Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MFANYABIASHARA AJENGA ZAHANATI YENYE VIFAA VYA KISASA NA KUIKABIDHI SERIKALINI

$
0
0
 Mfanyabiashara, Emmanuel Mallya (katikati) akisaini hati na mkataba wa zahanati EB, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Michael Kilawila kwenye hafla hiyo ya makabidhiano. Kushoto ni mke wa Bw. Mallya, Bi. Marry Mallya akishuhudia makabidhiano hayo.
 Mfanyabiashara, Emmanuel Mallya (kushoto) akimkabidhi hati na mkataba wa zahanati EB Zahanati Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Michael Kilawila kwenye hafla hiyo ya makabidhiano.

Na Mwandishi Wetu, Moshi
MFANYABIASHARA na mzaliwa wa Kijiji cha Uchau Kaskazini wilaya ya Moshi Vijijini, Emmanuel Mallya, ameikabidhi serikali zahanati ikiwa na vifaa vya kisasa vikiwamo vitanda vya wagonjwa vinavyotumia nishati ya umeme.

Zahanati hiyo inayojukana kwa jina la EB zahanati, imejengwa na mfanyabiashara huyo kwa kutumia nguvu zake mwenyewe bila kuhusisha msaada kutoka Halmashauri ya wilaya ya Moshi wala serikali kuu.

Akizungumza katika hafla fupi ya kuikabidhi zahanati hiyo kwa serikali, mfanyabiashara huyo alisema wazo la kujenga zahanati hiyo lilitokana na kuwepo na changamoto za umbali wa huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo.

Alisema changamoto hiyo ilipelekea kuwepo na vifo vya watu wengi vilivyochangiwa na umbali wa upatikanaji wa vituo vya afya na kwamba changamoto hizo ndizo zilizomsukama kuona haja ya kujenga zahanati hiyo.

Alitoa wito kwa mamlaka husika kuitunza zahanati hiyo pamoja na vifaa vitakavyotumika katika kuwahudumia wagonjwa huku akitoa wito kwa watu wengine wenye uwezo kujitolea katika kuwahudumia wananchi wasio nacho.

“Utajiri unatokana na moyo wa mtu alionao, unaweza ukawa na utajiri na usiwe na moyo wa kuwasaidia wengine, kila mtu amepewa karama na mwenyezi Mungu, muhimu hapa ni namna ya kuzitambua hizo karama,” alisema.

Kabla ya ujenzi huo ulioanza julai mwaka 2013, familia iliyokuwa ikishi mahali ilipojengwa shule hiyo iliridhia ombo la mfanyabaishara huyo la kuachia eneo hilo na kupelekwa kwenye eneo jingine kwa ushirikiano wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha Kimasio.

Aliwapongeza familia hiyo kwa kukubali ombi lake la kuliachia eneo hilo na kuongeza kuwa, bila familia hiyo kuridhia kuondoka katika eneo hilo ndoto zake za kujenga zahanati katika eneo hilo zingeishia ukingoni.

Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, Anthony Komu alihimiza usimamizi wa karibu wa zahanati hiyo kwa wale watakakuwa wasimamizi baada ya aliyeijenga kuikabidhi kwa serikali.

"Mhehsimiwa Mkuu wa Wilaya, uzoefu unaonyesha kuwa, miradi mingi inayojengwa na wafadhili imekuwa ikiharibika kutokana na kutokuwepo na usimamizi wa karibu, ni rai yangu kuwa tuitunze zahanati hii isijekuwa mazalia ya popo kama ambavyo tumekuwa tukishuhudia kwa baadhi ya zahanati na vituo vya afya,” alisema.

Alisema mfanyabiashara huyo ametenda wema wa hali ya juu kwa wananchi wa Wilaya ya Moshi Vijijini na Vunjo kwa ujumla  na kwamba wema huo kamwe hautafutika ndnai ya mioyo ya wananchi hao. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Michael Kilawila, alitoa wito kwa wananchi wa wilaya hiyo kuchangishana kwa kile kidogo walichonacho ili wanunue gari la wagonjwa ambalo litahudumia zahanati hiyo kwa muda wa saa 24.

Alisema uwepo wa gari la wagonjwa katika zahanati hiyo utarahisisha kuwapeleka wagonjwa katika Hospitali kubwa ikiwamo ya Kibosho, Mawenzi na KCMC kwa wale ambao watahitaji kupewa rufaa.

Alisema maendeleo yanahitaji umoja na mshikamano na kuonya kuwa maendeleo hayana itikadi yoyote ya kisiasa kwani zahanati hiyo itahudumia wananchi wote bila kujali huyu ni wa chama gani.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa wilaya ya Moshi, Kippi Warioba alipongeza moyo ulioonyeshwa na mfanyabiashara huyo wa kusaidia watu wenye mahitaji. Pia alitoa wito kwa serikali ya kijiji hicho kuanza mazungumzo na wananchi wanaoishi karibu na zahanati hiyo kuachia maeneo yao ili zahanati hiyo ipanuliwe na kufika hadhi ya kituo cha Afya.

Alitoa wito kwa kila mtu kuchangia chochote alichonacho ndani ya jamii na si lazima iwe pesa na kuwapongeza walioachia eneo ilipojengwa zahanati hiyo wametoa mchango mkubwa sana kwa jamii.


FAMILIA YA NGUZA VICKING YAKUTANA NA RAIS DKT MAGUFULI IKULU DAR ES SALAAM

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na mwanamuziki Nguza Viking "Babu Seya" na wanae Johnson Nguza "Papii Kocha', Francis Nguza na Nguza Mbangu walipokwenda Ikulu jijini Dar es salaam leo January 2, 2018 kumshukuru kwa kuwapa msamaha wa kifungo cha maisha Babu Seya na mwanae Papii Kocha walichokuwa wanatumikia toka wahukumiwe miaka 13 iliyopita.
Mwanamuziki Nguza Viking "Babu Seya" na wanae Johnson Nguza "Papii Kocha', Francis Nguza na Nguza Mbangu walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo January 2, 2018 kumshukuru Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwapa msamaha wa kifungo cha maisha Babu Seya na mwanae Papii Kocha walichokuwa wanatumikia toka wahukumiwe miaka 13 iliyopita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mwanamuziki Nguza Viking "Babu Seya" ambaye pamoja na wanae Johnson Nguza "Papii Kocha', Francis Nguza na Nguza Mbangu walipokwenda Ikulu jijini Dar es salaam leo January 2, 2018 kumshukuru kwa kuwapa msamaha wa kifungo cha maisha Babu Seya na mwanae Papii Kocha walichokuwa wanatumikia toka wahukumiwe miaka 13 iliyopita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na  Johnson Nguza "Papii Kocha' walipokwenda Ikulu jijini Dar es salaam leo January 2, 2018 kumshukuru kwa kuwapa msamaha wa kifungo cha maisha Babu Seya na mwanae Papii Kocha walichokuwa wanatumikia toka wahukumiwe miaka 13 iliyopita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa kashikana mikono huku wakiomba dua  na mwanamuziki Nguza Viking "Babu Seya" na wanae Johnson Nguza "Papii Kocha', Francis Nguza na Nguza Mbangu walipokwenda Ikulu jijini Dar es salaam leo January 2, 2018 kumshukuru kwa kuwapa msamaha wa kifungo cha maisha Babu Seya na mwanae Papii Kocha walichokuwa wanatumikia toka wahukumiwe miaka 13 iliyopita.
Mwanamuziki Nguza Viking "Babu Seya" na wanae Johnson Nguza "Papii Kocha', Francis Nguza na Nguza Mbangu wakiondoka  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 2, 2018 baada ya kumuona na kumshukuru Rais Dkt John Pombe  Magufuli kwa kuwapa msamaha wa kifungo cha maisha Babu Seya na mwanae Papii Kocha walichokuwa wanatumikia toka wahukumiwe miaka 13 iliyopita.
Johnson Nguza "Papii Kocha' akionesha tatoo ya "JPM" aliyojichora mkononi  walipokwenda Ikulu jijini Dar es salaam leo January 2, 2018 kumshukuru kwa kuwapa msamaha wa kifungo cha maisha Babu Seya na mwanae Papii Kocha walichokuwa wanatumikia toka wahukumiwe miaka 13 iliyopita. Picha na Ikulu

RAIS MAGUFULI AMPA POLE KANGI LUGOLA KWA KUFIWA NA MKEWE

$
0
0
*Lugola atoa ratiba ya maziko ya mkewe, 
kuagwa Dar, kuzikwa Mwibara

Na Said Mwishehe, Blogu ya Jamii

RAIS Dk.John Magufuli ametia saini Kitabu cha Maombolezo na kumpa pole, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu Muungano na Mazingira  Kangi Alphaxd Lugola aliyefiwa na mkewe Kamishina Msaidizi wa Polisi Mary Lugola.

Kamishna Mary amefariki dunia jana asubuhi akiwa katika Hospitali ya  Rabinisia jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Rais Dk.Magufuli alifika nyumbani kwa Kangi Lugola Gerezani Railway jijini Dar es  Salaam ambako ndiko msiba ulipo. Akiwa msibani Rais Magufuli ametia saini kitabu cha maombolezo na kumpa pole Lugola kwa kufiwa na mkewe Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola. 

Wakati huohuo,  akizungumza na Michuzi blog kwa njia ya simu leo,Kangi Lugola amesema mkewe anatarajiwa kuagwa Januari 4 mwaka huu, kuanzia saa nne asubuhi nyumbani kwake Gerezani.

Amesema mwili utawasili nyumbani kutokea Hospitali ya Lugalo asubuhi na kisha waombolezaji wataaga mwili. Saa nane mchana mwili utasafirishawa kuelekea kijijini Mwibara mkoani Mara kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Januari 5 mwaka huu.

"Tunatarajia kuaga mwili wa marehemu mke wangu January 4 mwaka huu, na ikifika saa nane mchana tutausafirisha kwenda Mwibara,"amesema Kangi Lugola. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli    akimfariji  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola  kwenye msiba wa  mkewe MarehemuKamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola Gerezani Railyways Club jijinio Dar es salaam leo January 2, 2018 .Picha na Ikulu.

WATUMISHI WA SERIKALI ZA MITAA, ASKARI WA MBELE VITANI - WAZIRI JAFO

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Arusha Dc wakati wa ziara yake katika Halmashauri hiyo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (katikati) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kushoto) pamoja na kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Iddi Kimanta kwenye kikao na watumishi wa Halmashauri ya Arusha Dc.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Dc Dr.Wilson Mahera Charles akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Nchi Mhe.Selemani Jafo(hayupo pichani) na watumishi wa Halmashauri hiyo.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Arusha Dc wakifuatilia Kikao wakati Waziri wa Nchi Mhe.Selemani Jafo alipowatembelea na kufanya kikao na watumishi  wa Halmashauri hiyo.

Nteghenjwa Hosseah, Arusha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo  amesema watumishi wa Mamlaka hii ndio askari wa mbele katika harakati za maendeleo na kuleta mabadiliko kwa wananchi wa Nchi hii.

Waziri Jafo amesema shida zote za wananchi zitapata ufumbuzi wa kina endapo watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wataacha kufanya kazi kwa mazoea na kutimiza wajibu wao ipasavyo.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Arusha Dc kwenye ziara yake ya Siku moja katika Halmashauri hiyo na kuzungumza na watumishi, kukutana na wananchi na kuskiliza kero zao sambamba na kukagua miradi ya maendeleo.

Amesema "Ili kufikia agenda ya mabadiliko katika Nchi hii lazima sisi tunaohudumu katika Ofisi hii tuongee lugha moja, tujitume, tuwajibe kwa moyo katika kuwaletea maendeleo wananchi wetu.

Aliongeza kuwa Upimaji wa utendaji kazi wetu usiwe ule wa kujaza Opras kama mazoea  ila uwe ni Mkataba wa Makubaliano ya kazi na mpimane kulingana na yale mliokubaliana kwa mujibu wa Mkataba.

Aliupongeza Mkoa huu kwa kuanzisha mpango wa kupima wanafunzi wa Sekondari na kushauri kuboresha mpango huo kwa kuanzisha Kampeni ya Kuondoa Zero katika Mkoa wa Arusha.

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akimkaribiha Waziri wa Nchi amesema watumishi waliopo katika Halmashauri ndio Timu ya Ushindi ya Mkoa wa Arusha hivyo wakurugenzi wote wanatakiwa kuwasimamia na kuwaongoza kwa Weledi ili waweze kufikia malengo.

Pia alikumbushia maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wanaanza masomo wiki ijayo na kuwaelekeza wakurugenzi kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa wanaaza masomo kwa wakati huku miundombinu ikiwa imekamilika na walimu kujiandaa kwa mapokezi  hayo.

Akielezea mpango wa Mkoa wa Arusha wa kusimamia  ubora wa Elimu kwa wanafunzi wa Sekondari kwa kuanzisha Mtihani  Maalumu wa kupima uwezo wa mwanafunzi katika kila kidato amesema ili kuweka uelewa wa pamoja katika shule zote za Sekondari Mkoa umeamua kusimamia mpango huu  na maandalizi ya uratibu wa mtihani huo yameshakamilika na yako chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Naye Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Iddi Kimanta  amesema wamefurahi kuwa watumishi wa kwanza kwa mwaka huu kutembelewa na Waziri wa Nchi Sambamba na viongozi wa juu wa Mkoa na bika shaka ari waliyoipata leo itaendelea kujidhihirisha katika maeneo yao ya Utendaji katika kipindi cha mwaka Mzima.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe.Selemani Jafo ameanza ziara ya kwanza ya kikazi kwa mwaka 2018 na ataendelea na ziara hii katika Mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es salaam, Iringa, Mbeya, Mtwara na Lindi.

RUSHWA IMECHANGIA WAKANDARASI KUJENGA BARABARA CHINI YA KIWANGO-DC HAPI

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akionesha sehemu   ya Udongo ambao umechanganyika na takataka zilizokuwa chini ya barabara ya Msasani CCBRT ,ambayo imekuwa ikimeguka kila siku kutokana na mkandarasi wa awali  aliojenga barabara hiyo kuipitisha juu ya udongo wenye takataka na kusababishia hasara kwa serikali kila Mwaka.DC Hapi alieleza kuwa ujenzi  huo wa awali umeiingiza Serikali Hasara kutokana na baadhi ya watendaji wa Serikali kula rushwa na kufumbia macho ujenzi huo wa barabara juu ya dampo. 
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akiwaonya wakazi wa Tandale kwa Tumbo juu ya utupaji taka hovyo katika mitaro ya Maji iliyopo pembezoni mwa barabara,kama ionekanavyo pichani ikiwa imejaa maji taka na kuhatarisha afya za wakazi wa eneo hilo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akionesha barabara ya Magomeni Kondoa inayokarabatiwa na Wakala wa Barabara nchini Tarura  mara baada ya kuwa na Mashimo mengi na kufanya kushindwa kupitika
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akichota sehemu ya udongo uliokuwa ukisumbua barabara ya Msasani CCBRT ambao ulikuwa umechanganyika na Taka.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akikagua barabara ya kuelekea Sleepway Masaki Jijini Dar es Salaam ambayo imeharibika na Mashimo Makubwa na sasa inakarabatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

DK. KIGWANGALLA NA MKURUGENZI MKAZI WA UNDP KUANZISHA KIKOSI KAZI CHA KUCHUNGUZA TUHUMA ZA UJANGILI WA TEMBO KATIKA HIFADHI YA RUAHA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY wamekubaliana kuanzisha kikosi kazi cha pamoja cha kuchunguza tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na kituo cha habari cha ITV LONDON kuhusu ujangili wa Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo Mkoani Iringa.

Dk. Kigwangalla na Mkurugenzi huyo, wamefikia makubaliano hayo leo Januari 2, 2018 wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Waziri Kigwangalla amemueleza Mkurugenzi huyo kuwa Wizara yake inaandaa mikakati mbalimbali ya kuongeza idadi ya watalii nchini na mapato ikiwemo kuwashirikisha wananchi kuandaa mwezi maalum wa Urithi wa Tanzania pamoja na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwa njia za kielektroniki katika vituo mbalimbali ya Utalii.

Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo amemuahidi Waziri Kigwangalla kuendelea kumpa ushirikiano katika nyanja mbalimbali za kuendeleza Utalii nchini na uhifadhi wa misitu na wanyamapori kwa ujumla.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akiagana  na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo.

DK. KIGWANGALLA NA MKURUGENZI MKAZI WA UNDP KUANZISHA KIKOSI KAZI CHA KUCHUNGUZA TUHUMA ZA UJANGILI WA TEMBO KATIKA HIFADHI YA RUAHA

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY wamekubaliana kuanzisha kikosi kazi cha pamoja cha kuchunguza tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na kituo cha habari cha ITV LONDON kuhusu ujangili wa Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo Mkoani Iringa.

Dk. Kigwangalla na Mkurugenzi huyo, wamefikia makubaliano hayo leo Januari 2, 2018 wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Waziri Kigwangalla amemueleza Mkurugenzi huyo kuwa Wizara yake inaandaa mikakati mbalimbali ya kuongeza idadi ya watalii nchini na mapato ikiwemo kuwashirikisha wananchi kuandaa mwezi maalum wa Urithi wa Tanzania pamoja na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwa njia za kielektroniki katika vituo mbalimbali ya Utalii.

Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo amemuahidi Waziri Kigwangalla kuendelea kumpa ushirikiano katika nyanja mbalimbali za kuendeleza Utalii nchini na uhifadhi wa misitu na wanyamapori kwa ujumla.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akiagana  na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo.

WAZIRI MWIGULU ATOA TAARIFA YA MWAKA 2017 NA MIPANGO YA WIZARA 2018

$
0
0
“kwa mwaka 2017 matukio yaliyoniudhi zaidi ni tukio la kushambuliwa kwa askari polisi na wananchi maeneo kibiti na kushambuliwa kwa kiongozi mda wa mchana tena katikati ya mji wa serikali na watu kupotea sehemu kusiko julikana hivyo nawataka wananchi kuwa mbele ya matukio kwa kutoa taarifa na kama wizara sisi tupo vitani mda wote kuwasaka waharifu na kuzia uharifu kwa mwaka 2018” Waziri Mwigulu.

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA KIBIASHARA NCHINI ARGENTINA

MILIONI 400 ZA OFISI YA RAIS – TAMISEMI KUJENGA NA KUKARABATI KITUO CHA AFYA MALANGALI HALMASHAURI YA MUFINDI

$
0
0
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mufindi itatumia jumla ya shilingi Milioni Mianne (400) kujenga na kufanya ukarabati mkubwa wa kituo cha Afya Malangali, kilichopo kata ya Malangali Halmashauri ya Wilayani Mufindi, ikiwa ni mkakati wa Serikali kuimarisha sekta muhimu ya Afya hususani Afya ya Mama na Mtoto.

Ujenzi na ukarabati wa kituo hiki cha Afya, unaotarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa, unafanyika baada ya Ofisi ya Rais – Tamisemi, kutoa kiasi cha Shilingi Milioni mianne (400) kwa lengo la kuimarisha miundombinu ya kituo hicho ili kiweze kukidhi haja ya kutoa huduma bora za Afya kwa zaidi ya Wananchi elfu arobaini na nane (48,000) wa Tarafa ya Malangali watakao pewa rufaa kutoka kwenye Zahanati za Vijiji.

Matumizi ya kiasi hicho cha fedha, ni pamoja na kujenga jengo la kisasa la Maabara, Nyumba ya Mganga, kukamilisha ujenzi unaoendelea wa chumba cha upasuaji sanjari na kufanya ukarabati mkubwa wa Wodi maalum ya wazazi / Mama na Mtoto.

Ujenzi na ukarabati wa kituo, utatekelezwa kwa mfumo wa (Force Account) ambapo, Halmashauri itatumia Mafundi wenyeji watakaothibitishwa kuwa na uwezo unaokubalika wa kutekeleza jukumu hili kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu, badala ya mtindo uliozoeleka wa kutumia Wakandarasi. Pia, ili kuhakikisha mradi huu unatekelezwa kwa viwango vinavyokubalika, Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji, imeunda Vikosi kazi vitatu (03) vikijumuisha Maofisa kutoka idara mbalimbali maalum kwa kuratibu na kusimamia mradi huu kwa kuzingatia wakati na ubora.

Aidha, kwa kuwa uboreshaji wa kituo hiki, utatekelezwa kwa mfumo wa (Force Account) kama ambavyo imefafanuliwa hapo juu, Mkurugenzi Mtendaji anawahamasisha wananchi wote wa Tarafa ya Malangali kujitolea nguvu kazi pindi itakapohitajika wakati wa utekelezaji wa mradi huu kwa ustawi wa Afya ya kila mkazi wa Tarafa ya Malangali na Halmashauri ya Mufindi kwa ujumla.

Imetolewa na,

Ndimmyake Mwakapiso,
Ofisa Habari na Mawasiliano Halmashauri ya (W) Mufindi.
Profesa Riziki Shemdoe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi.
 

MAMIA YA WAKAZI DAR WAMUAGA MWANAHABARI JUSTINE LIMONGA

$
0
0
Dotto Mwaibale na Kulwa Mwaibale
Katibu  wa Itikadi na Uenezi  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamphrey Polepole, ameongoza mamia ya waombolezaji katika ibada ya kuaga mwili wa mwanahabari, Justine Limonga iliyofanyika Viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam leo mchana.

Akizungumza katika ibada hiyo, Polepole alisema CCM na tasnia ya habari imepoteza mtu muhimu ambaye alikuwa bado akitegemewa.

"Tumempoteza mtu muhimu ambaye alikuwa akitegemewa kama chama tutaangalia namna ya kuisaidia familia yake," alisema Polepole.

Mkurugenzi wa Nduvini Auto Garage, Alhaji Ahmed Msangi alizungumza jinsi alivyomfahamu marehemu ambapo aliahidi kampuni yake kwa kipindi hiki cha kufunguliwa kwa shule itawanunulia vifaa vya shule, sare na kuwalipia karo wakati wakisubiri kukaa na familia kuona namna ya kuwazesha watoto hao kielimu.

Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angel Akilimali alisema kifo cha mwanahabari huyo aliyekuwa mwajiriwa wao kimeacha pengo kubwa ambalo halitazibika.
 Waombolezaji na wanahabari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mwanahabari wa Uhuru FM, Justine Limonga wakati ukiwasili Viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa kabla ya kufanyika mazishi yake Makaburi ya Saku yaliyopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo.
 Katibu  wa Itikadi na Uenezi  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamphrey Polepole, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la mwanahabari, Justine Limonga.
 Waombolezaji wakisubiri kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu kwenda eneo maalumu ilipo kufanyika ibada hiyo.
 Familia ya marehemu ikiwa kwenye ibada hiyo.
 Kwaya ya Mtakatifu Kizito ya Parokia ya Kutukuka kwa Msalaba Kizuiani, ikitoa burudani.
 Katekista wa Parokia ya Kutukuka kwa Msalaba Kizuiani,  Philo Mbunda, akitoa mahubiri.
 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Ibada ikiendelea

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAKWIMU ZA BEI ZANZIBAR KWA MWEZI WA NOVEMBA NA DISEMBA ZATOLEWA

$
0
0
 Mkuu wa Takwimu za Bei katika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar Khamis Abdul-Rahman Msham akiwasilisha Takwimu za Bei kwa Waandishi wa Habari kwa mwezi wa Novemba na Disemba ambapo zimeoneka kupanda kutoka asilimia 5.0 hadi 5.9 hafla iliofanyika katika Ofisi ya Takwimu Mwanakwerekwe Zanzibar.
 Mhadhiri wa Uchumi Chuo Kikuu Cha Taifa SUZA Dk,Suleiman Msaraka akitoa ufafanuzi wa Takwimu za Bei  kwa Waandishi wa Habari kwa mwezi wa Novemba na Disemba ambapo zimeoneka kupanda kutoka asilimia 5.0 hadi 5.9 hafla iliofanyika katika Ofisi ya Takwimu Mwanakwerekwe Zanzibar.
 Mwandishi wa Habari wa ITV Farouk Kariym akiuliza maswali katika mkutano wa Waandishi wa Habari kuhusiana na Takwimu za Bei  kwa mwezi wa Novemba na Disemba ambapo zimeoneka kupanda kutoka asilimia 5.0 hadi 5.9 hafla iliofanyika katika Ofisi ya Takwimu Mwanakwerekwe Zanziba.
 Meneja wa Uchumi Benki Kuu Tawi la Zanzibar Moto Ng'winganele Madeshi Hugobi katikati akijibu maswali yalioulizwa na Waandishi wa Habari kuhusiana na Takwimu za Bei  kwa mwezi wa Novemba na Disemba ambapo zimeoneka kupanda kutoka asilimia 5.0 hadi 5.9 hafla iliofanyika katika Ofisi ya Takwimu Mwanakwerekwe Zanziba.kulia yake ni Mhadhiri wa Uchumi Chuo Kikuu Cha Taifa SUZA Dk,Suleiman Msaraka na kushoto yake ni Mkuu wa Idara ya Takwimu za kiuchumi Zanzibar Abdul Ramadhan Abeid.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano kuhusiana na Takwimu za Bei  kwa mwezi wa Novemba na Disemba ambapo zimeoneka kupanda kutoka asilimia 5.0 hadi 5.9 hafla iliofanyika katika Ofisi ya Takwimu Mwanakwerekwe Zanzibar. 
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 02.01.2018

Kombe la Mapinduzi: Simba na Mwenge zatoka sare ya Bao 1-1

$
0
0
 Kaimu kocha mkuu wa Simba akishauriana jambo na wachezaji wake wakati wa mchezo wao na Mwenge wa Kombe la Mapinduzi katika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar leo. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. 
  Mshambuliaji wa Simba Said Hamis Juma "Ndemla"  akimiliki mpira  wakati wa mchezo wao na Mwenge wa Kombe la Mapinduzi katika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar leo. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. 
 MSHAMBULIAJI wa Timu ya Mlandege Khamis Abuu akimpita beki wa Timu ya Zimamoto Suleiman Said wakati wa mchezo wa Kombe la Mapinduzi mchezo uliofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Mlandege imeshinda bao 2-1
 MSHAMBULIAJI wa Timu ya Zimamoto Ibrahim Hilika akimpita beki wa Timu ya Mlandege Edwin Charles wakati wa mchezo wa Kimbo la Mapinduzi mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Mlandege imeshinda bao 2-1. Picha zote na Othman Maulid.

MAZISHI YA MKE WA MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA MWANANCHI MKOANI TANGA

$
0
0

 Sehemu ya waombolezaji wakiwa msibani eneo la Magomeni Jijini Tanga

 Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Mkoani Tanga,Burhan Yakub kushoto ambaye amefiwa na mkewe akiwa na ndugu jamaa wakati wa msiba huo nyumbani kwake eneo la Magomeni Jijini Tanga.

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella katikati akiwa eneo la msibani Magomeni Jijini Tanga kulia ni Katibu Itikadi na Uenezi CCM wilaya ya Tanga, Lupasio Kapange


Wananchi wakifukia mwili wa aliyekuwa mke wa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi mkoani Tanga,Burhan Yakub

  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akisalimiana na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Tanga,Hassan Hashimn akiteta jambo na wandishi wa habari mkoani Tanga wakati wa msiba huo. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Kituo cha Afya Nduruma kupata miundombinu zaidi ya Afya - Mhe Jafo

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, Nduruma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe. Selemani Jafo ameagiza ujenzi wa miundombinu ya Afya unaoendelea katika kituo cha Afya Nduruma Wilayani Arumeru mkoa wa Arusha uongezewe jengo jipya la chumba cha Upasuaji na kile kilichoanza kujengwa kitatumika kwa kazi nyingine.
Waziri Jafo amesema hayo wakati alipotembelea kituo hicho na kuweka Jiwe la Msingi katika kituo hicho sambamba na kukagua ujenzi wa majengo mbalimbali ya Afya yanayoendelea kujengwa.
"Nimeridhishwa na ujenzi wa miundombinu hii ya Afya na kazi inaenda vizuri kabisa ila kutokana na hali niliyoiona na mahitaji ya arneo hili naagiza Mjenge jengo jipya la Chumba cha upasuaji na lile ambalo mliliendeleza litatumika kwa matumizi mengine".
"Baada ya Ujenzi huu kukamilika hiki ndio kituo cha Afya ambacho kitakua kimepata Majengo mengi zaidi katika mpango wetu huu wa uboreshaji lakini yote ni Kwa sababu ya mahitaji ya wananchi wa eneo hili ambao Idadi yao ni kubwa wanaotegemea huduma kutoka katika kituo hiki" Alisema Jafo.
Akizungumza katika Mkutano wa hadhara Mbungu wa viti maalumu anayewakilisha Mkoa wa Arusha Mhe. Amina Mollel amesema Wananchi wa Nduruma wanaishkuru Serikali kwa kuwaboreshea kituo cha Afya Nduruma na wanaomba zaidi msaada wa kupata Gari la kubebea wagonjwa ili iwe rahis kuwatoa katika kituo hicho na kuwapeleka katika Hospital ya Mkoa.
" Mhe Waziri sisi wananchi wa Nduruma tunakushkuru sana kwa namna ambavyo Serikali inatuboreshea huduma za Afya lakini bado shida zetu hazijaisha, tunaomba mtusaidie Gari la kubebea wagonga na matengenezo ya barabara yetu tutashukuru zaidi" alisema Mhe. Mollel.
Waziri Jafo aliahidi kuyashughulia maombi yote yaliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Mollel na kwa kuanzia amemuagiza Manaja wa Tarura Wilaya kuanza ukarabati mdogo wa barabara hiyo huku wakiendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati mkubwa na wa kudumu na mahiaji mengine yote ya Afya ameahidi kuyashughulikia kadiri ya upatikanaji wa fedha.
Baada ya ujenzi wa miundombinu hii ya Afya Kituo cha Afya Nduruma kitakua kimepata jengo la Wodi ya Kinamama, Maabara, Chumba cha Upasuaji, Chumba cha kuhifadhia maiti, kichomea Taka, Sehemu ya kufulia na jengo lililokuwa litumike kama chumba cha upasuaji hapo awali litapangiwa matumizi mengine.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Kata ya Nduruma kwenye Mkutano wa hadhara (hawapo pichani) baada ya kuweka jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa miundombinu ya Afya katika kituo cha Afya Nduruma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Selemani Jafo(kulia) akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha Dc Ndg.Wilson Mahera Charles pamoja na Mbunge wa Viti Maalum  Mhe. Amina Mollel kwa kusimamia ujenzi wa miundombinu ya Afya kwenye kituo cha Afya Nduruma.
 Jengo la wodi ya Kinamama ni mojawapo ya majengo yanayoendelea kujengwa katika uboreshaji wa kituo cha Afya Nduruma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Selemani Jafo(katikati mbele) akisimikwa kuwa Chifu wa Kimaasai maarufu kama Leigwanani wakati wa ziara yake katika kituo cha Afya Nduruma ambapo aliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa miundombinu ya Afya.
 Viongozi wa Halmashauri hiyo wakimskiliza Waziri wa Nchi Mhe.Selamani Jafo akizungumza na wananchi wa kata ya Nduruma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Selemani Jafo akiwaaga  wananchi wa Nduruma baaa ya ziara yake katika Kituo cha Afya Nduruma.

MAGAZETI YA JUMATANO LEO JANUARY 3,2018

WAZIRI MWIJAGE ZIARANI MKOANI SIMIYU, AFUNGUA OFISI ZA SIDO NA KUKABIDHI ENEO KWA MKANDARASI KWA AJILI YA UJENZI WA VIWANDA

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage afanya Ziara katika mkoa wa Simiyu leo tarehe 2/1/2018. Katika ziara yake Mhe. Mwijage amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka na kufanya mazungumzo mafupi kabla ya kushiriki zoezi la ufunguzi wa ofisi za SIDO mkoa wa Simiyu.

Mara baada ya Ufunguzi wa Ofisi hizo Mhe. Waziri alipata furesa ya kuzungumza machche na kutoa maagizo ya Utekelezaji. Kwanza alianza kwa kuupongeza uongozi wa SIDO kwa kujenga Ofisi hizo ambapo ameagiza kuwepo madarasa maalumu ya mafunzo kwa vitendo. Mhe. Waziri amesema “Uchumi wa Viwanda utajengwa na Viwanda vidogo hivyo Uzinduzi wa ofisi hizi za SIDO ndio chachu ya maendeleo ya Viwanda katika Mkoa wa SIMIYU”. Aidha Mhe. Waziri alitembelea eneo la Viwanda na kukabidhi eneo hilo kwa Mkandarasi ambaye anatakiwa kujenga kwa haraka ili watanzania wapate fursa ya kuanzisha Viwanda.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jingo la ofisi za SIDO Mkoa wa Simiyu.

Pia Waziri alihitimisha ziara yake kwa kuklutana na Viongozi wa Serikali, Vipongozi wa Dini, Viongozi wa Vyama, Wawekezaji na Wafanyabiashara na kuzungumza nao juu ya Serikali ya awamu ya tano ilivyojipanga katika kuendeleza Viwanda nchini. Mhe. Waziri alieleza kuwa, wananchi wa Mkoa wa Simiyu sasa watapata fursa za kuwekeza, kufanya biashara, waatapata ajira pamoja na mikopo nafuu mara baada ya ujenzi wa eneo la Viwanda.

Mhe. Waziri alieleza kuwa kujenga uchumi wa Viwanda ambao ni shughuli ya kiujumla inayomtaka kila mmoja kushiriki katika kuhakikisha tunafanikisha adhma ya kuwa nchi ya Viwanda ifikapo mwaka 2025. Pia aliongeza kuwa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ndiyo injini ya mafanikio katika uchumi kwa vile uchumi wa nchi yoyote hubebwa na Viwanda ambavyo huzalisha bidhaa zitokanazo na malighafi zinazozalishwa sehemu husika na kutumika katika eneo husika.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, akiwa katikla eneo litakalojengwa Viwanda.

Mhe, Waziri amesema kuwa tunataka nchi yetu tujivunie bidhaa zinzozalishwa nchini kwa kuhamasisha kila mwananchi kupenda na kununua bidhaa Bidhaa za Tanzania kwa sasa zinakubalika Supermarket nyingi kwa kuwa zinakidhi ubora kupitia TBS na TFDA, aliongeza kwa kusema kuwa Kiwanda ni uongezwaji thamani kutoka malighafi na kuwa bidhaa ambapo Lengo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ni kuwa na Viwanda vingi vizalishe bidhaa bora ili tuuze katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Mhe. Waziri amesema kuwa Wawekezaji na Wafanyabiashara kujifunza na kuzoea kufanya uwekezaji unaokubalika kisheria (Legal Business Practices) fuateni taratibu za nchi, kulipa kodi zinazowahusu na kuzalisha bidhaa bora na Serikali itasaidia kurahisha shughuli zao.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Viongozi wa dini pamoja, wafanyabiashara na wawekezaji waliohudhuria mkutano huo, pembeni ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Athony Mtaka.

Pia Mhe. Waziri amehimiza Matumizi ya Teknolojia kwa maendeleo ya biashara ambapo amesema ni muhimu kwa wawekezaji hasa wa ndani kwenda sambamba na mahitaji ya teknolojia katika kuzalisha na kuuza bidhaa. Mhe. Waziri amemaliza kwa kusema kusema kuwa Serikali imewekeza nguvu kubwa kwa SIDO katika ujenzi wa Viwanda nchi nzima ambapo Wizara inapokea changamoto mbalimbali zinazokwamisha biashara zao na kuzifanyia kazi kupitia anuani ya dawatilamsaada@mit.go.tz

Mhe. Waziri ataendelea na ziara yake kesho Tarehe 3 Januari, 2018 katika Mkoa wa Geita.
Viongozi wa Serikali na Wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano wa Mhe. Waziri katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambapo mambo mbalimbali yalijadiliwa.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akivalishwa scarf ya heshima kutoka kwa Vijana wa Skauti wa Mkoa wa Simiyu.

WATOTO WANAOELELEWA VITUONI WAASWA KUJITAMBUA

$
0
0
WATOTO wanaolelelewa katika vituo vya kulea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi wametakiwa kujitambua na kujikubali ili kutekeleza wajibu wao wa kupokea malezi mema. Aidha imeelezwa kuwa watoto wanathaminika sana ndio maana wapo watu wameamua kujitolea kuhakikisha wanaishi maisha ya kawaida na kuwa watu muhimu katika jamii. Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, wakati akizungumza na watoto wa wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis hivi karibuni. akimkabidhi Mama mlezi wa kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam, Getrude Nyalubamba (kushoto) akiwa ameongozana na Mwenyekiti kamati ya Msamaria mwema ya kanisa la Ukombozi, Leonard Masano (kulia) walipowasili kituoni hapo kwa ajili ya kukabidhi misaada mbalimbali.[/caption] Mchungaji huyo na kundi la wanawake na wanaume wa kanisa hilo walifika kituoni hapo kutembelea watoto hao na kuwapa zawadi mbalimbali. Alisema katika hafla hiyo kwamba watoto hao wanapojiamini, kujikubali na kujithamini wataona manufaa yake hasa kwa kukubali malezi na kutambua uwepo wa walezi ambao wanajali maslahi yao. Aidha alisema kwamba ni wajibu wa jamii na kanisa kwa ujumla kutekeleza kwa vitendo kujali yatima wajane na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa kuwa kitendo hicho kina Baraka kubwa. Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko (kulia) wa Kanisa la Ukombozi, akibeba gunia la unga kuingiza katika eneo la kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam hivi karibuni. Anayemsaidia ni mmoja wa wakazi wa kituo hicho Elizabeth Samweli anayesoma shule ya sekondari ya Pomerini, Iringa. Wanawake na wababa wa kanisa la Ukombozi walifika kituoni hapo wakiongozwa na mchungaji huyo kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali.[/caption] Alisema kwamba amefurahishwa kufika katika kituo hicho na kutekeleza wajibu wa kukaa pamoja na watoto hao na kumpongeza mama mlezi kwa kazi yake kubwa anayoifanya katika kuwahudumia watoto takribani 31 wanaoishi hapo. Aliwataka watanzania kuwa na tabia ya kujali watoto hao kwa kuhakikisha wanapata mahitaji yao kila siku na sio siku ya sikukuu tu. Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilihamishwa kutoka Stop Over kwenda Mbezi Luishi ili kupisha matakwa ya sheria ya barabara ya Morogoro. 

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

MELI YA WATALII 570 YATIA NANGA BANDARI YA DAR ES SALAAM.

$
0
0
Bodi ya Utalii Tanzania imeshiki kutoa taarifa za utalii wa Tanzania kwa watalii takribani 570 waliowasili kwa meli ya kitalii ya kampuni ya Nautical Majuro katika Bandari ya Dar es Salaam .

Ujio wa Meli hii ya kitalii ni mwendelezo wa juhudi zinazofanywa kwa kushirikiana na wadau wa Utalii wa Tanzania kwa dhamira ya kuwajulisha watalii kutoka katika nchi mbalimbali duniani kuwa wanaweza kuja kuvitembelea vivutio vya utalii vya Tanzania kwa kutumia njia mbali mbali za usafiri (meli, ndege na njia ya barabara).

Watalii hawa wameweza kutembelea Pori la Akiba la Selous, eneo la Mlima Kilimanjaro, Mji wa Kihistoria wa Bagamoyo na jiji la Dar es Salaam.

Meli hii imeanza safari zake katika bara la ulaya imewasili Tanzania tarehe 2/01/2018 saa 2 asubuhi na kuondoka saa moja usiku.
Baadhi ya Watalii wakishuka kutoka kwenye meli ya kitalii ya kampuni ya Nautica Majuro katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mtalii wakipiga picha “Selfie” punde baada ya kuwalisili katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mtalii akicheza ngoma baada kunogewa na mrindimo wa ngoma ya utamaduni wa Tanzania.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images