Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

MKURUGENZI DODOMA KUWAKATIA BIMA YA AFYA 133 WANAOSAFISHA BARABARA MJINI, AWAPA ZAWADI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA

0
0
NA RAMADHANI JUMA,OFISI YA MKURUGENZI

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi ameahidi kuwakatia Bima ya Afya wafanyakazi 133 wanaosafisha mitaa na barabara zote za Mji wa Dodoma ili wawe na uhakika wa matibabu wao na familia zao.

Alitoa ahadi hiyo jana alipofanya mkutano na wafanyakazi hao katika viwanja vya Nyerere katikati ya Mji wa Dodoma ambapo pia aliwapatia fedha taslimu Shilingi 10,000 na mche mmoja wa sabuni kila mmoja kama zawadi kuelekea mwisho wa mwaka 2017.

Mkurugenzi Kunambi alisema kuwa, yeye kwa niaba ya Uongozi wa Manispaa ametoa zawadi na ahadi ya kuwakatia Bima ya matibabu baada ya kufurahishwa na uchapa kazi wao unaopelekea mitaa na barabara za Mji kuwa safi na kupendeza muda wote.

“Hiki tunachowapa leo hakina thamani yeyote kwa kazi kubwa mnayoifanya, bali ni kuonesha kuguswa kwetu tu kama Manispaa…ninyi ni kundi maalum na ni wafanyakazi muhimu sana” alisema Kunambi akizungumza na watumishi hao.

“Nimefurahi kukutana na kuzungumza na ninyi kipindi hiki cha mwisho wa mwaka…nawaahidi mapema mwakani Manispaa itawakatika Bima za Afya wote itakayomwawezesha kila mmoja kutibiwa yeye na wategemezi wake watatu” alifafanua.

Kwa upande wao, wafanyakazi hao ambao wengi wao ni akina Mama walimshukuru Mkurugenzi huyo kwa niaba ya Manispaa kwa kuwajali licha ya kuwa wao ni watumishi wa kada ya chini na wanaofanya kazi kwa mkataba isiyo ya kudumu.

“Tumefurahi sana leo Mkurugenzi wetu umekuja kuongea na sisi na kutupa zawadi na fedha tena katika kipindi cha Sikukuu za mwisho wa mwaka…umetujali sana na sisi tunakuombea kwa Mugu”… alisema mmoja ya akia mama hao akimshukuru Mkurugenzi wa Manispaa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (kulia) akimkabidhi mche wa sabuni mmoja ya wafanyakazi wanaosafisha barabara na mitaa mbalimbali ya Mji wa Dodoma mara baada baada ya kuzungumza na wafanyakazi hao katika Viwanja vya Nyerere Mjini Dodoma jana. Mkurugenzi huyo aliwapatia wafanyakazi hao wapatao 133 zawadi ya Shilingi 10,000 na Mche mmoja wa sabuni kila mmoja ikiwa ni motisha hususan katika kipindi hiki cha Sikukuu za mwisho wa Mwaka.
Baadhi ya wafanyakazi wanaosafisha Barabara na Mitaa mbalimbali ya Mji wa Dodoma wakifurahia hotuba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (hayupo pichani) wakati alipofanya nao mkutano katika Viwanja vya Nyerere Mjini Dodoma jana.
Mkuu wa Idara ya Mazingira na Usafishaji Manispaa ya Dodoma Dickson Kimaro (kushoto) akizungumza na wafanyakazi wanaosafisha barabara na mitaa mbalimbali ya Mji wa Dodoma kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Godwin Kunambi (katikati) kuzungumza na wafanyakazi hao. kulia ni msimamizi wa wafanyakazi hao John Lugendo.
Wafanyakazi 133 wanaosafisha barabara na mitaa mbalimbali ya Mji wa Dodoma wakikabidhiwa Fedha taslim Shilingi 10,000 na mche wa sabuni kila mmoja ikiwa ni zawadi ya motisha iliyotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (hayupo pichani) jana katika Viwanja vya Nerere Mjini Dodoma. Wanaokabidhi ni Mkuu wa Idara ya Mazingira na Usafishaji Manispaa ya Dodoma Dickson Kimaro (wa pili waliokaa) na Afisa Mazingira ambaye ni Msimamzi wa Wafanyakazi hao John Lugendo (wa kwanza waliokaa).
Sehemu ya wafanyakazi wanaosafisha Barabara na Mitaa mbalimbali ya Mji wa Dodoma wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (hayupo pichani) wakati alipofanya nao mkutano katika Viwanja vya Nyerere Mjini Dodoma jana. Kando ni maboksi ya sabuni ambapo kila mmoja alizawadia mche mmoja na fedha taslimu Shilingi 10,000 na Mkurugenzi huyo huku akiwaahidi kuwakatia Bima ya Afya. 
PICHA: RAMADHANI JUMA-OFISI YA MKURUGENZI


MAHAFALI YA 16 YA CHUO KIKUU MZUMBE KAMPASI YA DAR

0
0

Mlau, Prof. Binamungu akiongoza maandamano kuelekea sehemu ya mahafali.

Baadhi ya wahitimu wa shahada mbalimbali wakiwa katika mahafali hayo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam.

Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Lucy Massoi, akiwatambua wanachuo na wahadhiri waliofanya vizuri.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Jaji mstaafu, Barnabas Samatta, akimkabidhi cheti mmoja wa wanachuo aliyefanya vizuri, Gloria Mbigiri wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Jaji mstaafu, Barnabas Samatta, akimkabidhi cheti mmoja wa wanachuo aliyefanya vizuri, Elihuruma Mabelya wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

DK MNDOLWA KULIPA MADENI YA WATENDAJI JUMUIYA YA WAZAZI NDANI YA SIKU 100 [19:04, 12/23/2017] Yassir:

0
0
Na Said Mwinshehe-Globu ya Jamii.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Dk.Edmund Mndolwa amesema ndani ya siku 100 kuanzia jana atahakikisha analipa madeni yote wanayodai watendaki wa jumuiya hiyo huku akitoa onyo kwa wale wenye tabia ya kutengeneza makundi.

Amesema hayo wakati anazungumza na Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kumpokea rasmi ambapo amesisitiza kusimamia vema majukumu yake kwa maslahi ya jumuiya na CCM kwa ujumla.

Kuhusu madeni,amesema anatambua changamoto zilizopo ikiwamo ya watendaji wa ngazi mbalimbali kudai fedha zao lakini hilo atalishughulikia ndani ya siku 100 kwani fedha zipo."Najua changamoto zilizopo kwenye jumuiya yetu,nitumie nafasi kuwahakikishia watendaji wanaodai ndani ya siku 100 tutalipa madeni yote.

" Nitaboresha maslahi na kubwa zaidi tutanunua vitendea kazi kwani vilivyopo vimechakaa na viachache.Lengo na kuifanya jumuiya yetu kutimiza majukunu yake na tutaendelea kujiimarisha hatua kwa hatua,"amesema.Ametumia nafasi hiyo kuelezea kusikitishwa kwake na tabia ya uwepo wa makundi ambayo kimsingi hayana nia njema zaidi ya  kukiharibu chama chao ,hivyo lazima wakomeshe makundi .

"Atakayebainika anajihusisha na makundi atachukuliwa hatua,sisi ni wamoja na lazima tusimame katika hilo.Chaguzi zimekwisha ndani ya jumuiya ,sasa tufanye kazi," amesema Dk.Mndolwa.Ametoa onyo kuhusu tabia ya watu kuwa na tabia ya kuzungumzia mambo ya jumuiya na chama bila kufuata utaratibu.

Hivyo amesema lazima anayetaka kuzungumza basi ahakikishe anatumia vikao halali ambapo atajenga hoja na kusikilizwa."Atakayezungumza bila kufuata utaratibu hatutamuacha,lazima kanuni na taratibu ziheshimiwe na kila mmoja wetu,"amesisitiza.

MAJALIWA AZIAGIZA HALMASHAURI ZA WILAYA NCHINI KUSIMAMIA KILIMO CHA ZAO LA PAMBA ILI LIWE NA TIJA

0
0
Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi Kishapu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameziagiza halmashauri za wilaya nchini kuhakikisha zinasimamia kikamilifu kilimo cha zao la pamba ili kiwe na tija.

Ametoa agizo hilo katika kikao na wadau wa pamba kilichofanyika mjini Shinyanga ambapo alizitaka halmashauri hizo kuratibu shughuli za kilimo hicho kwa kuwapangia ratiba maafisa ugani kuwatembelea wakulima kuwapa elimu.

Akizungumza katika kikao hicho kilichoikutanisha mikoa zaidi ya 10 inayolima pamba aliwataka watendaji wakuu wa halmashauri hizo kuhakikisha kila kata na kijiji kunawepo na maafisa ugani ili wasimamie kikamilifu kilimo.

Majaliwa aliwataka maafisa ugani waliopo katika halmashauri hizo kuwafikia wakulima mashambani ili kuwapa elimu na kutatua changamoto zinazowakabili kuhusu kilimo hususan cha pamba.“Tunataka kuhahakikisha pamba inaleta heshima na inaongeza mapato ya mkulima mmoja mmoja na hata taasisi zetu yaani halmashauri na mikoa zinaingiza mapato kupitia zao la pamba hivyo kila mmoja awajibike,” alisisitiza.

Pia, aliagiza pia ziweke mpango kazi wa namna ya kukiletea mafanikio kilimo hicho huku akisisi kuwa na kwamba atafanya ziara kukagua akisema atataka apewe taarifa ya maendeleo ya kilimo hicho.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao na wadau wa pamba kilichofanyika mjini Shinyanga. Wengine picha ni kuanzia kushoto ni Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba.
Sehemu ya wakuu wa mikoa inayolima zao pamba wakifuatilia matukio katika kikao cha wadau wa pamba kilichofanyika mjini Shinyanga
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati mwenye miwani) akifurahia wimbo na viongozi wengine mara baada ya kuwasili ukumbini kwa ajili ya kikao hicho. Wengine pichani kuanzia kushoto ni Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.

Wakuu wa wilaya za Shinyanga ambazo ndizo miongoni mwa wakulima wa pamba, kuanzia kushoto ni Fadhil Nkurlu (Kahama), Nyabaganga Taraba (Kishapu) na Josephine Matiro (Shinyanga) na kulia pichani Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi wakifuatilia matukio.
Sehemu ya wakuu wa mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza kwenye kikao cha wadau wa pamba kilichofanyika mjini Shinyanga.

SERIKALI YATOA SIKU SABA MKANDARASI WA BWAWA LA RUNGWA-ITIGI, KULETA VIFAA MUHIMU VA UJENZI

0
0
Mkandarasi anayejenga bwawa la Rungwa katika Halmashauri ya Itigi amepewa siku saba na Serikali Mkoani Singida kuhakikisha anapeleka vifaa muhimu vitakavyoongeza kasi na ufanisi wa ujenzi wa bwawa hilo.

Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Serikali za Mitaa Mwajabu Nyamkomola ametoa agizo hilo mapema jana mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa hilo na kukuta ukiwa katika asilimia 35 wakati ulitakiwa kuwa asilimia 60 huku baadhi ya vifaa muhimu vikikosekana.

Nyamkomola amemueleza Mhandisi mwakilishi wa kampuni ya Proactive Independent Group Ltd Elias Gamba kuwa wananchi wa Rungwa hawana maji na juhudi za serikali kuwapatia maji kupitia mradi huo wenye thamani ya zaidi ya milioni mia saba unatakiwa kufanyika kwa kasi na ufanisi wa hali ya juu.

Ameeleza kuwa baada ya kufanya ukaguzi katika bwawa hilo wamebaini kuwa baadhi ya kazi zimekuwa zikifanywa kwa kasi ndogo kutokana na kutokuwepo kwa mashine na badala yake kazi hizo kufanywa na vibarua huku vifaa vingine vikiwa pungufu tofauti na makubaliano katika mkataba.
Mhandisi wa Maji Mkoa wa Singida Lydia Joseph (aliyevaa kofia nyeupe) akiendelea na ukaguzi wa bwawa la Rungwa-Itigi, nyuma yake ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Serikali za Mitaa Mwajabu Nyamkomola.
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Serikali za Mitaa Mwajabu Nyamkomola akiwa na watendaji wa serikali na wawakilishi wa Mkandarasi wa bwawa la Rungwa wakitembelea eneo la Bwawa hilo mapema jana.
Baadhi ya vibarua wakiendelea na zoezi la kuchanganya zege kwa ajili ya ujenzi wa ukuta katika bwawa la Rungwa – Itigi, Serikali Mkoani Singida imeagiza kazi hio ifanywe na mashine ili kuleta ufanisi na kasi huku vibarua hao wakitakiwa kuendelea na kazi nyingine katika bwawa hilo.
Sehemu ya Bwawa la Rungwa –Itigi linalojengwa na serikali kwa zaidi ya shilingi milioni mia saba ili kutatua kero kubwa ya maji katika kijiji cha Rungwa.


WAZIRI MKUU AWATOA HOFU WAKAZI WA SONGEA

0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatoa hofu wakazi 1,000 wa Manispaa ya Songea wanaoidai fidia ya sh. bilioni 3.8 ya eneo lao ambalo limechukuliwa na kuwa eneo la kiuchumi mkoani Ruvuma (Ruvuma SEZ) kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.

Ametoa ahadi hiyo leo (Jumamosi, Desemba 23, 2017) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mwengemshindo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Manispaa hiyo.Amesema Serikali ya awamu ya tano inatambua kilio chao ambacho alisema ni cha muda mrefu na kwamba alishawahi kupata ombi maalum kutoka kwa mbunge wao wa zamani, Bw. Leonidas Gama ambaye sasa ni marehemu.

“Alipotoka kutibiwa India alikuaja ofisini kwangu na kunieleza kwamba ana mambo mawili ambayo nikifanya ziara mkoani Ruvuma anaomba niyatafutie ufumbuzi. La kwanza lililkuwa ni hili la fidia kwa wakazi wa Mwengemshindo na la pili lilikuwa ni la ujenzi wa kituo cha mabasi cha mabasi cha mjini Songea,” alisema.

“Leo nimefanya ziara maalum kwa ajili yenu kwa sababu serikali ya awamu ya tano iko kwa ajili yenu na hasa wananchi wanyonge. Na tatizo hili inalijua. Kabla sijafika hapa, nilipita kwenye eneo husika na afisa mipango miji akanionyesha ramani ya eneo lenu hili,” alisema.

Waziri Mkuu aliwaeleza wakazi hao kwamba eneo hilo limetengwa na Manispaa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda ambapo wawekezaji watatu tayari wamekwishajitokeza na wanataka kujenga viwanda vitatu. “Kutakuwa na kiwanda cha kusindika mahindi, kutengeneza pumba za kuku na ng’ombe na mbolea. Kiwanda cha pili kitakuwa ni cha kusindika kahawa na cha tatu kitakuwa ni cha kukamua mafuta ya mbegumbegu,” alisema na kuongeza kwamba reli ya kutoka Mtwara kwenda Mbaba Bay inatarajiwa kupita kwenye eneo hilo. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia wakazi wa kata ya Mwengemshindo katika Manispaa ya Songea leo Desemba 23, 2017 ambako alienda kusikiliza kero yao ya muda mrefu ya kutolipwa fidia.
Mkazi wa Msamala katika Manispaa ya Songea, Bibi Monica Joseph Miti akitoa maelezo yake mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mwengemshindo. Bibi Miti aliomba asaidiwe kurejeshewa nyumba yake aliyotapeliwa na mtumishi wa Manispaa hiyo baada ya mumewe kufariki.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


HAFLA YA UZINDUZI WA KITABU CHA SOTE TUNAWEZA ILIVYOBAMBA DAR

0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave-Maria Semakafu (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi Kitabu cha 'Sote Tunaweza', wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika kwenye Bustani ya Target Mbezi Beach Dar es Salaam, jana usiku. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Viva Legancy Ltd, Fortunata Temu (kulia) ni Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, Gaudence Temu. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Viva Legancy Ltd, Fortunata, akizungumza jinsi alivyoweza kuandaa, kuandika hadi kuprinti kitabu hicho pamoja na changamoto alizopitia hadi kukamilika.
Dkt. Ave-Maria Semakafu, akikielezea kitabu hicho jinsi kilivyosheheni masuala mbalimbali yanayohusu fursa na hasa kwa vijana.
Baadhi ya Warembo wa Kampuni hiyo waliokuwapo katika hafla hiyo kuhakikisha kila jambo linakwenda sawa.

“VIONGOZI WA DINI WASIKATISHE TAMAA WAUMINI KUKABILI UKIMWI”- DK. MABOKO

0
0
VIONGOZI wa madhehebu mbalimbali ya kidini wameombwa kusaidia kuondoa unyanyapaa wa wagonjwa wa Ukimwi ikiwa ni sehemu kamili ya kukabiliana na janga hilo nchini. Aidha wametakiwa kutumia program mbalimbali walizonazo katika mahubiri na kazi zao kuhakikisha kwamba taifa haliwi na maambukizi mapya ya Ukimwi na wale waliokuwa nao wanathaminika.
 Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko katika mkutano wa kuimarisha uratibu wa Afua za Ukimwi katika Taasisi za Kidini uliofanyika Chuo cha Maendeleo na Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo. Alisema wakati taifa linapata maambukizi mapya 81,000 kwa mwaka, si sahihi kwa viongozi hao wa kidini kuupambanisha ugonjwa huo na mshahara wa dhambi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akizungumza wakati akifungua mkutano wa kuimarisha uratibu wa Afua za Ukimwi katika Taasisi za Kidini uliofanyika Chuo cha Maendeleo na Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo.(Picha zote na The Beautytz)
Alisema pamoja na ukweli kuwa mshahara wa dhambi ni mauti, lakini ni kweli pia kwamba wapo ambao wanapata ugonjwa huo bila wao kufanya chochote kile. “Mke yupo nyumbani, mme anachepuka na kuleta ukimwi nyumbani kwa mama… kama tukisema Ukimwi ni dhambi, huyo mama ana dhambi yake nini? Na mtoto aliyezaliwa na Ukimwi, tatizo la mtoto nini?” aliuliza Mkurugenzi akisisitiza haja ya kuondokana na unyanyapaa na kusaidia kwa pamoja kukabiliana na janga hilo. Unapotoa hotuba na kusema kwamba utakufa na Ukimwi wako, haitoi tumaini kwa mgonjwa na wewe unaweza kuwa sababu ya yeye kuamua kuambukiza watu zaidi alisema Mkurugenzi huyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akizungumza na washiriki wa mkutano wa kuimarisha uratibu wa Afua za Ukimwi katika Taasisi za Kidini uliofanyika Chuo cha Maendeleo na Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo.
 “madhehebu yana nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko katika shughuli za Ukimwi” anasema Mkurugenzi na kuongeza kuwa yuko katika mapambano na Ukimwi kwa miaka 22 na ana kila sababu ya kusema kwamba madhehebu ya dini yana mchango mkubwa katika kampeni dhidi ya Ukimwi. Anasema akiwa mchungaji (alitolewa katika kazi hiyo) anaamini ipo haja ya kuwapo na mabadiliko ikiwa mapambano hayo yanatakiwa yafanikiwe. Mwakilishi wa UNESCO katika mkutano huo, Herman Mathias ambaye pia ni Mratibu wa Ukimwi Unesco akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kuimarisha uratibu wa Afua za Ukimwi katika Taasisi za Kidini uliofanyika Chuo cha Maendeleo na Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo uliofadhiliwa na UNESCO.
Katika mkutano huo ambao umefadhiliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) alisema kwa muda sasa imekuwa ukisimama na kutaja Ukimwi unaonekana kama umetaja dhambi hali ambayo inaongeza unyanyapaa na pia kuwafanya watu wasiwe wa wazi na afya zao. Aidha alisema kwamba kwa sasa kuna tatizo la wanaume wengi kutopima afya zao na hata wakipima hawafuati maelekezo na wanakuwa wa kwanza kufa kutokana na kushindwa kutumia dawa inavyotakiwa. Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mwitikio wa Kitaifa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Audrey Njelekela akizungumza kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika kuleta mabadiliko ya mapambano dhidi ya Ukimwi kwenye mkutano wa kuimarisha uratibu wa Afua za Ukimwi katika Taasisi za Kidini uliofanyika Chuo cha Maendeleo na Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo kwa ufadhili wa UNESCO. Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa kuimarisha uratibu wa Afua za Ukimwi katika Taasisi za Kidini uliofanyika Chuo cha Maendeleo na Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo kwa ufadhili wa UNESCO.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAHAFALI YA 16 YA CHUO KIKUU MZUMBE KAMPASI YA DAR

0
0

Mlau, Prof. Binamungu akiongoza maandamano kuelekea sehemu ya mahafali. 



Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Prof. Mathew Luhanga, akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam.


Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Lucy Massoi, akiwatambua wanachuo na wahadhiri waliofanya vizuri.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Jaji mstaafu, Barnabas Samatta, akimkabidhi cheti mmoja wa wanachuo aliyefanya vizuri, Gloria Mbigiri wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Jaji mstaafu, Barnabas Samatta, akimkabidhi cheti mmoja wa wanachuo aliyefanya vizuri, Elihuruma Mabelya wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam.



Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya Umahiri ya Uongozi wa Biashara katika Menejimenti ya Biashara wakitunukiwa shahada zao na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji mstaafu, Barnabas Samatta (hayupo pichani), wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MWANJELWA WATOA NENO JUU YA NGUO ZA NDANI KUBWA KULIKO ZOTE JIJINI MBEYA

MAGAZETI YA JUMAPILI LEO DECEMBER 24,2017

Maandalizi ya Sherehe za kutimia Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar yapamba moto

0
0
Jumla ya Miradi 49 ya Kiuchumi, Maendeleo na Ustawi wa Jamii inatarajiwa kuzinduliwa na kuwekewa Mawe ya Msingi ndani ya Kumi la shamra shamra za maadhimisho ya Sherehe za kutimia Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.
Miongoni mwa Miradi hiyo 33 inazinduliwa rasmi baada ya kukamilika kwake wakati miradi 16 inatarajiwa kuwekewa Mawe ya msingi ikijumuisha pamoja na ile ya Taasisi za Umma, miradi ya Jamii sambamba na miradi ya Wawekezaji vitega uchumi.
Hayo yalibainika wakati wa Kikao cha Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa kilichokutana chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na kufanyika katika Jengo la Makumbusho Kifalme liliopo Forodhani Mjini Zanzibar.
Wajumbe wa Kikao hicho cha Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika majadiliano yao walifikia maamuzi ya kuipunguza Miradi Mitatu iliyoainishwa kuingizwa katika ratiba ya sherehe hizo baada ya kubaini kutofikia kiwango kinachokubalika katika uzinduzi pamoja na kuwekewa Mawe ya Msingi.
Hata hivyo Baadhi ya Wajumbe wa Kikao hicho walipendekeza kubadilishwa kwa nyakati na siku za uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi kwa kuzingatia  ratiba za viongozi Wakuu kuepuka kusafiri zaidi ya mara moja wakati wanaposhiriki katika matukio mbali mbali ndani ya Kumi hilo la Sherehe.
Naye Kaimu Kamanda wa Brigedia Nyuki Kanali Said Khamis Said alisema kutakuwa na mabadiliko kidogo ya Gwaride la Mwaka huu  kutokana na Siku ya kilele cha sherehe za maadhimisho ya kutimia Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar kuangukia Ijumaa.
Kanali Said alisema siku hiyo imezingatiwa  vyema na Kamati ya Sekriterieti ya Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa ili kuwapa fursa Wananchi kumaliza mapema sherehe hizo kwa lengo la kujiandaa na ibada ya Sala ya Ijumaa.
Mapema Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Idriss Muslim Hijja alisema miradi yote iliyopendekezwa kuingizwa katika maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar Mwaka huu imefuatiliwa na kutolewa Taarifa kwa  Sekriterieti  ya Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa.
Dr. Hijja alisema yapo marekebisho yaliyofanywa na Kamati hiyo katika kupembua miradi inayostahiki kuingizwa ndani ya ratiba ya sherehe na kufikia maamuzi ya kuitoa ile miradi iliyoshindwa kufikia kiwango kinachohitajika kuingizwa kwenye mtiririko huo.
Katika uzinduzi na uwekaji wa Mawe ya msingi ya miradi iliyomo ndani ya sherehe hizo Viongozi wa Kitaifa wa Serikali zote mbili wamejumuishwa katika ratiba hizo wakiwemo Marais, Mawaziri pamoja na Viongozi wastaafu wa pande zote mbili.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa kwanza Kulia akikiongoza Kikao cha Halmashauri hiyo kilichokutana katika Jengo la Makumbusho ya Kifalme Forodhani Mjini Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.

SALAMU ZA MSIMU KUTOKA THE NGOMA AFRICA BAND YA UJERUMANI

0
0
   Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya The Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibuni inayoongozwa na Kamanda  Ras Makunja yenye maskani nchini Ujerumani inawatakieni kila la heri katika siku kuu ya  Krismasi kwa wadau wote  wakiwatakia amani, upendo, furaha na mshikamano bila kusahau kupata muziki at www.ngoma-africa.com au www.reverbnation.com/ngomaafricaband na pia jumuika nao at www.facebook.com/ngomaafricaband
 The Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibuni inayoongozwa na Kamanda  Ras Makunja
 The Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibuni inayoongozwa na Kamanda  Ras Makunja kazini
Nyomi  ya The Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibuni inayoongozwa na Kamanda  Ras Makunja

MAGIC FM BAMIZA TOP 20 COUNT DOWN DECEMBER 23, 2017

Article 9


WAGONJWA WA HOMA YA INI WAONGEZEKA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MTAKATIFU GASPARI ITIGI,WILAYANI MANYONI

0
0
NaJu mbe Ismailly ITIGI  

DAKTARI wa magonjwa ya ndani ya watu wazima,katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari Itigi,DK.Kazaura Joseph amesema kumekuwa na ongezeko la ugonjwa wa homa ya ini katika Hospitali hiyo ambapo kati ya watu 100,watu wanane wanaweza kuwa na maambukizi sugu ya ugonjwa huo.
Daktari huyo aliyasema hayo wakati akiongea na kituo hiki alipokuwa akielezea madhara ya ugonjwa wa homa ya ini kwa binadamu katika kipindi cha mwaka 2015/2016 hadi 2017/2018 katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari,Itigi,wilayani Manyoni,Mkoani Singida.
Aidha mtaalamu huyo aliweka bayana pia kwamba maambukizi ya ugonjwa huo ni makubwa zaidi ya mara kumi ya maambukizi ya VVU na kwamba kutokana na ongezeko kubwa la maambukizi hayo, shirika la afya duniani lilitenga julai,28 ya kila mwaka kuwa siku ya homa ya ini duniani(World Hepatitis Day). Kwa mujibu wa Dk.Kazaura sababu zinazochangia kuongeza idadi ya watu wenye maambukizi hayo ni pamoja na njia za maambukizi yake ni rahisi sana ikiwemo kujamiiana,elimu ndogo kwa jamii na imani potofu kuhusu ugonjwa huo.
Kuhusu madhara yanayoweza kuwapata wagonjwa wa ugonjwa huo,daktari huyo aliyataja kuwa ni pamoja na ini kunyauka na kushindwa kufanya kazi,kupata saratani ya ini na kuharibika kwa viungo vingine kama figo.Hata hivyo Dk.Kazaura alisisitiza pia kwamba ili kukabiliana na ugonjwa huo alishauri elimu iendelee kutolewa kwa jamii kuhusu homa ya ini,kuendelea kutoa huduma za upimaji wa homa ya ini bure na kutoa chanjo ya homa ya ini kwa watu wote ambao hawajaambukizwa.
Kutokana na ongezeko hilo Daktari huyo wa magonjwa ya ndani ya watu wazima alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa watu wanaopatwa na ugonjwa huo kuwahi kwenda haraka kwenye huduma  za afya ili wapate matibabu.Ushauri mwingine ni jamii kuacha imani potofu kuwa ini linasababishwa na imani za kishirikina na kuongeza kuwa homa ya ini ikifikia kwenye hatua za saratani ya ini hakuna tiba lakini kuna matibabu ya kupunguza kasi ya ugonjwa huo.
Kuhusu watu ambao hawajui hali zao kama wameambukizwa au la,Dk.Kazaura aliwataka watu hao kwenda kwenye vituo vya afya ili kupima homa ya ini na kupatiwa matibabu. Homa ya ini iligunduliwa na Dk.Barack Blumberg mnamo mwaka 1963 na kwamba mwaka 1969 Dk.Brack na wenzake waligundua chanzo cha homa ya ini inayosababishwa na Hepatitis B virus.
 Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari Itigi,Dk.Lesiriam Serafina(wa kwanza kutoka kushoto) akiwa na mgeni rasmi katika maadhimisho hayo,Padri Chesco Msaga( wa pili kutoka kushoto) wakijiandaa kuingia katika ukumbi wa mikutano wa kumbukumbu ya Mtakatifu Papa John Paul wa pili,uliopo mjini Itigi,wilayani Manyoni
 Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Itigi,wilayani Manyoni waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya juma la Mtakatifu Gaspari wakisikiliza matangazo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa shirika hilo.
 Mratibu wa maadhimisho ya sherehe za juma la kumbukumbu ya kumuenzi Mtakatifu Gaspari,yaliyofanyika katika viwanja vya Hospitali hiyo,mjini Itigi,Dk.Peter Nyira akitangaza washindi wa mashindano ya michezo mbali mbali. 
Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi ya Yesu Tanzania,Padri Chesco Msaga ( wa pili kutoka kulia) akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mbio za magunia.Picha zote Na Jumbe Ismailly

Kila Mchezaji Wa Zanzibar Heroes Apewa Shilingi Milioni 3 na Kiwanja Kimoja na Rais Dkt. Shein

RC GAMBO AONGOZA WANA-ARUSHA KUJENGA HOSPITALI YA WILAYA

0
0
 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amezindua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Arusha mjini katika eneo la Njiro kontena. Shughuli ambayo ilihidhuriwa na mamia ya wakazi wa Jiji hilo. Akizungumza na wananchi hao Gambo alisema “Nina furaha sana kushuhudia tukio hili litakaloacha alama katika maisha ya watu wetu wa Arusha,kwani wakati wa kampeni Mhe Rais Magufuli aliahidi na tunatekeleza kwa vitendo.” 
 Hospitali hiyo inatarajiwa kuhudumia wakazi zaidi ya laki nne kutoka wilayani humo na maeneo ya jirani ili kupunguza idadi ya wagonjwa wanasababisha hospitali ya mkoa ya Mount Meru kuelemewa. 
 Vile vile Gambo anasema kwa sasa mapato yanayokusanywa na Jiji la Arusha kwa mwaka bado hayatoshelezi hata kulipa mishahara ya watumishi wake na kwa maana hiyo ni muhimu kuweka mifumo thabiti ya ukusanyaji wa mapato jijini humo.
 “Jiji la Arusha mapato yake ya ndani kwa mwaka hayazidi bilioni 12 na mishahara pekee ya watumishi wa halmashauri ni zaidi ya bilioni 40, sasa hapo ukilipa tu mishahara hela yote inakwisha na bado unakua na deni, sasa hata fedha za maendeleo zitatoka wapi zaidi ya kutegemea hela zinazoletwa na Magufuli?? Gambo alihoji. 
 Ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Arusha kwa awamu ya kwanza unafanyika katika moja ya maeneo ya wazi yaliyo kuwa yakimilikiwa kinyemelela na baadhi ya wajanja wachache na kwa sasa ujenzi umeanza ambao utagharimu kiasi cha shilingi milioni 500 hii ikiwa ni jengo la Ghorofa moja kwa ajili ya wagonjwa wa nje. 
Naye mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athuman Kihamia alimshukuru Mhe Gambo kwa kuweza kulipigania eneo hilo mpaka limeweza kurudi kwenye mikono ya wananchi. 
 “Kwakweli kama sio jitihada zako eneo hili lilishaondoka mikononi mwetu hivyo kwa niaba ya wananchi wa Arusha ninakushukuru sana, pia nikuahidi tutazingatia ushauri wako wa kulitumia eneo hili vizuri kwa kujenga majengo ya ghorofa kuanzia tano ili kulitumia eneo hili vizuri” alisema Kihamia.  Ujenzi wa Hospitali hiyo unatarajiwa kukamilika June mwaka 2018 ambapo zaidi ya wakazi laki 4 watapata huduma ya afya karibu na makazi yao tofauti na ilivyo.
 Mhandisi wa Majengo Jiji la Arusha akitoa maelezo ya mradi huo kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (kulia) na mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe Fabian Daqqaro ( katikati).
 Mhe Gambo akiweka zege katika msingi wa jengo la wagonjwa wa nje OPD kuashiria kuanza rasmi kwa ujenzi wa hospitali hiyo wilaya.
 Mhe Gambo akimwagia maji kabla ya kuweka zege katika msingi wa jengo la wagonjwa wa nje OPD kuashiria kuanza rasmi kwa ujenzi wa hospitali hiyo wilaya.
Mhe Gambo akiweka zege katika msingi wa jengo la wagonjwa wa nje OPD kuashiria kuanza rasmi kwa ujenzi wa hospitali hiyo wilaya.

JUMUIYA YA WAZAZI TANZANIA MKOA WA DAR ES SALAAM, WAMPOKEA KWA KISHINDO MWENYEKITI WA TAIFA WA JUMUIYA HIYO DK. EDMUND MNDOLWA

0
0
 Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akisalimia baadhi wa wana CCM waliofurika katika ukumbi wa Tawi la CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam, ambao walifika kumlaki katika mapokezi yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo mkoa wa Dar es Salaam.
 Mama Patricia Rukia Mndolwa akisalimia
 Dk. Mndolwa akipokea kwa ukakamavu saluti ya kijana wa CCM baada ya kuvishwa skafu
 Baadhi ya viongozi na wananchi waliohudhuria mapokezi hayo wakiwa ukumbini
Ndugu Omari  Kimbau aliyewahi kuhamia CUF akitangaza kurudi CCM mbele ya Dk. Mndolwa.Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

MPINA AAGIZA MKATABA WA OVENCO KUVUNJWA NA KUUNDWA KWA MKATABA MPYA.

0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina ameagiza kuvunjwa kwa mkataba ulioundwa baina ya RANCHI ya Taifa NARCO na kampuni ya Overland  kwa pamoja na kuunda kampuni ya OVENCO uliyokuwa na mapungufu ya kisheria na kiutendaji kufunjwa ifikapo mwisho wa mwezi huu wa December na kutoa mwezi mmoja kwa  NARCO kuunda mkataba mpya wenye mwongozo wa kisheria.
Mpina aliyasema hayo jana alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa Ranchi ya Mzeri iliyopo wilayani Handeni Mkoani Tanga yenye ukubwa kwa Hekta 41,000  ambapo hekta 21,000 zinamililiwa na Muwekezaji kampuni ya Overland muwekezaji ambaye, amekuwa na mgogoro wa muda mrefu na  NARCO ambapo baada ya Waziri Mpina kusililiza pande zote mbili na kujiridhisha  na kumuona muwekezaji kutokuwa na uwezo wa kufikia malengo ya kuendeleza eneo lote la ardhi  ambalo amekuwa akiliendeleza bila makubaliano yoyote ya kisheria, jambo ambalo limempelekea Waziri Mpina kuagiza  NARCO  kuingia katika hatua ya kuunda mkataba mpya baina yake na muwekezaji huyo utakaozingatia masharti mapya ya kisheria ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa muwakilishi wa NARCO Katika kitalu hicho.
Aidha Waziri Mpina ameagiza muwekezaji huyo asihamishwe kwa kuwa ameonyesha nia ya kuendeleza eneo hilo kwa kuwepo kwa ng’ombe wambegu aina ya Borani pamoja na miundombinu mingine
Akizungumzia eneo la hekta 20,000 linalomilikiwa na wawekezaji wengine wadogo, Mpina aliwataka wawekezaji hao kulipa na kumaliza madeni yote ya kodi ya serikali wanayodaiwa  katika vitalu vyao ifikapo January mosi 2018.
“Wawekezaji wengine wengine wanaomiliki vitalu katika ranchi hii ya Mzeri mnatakiwa kulipa madeni yote ya kodi mnayodaiwa na Serikali kodi mnayolipa ya shilingi elfu moja (1000) kwa mwaka ni kidogo sana lakini bado hamlipi, kinyume na hili ni bora muondoke wenyewe au tutawaondosha kwa nguvu muda huo ukifika. “ Alisisitiza Mpina.
“Baada ya kumaliza kulipa nawagiza NARCO kuwapa miezi mitatu wawekezaji hawa kuhakikisha wanaweka miondombinu inayolingana na ukubwa wa eneo na matumizi ya ardhi , tunataka wawekezaji wafikie malengo na mashamba haya yafanye kazi.” Alisema Mpina.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe alisema kuwa, Wiaya ya handeni itaendelea kulinda  mazao na rasilimali za Mifugo kupitia sheria ndogondogo ambazo wilaya hiyo imejiwekea.
Akizungumza kwa namna ambavyo ameyapokea maagizo wa Waziri Mpina , mmiliki wa kampuni ya Overland Bw. Faisal Edha alisema kuwa amekubalina na maagizo ya Mpina na yupo tayari kuendelea na uwekezaji na anaamini kuwa mkataba mpya utanufaisha pande zote mbili.
Awali akipokea taarifa ya Mifugo ya wilaya ya Handeni, Waziri Mpina alimpongeza Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Godwin Gondwe  kwa kuzitambua sheria za usimamizi wa mifugo na kuzitumia jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kutokuwepo kwa uonevu kwa watu wa jamii ya wafugaji na kuzitaka wilaya nyingine nchini kuiga mfano wa wilaya hiyo kwa kuunda sheria ndogo ndogo zitakazowaongoza katika sekta  ya mifugo.
 Ng’ombe aina ya Borani inayomilikwa na muwekezaji kampuni ya Overland katika Ranchi ya Mzeri , Wilayani Handeni Mkoani Tanga.

 Katikati Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Mhe. Luhaga Mpina akiongea  vyombo vya habari baada ya ziara ya ukaguzi wa  baadhi ya vitalu katika Ranchi ya Mzeri iyopo Wilayani Handeni Mkoani Tanga, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe, na kulia ni mkurugenzi wa kampuni ya Overland Bw. Faizal Edha.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina kati kati na Mkuu wa Wilaya ya Handeni kulia Godwin Gondwe pamoja na wataalam kutoka Wizarani na Mkoani Tanga wakiwa katika zoezi la kukagua baadhi ya vitalu  vilivyopo katika Ranchi ya Mzeri Wilayani Handeni.
Aliyesinama wa pili kulia ni Waziri wa Mifugo na uvuvi Luhana Mpina, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe wakiangalia sehemu ya kunyweshea ng’ombe maji katika ranchi ya Mzeri wilayani Handeni.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images