Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live

WAFUGAJI WAMUANGUKIA NAIBU WAZIRI ABDALLAH ULEGA WAOMBA SHERIA IREKEBISHWE KWANI INAWAACHA MASIKINI

$
0
0
Na Joel Maduka, Geita

Wafugaji Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita,wamemuomba Naibu waziri wa mifugo na uvuvi,Abdallah Ulega kuingilia kati manyanyaso ambayo wamekuwa wakiyapata kutoka kwa  watu wa maliasili ambao wamekuwa wakichukua mifugo yao na mwisho wa siku kupigwa  mnada bila ya kufikisha mahakamani hali ambayo imekuwa ikiwasababishia umasikini.


Imeelezwa kuwa baadhi ya Minada ya Ng’ombe wanaokamatwa katika Mapori ya Hifadhi imekua ikifanyika kinyume na kwa udanganyifu hasa ambapo katika mnada uliofanyika hivi karibuni Wilayani Bukombe imegundulika katika Ng’ombe waliopigwa mnada 1600 kati yao 500 haijulikani ilipo huku kukiwa na malalamiko mengi kutoka kwa Wafugaji.


Akizungumza kwa niaba ya wafugaji Bw,kwa niaba ya wafugaji Bw,Emmanuel Maricholi wanzake amemweleza naibu waziri kuwa wamekuwa wakikutana na shida kubwa pindi mifugo yao inapokamatwa na kwasasa wafugaji wengi wamefilisika kutokana na hali ya mifugo yao kukamatwa na kupigwa mnada bila ya kuwepo kwa maelewano baina yao na watu wa maliasili na kwamba ni vyema wakaitazama kwa makini sheria ambayo inafanyiwa kazi kwa sasa kwani imewafanya kuwa masikini zaidi.

   
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto  Biteko alisema ana taarifa ya  baadhi ya Watu wanafaidika na Mnada huo kwa manufaa yao wenyewe lakini pia amewataka Wafugaji kuvuta subiri juu ya mabadiliko ya sheria ambayo yanaendelea kwani ukiangali sheria ya Wanyamapori ya Mwaka 2009 ilikua inatoa adhabu ya vitu vitakavyokamatwa katika Mapori ni kutaifishwa na Marekebisho yameplekwa bungeni na ishasomwa mara moja yenyewe inaondoa adhabu ya kutaifisha na badala yake kuna faini.


Aidha,Mh Doto Biteko ameongeza kuwa anatambua  serikali imeendelea kujishughulisha na watu masikini na kwamba ni lazima wafugaji wakaelimishwa hili wajue sheria na wajue kuyatunza mazingira kabla ya kuendelea kuwahukumu kuwa wanaharibu mazingira na kwamba kuna watu ndani ya idara wamekuwa na tabia ya kukamata mifugo kwaajili ya kujipatia fedha hata kabla ya mnada.


Hata hivyo kwa upande wake Naibu waziri wa mifugo na uvuvi,Abdallah Ulega,amewataka wafugaji kutokukataa tamaa na kusubili hadi pale watakapo kuwa wameweka sheria mpya  huku  akivitaka Vyombo vya Dola kuchunguza tuhuma za uendeshaji wa minada ya Ng'ombe na hatua za haraka zichukuliwe kwa wote ambao wamefanya minada hii kujinufaisha na kuwanyanyasa .
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega  akizungumza na wafugaji wa Ng'ombe kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe wakati alipofika kuwasikiliza kilio chao.

Naibu Waziri akifatilia kero mbalimbali ambazo zimetolewa na Wafugaji ikiwemo kukamatwa kwa Ng'ombe zao lakini hawapewi taarifa ya aina yoyote hata wakipelelkwa mahakamani na matokeo yake Ng'ombe zao zinapotea katika mazingira ambayo yanadaiwa ni ya uonevu.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko akizungumza na kuelekezea matatizo ambayo yameendelea kuwakumba wafugaji ambao wapo kwenye jimbo analoliongoza ndani ya wilaya ya Bukombe.

Baadhi ya Ng;ombe ambao wamepigwa mnada.



SALAMU ZA MHE. SPIKA ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA 2018

EFM REDIO YASHEHEREKEA SIKUKUU YA KRISMASI NA WASIKILIZAJI WAKE

$
0
0
 Katika kusheherekea sikukuu ya Krismasi EFM redio imetoa zawadi ya kapu la siku kuu kwa wasikilizaji wake lililosheheni mazagazaga ya chakula pamoja na king’amuzi cha DSTV katika mikoa ya Dar es salaam , Pwani, Mwanza,  Mbeya, Mtwara, na Tanga ikiwaa ni ishara ya kuwajali na kuwathamini katika kipindi hiki cha sikukuu.
 Jumla ya makapu yaliotolewa ni 25 kwa mikoa yote ambapo washindi wa kapu hilo walipatikana kupitia maswali yaliokua yakiulizwa katika vipindi tofauti vya redio hiyo pendwa.
 Washindi wa kapu la sikukuu wakiwa katika picha ya pamoja na zawadi zao ambazo ni kapu lenye kila aina ya chakula ndani pamoja na king’amuzi cha DSTV
 Kulia ni Mkuu wa mawasiliano DSTV Tanzania Bw. Johnson Mshana akielezea jambo kwa mshindi alipokua akikabidhi zawadi
 Meneja matukio wa EFM redio  Bi. Jesca Mwanyika (kushoto) pamoja na mkuu wa mawasiliano DSTV Bw. Johnson Mshana (kulia) wakikabidhi zawadi kwa mshindi wa kapu.
 Mshindi wa kapu la sikukuu kutoka 88.9 Tanga akiwa na kapu lake kutoka Efm redio
Washindi wa kapu kutoka 91.3 Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja na muwakilishi kutoka Efm redio Emanuel Meshack (wa kwanza kushoto)

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII IMEANDAA MKUTANO NA WADAU WA VITALU VYA UWINDAJI WA KITALII MJINI DODOMA, DESEMBA 28

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII IMEANDAA MKUTANO NA WADAU WA VITALU VYA UWINDAJI WA KITALII MJINI DODOMA, DESEMBA 28

TASAF YAWANUSURU WANANCHI WA DONGE VIJIBWENI KISIWANI ZANZIBAR.

$
0
0

NA Estom Sanga-ZANZIBAR

Takribani wananchi 14,420 wa Shehia za Vijibweni ,Mbiji,Karange,Mtambile na Njia ya Mtoni Kisiwani Zanzibar wamepunguziwa adha ya kufuata huduma ya vipimo vya afya mbali na eneo lao baada ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kugharamia ununuzi wa kifaa tiba kilichokosekana tangu kuanza kwa kituo hicho .

Akikabidhi Kifaa hicho kwa uongozi wa kituo cha Afya cha Donge Vijibweni, Naibu Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ Mhe. Mihayo Juma Nung’a amepongeza hatua hiyo ya TASAF ambayo amesema inatekeleza kwa vitendo lengo la serikali la kuwaondolea wananchi kero ya upatikanaji wa huduma mbalimbali ikiwemo ile ya afya.

“ninawaagiza kutunza mashine hii ili wananchi waweze kunufaika kwa muda mrefu na kusahau madhira waliyokumbana nayo kabla ya kupata mashine hiyo” alisisitiza Mhe.Mihayo.

Aidha Naibu Waziri huyo amezungumzia umuhimu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF kuwa ni mkombozi kwa wananchi waliokuwa wanaishi katika umaskini mkubwa na hivyo kuzitaka kaya husika kutumia ruzuku inayotolewa kwa uangalifu huku akitilia mkazo suala la uanzishaji wa miradi ya kiuchumi ili kujiongezea kipato.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ambaye pia alihudhuria hafla ya kukabidhi mashine hiyo amesema taasisi yake itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha maisha ya wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo ile ya afya.

Amesema kwa kutambua umuhimu wa uboreshaji wa afya za wananchi, TASAF imeweka kipengele cha afya kuwa moja ya masharti katika Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambapo watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wanapaswa kuhudhuria kliniki kila mwezi.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kituo hicho Miza Ali Ussi amesema kituo kilikuwa na ukosefu mkubwa wa mashine hiyo na hivyo kuwalazimu wananchi kufuata huduma hiyo katika maeneo yaliyoko mbali na eneo hili jambo lililokuwa linawatatiza kwa kiwango kikubwa. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe.Mihayo Juma Nung’a (aliyevaa shati la drafti) akimkabidhi mashine ya kupimia damu afisa tabibu Miza Ali Ussi wa kituo cha afya cha Donge Vijibweni kisiwani Zanzibar.Kifaa hicho kimenunuliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF-.Kushoto nio Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,bw. Ladislaus 
Mwamanga.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga,(aliyesimama) akizungumza katika hafla ya kukabidhi mashine ya kupimia maradhi kilichonunuliwa na TASAF kwa ajili ya kituo cha Donge Vijibweni kisiwani Zanzibar.Kushoto kwake ni Naibu Waziri katika ofisi ya makamu wa pili wa Rais wa SMZ,Mhe. Mihayo Juma Nung’a.
 Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ,Mhe. Mihayo Juma Nung’a  (hayupo pichani) katika hafla ya kukabidhi mashine ya kupimia maradhi iliyonunuliwa na TASAF kwa ajili ya kituo cha Afya cha Donge Vijibweni huko Zanzibar. 
 Sehemu ya jengo la kituo cha Afya kinachohudumia takribani wananchi 14,420 kilichojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF katika eneo la Donge Vijibweni kisiwani Zanzibar.  

NAIBU WAZIRI SHONZA AFUNGA TAMASHA LA MICHEZO KARATU

$
0
0
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Juliana Shonza (Wa pili kushoto) akipiga risasi hewani kuashiria kuanza kwa mbio za Kilomita kumi wakati wa kufunga Tamasha la Michezo Karatu lililofanyika mjini Karatu tarehe 23/12/2017, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe Teresia Mahongo.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Juliana Shonza akishiriki mbio za Kilomita tano wakati wa kufunga Tamasha la Michezo Karatu lililofanyika mjini Karatu tarehe 23/12/2017. Kutoka Kulia wakwanza ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi. Teresia Mahongo, Afisa Utamaduni na Michezo Ndg.Laurent P. Manonga na wakwanza kulia kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Karatu Ndg. Waziri Mourice.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mhe Juliana Shonza (Wa mbele katikati) akimaliza mbio za Kilomita tano aliposhiriki kufunga Tamasha la Michezo Karatu lililofanyika mjini Karatu tarehe 23/12/2017.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza akimkabidhi  zawadi ya fedha taslimu shilingi laki tano mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita kumi Ndg Emmanuel Giniki wakati wakufunga Tamasha la Michezo Karatu lililofanyika mjini Karatu tarehe 23/12/2017.
 Washiriki wa mbio za kilomita kumi wakijiandaa kutimua vumbi wakati wakufunga Tamasha la Michezo Karatu  lililofanyika mjini Karatu tarehe 23/12/2017.
Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania na Mratibu Mkuu wa Tamasha la Michezo Karatu Ndg. Filbert Bayi akizungumza wakati wa kufunga Tamasha  hilo lililofanyika mjini Karatu tarehe 23/12/2017. Waliokaa wakwanza kulia ni Ndg. Waziri Mourice Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Karatu, wapili ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi Teresia Mahongo na  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza.

WAZIRI MKUU AKEMEA MAKUNDI MANISPAA YA SONGEA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakemea watumishi wa umma na madiwani ambao wameunda makundi ndani ya Manispaa ya Songea kwa kuweka mbele maslahi yao binafsi na akawataka wajirekebishe mara moja.

Ametoa onyo hilo jana (Jumamosi, Desemba 23, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa manispaa na madiwani kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Songea, mjini Songea mkoani Ruvuma.

“Watumishi wa umma ni lazima muelewe kwamba katika Halmashaurti zenu mnafanya kazi na waheshimiwa madiwani sababu mnatekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi, na mnapotekeleza majukumu yenu mzingatie maslahi ya umma. Mnalo jukumu la kuhakikisha Halmashauri yenu inaongozwa kitaalamu,” alisema.

“Nanyi waheshimiwa madiwani, mtambue kuwa mnaongoza wataalamu wa fani tofauti. Lakini hapa Songea, madiwani mmeigawa Halmashauri, mnaiendesha vibaya. Miradi haiendi vizuri kwa sababu mmejiingiza kwenye kujali maslahi yenu binafsi,” alisema Waziri Mkuu.

“Mmebishana sana katika miradi ya maji, ujenzi wa kituo cha mabasi kwa sababu kila mmoja anataka mtu wake aingie. Wakati mwingine pesa zinatumwa, nyie mnaanza kubishana tu, sasa ni mwisho. Mkitaka kutuangusha Serikali, ama tutawafukuza uanachama ama tutavunja Halmashauri. Tunao uwezo wa kulivunja Baraza la Madiwani,” alionya.

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kumpongeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bi. Tina Sekambo kwa uamuzi wake wa kuruhusu mradi mmoja uendelee baada ya kuona kuna malumbano ya kimaslahi miongoni mwa madiwani.

“Mkurugenzi chapa kazi, na usimuogope mtu yoyote, iwe ni Diwani au Mstahiki Meya. Simamia sheria kama ulivyofanya kwenye mradi ambao ulileta maneno, ukaamua Naibu Meya asaini nyaraka, na mradi ukaendelea. Kisheria, Naibu Meya anaruhusiwa kusaini,” alisema.

Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali inakusanya kodi ili wananchi wapate maendeleo na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano haina subira na mtu anayeharibu kazi. Aliwaagiza Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa wasimamie kazi na yeyote atakayeleta uzembe, wamripoti kwake.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuonya Afisa Elimu wa Manispaa hiyo, Bi. Edith Kangomba na kumtaka aache tabia ya kuchochea migomo kwa madiwani.

“Mkurugenzi wa Manispaa mpe taarifa akirudi kwamba tutamfukuza kazi kwa sababu anashirikiana na baadhi ya madiwani kuleta migomo kwenye utekelezaji wa miradi. Mwambie leo ninamuomya, siku nyingine nitamfukuza hapa hapa kwenye kikao,” alielekeza Waziri Mkuu kwa vile Afisa Elimu huyo hakuwepo kwenye kikao hicho kwa sababu yuko likizo.

“Nasema hivi kwa sababu hao washirika wake, wako hapa hapa na wamesikia ujumbe huu. Serikali inahangaika, tunaleta fedha ajili ya elimu, lakini zikifika mnachaguana, na Manispaa yenu iko nyuma kielimu,” alisema.

Aliwataka wakuu wa idara wasimamie idara zao na kuziongoza kwa uadilifu na kuwaeleza kuwa Serikali inatambua upungufu wa watumishi unaozikabili Halmashauri nyingi uliosababishwa na zoezi la uhakiki wa vyeti. “Tunaajiri kidogo kidogo kwa awamu ili kuziba pengo la vyeti feki. Tunajua sekta za afya na elimu ndizo zimeathirika zaidi. Lakini nasisitiza tena, tunataka watumishi waadilifu, waaminifu na wawajibikaji. Endeleeni kuchapa kazi,” alisisitiza.

Waziri Mkuu alimaliza ziara yake ya siku moja mkoani Ruvuma jana hiyohiyo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, DESEMBA 24, 2017

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI

$
0
0
Na.Mwandishi Maalum.

Katika moja ya jitihada za kuhakikisha mafanikio ya mkakati wa kujenga Uchumi wa Viwanda nchini serikali imeendelea Kuboresha mazingira bora ya biashara kwa wawekezaji kwa kuendeleza kilimo ili kuchochea maendeleo na sekta ya kilimo kupitia Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).

Akizungumza baada ziara ya Kukagua shughuli za SAGCOT mkoani Iringa kwa kutembelea kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku Silverlands na kiwanda cha kusindika Maziwa cha Asas Diary Milk, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora alifafanua kuwa njia ya kuliwezesha Taifa kuwa na uchumi imara utakaohimili ushindani katika masoko ya kikanda na kimataifa ni kuboresha mazingira ya Uwekezaji.

“Tunaweka mazingira wezeshi ya kisera na kisheria ili kuhakikisha ukuaji endelevu wa kiuchumi katika sekta ya kilimo hasa kwa kuishirikisha sekta binafsi na kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija, tunao Mpango wa SAGCOT tunataka kutumia fursa hizi katika kilimo kukuza uchumi, tuondokane na kilimo cha kujikimu na kuhamia kilimo biashara. Wawekezaji wanahitaji kuona utayari wa wakulima ili wawekeze. Tukumbuke zaidi ya asilimia 70 ya malighafi za viwanda zinatokana na kilimo”, alisema Kamuzora.

Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa ,Wamoja Ayoub, alifafanua kuwa tayari mkoa huo umeanza kupata mafanikio kwa utekelezaji wa SAGCOT mkoani humo kwa wakulima kuweza kulimochenye tija , kuongeza thamani mazao yao na kupata masoko ya uhakika.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akifurahia maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Geoffrey Kirenga wakati alipotembelea shamba la mahindi la Kiwanda cha Kuzalisha Viranga na chakula cha Kuku, Silverlands mkoani Iringa, wengine ni Mkurugenzi wa Mashamba na Mifugo Kiwanda cha, Rob Nethersole na Mratibu wa SAGCOT Ofisi ya Waziri Mkuu, Girson Ntimba.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha uendelezaji kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Geoffrey Kirenga wakati alipotembelea shamba la mahindi la Kiwanda cha Kuzalisha Viranga na chakula cha Kuku, Silverlands mkoani Iringa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kusindika Maziwa, Asas Diary Milk, Fuad Faraj, wakati alipofanya ziara mkoani Iringa, kukagua viwanda vinavyofanya kazi na Kongani ya Ihemi inayotekelezwa na Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

VIDEO:RPC RUVUMA APIGA MARAFUKU DISKO TOTO .

$
0
0
Jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma limewatahadharisha vijana na makundi mbalimbali kutojihusisha matukio mabaya katika kuelekea sikukuu ya Chrisimasi na Mwaka mpya juu ya matumizi sahihi ya barabara na mali zao,hayo yamesemwa na kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Gimmin Mushy habari kamili hii hapa video yake. 

WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA KUENDELEZA PAMBA

$
0
0
*Aaagiza wahusika wachunguzwe

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuvunja Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza zao la Pamba (CDTF) na amegiza wahusika wote wachunguzwe ili kubaini fedha walizokusanya zimetumikaje.

Alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki (Ijumaa, Desemba 22, 2017) wakati akizungumza na wadau wa zao hilo kwenye kikao alichokiitisha mkoani Shinyanga kufanya ufuatiliaji wa maagizo ambayo alikwishakuyatoa. Waziri Mkuu alishafanya vikao vitatu na wadau mbalimbali wa zao hilo.

Alichukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa watendaji wa mfuko huo hawajatekeleza majukumu ya kuundwa kwa mfuko huo lakini pia majukumu yao yanaingiliana na yale ya Bodi ya Pamba Tanzania (TCB).

“Kuna CDTF katika zao la pamba lakini hakuna inachofanya ambacho kinawalenga wakulima moja kwa moja. Tunaiondoa CDTF na kazi zake kuanzia sasa zifanywe na Bodi,” alisema.

“Waziri wa Kilimo peleka timu ya ukaguzi kuona wamefanya nini hadi sasa. Tunataka Bodi ifanye kazi na iulizwe maswali kuhusu zao hili. Endapo kuna jambo halijafanyika, Bodi iwe na uwezo wa kutoa majibu si kusubiri tena mtu wa chombo kingine aje kutoa majibu,” alisema Waziri Mkuu.

“Kwa muundo huu, Mkurugenzi wa Bodi anakaa tu, wakati akisubiri kazi yake ifanywe na CDTF,” aliongeza.

Mfuko wa CDTF unaundwa na wajumbe sita ambao ni wawakilishi wa wakulima wawili, wawakilishi wa wenye viwanda vya kuchambua pamba wawili, Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba na Mkurugenzi wa Mazao kutoka Wizara ya Kilimo.

Mfuko huu uliundwa mwaka 1999 na Bodi ya Pamba (TCB) ili uwashirikishe wadau wa zao hilo kuondoa matatizo yaliyojitokeza kwenye sekta hiyo baada ya Serikali kujitoa kwenye uendeshaji wa moja kwa moja wa mazao nchini ikiwemo uzalishaji na biashara kutokana na mfumo wa soko huria.

Desemba mwaka jana, Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba alifikia uamuzi kama huo na kuamua kusimamisha shughuli zilizokuwa zinafanywa na Mfuko wa Kuendesha Zao la Korosho Nchini (CIDTF) ili kupisha uchunguzi wa matumizi ya fedha za mfuko huo.

Akitangaza uamuzi huo jijini Dar es Salaam, Waziri Tizeba alisema hatua hiyo ilichukuliwa baada ya mfuko huo kushindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu pamoja na kuwapo kwa malalamiko ya muda mrefu kuhusu utendaji wa mfuko huo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMAPILI, DESEMBA 24, 2017

Maandalizi wa sikuku ya xmass mjini songea leo

$
0
0

 Wananchi wa mji wa Songea wakiwa katika pilika pilika za kununua mahitaji mbalimbali kwenye soko kuu la Songea Mkoani Ruvuma, kuelekea sikukuu za Krismas na Mwaka mpya

WAZIRI JAFO AAHIDI KULIVALIA NJUGA SUALA LA WAKANDARASI NCHINI AMBAO NI WAZEMBE KATIKA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
Na Victor Masangu, Kisarawe
WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo ameahidi kulivalia njuga suala la baadhi ya wakandarasi hapa nchini ambao ni wazembe na wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati waliopangiwa ikiwemo sambamba na watendaji wavivu ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha juhudi za seriklali ya awamu ya tano katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi na badala yake watachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani.
Jafo ametoa kaui hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja katika Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu, miundombinu ya barabaraba, afya pamoja na sekya sambamba na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi ii kuweza kusisikiliza na kizitafutia ufumbufu wa kudumu.
Alisema kwamba alibaini kuna wakandarasi wengine wanapewa kazi lakini cha kushangaza wanakamilisha mradi ambao unajengwa chini ya kiwango kinachotakiwa hivyo amesema kamwe hawezi kulifumbia macho suala hilo na kuongeza kuwa atakayebainika amehusika kuhujumu miradi hiyo atafikishwa mahakamani pamoja na kufukuzwa kazi ii iwe fundisho kwa wengine.
Hata hivyo katika hatua nyingine Jafo aliwatoa wasi wasi wananchi wa Kisarawe, Mkoani Pwani kuimaliza changamoto sugu ya iliyodumu kwa kipindi cha muda mrefu cha ukosefu wa upatikanaji wa huduma ya maji ambapo amebainisha serikali ya awamu ya tano imetenga kiasi cha shilingi bilioni 10 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji ambao chanzo chake kitaanzia mto Ruvu na kusambazwa katika maeneo mbali mbali ya Kisarawe.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Selemani Jafo akikagua daraja la Gologombe ambalo limejengwa katika kata ya mafizi wakati alipofanya ziara yake ya kikazi ya siku moja Wilayani Kisarawe kwa ajili ya kuweza kutembelea miradi mbali mbali ya maenedeleo na kujione a changamoto zilizopo.
Waziri Jafo baada ya kutembelea mradi wa shule ya msingi Mtengwe ambayo kwa sasa inafanyiwa ukarabati wa baadhi ya madarasa ambayo yalikuwa yapo katika hali mbaya kutokana na uchakavu wa miundombinu yake.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Seleman Jafo wa kulia akitoka kukagua mradi wa bwawa kubwa la kuhifadhia maji lililopo kata ya Chole ambalo litaweza kuwanufaisha wakazi wa eneo hilo na maeneo mengine ya jirani kuweza kupata huduma ya maji.PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU.


SALAMU ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA 2018 KUTOKA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

RAIS DKT.SHEIN AWAPA KILA MMOJA KIWANJA NA SH.MILIONI TATU WACHEZAJI WA ZANZIBAR HEROES

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ametoa zawadi ya kiwanja kwa kila mchezaji wa Zanzibar Heroes na shilingi milioni tatu kwa kila mchezaji.

Dkt.Shein ametoa zawadi hizo katika hafla ya kuwapongeza wachezaji wa Zanzibar Heroes baada ya kufanya vizuri katika michuano ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA.

“Mmeonyesha kwamba mnaweza soka katika michuano ya CECAFA, kama serikali inabidi tuwatunuku zawadi, jumla mko thelathini na tatu pamoja na wachezaji na viongozi wa timu, kwa hiyo natoa pesa shilingi milioni tatu kwa kila mchezaji na viongozi wenu pamoja na kiwanja kwa kila mchezaji na kiongozi, na viwanja vyote vitakuwa sehemu moja mtaanzisha kijiji chenu,” amesema Shein

Zanzibar Heroes walimaliza katika nafasi ya pili katika michuano ya CECAFA, huku wakiwa na rekodi nzuri baada ya kumtoa bingwa mtetezi Uganda na kuwafunga ndugu zao Kilimanjaro Stars.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akizungumza wakati wa hafla ya Chakula cha usiku aliowaandalia Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes, iliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni na kuwazawadia Fedha na Viwanja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi cheti ya shilingi miliono tatu Mchezaji wa Timu ya Zanzibar Heroes Ibrahim Hamad Hilika,
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheki ya shilingi milioni Tatu Nahodha Timu ya Zanzibar Heroes Suleiman Kassim Selembe, wakati wa hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar katika ukumbi wa Zamani wa Baraza Kikwajuni
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheki Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes Abdulazizi Makame, wakati wa hafla ya chakula cha usiku katika ukumbi wa Zamani wa Baraza Kikwajuni
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi cheki Kocha Mkuu wa Timu ya Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Moroco
BAADHI ya Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa kukabidhi zawadi kwa Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes katika ukumbi wa zamani wa baraza kikwajuni Zanzibar
WACHEZAJI wa Timu ya Zanzibar Heroes wakifuatilia hafla hiyo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikabidhi Jezi ya Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes na Nahodha wa Timu hiyo Suleiman Kassim Selembe, wakati wa hafla maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar kuwazawadi zawadi wachezaji hao katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni.
KOCHA Mkuu wa Timu ya Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Moroco, akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati wa hafla maalumu ilioandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi kikwajuni Zanzibar.Picha na Ikulu


NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, JAPHET HASUNGA AMEIAGIZA TFS KUANZA MCHAKATO WA KUUNDA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA MISITU TANZANIA

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ianze mchakato wa kuandaa sheria ya kutoka Wakala kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Misitu Tanzania ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa vile ikiendelea kubaki kuwa Wakala kuna baadhi ya mambo itashindwa kuyashughulikia

Wakala ni Idara za Serikali zilizoondolewa kwenye serikali kuu na zina nusu mamlaka na hazina mamlaka kamili ya kujiamulia mambo yake zenyewe.Amesema uanzishwaji wa Mamlaka hiyo itasaidia kupunguza migongano kati ya misitu iliyo chini ya Tamisemi pamoja na vijiji kwa vile kutakuwa na Mamlaka moja ya kusimamia misitu tofauti na ilivyo sasa.

Ameyasema hayo jana wakati akizungumza na Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzani (TFS) makao makuu jijini Dar es Salaam.Amesema TFS kwa hatua iliyofikia kwa sasa haistahili kuwa Wakala kutokana na kazi kubwa iliyonayo hivyo inahitaji kuwa Mamlaka ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa uhuru zaidi.

Wakati akizungumza na Watumishi, Naibu Waziri Hasunga amemtaka Mtendaji Mkuu wa TFS, Dos Santos Silayo ahakikishe katika mpango mkakati utakaoandaliwa hivi sasa suala la uanzishwaji wa Mamlaka lipewe kipaumbele.Katika hatua nyingine, Ameiagiza TFS iunde chombo cha kusimamia na kudhibiti ubora wa mazao ya misitu.

Amesema chombo hicho kitakuwa kikipanga mazao ya misitu kulingana na ubora wake na sio kama sasa inavyofanyika mbao zozote zile zimekuwa zikiuzwa sokoni pasipo kujali ubora wake.Amesema kuna changamoto ya bei za mbao sokoni na pia kuna changamoto ya ubora wa mbao zilizoko sokoni, Mbao nyingi zimetengenezwa kwa miti ambayo imevunwa ikiwa na miaka sita au kumi ni lazima ubora wake uwe hafifu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na  Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) makao makuu jijini Dar es Salaam jana . Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa TFS, Dos Santos Silayo
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki Dkt. Ezekiel Mwakalukwa (kulia) akizungumza na Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) kuzungumza na Watumishi wa TFS makao makuu jijini Dar es Salaam jana .
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Dos Santos Silayo akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga baada ya kuzungumza na Watumishi wa TFS makao makuu jijini Dar es Salaam jana .
Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam. (Picha na Lusungu Helela-MNRTBaadhi ya Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam.
Picha na Lusungu Helela-MNRT


DKT MWANJELWA AWATAKA WAKUFUNZI WA VYUO VYA KILIMO NCHINI KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA

$
0
0
Na Mathias Canal, Mtwara

Wakufunzi wa Vyuo vya Kilimo kote nchini wametakiwa kutofanya kazi kwa mazoea badala yake kufanya kazi kwa Weledi, Ubunifu na Maarifa ili kuongeza tija katika majukumu yao ya kufundisha wanafunzi ambapo baadae wanazalisha wataalamu mbalimbali katika sekta ya Kilimo.

Kauli hiyo imetolewa juzi 22 Disemba 2017 na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati akizungumza na Wakuu wa Idara na Wafanyakazi wa Chuo cha Kilimo (MATI) Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini.

Alisema kuwa watendaji hao wanapaswa kuwa wabunifu katika nyanja mbalimbali zitakazowawezesha kuwa na kipato cha ziada kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni.

Alisema kuwa kufanya hivyo kutawanufaisha kuwa na kipato kitakachowawezesha kuendesha chuo pasina kutegemea serikali kwa kina jambo ambalo litapunguza malalamiko dhidi ya serikali kufanya kila kitu.

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Kitalu Nyumba (Green House) katika ziara yake ya kikazi alipotembelea Chuo cha Kilimo Mtwara Kilichopo katika kijiji ch a Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kilimo Mtwara Ndg Elias L. Maijo, Juzi 22 Disemba 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mashamba mbalimbali ya uzalishaji wa mazao ya kilimo katika ziara yake ya kikazi alipotembelea Chuo cha Kilimo Mtwara Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Juzi 22 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na Wakuu wa Idara na Wafanyakazi wa Chuo cha Kilimo (MATI) Mtwara Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Juzi 22 Disemba 2017.

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo mara baada ya kukagua mashamba mbalimbali ya uzalishaji wa mazao ya kilimo katika ziara yake ya kikazi alipotembelea Chuo cha Kilimo Mtwara Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Juzi 22 Disemba 2017.

JAFO APONGEZA KAMATI YA UJENZI WA MIRADI ZA VIJIJI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo amezipongeza kamati zinazosimamia ujenzi wa miradi kwa kutumia utaratibu wa ‘Force Account’ hapa nchini kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo yenye ubora na inayozingatia thamani ya fedha.

Jafo alitoa pongezi hizo alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo wilayani Kisarawe ambapo alifanikiwa kukagua ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule za msingi Mitengwe, Kitonga Mango, Boga, mapoja na kituo cha Afya Maneromango.

Amesema ujenzi huo umetumia utaratibu huo wa ‘Force Account’ ambapo miundombinu mbalimbali imejengwa kwa gharama nafuu pamoja na kutoa ajira kwa mafundi wanaopatikana katika maeneo miradi hiyo inapotekelezwa. Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amefanikiwa pia kukagua jengo jipya la upasuaji, maabara, wodi ya kinamama, nyumba ya daktari, jengo la kuhifadhi maiti, vyumba 12 vya madarasa mapya, matundu ya vyoo 30, pamoja na Ofisi za walimu 3.

Mbali na hilo, Waziri Jafo amekagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Kwala-Chole ambao unagharimu zaidi ya sh. billion 1.8 na ameagiza mradi huo ukamilike ifikapo mwishoni mwa mwezi Machi 2018. Amewataka wananchi kote nchini kushiriki kulinda na kusimamia rasilimali fedha zinazopelekwa katika vijiji vyao kwaajili ya maendeleo.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa ameambatana  na viongozi wa wilaya ya Kisarawe katika ukaguzi wa mradi wa maji Kwala-Chole.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Kisarawe wakikagua ujenzi unaoendelea wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Mitengwe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akikagua nyumba ya daktari ambayo ipo kwenye hatua za mwisho za ujenzi katika kituo cha Afya Maneromango.
Baadhi ya miondombinu iliyojengwa kwenye Kituo cha Afya Maneromango.

WAZIRI MKUU AKEMEA MAKUNDI MANISPAA YA SONGEA

$
0
0
Ataka madiwani, watumishi wajali maslahi ya wananchi
Aonya wasipojirekebisha, Serikali itavunja Baraza la Madiwani

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakemea watumishi wa umma na madiwani ambao wameunda makundi ndani ya Manispaa ya Songea kwa kuweka mbele maslahi yao binafsi na akawataka wajirekebishe mara moja.
Ametoa onyo hilo jana (Jumamosi, Desemba 23, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa manispaa na madiwani kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Songea, mjini Songea mkoani Ruvuma. 
“Watumishi wa umma ni lazima muelewe kwamba katika Halmashaurti zenu mnafanya kazi na waheshimiwa madiwani sababu mnatekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi, na mnapotekeleza majukumu yenu mzingatie maslahi ya umma. Mnalo jukumu la kuhakikisha Halmashauri yenu inaongozwa kitaalamu,” alisema. 
“Nanyi waheshimiwa madiwani, mtambue kuwa mnaongoza wataalamu wa fani tofauti. Lakini hapa Songea, madiwani mmeigawa Halmashauri, mnaiendesha vibaya. Miradi haiendi vizuri kwa sababu mmejiingiza kwenye kujali maslahi yenu binafsi,” alisema Waziri Mkuu. 
“Mmebishana sana katika miradi ya maji, ujenzi wa kituo cha mabasi kwa sababu kila mmoja anataka mtu wake aingie. Wakati mwingine pesa zinatumwa, nyie mnaanza kubishana tu, sasa ni mwisho. Mkitaka kutuangusha Serikali, ama tutawafukuza uanachama ama tutavunja Halmashauri. Tunao uwezo wa kulivunja Baraza la Madiwani,” alionya. 
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kumpongeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bi. Tina Sekambo kwa uamuzi wake wa kuruhusu mradi mmoja uendelee baada ya kuona kuna malumbano ya kimaslahi miongoni mwa madiwani. 
“Mkurugenzi chapa kazi, na usimuogope mtu yoyote, iwe ni Diwani au Mstahiki Meya. Simamia sheria kama ulivyofanya kwenye mradi ambao ulileta maneno, ukaamua Naibu Meya asaini nyaraka, na mradi ukaendelea. Kisheria, Naibu Meya anaruhusiwa kusaini,” alisema.

Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali inakusanya kodi ili wananchi wapate maendeleo na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano haina subira na mtu anayeharibu kazi. Aliwaagiza Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa wasimamie kazi na yeyote atakayeleta uzembe, wamripoti kwake. 
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuonya Afisa Elimu wa Manispaa hiyo, Bi. Edith Kangomba na kumtaka aache tabia ya kuchochea migomo kwa madiwani. 
“Mkurugenzi wa Manispaa mpe taarifa akirudi kwamba tutamfukuza kazi kwa sababu anashirikiana na baadhi ya madiwani kuleta migomo kwenye utekelezaji wa miradi. Mwambie leo ninamuomya, siku nyingine nitamfukuza hapa hapa kwenye kikao,” alielekeza Waziri Mkuu kwa vile Afisa Elimu huyo hakuwepo kwenye kikao hicho kwa sababu yuko likizo. 
“Nasema hivi kwa sababu hao washirika wake, wako hapa hapa na wamesikia ujumbe huu. Serikali inahangaika, tunaleta fedha ajili ya elimu, lakini zikifika mnachaguana, na Manispaa yenu iko nyuma kielimu,” alisema. 
Aliwataka wakuu wa idara wasimamie idara zao na kuziongoza kwa uadilifu na kuwaeleza kuwa Serikali inatambua upungufu wa watumishi unaozikabili Halmashauri nyingi uliosababishwa na zoezi la uhakiki wa vyeti. “Tunaajiri kidogo kidogo kwa awamu ili kuziba pengo la vyeti feki. Tunajua sekta za afya na elimu ndizo zimeathirika zaidi. Lakini nasisitiza tena, tunataka watumishi waadilifu, waaminifu na wawajibikaji. Endeleeni kuchapa kazi,” alisisitiza.Waziri Mkuu alimaliza ziara yake ya siku moja mkoani Ruvuma jana hiyohiyo.

 Watumishi wa manispaa na madiwani manispaa ya Songea mkoani Ruvuma  wakimsikiliza Waziri Mkuu Mhe.  Kassim Majaliwa  kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Songea, mjini Songea Mkoani Ruvuma
Waziri Mkuu Mhe.  Kassim Majaliwa  akizungumza na watumishi wa manispaa na madiwani wa Songea kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Songea, mjini Songea Mkoani Ruvuma

MAPOKEZI YA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR LEO UKUMBI WA CCM MKOA WA MJINI AMAAN UNGUJA

$
0
0
 MAKAMU Mwenyekiti  wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Talib Ali Talib, alipowasili katika viwanja vya Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani wakati wa mapokezi yake.
wa Mjini Amaan
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akifungwa kiskafu na Vijana wa Chipukizi wa Mkoa wakati wa mapokezi yake alipowasili katika Viwanja vya Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amaan
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiangalia ngoma ya kibati wakati wa mapokezi yake yalioandaliwa katika viwanja Afisi Kuu ya CCM Mkoa wa Mjini Amani, baada ya kuwasili Zanzibar wiki iliopita akitokea Dodoma katika Mkutano Mkuu wa CCM na kuchaguliwa tena kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar kwa kura nyingi.
 WANACHAMA wa CCM wa Mikoa ya Zanzibar wakimpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, alipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani wakati wa mapokezi yake.
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa CCM meza kuu wakisimama baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA


Viewing all 110021 articles
Browse latest View live




Latest Images