Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109604 articles
Browse latest View live

MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA KHEIR JAMES AKUTANA NA WENYEVITI NA MAKATIBU WA MKOA MJINI DODOMA

0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Ndg Kheir James  (MCC) amekutana na kufanya mazungumzo na Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa yote nchini wa UVCCM.  

Kikao hiko kimefanyika ukumbi wa mikutano CCM Mkoa wa Dodoma kilihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM  Ndg Tabia Mwita Maulid na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka.
 Baadhi ya Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa yote nchini wa UVCCM wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Ndg Kheir James  (MCC) akizungumza mapema jana alipokutana na kufanya mazungumzo na Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa yote nchini wa UVCCM.
  Baadhi ya Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa yote nchini wa UVCCM wakifurahia jambo 
.

UTENGANISHAJI WA UPELELEZI NA UENDESHAJI KESI UMEKUWA NA TIJA –DPP

0
0
Na Mwandishi Maalum,

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Magaga,(DPP) amesema , utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kutengenisha jukumu la upepelezi na upelelezi mashataka umekuwa wa mafanikio makubwa yakiwamo yakupunguza mlundikano wa mahabusu.

Mkurugenzi wa Mashtaka ameyasema hayo wakati alipokuwa akielezea utekelezaji wa mpango huo tangu ulipoanzishwa kwa sheria ya mfumo wa mashtaka 2007,mbele ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali linalokutana kwa siku mbili mkoani Dodoma.

“ Tangu kuanza kwa mpango huu tumepata mafanikio makubwa, kwani kwa sasa kumekuwa na wafungwa wengi kuliko mahabusu kwa maana kwamba idadi ya mahabusu imezidi kwa 2000 kama ilivyo kuwa huko nyuma ”. Akabainisha Mkurugenzi wa Mashtaka.Mpango wa serikali wa kutenganisha shughuli za upelelezi na mashtaka ulilenga kuondoa tatizo la haki kuchelewa kutendekea na kesi kuchukua muda mrefu mahakamani kwa sababu ya muda mrefu unaotumika katika upelelezi.

Mafanikio mengine kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashtaka ni jamii kurejesha imani kwa vyombo vya sheria kutokana na haki kutendeka na kwa wakati na hivyo kupunguza vitendo vya wananchi kujichukulia hatua mkononi.Mafanikio mengine kesi zinazoendeshwa na Mawakili wa Serikali zimekuwa na mafanikio makubwa ikilinganishwa na zile ambazo zinasimamiwa na mawakili wakujitegemea. Kiasi cha kusababisha kupunfua kwa ukataji wa rufaa na mashauri ya jinani kupugua kutokana na jamii kutambua uhalifu haulipi.

“ Kutokana na utekelezaji wa mpango huu, siyo tu kumepunguza rufani zinazopelekwa Mahakama ya Rufaa kwa wakata rufaa kupungua kutokana na weledi wa mawakili na kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya kuiwakilisha serikali Mahakamani”.Amebainisha Mkurugenzi wa Mashtaka.

Akaongeza pia kwamba hata barua za malalamiko kutoka kwa wananchi zimepungua kiasi kwamba mafaili hayajai tena barua za malalamikio kama ilivyokuwa huko nyuma na hiki ni nikielelezo kikubwa kwamba wananchi wanapata huduma za kisheria kwa ufanisi mkubwa” akasisitiza Mkurugenzi wa Mashtaka. 

Pamoja na mafanikio hayo, Mkurugenzi wa Mashtaka ameelezea baadhi ya changamoto ni kutokuwapo kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika baadhi ya Wilaya hususani katika baadhi ya Wilaya ambazo zinamtukio mengi ya jinai.Amesema ufinyu wa bajeti na upungufu wa raslimali watu ndiyo unaochangia au kurudisha nyuma kasi ya ufunguzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kila wilaya ili kuwafikishia huduma kwa karibu wananchi.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Mashtaka ametoa rai kwa Mawakili Wafawidhi pamoja na Mawakili wote kutekeleza majukumu yao ya kuisimamia Serikali bila woga na kwa kuzingatia maadili na weledi na wasikubali kuyumbishwa.“Tekelezeni majukumu yenu kwa mujibu wa taaluma yenu, msiogope kusimamia ukweli na kile mnachokiamini katika utekelezaji wa majukumu yenu”. Akasisitiza Mkurugenzi wa Mashtaka.
Mkurugenzi wa Mashtaka ( DPP) Bw. Biswalo Magaga akiwaeleza wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu namna utekelezaji wa utenganishaji wa shughuli za uendeshaji mashtaka na upelelezi unavyoleta tija na mafanikio yakiwamo ya kupunguza msongamano wa mahabusu magerezani. wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju, Makamu Mwenyekiti, Bw, Gerson Mdemu na Katibu Msaidizi wa Baraza, Bw. Michael Masanja
Wakili wa Serikali Mwandamizi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoa wa Mwanza, Revinna Tibilengwa akichangia majadiliano kuhusu utekelezaji wa utenganishaji wa shughuli za mashtaka na upelelezi
Wakili Mfawidhi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Mkoa wa Ruvuma, Bw. Renatus Mkude, akiwasilisha taarifa kwa niaba ya Mawakili Wafawidhi wa Mikoa na Wilaya ambako zipo Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali mbele ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali 

Ziara ya Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Mkoa wa Kusini Pemba

0
0
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (kushoto) akikagua baadhi ya magari chakavu yaliyopo katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, yanayosubiri kupigwa mnada baada ya kukamilika kwa taratibu za uuzaji wa Mali za Serikali. Wakati wa ziara ya kikazi Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 – 19 Disemba, 2017. Pamoja na kutembelea maeneo mbali mbali ya utendaji kazi Mkoani humo ikiwemo Bandari ya Mkoani, Bandari ya Wesha iliyopo Chake Chake na Bandari bubu kadhaa. Kulia kwake ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdi Bulushi. 
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia za Kengeja na Muwambe, Kusini Magharibi mwa kisiwa cha Pemba, kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii, ambazo hutumika kama vipenyo kwa watu kuingia na kutoka visiwani humo kinyume na taratibu za Uhamiaji. Wakati alipofanya ziara ya kikazi maeneo mbali mbali ndani ya Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 Disemba, 2017. 
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akitoa nasaha zake kwa Maafisa, Askari na watumishi Raia wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, wakati akihitimisha ziara ya kikazi Mkoani humo Leo tarehe 19 Disemba, 2017. Aidha, Kamishna Sururu aliwataka watumishi wote kuzingatia maadili ya kazi, pamoja na kutilia mkazo matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii. “Naelewa tupo kwenye utandawazi, lakini narudia kuwasihi matumizi ya Mitandao ya kijamii itumike kwa kuzingatia Kanuni na Miongozo ya Serikali, pia mjiepushe na utoaji wa Siri na Taarifa za serikali, ni mwiko kutoa taarifa yoyote. fuateni Sheria na Taratibu tulizowekewa”. 
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia za Kengeja na Muwambe, Kusini Magharibi mwa kisiwa cha Pemba, kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii, ambazo hutumika kama vipenyo kwa watu kuingia na kutoka visiwani humo kinyume na taratibu za Uhamiaji. Wakati alipofanya ziara ya kikazi maeneo mbali mbali ndani ya Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 Disemba, 2017. 
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdi Bulushi akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili kulia) na Maafisa Uhamiaji aliombatana nao, matunzo na usafi wa mazingira katika nyumba za Makaazi ya Askari wa Uhamiaji, zilizoko eneo la Ndugukitu, Wilaya ya Chake chake, Mkoa wa Kusini Pemba. Kamishna Sururu yupo Mkoa wa Kusini Pemba kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 18 – 19 Disemba, 2018. Aidha, Nyumba hizo zilifunguliwa rasmi na Mhe. Makamo wa Pili wa Rais, Balozi Seif Iddi mapema mwezi Januari, 2017.
Mojawapo ya nyumba za Makaazi ya Askari wa Uhamiaji, zilizoko eneo la Ndugukitu, Wilaya ya Chake chake, Mkoa wa Kusini Pemba. Kamishna Sururu yupo Mkoa wa Kusini Pemba kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 18 – 19 Disemba, 2018. Aidha, Nyumba hizo zilifunguliwa rasmi na Mhe. Makamo wa Pili wa Rais, Balozi Seif Iddi mapema mwezi Januari, 2017.


TMRC YAWEZESHA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO WANNE

0
0
 Kampuni ya Tanzania Mortgage Refinance Limited (TMRC), imetoa msaada wa kiasi cha Shilingi milioni Nane (Shilingi 8,000,000) kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto wanne jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi mfano wa hundi hiyo ya Shilingi milioni Nane kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (JKCI), Profesa Mohamed Janabi, Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa TMRC, Oscar Mgaya, alisema kuwa wameamua Kuitikia wito huu wa kuwasaidia watoto hao ambao hawana uwezo na bila msaada huo pengine wasingeweza kupata huduma hiyo na maisha yao yangekua hatarini.
"Tumeamua kusaidia tiba kwa hawa watoto baada ya kuona tangazo kwenye kituo cha televisheni cha Clouds. Hivyo basi, tukaona umuhimu wa kufanikisha malipo kwa ajili ya upasuaji wa watoto hawa wanne," Bw. Mgaya alisema.
Aidha, Mtendaji Mkuu huyo, alisema taasisi yake hiyo ambayo inatoa mikopo ya ujenzi au ununuzi wa nyumba kupitia mabenki na taasisi nyingine za fedha kuwa, waliamua kutoa kiasi cha Shilingi milioni mbili (Shilingi 2,000,000) kwa upasuaji wa kila mtoto kwa kuwa ni taifa la kesho.  Hii ni sehemu ya kutekeleza wajibu wetu katika jamii (corporate social responsibility).   
"Tumeamua kutoa kiasi kidogo  kwa watoto hawa wadogo ambao miongoni mwao wana ndoto za kuwa wataalamu wa benki, madaktari, marubani n.k. Hivyo, taasisi yetu imeona umuhimu wa kufanya ndoto za hawa watoto kutimia kwa kuwawezesha kupata tiba," alisema.
Bw. Mgaya ametoa rai kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia wenye uhitaji wa tiba hii ya moyo hasa kwa wale wenye maisha duni ambapo uhitaji unaelezewa kuwa ni mkubwa.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (JKCI), Profesa Mohamed Janabi, alisema kwamba taasis yake imejipanga kuhakikisha kuwa inaendelea kupunguza idadi ya wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje ya nchi, kutokana na magonjwa ya moyo na badala yake kutibiwa nchini kwa gharama nafuu.
"Licha ya kuwasaidia watanzania kupunguza gharama kwa matibabu ya moyo hapa nchini badala ya nje ya nchi, pia hii imepunguza sana gharama ambazo serikali imekuwa ikizitumia kila mwaka kutibu maradhi kama hayo nje ya nchi," Prof Janabi alisema.
Tangu taasisi yetu ianze kutoa tiba hii mwaka 2008, tumeweza kupunguza kwa kiwango kikubwa idadi ya watanzania wanaotibiwa nje ya nchi. Hata hivyo, ameishukuru TMRC, kwa msaada wa fedha kwa ajili ya tiba kwa watoto hao wanne na kuziomba taasisi nyingine kuiga mfano.

TANESCO YAHIMIZA MATUMIZI BORA NA ENDELEVU YA MTO PANGANI NA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU

0
0
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MATUMIZI bora ya bonde la Mto Pangani, ndio njia pekee itakayosaidia kutunza vyanzo vya maji ambayo hutumika kuzalisha umeme kwenye vituo vya Pangani Hydro Systems, Meneja wa vituo hivyo, Mhandisi Mahenda S Mahenda amewaambia wahariri wa vyombo vya habari wanaotembelea bwawa la Nyumba ya Mungu lililoko mpakani mwa wilaya ya Mwanga na Simanjiro.

“Tanesco kama wadau wakubwa wa Mto huu, tumeona Mto umeingia mchanga na mchanga huo unatakiwa kuondolewa ili kuweza kuzalisha maji mengi zaidi kutoka bwawa la Nyumba ya Mungu na maji hayo yaweze kupatikana kwenye vituo na hatimaye kuzalisha umeme kama ambavyo inatakiwa.” Alisema Mhandisi Mahenda.
Pangani Hydro Systems ni mkusanyiko wa vituo vitatu vya kufua umeme vinavyofuatana ambavyo vimejengwa sehemu tofauti tofauti katika Mto Pangani.
Vituo hivyo ni pamoja na Nyumba ya Mungu, kituo cha Hale na kituo cha New Pangani Falls na vyote kwa ujumla wake huzalisha umeme wa Megawati 97 ambazo huingizwa kwenye Gridi ya Taifa, alisema Mhandisi Mahenda.
Kituo cha Nyumba ya Mungu, kilizinduliwa mwaka 1964 na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, na kina mashine mbili za kufua umeme zilizofungwa tangu mwaka huo na kila moja inao uwezo wa kuzalisha Megawati 4 za Umeme na kufanya jumla ya Megawati 8
Hata hivyo changamoto kubwa inayokikabili kituo hicho na vituo vingine ambavyo vyote huendeshwa kwa kutumia nguvu za maji, ni mabadiliko ya tabia nchi na ongezeko la shughuli za kibinadamu kandokando ya Mto huo pamoja na kwenye bwawa lenyewe na hivyo kupelekea upungufu wa mara kwa mara wa maji ya kutosha kuendesha mitambo.
“Tunashirikiana na wenzetu wanaosimamia bonde la Mto Pangani, kwa kufanya doria za mara kwa mara ili kuwaelimisha wananchi matumizi bora na endelevu ya maji ya Mto huo ili kuleta manufaa kwa pande zote, amesema Mhandisi Mahenda.
Mhandisi Mahenda S. Mahenda(kulia), akifafanua mambo mbalimbali kwa wahariri kwenye bwawa la Nyumba ya Mungu Desemba 19, 2017

WAHAMIAJI HARAMU 55 WAMAKATWA WILAYANI MKINGA

0
0
ZAIDI ya wahamiaji 50 raia kutoka nchini Ethiopia wameka matwa eneo la Duga wilayani Mkinga mkoani Tanga kwa kosa la kiungia nchini kinyume cha sheria.

Wahamiaji hao wamekamatwa ndani ya kipindi cha mwezi Desemba mwaka huu kutokana na operesheni ambazo zimekuwa zikiendeshwa na Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ya kuhakikisha wanazibiti wimbi la uingiaji huo.


Hayo yalisemwa jana na Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Tanga DCI, Crispian Ngonyani wakati akizungumza ofisi kwake ambapo alisema wahamiaji hao hivi sasa wanaendelea na kesi zao zinazowakabili kutokana na kuingia nchini kinyume na utaratibu uliopo.


Alisema hatua ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao inatokana na kuwepo kwa misako ya kushtukiza katika maeneo mbalimbali hasa ya mipakani mkoani hapa ambapo wahamiaji hao wamekuwa wakitumia kama njia ya kuingilia.


“Sisi kama Uhamiaji mkoani Tanga tumejipanga vizuri kuhakikisha wimbi la wahamiaji haramu hawaingii kutokana na doria ambazo tumekuwa tukizifanya mara kwa mara lakini kubwa zaidi ni kuwepo kwa vituo eneo la mipakani hususani Horohoro “Alisema.


Aidha alisema pia ili kuhakikisha suala hilo linazibitiwa kwa vitendo tayari wamekwisha kuweka kituo eneo la Vijinga wilayani Mkinga kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wanakagua magari ambayo yamekuwa yakitokea nchini Jirani ya Kenya  ili kuweza kubaini iwapo wahamiaji haramu wamebebwa.


Hata hivyo alisema kuelekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya wamejiandaa vizuri kuweza kukabiliana na wimbi la wahamiaji haramu wanaoweza kuingia mkoani hapa kwa kuendelea operesheni kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo nyumba za kulala wageni na kwenye hoteli.


“Licha ya kuendelea na operesheni hizo lakini nisema idadi ya wahamiaji haramu wanaoingia mkoani Tanga kwa sasa imepungua kwa sababu wakiwakamata wanawapeleka mahakamani pamoja na mawakala wao"Alisem

Afisa Uhamiaji huyo alisema lakini bado tunaendelea kuhakikisha ina koma kabisa kwa kuwachukulia hatua kali na watanzania ambao watabainika wanashirikiana nao kuwaingia mkoani hapa(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

MATUKIO YANAYOJIRI KATIKA ZIARA YA KIKAZI YA BALOZI MAHIGA NCHINI CHINA

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiongea jambo wakati alipokuwa katika mazungumzo rasmi na Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian Keming jijini Beijing. 
Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian Keming akisisitiza jambo alipokuwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt.Augustine Mahiga leo jijini Beijing. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa na ujumbe wake aliongozana nao katika ziara ya kikazi nchini China. Kutoka kushoto ni Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China, Kanali Remigius Ng'umbi anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Thomas Kashililah na Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki.
Wajumbe wa pande mbili za China na Tanzania wakiwa katika mazungumzo. 
Wajumbe wengine wa Tanzania wakifuatilia mazungumzo. Kutoka kulia ni Kamishna Msaidizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Malmeltha Mutagwaba, Naibu Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango kutoka Serikali ya Zanzibar, Bw. Khamis Omar.
Balozi Mahiga akitoa zawadi ya picha kwa Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian Keming. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Mlimani City Mall yatangaza zawadi ya X-Mas na Mwaka Mpya

0
0
Katika kusherehekea Sikukuu za X-Mas na Mwaka Mpya, uongozi wa Mlimani City kwa kushirikiana na wafanyabiashara wenye maduka ndani yake umetangaza ofa maalumu kwa wateja  wake watakaofanya manunuzi katika msimu huu wa sikukuu.
Ofa hiyo inatoa fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali ambazo zimegawanywa kwa makundi matano ambapo kila wiki washindi 20 watajishindia vocha yenye thamani ya kufanya shoping kwa vitu vya thamani ya Shilingi 100,000 lakini pia watakuwa mwameingia moja kwa moja kwenye droo kubwa ya mwisho ambayo mshindi wa kwanza atajishindia vocha ya manunuzi ya bidhaa za nyumbani yenye thamani ya Shilingi Milioni 10, na mshindi 5 watajinyakulia vocha yenye thamani ya shilingi milioni 1, kila mmoja.  
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja mkuu wa Mlimani City Ndugu Pastory Mrosso alisema kuwa washindi wa kila wiki watafanya manunuzi katika duka lolote ndani ya Mlimani City kwa kutumia vocha zao.
Promosheni hii maalumu imeanza Desemba 15 na inatarajia kufikia mwisho Januari 14, 2018, ambapo droo kubwa ya kupata mshindi wa kwanza wa Vocha yenye thamani ya Shilingi milioni 10.
Meneja huyo aliwaomba watanzania kuendelea kufanya manunuzi yao katika maduka ya Mlimani City, kutokana na kuwajali wateja wake na kutoa huduma zinazokwenda na wakati na hasa katika kipindi hiki cha X-Mas na Mwaka Mpya.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Secta Binafsi nchini Tanzania(TPSF), Godfrey Simbeye akichagua kuponi ya mshindi wa kwanza wa promosheni ya ‘Fanya shoping mlimani City na ushinde zawadi katika kipindi hiki cha siku kuu ya Chrismass na Mwaka Mpya iliyozinduliwa rasmi jana Mlimani City.Kushoto kwake ni Meneja wa Mlimani City, Pastory Mroso na wengine mabalozi wa kampeni hiyo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Secta Binafsi nchini Tanzania(TPSF), Godfrey Simbeye akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya ‘Fanya shoping mlimani City na ushinde zawadi katika kipindi hiki cha siku kuu ya Chrismass na Mwaka Mpya iliyozinduliwa rasmi jana Mlimani City.Kulia ni Meneja wa Mlimani City, Pastory Mroso.

RAIS MAGUFULI ATOA ONYO KWA WALE WANAOPOTOSHA TAKWIMU.

0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa onyo kwa wale wote wanaotoa takwimu za upotoshaji kuacha mara moja na kuzitaka mamlaka husika kuwachukulia hatua.

Rais Magufuli ametoa onyo hilo leo mjini Dodoma wakati wa uwekaji jiwe la msingi la jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dodoma.

“Watanzania mfuate takwimu zinazotolewa na vyombo husika,ukitaka takwimu zozote nendeni kwa wataalamu na wahusika wanaotoa takwimu sahihi kwa sababu ukikosea kutoa takwimu sahihi umeichafua nchi” ameongeza Dkt. Magufuli.

Dkt Magufuli ameongeza kuwa takwimu ni muhimu katika Nyanja zote ikiwemo kusaidia kupanga mipango ya maendeleo ya nchi ambapo husaidia kuweka malengo, kupanga malengo na pia kuliwezesha taifa kujipima kiasi gani imefikia maendeleo.

Aidha,akizungumzia hali ya ukuaji wa uchumi nchini Dkt Magufuli amesema kuwa katika nusu ya mwaka huu uchumi umekuwa kwa asilimia 6.8 ambao umepelekea kuongoza kwa nchi za Afrika Mashariki na kuwa miongoni mwa nchi za Afrika ambapo uchumi wake unaokuwa kwa kasi.

Wakati huo huo, Dkt Magufuli amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango kufuatilia Kampuni ya Airtel kujua ukweli ya kwamba Kampuni hiyo ni sehemu ya Kampuni ya TTCL.

Mbali na hayo Dkt. Magufuli ameishukuru Benki ya Dunia, Serikali ya Canada na Shirika la misaada la Uingereza (DFID) kwa misaada wanayoendelea kuipatia nchi na kuwaahidi kuwa kila senti ya msaada itakayotolewa na mashirika hayo itatumika ipasavyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) amesema kuwa Tanzania imekuwa nchi ya pili barani Afrika baada ya Afrika Kusini katika utoaji wa Takwimu bora kati ya nchi 54 ikiwa ni tathimini ya Benki ya Dunia mwaka 2016.

“Tumeendelea kutoa mafunzo kwa wanatakwimu katika taasisi za Serikali, Idara na Wizara ili kuendana na mabadiliko katika eneo la takwimu” ameongeza Dkt. Chuwa.

Nae Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ameongeza kuwa ujenzi wa jengo hilo ni matokeo ya agizo la uhamasishaji wa Serikali kuhamia Makao Makuu ya nchi Dodoma.

“Ujenzi wa jengo hili unagharimu shilingi Bilioni 11.6 mpaka kukamilika kwakwe na pia ujenzi umetoa ajira za muda wa wastani kwa vijana 120 kila siku huku asilimia 100 ya vifaa vinavyotumika katika jengo hili ni vifaa kutoka ndani ya nchi, ujenzi wa jengo hili unatarajiwa kumalizika mwezi Januari, 2018” amefafanua Dkt. Mpango.

Pia Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird ameipongeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kuwa miongozi mwa Ofisi bora katika utoaji wa takwimu.

“Tanzania imefanya maendeleo makubwa katika uhifadhi wa takwimu, hivyo Benki ya Dunia itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Takwimu ili kuweka mifumo thabiti ya kukuza uchumi wa viwanda” amefafanua Mkurugenzi huyo.

Akizungumzia kuhusu upotoshaji wa takwimu hasa kwa vyombo vya habari nchini, Mkurugenzi Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas amevitaka vyombo vya habari na wanahabari nchini kuhakikisha wanatumia takwimu sahihi na zinazotoka katika vyombo sahihi ili kuendeleza weledi wa taaluma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia  wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu mjini Dodoma leo Desemba 20, 2017.

PICHA NA IKULU

UKAGUZI WA MABASI UBUNGO NI ENDELEVU KATIKA KULINDA USALAMA SAFARI ZA ABIRIA –KAMANDA SOLOMON

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo amesema kuwa ukaguzi wa basi katika kituo cha Ubungo ni endelevu ikiwa ni kulinda usalama wasafiri wanaokwenda mikoani na si vinginevyo.

Kamanda Mwangamilo ameyasema hayo leo wakati ukaguzi wa basi za mikoani katika kituo kikuu cha basi Ubungo jijini Dar es Salaam, amesema kuwa katika kufanya ukaguzi pamoja na kuangalia wananchi wanasafiri kwa bei elekezi zilizotolewa na serikali kutokana na baadhi ya watu wa kupandisha nauli kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Amesema kuwa baadhi ya basi 10 zimetolewa namba za usajili kutokana na kubainika kuwepo kwa makosa ya kiufundi na baada ya kufanyiwa marekebisho watarejea na safari.

Kamanda Mwangamilo amesema kuwa kusitisha kwa basi lisifanye safari likiwa na abiria hakuna nia mbaya bali kuangalia usalama wananchi kuwa safari kuwa ya uhakika.

Nae Afisa Elimu wa Baraza la  Walaji  la Mamlaka ya Usafri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRACC), Nicholous Kinyariri amesema kuelekea mwisho wa mwaka kuna baadhi ya kampuni zinapandisha nauli hivyo lazima liangaliwe .

Kinyariri amesema kuwa  katika kipindi hiki wanataka ushirikiano kwa wananchi pale wanapoona kuna vitu vinakwenda nje ya utaratibu ili sheria ichukue mkondo wake.

 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo akitoa maelekezo katika kwa askari wa usalama barabarani katika kituo kikuu cha basi Ubungo jijini Dar es Salaam.
Askari wa kikosi cha Usalama barabarani  aking'oa namba ya usajili wa basi la kampuni ya Muro Princess baada ya kukutwa na makosa hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa abiria leo jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo akimpa maelezo Mkaguzi wa Ukaguzi wa mabasi katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo, Ibrahim Samwix wakati ukaguzi mabasi katika kituo hicho.es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU MJINI DODOMA LEO

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Mhe. Bella Bird  wakifungua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu mjini Dodoma leo Desemba 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akipeana mikono na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Mhe. Bella Bird  wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa  jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu mjini Dodoma leo Desemba 20, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akipeana mikono na Mwenyekiti wa Bodi ya  Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Andrew Wilson Massawe wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu mjini Dodoma leo Desemba 20, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akipeana mikono na Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Miles wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu mjini Dodoma leo Desemba 20, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa Majaliwa wakizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu mjini Dodoma leo Desemba 20, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akipokea kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ramani ya Tanzania yenye kuonesha takwimu ya hali ya  maambukizi ya VVU kimkoa wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu mjini Dodoma leo Desemba 20, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia  wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu mjini Dodoma leo Desemba 20, 2017.

PICHA NA IKULU

INASIKITISHA! MAKOSA YA UBAKAJI, KUNAJISI YASHIKA KASI MWAKA 2017

0
0
Said Mwishehe, Blogu ya jamii
INASIKITISHA! Ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Jeshi la Polisi nchini kusema kuwa mwaka huu wa 2017 matukio ya ubakaji na kunajisi watoto yameongezeka na kushika kasi ikilinganishwa na mwaka 2016

Imefahamika sababu ya kuongezeka kwa matukio hayo ni ushirikina, tamaa ya mwili na mmomonyoko wa maadili kwenye jamii ya Watanzania

Akizungumza Dar es Salaam leo, kwenye  Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI) Robert Boaz amefafanua makossa dhidi ya binadamu yanayojumuisha mauaji, kubaka, kulawiti, wizi wa watoto, kutupa watoto, kunajisi na kusafirisha binadamu yameripotiwa

“Katika kundi hili makosa ambayo yameonekana kuongezeka ni makosa ya kubaka na kunajisi.Zipo sababu nyingi lakini kubwa ni ushirikina, kukosekana kwa maadili na tamaa ya mwili.

“Jeshi la Polisi tutaendelea kufuatilia wanaojihusisha na matukio hayo na kisha sharia ichukue mkondo wake.Tunaomba  jamii nayo ishirikiane na jeshi lao kutoa taarifa dhidi ya wanaojihusisha na matukio ya aina hiyo,”amesema.

Ameongeza takwimu zinaonesha makosa ya kubaka na kunajisi yameongezeka. Novema mwaka 2016 makosa ya kubaka yaliyoripotiwa yalikuwa 6,985 ikilinganishwa na makosa 7,460 ambayo yameripotiwa mwaka huu.

Amesema hilo ni ongezeko la makosa 478 sawa na asilimia 6.8, wakati makosa ya kunajisi yalikuwa 16 kwa mwaka 2016 ikilinganishwa na makosa 25 mwaka huu wa 2017 na kufanya ongezeko la makosa 9 sawa na asilimia 56.3.

Kuhusu matukio ya wizi wa mali kwa kutumia silaha, unyang’anyi ,wizi wa pikipiki , wizi wa magari ,wizi wa mifugo na kuchoma moto nyumba. Amesema matukio ambayo yaliripotiwa mwaka 2016 yalikuwa makosa 34,830 wakati mwaka huu yameripotiwa makosa 29,677.Pungufu ni makosa 5,153.

Akizungumzia uhalifu wa fedha yanayohusu makosa ya noti bandia , wizi katika benki, wizi kwenye mashirika ya umma na makosa ya kughushi mwaka 2016, makosa yalikuwa 1,861 ikilinganishwa na makosa 1,526 yaliyoripotiwa kwa kipindi kama hicho mwaka huu.

Kuhusu ajali za barabarani, Boaz amesema ajali zilizotokea zimesababisha vifo vya watu 3,108 na majeruhi 8,898 kwa mwaka 2016 wakati mwaka huu watu waliokufa ni 2,491 na majeruhi ni 5,696.

“Uchunguzi wetu umebaini ajali nyingi zinasababishwa na vyanzo vikuu vitatu ambavyo zikiwamo za kibinadamu, ubovu wa vyombo vya usafiri  na sababu za kimazingira.

“Sababu za kibinadamu ni pamoja na mwendo kasi,uzembe wa watembea kwa miguuu,”amesema.

Jeshi hilo limetoa rai kwa wananchi kuwa wepesi katika kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovote vya uhalifu katika maeneo yao ya makazi au maeneo ya biashara.

“Tunaomba wananchi kutumia namba za simu za bure 111,112 na 0787 668306 ambayo hutumika na Jeshi la Polisi katika kupokea taarifa za uhalifu na wahalifu,”amesema Boaz.

 Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ropert Boaz akizungumza kuhusu hali ya usalama nchini huku akieleza kuwa makosa ya ubakaji na unajisi yakizidi kuongezeka alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari leo katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini.

NEC YATOA UFAFANUZI KUHUSU MGOMBEA WA CHADEMA SINGIDA KASKAZINI

SHIRIKA LA POSTA NCHINI LAZINDUA NEMBO MPYA YA SHIRIKA HILO YENYE KAULI MBIU YA TWENZETU

0
0
 Naibu Waziri Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa  akizindua nembo mpya ya Shirika la Posta nchini ambayo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam katika Kuboresha huduma za shirika hilo kuwa la kisasa.
 Naibu Waziri Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa, akimpongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta nchini, Dr Haroun Kondo mara baada ya kuzindua nembo mpya ya shirika hilo jijini Dar es Salaam leo
 Naibu Waziri Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akishuka katika mabasi mapya ya Shirika la Posta nchini mara baada ya kuzindua huduma ya mabasi ya shirika hilo ambayo yatakuwa yanabeba abiria na vifurushi
 Naibu Waziri Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa, akizungumza mara baada ya kuzindua Nembo mpya ya  Shirika la Posta nchini
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta nchini, Dr Haroun Kondo  akizungumza kabla yakumkaribisha mgeni rasmi kuzindua nembo mpya ya shirika la Posta nchini.

UMUHIMU WA KUMLINDA MTOTO ENEO LAKO LA KAZI.

0
0
Mwanamke Mfanyabiashara ya Matunda akikatiza katika Barabara ya Garden  Avenue akiwa amembeba Mtoto bila ya kumfunika na kitu chochote wakati jua kali likiwaka, hali inayoweza kuhatarisha afya ya Mtoto huyo ambaye atapigwa na jua kwa muda mrefu.

AZAM KUMPELEKA MBARAKA YUSUPH AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU

0
0

MSHAMBULIAJI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Mbaraka Yusuph, anatarajia kuondoka nchini kesho Jumatano jioni kuelekea jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa uchunguzi wa goti lake la kushoto baada ya kuumiza ‘meniscus’ (washa).



Yusuph alipata majeraha hayo akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ wakati ikicheza na Libya kwenye mchezo wa michuano ya Kombe la Chalenji ulifanyika nchini Kenya Desemba 3 mwaka huu.


Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, alisema kuwa tayari uongozi wa timu hiyo wameridhia na atakwenda sambamba na Makamu Mwenyekiti, Abdulkarim Nurdin ‘Popat’, atakayekuwa akishughulikia taratibu zake zote za matibabu.
“Mbaraka atakwenda kufanyiwa kwanza uchunguzi zaidi baada ya kupata uchunguzi wake na kupata majibu kwamba ni kitu gani kinamsumbua zaidi wao ndio watajua kuwa Mbaraka anahitaji operesheni au atapewa tiba mbadala,” alisema.

Katika hatua nyingine, Jaffar alithibitisha kuwa tayari timu hiyo imepokea vibali vya kufanya kazi nchini kwa mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Bernard Arthur, ambaye sasa ni rasmi ataruhusiwa kucheza kwenye mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) dhidi ya Area C United ya Dodoma utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Jumamosi hii saa 1.00 usiku.


“Bernard Arthur yupo huru kucheza mashindano yote ambayo yanahusu Azam FC kwa maana kwamba taratibu za kupata vibali vyake vya kufanya kazi nchini zimekamilika, sisi Azam FC tunamatumaini kwamba kwa kushirikiana na wenzake atatoa mchango mkubwa na vilevile kuweza kuhakikisha kuwa safu yetu ya ushambuliaji itazidi kuchangamka zaidi,” alisema.


Arthur amesajiliwa akitokea Liberty Professional ya Ghana kwa mkataba wa miaka miwili, ambapo hadi sasa ameshafunga mabao matatu kwenye mechi za kirafiki alizocheza akifunga la kwanza dhidi ya Friends Rangers katika sare ya bao 1-1 kabla ya kutupia mawili, Azam FC ilivyoilaza Villa Squad mabao 7-1.


WANANCHI WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA HUDUMA KATIKA KITUO CHA USULUHISHI (CRC)

0
0

Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia ( CRC) kimejizatiti katika kusaidia kuleta uelewa kwa jamii kwa kwenda kutoa huduma kwenye maeneo mbalimali ikiwemo kuwa karibu zaidi na jamii.

Huduma hiyo iliyoanza kutolewa Desemba 11 na Kituo cha Usuluhishi –CRC, kilichopo chini ya Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) imelenga kusogeza karibu na wananchi huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo hususani kwa wanawake na watoto wadogo.
 Daktari Mateu Innocent akimhudumia moja ya wateja waliojitokeza kwa ajili ya kupata huduma kwenye kituo cha usuluhishi (CRC) ikiwa ni katika mikakati ya kupinga na kudhibiti ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto pamoja na kutoa huduma kwa elimu ya wananchi.
Huduma hizo za pamoja zilianzia katika Kata ya Saranga eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam na wananchi wengi waliweza kujitokeza ambapo awamu ya pili ilikuwa ni Kata ya Kawe.

Huduma zilizotolewa ni pamoja na msaada wa kisheria kwa waathirika wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia, Ushauri nasihi na kuwepo kwa Dawati la Jinsia linalohudumiwa na Jeshi la Polisi, ustawi wa jamii  sambamba na huduma za kisheria kutoka kwa wanasheria.

Baadhi ya wananchi waliopatiwa huduma kituoni hapo walisema wanafurahishwa na huduma hizo muhimu kutolewa eneo moja jambo ambalo linawapunguzia mzigo na urasimu wanapoziitaji pia wameweza kupatiwa huduma kwa wakati na ikiwemo mashauri mengine kusikilizwa hapo hapo na kupatiwa ufumbuzi huku mengine yakienda mbele zaidi kisheria.

Daktari Matau Innocent amesema kuwa kituo cha usuluhishi kimeweza kuwasaidia wananchi wanaokutana nao kupata huduma kwa urahisi zaidi na pia inafanya wigo wa  huduma kuwa mkubwa sana. Matau amesema kuwa huduma wanazozitoa ni pamoja na upimaji wa maambukizi ya VVU, ushauri nasaha ukiachana na masuala ya ukatili wa kijensia hususani kwa wanawake na watoto.

Huduma za usuluhishi kutoka katika kituo cha CRC zimeweza kuleta hamasa kubwa kwa wananchi kutoka maeneo mbalimbali  wanaishi ndani ya vitendo vya unjanyasaji lakini wanashindwa kujitokeza kutokana na umbali na urasimu uliopo katika kupata huduma hizo, hivyo kuwa na huduma hizo karibu zinaweza kusaidia katika kutoa elimu na kupunguza ukatili wa kijinsia na masuala ya kijamii kwa ujumla.

Hivi karibuni Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi –CRC, Bi. Gladness Munuo kilichopo chini ya TAMWA, aliishauri Serikali kuongeza idadi ya vituo vinavyotoa huduma ya pamoja kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ ili kuwasaidia waathirika wa matukio hayo.
 Christina Onyango kutoka dawati la kijinsia kituo cha Polisi Stakishari (kulia) akimsikiliza mteja aliyekwenda kupata huduma kwenye kituo cha usuluhishi (CRC) ikiwa ni katika mikakati ya kupinga na kudhibiti ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto pamoja na kutoa huduma ya elimu kwa wananchi.
 Wananchi wakisubiri huduma kutoka kituo  cha usuluhishi (CRC).

MPOTO AWASIHI WATANZANIA WAENDELEE KUTUMA BARUA KUPITIA SHIRIKA LA POSTA KUJENGA UZALENDO

0
0
 Msanii wa Muziki wa kughani kutoka Mjomba Band Mrisho Mpoto akiimba wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya Shirika la Posta Tanzania, Mbali na kuimba mpoto alitumia muda huo kuwaeleza Watanzania juu ya kuwa wazalendo kwa kutumia Barua kama chombo pekee ya kuonesha thamani kwa mtu unayempenda na kumjali, Mpoto amesema kuwa hapo zamani wahenga walitumia Barua kama chombo pekee cha kuonesha namna gani mtu anamjali mwenzie hasa nayakati zile wakiwa wanasoma shule za bweni .
 Wasanii wa kundi la Mjomba Band wakitumbuiza wakati wa bendi hiyo ilipokuwa inaimba wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya Shirika la Posta nchini.
 Mpiga Drums Maharufu nchini James Kibosho akikaanga chipsi pamoja na Mjomba Band jijini Dar es Salaam leo
 Wanamuziki wakicharaza magitaa wakati wa Bendi ya Mrisho Mpoto ilipokuwa inatumbuiza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya shirika la Posta nchini.

MATUKIO YA ZIARA YA WAZIRI WA MAMBO YA NE NCHINI CHINA

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiongea jambo wakati alipokuwa katika mazungumzo rasmi na Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian Keming jijini Beijing. 
Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian Keming akisisitiza jambo alipokuwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt.Augustine Mahiga leo jijini Beijing. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa na ujumbe wake aliongozana nao katika ziara ya kikazi nchini China. Kutoka kushoto ni Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China, Kanali Remigius Ng'umbi anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Thomas Kashililah na Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki. 
Wajumbe wa pande mbili za China na Tanzania wakiwa katika mazungumzo. 
Wajumbe wengine wa Tanzania wakifuatilia mazungumzo. Kutoka kulia ni Kamishna Msaidizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Malmeltha Mutagwaba, Naibu Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango kutoka Serikali ya Zanzibar, Bw. Khamis Omar 
Balozi Mahiga akitoa zawadi ya picha kwa Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian Keming. Mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mipango ya China 

TUME YA ARDHI KUANZISHA KANZIDATA YA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI

0
0
Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) ipo mbioni kuanzisha Kanzidata (Database) ya mipango ya matumizi ya ardhi iliyofanyika nchini na wadau mbalimbali wa sekta ya ardhi.

Kwa kushirikiana na wadau wa upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi wa taasisi za serikali pamoja na asasi za kiraia, Kanzidata hiyo itabeba taarifa zitakazoonyesha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali kama vile kilimo, malisho, huduma za jamiii, n.k itarahisisha utendaji kazi kwa Tume, mamlaka zingine za upangaji, wadau pamoja na wananchi kwa ujumla ambao watatumia teknolojia kujua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali nchi nzima
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya mipango ya matumizi ya Ardhi(NLUPC) Dkt. Stephen Nindi akifungua mkutano wa kikosi kazi kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzidata ya mipango ya matumizi ya ardhi,Mjini Morogoro
Mwenyekiti wa Kikao Bw. Jamboi Baramayegu kutoka ujamaa Community akielezea utaratibu wa namna kazi itakavyofanyika
Afisa Tehama kutoka wakala wa Serikali Mtandao Bw. Thomas Malinga akitoa maelezo ya malengo ya wao kushiriki katika mchakato wa uanzishwaji wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango na matumizi ya ardhi.
Wadau wakiendelea na mkutano huo.Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa Tanzania .


Viewing all 109604 articles
Browse latest View live




Latest Images