Na.Vero Ignatus Arusha.
Katibu mkuu baraza la Sanaa Tanzania amewataka wazazi na walezi wa hapa nchini kuwalea watoto na kuhakikisha kuwa wanaishi katika maadili ili kuzuia mmomonyoko wa maadili.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa tamasha la kwanza la Tanzania Tukuza Utalii Genesis 1,Godfrey Ngereza alisema kuwa tanzania imebarikiwa kwa tunu mbali mbali hivyo watanzania hawana budi kuzitunza na kuzilinda.
Aidha alisema kuwa wazazi hawana budi kuwafundisha watoto uzalendo na kuhakikisha kuwa tamaduni zilizopo haziishi."Waswahili walisema samaki mkunje Angali mbichi tukiwalea watoto vizuri ni ngumu kuona maadili yanamomonyoka kwa kuwa tutakuwa tumetengeneza watoto wema" Alisema Godfrey
Kwa upande wake Raisi wa Mtandao wa wasanii wa nyimbo za Injili Tanzania(TAGOANE)Dkt.Godwin Maimu Nnyaka alisema kuwa watoto yatima hawahitaji mavazi na chakula peke yake bali kujengewa msingi bora wa maisha yake.
Katibu mkuu mtendaji Baraza la sanaa nchini( Basata)Godfrey Mngereza akiwa anazungumza katika ufunguzi wa Tamasha hilo.Picha zote kwa Idhini ya Vero Ignatus Blog
Rais wa Mtandao wa Wasanii wa wasanii wa Muziki wa Injili Tanzania na maandili nchini Tanzania (TAGOANE) Dkt.Godwin Maimu akiwa anazungumza katika ufunguzi wa Tamasha la Tukuza utalii Tanzania lililozinduliwa rasmi Jijini Arusha.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu mtendaji kutoka Baraza la sanaa nchini (BASATA) pamoja na Rais wa Tagoane nchini wakikata keki kama ishara ya Ufunguzi wa Tamasha la Kuza Utalii Tanzania .
Mgeni rasmi kutoka Baraza la sanaa la Taifa (Basata)Godrey Mngereza akifurahi pamoja na watoto yatima katika tamasha lililoandaliwa na Tagoane Jiiini Arusha.
Meza kuu Rais wa Tagoane,Katibu Mkuu mtendaji kutoka Baraza la Sanaa nchini (Basata)Katibu mkuu Tagoane,na wakurugenzi wa vituo vya kulelea watoto yatima Jijini Arusha.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog.