Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

INTRODUCING NEW SINGLE AUDIO "WISH YOU" BY BARAKA THE PRINCE


BARAZA LA WAFANYAKAZI WA MFUKO WA WCF LAZINDULIWA JIJINI DAR

0
0
NA K-VIS BLOG, FELIX ANDREW 
WAAJIRI Tanzania Bara wametakiwa kuwashirikisha wafanyakazi wao kabla ya kufanya maamuzi mbali mbali ili kuendelea kudumisha amani na mshikamano maeneo ya kazi.

Ushauri huo ulitolewa jjini Dar es Salaam jana na Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde, wakati akizindua baraza la wafanyakazi wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WFC)

Alisema kuwa uongozi shirikishi na wa pamoja ndiyo njia pekee itakayopunguza migogoro maeneo ya kazi, hivyo waajiri hawana budi kuhakikisha jambo hilo linazingatiwa ipasavyo.
“Lengo kuu la uongozi shirikishi na wa pamoja ni kujadiliana changamoto mbali mbali na kuzitatua kwa nia ya kufikia malengo,” alisema.

Mavunde aliwaasa wafanyakazi nchini kuondokana na urasimu katika kutoa huduma mbali mbali kwa jamii.
“Urasimu katika utoaji wa huduma ni changamoto kubwa sana ambayo inaisumbua nchi naomba sana msifanye hivyo kwa manufaa ya taifa letu,” alisema.
Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde (wakwanza toka kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Masha Mshomba (wa pili toka kushoto) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Baraza za Wafanyakazi mapema leo jijini Dar es Salaam. Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Masha Mshomba (kulia) wakionyesha
Wafanyakazi wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WFC) wakifurahia uzinduzi huo. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

INTRODUCING "VUMBA" BY Shetta Ft G Produced By Yogobeats

WANANCHI WA KATA YA GAIRO WAOMBWA KUENDELEA KUCHANGIA SEKTA YA ELIMU

0
0
 Wananchi wa Wilaya ya Gairo wameombwa kuendelea kujitoa kwa hali na mali katika maendeleo ya sekta ya elimu ili kupata matokeo bora. 
 
Kauli hiyo imetolea Disemba 21, 2017 wakati wa kuwasomea mapato na matumizi ya michango ya elimu kwa wananchi wa Kata ya Chakwale na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe wakati akabidhi tani mbili na nusu ya mifuko ya saruji kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno. 

Mhe. Mchembe alisema kuwa saruji hiyo itasaidia kuendeleza zoezi la kufyatua matofali ambapo mpaka sasa wameshafyatua matofali 5,600. Aidha amekaribisha wadau mbalimbali kuendelea kuchangia baada ya wananchi kuchangia shilingi milioni 33 ndani ya miezi mitatu.
 
 "Hamasa ni kubwa kwani watoto wanatembea kilometa zaidi ya Sita kwenda shule. Hili limekuwa ni jaribu kwa watoto wa kike. Vijana wa bodaboda wanatuharibia watoto wa kike. Shule ikiwa karibu itapunguza changamoto hii. 

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akimkabidhi mifuko ya saruji kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno ili iweze kusaidia katika ujenzi wa madarasa, ofisi za walimu na nyumba za walimu. Mkutano huo ulifanyika Disemba 21, 2017 katika Kata ya Chakwale, Gairo.

Wananchi wa Kata ya Chakwale wakisomewa taarifa ya michango yao shilingi milioni 33. Aidha Wenyeviti wa vijiji vitatu walirudishiwa shilingi milioni 10 ikiwa ni kwa ajili ya shughuli za Maendeleo ya vijijini.
 
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akikabidhi hundi ya milioni kumi kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno ili awagawie Wenyeviti  wa kata yake. Mkutano huo ulifanyika Disemba 21, 2017 katika Kata ya Chakwale, Gairo. 
 

WANANCHI WA KATA YA GAIRO WAOMBWA KUENDELEA KUCHANGIA SEKTA YA ELIMU

0
0
Na Mwandishi Wetu. Wananchi wa Wilaya ya Gairo wameombwa kuendelea kujitoa kwa hali na mali katika maendeleo ya sekta ya elimu ili kupata matokeo bora. 
Kauli hiyo imetolea Disemba 21, 2017 wakati wa kuwasomea mapato na matumizi ya michango ya elimu kwa wananchi wa Kata ya Chakwale na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe wakati akabidhi tani mbili na nusu ya mifuko ya saruji kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno. Mhe. Mchembe alisema kuwa saruji hiyo itasaidia kuendeleza zoezi la kufyatua matofali ambapo mpaka sasa wameshafyatua matofali 5,600. Aidha amekaribisha wadau mbalimbali kuendelea kuchangia baada ya wananchi kuchangia shilingi milioni 33 ndani ya miezi mitatu. 
"Hamasa ni kubwa kwani watoto wanatembea kilometa zaidi ya Sita kwenda shule. Hili limekuwa ni jaribu kwa watoto wa kike. Vijana wa bodaboda wanatuharibia watoto wa kike. 
Shule ikiwa karibu itapunguza changamoto hii,"  alisema Mkuu wa Wilaya akiipongeza Kamati ya Ujenzi kwa kazi nzuri ya kukusanya michango ya maendeleo na kazi ya ujenzi ambayo tayari imeanza. 
"Tunategemea kuanza ujenzi mapema Januari katika eneo la ekari 15. Wilaya ya Gairo ina madarasa zaidi ya 30 yote yamejengwa kwa nguvu ya wananchi hadi ngazi ya boma, bado kuezeka. Madarasa haya ni nje ya madarasa 16 yaliyomalizika ndani ya mwaka mmoja. 
"Mpaka sasa hatuna darasa la nyasi wala wanafunzi wanaokaa chini. Tumemaliza nyumba za waalimu 8, maabara 6 na tuna maboma yanahitaji nguvu ya ziada," alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akimkabidhi mifuko ya saruji kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno ili iweze kusaidia katika ujenzi wa madarasa, ofisi za walimu na nyumba za walimu. Mkutano huo ulifanyika Disemba 21, 2017 katika Kata ya Chakwale, Gairo.
Wananchi wa Kata ya Chakwale wakisomewa taarifa ya michango yao shilingi milioni 33. Aidha Wenyeviti wa vijiji vitatu walirudishiwa shilingi milioni 10 ikiwa ni kwa ajili ya shughuli za Maendeleo ya vijijini.
Mkuu wa Wilaya akikabidhi hundi ya milioni kumi kwa Mhe.  Maneno ili awagawie Wenyeviti. Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akikabidhi hundi ya milioni kumi kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno ili ili awagawie Wenyeviti wa kata yake. Mkutano huo ulifanyika Disemba 21, 2017 katika Kata ya Chakwale, Gairo. 

Introducing Critical's "Sawa" Official Video

0
0
Ni kazi mpya ya msanii Critical ambaye ameanza muziki akitokea katika studio ya Maxmizer. Video imeandaliwa na Director Khalifan.

DKT MWANJELWA AIAMURU TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO NALIENDELE MTWARA KUWAONGEZA MALIPO WAFANYAKAZI WAKE

0
0
Na Mathias Canal, Mtwara
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele (NARI) ambayo Kitaifa inaratibu Utafiti wa zao la Korosho, Mbegu za mafuta na mazao jamii ya mizizi (Muhogo na viazi vitamu) Dkt Omari Mponda ameagizwa kuwaongeza malipo ya kazi wafanyakazi wa kituo hicho katika mradi wa kubangua Korosho.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa leo 22 Disemba 2017 wakati akizungumza na wafanyakazi wa kituo hicho cha Utafiti Mara baada ya kutembelea kiwanda kidogo cha kubangua Korosho na kubaini kuwa wafanyakazi hao wanalipwa shilingi 600 kwa kila kilo moja ya korosho wanayobangua kiasi ambacho hakiakisi ufanisi wa kazi kubwa wanayoifanya.
Katika maelekezo yake Naibu Waziri huyo amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho kuongeza kiasi cha malipo walau kufikia shilingi 1000 kwa kila kilo moja wanayobangua ili wafanyakazi hao waweze kupata malipo ambayo yatamudu gharama za maisha.
Sambamba na hayo pia ameupongeza Uongozi wa kiwanda hicho kwa kubuni ajira hizo mpya za mradi huo wa korosho zinazowanufaisha wananchi wa Mtwara sambamba na pongezi za kuajiri wafanyakazi wengi ambao asilimia kubwa ni wanawake.
Aidha, amesisitiza kuongeza bidii ya utoaji Elimu kwa wananchi kufahamu umuhimu wa mazao ya muhogo, Njugu na Mbaazi ili yaweze kutumika zaidi kwani ni fahari kwa wakulima na wananchi kwa ujumla.


Katika hatua nyingine Mhe Mwanjelwa ameipongeza Taasisi hiyo kwa kufanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza Afrika kutoa/kugundua na kusajili mbegu bora 54 za korosho kwa ajili ya matumizi kwa wakulima mwaka 2006 (Aina 16), Mwaka 2015 (Aina 22 mbegu chotara), na Mwaka 2016 (Aina 16 mbegu fupi).
Alisema Aina hizo za mbegu hizo zina uwezo wa kuzaa korosho nyingi na bora, Zina uwezo wa kuvumilia magonjwa na wadudu waharibifu na kufanya Utafiti kupendekeza zaidi ya Aina 30 za viuatilifu vya kudhibiti visumbufu vya Korosho.
Taasisi ya Utafiti wa kilimo Naliendele (NARI) imepewa jukumu la kufanya Utafiti ili kuongeza tija katika Kilimo katika kanda ya kusini mikoa ya Lindi, Mtwara na Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua miche ya Korosho wakati alipotembelea Kitalu Nyumba (Green House) katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele (NARI) Mkoani Mtwara Mwingine ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele (NARI) Dkt Omari Mponda, leo 22 Disemba 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Tanki linalohifadhi maji kwa ajili ya Skimu ya umwagiliaji wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele (NARI) Mkoani Mtwaraleo 22 Disemba 2017.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akishiriki kazi ya kubangua korosho wakati alipotembelea Kiwanda cha Korosho na Juice katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele (NARI) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Mtwaraleo 22 Disemba 2017.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua shamba lenye mfumo wa kisasa wa umwagiliaji kwa Skimu ya umwagiliaji wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele (NARI) Mkoani Mtwaraleo 22 Disemba 2017.

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akishiriki kazi ya kubangua korosho wakati alipotembelea Kiwanda cha Korosho na Juice katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele (NARI) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Mtwaraleo 22 Disemba 2017.




VIONGOZI 19 WA wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya SHIRECU, NYANZA WANUSURIKA KWENDA SELO

0
0

Ataka wampe maelezo ya kina upotevu wa mali za mabilioni

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewanusuru viongozi 19 wa vyama vikuu vya ushirika vya mikoa ya Shinyanga (SHIRECU) na Mwanza (NCU) kwenda selo na badala yake amewapa siku 23 wampe maelezo yatakayomridhisha juu ya mahali zilipo mali za vyama hivyo viwili.

Amefikia uamuzi huo leo Ijumaa, Desemba 22, 2017 wakati akifunga kikao cha siku moja cha wadau wa zao la pamba alichokiitisha mkoani Shinyanga. Viongozi hao wanatuhumiwa kwa upotevu wa mali zilizokuwa zikimilikiwa na vyama hivyo vya ushirika. 
“Nataka kila mtu akaandae taarifa kuhusu mali za ushirika zilipo, au zimeenda wapi na kama mlizikopea, mseme ni wapi, lini na kwa ridhaa ya nani. Nataka maelezo ya kutosha kuniridhisha mali za ushirika zimeenda wapi,” alisema Waziri Mkuu. 
“Hawa nitakaowataja walipaswa kuchukuliwa na RPC, wakatoe maelezo yao na hatua dhidi yao zichukuliwe. Sasa nataka nikutane nao Dodoma ifikapo Januari 15, 2018 saa 3:30 asubuhi ofisini kwangu,” alisisitiza. 
Kuhusu tuhuma za viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Mwanza (Nyanza Cooperative Union - NCU), Waziri Mkuu alisema chama hicho kati ya mwaka 2001 na 2017, kilikuwa jumla ya mali 10 ambazo ziliuzwa kinyemela katika mazingira yenye utata na kwa bei ndogo ikilinganishwa na thamani halisi ya mali hizo zilizopo jijini Mwanza. 
Aliwataja viongozi waliohusika na upotevu huo ambao wanatakiwa kutoa maelezo yao kuwa ni  Murtazar Alloo ambaye ni mnunuzi wa maghala matatu mali ya NCU, Bw. Samson Ng’halida (mnunuzi wa New Era Oil Mills), Bw. Amos Njite Lili (mnunuzi wa ghala la Igogo), Bi. Antonia Zacharia (mnunuzi wa jengo la KAUMA), Bw. Timothy Kilumile (mnunuzi wa jengo la KAUMA), Bw. Robert Kisena (mnunuzi wa pili wa New Era Oil Mills), Bw. Peter Ng’hingi (aliyekuwa Mjumbe wa Bodi), Bw. Daniel Lugwisha (aliyekuwa Mhasibu Mkuu - NCU), Bw. George Makungwi (aliyekuwa Afisa Miliki - NCU) na Bw. Sospeter Ndoli (aliyekuwa Afisa Utumishi -NCU). 
Kuhusu mali za Nyanza zinazoshikiliwa na benki ya CRDB. Waziri Mkuu alisema benki hiyo inaidai NCU mikopo yenye thamani ya sh. bilioni 2.123 na kwamba benki hiyo inashikilia mali 16 zenye thamani ya sh. bilioni 18.132. Alitaka vyombo vya dola vifanye uchunguzi ili kubaini uwiano wa mikopo na mali zinazoshikiliwa na benki ya CRDB. 
Kwa upande wa viongozi wa SHIRECU, Waziri Mkuu alisema wanatuhumiwa kwa upotevu wa zaidi ya sh. bilioni 11 ambazo wanadaiwa na benki ya TIB yakiwemo madeni ya mishahara ya watumishi ambayo yanafikia sh. bilioni 1.2.  
“SHIRECU kwa sasa haina mali zozote kwa sababu mali zote zinashikiliwa na TIB kutokana na mikopo,” alisema.  
Aliwataja viongozi wa SHIRECU ambao wanatakiwa kutoa maelezo yao kuwa ni Bw. Joseph Mihangwa (Meneja Mkuu), Bw. Sillu Mbogo (Kaimu Mhasibu Mkuu), Bw. Maduhu Nkamakazi (Kaimu Mkaguzi wa Ndani), Bw. James Kusekwa (Kaimu Meneja Uendeshaji) na wajumbe wa Bodi ya SHIRECU.  
Wajumbe hao wa Bodi ni Bw. Robert Mayongela (Mwenyekiti), Bi. Mary Mabuga (Makamu Mwenyekiti), Bw. Sigu Maganda (Mjumbe), Bw. Clement Bujiku (Mjumbe) na Bw. Charles Lujiga. 
Waziri Mkuu ambaye aliwasili mkoani humo leo asubuhi, alikwenda kwanza kukagua kiwanda cha kutengeneza nyuzi cha JOC na kisha kurejea ukumbini kuendelea na kikao cha wadau wa pamba ambacho kimeshirikisha wakuu wa mikoa 16, wabunge, ma-RAS, wakuu wa wilaya, wakulima, wanunuzi wa pamba na wenye viwanda.
Waziri Mkuu ameondoka Shinyanga kuelekea Ruvuma ambako atakuwa na ziara ya siku moja.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) akitaka ufafanuzi kuhusu aina ya nyuzi zinazozalishwa na kiwanda cha JOC kutoka kwa Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Bw. Jim Liu katika ziara fupi aliyofanya kiwandani hapo leo asubuhi, Desemba 22, 2017. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bibi Maimuna Tarishi na wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Tellack.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) akipatiwa maelezo na Meneja Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza nyuzi cha JOC, Bw. Jim Liu wakati alipozuru kiwanda hicho kuona uzalishaji mjini Shinyanga leo asubuhi, Desemba 22, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Tellack.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia bandali la nyuzi zilizosokotwa na kiwanda cha kutengeneza nyuzi cha JOC, mjini Shinyanga leo Desemba 22, 2017 na kubainishwa kwamba zimetoka Tanzania. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, Bw. Jim Liu. 
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


RAIS WA ZANZIBAR AWAANDALIA CHAKULA CHA MCHANA WACHEZAJI WA ZANZIBAR HEROES IKULU LEO

0
0
 Wachezaji wa Zanzibar Heroes wakipata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein. Ikulu Zanzibar, kuipongeza Timu hiyo kwa ushujaa wake katika michuano ya Kombe la Chalenji nchini Kenya hivi karibuni ambapo walitinga fainali na kushindwa kwa taabu kwa njia ya penati
 Viongozi wa Timu ya Zanzibar Heroes wakijumuika katika chakula cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Ikulu Zanzibar leo
 Kocha Mkuu wa Zanzibar Heroes Hemed Moroco akitowa shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili yao katika viwanja vya Ikulu
 Rais wa nzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimpongeza Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Morocco kwa kwa jitihada zake alizoonesha kwa Timu ya Taifa ya Zanzibar kufikia hatua ya Fainali katika michuano ya Chalenji wiki iliyo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwapongeza wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes na Wachezaji wa Zamani wa Zanzibar, baada ya hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili yao Ikulu Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wakipata picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes na Wachezaji wa Zamani wa Zanzibar, baada ya hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili yao Ikulu Zanzibar. Picha na IKULU



SALAMU ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA KUTOKA KWA IGP SIMON SIRRO

MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO DECEMBER 23,2017

DKT MNDOLWA APOKELEWA KWA KISHINDO JIJINI DAR,ATOA YA MOYONI.

MATENGENEZO MAKUBWA MASHINE NAMBA MOJA YA KUFUA UMEME KIDATU YAFIKIA ZAIDI YA ASILIMIA 95 KUKAMILIKA

0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Kidatu.

MATENGENEZO makubwa ya mashine namba moja kati ya nne za kufua umeme wa maji kwenye Kituo cha kufua umeme wa maji Kidatu mkoani Morogoro yamefikia zaidi ya asilimia 95 kukamilika.

Msimamizi wa matengenezo ya mashine hiyo Mhandisi Rajabu Kindunda amewaambia wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea kituo hicho Desemba 22, 2017.


"Kwa sasa tumeanza majaribio ya mashine kuzunguka bila kutumia nguvu za maji, mafundi wanazungusha mashine hiyo kwa kutumia mikono ili kuangalia usahihi wa unyookaji wa shafti,”alisema.


Alisema hatua itakayofuata ni kuunganisha kipande yanapoingilia maji ili kuzungusha huo mtambo na sehemu ya kuzalishia umeme na Jumapili mafundi hao wanaoshirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya Concar kutoka Croatia wataanza majaribio ya kuzungusha mtambo wenyewe.
Aidha Meneja wa Kituo hicho, Mhandisi Anthony Mbushi Amesema Kidatu kuna mitambo minne na kila mmoja unauwezo wa kuzalisha umeme Megawati 51 na hivyo kufanya jumla ya Megawati 204 za umeme ambao unaingizwa kwenye Gridi ya Taifa.


”Tuliona tufanye matengenezo makubwa kwani kila baada ya miaka 20 huwa tunafanya zoezi kama hili ili kurejesha mashine kufanya kazi bora kwa kipindi hicho ili kuhakikisha mtambo unarejea kwenye hali yake ya kawaida.” Alisema.

 Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), wakishirikiana na wakandarasi kutoka kampuni ya Concar kutoka Croatia, wakifanya matengenezo makubwa ya mashine namba moja ya kufua umeme, kwenye Kituo cha kufua umeme wa maji Kidatu mkoani Morogoro Desemba 22, 2017. Kituo hicho kina jumla ya mashine 4 (Turbines) za kufua umeme wa Megawati 204.
Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine turbines kwenye bwawa la Kidatu mkoani Morogoro.
 Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine za kufua umeme wa maji Kidatu.
  Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine za kufua umeme wa maji Kidatu.
Wasimamizi wa chumba cha kudhibiti mifumo ya umeme wakiwa kazini wakati walipotembelewa na wahariri wa vyombo vya habari Kituo cha Kidatu mkoani Morogoro.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MARIAM MWEMA, BINTI ALIYESHINDWA KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE AOMBA MSAADA WA MATIBABU

JESHI LA ZIMAMOTO LAFANYA TAMASHA LA UTOAJI ELIMU KWA UMMA

0
0
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini wakionesha utayari wakukabiliana na majanga ya moto.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (Katikati), akizungusha king’ora kama ishara ya Uzinduzi rasmi wa Tamasha la Zimamoto la utoaji elimu kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Thobias Andengenye, wakati wa Tamasha la hilo lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo eneo la Kawe mapema jana asubuhi tarehe 22/12/2017.

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, akizungumza na Wananchi wa Jiji la Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi rasmi wa Tamasha la Zimamoto la utoaji elimu kwa Umma, wakati wa Tamasha hilo lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo eneo la Kawe mapema mapema jana asubuhi tarehe 22/12/2017.

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (Watatu Kulia), akiwa kwenye banda la mmoja wa mdau aliyeshiriki katika tamasha hilo, wakati wa Tamasha la Zimamoto la utoaji elimu kwa umma lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo eneo la Kawe mapema mapema jana asubuhi tarehe 22/12/2017.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Mrakibu wa Zimamoto Peter Mabusi (wanne kushoto) akitoa maelezo kwa Kamishna wa Operesheni Billy Mwakatage (watatu kushoto), Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Benedict Kitalika (Wapili Kushoto), na Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Temeke Laizer Loshpy (kushoto), pindi vikosi mbalimbali vya zimamoto vilivyokuwa vikioonesha zoezi la utayari wakati wa tamasha la Zimamoto na Uokoaji la utoaji elimu lililofanyika katika viwanja vya Kawe Tanganyika Packers mapema mapema jana asubuhi tarehe 22/12/2017.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

JESHI LA POLISI MKOANI PWANI KUWATIA HATIANI WAHALIFU KIPINDI CHA SIKUKUU-RPC SHANNA

0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

JESHI la polisi Mkoani Pwani limetoa onyo kali kwa wale wenye nia ya kutenda uhalifu, katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka ,wabadili mawazo yao kabla ya hatari kwani jeshi hilo limejipanga kikamilifu kulinda raia na mali zake.

Aidha jeshi hilo limewataadharisha watu wote wanaokwenda ndani ya Mkoa huo hususan kwenye fukwe za bahari ya Hindi zilipo kwenye wilaya ya Bagamoyo ,kuwa wastaarabu na kutii sheria za nchi na watakaokiuka hawatakuwa na muhali nao ili iwe mfano kwa wengine.

Kamanda wa polisi Mkoani Pwani (ACP)Jonathan Shanna ,alitoa wito huo viwanja vya Mailmoja Kibaha wakati akizungumza na waandishi wa habari na baadhi ya wananchi waliojitokeza kujionea askari waliokuwa wakifanya mazoezi ,kuelekea kipindi cha sikukuu ya X-Mas na mwaka mpya.

Alitoa wito, kwa wenye kumbi za starehe kuzingatia sheria za usalama kwa kutojaza idadi kubwa ya watu kwenye kumbi zao na wale watakaokaidi watakiona .Pamoja na hayo ,kamanda Shanna aliwataka wananchi kuhakikisha wanapotoka majumbani mwao ,wasitoke wote na waache walinzi kwenye nyumba zao. 

Aliwaasa pia wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwaachia watoto wao kwenda kwenye shamrashamra za sikukuu pasipo kuwa na wangalizi ili kuepuka upotevu wa watoto.Kamanda Shanna alieleza kuwa ,askari wa jeshi hilo Mkoa wapo kamili ,shupavu na majasiri katika kuzuia matukio ya uhalifu kupitia mbinu za kimedani walizowapatia .

“Sisi jeshi la polisi Mkoa tumejipanga katika kuhakikisha usalama ndani ya mkoa wetu unakuwa ni jambo endelevu sio wakati huu wa sikukuu pekee ,ili kuunga mkono kauli mbiu ya serikali yetu ya Tanzania ya na Tanzania yenye amani’alisema Kamanda Shanna.Kamanda huyo Mkoani hapo alielezea kwamba,usalama ni bidhaa adimu ,usalama unapotoweka watu huweza kukimbia nchi yao na kuitwa walimbizi katika nchi nyingine .

Hivyo ,Kamanda Shanna alisema watahakikisha wanatunza tunu ya amani iliyopo ili kuweza kuwavutia wawekezaji kuendelea kuwekeza katika Mkoa huo.Jeshi hilo limeahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaojaribu kuchezea usalama uliopo mkoani humo .

Katika hatua nyingine aliwashukuru waandishi wa habari mkoani hapo ,kwa ushirikiano wanaouonyesha kwa jeshi hilo .Kamanda Shanna alibainisha ,ushirikiano huo umemsaidia kwa kiwango kikubwa katika mapambano ya kuzuia na kutanzua uhalifu.Aliwaomba ushirikiano uendelee ili kuhabarisha umma juu ya matukio yanayotokea na mikakati wanayoendelea nayo




Kamanda wa polisi Mkoani Pwani ,Jonathan Shanna mwenye kifimbo akiwa pamoja na askari wa polisi Mkoani hapo ,wakati wakijifua na mazoezi kuelekea kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka,viwanja vya Mailmoja Kibaha.Picha na Mwamvua Mwinyi

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Bodi ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania yakutana leo JNIA

0
0
Bodi ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, leo wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) katika kikao cha kawaida cha 33 cha kujadili masuala mbalimbali ya utendaji ya mamlaka kwa kipindi cha robo ya kwanza na pili ya mwaka wa fedha 2017/2018.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) leo akimweleza jambo Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya mamlaka hiyo, Prof. Mhandisi Ninatubu Lema (katikati), katika kikao cha 33 cha Kawaida cha kujadili robo ya kwanza na pili ya mwaka wa fedha 2017/2018 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, wakiwa katika kikao cha kawaida cha 33 cha kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kwa kipindi cha robo ya kwanza na pili ya mwaka wa fedha 2017/2018 kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Mjumbe wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Dr. Frederick Mwakibinga (kushoto) akizungumza jambo kwenye kikao cha 33 cha bodi hiyo cha kujadili robo ya kwanza na pili ya mwaka wa fedha 2017/2018, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

wengine watatu wa tatumzuka waibuka na vitita vya milioni 10 kuelekea funga Mwaka

0
0
Wasimamizi wa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka wametoa washindi watatu wa sh. Milioni 10 katika droo maalumu ya mwisho wa mwaka ili kuwapa wachezaji wa droo hiyo kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana jijini Dar,wakati wa kukabidhi hundi hizo kwa washindi hao, Mmoja wa Maafisa Habari wa Tatu Mzuka, Dina Marious amesema droo hiyo inachezwa majira ya saa tatu na nusu usiku ambayo inakwenda hadi mwishoni wa mwaka.

Dina aliwataja washindi hao watatu kuwa ni Hilda Mwaibako,Asha Hamisi pamoja na Anna Ankya,ambao wanatoka katika vitongoji tofauti lakini wote ni wakazi wa jiji la Dar Ess Salaam.

Dina amesema kuwa washindi wote waliopewa hundi ni kutokana na kushinda mchezo huo kwa kufuata taratibu zilizowekwa za mchezo,Amesema Watanzania waendelee kuchangamkia fursa ya mchezo huo na kuibuka washindi na kufurahi msimu wa sikukuuu na ziku zinazoendelea.''Droo ya walioshinda ni maalumu na wakiona umuhimu wataweza kuitumia na droo zingine zikiendelea,''alisema Dina.

Afisa Habari wa Tatu Mzuka, Dina Marious akimkabidhi hundi ya milioni 10 kwa mshindi wa droo ya Tatu Mzuka, Anna Nkya kwenye mkutano na Wanahabari (hawapo pichani), uliofanyika jana jijini Dar. Afisa Habari wa Tatu Mzuka, Dina Marious akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) ,mapema jana jijini Dar,kuhusiana na washindi watatu wa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka waliojishindia kitita cha Milioni 10 kwa kila mmoja, katika droo maalumu ya mwisho wa mwaka.
Washindi watatu wa mchezo wa kubahatisha wa Tatu Mzuka waliojishindia kitita cha Milioni 10 kwa kila mmoja, katika droo maalumu ya mwisho wa mwaka,wakia katika nyuso za furaha kabisa.

NAIBU WAZIRI WA MICHEZO JULIANA SHONZA AFUNGUA TAMASHA LA MICHEZO KARATU LEO

0
0
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza (katikati) akimaliza mbio za kilomita tano wakati wa kufunga Tamasha la Michezo Karatu lililofanyika mjini Karatu leo tarehe 23/12/2012
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza (katikatika) akishiriki mbio za kilomita tano wakati wakufunga Tamasha la Michezo Karatu lililofanyika mjini Karatu leo tarehe 23/12/2017, kutoka kulia wakwanza ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi Teresia Mahongo,Afisa utamaduni na michezo wiliya ya Karatu Ndg Laurent P. manonha na wakwanza kushoto kulia kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Karatu Ndg. Waziri Mourice

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza akipiga risasi juu kuashiria kuanza kwa mbia za kilomita kumi wakati wakufunga Tamasha la Michezo Karatu lililofanyika leo tarehe 23/12/2017 mjini Karatu,kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi Teresia Mahongo.
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images