Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live

TIMU YA TAIFA YA BEACH SOCCER YAZIDI KUJIFUA KUJIANDAA NA MICHUANO YA COPA DAR ES SALAAM

0
0
Kocha wa timu ya Taifa ya soka la ufukweni, John Mwansasu ameita kikosi cha  wachezaji 16 walioingia  kambini mwishoni mwa wiki iliyopita kujiandaa na michuano ya Copa Dar es Salaam itakayofanyika kwa siku mbili kwenye fukwe ya Coco.

Kikosi hicho cha wachezaji 16 kimeingia  kambini kwa muda wa wiki moja ikiwa ni kujiandaa na mashindano hayo ya kimataifa yatakayojumuisha timu nne ambazo ni Malawi, Uganda, Zanzibar na wenyeji Tanzania Bara.

Wachezaji walioitwa ni pamoja na Rajabu Ghana (Huru), Khalifa Mgaya (Chuo cha CBE), Juma Kaseja (Kagera Sugar), Juma Sultan (Chuo Kikuu Ardhi), Ally Rabby (Huru), Mwalimu Akida (Huru), Samwel Salonge (Huru), Athuman Idd 'Chuji' (Coastal Union) na Kenan Mwandisi (Huru).
Wengine ni John Pauseke (Huru), Joseph Jafet (Huru), Jaruph Rajab Juma (Chuo cha DIT), Mbwana Mshindo (Chuo cha DSJ), Rolland Msonjo (Singida United), Jerry Francis Robert (Huru) na Haruna Moshi (Friends Rangers)
Benchi la ufundi linaongozwa na Mwansasu mwenyewe akisaidiwa na kocha wa makipa Peter Manyika, Meneja Deo Lucas na daktari wa timu Richard Yomba.

Kocha John Mwansasu amesema mashindano hayo ya Copa Dar es Salaam yatakayofanyika Desemba 25 na 26, 2017 yatasaidia kuwaongezea uzoefu zaidi katika mchezo huo wa soka la ufukweni.
  Timu ya Taifa ya Beach Soccer ikiendelea na mazoezi kwenye Ufukwe wa Coco kujiandaa na mashindano ya kimataifa ya Copa Dar Es Salaam yatakayofanyika Desemba 25-26 mwaka huu kwenye Ufukwe wa Coco.

SUMATRACC :HAKUNA NAULI KUPANDISHWA KWA BASI YAENDAYO MIKOANI KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Baraza la Ushauri la walaji la Mamlaka ya Usafiri wa nchi kavu na Majini (SUMATRA –CC) imesema kuwa hakuna kupandisha nauli na watakaopandisha nauli watakuwa wamekiuka masharti ya leseni ya usafirishaji abiria.

Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa SUMATRA-CC , Dk. Oscar Kikoyo amesema kuwa kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka kuna baadhi wamekuwa wanakiuka leseni zao.

Amesema kuwa wananchi wanaosafiri wanatakiwa kutoa taarifa kwa baadhi ya basi ambazo zinapandisha nauli ili hatua zichukuliwe katika kukomesha suala hilo.

Dk. Kikoyo amesema kuwa na wale ambao wanachukua tiketi za basi na baadaye kuuza kwa abiria kwa bei ya juu, abiria wanatakiwa kutoa taarifa kwa vyombo husika ili kuchukuliwa hatua kwa mmiliki wa basi.

Aidha  amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano pale wanapoona watu wanauliza ndani ya basi juu masuala mbalimbali ili kubaini vitu ambavyo vimekwenda nje ya utaratibu.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la walaji la Mamlaka ya Usafiri wa nchi kavu na Majini (SUMATRA –CC) , Dk. Oscar Kikoyo akizungumza na waandishi habari kuhusu masuala mbalimbali ya usafirishaji wa abiria kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka leo jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MWAKYEMBE AIPONGEZA TIMU YA ZANZIBAR HEROES

BARAZA LA WATOTO TAIFA LATOA ELIMU YA MATUMAINI KWA WATOTO WA MITAANI

0
0
Na Anthony Ishengoma
Wajumbe  wa Balaza  la Watoto  la Taifa leo wameungana na watoto wanaotunzwa katika kituo cha kulelea watoto wa mitaani Amani kilichopo katika Manispaa ya Singida ili kuwafariji na kuwapatia elimu juu ya umuhimu wa kuishi katika familia kama ilivyo kwa watoto wengine wanaoishi na wazazi  wao.

Watoto  hao wanalelewa katika kituo hicho baada yakuwa wamejiingiza mjini na kuanza maisha kabla ya wakati jambo  ambalo uwalazimisha kuishi katika mazingira hatarishi ikiwemo  wizi na kuvutishwa bangi na madawa ya kulevya.

Mkuu wa kituo cha kulelea watoto hao katika kituo cha Amani Street Children centre Bi. Getruda Kifumu ametaja chanzo cha kuongezeka kwa watoto wa mitaani kuwa ni umasikini wa kipato katika familia, ugonvi katika ndoa, kuachana kwa familia ikiwemo imani potofu ya kuwa mjini kuna nafuu  ya maisha.

Aidha Bi. Getruda amesema kituo chake kina zaidi ya watoto 50 ambao tayari wamerudishwa kwa familia baada ya kuwa wamezungumza na familia lakini pia na watoto wenyewe japokuwa baadhi ya watoto utoroka.
Mkurugenzi  wa Idara ya Watoto Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Bi. Margaret Mussai  akikabidhi zawadi ya Vyandarua kwa Mratibu wa   kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Amani Street Children Centre kilichopo katika Manispaa ya Singida. 

 Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa, Joel Festo akikabidhi zawadi ya Vyandarua kwa Mratibu wa   kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Amani Street Children Centre kilichopo katika Manispaa ya Singida.
 Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Watoto Taifa wakishiriki kufanya usafi katika  kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Amani Street Children Centre kilichopo katika Manispaa ya Singida.
 Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Watoto Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa  kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Amani Street Children Centre kilichopo katika Manispaa ya Singida.

RAIS MAGUFUL ATOA MILIONI 210 KWA AJILI YA UJENZI WA MRADI WA UMEME SONGEA HADI MAKAMBAKO.

0
0
Serikali Kupitia Wizara Ya Nishati Imetoa Kiasi Cha Shilingi  Milioni 210 Kwa Ajili Ya Mradi Wa Umeme Kupitia Makambako Hadi Mkoani Ruvuma ambao utakuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi zaidi ya 22,000 sawa na vijiji 120 kwa mikoa yote miwili RUVUMA na NJOMBE.

MKURUGENZI MTENDAJI WA TASAF AWATAKA WATUMISHI WA TAASISI HIYO KUZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI WA UMM KWA VITENDO.

0
0
Estom Sanga- TASAF

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF- bwana Ladislaus Mwamanga amefungua kikao kazi cha Watumishi wa taasisi hiyo jijini Dar es salaam na kuwaagiza wazingatie misingi ya Utumishi wa Umma ili kufanikisha jukumu la kuwahudumia wananchi na hivyo kusaidia jitihada za serikali za kupambana na umaskini kwa vitendo.

Bwana Mwamanga amesema Watumishi wa taasisi hiyo wanalo jukumu kubwa mbele yao katika kutekeleza mkakati wa kuwaondolea wananchi kero ya umaskini kazi ambayo amesema mafanikio yake yatapimwa kulingana na mabadiliko ya maisha ya wananchi wanaohudumiwa na Mfuko huo kupitia Mpango wake wa Kunusuru Kaya Masikini-PSSN.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amewakumbusha wajibu wa watumishi wa taasisi hiyo kuzingatia maadili bora ya utumishi wa umma na kutumia waledi walionao katika kutoa huduma bora kwa walengwa na wananchi wanaotegemea huduma zake kote nchini.

Akizungumzia mafanikio ya PSSN, Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema tangu kuanza kwa Mpango huo, Walengwa wake wameonyesha nia ya dhati ya kuondokana na umaskini kwa kuanzisha miradi midogo midogo huku wengine waboresha makazi yao na kuzingatia masharti ya Mpango katika sekta za elimu, afya na lishe.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga (aliyeshika kipaza sauti) akifungua kikao kazi cha watumishi wa taasisi hiyo(hawapo pichani ) kinachofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyi mjini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa fedha Bi. Chiku Thabiti, na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Miradi bw. Amadeus Kamagenge. 

Watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF wakisimama kwa dakika moja kuwakumbuka baadhi ya watumishi waliopoteza maisha au kupoteza ndugu na jamii zao katika kipindi cha mwaka huu kabla ya ufunguzi rasmi wa kikao kazi chao kinachofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo jijini Dar es salaam.


Baadhi ya Watumishi wa TASAF wakiwa katika kikao kazi chao cha kufunga Mwaka katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo,bwana Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani) alipofungua kikao hicho.
Watumishi wa TASAF wakifuatialia kwa makini hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi chao kilichoanza leo ,kilichofunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wake Bwana Ladislau Mwamanga (hayupo pichani.

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) YATOA ORODHA YA UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI

0
0
Na Mwandishi Wetu

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa orodha ya wanachama 15 wa vyama vya siasa walioteuliwa kugombea ubunge katika majimbo ya Singida Kaskazini na Longido.

Tume pia imetoa orodha ya majina ya wanachama wengine 15 wa vyama mbalimbali ambao wamejitokeza kugombea udiwani katika uchaguzi mdogo unaofanyika kwenye kata sita.

Walioteuliwa kugombea ubunge katika jimbo la Longido ni Kisiongo Mayasek Olokuya (CUF), Francis Ringo (CCK), Dk Steven KIruswa (CCM), Mgina Mustafa (AFP), Godwin Sarakikya (ADA TADEA), Feruziy Furuziyson (NRA), Ngilisho Paul (Demokrasia Makini), Simon Bayo (SAU) na Robert Lukumy (TLP). 

Waliojitokeza kugombea ubunge katika jimbo la Singida Kaskazini ni Omari Sombi (AFP), Dalphina Mlelwa (CUF), Monko Joseph (CCM), David Djumbe (Chadema), Aloyce Nduguta (ADA TADEA) na Mchungaji Yohana Labisu (CCK)

Katika uteuzi huo pia kuna walioteuliwa kugombea udiwani katika kata ya Kimandolu ambako kuna wanachama wa vyama vitano vya Gaudence Lyimo (CCM), |Rashid Nyawaya (CUF), Hamis Mgoya ( NRA), RAmadhani Mcharo (Demokrasia Makini), na  Shafii Kiktunda (SAU).

Katika kata ya KIhesa halmashauri ya Iringa Mjini ameteuliwa Sawani Juli (CCM), Kata ya Keza wilayani  Ngara walioteuliwa ni Eradiu8s Bitemele (NCCR Mageuzi), Bakundukize Gwaibondo (CCM), Philipo Bazubwenge (CUF). Kata ya Kurui wilayani Kisarawe wagombea ni Kunikuni Salumu (CCM) na Kikumbi Mwalimu (CUF),

Kata ya Bukumbi wilaya ya Uyui wagombea ni Kasoga Sizya (CCM), Edward Msigala wa (CUF) wakati kata ya Kwagunda wilaya ya Korogwe walioteuliwa ni Said Shenkawa (CCM) na Yusuf Senkawa wa CUF.

WAZIRI KIGWANGALLA ATENGUA UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA NGORONGORO


MKURUGENZI MTENDAJI WA DCB AAGA RASMI, AMTAMBULISHA MKURUENZI ANAYECHUKUA NAFASI YAKE

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MKURUNGEZI Mtendaji wa Benki ya DCB Edmund Mkwawa ameaga rasmi wanahabari pamoja na wateja wa benki hiyo baada ya kuwa kwenye kiti hicho kwa miaka 16 sambamba na kumuachia kijiti mkurungenzi mpya anayekuja kuchukua nafasi yake.

Mkwawa amemkaribisha rasmi Mkurugenzi Mtendaji anayetarajia kukalia kiti chake Godfrey Ndalahwa wakati wa mkutano wake na wanahabari leo Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza baada ya utambulisho, Mkwawa amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 16 benki  ya DCB iliweza kufanya vizuri na katika kipind cha miaka mitatu mfululizo wameweza kuanzia 2012 hadi 2014 wameshika nafasi ya tatu miongoni mwa benki zote kiujumla kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za mahesabu ya kibenki.

Mbali na tuzo hiyo, pia wameweza kushinda na kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za mahesabu ya benki kwa mwaka 2016 kwa sekta za benki ndogo na za kati kwa ubora ikiwa ni kwa mwaka wa pili mfululizo kuanzia 2015 ambapo tuzo hizo huandaliwa na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu NBAA.

Godfrey Ndalahwa nayetarajia kuchukua nafasi Mkurugenzi Mtendaji, amesema kuwa Benki imejipanga kuendeleza malengo yake na kuhakikisha inakuwa chaguo la kwanza la wateja katika utoaji huduma za kifedha. Katika kutimiza malengo haya, benki itatumia teknolojia ya kisasa katika utoaji wa huduma zake kupitia huduma ya DCB Pesa (kupitia simu ya mkononi) na DCB Jirani (Huduma kupitia wakala) kwa lengo la kuwafikia wateja wengi walengwa ambao ni wajasiriamali wadogo na wa kati waliosambaa kote nchini hadi vijijini.


Mojawapo ya malengo ya benki kwa mwaka unaokuja wa 2018 ni kuhakikisha inaongeza wigo na viwango vya utoaji huduma na kuwafikia wateja wengi zaidi wanaohitaji huduma za kibenki ikiwemo wamiliki wa Vikoba na Wafanyabiashara wa kati ambao wamehitimu hatua za mikopo ya awali katika benki hii. Hii ni kuhakikisha benki inakua pamoja na wateja wake na haitowaacha kuwahudumia katika mahitaji yao hata wakiongeza wigo wa biashara zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Edmund Mkwawa akizungumza na waandishi wa habari na kuwaaga rasmi kna nafasi yake kuchukuliwa na Godfrey Ndalahwa leo Jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MAKAMBA AZINDUA KAMATI YA KITAIFA YA USHAURI WA MAZINGIRA(NEAC) MKOANI DODOMA

DOKTA MPANGO AALIKA WAWEKEZAJI KUTOKA NORWAY

0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway hapa nchini Bi. Hanne-Marie Kaarstad na kutoa wito kwa wawekezaji kutoka Norway kuja kuwekeza Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwemo Nishati, misitu, kilimo, gesi na mafuta.

Dkt. Mpango amemweleza Balozi huyo kwamba Tanzania iko katika hatua mbalimbali za kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda na kwamba wawekezaji kutoka Norway watakuwa na mchango mkubwa wa kuiwezesha Tanzania kufikia lengo hilo.

Aliyataja maeneo ya kuongeza thamani ya mazao ya misitu, mifugo, uvuvi, nishati, kilimo na mengine mengi kwamba yataongeza tija katika sekta hiyo na kwamba malighafi za kilimo zitatochea uzalishaji katika viwanda na kuinua kipato cha wananchi.

“Tumeamua kujenga Reli ya Kati kwa viwango vya kimataifa-SGR ambayo inahitaji umeme wa kutosha kwa hiyo bado tunahitaji mchango wa wadau mbalimbali ikiwemo Norway ili kuhakikisha kuwa tunakuwa na nishati ya umeme ya kutosha na ya uhakika ili kufanikisha mradi huo mkubwa” aliongeza Dkt. Mpango

Kuhusu Sekta Binafsi, Dkt. Mpango amesema kuwa Serikali imeendelea na majadiliano na Sekta hiyo ili kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili ikiwemo masuala ya kodi pamoja na kujenga kuaminiana kati ya pande hizo mbili.Amefafanua kuwa Sekta Binafsi ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa Taifa na kwamba vikao hivyo vya mara kwa mara vimeanza kuzaa matunda.






Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akizungumza jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad, (hayupo pichani) mjini Dodoma.
Katibu wa Waziri wa Fedha na Mipango Bw. Edwin Makamba (kushoto) na Mchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango-Idara ya Fedha za Nje Bw. Anayeshughulikia dawati la Norway Bw. Warioba Nyakua, wakifuatilia majadiliano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na mgeni wake, Balozi wa Norway hapa nchini Bi. Hanne-Marie Kaarstad, mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akiteta jambo na Kamishna wa Bajeti wa Wizara hiyo Bi. Mary Maganga (kushoto) na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. John Rubuga, wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad, (hayupo pichani) mjini Dodoma.
Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad, (kulia) akizungumza jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati) mjini Dodoma. Kushoto ni Kamishna wa Fedha za Nje-Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga.

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AKUTANA NA UONGOZI WA TAASISI YA MWALIMU NYERERE DODOMA

0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akizungumza jambo kwa viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere walipomtembelea ofisini kwake Desemba 19, 2017 Dodoma.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akizungumza jambo kwa viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere walipomtembelea ofisini kwake Desemba 19, 2017 Dodoma.


Katibu Muyeka Msitaafu wa Hayati Mwalimu J. Kambarage Nyerere akieleza jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora walipomtembelea Ofisi kwake Dodoma.
Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akizungumza jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora walipomtembelea ofisini kwake Dodoma na kufanya mazungumzo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere walipomtembelea Dodoma Leo.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Joseph Butiku na kushoto ni Bw.Samwel Hussein Kasori.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA

JKT RUVU KUTUMIA MCHEZO WA FA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA WANAJESHI 14

0
0

Kikosi cha timu ya JKT Ruvu kesho kinatarajia  kushuka dimbani kumenyana na timu ya Mvuvumwa FC katika mchezo wa kombe la FA unaotarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Azam Complex kuanzia saa moja usiku.

JKT Ruvu inayoshiriki ligi daraja la kwanza wanakutana na Mvuvumwa kwa ajili ya kusaka nafasi ya kuingia nafasi inayofuata ya michuano ya Azam Sports HD inayojulikana kama FA huku wakiratajia kutumia mchezo huo kwa ajili ya kuwakumbuka na kutoa heshima ya mwisho kwa askari wa JWTZ waliofariki wakiwa kwenye majukumu ya kikazi nchini Demokrasia ya Congo.


Afisa Habari wa timu ya JKT Ruvu,Costantine Masanja alisema kwamba kikosi cha timu hiyo ambacho kinaongozwa na kocha Bakari Shime kipo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao anaamini utakuwa na ushindani wa hali juu.


Alisema kwamba timu ya JKT Ruvu katika mchezo huo itafunga vitambaa vyeusi na kusimama kwa dakika moja kabla ya mchezo ikiwa ni kumbukumbu na heshima kwa askari wa JWTZ 14 waliokufa nchini Congo katika jukumu la ulinzi wa Amani chini ya umoja wa mataifa.

JKT Ruvu iliyochini ya Jeshi la Wananchi imejipanga kuhakikisha inarejea ligi kuu msimu ujao wakiwa wamejizatiti ambapo mpaka sasa wameshajinyakulia alama 25 wakiongoza kundi A wakifuatiwa na African Lyon wenye alama 17 na mpinzani wake katika mchezo wa FA Mvuvumwa akiwa anashikilia mkian kwa alama 4.

Balozi, Dkt. Ramadhani Dau Awasilisha Hati Za Utambulisho kwa Mtukufu Mfalme Wa Cambodia

0
0
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia anayewakilisha pia nchini Cambodia, Mhe. Dkt. Ramadhani Kitwana Dau (kushoto) akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mfalme wa Cambodia, Mtukufu Preah Bat Samdech Preah Boromneath NORDOM SIHAMON. Makabidhiano hayo yalifanyika tarehe 28 Novemba 2017 Jijini Phnom Pen, Cambodia. 
Mhe. Balozi Dkt. Dau (wa pili kushoto) akiwa katika mazungumzo na Mtukufu Mfalme mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. Wanaoshuhudia kulia ni maafisa wa Serikali ya Cambodia na kushoto ni Afisa wa Ubalozi wa Tanzania.

Mazungumzo yao yalijikita katika kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo ambao ulianzishwa rasmi mwaka 1995. Pia kuimarisha ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji. Vilevile Mtukufu Mfalme aliahidi kumpa ushirikiano Mhe. Balozi Dkt. Dau katika utekelezaji wa majukumu yake. 
Mhe. Balozi Dkt. Dau akimtambulisha Afisa wa Ubalozi wa Tanzania, Bw. Khatib Makenga aliyeambatana naye katika hafla ya makabidhiano ya Hati za Utambulisho 
Mhe. Balozi Dkt. Dau akipokelewa mara baada ya kuwasili jijini Phnom Penh, Cambodia. 

MATUKIO YA USALAMA BARABARANI MKOA WA PWANI

0
0
Dereva na abiria wakiwa hawajavaa kofia ngumu (helment) na kuhatarisha maisha yao.
Matukio ya usalama barabarani bado ni changamoto kwa watumiaji wa vyombo vya moto kwa kushidnwa kufuata sheria zinavyotaka.

Kampuni 3 Kuuza Tanzanite katika Mnada Wa Mirerani

0
0
Na Zuena Msuya, Manyara.

Kampuni tatu za uchimbaji madini ya Tanzanite zimejitokeza kuuza madini hayo katika mnada wa tatu wa madini ya Tanzanite unaofanyika katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Mshindi wa mnada huo atatangazwa Desemba 21 katika eneo la Naisinyai lililoko kwenye mji mdogo wa Mirerani.Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka amezitaja kampuni hizo kuwa ni Tanzaniteone yenye ubia na Shirika la Madini Tanzania( STAMICO), Tanzanite Afrika na Classic Gems.

Akizungumzia mnada huo, Kamishna Mchwampaka alisema kuwa utaratibu wa kufanya Mnada wa Tanzanite ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo nje nchi na pia kuwasaidia wachimbaji na wafanyabiashara wazalendo kuuza madini yao kwa bei ya ushindani inayoendana na soko la dunia.

Mchwampaka alifafanua kuwa, mnunuzi atakayefanikiwa kununua madini katika mnada huo ni yule tu atakayetoa bei ya juu ambayo imefikia au kuvuka bei inayotokana na Wathamini wa Serikali (Reserve Price).
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila( katikati) akielezwa jambo na Vikosi vya ulinzi na usalama, katika eneo linalotumika kufanyia mnada wa Madini ya Tanzanite katika eneo la Naisinyai lililoko kwenye mji mdogo wa Mirerani.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila( katikati) akiangalia mapambo na vitu mbalimbali vinavyotengezwa na Kituo cha Uongezaji thamani Madini ya vito na Miamba( TGC),kilichopo mkoani Arusha, wakati Mnada wa Madini ya Tanzanite unaofanyika katika Mji mdogo wa Mirerani mkoani Manyara.
Wanunuzi kutoka mataifa mbalimbali wakifanya uthamini wa Madini ya Tanzanite kabla ya mnada kufanyika katika eneo la Naisinyai lililoko kwenye mji mdogo wa Mirerani.
Vifaa maalum( drum) vilivyohifadhia madini ya Tanzanite.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

SHUWASA,POLISI WATEKETEZA VIFAA VINAVYOTUMIKA KUHARIBU VYANZO VYA MAJI BWAWA LA NING'WA SHINYANGA

0
0
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA) kwa kushirikiana na jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga wameendesha zoezi la kuteketeza vifaa vinavyotumika kuharibu vyanzo vya maji katika bwawa la Ning’wa.

Miongoni mwa vifaa vilivyoteketezwa kwa moto ni nyavu za kuvulia samaki,mitumbwi na vibanda vinavyotumiwa na wavuvi kujihifadhi karibu na bwawa hilo.Zoezi hilo limefanyika leo Jumanne Desemba 19,2017 katika bwawa hilo lenye mita za ujazo milioni 10.9 linalopatikana katika kata za Old Shinyanga,Chibe na Pandagichiza zilizopo katika wilaya ya Shinyanga. 

Akizungumza wakati wa zoezi hilo,Mkurugenzi wa SHUWASA,Injinia Sylivester Mahole alisema lengo la oparesheni hiyo aliyodai ni endelevu, ni kuhifadhi vyanzo vya maji kwani bwawa hilo ni moja vya vyanzo muhimu vya maji vya mamlaka hiyo ukiachilia mbali Ziwa Victoria. 

“Tumeteketeza kwa moto vifaa vilivyokuwa vinatumika kwa shughuli za uvuvi katika bwawa hili ikiwemo mitumbwi,nyavu na vibanda vilivyokuwa vinatumiwa na wavuvi,tunataka waache mara moja kufanya uvuvi hapa kwani wanaharibu vyanzo vya maji”,alieleza Injinia Mahole. 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA),Injinia Sylivester Mahole akielezea lengo la kuendesha oparesheni ya kuteketeza kwa moto vifaa vinavyotumiwa na wananchi kuharibu vyanzo vya maji katika bwawa la Ning'wa.Kulia ni mwandishi wa habari wa Radio Faraja na DW,Veronica Natalis - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA),Injinia Sylivester Mahole akionesha mifugo katika bwawa la Ning'wa 
Askari polisi akishirikiana na mwananchi kuondoa mtego wa samaki katika bwawa la Ning'wa  
Askari polisi akimwaga mafuta kwa ajili ya kuchoma moto nyavu zinazotumika kuvua samaki katika bwawa la Ning'wa 
Moto ukiteketeza nyavu .

AIRTEL YAENDELEA KUTAMBA NA SMATIKA, YATOSHA INTANETI MPYA..

DIWANI WA CHADEMA SIHA AJIUNGA NA CCM

0
0


Diwani wa Chadema wa Kata Donyomurwak, Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro, Ndg. Lwite Ndossi almaarufu “Nsonuu”, leo tarehe 19 Disemba 2017 amejivua uanachama wa Chadema, na amejiuzuru Udiwani wa Kata hiyo na ametangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Ndugu Ndossi ameeleza sababu za kujiunga kwake na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa ni kujiunga na watu wanaofanya siasa za kufanya kazi za maendeleo na si kulumbana na maneno matupu.


Imetolewa na,


IDARA YA ITIKADI NA UENEZI


CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

BARAZA LA WATOTO TAIFA LA CHAGUA WAWILI KUIWAKILISHA TANZANIA MKUTANO WA KIMATAIFA WA KUZUIA UKATILI FEBRUALI MWAKANI NCHINI SWEDEN

0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto wa Wilaya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam Yusra Mohamed pamoja na Katibu wa Baraza la Watoto Mkoa wa Arusha Raphael Denis wamechaguliwa na wajumbe wa Baraza la Watoto Taifa kuiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa kimataifa wa kuzuia ukatili dhidi ya watoto utakaofanyika Nchini Swedeni Februari 2018.

Watotao hao wamechaguliwa baada ya kupita katika Mchujo mkali uliowakutanisha wagombea kutoka Mikoa ya Bara na Visiwani na wataiwakilisha Tanzania katika Mkutano huo ambao Tanzania ni moja ya Nchi chache Barani Afrika kupewa kipaumbele cha ushiriki kufuatia hatua kubwa iliyofikia katika juhudi zake za kupambana na ukatili dhidi ya watoto.

Kwasasa Tanzania inatekeleza mkakati wake wa miaka mitano wa kutokomeza kabisa ukatili dhidi ya wanawaka na watoto unaotekelezwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na wadau mbalimbali wa wanaopambanakuhakikisha Tanzania inakomesha kabisa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto wa Wilaya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam Yusra Mohamed kulia pamoja na Katibu wa Baraza la Watoto Mkoa wa Arusha Raphael Denis kushoto mara baada ya kuchaguliwa na wajumbe wa Baraza la Watoto Taifa kuiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa kimataifa wa kuzuia ukatili dhidi ya watoto utakaofanyika Nchini Swedeni Februari 2018.
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live




Latest Images