Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

VITUKO, VITIMBI VYATAWALA UCHAGUZI WA NAIBU MEYA DAR


BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 03.02.2018

IGP SIRRO AFANYA ZIARA BANDARI YA DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akiwa ameongozana na baadhi ya maofisa wa Jeshi hilo alipofanya ziara katika bandari ya Dar es salaam, leo kwa lengo la kukagua magari 119 ya Jeshi hilo ambayo yameshawasili bandarini hapo, magari hayo ni miongoni mwa magari 777 yaliyoagizwa na Jeshi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akikagua baadhi ya magari 119 ya Jeshi hilo ambayo yameshawasili bandari ya Dar es salaam, yakiwa ni miongoni mwa magari 777 yaliyoagizwa na Jeshi hilo kwa ajili ya shughuli mbalimbali. 
Picha na Jeshi la Polisi.

WANANCHI WAFURIKA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOANI RUVUMA

$
0
0

Mamia ya Wananchi wa Wilaya za mkoa wa Ruvuma wamejitokeza kwa wingi kwenye vituo vya Usajili zoezi la Vitambulisho vya Taifa huku baadhi wakiwataka viongozi kusimamia utekelezaji wa agizo la Serikali la usajili Vitambulisho vya Taifa kuwa ni bure.

Wito huo umetolewa na wananchi wa Wilaya ya Songea wakidai kutozwa kiasi cha shs.2000/ za picha za kubandika kwenye kwenye fomu za utambulisho za Serikali za Mitaa wanakoishi na kudai gharama hizo ni kubwa kulinganisha na hali halisi ya maisha.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Mtaa wa Makambi Bwana Anuari Methodi Nyoni ametolea ufafanuzi suala hilo na kueleza wananchi wanaoagizwa kuleta picha picha ndogo za passport size ni wale ambao wamekosa viambatisho muhimu vya kuwatambulisha na hivyo ili kujiridhisha kuwa mwananchi wanayemthibitisha kuwa ni mkazi wa eneo lao basi ni vema kuwa na picha yenye taswira yake ili kuepuka matumizi mabaya ya fomu za kuwatambulisha zinazotolewa na Serikali ya Mtaa.

Aidha amesisitiza Serikali yake ya Mtaa kusimamia na kutekeleza agizo la Serikali la kwamba zoezi la Vitambulisho vya Taifa ni bure na kusisitiza umuhimu wa wananchi kuelewa Serikali inaposema zoezi ni bure haina maana kwamba Serikali itafanya kila kitu; ikutolee copy viambatisho vyako au kukulipia gharama za picha hilo haliwezekani. Amesema wao kama wasimamizi wa zoezi hilo wanasisitiza mwananchi kufika kwenye kituo na picha yake au nakala ya viambatisho vyake na huduma nyingine zote mwananchi atazifuata mtaani zinazkotolewa.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Bi. Rose Joseph amesema Mamlaka ina mashine zake za kuwapiga picha wananchi na kwamba mwananchi anayefika kusajiliwa hapaswi kuja na picha ya passport size kama inavyoelezwa; ila changamoto kubwa ni kwa wale wananchi ambao hawana viambatisho vyovyote vya kuwatambulisha na wanahitaji kupata barua ya utambulisho wa Serikali za Mitaa wanakoishi. 
Wananchi wakazi wa Kata ya Ndilima Mtaa wa Makambi Ndilima Wilaya ya Songea, wakikagua fomu zao kabla ya kwenda kwenye maalumu cha uchukuaji taarifa kwa maana ya kupigwa picha, uchuaji alama za kibaiolojia na saini ya Kielekrtoniki. Waliopo pichani ni Bi. Hadija Yahaya (mwenye gauni la Pinki kushoto) na Bwana Hussein Nyoni (Mwenye kofia kichwani) wote wakazi wa Mtaa wa Makambi Songea. 
Hawa ni baadhi tu ya wakazi wa Kata ya Ndilima Wilaya ya Songea wakisubiri huduma ya Usajili Vitambulisho vya Taifa unaoendelea kwenye shule ya msingi ya Matogo na kuhusisha wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea. Kwa Wilaya ya Songea Kata zilizoanza zoezi ni Kata ya Ndilima na Seed-farm zoezi ambalo litafanyika wa siku saba tu kabla ya kuhamia Kata zingine za Wilaya hiyio.

Akionekana mwenye furaha ni Bi Haruna Thabiti Majwila wa Mtaa wa Makambi Ndilima mara baada ya kukamilisha hatua za usajili kwa maana kupigwa picha na kuchukuliwa alama za Kibaiolojia. Na hapa ya akiangalia muonekano wa Kitambulisho chake utakavyokua na kukagua picha yake kujiridhisha endapo picha yake imetoka vizuri. Kulia ni Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bwana Agaton Magnus Komba. 

WAZIRI MWIJAGE: NJIA NZURI YA KUFIKIA UCHUMI WA KATI NI UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema njia nzuri ya kufikia Uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025 ni kupitia Uchumi wa Viwanda jumuishi. 

Waziri Mwijage ameyasema hayo alipozungumza na wadau wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake Mkoani humo, ambapo alisisitiza juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda ulio imara, shindani na endelevu, utakayozingatia mambo muhimu matatu ambayo ni soko, malighafi na teknolojia.

Amesema lengo la Serikali ni kuhamasisha ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Jumuishi ambao unawahusisha watu wengi kupitia viwanda vidogo na vya kati,vitakavyotumia malighafi zitakozozalishwa hapa nchini vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini, ukiwepo mkoa wa Simiyu ambao umeonekana kufanya vizuri katika eneo hilo.

“Safari ya Simiyu imeanza vizuri na lengo la safari ni kuhamasisha Watanzania kujenga uchumi wa viwanda jumuishi, viwanda ambayo malighafi yake inazalishwa na wananchi wenyewe, vitatoa ajira kwa wananchi walio wengi, vitatumia malighafi asilia na kutoa mazao yenye matumizi makubwa” alisema Mwijage.

Waziri Mwijage amepongeza juhudi zinazofanywa na Mkoa wa Simiyu katika Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda kupitia Falsafa ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja” ambapo sasa umejipanga kuelekea kwenye “Kijiji Kimoja Bidhaa Moja”.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.Charles Mwijage akifungua Ofisi ya Muda ya Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) iliyoko Mtaa wa Malambo mjini Bariadi wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu. 

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe..Charles Mwijage akizungumza na wadau wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Mkoa wa Simiyu wakati wa Ziara yake Mkoani humo 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.Charles Mwijage akizungumza na wadau mara baada ya kutembelea eneo itakapojengwa Ofisi Mpya ya SIDO Isanga Mjini Bariadi, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu. 
Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu 

DKT. MWAKYEMBE AUNDA KAMATI YA NGUMI

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) leo tarehe 3 Januari, 2018 amekutana na wadau wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini. Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vya Mhe. Waziri na Wadau hao ili kutatua migogoro iliyodumu kwa muda mrefu katika mchezo huo wa masumbwi ya kulipwa, vikao hivyo vilianza mwishoni mwa mwaka 2017. 

Katika kikao kilichofanyika leo, Mhe. Waziri aliwaagiza wadau hao kufanya kazi kwa pamoja katika kuunda mfumo mpya utakaolinda maslahi ya mabondia na wahusika wengine wa mchezo wa ngumi za kulipwa na kuliletea Taifa letu heshima kwa kupitia mchezo huo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Ili kupiga hatua, Waziri Mwakyembe ameunda kamati ya watu kumi na moja (11) itakayokusanya maoni ya wadau na kupitia upya katiba ya kuunda Chombo kitakachosimamia mchezo wa ngumi za kulipwa hapa nchini. Kamati hiyo imeanza kufanya kazi leo  tarehe  03 Januari, 2018 na itakamilisha kazi yake tarehe 31 Januari, 2018. Kamati itasimamiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na itakuwa na wajumbe wafuatao:-:
  1. Ndg. Emmanueli Salehe         –     Mwenyekiti
  2. Ndg. Joe Enea                      –     Makamu Mwenyekiti
  3. Ndg. Yahya Pori                    –     Katibu
  4. Ndg. Habibu A. Nyogoli         –     Mjumbe
  5. Ndg. Shomari Kimbau           –     Mjumbe
  6. Ndg. Fike Wilson                  –     Mjumbe
  7. Ndg. Anthony Ruta               –     Mjumbe
  8. Dkt. Killaga M.Killaga           –     Mjumbe
  9. Ndg. Ally B. Champion         –     Mjumbe
  10. Ndg. Rashidi Matumla          –     Mjumbe
  11. Ndg. Karama Nyilawila         –    Mjumbe
Aidha, Waziri Mwakyembe ameeleza kwamba katika kipindi cha mpito shughuli za kutoa vibali kwa mapambano ya ndani na kwa mabondia wanaosafiri nje ya nchi zitaendelea kutekelezwa na BMT. “BMT endeleeni kusimamia vibali vya mapambano ya ndani na vibali vya safari za nje ya nchi za mabondia kwa kuzingatia uzalendo, weledi, kanuni na sheria za nchi bila kumwangalia mtu usoni wala kumuonea aya”, amesisitiza Waziri Mwakyembe.

Imetolewa na
Octavian F. Kimario
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

03/01/2018

Kampeni ya Uzalendo yapata Mapokeo Chanya

$
0
0
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe akiwapongeza wajumbe wa kamati ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo kwa ubunifu waliyofanya katika siku ya uzinduzi uliyofanywa hivi karibuni na Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, katika Kikao cha Tathimini  ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo  kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bi. Leah Kihimbi ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sanaa kutoka Wizara Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo Bi.Shani Kitogo ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo Bi.Leah Kihimbi (kulia) ambaye ni Mkurugenzi  Msaidizi Idara ya Sanaa  kutoka Wizara Habari Utamaduni Sanaa na Michezo akieleza mafanikio ya uzinduzi wa kampeni hiyo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) ikiwemo kupokea maombi kutoka taasisi mbalimbali kuomba wanakamati kwenda kutoa mafunzo kuhusu suala la uzalendo kwa watumishi wa ofisi zao,katika kikao cha tathimini ya uzinduzi wa Kampeni hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa Kamati ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo Bi.Joyce Fissoo ambaye ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini akitoa mapendekezo katika kikao cha tathimini ya uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuhusu Makala ya viongozi na wadau waliyozungumzia suala la uzalendo kwa taifa itakapo kamilika iweze kusambazwa nchini nzima katika Shule za Msingi na Sekondari kwa ajili ya kuwapa fursa watoto hao kujifunza kuhusu uzalendo.



Mjumbe wa Kamati ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo Bw.Mrisho Mpoto akitoa maoni ya mambo mbalimbali yanayoweza kufanikisha kampeni hiyo kuwa endelevu ikiwemo wajumbe kufanya tafiti kwa nchi zenye uzalendo kama China kwa lengo la kuhakikisha taifa linaelewa umuhimu wa uzalendo na manufaa yake katika kikao cha tathimini ya uzinduzi wa kampeni hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

TANZIA


AZAM NA JAMUHURI UWANJA WA AMAAN ZANZIBAR

$
0
0
KIPA wa Timu ya Jamuhiri Ali Khamis akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na Mshambuliaji wa Timu ya Azam Benard Arthur akifunga bao la kwanza kwa Timu yake katika dakika ya 26 ya mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar . Timu ya Azam imeshinda mchezo huo kwa bao 4. -0 dhidi ya Timu ya Jamuhuri katika michuano ya Kombe la Mapinduzi , doli la PIli la Timu ya Azam limefungwa na mshambuali Salmin Hoza katika dakika ya 48 ya mchezo huo kipindi cha pili na Bao la Tatu la Azam limefungwa na katika dakika ya 56 ya mchezo huo kupitiamchezaji wake Yahya Zayd.Timu ya Azam imefunga mchezo huo kwa kuandika bao la nne kupitia mshambuliaji wake Peter Paul katika dakika ya 79 ya mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa amaan Zanzibar.
WACHEZAJI wa Timu ya Azam wakishangilia bao lao la ushindi la nne lililofungwa na mshambuliaji wake Peter Paul katika kipindi cha pili cha mchezo huo.
BEKI wa Timu ya Jamuhuri Abdallah Juma akijaribu kumzuiya mshambuliaji wa Timu ya Azam wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Azam imeshinda bao 4 -0.
MSHAMBULIAJI wa Timu ya Azam Bruce Kangwa akiruka kiunzi cha Beki wa Timu ya Jamuhuri Abdullatif Omar, wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya Azam. imeshinda bao 4 -0.
KIPA wa Timu ya Jamuhuri Ali Khamis akidaka mpira huku mshambuliaji wa Timu ya Azam Benard Arthur akiwa tayari kutowa mashambulizi wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Azam imeshinda bao 4 -0.
BEKI wa Timu ya Jamuhuri Yussuf Makame akiokoa mpira golini kwao huku mshambuliaji wa Timu ya Azam Bruce Kangwa akijiandaa kuchukua mpira huo, wakati wa michuano ya Kombe la Mapinduzi mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Azam imeshinda bao 4 -0/uul wa tayari kul .(Picha na Othman Maulid)

MASAUNI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA JAPAN, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimfafanulia jambo Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japan. Katikati ni Msaidizi wa Balozi huyo, Takashi Ban.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida wakati Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japan. Katikati ni Msaidizi wa Balozi huyo, Takashi Ban. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

TAARIFA YA MATUKIO MAKUBWA NA MADOGO YA JINAI KATIKA MKOA WA MBEYA

$
0
0



 Ifuatayo ni taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kipindi cha Januari hadi Disemba, 2017. Taarifa hii inaonesha matukio makubwa na madogo ya uhalifu, matukio ya usalama barabarani, matukio yaliyovuta hisia kwa jamii,  hali ya ulinzi na usalama kipindi cha sikukuu ya Kristmasi na mwaka mpya 2018, mpango mkakati wa Jeshi la Polisi Mbeya na mafanikio yaliyopatikana kutokana na operesheni, misako na doria.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu kwa mwaka huu 2017.
  1. MATUKIO MAKUBWA NA MADOGO YA JINAI.
Jumla ya makosa ya jinai 26,009 yaliripotiwa kutokea mkoa wa Mbeya kwa kipindi cha mwaka 2017 ikilinganishwa na matukio 32,943 yaliyoripotiwa kipindi kama hicho  Mwaka 2016. [-21].

Makosa makubwa yaliyoripotiwa mwaka 2017 yalikuwa ni 2,234 ikilinganishwa na matukio 2,071  yaliyoripotiwa mwaka 2016. [+8] Makosa madogo 23,775 yaliripotiwa  mwaka 2017,  ikilinganishwa na makosa 30,872 yaliyoripotiwa mwaka 2016. [-23].

Aidha jumla ya makosa 734 yaliripotiwa mwaka 2017 kutokana na jitihada za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine kupitia misako, doria na operesheni mbalimbali ikilinganishwa na matukio 565 yaliyoripotiwa mwaka 2016. [+30].
MOHAMMED R. MPINGA – DCP]
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KIPINDI CHA MWAKA 2017

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, DCP Mohamed Mpinga.

KIPINDI MAALUM.MHE.RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA MAGAVANA WA BOT IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JANUARI 3,2018.

TRA YAJIZATITI KUONGEZA IDADI YA WALIPAKODI

$
0
0



Na: Veronica Kazimoto, 04 Januari, 2018, 
Dar es Salaam. 

Mwaka huu wa fedha wa 2017/18, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imedhamiria kuongeza idadi ya walipakodi kwa ajili ya kuisaidia nchi yetu kupunguza kutegemea misaada kutoka kwa wahisani. 

Lengo kuu la kuongeza walipakodi ni kupanua wigo na kuongeza makusanyo ambayo hutumika katika kuleta maendeleo na kujenga uchumi wa nchi. 

TRA ina mikakati mbalimbali ambayo imechukuliwa na inaendelea kutekelezwa ili kuhakikisha kuwa, walipakodi wanaongezeka na hatimaye kuongeza mapato ya Serikali. 

Mikakati hiyo ni pamoja na kusajili walipakodi ambapo Mamlaka imezindua kampeni ya usajili wa walipakodi nchi nzima ili kuhakikisha kwamba kila mfanyabiashara anasajiliwa na kupata Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) kwa urahisi na haraka. 

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Kamishna wa Kodi za Ndani Elijah Mwandumbya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania alisema, usajili wa walipakodi ni chanzo cha kuongeza idadi ya walipakodi na mapato kwa ujumla. 

"Moja ya majukumu ya msingi ya TRA ni Usajili wa Walipakodi ambao huongeza idadi ya walipakodi, wigo wa ulipaji kodi, makusanyo pamoja na kutoa taarifa sahihi za walipakodi wanaostahili kukadiriwa na kutozwa kodi ili kuchangia Pato la Taifa", Alisema Mwandumbya. 

Mwandumbya alisisitiza kuwa, walipakodi wadogo wanaostahili kulipa kodi kwa njia ya makadirio, watalipa robo ya kwanza ndani ya siku tisini (90) kuanzia waliposajiliwa tofauti na utaratibu uliokuwepo kwa kulipa kodi hiyo hata kabla mfanyabishara hajaanza kufanya biashara husika. 

"Wananchi wanaostahili kusajiliwa kama walipakodi ni watu wote wanaotarajia kuanzisha biashara, kumiliki vyombo vya usafiri kama vile gari na pikipiki, wanaostahili kulipa kodi ya majengo, wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya nchi na wanaotarajia kupata leseni za udereva", alifafanua Mwandumbya. 

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI, WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UGANDA SAM KUTESA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjumbe maalum wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mjumbe maalum wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ujumbe Maalum uliotoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni na kuwasilishwa kwake na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiufungua na kuusoma Ujumbe huo maalum uliotoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni na kuwasilishwa kwake na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mjumbe maalum wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mjumbe maalum wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje kwa upande wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI RUVUMA KWA ZIARA.

$
0
0
Waziri mkuu Kassim Kajaliwa amewasili mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku sita ambapo katika ziara hii waziri mkuu atatembelea halimashauri ya MBINGA,na NYASA na kuhitimisha katika Manispaa ya SONGEA ,nakuzungumza na wananchi katika uwanja wa majimaji,huku miradi mbalimbali anatarajia kutembelea ikiwemo kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la TANESCO.

WAZIRI MWAKYEMBE AUNDA KAMATI YA KUPITIA KATIBA YA MCHEZO WA NGUMI.

$
0
0
Na Shamimu Nyaki-WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ameunda kamati ya watu kumi na moja watakaopitia Katiba ya kusimamia mchezo wa ngumi  za kulipwa hapa nchini pamoja na kukusanya maoni  namna bora ya kuendesha mchezo huo itakayoanza kazi  kuanzia Januari 03 hadi 31 ambapo  itakuwa chini ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) .

 Akizungumza na wadau wa mchezo huo Jijini Dar es Salaam Mhe.Waziri ameiagiza Kamati hiyo kufanya kazi kwa pamoja katika kuunda mfumo mpya utakaolinda maslahi ya mabondia na wahusika wote wa mchezo huo ili kuleta heshima ya mchezo huo hapa nchini.

“Naomba mshirikiane katika kazi hii vunjeni makundi yenu ili mfanye kazi kwa maslahi ya Taifa na wanamasumbwi wetu,mkifanya hivyo tutaleta hamasa kubwa kwa watu wengi kujiunga na mchezo huu ambao unaleta ajira kwa vijana wetu”.Alisema Mhe.Waziri Mwakyembe.

 Kamati hiyo itaongozwa na mwenyekiti Emmanueli Salehe ambaye ni mdau mkubwa wa ngumi hapa nchini,akisaidiwa na makamu Mwenyekiti Joe Enea ambaye ni Mwalimu wa ngumi pamoja na katibu Bw.Yahya Pori ambae pia ni mdau wa mchezo huo.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza leo Jijini Dar es Salaam na Wadau wa mchezo wa ngumi hapa nchini ambapo ameunda Kamati ya Watu kumi na moja watakaoandaa Katiba ya mchezo huo ndani ya mwezi huu. 
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Bw. Yusuph Singo(aliyesimama) akizungumza leo Jijini Dar es Salaam na Wadau wa mchezo wa ngumi hapa nchini  kabla ya Mhe Waziri Mwakyembe wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kuuunda Kamati ya Watu kumi na moja watakaoandaa Katiba ya mchezo huo ndani ya mwezi huu.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamedi Kiganja akitoa muongozo wa kikao  baina ya Mhe.Waziri  Harrison Mwakyembe (aliyekaa katikati) na wadau wa ngumi nchini leo Jijini Dar es Salaam.
 Mwanamasumbwi wa zamani Bw.Yassin Ustadhi akichangia mawazo wakati wa kikao cha Mhe. Waziri Mwakyembe wa Wizara ya Habari  Utamaduni Sanaa na Michezo na wadau wa mchezo wa ngumi leo Jijini Dar es Salaam.

WANANCHI WILAYA YA CHEMBA WAHAMASISHWA KUTUMIA FURSA YA KUJIPATIA KIPATO KWA KUTUMIA MIFUGO WALIYONAYO

$
0
0

Na Shani Amanzi,

Wananchi wa Wilaya ya Chemba wamehamasishwa kutumia fursa ya mifugo waliyonayo katika kuwapatia kipato na siyo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani pekee kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na wingi wa mahitaji ya kifedha kwa ajili ya shughuli zao za kimaendeleo.

Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Simon Langoi aliyazungumza hayo mapema leo 04/1/2018 alipokuwa ofisini kwake Halmashauri ya Wilaya ya Chemba na kueleza changamoto waliyokuwa nayo ni upungufu wa rasilimali watu na upatikanaji hafifu wa chanjo mbalimbali za mifugo(Kichaa cha mbwa,CBPP,CCPP n.k )

Bw. Simon alisema “kumekuwepo na mwitikio mdogo wa Wafugaji katika uchanjaji wa Mifugo yao hasa Mbwa (kichaa cha Mbwa) na Kuku dhidi ya Kideri ,Ukosefu wa Malisho na Maji katika maeneo mbalimbali”.

“Lakini katika maboresho ya mikakati endelevu ya Idara ya Mifugo na Uvuvi kwa Wananchi tumepiga hatua kwa kukinga mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali kama Kichaa cha Mbwa (Rabies) na Kideri kwa Kuku (Newscastle desease) kwa kuwachanja ili kupunguza vifo toka 20% mpaka 10% , kutibu Mifugo na kutoa tiba kwa Mifugo dhidi ya Magonjwa mbalimbali kama FMD, Minyoo na Magonjwa ya Ngozi”.

Kumekuwepo na migogoro baina ya Wakulima na Wafugaji juu ya matumizi bora ya ardhi hasa maeneo ya malisho na kilimo. Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kwa kushirikiana na wataalam wa Wizara ya Mifugo,Viongozi wa Serikali za mitaa pamoja na wananchi, imekuwa katika kufanya maamuzi ya pamoja katika kutenga maeneo ya malisho ili kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji.

Wito kwa wafugaji wa Wilaya ya Chemba ni kuhakikisha wanajitokeza kupiga chapa kwa maendeleo ya sekta na pia wanafuga mifugo michache yenye tija na inayoendana na rasilimali zilizopo.

Zoezi la Upigaji Chapa ni endelevu na tayari kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba tumefanya zoezi kwa zaidi ya 103% ya lengo, kuelimisha wafugaji wa mbuzi wa maziwa katika vijiji vya Mondo ,Hamai na Songolo ili kuongeza kipato chao na kuboresha lishe zao huku mbinu shirikishi (PPP) ikitumika kati ya Halmashauri na Kanisa la KKKT- Arusha kwenye mradi wa Mbuzi wa Maziwa.

Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Simon Langoi akizungumza mapema leo Ofisi kwake,kwa lengo la kuwahamasisha Wananchi wa Wilaya ya Chemba kutumia fursa ya kujipatia kipato kwa kutumia mifugo waliyonayo,mbali ya fursa zilizopo kwa Wananchi hao pia alibanisha baadhi ya changamoto zilizopo ndani ya Idara yake kwa mwaka jana ( 2017)  kuwa ni upungufu wa rasilimali watu pamoja upatikanaji hafifu wa chanjo mbalimbali za mifugo (Kichaa cha mbwa,CBPP,CCPP n.k ) .

WAZIRI MPANGO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA GAVANA MTEULE WA BoT

$
0
0
 Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, akisaini kitabu cha wageni alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwa katika mazungumzo na Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

BOT YAPIGA STOP BENKI TANO KUJISHUGHULISHA NA MASUALA YA KIBENKI

$
0
0
Na: Frank Shija - MAELEZO
Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezifutia leseni za uendeshaji wa shughuli za kibenki Benki tano ambazo zimeshindwa kukidhi matakwa ya sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.
Akizungumza kuhusu hatua hiyo Gavana wa Benki Kuu anayemaliza muda wake amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa kufuatia benki hizo kushindwa kutekeleza matakwa ya kisheria yaliyozitaka benki zote za kijamii kuongeza kiwango hicho cha mtaji ili ziweze kujiimarisha licha ya kupewa muda wa kipindi cha miaka mitano ulifikiwa tamati tarehe 31 Juni 2017.
“Maamuzi haya tunayafanya baada ya Benki zote nchini kupewa muda wa miaka mitano na nusu yakuweza kukidhi matakwa ya sheria, lakini mpaka ilipofika tarehe 31 Desemba 2017 jumla ya benki Nane zilishindwa kuongeza mtaji uliohitajika kati ya hizo Benki  Tano zilishindwa kuwasilisha mpango kazi wa kuonyesha namna zitakavyo kuwa endelevu,” alisema Profesa Ndulu.
Profesa Ndulu alizitaja Benki hizo kuwa ni pamoja na Convenant Bank for Women (T) Limited, Efatha Bank Ltd, Njombe Community Bank Ltd, Kagera Famers’ Cooperative Bank Ltd na Meru Community Bank Ltd.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) anayemaliza muda wake Profesa Beno Ndulu akisisitiza jambo alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu kuzifutia leseni ya uendeshaji wa shughuli za kibenki baadhi ya benki hapa nchini  katika mkutano uliofanyika BoT Jijini Dar es Salaam leo.  Takribani benki tano zimefutiwa leseni zao na nyingine tatu zimeongezewa muda ili kukidhi vigezo. Katikati ni Gavana Mteule wa BoT Profesa. Florens Luoga na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Amana Richard Malisa.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano baina yao na  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzani (BoT) anayemaliza muda wake Profesa Beno Ndulu akiwa ameambatana na Gavana mteule wa Benki hiyo Profesa Florens Luoga leo jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) anayemaliza muda wake Profesa Beno Ndulu akipeana mkono wa kwaheri na Gavana mteule wa Benki hiyo Profesa Florens Luoga. (Picha na Frank Shija – MAELEZO)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>