Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

WIZARA YA ELIMU YATOA VITABU 16985 KWA SHULE ZA SEKONDARI SIMIYU

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akikabidhi vitabu vya matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari (baseline course), kwa Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Mwl. Esthom Makyara vilivyotolewa na wadau wa Elimu, wakati wa zoezi la ugawaji wa vitabu hivyo lililofanyika kimkoa Mjini Bariadi.

Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu

Wizara ya Elimu pamoja na wadau wengine wa Elimu wametoa vitabu 16,985 kwa shule za Sekondari za Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya  matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza na elimu ya sekondari (baseline course).

Akikabidhi vitabu hivyo kwa Maafisa Elimu wa Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka amesema vitabu hivyo ni msaada mkubwa kwa Mkoa huo, vikitumiwa vizuri na walimu wenye nia ya kufanya mapinduzi ya elimu na kuwasaidia wanafunzi kujua maana halisi ya vitabu hivyo, vitasaidia  Mkoa wa Simiyu kufikia malengo ya kiushindani katika Elimu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Maafisa Elimu Sekondari na baaadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi(hawapo pichani), kabla ya kukabidhi vitabu vya matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari (baseline course), kwa maafisa elimu wilaya vilivyotolewa na wadau mbaimbali wa Elimu.

Ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata vitabu pamoja na mahitaji mengine ikiwa ni pamoja na madawati, walimu, vyumba vya madarasa vinavyotolesheleza hivyo akasisitiza vitabu hivyo vikatumike kwa kusoma ili viwasaidie. “Vitabu hivi mtakapogawiwa mkavitumie kwa ajili ya kusoma visiwe mapambo na kama mwanafunzi hujui uliza, jibidiishe kujua kitabu hicho kinahusu nini na kama hujaelewa muulize mwalimu ili kesho kwenye mtihani ufaulu kama wenzako wananvyofaulu” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amewataka Maafisa Elimu mkoani humo kuzungumza na walimu kabla ya kugawa vitabu hivyo ili vitakapogawiwa katika shule vigawiwe katika utaratibu mzuri utakowawezesha walimu kuwasadia wanafunzi kuvitumia kwa manufaa. Akitoa taarifa juu mapokezi ya vikao hivyo Katibu Tawala Mkoa amesema Mkoa huo umepokea jumla ya vitabu 16,000 kwa ajili ya wanafunzi na vitabu 985 kwa ajili walimu(kiongozi cha mwalimu).
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akikabidhi vitabu vya matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari (baseline course), kwa Afisa Elimu (Sekondari) wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mwl. Jumanne Yasini vilivyotolewa na wadau wa Elimu, wakati wa zoezi la ugawaji wa vitabu hivyo lililofanyika kimkoa Mjini Bariadi.

Akizungumza kwa niaba ya Maafisa Elimu Sekondari mkoani humo,  Afisa Elimu Sekondari wa Halmahauri ya Mji Bariadi Mwl. Esthom Makyara amesema vitabu hivyo ni msingi mzuri kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza na Maafisa Elimu hao wanapaswa  kuwaelekezaWakuu wa shule kutofungia vitabu hivyo  stoo badala yake wanafunzi wapewe ili wavisome.

Naye Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Ndg.Charles Maganga amesema Maafisa Elimu Sekondari wahakikishe vitabu hivyo vinagawiwa kwa wakuu wa shule kabla ya shule kufunguliwa Januari 08, 2018, ili wanafunzi wa kidato cha kwanza wanapoanza masomo wavikute shuleni. Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Bariadi walioshuhudia zoezi la ugawaji wa vitabu hivyo kimkoa wamesema, vitabu hivyo vitawasaidia wenzao wa kidato cha kwanza kujenga msingi  mzuri wa maarifa ya jumla na lugha ya Kiingereza.

Vitabu hivi vimetolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Msaada wa Watu wa Marekani(UKAID) kupitia Mpango wa Taifa wa Kuinua Ubora wa Elimu hapa nchini EQUIP-T.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akikabidhi vitabu vya matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari (baseline course), kwa Afisa Elimu (Sekondari) wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Mwl. Joseph Mashauri vilivyotolewa na wadau wa Elimu, wakati wa zoezi la ugawaji wa vitabu hivyo lililofanyika kimkoa Mjini Bariadi.

TAARIFA: UKAGUZI WA KINGA NA TAHADHARI DHIDI YA MOTO

$
0
0
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeundwa na linatekeleza majukumu yake chini ya Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji namba 14 ya mwaka 2007 (Fire and Rescue Force Act No. 14 of 2007). Majukumu makubwa ya Jeshi hili ni kuokoa Maisha na Mali katika majanga yatokanayo na moto, mafuriko, tetemeko la ardhi, ajali za barabarani pamoja na majanga mengine.

Sambamba na majukumu hayo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linafanya ukaguzi kwenye vyombo vya usafiri na usafirishaji, na kutoa ushauri uwekaji wa vifaa vya kinga na tahadhari. Ukaguzi huu unafanyika kwa mujibu wa sheria namba 14 ya mwaka 2007 ikisomwa pamoja na kanuni ya Vyeti na Usalama wa moto Mwaka 2008 na marekebisho ya mwaka 2014 (Fire and Rescue Force Safety Inspections and Certificates Regulations of 2008 GN.106 and its Amendment GN 63 of 2014.)

Pamoja na kanuni ya tahadhari dhidi ya moto kwenye majengo ya mwaka 2015 (Fire and Rescue Force Fire Safety Precaution in Building Regulations of 2015 GN 516.) Kwa kuzingatia majukumu hayo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linajulisha umma kuwa, halifanyi biashara ya kuuza vifaa vya kuzimia moto wala kuvifanyia matengenezo (service) vifaa hivyo pamoja na mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto. Bali Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linasimamia na kuhakiki ufungwaji wa vifaa hivyo.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatoa rai kwa wamiliki wa majengo na vyombo vya usafiri na usafirishaji, wafanyabiashara na wananchi wote kuhakikisha wananunua au kufanyia matengenezo (service) vifaa na mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto kwa Mawakala waliosajiliwa kuuza vifaa vya Zimamoto (Fire Dealers) kwa mujibu wa sheria ya Jeshi.

Imetolewa na;
Ofisi ya Habari na Elimu kwa Umma
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
03 Januari, 2018

MAPINDUZI CUP, FULL HIGHLIGHTS: YANGA 2-1 MLANDEGE"

Azam TV - MAPINDUZI CUP, FULL HIGHLIGHTS: SIMBA SC 1-1 MWENGE SC

MKAZI MIWNGINE WA TEMEKE MIKOROSHINI AIBUKA NA KITITA CHA MILIONI 50 ZA TATUMZUKA.

$
0
0
  Katibu Tawala wilaya ya Temeke, Ndugu Hashim Komba akikabdhi  mfano wa hundi kwa mshindi wa mchezo wa bahati nasibu wa Tatumzuka  Enirisha Kilango mapema leo kwenye ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Temeke.Enirisha Kilango ambaye ni Mkazi wa Temeke Mikoroshini anaejishughulisha na biashara zake ndogo ndogo alijishindia milioni 50 mwishoni mwa wiki
Enirisha Kilango ambaye ni Mkazi wa Temeke Mikoroshini anaejishughulisha na biashara zake ndogo ndogo akizungumza mapema leo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) ndani ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke,kufuatia ushindi wake wa kujinyakulia milioni 50 mwishoni mwa wiki katika mchezo huo wa kubahatisha.
 Katibu Tawala wilaya ya Temeke, Ndugu Hashim Komba akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Temeke, mbele ya Waandishi wa habari  (hawapo pichani) mapema leo,kabla ya kukabidhi mfano wa hundi kwa mshindi wa mchezo wa bahati nasibu wa Tatumzuka kwa mshinidi aliyejinyakulia Enirisha Kilango aliyejishindia milioni 50 mwishoni mwa wiki .

Ndugu Komba amewashukuru Tatumzuka kwa kuendelea kuwawezesha wananchi wa wilaya hiyo ya Temeke kupitia mchezo huo wa bahati nasibu,kwa kumpata mshindi mwingine ndani ya wilaya hiyo kwa mara nyingine tena,Komba amewasisitizia wananchi wake kuendelea kucheza zaidi na zaidi kwani mchezo ambao upo kisheria na hauna makando kando yoyote,ukishinda umeshinda kweli na fedha zako unakabidhiwa.

Mh Komba aliongeza kuwa kama Tatumzuka itawapatia shilingi Milioni Tano ambayo  imepatikana mara baada ya mshindi huyo kupatikana,basi watazitumia fedha hizo kuimarisha suala la ulinzi na usalama, tutakwenda kujenga kituo cha polisi na kuzitumia fedha hizo kununua mabati ili kukamilisha ujenzi wa vituo hivyo.

KUMBUKUMBU

CHOMBO KIMEKATA KATIKATI YA SAFARI

$
0
0
 Dereva wa chombo hicho akitafakari namna ya kufanya, baada ya kukata kiwese akiwa njiani kupeleka ng'ombe kwa Bosi wake.

HESLB kuanza kuwasaka wadaiwa sugu 119,497 jumatatu ijayo

$
0
0
*  Wanadaiwa Tshs 285 bilioni
*  Ukaguzi kwa waajiri pia kufanyika

Na Mwandishi Wetu
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wiki ijayo (Jumatatu, Januari 8, 2018) inatarajia kuanza kuwasaka jumla ya wanufaika 119,497 nchini kote ambao wamekiuka sheria iliyoanzisha Bodi hiyo kwa kutoanza kurejesha mikopo yenye thamani ya TZS 285 bilioni waliyokopeshwa tangu mwaka 1994/1995 na mikopo yao imeiva lakini hawajaanza kurejesha.

Aidha, Bodi ya Mikopo inatarajia kuanza kufanya ukaguzi kwa waajiri mbalimbali nchini kote ili kubaini kama katika orodha za waajiriwa wao (payrolls) kuna wanufaika wa mikopo ambao hawajaanza kurejesha.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru (pichani) amesema leo (Jumatano, Januari 3, 2018) jijini Dar es Salaam kuwa msako huo utafanywa kwa miezi mitatu kuanzia wiki ijayo (Jumatatu, Januari 8, 2018).

Bw. Badru ametoa kauli hiyo wakati akitoa tathmini ya utekelezaji wa majukumu ya Bodi ya Mikopo kwa nusu ya mwaka wa fedha wa 2017/2018 uliomalizika Desemba 31, 2017. Katika tathmini hiyo, Bw. Badru alizungumzia mafanikio, changamoto na mipango ya kuboresha ufanisi katika utoaji wa mikopo ya elimu ya juu na ukusanyaji wa mikopo iliyoiva.

Maafisa wa Bodi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Serikali wamejipanga katika kutekeleza hili ili kuongeza makusanyo ya mwezi kutoka wastani wa TZS 13 bilioni hivi sasa hadi kufikia TZS 17 bilioni mwezi Juni, 2018.

Orodha kamili ya waajiri na wanufaika wa mikopo ambao wanakiuka Sheria ya Bodi ya Mikopo (SURA 178) kwa kutowasilisha makato au kurejesha mikopo ya elimu ya juu inapatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz) kuanzia leo (Jumatano, Januari 3, 2018).
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Abdul-Razaq Badru akiongea na wanahabari leo (Jumatano, Jan. 3, 2018) jijini Dar es Salaam ambapo alielezea utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake katika nusu ya mwaka 2017/2018 na kuanza kwa kampeni ya kuwasaka wanufaika sugu wa mikopo 119,497 ambao hawajaanza kurejesha. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Upangaji Mikopo Dkt. Veronika Nyahende na kushoto ni PHIDELIS Joseph, Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo (Picha na Happiness Kihwele- HESLB).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU WAZIRI MGALU AWATOA HOFU YA BEI YA UMEME WANANCHI WA KIWANGWA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza katika Mkutano na wananchi wa Kata ya Kiwangwa kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu kuzungumza na Wananchi wa kata hiyo, kuhusu mipango ya kupeleka Nishati ya Umeme Vijijini. 
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alifafanua juu ya Mabadiliko ya bei za umeme kufuatia taarifa kuwa bei zimebadilika toka Elfu 27 hadi Shilingi 180,000. alisema kuwa hakuna mabadiliko katika bei, hivyo wananchi wa kata hiyo wasiwe na wasiwasi na hakuna kitongoji kitakachoachwa kupatiwa umeme hasa maeneo yenye mahitaji maalum kama Hospitali, shule na kwenye shughuli za kijamii kama ofisi za kuhudumia wananchi.
Sehemu ya Wananchi wa moja ya vitongoji vya Kata ya Kiwangwa, wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete.

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MSIBA WA MKE WA KANGI LUGOLA

$
0
0
​Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 3, Januari, 2018 amehani msiba wa Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola ambaye ni Mke wa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola alipofika kutoa pole ya msiba wa mke wa Kangi Lugola, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola aliyefariki siku ya tarehe 01, Januari, 2018 katika hospitali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa mke wa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Kangi Lugola, Kamishna Msaidizi wa Polisi marehemu Mary Lugola aliyefariki siku ya tarehe 01, Januari, 2018 katika hospitali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiifariji familia ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Kangi Lugola wakati alipoenda kuwapa pole ya msiba wa Kamishna Msaidizi wa Polisi marehemu Mary Lugola nyumbani kwao klabu ya reli, Gerezani, jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Kangi Lugola wakati alipoenda kutoa pole ya msiba wa mke wake Kamishna Msaidizi wa Polisi marehemu Mary Lugola aliyefariki siku ya tarehe 01, Januari, 2018 katika hospitali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapa pole watoto wa  marehemu Mary Lugola , mke wa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola aliyefariki siku ya tarehe 01, Januari, 2018 katika hospitali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WADAU WAPONGEZWA KWA KUTIMIZA MIAKA 50 YA NDOA ( 1967-2017)

$
0
0
 Bwana. Hamisi Kambona na Mkewe Bibi. Hawa Salimu wakiwa katika hafla fupi ya kuadhimisha miaka hamsini (50) ya ndoa yao iliyofanyika Disemba 30, 2017 nyumbani kwake Mkoani Morogoro. Bwana. Hamisi Kambona na Bibi. Hawa Salimu walifunga ndoa mwaka 1967. Watoto, Marafiki, Ndugu na Jamaa wanawapongeza sana, wanawatakia heri nyingi na Mungu aendelee kuwabariki.

NAIBU MEYA JIJI LA MBEYA (CHADEMA) AAHIDI USHIRIKIANO NA WATEULE WA RAIS MAGUFULI AMSIFU MHE MWANJELWA KUSHIRIKIANA NA VYAMA VYA UPINZANI

$
0
0

Na Mathias Canal, Mbeya

IMEBAINIKA kuwa tofauti za kiitikadi baina ya madiwani katika Halmashauri nyingi nchini, zimekuwa ni kikwazo kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye tija kubwa kwa wananchi.

Tofauti hizo zimekuwa chanzo kikubwa katika utekelezaji wa miradi inayobuniwa na Halmashauri husika, au inayoletwa na Serikali Kuu na wafadhili. Mitazamo ya kisiasa, tofauti ya uwakilishi wa vyama na ubinafsi, ndio sababu kuu.

Katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya inayoongozwa na Meya na Naibu Meya wanaotokana na vyama vya upinzania hali imekuwa tofauti kwani asilimia kubwa ya madiwani wanaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli tofauti kabisa na Halmashauri zingine.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Jana 2 Januari 2018 uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina, Kata ya Sinde Naibu Meya wa Jiji la Mbeya Mhe Fanuel Kyanula ambaye ni Diwani wa Kata ya Sinde alisema kuwa utendaji wa Rais Magufuli ni faida ya watanzania wote hivyo kuna kila sababu ya wananchi kuunga mkono juhudi za serikali yake.

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Meya wa Jiji la Mbeya Mhe Fanuel Kyanula ambaye ni Diwani wa Kata ya Sinde akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa Vyumba vya madarasa Shule ya Sekondari Sinde kabla ya kuzungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NEC YATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA KWA UCHAGUZI MDOGO KATIKA JIMBO LA SIHA NA KINONDONI PAMOJA NA KATA 4 ZA TANZANIA BARA

$
0
0
Subira Kaswaga – NEC 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa uchaguzi mdogo katika majimbo ya Siha mkoani Kilimanjaro na Kinondoni mkoani Dar es Salaam pamoja na Kata nne za Tanzania Bara utafanyika Februari 17, 2018 kufutia waliokuwa Wabunge katika majimbo hayo kujivua Uanachama na kukosa sifa za kuendelea kuwa wabunge.

Taarifa ya Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmod Hamid imeeleza kuwa pamoja na Majimbo hayo,pia Kata nne za Isamilo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Manzase Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Madanga Halmashauri ya Wilaya ya Pangani mkoani Tanga na Kimagai Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma zitafanya Uchaguzi mdogo

Aidha, Jaji Mkuu (Mst. Zanzibar) Hamid Mahmoud Hamid amesema kuwa, Tume inaendesha uchaguzi huo baada ya kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mh. Job Ndugai kuhusu uwepo wazi wa jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam na Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro.

Jaji Mahmoud amesema kuwa, barua hiyo ilieleza kuwa majimbo hayo yapo wazi baada Maulid Mtulia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kujivua uanachama wa CUF na Dr. Godwin Mollel wa jimbo la Siha kujiuzulu uanachama wa CHADEMA na hivyo wote kukosa sifa za kuwa Wabunge.

Pia, ameeleza kuwa Tume ilipokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ikiitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Udiwani katika kata nne za Tanzania Bara.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmod Hamid  
 

VIBWEKA, VITUKO VYATAWALA UCHAGUZI NAIBU MEYA DAR

$
0
0
* Meya wa Temeke, Ubungo nusura kuzichapa
 
Na Said Mwishehe, Blogu ya jamii

VITUKO, Vibweka, vitimbi na kila aina ya kejeli zimetawala wakati wa uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam.

Ilikuwa kama wanaigiza filamu lakini kumbe ndio ilikuwa namna ya kufanya uchaguzi huo ambao kwa sehemu kubwa majibizano yalichukua nafasi kubwa.

Uchaguzi wa kumpata Naibu Meya wa Jiji la Dar es Saalam umefanyika leo mchana na ulihusisha mgombea wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mariam Lorida na mgombea wa Chama cha Wananchi(CUF) Mussa Kafana.

ILIKUWA HIVI
Kabla ya uchaguzi huo kufanyika, vibweka, vitimbi na majibizano yalitawala kati ya Vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi(Ukawa)dhidi ya upande wa CCM.

Ukawa hawakuwa tayari uchaguzi huo kufanyika kwani mgombea wao hakuwepo ukumbini huku CCM wakiona ipo haja ya kufanyika uchaguzi wa kumpata Naibu Meya ili shughuli za kimaendeleo zifanyike.

Wakati mjadala huo unaendelea Meya wa Jiji la Dar es Salaam Issaya Mwita hakuwepo ukumbini.Hivyo CCM na Ukawa wakawa wanalumbana aidha kufanyika au kutofanyika uchaguzi huo.
Wakati wanalumbana ziliibuka baadhi ya kauli ambazo CCM hawakuridhika nayo na hasa ile iliyodaiwa kutolewa na Meya wa Ubongo Boniphance Jacob baada ya kudai huenda mgombea wao ametekwa.
Kauli ambayo iliwakera baadhi ya wajumbe wa upande wa CCM na hasa Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo kutaka Jackob afute kauli yake.

MEYA UBUNGO, TEMEKE NUSURA WAZICHAPE
Baada ya matokeo kutangazwa Meya Jackob alimkaba koo Meya wa Temeke Chaurembo.Sababu ni pale Chaurembo alipotaka kusogelea karatasi za kura.

Hivyo kukaibuka malumbano baina ya pande mbili, kiasi cha baadhi  askari polisi waliokuwa wamevaa kiraia kuamua kuingilia kati ili amani iendelee.

UKAWA WASHANGILIA
Matokeo ya uchaguzi huo yaliibua shangwe kwa Ukawa kwani ushindi huo wameamini umemeliza kiu yao ya kuitaka nafasi hiyo.Kwa mujibu wa nafasi ya Naibu Meya kila baada ta miezi sita wanafanya uchagizi.Hivyo Kafana amerudi tena kwenye nafasi hiyo.

CCM WATAFUTA MCHAWI
Ushindi wa mgombea wa Ukawa ukasababisha CCM kuanza kutafuta nani amewasaliti kwani kwa idadi ya washiriki walikuwa idadi sawa.Hivyo kwa matokeo hauo kuna Diwani wa CCM amewasaliti wenzake .Hali iliyoibua maswali.
  Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob  na Meya wa Manispaa ya Temeke Abdalah Chaurembo (aliyekaa chini) wakiwa wanaamuliwa na madiwani wengine  wakati wa uchaguzi wa kumtafuta Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam leo ambapo  uchaguzi huo ulijawa visa, vituko na vurugu za hapa na pale.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mussa Kafana (CUF) akiwa amelala ndani ya ukumbi wa Karimjee wakati wa  Uchaguzi wa kumtafuta  Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliofanyika leo jijini Dar es salaam na kuibuka mshindi baada ya kumshinda Mariam Rolida diwani wa  CCM kwa kura ya 12 dhidi ya 10.

 Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdalah Chaurembo akizuiwa kuongoza kikao na Diwani wa Chadema Patrick Asenga wakati wa mchakato wa uchaguzi wa kumtafuta Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
 Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob (wa kwanza kulia) akizungumza na Madiwani wa Chama cha Mapinduzi wakati wa mkutano wa kumtafuta Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam leo.
  Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mussa Kafana akiwa anawasili katika ukumbi wa uchaguzi huku ameshikiliwa na madiwani wenzake  kufanikisha uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji.

TRA INATARAJIA KUSAJILI WAFANYABIASHARA WADOGO MILIONI MOJA NCHI NZIMA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imesema kuwa wanatarajia kusajili walipakodi wapya milioni moja (1,000,000)  ambao watalipa kodi ya shilingi Bilioni 1.5.

Kodi  zinazolipwa ndizo zinafanya serikali kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwemo  miundombinu ya barabara, afya, maji na huduma nyinginezo.

Akizungumza katika usajili wa kituo cha kusajili wafanyabiashara wadogo wadogo  cha Chanika, Kamishna wa Kodi za Ndani, Elijah Mwandumbya amesema kuwa kampeni ya kusajili wafanyabiashara wa dogo ni endelevu.

Elijah amesema kuwa wananchi Wajitokeze kusajiliwa kadri kodi zinavyolipwa ndiyo zinafanya maendeleo ya nchi.

Amesema kuwa uhamasishaji wa ulipaji kodi na usajili utaendelea kwa kuweka vituo karibu na wafanyabiashara hao.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka hiyo, Richard Kayombo amewataka wananchi wa naoishi maeneo hayo kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kujiandikisha  na kusema kuwa zoezi hilo katika Kituo hicho Litadumu kwa muda wa juma moja.

Kayombo amesema wakitoka Manispaa ya Ilala watakwenda Manispaa ya  Temeke na baadaye  kufungua vituo katika maeneo mbalimbali" alisema Kayombo.

Aidha Kayombo amesema, Mamlaka hiyo imeamua kuja na kampeni hii  baada ya kutambua kuwa kulikuwa na usumbufu kwa Wafanyabiashara kupata TIN namba, kutokana na umbali kutoka wakazi wa eneo hilo hadi Vingunguti, na sasa wamesomea huduma hiyo na kwamba watakaojiandikisha hawana ulazima kulipa kodi siku hiyo hiyo.

Pamoja na hayo amewatahadhalisha wananchi kutolaghaiwa na matapeli kwani kazi hiyo inafanywa na TRA yenyewe na hakuna wakala aliye pewa kazi hiyo.
  Kamishna wa Kodi za Ndani, Elijah Mwandumbya akizungumza na waandishi habari juu ya usajili wa wafanyabiashara wadogo katika kituo cha Chanika jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Regina Urio (kulia)  akimhudumia mfanyabiashara (kushoto) aliyefika katika kituo maalum kilichoteuliwa na mamlaka hiyo kilichopo Chanika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusajili na kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).

MAGONJWA YASIYO YAKUAMBUKIZA YACHANGIA ASILIMIA 27 YA VIFO VYOTE NCHINI

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yasema kuwa magonjwa yasiyo yakuambukiza yanachangia kiasi kikubwa katika vifo vyote vinavyotokea hapa nchini. 

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa magonjwa yasiyokuwa yakuambukiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Sarah Maongezi wakati akipokea tuzo kutoka kwa TANCDA waliopata mwishoni mwa mwaka huu kutoka katika Shirikisho la Kimataifa la Magonjwa yasiyo yakuambukiza.

“Muongeze juhudi katika kupambana na magonjwa hayo ambayo yanachangia asilimia27 ya vifo vyote hapa Tanzania” Alisema Dkt Maongezi.

Dkt Maongezi aliendelea kusema kwamba Serikali imedhamiria kwa nia kabisa katika kupambana na magonjwa haya kwa kuamua kushirikiana na Asasi mbali mbali nchini ili kutimiza azma hiyo ya kupambana na magonjwa haya.

“Serikali pekee yetu hatuwezi na ndio maana tukashirikiana na Asasi kama TANCDA inayojumuisha vyama vingine kama vile, Taasisi ya Saratani, Taasisi ya Magonjwa ya Moyo, Taasisi ya Mfumo wa Hewa na Taasisi ya Kisukari ambazo kwa ujumla zimejenga ushirikiano katika kupambana na magonjwa haya” Aliongeza Dkt. Maongezi.
Kaimu Mkurugenzi magonjwa yasiyo yakuambukiza Dkt. Sarah Maongezi akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo katika picha) katika kikao kilichofanyika mapema leo katika ukumbi wa Hospitari ya Saratani ya Ocean Road kikihusu tuzo ya Elimu kwa jamii waliopata kutoka Shirikisho la kimataifa la magonjwa yasiyo yakuambukiza mwishoni mwa mwaka katika mkutano wa kimataifa uliofanyika katika falme zakiarabu. 
Kaimu Mkurugenzi magonjwa yasiyo yakuambukiza Dkt. Sarah Maongezi akipokea tuzo ya Elimu kwa jamii kutoka kwa Mwenyekiti wa TANCDA Dkt. Tatizo Waane mapema leo katika ukumbi wa Hospitari ya Saratani ya Ocean Road, Wapili kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TANCDA Andrew Swai. 
Kaimu Mkurugenzi magonjwa yasiyo yakuambukiza Dkt. Sarah Maongezi akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo katika picha) katika kikao kilichofanyika mapema leo katika ukumbi wa Hospitari ya Saratani ya Ocean Road kikihusu tuzo ya Elimu kwa jamii waliopata kutoka Shirikisho la kimataifa la magonjwa yasiyo yakuambukiza mwishoni mwa mwaka katika mkutano wa kimataifa uliofanyika katika falme zakiarabu, pembeni yake ni Mwenyekiti wa TANCDA Dkt. Tatizo Waane. 

RAIS MAGUFULI AAGANA NA GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) ANAYEMALIZA MUDA WAKE PROF. BENNO NDULU PAMOJA NA KUKUTANA NA GAVANA MTEULE WA (BOT) PROF. FLORENS LUOGA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na na Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo  na Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga wa kwanza (kushoto) pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu wa kwanza (kulia) mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na na Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga wa kwanza (kushoto) pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu wa kwanza (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TANESCO TABATA WALALAMIKIWA KUTELEKEZA NYAYA, NGUZO ZA MRADI KIFURU,

$
0
0
WAKAZI wa Kata ya Kinyerezi eneo la Kifuru kwa Kinana wameulalamikia uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kituo cha Tabata jijini Dar es Salaam kwa kitendo cha kutelekeza nguzo na nyaya za mradi wa umeme eneo hilo ambapo zimegeuka kero. 

Wakizungumza jana eneo hilo kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi wakazi hao, wamesema TANESCO kituo cha Tabata walileta nguzo na nyaya tangu mwaka jana na kuziweka barabara inayoelekea King'azi (Kwa Godoro) Mtaa wa Tanganyika ambapo baada ya mvua za mwishoni mwa mwaka jana 2017 baadhi ya nguzo zilianguka na nyaya kutandaa chini jambo ambalo limekuwa kero baada ya kuziba barabara ya mtaa huo na magari kupita kwa taabu.

Mkazi wa Mtaa wa Tanganyika, Rashid Abdallah alisema mradi huo umechukua zaidi ya miaka miwili sasa huku wateja walioomba umeme eneo hilo wamekuwa wakizungushwa kwamba wasubiri mradi huo bila ya mafanikio. 

"...Tumeomba umeme muda mrefu sana tunaambiwa kusubiri mradi lakini mradi ndio kama hivyo wamekuja wamefunga nyaya baada ya mvua kunyesha zimeanguka na wamezitelekeza hapo hapo chini...tunapita kwa shida na wengine kwa hofu maana 
nyaya za umeme zipo chini kabisa si wote wapita njia hazijafungwa umeme sasa hii ni hatari," alisema Mkazi huyo wa Mtaa wa Tanganyika.

Alisema kwa sasa wamekuwa kama walinzi wa nguzo na nyaya hizo za TANESCO mtaani hapo maana wanahofia zikiibiwa huenda matumaini ya mradi huo wanaoahidiwa kila kukicha kukamilika ukatoweka kabisa. "Sasa hivi tumegeuka walinzi maana tunajitahidi haya manyaya yao (waya za TANESCO) waliotelekeza hapo chini baada ya kuanguka yasiibiwe...," alisema Abdallah.
 Gari na pikipiki zikipita kwa shida Mtaa wa Tanganyika, Kifuru Kata ya Kinyerezi jijini Dar es Salaam, eneo ambalo nyaya na nguzo za mradi wa umeme unaodaiwa kutelekezwa na TANESCO kituo cha Tabata kwa muda sasa baada ya kuangushwa na mvua za mwishoni mwa mwaka 2017.
Baadhi ya nguzo na nyaya za TANESCO Kituo cha Tabata Dar es Salaam zinazodaiwa kutelekezwa na kituo hicho kwa muda sasa baada ya kung'olewa na mvua. Wakazi wa eneo hilo wameilalamikia TANESCO kwa kushindwa kutatua kero hiyo na kukamilisha mradi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AOMBOLEZA MSIBA WA MKE WA NAIBU WAZIRI KANGI LUGOLA

$
0
0



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimfariji  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola  kwenye msiba wa  mkewe MarehemuKamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola Gerezani Railyways Club jijinio Dar es salaam leo January 3, 2018 (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
PMO_4794
Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo alipofika Gerezani Railways Club jijini Dar es salaam leo January 3, 2018  kwenye msiba wa Marehemu Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola aliyekuwa mke wa  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola aliyefariki jana.
PMO_4800
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,akitoa pole kwa wafiwa alipofika Gerezani Railways Club jijini Dar es salaam leo January 3, 2018  kwenye msiba wa Marehemu Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola aliyekuwa mke wa  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola aliyefariki juzi tarehe 1/1/2018.
PMO_4808
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,akitoa pole kwa wafiwa alipofika Gerezani Railways Club jijini Dar es salaam leo January 3, 2018  kwenye msiba wa Marehemu Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola aliyekuwa mke wa  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola aliyefariki juzi tarehe 1/1/2018.

MAGAZETI YA ALHAMIS LEO JANUARY 4,2018

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images