Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live

WATU BILIONI 7 DUNIANI WAPINGA AZIMIO LA TRUMP

$
0
0
Marekani imefeli  kuulazimisha ulimwengu kukubaliana na azimio lake lililokinyume na sheria, wakati mkutano mkuu  wa Umoja wa Mataifa ulipopitisha kwa idadi kubwa ya wanachama wake, kupinga azimio la Trump linaloitambua Jerusalem kama Mji Mkuu wa Israeli.
Pamoja na vitisho vya Marekani kwa nchi za dunia kuwa itainyima misaada ya kifedha, kupitia Mwakilishi wake katika Umoja huo wa Mataifa kwamba “Aidha fedha au kulipitisha azimio”, Marekani na Israeli pamoja na nguvu zao hazikuweza  isipokuwa kuzikinaisha nchi 7 tu, katika kupigia kura ya hapana azimio hilo zikiwemo zenyewe.
Nchi 128 zimelipigia kura ya ndio azimio hilo,ambazo ni sawa na watu bilioni 7 walio ulimwenguni, sawa na asilimia zaidi ya 90% ya wakazi wote, huku azimio hilo likiwa linalazimisha kuwa kwake, kwa kupata zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe wakamati kuu ya mkutano mkuu, likiwa na uzito sawa na maazimio ya Baraza la Usalama.
Tanzania vilevile imepigia kura ya ndio azimio hilo ikiwa pamoja na nchi nyingi duniani, zikiwemo China, India, Urusi, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na idadi kubwa ya nchi za Umoja wa Ulaya, nchi zote za kiislamu na kiarabu pia nchi nyingi za  Amerika ya Kusini.
Kilichoshangaza zaidi ni kuona dola ya Vatikani imepinga azimio la Trump, dola ambayo yenyewe  inawakilisha ulimwengu wa kikristo, huku yakiwa makubaliano ya kiislamu, kikristo na kibinaadamu yote yanapinga azimio la Trump lisilo la kisheria na si la kiuadilifu, ambalo pia linakwenda kinyume na kanuni na sheria zote za kimataifa.


WAKULIMA 14 WA PAMBA WAINGIA MATATANI WILAYANI IGUNGA KWA KUVUNJA SHERIA YA PAMBA.

$
0
0
WATU 14 wilayani Igunga wamekamatwa na Serikali ya Mkoa wa Tabora kwa tuhuma za kukaidi maagizo ya kuwataka kulima pamba kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo cha pamba na kujikuta wakivunja Sheria ya Pamba ya mwaka 2001 na kanuni zake.

Watu hao walikamatwa hivi karibuni na Uongozi wa Wilaya ya Igunga kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri.

Alisema kuwa watuhumiwa hao walikutwa katika mashamba yao ya pamba wakiwa wamepanda pamba kwa mtindo wa kizamani ambao hauzingatia Sheria ya Pamba ya 2001 wengine wameacha maotea ambalo ni kosa.

Kufuatia hatua hiyo Mkuu wa Mkoa aliwaagiza Maofisa Ugani wote kukagua shamba yote ili kujiridhisha kama wakulima waliobaki wamezingatia ulimaji wa kufuata Sheria na endapo watabainika kuwepo na waliokiuka wachukuliwe hatua haraka.

Alisema kuwa endapo atakuta katika eneo la Ofisa Ugani alilopangiwa kukagua mashamba kuna mkulima amelima bila kuzingatia Sheria na hajachukuliwa hatua itabidi amfukuze kazi.

Awali Katibu Tawala wa Wilaya ya Igunga Godslove Kawishe alisema kuwa wakulima walikamatwa kwa tuhuma za kukutwa wamepanda pamba kwa kurusha rusha mbegu ovyo bila kuzingatia matakwa ya kupanda kwa mistari na wengine walikutwa wameacha maotea yakiwa yameota na yamechanganyikana na shamba la mahindi.

Alisema kuwa miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji na Vitongoji ambao ndio waliokuwa wakituhumiwa kwa kosa la kushindwa kusimamia hadi wakulima kulima bila kuzingatia Sheria.

Kawishe aliongeza kuwa hata walipokuwa wakiombwa taarifa za wakulima wao walikuwa hawatoi ushirikiano kwa maafisa Ugani wa eneo husika.

Sheria ya Pamba 2001  na Kanuni zake za mwaka 2011 sehemu ya tatu katika kipengele cha 12 kinakataza kulima bila kuzingatia kanuni za kilimo bora, kipengele cha 13 kinakataza kuchanganya pamba na mazao mengine na kipengele cha 14 kinakataza kuacha maotea.

Kwa mujibu wa Sheria hiyo Bodi ya Pamba imepewa mamlaka ya kuharibu shamba kwa gharama za mkulima pia mkulima anayebainika na kosa hilo atahukumiwa kulipa faini isiyopungua shilingi laki moja au kifungu kisichopungua  miezi mitatu au vyote kwa pamoja.

NAIBU SPIKA AKABIDHI MISAADA MBALIMBALI WILAYANI RUNGWE

$
0
0
Naibu Spika Dk Tulia Ackson amefanya ziara katika baadhi ya maeneo Wilayani Rungwe mkoani  Mbeya ikiwa ni kutekeleza baadhi ya ahadi alizowahi kuzitoa katika kusaidia maendeleo, kwanza alianza kwa kutoa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni tano katika shule ya sekondari Bujela
 Akizungumza katika shule ya  Bujela Dk. Tulia amesema  kuwa  ahadi lazima zitekelezwe jambo  ambalo hata Rais  Dk. John Pombe Magufuli i husisitiza kutoigiza  siasa kwenye mambo ya maendeleo.

"Leo kama  Tulia Trust  tuliahidi vifaa vyenye thamani ya Milioni tano na tayari tumetekeleza kwa kuja navyo vikiwemo bati, mbao, mchanga, saruji, chokaa, rangi, vioo, nondo .amesma  Dk Tulia"
 Amesema kufanya hayo  yote ni kwa ajili ya kuhakikisha tunawatengenezea watoto wetu mazingira mazuri ya kujisomea na baadae watuletee maendeleo sisi wazazi wao hivyo niwaombe viongozi wote tushikamane.
Katika ziara yake hiyo alitembelea  Kanisa la Bujela ambalo liliharibiwa na upepo uliosababishwa na mvua huko  ambapo Dk.Tulia alichangia jumla ya mabati 100 yenye thamani zaidi ya milioni mbili Kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa kanisa hilo ambalo tayari ujenzi wake ulianza kwa jitihada za waumini wenyewe kuchangishana.

Aidha Dk.Tulia aliwahimiza waumini pamoja na viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa la Tanzania amani pamoja na kumuombea Rais Magufuli ili aendelee kuiongoza nchi salama.

DK NDUGULILE AZINDUA PROGRAMU YA KIKUNDI MLEZI KWA WANAWAKE WAJASILIAMALI

$
0
0
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amezindua programu ya Kikundi Mlezi yenye lengo la kuwawezesha wanawake wajasilimali  wasio katika Sekta rasmi kuleana wenyewe katika kuanzisha na kuendeleza mitaji na biashara zao.

Dkt. Ndugulile amezindua programu hiyo wakati alipofanya ziara Wilayani Kisarawe mkoani Pwani katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi kujishughulisha katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Dkt.Ndugulile amesema kuwa  ili kufanikisha kufikia Tanzania ya viwanda Serikali itaendelea kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo hasa wanawake katika kuwawezesha kuanzisha vikundi vitakayoanzisha viwanda vidogo vidogo na vya kati.

Ameongeza kuwa lengo la kuzindua Programu ya Kikundi Mlezi ni inalenga kuwawezesha wanawake wasio katika Sekta rasmi kwa kuwashirikisha wanawake wajasilimali waliokomaa katika biashara kuwalea na kuwasaidia wanawake wajasiliamali wanaoanza shughuli hizo.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na vikundi vya wanawake wajasiliamali wa Wilaya ya Kisarawe na maeneo jirani wakati wa uzinduzi wa Programu ya Kikundi Mlezi.
 Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi.Sihaba Nkinga akieleza jinsi programu ya Kikundi Mlezi itakavyowasaidia wanawake kuleana na kusaidiana katika biashara zao ili kujikwamua kiuchumi wakati wa uzinduzi wa programu hiyo wilayani Kisarawe.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikata utepe kuzindua rasmi Programu ya kikundi Mlezi itakayowezesha wanawake kusaidiana na kuleana wenyewe kwa wenyewe katika kuanzisha biashara ili kujikwamua kiuchumi.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akionesha kibao kinachoonesha kuzinduliwa rasmi Programu ya kikundi Mlezi itakayowezesha wanawake kusaidia na kuleana  wenyewe kwa wenyewe katika kuanzisha biashara ili kujikwamua kiuchumi.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara, viongozi wa Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Kisarawe na wanawake wajasiliamali kutoka Wilaya ya Kisarawe mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi mkoani hapo. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAVUNDE ATEMBELEA UJENZI WA DARAJA LA CHIHANGA-GAWAYE NA ZAHANATI YA ZEPISA, HOMBOLO MAKULU-DODOMA MJINI

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Peter Mavunde leo ametembelea ujenzi wa Daraja linalounganisha vijiji vya Chihanga na Gawaye kata ya Chihanga Jimbo la Dodoma Mjini na kupongeza kasi ya ujenzi inayofanywa na Mkandarasi katika kuhakikisha daraja hilo linakamilika mapema ili wananchi waondokane na adha kubwa ya kutokupitika eneo hilo kipindi cha masika.

Daraja hilo lenye thamani ya Tsh 49m linatarajiwa kukamilika mapema January 2018 na hivyo kuondoa kero ya muda mrefu ya kutopitika kwa eneo hilo.

Aidha Mh Mavunde pia ametembelea ujenzi wa Zahanati ya Zepisa akiongozana na Mkurugenzi wa Global Space East Africa Ltd Ndg Gaston M. Francis pamoja na Mhandisi Malcom kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Mbunge Mavunde katika kukamilisha ujenzi wa Zahanati hiyo ambapo Mavunde ameahidi kuchangia matofali 1000 na saruji mifuko 100,Manispaa ya Dodoma 10m na Ndg Gaston M. Francis kwa niaba ya Kampuni ya Global Space East Africa Ltd ameahidi kuchangia mifuko 50 ya saruji na vifaa vya ndani vya Zahanati baada ya kukamilika.


Diwani wa kata ya Hombolo Ndg Jacob Lemanya kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo wamemshukuru Mbunge Mavunde kwa jitihada kubwa anazofanya za kuwasaidia katika ujenzi wa Zahanati kwa kutafuta wafadhili mbalimbali ili kufanikisha ujenzi huu wa zahanati na kuahidi kuunga mkono jitihada hizo kwa wao kujitolea katika shughuli mbalimbali za ukamilishwaji wa zahanati hiyo. 
  Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akikagua ujenzi wa daraja la Chihanga-Gawaye linalounganisha vijiji vya Chihanga na Gawaye kata ya Chihanga Jimbo la Dodoma Mjini.
 Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akitembelea ujenzi wa Zahanati ya Zepisa akiongozana na Mkurugenzi wa Global Space East Africa Ltd Ndg Gaston M. Francis aliyeoongozana na Mhandisi Malcom 

KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR ATANGAZA NEEMA

$
0
0
 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu.

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari M. Sururu amewataka Askari na Maafisa wa Jeshi la Uhamiaji kufanyakazi kwa Uweledi na kujituma ili kuweza kutekeleza vyema majukumu yao ya msingi ya kusimamia na kudhibiti Uingiaji, Ukaaji na Utokaji wa Watu Nchini. “Ili kuimarisha utendaji wetu ni vyema kuacha kufanya kazi kwa mazoea na muda wote, tutoe huduma za Uhamiaji bila ya Upendeleo, Unyanyasaji au Ucheleshwaji usio wa lazima. Tumieni lugha nzuri, zingatieni kwa vitendo dhana ya kumjali Mteja na Epukeni vitendo vya Rushwa wakati mkitoa huduma mbali mbali za Uhamiaji kwani Rushwa ni Adui nambari moja wa Haki” alisema Kamishna Sururu.
Kufanyakazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu ndio mhimili mkuu wa mafanikio ya Taasisi yoyote ile ikiwemo ya Uhamiaji. Maafisa na Askari wa Uhamiaji wanapaswa kuheshimu na kutii Kanuni zote za kijeshi, “Idara yetu imeingia rasmi kwenye mfumo wa Kijeshi nasi hatuna budi kufanyakazi kwa Kasi, Ari na Mori kuhakikisha kwamba jukumu la Ulinzi na Usalama wa Mipaka ya Nchi yetu linatekelezwa ipasavyo” alisema hayo wakati akizungumza na Askari na Maafisa wa Uhamiaji waliopo Mkoa wa Kaskazini Pemba, akihitimisha ziara ya kikazi katika Mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba iliyoanza tarehe 18 – 21 Disemba, 2017. 
Aidha katika ziara hiyo, Kamishna Sururu alipata fursa ya kutembelea maeneo mbali mbali yenye changamoto za uwepo vipenyo na Bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa maeneo hayo, kwa shughuli mbali mbali zikiwemo za uvuvi na biashara, baina ya visiwa vya Pemba na Mombasa, Kenya. Kisiwa cha Pemba kinasemekana kuwa na Bandari bubu zaidi ya mia tatu (300) ambapo inaelezwa kuwa ni kimbilio kwa baadhi ya Raia wa Kenya na Raia wa Somalia ndani ya visiwa vidogo vidogo vilivyomo ndani ya Wilaya za Micheweni, Wete na Mkoani, Pemba. 

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akipokea salamu kutoka kwa Askari wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati akiwasili Ofisi hapo kwa ziara ya kikazi Mkoani humo tarehe 20 - 21 Disemba, 2017. Kushoto ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Asumsio Achacha.

Kamishna Sururu aliwasisistiza Askari wa Uhamiaji kuongeza Doria na Misako ili kuwabaini wale wote wanaojipenyeza na kuishi nchini kinyume cha Sheria za Uhamiaji nchini. “Pamoja na changamoto zilizopo kutokana na Jiografia ya Visiwa vya Unguja na Pemba, hatuna budi kusimamia vyema jukumu la Udhibiti wa Ungiaji na Utokaji wa Watu” “Kama mnavyoelewa jitihada mbali mbali zinazochukuliwa na serikali zetu zote mbili katika kuboresha utendajikazi wetu, Idara inatarajia kupata vitendeakazi pamoja na vyombo vya usafiri yakiwemo Magari na Pikipiki, ambavyo vitasaidia kuboresha utoaji wa huduma zetu kwa Jamii” alifafanua Kamishna Sururu.

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Said M. Samaki akichangia hoja katika kikao cha pamoja na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar na Wafanyakazi wote wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA 

UVCCM YATAJA MAJINA YA WATAKAOHAKIKI MALI ZA JUMUIYA YAO

$
0
0
Na Said Mwishehe, Blogu ya Jamii

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) imetaja majina sita kati ya wanane ya wajumbe walioteuliwa  katika Kamati ya kuchunguza na kufuatilia mali za chama.

Hatua hiyo imekuja kutokana na maagizo ya Mwenyekiti wa Umoja huo Kheir James kutaka kuhakikiwa kwa mali zote za umoja huo.

Akizungumza leo katika Makao Makuu ya umoja huo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa umoja huo Shaka Hamdu Shaka ametaja majina ya wajumbe wa kamati hiyo ambayo itaongozwa na Mwenyekiti Maria Chaurembo.

Wengine ni Peter Kasera, Zelote Saitoti, Rose Manumbu, Sofia Kizigo na Elly Ngowi.

"Jukumu la kamati hiyo ni kufuatilia mali zote za umoja wetu, namna ambavyo zinatumika na mlolongo wa matumizi yake.

" Itaanza kazi haraka na wajumbe wengine wawili wa kamati hii wataungana na wenzao kufanikisha majukumu waliyopewa. Itakapomaliza kazi tutakuja kwenu kuelezea ambacho tumekibaini na nini cha kufanya,"amesema Shaka.

Amesema Mwenyekiti wao baada ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo moja ya majukumu ambayo ameamua kuanza nayo ni kufuatilia mali za chama na jukumu langu ni kuhakisha maagizo ya mwenyekiti wetu yanafanyiwa kazi tena kwa uhakika,"amesema Shaka.

MKURUGENZI MKUU WA SUMATRA ATINGA KITUO CHA UBUNGO KUANGALIA HALI YA USAFIRI KATIKA KUELEKEA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti ya  Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Gilliard Ngewe akipata maelezo kutoka kwa Kamanda wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo(kushoto) wakati ukaguzi wa mabasi katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti ya  Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Gilliard Ngewe(kulia)  akimpa  maelezo Mkaguzi wa mabasi wa Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo, Insp. Ibrahimu Samwix(kushoto) wakati wa ukaguzi wa mabasi katika kituo kikuu cha Mabasi leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa barabara wa  Sumatra, SACP Johansen Kahatano(kushoto) akimpa maelezo Mkaguzi wa mabasi wa Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo, Insp. Ibrahimu Samwix (kulia) wakati wa ukaguzi wa mabasi katika kituo kikuu cha Mabasi leo jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo(kushoto) akiangalia ukaguzi unaofanywa na Mkaguzi wa mabasi wa Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo, Insp. Ibrahimu Samwix(kulia)  leo wakati wa ukaguzi wa mabasi katika kituo kikuu cha mabasi ubungo leo jijini Dar es Salaam.
 Askari wa Usalama barabarani wa ukaguzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo, Nuru Hussein akimpa maelekezo dereva wa basi katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya abiria wakiwa katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo wakisubiri muda wa basi kuondoka katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo leo jijini Dar es  Salaam.

DED MOROGORO VIJIJINI KUCHUNGUZWA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo ameagiza kufanyika uchunguzi wa haraka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya morogoro Vijijini Sudi Mussa Mpiri kutokana na utendaji wake kutoridhisha ikiwemo kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo.

Pia ameshindwa kutoa ufafanuzi wa fedha zilizopokelewa na Halmashauri hiyo kiasi cha sh.milioni 1.6 ya mapato ya ndani kutoka kampuni ya Dimond ambapo matumizi ya fedha hiyo zaidi ya asilimia 90 hayafahamiki kilichofanyika. 

Kadhalika, Mkurugenzi huyo anadaiwa kuwa na mahusiano mabovu kati yake na watumishi wa Halmashauri hiyo.Jafo alitoa agizo hilo akiwa Kijijini Mvuha kwenye makao makuu ya Halmashauri ya morogoro vijijini.

Kutokana na hali hiyo,Jafo ameagiza kitengo cha uchunguzi na ufuatiliaji kilichopo Ofisi ya Rais TAMISEMI kufika haraka kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini mwenendo wa mkurugenzi huyo kwa lengo la kuchukua hatua stahiki endapo itabainika kuna ufisadi na mapungufu ya kiuongozi kwa mkurugenzi huyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Jafo hajarishishwa kabisa na miradi aliyo itembelea wilayani humo kutokana na miradi hiyo imeonyesha wazi kwamba Halmashauri hiyo imefanywa kama shamba la bibi. Jafo amewataka madiwani wa Halmashauri hiyo kufahamu kwamba wao wapo kwa niaba ya wananchi wanyonge hivyo wanapaswa kulinda na kusimamia rasilimali za Halmashauri hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya morogoro vijijini katika ukaguzi wa miradi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya morogoro vijijini akiwemo Mbunge wa Morogoro vijijini Omary Mgumba katika ukaguzi wa miradi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Morogoro vijijini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Morogoro vijijini.

Article 5

ULEGA ASHUHUDIA UCHOMWAJI WA ZANA HARAMU ZA UVUVI MKOANI KIGOMA

$
0
0
Kufuatia Wimbi la Uvuvi haramu mkoani Kigoma 
,Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalla Hamisi Ulega jana alishuhudia uchomwaji wa zana haramu za Uvuvi katika kijiji cha Buhingu  kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza,mkoani Kigoma.

Mwenyekiti wa kikundi cha Usimamizi shirikishi rasilimali za Uvuvi (BMUs) katika Kijiji cha Buhingu Bw.Richard Nkayamba amemweleza naibu Waziri kuwa kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanakomesha Uvuvi haramu katika Kijiji cha Buhingu na kuweka mazingira safi.

"Kwa kiasi kikubwa tumedhibiti  Uvuvi haramu pamoja na kutoa elimu kwa Jamii za Wavuvi, kuhusu Umuhimu wa Uvuvi endelevu kwa kushirikiana na vikundi vya Ulinzi shirikishi BMUs 21 pamoja na shirika lisilokuwa la kiserikali la Tuungane lililopo katika kijiji cha Buhingu"alisema Nkayamba

Aliongeza,"Tunakamata nyavu haramu bila kujali ni za nani,na hii inatujengea chuki kwa wamiliki wa Nyavu husika"Akiongea na uongozi wa Halmashauri ya Uvinza pamoja na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo,Ulega amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Uvinza kuona ni namna gani wanaweza kuziwezesha BMUs zilizopo kijijini hapo.

"Naombeni sana mziwezeshe hizi BMUs wapeni tenda za kukusanya Maduhuri ya Samaki kwa Wavuvi hawa ili hizi BMUs ziweze kujiendesha zenyewe"Mhe.Ulega alisisitiza kuwa kama wakipewa BMUs kukusanya Maduhuri basi watakuwa wametengeneza ajira kwa Vijana hao.VileVile aliwaasa sana BMUs kuwa Waadilifu ili waweze kuaminiwa"

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akishuhudia uteketezaji wa zana haramu za uvuvi katika Ziwa Tanganyika,kwenye mwambao wa  kijiji cha Buhingu mkoa wa Kigoma.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na viongozi mbalimbali na wananchi wa kijiji cha Buhingu mkoani  Kigoma.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akimkabidhi cheti ndugu Mapango Thomas cha utambuzi ili waweze kusimamia ipasavyo rasilimali za uvuvi

Mkuu wa Wilaya ya Uviza,Mwavua Mrindo akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali katika kijiji cha Buhingu mkoa wa Kigoma.


MKAZI WA NANYAMBA MKOANI MTWARA ASAKWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MUME WAKE

$
0
0
Na Obligado-Mtwara.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamtafuta Zuhura Ismail Mkazi wa Halmashauri ya Nanyamba Mkoani Mtwara kwa Kosa la Kumuua Aliyekuwa Mume wake kwa Kuchoma nyumba waliyokuwa wakiishii kwa kutumia mafuta ya Petrol kutokana na Wivu wa kimapenzi.

Zuhura ambaye anatafutwa na jeshi la Polisi,Majira ya Usiku alifika Nyumbani kwa mume wake huyo ambaye walikuwa wametengana na Kuhisi kuwa Ndani ya nyumba Mumewe alikuwa amelala na mwanamke Mwingine Hivyo Kuchoma Nyumba Moto na Kutokomea Kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya amewaomba wananchii wanamfahamu kutoa taarifa popote watakapomuoa Mwanamke Huyo Zuhura Ismail.

Aidha kamanda Mkondya ameongeza kuwa Watu 12 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za Wizi wa pikipiki pamoja na Kuvunja nyumba za watu na kuiba Vifaa mbalimbali vya majumbani.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara Limewataka wananchi waliotoa taarifa za kuibiwa wafike kituo cha Polisi kwa ajili ya Kutambua na kuchukua mali zao.
Pichani.Kamanda Wa Police Mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya akiwaonesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) Samani za Ndani Zilizokamatwa baada ya Kufanya Opereshen ya Msako kwa Watuhumiwa wa wizi pamoja na Madumu ya Pombe haramu ya Gongo Lita 369 ambapo watu 15 wamekamatwa wakifanya Biashara ya Kuuza na Kusafirisha.

VIJANA NCHINI WATAKIWA KUWA WAZALENDO

$
0
0
 Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) Jeremiah John Jilili akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu mchango wa vijana kuelekea uchumi wa viwanda leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jonas Kamaleki na Waziri wa Katiba Sheria na Utawa Bora wa Daruso Ibrahim Bimbalirwa.
 Waziri wa Katiba Sheria na Utawa Bora wa Daruso Ibrahim Bimbalirwa akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu mchango wa vijana kuelekea uchumi wa viwanda leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) Jeremiah John Jilili na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Mambo ya Nje Jumuiya za Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Malisa Martine.
 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Mambo ya Nje Jumuiya za Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Malisa Martine akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu mchango wa vijana kuelekea uchumi wa viwanda leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Katiba Sheria na Utawa Bora wa Daruso Ibrahim Bimbalirwa. 
Baadhi ya W3aandishi wa Habari wakifuatilia mkutano baina yao na viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuhusu mchango wa vijana kuelekea uchumi wa viwanda leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Frank Shija - MAELEZO)

POLISI TANGA YAWATAHADHARISHA WANANCHI KUELEKEA SIKUKUU

$
0
0
JESHI la polisi mkoani Tanga, limewahadharisha wananchi kuelekea katika msimu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya, kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani kama ulipuaji baruti na fataki ikiwemo kuchoma moto matairi barabarani, kwa yeyote atakayefanya hivyo atachukulia hatua za kisheri. 

Kamanda mpya wa mkoa huo, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Edward Bukombe, alisema kwamba jeshi hilo linapiga marufuku kwa mtu yeyote kulipua au kusababisha milipuko ikiwemo baruti, fataki na Eksozi za magari, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria namba 13 ya sheria ya milipuko. 

“Hivyo wakazi wa mkoa wa Tanga, ni marufuku kuchoma matairi hovyo na kulipua baruti bila kibali, kufanya hivyo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za nchi. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakae kiuka agizo hili,” alisema RPC Bukombe. 

Alisema uzoefu unaonesha kuwa siku za sikukuu watu wengi hujisahau kujiwekea ulinzi ikiwemo kuwaangalia watoto hivyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi kuhakikisha wanachukua hatua za kuwalinda watoto pamoja na nyumba zao ili wahalifu wasitumie mwanya huyo kufanya uhalifu wa kuvunja au watoto kupotea mitaani. 

Kamanda Bukombe alisema kwamba jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kuwa wananchi wanasherehekea sikukuu hizo kwa amani na utulivu bali aliwakumbusha kuzingatia taratibu za kumbi za burudani kufungwa nyakati za saa 6:00 usiku na hata ibada za mkesha wa Krismasi na Mwaka mpya zimalizike muda huo. 
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Edward Bukombe akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio yaliyotokea kwa kipindi cha mwaka mzima ambapo alisema Jumla ya Silaha 14 za moto zilikamatwa kulia ni RCO wa mkoa wa Tanga,Justine Masejo .
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Edward Bukombe akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio yaliyotokea kwa kipindi cha mwaka mzima ambapo alisema Jumla ya Silaha 14 za moto zilikamatwa, kushoto ni Afisa Mnadhimu wa Jeshi hilo Mkoani Tanga,Leonce na kulia ni RCO wa mkoa wa Tanga,Justine Masejo(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Sehemu ya waandishi wa habari wakichukua taarifa 

RAIS WA TFF WALLACE KARIA KUKUTANA NA WAHARIRI WA HABARI DEC 27 MWAKA HUU

$
0
0
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia (kulia, akiwa na Makamu wake Michael Wambura) atakutana na Wahariri wa Habari za Michezo Jumatano Desemba 27, 2017.

Pamoja na mambo mengine Rais Karia atazungumzia miezi minne tokea uongozi uliopo umeingia madarakani pamoja na vitu vilivyofanyika katika muda huo.
Aidha Rais Karia ataelezea changamoto mbalimbali zilizopo TFF pamoja na njia gani inatumika/Itatumika kuweza kupiga hatua kwa mpira wa Tanzania.
Taarifa zaidi za mkutano huo wa Rais Karia na Wahariri,mahali utakapofanyika pamoja na mualiko utatolewa kwa vyombo vya habari.

Huu ni mkutano wa kwanza wa Rais Karia na Wahariri wa habari za Michezo tokea ameingia madarakani.
Rais Karia aliingia madarakani August 12, 2017 kwenye uchaguzi uliofanyika mkoani Dodoma baada ya kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi ambao pia uliwaingiza madarakani Michael Wambura kwenye nafasi ya makamu wa Rais. Wajumbe wa kamati ya utendaji waliongia madarakani kwenye uchaguzi huo ni pamoja na


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUWASILI MKOANI RUVUMA JIONI YA LEO

BALOZI SEIF ATAKA UWEKEZAJI KWENYE UCHAPISHAJI WA VITABU VYA KISWAHILI

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati umefika kwa Wafanyabiashara wakubwa Nchini kuwekeza katika uchapishaji wa Vitabu vya Kiswahili pamoja na kujenga Maduka makubwa ya kuuzia kazi za Kiswahili kwa vile bidhaa zinazotokana na lugha hiyo zinauzika.

Alisema Mwanataaluma au mswahili anayehitaji vitabu vya Waandishi Mahiri wa Lugha hiyo wa Zanzibar kama Profesa Said Ahmed Mohamed, Shafi Adam Shafi, Bwana Msa na wasanii wengine kama Mohamed Seif Khatibu kamwe kwa wakati huu anashindwa kuvipata.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati alipokuwa akilifunga Kongamano la Kimataifa la Siku mbili la Lugha ya Kiswahili lililokuwa likifanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliopo Mtaa wa Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Alisema ni faraja iliyoje kwa sasa kuona kiasi gani Lugha ya Kiswahili inavyoendelea kupata heshima ya kutambuliwa na kukubaliwa Kimataifa hasa kutokana na upatikanaji wa mwitiko mkubwa wa kuwa na Wataalamu waliobobea katika nyanja mbali mbali.
 Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akitoa vyeti kwa Mmoja wa Washiriki wa Kongamano la kwanza la Kimataifa la Kiswahili lililofanyika Zanzibar kwa Siku mbili.
Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kushoto akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bakiza Dr. Mohamed Seif wakiangalia baadhi ya vitabu vya Kiswahili vilivyotungwa na Magwiji wa Lugha ya Kiswahili na kusomeshwa katika skuli na vyuo mbali mbali ndani na nje ya Nchi.
Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na Dr. Khatib wakifurahia moja ya Kitabu  mashuhuri cha Mtungaji Gwiji Zanzibar Bwana Mohamed Said  (Maarufu Bwana Msa).Picha na – OMPR – ZNZ.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KITABU CHA KULETA MABADILIKO CHAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Kampuni ya Viva Legency inayohusika na mafunzo na ushauri elekezi imekuja na kitabu kinachojulikana kama "SOTE TUNAWEZA" kikiwa na lengo la kusaidia harakati za mabadiliko pamoja na kukuza utamaduni wa mtanzania.

Akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Viva Legency Fortunata Temu amesema kuwa kitabu cha "SOTE TUNAWEZA" kimeandikwa kwa lugha ya kiswahili na kinampa msomaji uwezo mkubwa wa kubadili fikra na kupiga hatua ya kimaendeleo.

"Kitabu cha sote tunaweza kimeandikwa kwa lugha ya kiswahili na kinampa uwezo msomaji kubadili kifikra na kupiga hatua kiamaendeleo" amesema Fortunata.Amesema kuwa katika uandishi wa kitabu hicho wametumia mifano ya watu mbalimbali kutoka Tanzania na sehemu nyingine za dunia waliofanikiwa na kusema kuwa wametumia mifano hiyo ili kumtia hamasa msomaji na kumfanya kufuata nyendo za hao watu waliofanikiwa.

Fortunata ameongeza kuwa mafanikio yanaweza kupatikana kwa kuangalia fursa zinazopatikana ndani ya jamii hivyo kuwataka watanzania kutumia lugha ya kiswahili kama fursa kwa kuhabarishana na kuelimishana .Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dk.Ave Maria Semakafu ameipongeza kampuni ya Vivalegency na kusema kuwa kitabu cha "SOTE TUNAWEZA" kimekuja wakati mwafaka kwa sababu nchi yetu ipo kwenye harakati za mabadiliko kuelekea uchumi wa kati.

"Sote tunaweza kimekuja wakati mwafaka kwa sababu nchi yetu ipo kwenye harakati za mabadiliko kuelekea uchumi wa kati" amesema Dk.Semakafu.

Amesema Tanzania inachangamoto kubwa katika utamaduni wa uandishi na usomaji vitabu na kuwaomba watanzania watumie fursa ya kuandika vitabu vyenye dhima yenye kuleta maana na kuachana na utamaduni wa kuandika vitabu ambavyo havina dhima yoyote ya kubadili fikra na kuleta chachu ya maendeleo.
 Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Viva Legacy (T) Bi. Fortunata Meela Temu akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa kitabu chaake cha "SOTE TUNAWEZA" leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt. Avemaria Semakafu na Mwajiri Msaidizi wa Viva Legacy (T) Ltd Bi. Neema Seleman.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa kitabu chaake cha "SOTE TUNAWEZA" leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus, na Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa VIVA lEGACY lTD (t) Bi. Fortunata Meela Temu.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Stadi Dkt. Avemaria Semakafu (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Viva Legacy Ltd (T) Bi. Fortunata Meela Temu wakiwaonyesha Waandishi wa Habari kitabu cha "SOTE TUNAWEZA"  leo Jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho kimetungwa kwa lengo la kuimarisha mfumo wa utendaji na hasa kuboresha rasilimali watu. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano baina yao na  na Mkurugenzi wa Viva Legacy (T) Ltd  alipokuwa akizungumzia kuhusu uzinduzi wa kitabu cha SOTE TUNAWEZA leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na: Frank Shija - MAELEZO)

YANGA YATEUA KAMATI YA MABADILIKO IKIONGOZWA NA ALEX MGONGOLWA

$
0
0

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Klabu ya Yanga imeuanza rasmi mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji kwa kumteua Wakili Alex Mgongolwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo..

Mgongolwa atasaidiwa na wajumbe watano ambao ni Mheshimiwa Said Mecky Sadick, Profesa Mgongo Fimbo, Felix Mrema, George Fumbuka na Mohammed Nyengi.

Kamati hiyo imetangazwa leo Ijumaa na Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Boniface Mkwasa ikiwa ni siku chache tu tangu watani wao Simba kupitisha mchakato huo na kumpata mwekezaji ambaye alishinda zabuni hiyo.

Yanga wao wamefuata Katiba yao ya mwaka 2010 inayoelekeza kuwa mwekezaji ni lazima awe na asilimia 49 na 51 ziwe za wanachama kwa maana ya klabu kama serikali ilivyofanya mabadiliko ya Katiba katika kipengele cha mfumo wa uendeshaji wa Hisa.

Mbali na hilo Kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga iliyokukutana jana hii tarehe 21/12/2017 makao makuu ya klabu hiyo katika kikao maalumu,imeteua majina 28 ya wanachama kuunda kamati mpya ya mashindano.

HIZI NDIO SABABU ZA AIRTEL KUWA MALI YA TTCL

Viewing all 110150 articles
Browse latest View live




Latest Images