 57 wa Taasisi hiyo ambao wameajiriwa hivi karibuni.Picha na JKCI

HIFADHI YA TAIFA TARANGIRE MAAFURU NYUMBA YA TEMBO YAZIDI KUVUTIA WATALII

0
0

Wanyamapori aina Tembo wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Tarangire inayopatika kwenye mikoa ya Manyara na Arusha ni kivutio kikbwa kwa wageni wanaotembela hifadhi hiyo.

Wanyamapori aina Tembo wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Tarangire inayopatika kwenye mikoa ya Manyara na Arusha ni kivutio kikbwa kwa wageni wanaotembela hifadhi hiyo.
Miti aina ya Mibuyu inaonekana kwa wingi na inaongeza mvuto kwenye hifadhi ya Taifa Tarangire.
Pundamilia ni sehemu ya kivutio cha watalii wa ndani na nje ya nchi .
Msururu wa magari ya watalii ukisubiri utaratibu wa malipo kwa njia ya kadi kuanza safari ya kutembelea hifadhi hiyo
Watalii wakiwa ndani ya Hifadhi

IGP AKAGUA MIRADI KINONDONI

0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akikagua mradi wa maendeleo ya Jeshi hilo unaotekelezwa katika Wilaya ya Kipolisi ya Magomeni jijini Dar es salaam, mradi ambao unatarajiwa kuanza kutumika kwa ajili ya kutoa huduma za Kipolisi hivi karibuni. Picha na Jeshi la Polisi. 
 Wananchi wa Kigogo Mburahati jijini Dar es salaam, wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, ambaye alifika eneo hilo kwa ajili ya kukagua moja kati ya miradi ya Jeshi la Polisi, ambapo IGP Sirro, aliwataka wananchi hao kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kuwafichua wahalifu katika maeneo yao. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akimsikiliza OCD wa  Wilaya ya Kipolisi ya Magomeni, Salim Marcuse, wakati alipotembelea moja kati ya miradi ya maendeleo ya  Jeshi hilo inayotekelezwa katika mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni jijini Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi.

MBUNGE WA LUSHOTO AMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUSAIDIA SEKTA YA AFYA JIMBONI KWAKE

0
0


Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi uliofanyika Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola wilayani Lushoto ambapo pamoja na kusikiliza kero zao aliishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kuijali kata hiyo kwa kupeleka fedha milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Kisasa katika Kata ya Mlola ambapo kati ya hizo milioni 300 kwa ajili ya kununulia vifaa wakati kituo hicho kitakapomalika huku milioni 400 zikiwa tayari wameingiziwa tayari kwa ajili ya ujenzi huo 
Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akizungumza katika mkutano wa hadhara kushoto ni Diwani wa Kata ya Mlola.
Diwani wa Kata ya Mlola (CCM) akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia aliyekaa kulia. 
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mbunge wao 
Mkazi wa Kijiji hicho Kata ya Mlola wilayani Lushoto akimuuliza swali Mbunge huyo
Mkazi wa Kijiji hicho akimuuliza swali Mbunge wa Jimbo hilo .

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

RIDHIWANI AONESHA MAENEO YANAYOHITAJI UMEME CHALINZE

0
0
Na Said  Mwishehe, Blogu ya jamii
MBUNGE wa  Chalinze mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete amemuonesha Naibu wa  Waziri wa  Nishati, Subira Mgalau maeneo yenye mahitaji maalumu ya kupatiwa nishati ya umeme. 

Akizungumza na wananchi wa  Kata ya Talawanda akiwa ameongozana na Waziri wa  Nishati, Subira Mgalau, Ridhiwani ametumia nafasi hiyo kuomba umeme na hasa  katika  hospitali kwa lengo la kufanikisha upatikanaji wa huduma za afya hasa kwa akina mama wajazito na watoto. 

Pia amemsisitiza umeme uwekwe kwenye shule ili kuwapa nafasi wanafunzi wa Kata ya Talawanda na Chalinze kwa ujumla kujisomea wakati wowote. 

"Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishati,  moja ya changamoto iliyopo jimboni kwetu na hapa katika Kata ya Talawanda ni zahanati yetu kutokuwa na umeme, hivyo tunaomba mtusaidie na pia katika shule.
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu na mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete wakiwasalimia wananchi wa kata ya Talawanda.
 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete(kushoto) akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu walipokuwa Kata ya Talawanda jimboni Chalinze kwa lengo la kuzungumza na wananchi.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalau(wa pili kulia) akizungumza na mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete wakiwa katika Kata ya Talawanda.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DROO YA TATU YA KOMBE LA FA YACHEZWA, YANGA NA AZAM ZATUPWA UGENINI

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Droo ya tatu ya Kombe la Shirikisho Azam Sports HD imechezwa leo na timu 32 kupangwa.

 KMC vs Toto Africans
 Majimaji vs Ruvu Shooting
Njombe Mji vs Rhino Rangers
Kiluvya United vs JKT Oljoro
 Ndanda vs Biashara United
Pamba SC vs Stand United
Polisi Tanzania vs Friends Rangers
 JKT Tanzania SC vs Polisi Dar
Mwadui vs dodoma fc
Green worries vs singida inited
Prisons vs bukinafaso mbeya
Kariakoo Lindi vs mbao
Ihefu FC vs Yanga SC
Maji maji rangers vsmtibwa sugar
Kagera sugar vs buseresere
 Shupavu vs Azam fc

MWILI WA MAREHEMU ATHUMAN HAMISI MSENGI WAZIKWA LEO KISUTU DAR ES SALAAM

0
0
 Mwili wa  Athumani Hamisi Msengi kumaliza ukiwa nyumbani kwake mara baada kuswaliwa Sinza Madukani. 
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Dkt.Jim James Yonas akizungumza jambo mara baada ya mwili wa  Athumani Hamisi Msengi kumaliza kuswaliwa swala ya Ijumaa Nyumbani kwake Sinza Madukani leo jijini Dar Es Salaam.
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadj Mussa Salum akizungumza jambo nyumbani kwa marehemu leo jijini Dar es Salaam
Kaka mkubwa wa marehemu Dkt Ibrahim Msengi akizungumza jambo mara baada ya mwili wa mdogo wake Athumani Hamisi Msengi kumaliza kuswaliwa swala ya Ijumaa Nyumbani kwake Sinza Madukani leo jijini Dar Es Salaam.
Mwili wa  Athumani Hamisi Msengi kumaliza ukipandishwa kwenye gari kuelekea kwenye makaburi ya Kisutu mara baada ya kuswaliwa swala ya Ijumaa Nyumbani kwake Sinza Madukani leo jijini Dar Es Salaam.
 Kaburi la Athumani Hamisi Msengi likiombwa mara baada ya kuzikwa

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DAWASCO WAANZA UKARABATI WA BOMBA VINGUNGUTI

0
0
Siku moja baada ya ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuhakikisha mabomba ya barabara ya Buguruni kwa Mnyamani yanaanza kutengenezwa hatimaye Dawasco imechukua jukumu hilo. 

Kazi hiyo imeanza mapema Jana Jioni ikihusisha wataalamu waandamizi kutoka Dawasco kukagua na kuanza hatua za awali za ubadilishaji wa bomba kubwa lenye ukubwa wa inchi 10 na kuweka bomba jipya.
Hadi tunaenda mitamboni bado mafundi wa Dawasco walikuwa wakiendelea na kazi.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images