Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

MAMA FISSOO ASISITIZA MAADILI KWA WASANII WA FILAMU AKIZINDUA FILAMU YA FROM NIGERIA

$
0
0
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akiwa katika pozi na Msanii aliyeigiza kama mhusika mkuu katika Filamu ya From Nigeria Stick Motela alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu hiyo mapema wikiendi hii.Filamu hiyo imeandalliwa na Kampuni ya Jumo Entertainment.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akielezea jambo alipokuwa alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Filamu ya From Nigeria iliyoandalliwa na Kampuni ya Jumo Entertainment mapema wikiendi hii. Katikati ni Msanii aliyeigiza kama mhusika mkuu katika filamu hiyo Stick Motela.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akisalimiana na Mkuu wa Promosheni na Matangazo wa Kampuni ya Duma Promosheni Daud Maichel (Duma) alipokutana naye katika uzinduzi wa Filamu ya From Nigeria mapema wikiendi hii. Kampuni ya Duma Promosheni ndiyo iliyoratibu shughuli nzima ya uzinduzi wa filamu hiyo.Picha na Frank Shija – MAELZO

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII , JAPHET HASUNGA ATEMBELEA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO NA KUZUNGUMZA NA WATUMISHI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( kulia) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Audax Mabula (kushoto) wakimsiliza kwa makini Mhifadhi Mila Mwandamizi, Wilbard Hema (mbele) wakati akiwapa maelezo kabla ya kutembelea baadhi ya nyumba za makabila 33 zilizopo kwenye Kijiji cha Makumbusho ambapo Naibu Waziri Hasunga alipofanya ziara mwishoni mwa wiki. Nyuma ya Naibu Waziri ni Kaimu Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho, Agnes Robert.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akinywa maji ya dafu mara baada ya kutembelea kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara mwishoni mwa wiki kujionea shughuli zinazofanywa kijijini hapo pamoja na kuzungumza na Watumishi. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Audax Mabula pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho, Agness Robert (wa tatu kushoto).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kulia) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Audax na Mabula ( wa tatu kulia) wakinywa maji ya dafu mara baada ya kutembelea kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara mwishoni mwa wiki kujionea shughuli zinazofanywa kijijini hapo pamoja na kuzungumza na Watumishi. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho, Agness Robert, Wengine ni watumishi wa Makumbusho ya Taifa makao Makuu jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kulia) akipewa maji ya dafu na mmoja wa Watumishi wa Kijiji cha Makumbusho mara baada ya kutembelea hapo wakati alipofanya ziara mwishoni mwa wiki kujionea shughuli zinazofanywa k pamoja na kuzungumza na Watumishi. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho, Agness Robert (wa pili kulia)
Baadhi ya Wasanii wakitumbuiza ikiwa ni ishara ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga alipotembelea Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara mwishoni mwa wiki kujionea shughuli zinazofanywa kijijini hapo pamoja na kuzungumza na Watumishi.
Picha na Lusungu Helela-MNRT

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI ATEMBELEA MKOA WA ARUSHA

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na uvuvi Mhe.Abdalla Hamisi Ulega amefanya ziara mkoani Arusha katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa lengo la kuhamasisha upigaji chapa mifugo.
Akizungumza na baadhi ya wafugaji katika halmashauri ya Ngorongoro Ulega amempongeza mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo, kwa utendaji mzuri wa kazi hususani katika kuhamasisha upigaji chapa mifugo mkoani humo.

Aidha Mhe Ulega amezitaja baadhi ya halmashauri zilizofanya vizuri katika zoezi la upigaji chapa kuwa ni pamoja na Chemba, Kondoa, Maswa, Mafinga na Misungwi.

Ambapo mhe. Ulega amewahimiza wafugaji kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upigaji chapa mifungo linaloendelea nchi nzima.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akishiriki zoezi la upigaji chapa mifugo katika hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizindua zoezi la upigaji chapa mifugo katika hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (wa kwanza kulia)akizungumza na wananchi wanaoishi katika hifadhi ya Ngorongoro baada ya kushuhudia zoezi la upigaji chapa mifugo mkoa wa Arusha. Katikati ni Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kushoto, Naibu Muhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt. Maurus Msuha.
Naibu Muhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,Dkt Maurus Msuha akishiriki zoezi la upigaji chapa mifungo mkoani Arusha.



KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Naibu Waziri Mgalu Awataka Wakandarasi Tanga kutoa Maelezo Ya kutokuanza Miradi

$
0
0
Na Greyson Mwase, Tanga

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amezitaka kampuni za Derm Electric, Njarita, Agwilla na Radi Services kutoa maelezo kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ya kutokuendelea na kazi katika maeneo yao ya miradi wakati walikwishalipwa malipo ya awali na Serikali.

Mgalu alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki tarehe 16 Desemba, 2017 alipofanya kikao na watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)- Ofisi ya Tanga baada ya kubaini wakandarasi hao hawapo katika maeneo hayo ya kazi na kutohudhuria kikao hicho kama alivyoagiza.

Kikao hicho kilishirikisha pia watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)

Alisema kitendo cha wakandarasi kutokuwepo katika maeneo yao ya kazi na kutohudhuria kikao kama ilivyoagizwa kinakwamisha utekelezaji wa miradi na hivyo kuutaka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kujulisha kampuni husika kuandika maelezo ya kutokuwepo kwenye maeneo ya kazi na kukwamisha juhudi za Serikali katika usambazaji wa umeme vijijini.

“ Kama Serikali tumeweka mikakati ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2019- 2021 vijiji vyote nchini vinafikiwa na huduma ya umeme, sasa inapotokea baadhi ya wakandarasi wanakwamisha juhudi hizi wakati wamekwishalipwa na Serikali ni lazima Serikali iwawajibishe kulingana na sheria na kanuni za nchi,” alisema Mgalu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akifafanua jambo mbele ya wanakijiji wa kijiji cha Mbuluni wilayani Mkinga mkoani Tanga (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na serikali wakisikiliza kero mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wanakijiji wa kijiji cha Mbuluni wilayani Mkinga mkoani Tanga (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto mbele) akiendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika kijiji cha Mbuluni wilayani Mkinga mkoani Tanga.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akifafanua jambo kwa wakazi wa kijiji cha Magumbani kilichopo wilayani Mkinga mkoani Tanga.



JAFO AAGIZA MATUMIZI YA ‘TILES’ KWENYE MAJENGO YA HALMASHAURI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewaagiza wahandisi wa ujenzi katika Halmashauri zote hapa nchini kuona uwezekano wa kutumia Tiles badala ya kuweka sakafu ya kawaida ili kuongeza uimara na mandhari majengo hayo.

Waziri Jafo ametoa maelekezo hayo alipokuwa akikagua ujenzi wa madarasa na mabweni ya shule ya sekondari Hamza na miundombinu mbalimbali ya kituo cha afya cha zogolo yakiwepo majengo ya upasuaji, maabara, na wodi ambapo majengo yote ameyakuta yamejengwa vizuri sana kwa kuwekwa Tiles. 

Ameeleza kwamba majengo mengi yanayojengwa na kuwekwa floor(sakafu) ya kawaida yanabomoka kwa muda mfupi na hivyo kuhitajika kufanyiwa ukarabati mara kwa mara.Waziri Jafo amesisitiza kwamba ujenzi wa kutumia Tiles kusaidia hata katika usafi wa majengo hayo. 

Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amewapongeza viongozi wa wilaya ya Nzega wakiwemo wabunge wao Hussein Bashe, Selemani Zedi, na Hamisi Kigwangwala kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwahudumia wananchi wao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
Viongozi wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora wakipata maelekezo ya matumizi ya Tiles kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora wakielekea kwenye kukagua jengo jipya la upasuaji katika Kituo cha Afya cha Zogolo.

Taasisi ya TYPF yazindua kituo cha ufundi Upanga

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF), yenye Makao yake Makuu jijini Dar es Salaam, imezindua kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha. 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Makamu Mwenyekiti wa TYPF Training Centre, Saida Babde alisema ndoto yao ni Taasisi yao kuwa dira ya mtoto wa kike nchini Tanzania kwa namna moja ama nyingine, huku uzinduzi huo ukihudhuliwa na watu mbalimbali akiwamo Mbunge wa Viti Maalum Zainabu Vullu na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mheshimiwa Naseem Al Najim.

"Ndoto yetu ni kumkomboa mtoto wa kike kwa kupitia kituo chetu ambacho kitakuwa kinafundisha mambo mbalimbali kama charahani, kompyuta na kazi nyingine za mikono.

"Nawaomba Watanzania kuchangamkia fursa hii ambapo tumeanzisha ndani ya uwapo wa Taasisi yetu ya TYPF, ambapo sote kwa pamoja tuna kiu ya kumkwamua Mtanzania,"Alisema.

Naye Mheshimiwa Zainabu, Mbunge wa Viti Maalum aliwashukuru TYPF kwa kuguswa na mambo ya kijamii, hususan dhamira ya kumkwamua na kumsaidia mtoto wa kike bila kusahau wale wanaoishi kwenye mazingira magumu.
 Mbunge wa Viti Maalum, Zaynabu Matitu Vulu pamoja na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem(wa pili kulia) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa taasisi isiyo Serikali ya DHE Nureiyne ya Iringa, Sheikh Said Bin Abri.
 Mkuu wa taasisi isiyo Serikali ya TYPF, Ally Bakry akitoa historia fupi ya uanzishwaji wa taasisi isiyo Serikali ya TYPF wakati wa uzinduzi wa kituo cha Ufundi uliofanyika kituoni hapo Upanga jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum, Zaynabu Matitu Vulu akizungumza na wageni waalikwa wakati wa  uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre pamoja na kuomba uongozi wa taasisi hiyo kujikita zaidi kwa wasichana walioko pembezoni mwa mkoa wa Dar Es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem akizungumza jambo wakati wa  uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha.
 Kaimu wa taasisi isiyo Serikali ya TYPF, Saida Babde akitoa ufafanuzi wa uendeshwaji wa kituo hicho na kazi zitakazofanyika kituoni hapo wakati wa uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha.
 Mkuu wa taasisi isiyo Serikali ya DYCCC, Hassan Akrabi(kushoto) akimkabidhi cheti cha heshima kwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem(kulia) kwa mchango waliounesha wakati wa uanzishwaji wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha.
 Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum, Zaynabu Matitu Vulu, Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem pamoja na Mkuu wa taasisi isiyo Serikali ya DHE Nureiyne ya Iringa, Sheikh Said Bin Abri wakiwa wamekaa kwenye viti wakitumia Tarakilishi mpakato (laptop computer) wakati wa  uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DK. KIGWANGALLA AFUNGA MAFUNZO YA 15 YA JESHI USU KWA MAAFISA WANYAMAPORI WA TAWA

$
0
0
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewaagiza wahifadhi wote nchini kushirikiana na wadau wengine hasa mamlaka za Mikoa na Wilaya katika maeneo yenye uvamizi wa mifugo na migogoro ya mipaka ya hifadhi ili kutatua changamoto hizo kwa namna shirikishi ikiwa ni pamoja na kuimarisha utoaji wa elimu kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo.

Ametoa agizo hilo  Disemba, 16, 2017 katika Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wakati akifunga mafunzo ya 15 ya mabadiliko ya kuelekea mfumo wa Jeshi Usu kwa Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa – TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.
“Kazi ya ulinzi wa rasilimali zetu za asili ni yetu na tutaiendeleza, Falsafa yetu ni kuwashirikisha wadau wote, kama kuna taasisi za kiraia kwenye eneo lako la kazi, taasisi za kijamii, mamlaka za mikoa na wilaya, wananchi, halmashauri husika mshirikiane nao ili kupunguza madhara ya operesheni zetu, na zoezi hili la uhifadhi liwe endelevu,” alisema Dk. Kigwangalla.
Aidha, alitoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuheshimu Sheria za nchi na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya hifadhi ikiwemo kuingiza mifugo, kuanzisha kilimo, makazi na ukataji wa miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na matumizi mengineyo.
Awali akizungumzia mafunzo hayo alisema, lengo ni kubadilisha utendaji katika sekta ya uhifadhi kutoka ule wa kiraia kwenda wa jeshi usu ambao utaongeza nidhamu, uwajibikaji, uadilifu na maadili kwa watumishi wote wa sekta hiyo ili waweze kusimamia ipasavyo uhifadhi endelevu wa maliasili za taifa.

RAIS MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA CCM MJINI DODOMA

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk.John Magufuli amewataka wanachama wa CCM kuchagua viongozi bila kuangalia maslahi urafiki, dini, kabila kadhalika amewasihi kutochagua viongozi watoa rushwa kwa kusema kuwa rushwa ni adui wa haki

Amesema kiongozi anapaswa kuwa mfano kwa wanachama na wananchi. Hapaswi kutuhumiwa kwa sifa mbaya kama ujambazi, madawa ya kulevya, rushwa n.k. Kuna msemo maarufu unasema 'mke wa Mfalme hapaswi kutuhumiwa kwa kuchepuka'
"Sio siri kuwa mageuzi tuliyoyafanya ni makubwa sana na hatuna budi kuyasimaia na viongozi waliochaguliwa ndio watakakuwa na majukumu hayo"  Alisema  Rais Magufuli
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk.John Magufuli akizungumza na wanachama wa chama cha Mapinduzi wakati akifungua kifungua mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma leo Jumatatu Desemba 18, 2017.






TASWIRAZZZ MBALIMBALI

SERIKALI KUTOA MWONGOZO KURATIBU VITUO VYA WARAIBU WA DAWA ZA KULEVYA NCHINI.

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini (DCEA) imesema ipo mbioni kutoa mwongozo wa kuratibu na kusimamia viwango vinavyowiana vinavyotarajiwa kutumika katika Vituo  vyote vya Upataji nafuu kwa watumiaji wa dawa za kulevya nchini.
Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Mashirika yasiyo ya Serikali NGO’s kutoka (DCEA), Salome Mbonile wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka minne ya kituo cha upataji nafuu kwa watumiaji wa dawa za kulevya (PEDDEREF) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mbonile alisema katika kuhakikisha kuwa mwongozo huo unaleta tija iliyokusudiwa, Serikali inatarajia kuwashirikisha wadau wote katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya ili waweze kutoa mapendekezo, ushauri na maoni ili kuweza kuisaidia jamii hususani makundi ya vijana katika kujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya.
"Kumekuwa na uwoga kwa wananjamii kutembelea Sober House (Nyumba za upataji nafuu kwa watumiaji wa madawa ya kulevya, lakini kupitia mwongozo huu tunataka kuweza viwango vinavyofanana ili kutoa fursa kwa watu wote kutembelea makazi haya" alisema Mbonile.
Mbonile alisema mapambano ya vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya nchini hayana budi kuungwa mkono na wadau mbalimbali wa maendeleo na hivyo Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa na asasi, taasisi mbalimbali ili kuhakikisha kuwa jamii ya Kitanzania hususani vijana inaendelea kuwa salama na kuondokana na matumizi ya dawa za kuelvya.
Aliongeza kuwa hadi sasa Tanzania ina jumla ya Nyumba za upataji nafuu kwa watumiaji wa dawa za kulevya 25 pamoja na Asasi 16 zinazotoa elimu na kuhamasisha jamii kutambua madhara mbalimbali yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo hatari ya maambuzi ya magonjwa mbalimbali pamoja na vifo.
 Mratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's) kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Bibi. Salome Mbonile akizungumza wakati wa hafla ya kusherehekea miaka minne tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Upataji nafuu kwa watumiaji wa Dawa za Kulevya (PEDDEREF) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Msimamizi wa Programu wa Kituo hicho Khamis Ajib Dimand  na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kituo hicho Bi. Nuru Salehe Ahmed.
 Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kituo hicho Bi. Nuru Salehe Ahmed akizungumza wakati wa hafla ya kusherehekea miaka minne tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Upataji nafuu kwa watumiaji wa Dawa za Kulevya (PEDDEREF) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Msimamizi wa Programu wa Kituo hicho Khamis Ajib Dimand  na Mratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali(NGO's) kutoka   Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Bibi. Salome Mbonile (katikati).
 Mmoja wa wanufaika wa Kituo cha upataji nafuu kwa watumiaji wa dawa za kulevya (PEDDEREF) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam Bi. Amina Mbonde akitoa ushuhuda namna alivyofanikiwa kuacha matumizi ya dawa za kulevya  wakati wa hafla ya kusherehekea miaka minne tangu kuanzishwa kwa kituo hicho jana. Kutoka kulia ni Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kituo hicho Bi. Nuru Salehe Ahmed, Msimamizi wa Programu wa Kituo hicho Khamis Ajib Dimand  na Mratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's) kutoka   Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Bibi. Salome Mbonile na Msimamizi wa Programu wa Kituo hicho Khamis Ajib Dimand.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

VODACOM TANZANIA FOUNDATION, DORIS MOLLEM FOUNDATION WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA HOSPITALI YA WILAYA YA CHATO, MKOANI GEITA

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza katika halfa ya kukabidhiwa msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kusadia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati kwa Hospitali ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita, uliotolewa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Vodacom Tanzania (Vodacom Tanzania Foundation) pamoja na Taasisi ya Doris Mollel (Doris Mollel Foundation). hafla hiyo imefanyika leo katika Hospitali ya Chato, Mkoani Geita.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akipokea moja ya mashine za kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kushoto) kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Chato, Mkoani Geita. Msaada huo umetotea kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Vodacom Tanzania pamoja na Taasisi ya Doris Mollel. Wanaoshuhudia ni Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njini nchini, Doris Mollel (wa pili kushoto) na Kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Chato, Dkt. Ligobert Kalasa.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akiteta jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia pamoja na Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njini nchini, Doris Mollel.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akimkabidhi zawadi ya Khanga Bi. Maria Maganga ambaye ni mzazi aliyekuwa katika Wadi ya Wazazi ya Hospitali hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia akimsalimia mmoja wa watoto waliozaliwa katika Hospitali ya Chato, Mkoani Geita leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (katikati) pamoja na Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njini nchini, Doris Mollel wakipanda mti katika eneo la Hospitali ya Chato ikiwa ni ishara ya mtoto anayezaliwa na kutunzwa katika mazingira bora.

BENKI YA EXIM IPO MSTARI WA MBELE KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VITANDA KWENYE HOSPITALI NCHI NZIMA.

$
0
0
 Mkuu wa kitengo cha masoko cha Exim Bank Tanzania, Stanley Kafu pamoja na wafanyakazi wa tawi la Arusha wakikabidhi vitanda na magodoro 40 kwa mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Dk Timothy Wonanji.

HOSPITALI na kliniki nyingi nchini zina tatizo la ukosefu wa dawa, vifaa na vitanda hasa katika hospitali za rufaa. Kama sehemu ya kampeni yake yenye lengo la kusherehekea miaka 20 ya kutumikia jamii, Benki ya Exim Tanzania imekabidhi vitanda na magodoro 40 kwa Hospitali ya mkoa ya Mount meru iliyoko Arusha.

Hospitali ya mkoa ya Mount Meru, Arusha, ni hospitali ya tano kupokea mchango huu, baada ya Hospitali ya rufaa Dodoma mwezi uliopita, hospitali ya rufaa Ligula, Mtwara mwezi Oktoba, Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar mwezi Septemba na Hospitali ya rufaa Temeke, Dar es Salaam mwezi wa nane mwaka huu. Tukio lilifanyika kwenye hospitali hiyo na mgeni rasmi alikwa Afisa wa matibabu wa Hospitali ya mkoa, Arusha Dr Vivian Wonanji.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya Exim, Bwana Stanley Kafu alisema, “ Mwaka huu benki ya Exim imefikia hatua muhimu sana. Tunasheherekea miaka 20 ya uvumbuzi na kujitolea kwa jamii. Kwa miaka mingi benki ya Exim imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya, mazingira na elimu nchini. Tunatambua juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya hivyo basi tumejitolea mwaka huu mzima kuwekeza katika hospitali za serikali katika maeneo mbalimbali nchini.” 

Afisa wa matibabu wa Hospitali ya mkoa Arusha Dr. Vivian Wonanji alipongeza Exim Bank Tanzania kwa ahadi yake ya kukabiliana na upungufu wa vitanda kwenye ma hospitali ambao unakabiliwa na taifa na kuleta juhudi zake kwa hospitali ya mkoa ya Arusha. Afisa wa matibabu wa Hospitali ya mkoa, Mount Meru alisema “Upungufu wa vitanda katika mahospitali ni changamoto kubwa. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 40 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii.”
Ikiwa kama sehemu ya mradi wa “miaka 20 ya kujali jamii” benki ya Exim itatoa msaada wa vitanda 500 na magodoro yake kwa hospitali katika mikoa ya Mbeya, Arusha, Morogoro, Tanga, Dodoma, Kigoma, Kilimanjaro, Shinyanga, Mtwara, Pemba na Unguja ambapo mpaka sasa Dar es Salaam, Unguja, Mtwara, na Dodoma tayari wameshapokea misaada.

VIJANA WAHAMASISHWA KUANZISHA VIWANDA

$
0
0
Said Mwishehe, Blogu ya jamii
MWENYEKITI wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(TID) Profesa Apollinaria Pereka amewataka vijana  wasisite kuanzisha viwanda nchini  kupitia elimu ya ufundi waliyoipata kwenye taasisi hiyo kwa manufaa ya taifa.

Pia  amesema  wasiogope changamoto watakazokumbana nazo na badala yake wawe wabunifu katika uanzishaji wa bidhaa zao.

Profesa Pereka amesema hayo jijini Dar es Salaam kwenye Mahafali ya 11 ya DIT ambapo amefafanua ,Serikali imejipanga kupiga vita umasikini, hivyo vijana ni vema wakaanzisha viwanda ili wajiajiri wenyewe.
Amewataka wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata kulijenga taifa na kuanzisha viwanda endelevu.

Ameongeza nchi yenye maendeleo makubwa ni ile yenye ujuzi wa ufundi,na wanaotumia teknolojia ya kisasa kwa ajili ya uwanzishaji wa viwanda.
Pia amesema kwa sasa  DIT imefikisha miaka 60 tangu ianzishwe  na imefanya kazi kubwa kueneza elimu ya ufundi nchini.

“Utimizaji wa miaka 60 ya DIT imeenda sambasamba na serikali ya awamu ya tano ya kuanzisha viwanda nchini kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi ,hivyo tutakwenda sambamba na serikali hiyo ili kutimiza azma ya Rais, Dk. John Magufuli,"amesema 

Awali Mkuu wa chuo hicho Profesa Preksedius Ndomba,amesema  Serikali ya awamu ya tano inalenga kuleta maendeleo ya viwanda vidogo,vya kati na vikubwa.

"Hivyo vijana wajiunge katika vyuo vya ufundi ili kuweza kupata ajira na kuanzisha viwanda vyao wenyewe.

“Elimu ya ufundi ina umuhimu mkubwa katika serikali hii ya awamu yatano kwa sababu ya uwanzishaji wa viwanda nchini, vijana mjifundishe ufundi sanifu kwa ajili ya manufaa yenu wenyewe”amesisitiza  Profesa Ndomba.

Ameongeza DIT ipo sambasamba na Serikali katika kufanikisha  uanzishwaji wa viwanda, hivyo wapo makini katika utoaji wa elimu yao ili vijana wao wakimaliza wawe wasanifu wazuri katika viwanda vinavyokuja na kwamba wataendelea kupia watalaamu.
Mwenyekiti wa Baraza Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT), Prof.  Apollinaria Pereka akizungumza kwenye Mahafali ya 11 ya taasisi hiyo jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya wahitimu  876 wamehitimu ngazi mbalimbali za kitaaluma za Stashahda, Shahada na Shahada za Uhandisi na Teknolojia.

ST ANNE MARIA YAPEWA NGAO KWA KUFAULISHA LASABA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
MKOA wa Dar es Salaam umeipatia Ngao Maalum shule ya St. Anne Maria kama sehemu ya kutambua mchango wake katika kuinua elimu hapa nchini.

Sherehe ya kuzawadia shule zilizofanya vizuri ilifanyika mwishoni mwa wiki ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Thelesia Mbando, kwenye kilele cha siku ya elimu Dar es Salaam, zilizofanyika ukumbi wa PTA Sabasaba.

Shule hiyo ilipewa ngao inayoonyesha kuwa ni miongoni mwa shule zilizofanya vizuri zaidi kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka 2016, Best Performing Primary School in Tanzania.

Akizungumza mara baada ya kupokea ngao hiyo, Mkuu wa Shule hiyo, Gladius Ndyetabura alisema ngao hiyo imewapa changamoto ya kuendelea kufundisha kwa bidii ili hatimaye wapate matokeo mazuri zaidi ya mwaka huu.

Alisema ingawa shule yake imefanikiwa kuingia kumi bora kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu, lakini hawajabweteka na badala yake wanafanya jitihada za kuwa namba moja.

“Kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu tumefanikiwa kuwa wa kwanza Wilaya ya Ubungo, tumekuwa wa pili Mkoa wa Dar es Salaam na tumekuwa wanane kitaifa sasa hii haitufanyi tubweteke tutapambana kupata nafasi za juu zaidi,” alisema  

Aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwapa ngao hiyo ambayo imewapa motisha na ari ya kuendelea kufundisha kwa bidiii ili kupata matokeo mazuri zaidi ya waliyopata mwaka huu.

“Shule ni nyingi na ushindani ni mkubwa sana hivyo bado tunakazi ya kufanya kuhakikisha tunaendelea kuwa kumi bora na hata kuwa wa kwanza kitaifa, ingawa shule ni nyingi sana hapa Dar es Salaam lakini tuliopewa ngao na vyeti ni wachache sana sasa hii inaonyesha namna gani mchango wetu unavyothaminiwa,” alisema
Mwalimu Mkuu wa Shule ya St Anne Maria ya Mbezi kwa Msuguri, Gladius Ndyetabura akifurahia pamoja na wanafunzi wa shule hiyo ngao ambayo shule hiyo imepewa na Mkoa wa Dar es Salaam kuipongeza kwa kufanikiwa kuwa ya nane kitaifa na ya kwanza Wilaya ya Ubungo kwenye matokeo ya darasa la saba.

WADAU WAKUTANA KUJADILI MAPENDEKEZO YA SHERIA YA KULINDA TAARIFA BINAFSIADA WA KULINDA BINAFSI

$
0
0
Imeelezwa kuwa kutungwa kwa sheria ya kulinda taarifa binafsi kutapunguza uhalifu unaohatarisha amani na kuongeza usalama wa mtu, jamii, nchi na dunia kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo, amesema hayo katika kikao cha wadau cha kupitia mapendekezo ya kutungwa kwa sheria ya kulinda taarifa binafsi na kusisitiza umuhimu wa kujielimisha kabla ya kusambaza taarifa.
“Ni muhimu kwa jamii kuelewa haki ya faragha ya mtumiaji wa mawasiliano na namna ya kushughulikia taarifa katika ukusanyaji, usambazaji, uchakataji na uhifadhi ili kuepuka kutenda uhalifu” amesema Dkt. Sasabo.
Dkt. Sasabo amezungumzia umuhimu wa jamii kuzingatia sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 na sheria ya miamala ya kielektroniki ya mwaka 2015 ili kuepuka makosa yasiyo yalazima na kuepuka usambazaji wa taarifa binafsi za watumiaji wa mawasiliano usiouwiana na maadili na wenye nia ovu.
“Ni vema jamii ikajua mitandao haina mipaka, hivyo ni muhimu kuwa na muongozo utakaosimamia haki za watumiaji na kulinda taarifa binafsi”, amesisitiza Dkt. Sasabo.
Naye, Afisa Sheria wa Sekta ya Mawasiliano, Bi. Eunice Masigati, amesema mabadiliko ya sayansi na teknolojia yamechangia ongezeko kubwa la makosa katika mawasiliano ya simu na intaneti hivyo uwepo wa sheria inayosimamia taarifa binafsi utapunguza changamoto za kimtandao na kuongeza haki ya faragha.
Dkt. Sasabo, alikuwa katika kikao kazi cha wadau kukusanya maoni ya mapendekezo ya kutungwa sheria ya kulinda taarifa za watumiaji ili kupunguza uhalifu na kuhakikisha usalama wa taarifa binafsi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
 Wadau wa Sekta mbalimbali, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo (hayupo pichani), wakati wa mkutano wa maoni kuhusu sheria ya kulinda taarifa binafsi,Mkoani Dodoma, leo.
 Afisa Sheria wa Sekta ya Mawasiliano, Bi. Eunice Masigati, akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa siku moja wa maoni kuhusu sheria ya kulinda taarifa binafsi, Mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Usalama Mtandao, Eng. Stephen Wangwe.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo, akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa siku moja wa maoni kuhusu sheria ya kulinda taarifa binafsi, Mkoani Dodoma, leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo, akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya wadau walioshiriki katika mkutano wa siku moja wa maoni kuhusu sheria ya kulinda taarifa binafsi, Mkoani Dodoma.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,.


WAKULIMA WA ZAO LA KARAFUU WA MKINGA WAIOMBA SERIKALI KUWAPATIA SOKO LA ZAO HILO

$
0
0
Na David John
WAKULIMA wa zao la Karafuu Kata ya Kigongoi Mashariki wilayani Mkinga mkoa wa Tanga wameiomba Serikali kuwapatia soko la uhakika la zao hilo kwani kuzalisha wanazalisha lakini hawana soko.

Wamesema kuwa katika kata yao hiyo wananchi wake wanalima kwa wingi zao la karafuu lakini pamoja na jitihada hizo za kulima lakini wanakosa soko la uhakika nakuwavunja moyo wa kuendelea kulima zao hilo.

Akizungumza kwaniaba ya wananchi wa kijiji cha Hemsambia Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho Stephen Komba alisema kuwa wananchi wake wanalima kwa wingi zao la karafuu lakini tatizo ni soko.

Alisema kuwa anaiomba serikali kupitia wizara inayohusika kufika kijiji hapo ili kujionea mwenyewe hali ilivyo na kuona namna ya kuwasaidia hususani kupatikana kwa soko la uhakika.

Mbali na changamoto hiyo ya soko la kukosekana kwa soko la karafuu pia kuna tatizo kubwa la miundombinu ya barabara na kwamba hata soko likiwepo tatizo barabara.

"Tunamuomba waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Charles Mwijage pamoja na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kufika eneo hilo kujionea miundombinu ya barabara."alisema Pia alisema kuwa Wilaya ya mkinga inatatizo kubwa hususani kwenye miundombinu ya barabara pamoja na masoko ya mazao ya wakulima wao.

TMRC YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA KIWALANI

$
0
0
Kampuni ya Tanzania Mortgage Refinance Company Limited (TMRC), imetoa zawadi ya Sikukuu ya Krismas zenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili (Shilingi 2,000,000) kwa Kituo cha Watoto yatima cha Kiwalani (Kiwalani Orphanage Centre) kilichopo jijini Dar es Salaam.
Zawadi hizo zimekabidhiwa leo na Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Bw. Oscar P. Mgaya kwa Mkurugenzi wa Kituo hicho, Mchungaji   Elias Mwakalukwa -, katika ghafla iliyofanyika kwenye Kituo hicho kilichopo jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa zawadi zilizotolewa kwa kituo hicho cha watoto yatima ni pamoja na mchele, mafuta ya kupikia, unga wa sembe, maharage, sabuni za kufulia na kuogea, sukari ,  chumvi,  dawa za meno, majani, kalamu na madaftari
“Kwa upendo wetu wa dhati kabisa tumeona umuhimu wa kushiriki pamoja na watoto yatima, ambao wapo katika mazingira magumu, katika kusherehekea Sikukuu ya Krimas mwaka 2017,” alisema Bw. Mgaya.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TTCL YAZINDUA DUKA JIPYA MLIMANI CITY

ZANTEL YAUNGANA NA BODI YA MAPATO ZANZIBAR KUKUSANYA KODI

$
0
0


Zantel kwa kushirikiana na Bodi ya Mamlaka ya Mapato ya Zanzibar wameingia katika makubaliano ambayo yatawawezesha wakazi wa kisiwani hapa kurahisisha huduma ya ulipaji kodi kwa njia ya simu kupitia huduma ya EzyPesa inayotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel.

Ushirikiano huo unawezesha wateja wote wa Bodi ya Mapato Zanzibar kuweza kufanya miamala ya malipo ya kodi bila usumbufu wowote kupitia EzyPesa. Hii inamaanisha kwamba walipa kodi wa ndani wataweza kulipa kodi zao husika ikiwamo ushuru wa forodha na kodi zingine kama PAYE na VAT kwenye uingizaji wa biadhaa kupitia mfumo wa EzyPESA.

Akizungumza wakati wa hafla ya kutiliana saini ya makubaliano hayo Alhamisi ya tarehe 14 Desemba 2017, Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Sherif El Barbary akiwa ameambatana na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Amour Hamil Bakari na Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Mussa (Baucha) alisema lengo kuu la huduma hiyo ni kuwawezesha wakazi wa Zanzibar kulipa kodi kwa urahisi zaidi kupitia huduma ya EzyPesa ya Zantel.

Alisema kuwa hatua hiyo ya makubaliano inaendana sawa na dira ya Bodi ya Mapato Zanzibar, yenye lengo la kuwa kitovu cha ukusanyaji mapato chenye ufanisi, jambo ambalo litaiwezesha nchi kuongeza pato la taifa la ndani kwa mwaka (GDP).

“Kama tunaweza kuongeza ukusanyaji wa mapato kupitia huduma ya EzyPesa na pato la Taifa GDP litaongezeka zaidi. Hii itasaidia kuimarisha uchimi wa Taifa zima, na kwa namna nyingine kipato cha mwananchi wa kawaida kitaongezeka.


Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Sherif El-Barbary (kulia) na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Ndugu Amour Hamil Bakari (Aliyekaa katikati) wakitia saini ya makubaliano ya kushirikiana katika kurahisisha huduma ya ulipaji kodi kwa njia ya simu kupitia huduma ya EzyPesa hivi karibuni mjini Zanzibar. Anayeshuhudia kulia ni Makamu wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Bi. Khadija Shamte Mzee.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Sherif El-Barbary (kulia) na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Ndugu Amour Hamil Bakari (Aliyekaa katikati) wakitia saini ya makubaliano ya kushirikiana katika kurahisisha huduma ya ulipaji kodi kwa njia ya simu kupitia huduma ya EzyPesa hivi karibuni mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Sherif El-Barbary (wa pili kushoto) na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Ndugu Amour Hamil Bakari (wa pili kulia) wakipeana mkono huku wakishuhudiwa na Makamu wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Bi. Khadija Shamte Mzee (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Mikakati na Utendaji wa biashara Zantel, Shinuna Kassim baada ya kutiliana saini ya makubaliano na ushirikiano katika kurahisisha huduma ya ulipaji kodi kwa njia ya simu kupitia huduma ya EzyPesa. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni mjini Zanzibar. 

WAKAZI DODOMA WALAMBA MILIONI 1 KWA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA MTAA WAO

$
0
0

NA RAMADHANI JUMA,OFISI YA MKURUGENZI, MANISPAA

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dokta Binilith Mahenge ameahidi kutoa motisha ya Shilingi 1,000,000 kwa wakazi wa mtaa wa Zahati uliopo Kata ya Kikuyu Kaskazini katika Manispaa ya Dodoma kufuatia wakazi hao kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usafi wa Mazingira unaofanyika kila Jumamosi katika Manispaa hiyo.

Mheshimiwa Mahenge alitoa ahadi hiyo wakati alipowaongoza wakazi hao katika zoezi la usafi wa Mazingira katika Mtaa huo mwishoni mwa wiki, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya kufanya usafi wa Mazingira kila Jumamosi aliyoianzisha yeye mara tu baada ya kuhamishiwa Mkoa humo, kwa lengo la kuuweka Mji Mkuu wa Nchi katika hali ya usafi wakati wote.

Alisema fedha atakazowapa wakazi wa Mtaa huo ni motisha na kuwaunga mkono kwa juhudi walizoonesha na kwamba zitawasaidia katika kuboresha hali ya usafi katika eneo lao kwa kununua vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi.

Alisema amefurahishwa na namna wakazi wa Mtaa wa Zahati walivyojitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo na kutoa wito kwa wakazi wa maeneo mengine katika Manispaa kuiga mfano huo ili kwa pamoja waweze kuufanya Mji wa Dodoma kuwa namba moja kwa usafi wa Mazingira nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dokta Binilith Mahenge (kulia) alipowaongoza wakazi wa Mtaa wa Zahanati Kata ya Kikuyu Kaskazini (pichani nyuma) kufanya usafi wa Mazaingira kila Jumamosi kufuatia Kampeni ya Usafi wa Mji aliyeianzisha yeye. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi.
Wakazi wa Mtaa wa Zahanati Kata ya Kikuyu Kaskazini Manispaa ya Dodoma wakifanya usafi wa Mazaingira wa kila Jumamosi kufuatia kampeni ya Usafi wa Mji iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa huo Dokta Binilith Mahenge.
Zoezi la usafi likiendelea katika Mtaa za Zahanati Kata ya Kikuyu Kaskazini Manispaa ya Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dokta Binilith Mahenge (kuli) akisikiliza kero mbalimbali za Wananchi wa Mtaa wa Zahanati Kata ya Kikuyu Kaskazini Manispaa ya Dodoma baada ya zoezi la usafi wa Mazingira wa kila Jumamosi. Mkuu huyo wa Mkoa amejiwekea utaratibi wa kusikiliza kero za wakazi wa Mtaa husika baada ya kufanya nao usafi wa Mazingira.PICHA: RAMADHANI JUMA-OFISI YA MKURUGENZI MANISPAA YA DODOMA.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images