Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

Tusiime yang’ara siku ya elimu Dar

$
0
0
SHULE ya Msingi Tusiime imeng'ara kwenye maadhimisho ya siku ya elimu  Dar es Salaam baada ya wanafunzi wake kumi kutunukiwa zawadi ya kuingia kumi bora kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka jana.

Tuzo hizo zimetolewa kwenye ukumbi wa TPA Sabasaba jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Thelesia Mmando.

Mbali na wanafunzi wa shule hiyo, shule hiyo ilinyakua tuzo vyeti viwili kutambua mchango wake na mafanikio kwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la nne na la saba. Akizungumza mara baada ya shule yake kupewa tuzo mbili, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi na Awali Tusiime, Philbert Simon, aliushukuru Mkoa wa Dar es Salaam kwa kutambua mchango wa shule hiyo katika elimu na kuwapa tuzo.

Alisema wanafunzi wote 200 waliomaliza darasa la saba shuleni hapo mwaka huu wamechaguliwa kujiunga na shule mbalimbali hali inayowapa matumaini kuwa wanafanya vizuri.

“Ushindani hapa Dar es Salaam ni mkubwa sana lakini kwa motisha kama huu tutaendelea kufanya vizuri maana Tusiime imekuwa ikiwa ya kwanza Mkoa wa Dar es salaam kwa muda mrefu, hata leo hapa watoto wengi waliopata zawadi ni kutoka Tusiime tunashukuru sana,” alisema

Justina Pius ambaye alipewa zawadi ya cheti na ngao kwa kuongoza Mkoa wa Dar es Salaam na kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka 2016, alisema ataendelea kusoma kwa bidii ili kuwa daktari.

“Bidii na maarifa, usikivu darasani ni vitu ambavyo wanafunzi wanapaswa kuvipa kipaumbele maan huwezi kufaulu kwa miujiza hivyo nawashukuru pia walimu wa Tusiime maana wanafanyakazi usiku na mchana,” alisema Justina.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Thelesia Mmando, akimkabidhi tuzo Justino Pius aliyekuwa akisoma shule ya msingi Tusiime na kuibuka mshindi wa kwanza kitaifa na kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka 2016. Tuzo hizo zilitolewa kwenye kilele cha maadhimisho ya elimu Mkoa wa Dar es Salaam jana. Wengine ni wageni mbalimbali kwenye sherehe hiyo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Thelesia Mmando, akimkabidhi tuzo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tusiime ya Tabata Dar es salaam, Philbert Simon, kwa shule yake kuongoza kwa kutoa wanafunzi wengi wa kumi bora mkoa wa Dar mwaka 2016. Hiyo ilikuwa  kwenye hafla ya siku ya elimu Mkoa wa Dar es salaam iliyofanyika kwenye viwanja vya sabasaba.

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi Atoa Ufafanuzi wa Ripoti ya IMF

$
0
0

  Msemaji Mkuu wa Serikali,Dkt Hassan Abbasi akifafanua jambo kwa msisitizo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo kwenye ofisi za Idara ya Habari MAELEZO mjini Dodoma,mambo mbalimbali ikiwemo na kuwakaribisha rasmi katika ukumbi mpya wa MAELEZO hapa Dodoma,kwamba Idara imeshahamia rasmi Dodoma na huduma zote zitakuwa zikitolewa hapo.
 Msemaji Mkuu wa Serikali,Dkt Hassan Abbasi akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo kwenye ofisi za Idara ya Habari MAELEZO mjini Dodoma,mambo mbalimbali ikiwemo na kuwakaribisha rasmi katika ukumbi mpya wa MAELEZO hapa Dodoma,kwamba Idara imeshahamia rasmi Dodoma na huduma zote zitakuwa zikitolewa hapo.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza  Msemaji Mkuu wa Serikali,Dkt Hassan Abbasi alipokuwa akitolea ufafanuzi mambo mbali ikiwemo ripoti ya IMF mapema leo kwenye ofisi za Idara ya Habari MAELEZO mjini Dodoma,pamoja na kuwakaribisha rasmi Wanahabari hao katika ukumbi mpya wa MAELEZO hapa mjini Dodoma,kwamba Idara imeshahamia rasmi Dodoma na huduma zote zitakuwa zikitolewa hapo.PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BALOZI SEIF AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUAGA MIILI YA WANAJESHI WA TANZANIA ( JWTZ ) WALIOUAWA DRC

$
0
0
Huzuni, Majonzi pamoja na simanzi ilitanda ndani ya Nyuso za Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar wakati ndege iliyochukuwa Miili ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) waliouawa Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ilipotua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume.


Miili ya Wanajeshi hao ililetwa Nchini Tanzania juzi kwa ndege Maalum ya Umoja wa Mataifa ikitokea DRC na kupelekwa moja kwa moja Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yaliyopo Lugalo Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kuiaga rasmi Kijeshi.



Ndege iliyowachukuwa Mashujaa hao wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya JW 8029 iliteremsha Miili ya Askari Nassor Daudi Ali, Issa Mussa Juma, Hassan Abdulla Makame na Hamad Mzee Kamna.

Wengine kati ya askari hao Tisa ambapo Mmoja anapelekwa Kisiwani Pemba ni Ali Haji Ussi, Iddi Abdulla Ali, Juma Mossi Ali, Mwinchum Vuai Mohamed na Hamadi Haji Bakari.

Akitoa salamu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema kuuawa kwa Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ} katika shambulio lililofanywa na Waasi wa ADF Nchini DRC ni la Kinyama lilikiuka misingi ya Haki za Binaadamu ambalo pia ni kinyume na makubaliano ya Ulinzi wa Amani wa Kimataifa.


Miili ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ} ikiteremshwa kwenye ndege ya JW 8029 katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume ikitokea Mjini Dar es salaam.
Balozi Seif pamoja na Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavu Meja General Sharif Sheikh Othman wakitoa heshima wakati Miili ya mwashujaa ikiteremshwa kwenye ndege.
Balozi wa Kuweit Nchini Tanzania Bwana Jassem Alnajem wa kwanza kutoka kushoto akijumuika pamoja na Viongozi wa Kiserikali katika kuipokea Miili ya askari wa Tanzania waliouawa Nchini DRC Wiki iliyopita.
Mawaziri mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakishuhudia kuwasili kwa Miili yaWanajeshi wa Tanzania waliouawa na waasi wa ADF Nchini DRC.
Balozi Seif akiongoza Viongozi na Wananchi wa Zanzibar katika kuipokea miili ya Makeshi ya Tanzania yaliyouawa Nchini Jamuhuri ya Kisemokrasi ya Congo.
Majeshi ya Wananchi wa Tanzania wakiichukuwa Miili ya Askari wenzao wakiwasili katika Viwanja vya Makao Makuu ya Brigedia Nyuki Migombani kwa ajili ya kuagwa rasmi Kiserikali.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa salamu za pole kwenye shughuli Maalum ya Kuiaga Miili ya Wanajeshi wa JWTZ hapo Migombani Mjini Zanzibar.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI KUWAFIKIA WALENGWA WA TASAF WALIOBAKI NDANI YA MUDA MFUPI –CAPTAIN MKUCHIKA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT

SERIKALI inatafuta fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa asilimia 30 ya kuziwezesha Kaya Masikini ambazo hazikuweza kuingizwa katika Mpango wa kunusuru kaya maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa ajili ya kuwaondoa kwenye umaskini. Kauli hiyo imetolewa leo mjini Tabora na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Captain (Mstaafu) George Mkuchika wakati wa ziara yake ya kutembelea kaya masikini.

Alisema kuwa kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa asilimia 100 ya kaya masikini nchini zinafikiwa kuwa na uwezo kupata chakula milo yote mitatu ,, sehemu ya kulala na mavazi. Captain (Mstaafu)  Mkuchika alisema kuwa hadi hivi ni asilimia 70 ya kaya masikini ndio wameshafikiwa na Mpango wa Kunusuru kaya masini unaosimamiwa na TASAF na hivyo kuwa uhakika wa kupata mahitaji muhimu.

Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania imelenga kuhakikisha kuwa inavifikia vijiji na kaya zote ambazo hazikufikiwa na Mpango wa Kunusuru Kaya masikini. Captain (Mstaafu) Mkuchika alisema kuwa Serikali inaendelea kutafuta fedha ambapo ndani ya mfupi wataweza kuzifikia kaya masikini zilizobaki  ili nao waweze kunufaika na kujinusuru na umaskini.

Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Nathaniel Linuma alisema kuwa hadi kufikia Agosti mwaka huu walengwa 39,293 walikuwa walipatiwa kiasi cha bilioni 20  ikiwa ni sehemu ya kuwezesha kaya maskini. Aliongeza kuwa jumla ya shilingi milioni 563 zililipwa kwa walengwa chini miradi ya kutoa ajira za muda kama vile uoteshaji miti, ukarabati wa mabwawa, miradi ya barabara. Baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya Masiki katika Manispaa ya Tabora walisema kuwa mpango huo umesaidia kuwa na uhakika wa watoto wao kuzoma na kula milo mitatu.

Mmoja wa wanufaika hao Cecelia Paulo alisema kuwa kabla ya kuanza kupata fedha za Mpango wa kunusuru kaya masikini alikuwa akitegemea vibarua katika mashamba yake ili aweze kumudu kupata walau mlo moja kwa ajili ya wajukuu wake aliachiwa na mwanae lakini hivi sasa analima katika shmaba lake na kupata chakula cha kutosha. Aliongeza kuwa hivi sasa wajukuu zake wanakwenda Shule bila matatizo kwa kwa sababu anazo fedha za kuwanunua mahitaji ya shule zikiwemo sare, madaftari na vitabu kwa sababu ya fedha ya TASAF.

Naye Hadija Jumanne alisema kuwa fedha za TASAF zimsaidia kuanzisha ufugaji wa bata na kuhudumia watoto wake na kuongeza kuwa hivi sasa hana tena shida ya chakula kama ilivyokuwa kabla ya hapo. Mariam Kaombwe alimweleza kuwa fedha hizo zimeweza kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii na kuanza kuapata matibabu bila shida. Alisema kuwa manufaa mengine ni pamoja na kupata mtaji wa kuanzisha biashara ya kuuza nyanya, vitunguu na ujenzi wa nyumba kwa kutumia matofali ya siment.

Mariam aliiomba Serikali iendelea kuwasaidia kupitia TASAF ili wakamilishe miradi yao waliyokwisha kuanzisha.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA MAPOKEZI YA MAKAMU WA RAIS KUHAMIA MKOANI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongaza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dodoma katika mapokezi rasmi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan baada ya kuhamia Mkoani Dodoma leo Desemba 15, 2017. kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa salamu za kumkaribisha Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan aliyehamia rasmi Mkoani Dodoma leo Desemba 15, 2017.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Januari Makamba wakicheza ngoma ya Mwinamila wakati wa Makaribisho ya Makamu wa Rais Mkoani Dodoma leo Desemba 15, 2017.
Balozi Job Lusinde akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa Dodoma kwakuhamia Makamu wa Rais Mkoani Dodoma.

Na Beatrice Lyimo, MAELEZO-DODOMA

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehamia rasmi Makao Makuu ya Nchi Dodoma leo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli alililitoa tarehe 25, Ju.

 Akizungumza wakati wa halfa ya kumkaribisha, Makamu wa Rais amesema kuwa mpaka sasa ni mwaka mmoja na nusu tangu tamko la kuhamia Dodoma litolewe hivyo Serikali ipo na inatekeleza majukumu yake.

“Siku ya leo ilikuwa mawazoni mwangu, ninafurahi imefika na pia ninamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa maandalizi mazuri ya kunipokea ” Alisisitiza Mhe. Samia

Aidha, Mhe. Samia amesema kuwa Ofisi yake imekuja na agenda ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani hivyo  wameandaa programu mbalimbali ikiwemo ya upandaji miti .

“Tarehe 21, Disemba mwaka huu kutakuwa na shughuli ya upandaji miti hivyo tunaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma kutuunga mkono ili kuweza kutimiza azma hii” ameongeza Mhe. Samia.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa Baba wa Taifa aliweka nia ya Serikali kuhamia Dodoma tangu mwaka 1973 na leo Serikali ya Awamu ya Tano imetimiza ndoto hiyo.

“Tunaendelea kuamini kwamba tamko la Rais linatekelezeka ambapo mpaka sasa watumishi 2816 tayari wameshahamia Dodoma na wanaendelea kutoa huduma za Serikali na  kuanzia Februari mwaka 2018 tunaendelea kupokea watumishi wengine” amefafanua Waziri Mkuu.

Naye aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Pancras Ndejembi ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutimiza historia ya Mwalimu Nyerere ya Dodoma kuwa Makao Makuu.

“Sikuwaza kama kuna siku Makao Makuu yatakuwa Dodoma kwa sababu siku nyingi mambo haya yanazungumzwa sasa yamekamilika kwa vitendo, leo nina furaha sana kuona ndoto ya tangu mimi kijana imetimia” ameongeza Mzee Ndejembi.

Kwa upande wake Balozi Job Lusinde amesema kuwa “leo Makamu wa Rais anahamia Dodoma, kweli Mungu hupanga na Mungu huweka wakati wake, leo imekuwa”.

Mbali na hayo Balozi Job Lusinde amesema kuwa Makamu wa Rai amekuja kipindi ambacho Mkoa wa Dodoma unaanza kuandaa mashamba kwa ajili ya kulima, hivyo kumpatia jina la kabila hilo “Mbeleje” likimaanisha kipindi cha kuandaa mashamba.

MAHAFALI YA 15 YA CHUO CHA TAIFA CHA UTALII YAFANA LEO JIJINI DAR.

$
0
0
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewataka wananchi kushirikiana na serikali katika kuvitangaza vivutio vya utalii ili kuongeza pato la taifa.

Amezungumza hayo leo wakati wa mahafali ya 15 ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika kwa kuunganisha matawi ya chuo hicho nchini.Hasunga amewatunikia wanafunzi 129 wakiweza kutunukiwa shahada na astashahada katika fani za upishi, usafi wa vyumba, uhudumu wa chakula na usafirishaji wa watalii.

Katika mahafali hayo, Niabu Waziri Hasunga amewataka wananchi smabamba na wadau mbalimbali wa utalii kushirikiana na serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kuutangaza utalii kwani ni sekta mtambuka.

Kwa sasa seriikali mfumo wa kuwasajili wanafunzi wote walisomea masuala ya utalii ili kuweza kufahamu idadi yao ukamili na pia kuweza kuwafahamu wale ambao wapo katika sekta ya utalii wakiwa hawajapitia katika mafunzo yoyote.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akifungua pamoja na kuzungumza na wahitimu na wageni waalikwa wakati mahafali ya kumi na tano(15) ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika leo katika kampasi ya Bustanini jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Taifa cha Utalii, Bernadetha Ndunguru akizungumza kuhusu namna bodi inavyofanya kazi yake ili kufanikisha Chuo hicho kinafikia malengo waliyojiwekea wakati wa mahafali ya kumi na tano(15) ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika leo katika kampasi ya Bustanini jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii. Dkt. Shogo Muzola akizungumza kuhusu mafanikio na hali ya elimu katika chuo hicho wakati wa mahafali ya kumi na tano(15) ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika leo katika kampasi ya Bustanini jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiwakabidhi baadhi ya wahitimu wa vyeti pamoja na zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri wakati wa masomo.

SERIKALI YATAMBUA MCHANGO WA TIA KUANDAA WATAALAM WA UHASIBU

$
0
0

Said Mwishehe, Blogu ya Jamii.

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Ashatu Kijaji amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na taasisi katika kuandaa wataalam wa tasnia ya uhasibu , biashara ,masoko na rasilimali watu.

Dk.Kijaji amesema hayo leo kwenye mahafali ya 15 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA), Dar es Salaam.Jumla ya wahitimu 3,538 wametunikiwa vyeti kwa ngazi mbalimbali za kitaaluma.

"Endeleeni kutekeleza majukumu yenu kwa weledi, na sisi Serikali tutaendelea kuwaunga mkono.Idadi kubwa ya wahitimu waliopo mbele yetu ni ushahidi tosha wa juhudi na ushirikiano mzuri baina ya Taasisi na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango,"amesema.

Kuhusu mahafali hayo, amesema amepata fursa kujua baadhi ya mafanikio,changamoto na matarajio ya TIA kupitia hotuba iliyotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wake Dk.Joseph Kihanda.

Amesema rasilimali zilizopo ni ndogo na vipaumbele ni vingi.Ili kutatua changamoto za taasisi hiyo ni muhimu kubuni mbinu mpya za kuimarisha mapambano kupata mafanikio makubwa zaidi.Pia amesema azma ya kuanzisha kozi ya Shahada ya pili nayo ni nzuri ili kuongeza nafasi ya kutoa mchango wao kwenye Taifa, na kuwa na mapato ya uhakika.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara Wakili Said Chiguma amesema Taasisi hiyo imekuwa na mafanikio makubwa na kuwezesha kutoa wahitimu wa sifa za kutukuka , kwa ushindi mkubwa kitaaluma na ufanyakazi wa utofauti sehemu mbalimbali kazini."Kwa miaka miwili mfululizo 2015/2016 na 2016/2017 imeongoza kutoa wafaulu wengi wa Shahada ya juu kitaaluma ya uhasibu na ile ya taaluma ya ugavi,"amesema.

Ameongeza pamoja na mafanikio ya kitaaluma na mipango ya kubadilisha mitaala kulingana na soko la ajira,Taasisi inachangamoto mbili kuu.Moja uhaba wa wahadhiri kulingana na idadi ya wanafunzi na upungufu wa miundombinu.
Ofisa Mtendaji Mkuu Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA), Dk. Joseph Kihanda akizungumza na wahitimu pamoja na wageni wakati wa mahafali ya 15 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam.

Uchumi wa Nchi Uko Imara - Dkt. Hassan Abbas

$
0
0
Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Serikali kupitia Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan imesema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Fedha Duniani  (IMF) uchumi wa nchi uko imara ukilinganisha na nchi zilizofanyiwa tathimini.


Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akiongea na vyombo vya habari juu ya maoni ya wataalam wa uchumi kutoka IMF ambao wamemaliza ziara yao hapa nchini Desemba 12, 2017.



"Ripoti ya IMF inaonesha katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017 uchumi umekua kwa asilimia 6.8 takwimu ambazo ni za juu katika chumi zinazokua kwa kasi na ikizidi nchi kadhaa zilizofanyiwa tathmini mwaka 2017 zikiwemo za Ulaya," amefafanua Dkt. Abba.

Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Serikali kupitia Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan imesema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Fedha Duniani  (IMF) uchumi wa nchi uko imara ukilinganisha na nchi zilizofanyiwa tathimini.
Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akiongea na vyombo vya habari juu ya maoni ya wataalam wa uchumi kutoka IMF ambao wamemaliza ziara yao hapa nchini Desemba 12, 2017.

"Ripoti ya IMF inaonesha katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017 uchumi umekua kwa asilimia 6.8 takwimu ambazo ni za juu katika chumi zinazokua kwa kasi na ikizidi nchi kadhaa zilizofanyiwa tathmini mwaka 2017 zikiwemo za Ulaya," amefafanua Dkt. Abba.


NAZARETI YAFUTA MAADHIMISHO YA KRISMASI

$
0
0
Na Kituo cha Habari cha Palestina (Tanzania)

 Meya wa jiji la Nazareti  Ali Salam ametangaza kufuta maadhimisho  yaliyopangwa  kufanyika katika jiji hilo yenye mnasaba wa  Mwaka Mpya,isipokuwa sherehe za uwashaji wa mti wa krismasi na maandamano husika ya kimila ya kila mwaka. Uamuzi huo wa Mheshimiwa Salam, unalenga kupinga tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump kuitambua Yerusalemu kama mji mkuu wa Israeli.
Salam alisema hayo leo Alhamisi wakati wa mkutano wake waandishi wa habari kwamba: "Ndugu zetu Wapendwa katika jiji hili la Nazareti  lililo la thamani na kituo chetu cha Kiarabu kwa ujumla,  Kwa muda mrefu tulisema tunapokea maadhimisho ya Krismasi mara hii,yakiwa yanakwenda sambamba na taarifa za rais wa Marekani juu ya Jerusalemu na kuiunganisha kama mji mkuu wa milele wa Israeli,pamoja na nia yake ya kuhamishia ubalozi.
Tumeingia msimu wa maadhimisho kwa matarajio makubwa, ya kwamba uamuzi huu wa marekani ni wa dhulma, umeliingiza eneo zima katika kuchanganyikiwa na kutuondolea furaha ya sherehe na shamrashamra zake. Nilikuwa katika taarifa za manispaa za awali, nimethibitisha kuwa tupo pamoja na nduguzetu katika kila hali, tutafurahi wakifurahi na tutaona maumivu wakipatwa na maumivu.
Jerusalemu ilikuwa na itabaki kuwa taifa pendwa takatifu la kiarabu, likiwa ni mji mkuu wa Palestina na dora ambayo ipo katika taji. Aidha ameongeza kusema kuwa,"Shughuli za manispaa zitakuwa ni  kibiashara na kiuchumi tu kwa kulinufaisha jiji kibiashara, ambayo tulizoea kukusudiwa na idadi kubwa ya wageni katika msimu huu, huku kukiachwa kuthamini ufanyaji wa shamra shamra kwa taasisi za kidini na kijamii kwa uhuru kabisa, unaokwenda sambamba na mtazamo wao hali iliyopo.


WATEJA WA TANESCO KANDA YA DAR ES SALAAM NA PWANI SASA WANAWEZA KULIPA BILI KUPITIA BENKI YA NMB

$
0
0
Meneja Masoko wa Tanesco, Mussa Chowo


NA K-VIS BLOG
WATEJA wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO ambao hawatumii mita za LUKU, sasa wanaweza kulipia bili zao za kila mwenzi kupitia benki ya NMB, na huduma hiyo inaanza kwa majaribio Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za TANESCO Mikocheni jijini Dar es Salaam Desemba 15, 2017, Meneja Masoko wa Tanesco, Mussa Chowo amesema, huduma hiyo ni kuwarahisishia wateja kuondokana na usumbufu wa kuzifikia ofisi za TANESCO kufanya malipo hayo na badala yake wanaweza kutumia benki ya NMB kufanya malipo.

“Tunaanza kwa majaribio katika kanda ya Dar es Salaam na Pwani na tukiona inakwenda vizuri tutapanua huduma hii kwenye mikoa mingine.” Alisema. Pichani Bw.Chowo (kulia), akitoa taarifa hiyo leo Desemba 15, 2017 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Meneja Tehama, Utafiti na utengenezaji mifumo, Evaristo Winyasi. 

MICHUZI TV: IGP SIMON SIRRO AIPONGEZA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA KATAVI

Dkt KALEMANI aendelea na ziara ya Kukagua Maendeleo ya Miradi ya Umeme

$
0
0
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ameendelea na ziara ya kukagua hatua iliyofikiwa katika ukamilishaji wa ujenzi wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme pamoja na njia ya kusafirisha umeme kutoka Makambako hadi Songea.

Lengo la ziara hiyo ni kukagua uimara wa mitambo ili Serikali kupitia TANESCO iweze kujipanga vizuri kwa kuwa na umeme wa uhakika.
Waziri wa Nishati Dkt MEDARD KALEMANI akiwa kwenye ziara ya Kukagua hatua iliyofikiwa katika ukamilishaji wa ujenzi wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme pamoja na njia ya kusafirisha umeme kutoka Makambako hadi Songea.

"Kama ilivyo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda, tunahitaji kuwa na umeme wa uhakika". Alisema Dkt. Kalemani. Habari Wakuu naomba Mpokee Codes kwa ajili ya Kuhabarisha Umma.....Natanguliza Shukrani Katika ziara hiyo pia amekagua miradi ya umeme Vijijini Awamu ya Tatu inayoendelea katika Mikoa hiyo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati. Akikagua mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 220 kutoka Makambako hadi Songea, Dkt. Kalemani alisema mradi huo utaiunganisha Mkoa wa Ruvuma katika Gridi ya Taifa. Pia, kukamilika kwa miradi hiyo kutaipunguzia gharama Serikali kwa kuondokana na mitambo ya mafuta.
Pichani ni Baadhi ya vituo vya kupoza na kusambaza umeme pamoja na njia ya kusafirisha umeme kutoka Makambako hadi Songea.

DC MCHEMBE AZINDUA KAMPENI YA KUPANDA MITI WILAYA YA GAIRO KATA KWA KATA

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe amezindua kampeni ya kupanda miti Kata kwa Kata. Akizungumza jana wakati akizindua kampeni hiyo iliyofanyika katika tarafa la Nongwe kata ya Chanjale, alisema kuwa wananchi ni lazima waheshimu kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti na si kuikata ovyo. 

Katika kampeni hiyo Mhe. Siriel aliambatana na Meneja wa Misitu Wilaya Bw. David Maiba waliweza kuwahamasisha wananchi kupenda mazingira maana ndiyo yamekuwa yakisababisha wao kupata nvua. "Nawaomba wananchi mpende kuhifadhi mazingira maana ndiyo uhai wetu ambao unasababisdha hata mvua kupatikana, sehemu ikiwa jangwa hamuwezi pata hata maji, niwaombe sana mtunze mazingira kwa ukaribu sana," alisema mhe. Siriel. Kampeni hiyo imeanzia Tarafa ya Nongwe Kata ya Chanjale. Tarafa hii ipo uwanda wa juu ambapo mvua tayari zimeanza. 

Viongozi wengine ambao aliambatana nao ni Diwani wa Chanjale Mhe. Maswaga Malima, Mtendaji Kata Bi. Stella Ngomano, Wenyeviti wa Vijiji, Watendaji wa Kata, Wazee Maarufu, Viingozi wa Dini na wananchi kwa ujumla. Kata ya Chanjale ina Misitu ya Hifadhi yenye ukubwa wa ekari 3,000. Aliongeza kuwa upandaji wa miti utakuwa ni zoezi endelevu na ameshaagiza kila kijiji kiwe na kitalu cha kuzalisha miti japo changamoto inayowakabili ni viriba, ambapo wanahitaji viriba zaidi ya milioni moja kwa Wilaya yote ya Gairo.
 Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe akizungumza machache na wananchi waliofika katika uzinduzi huo. 
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe akipanda mti kuashiria uzinduzi wa kampeni hiyo. 
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe akielekea eneo la tukio na wananchi eneo la tukio.

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK SHEIN AJUMUIKA KATIKA SALA YA IJUMAA NA WAUMINI WA KIISLAM KATIKA MASJID NUNGE DODOMA MJINI.

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislam Mkoani Dodoma baada ya kumaliza Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid Nunge Dodoma Mjini leo 15/12/2017. (Picha na Ikulu)
WAUMINI wa Dini ya Kiislamu Mkoani Dodoma wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitowa nasaha zake baada ya Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid Nungwe Dodoma Mjini leo 15/12/2017(Picha na Ikulu) 

DKT. MWAKYEMBE : MICHEZO YA VYUO VIKUU INATOA FURSA YAKUBAINI VIPAJI VIPYA


Mabondia Francis Cheka na Shabani Kaoneka wapima uzito leo,kuzichapa kesho uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara

$
0
0
Mabondia Francis Cheka na Shabani Kaoneka, wamepima uzito leo tayari kwa pambano lao linalotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi katika uwanja wa Umoja  Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara, ambapo Francis Cheka anatetea mkanda wake wa IBO Africa

Zoezi la upimaji Uzito likiwa linaendelea na kusimamiwa na Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi wa Ngumi za Kulipwa Tanzania Ally Bakari na kuthibitisha Ulinganifu wa Uzito.

Mara baada ya zoezi Hilo Franciss Cheka ambaye anatetea Mkanda IBO Afrika amewaomba mashabiki wa ngumi Mkoa wa Mtwara Kuweza kujitokeza kwa wingi na tayari amefanya mazoezs ya kutosha Kuweza kushinda

Pambano hilo la round Kumi, litasindikizwa na mapambano ya utangulizi yatakayowahusisha mabondia wa Mtwara dhidi ya mabondia kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Tanga sambamba na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii Sholo Mwamba na 20 Percent.
 

TAARIFA YA KUFUNGA MWISHO WA MWAKA KWA WANA TASNIA YA HABARI

WAZIRI LUKUVI AMALIZA MGOGORO WA ARDHI ULIODUMU MIAKA 10 CHAMWINO MKOANI DODOMA

$
0
0

WAZIRI wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi amefuta uamuzi wa viongozi wa Vijiji vya Membe na Mlimwa vilivyopo Kata ya Membe Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma wa kumpatia ardhi yenye ukubwa wa ekari 1756 mwekezaji David Mazoya Poli takribani miaka 10 iliyopita hali iliyosababisha mgogoro wa ardhi na kuhatarisha amani katika Kata hiyo.

Hali ya sintofahamu iliwagubika wakazi wa Kata hiyo kwani licha ya kukataa kutoa ardhi yao kwa mwekezaji huyo kupitia mikutano mikuu ya Vijiji, viongozi wao walimmilikisha Mwekezaji huyo ardhi hiyo  ikiwemo ekari 100 alizopewa na Kijiji cha Membe kwa makubaliano kuwa atawajengea Ofisi ya Serikali ya Kijiji ahadi ambayo hata hivyo hajaitekeleza.

Akizungumza na wakazi wa Kata hiyo kwenye mkutano wa hadhara jana, Waziri Lukuvi alisema kuwa amefuta maamuzi yote yaliyofanywa na Serikali za Vijiji hivyo kwani yalikiuka Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 1999 inayotoa mamlaka kwa Vijiji kumilikisha ardhi isiyozidi ekari 50 tu na sio vinginevyo.

“Kuanzia leo nimefuta maamuzi yote yaliyofanywa na viongozi wa Vijiji hivi kumpa mwekezaji huyu ardhi yenye ukubwa wa ekari 1756 kwani ni kinyume cha Sheria ya Vijiji…hata kama Vijiji vitakubali kutoa ardhi kupitia mikutano mikuu ya Vijiji bado maamuzi hayo hayatakuwa halali endapo ardhi inayotolewa itazidi ukubwa wa ekari 50” alifafanua Waziri Lukuvi.

Alimtaka Mwekezaji huyo ambaye alifika katika mkutano huo, kufuata taratibu za kumilikishwa ardhi inayozidi ukubwa wa ekari 50 endapo ana nia ya kuendelea kuwekeza katika Kata hiyo, ikiwa ni kuomba ardhi katika Vijiji hivyo na endapo vitaridhia, vitapendekeza kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye mwenye Mamlaka ya kumilikisha ardhi inayozidi ekari 50 baada ya ardhi hiyo kuhama kutoka katika Mamlaka ya Vijiji.

Wakazi wa Kata hiyo walimshukuru Waziri Lukuvi kwa uamuzi huo wa Serikali kwa madai kwamba wameteseka kwa kipindi kirefu ikiwa ni pampoja na kukosa maeneo ya kulima na malisho kwa ajili ya mifugo yao.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.  William Lukuvi akizungumza wakati wa Mkutano wa Hadhara katika Kata ya Membe Wilayani Chamwino jana ambapo alitoa uamuzi wa kuirudisha kwa Wananchi wa Vijiji vya Membe na Mlimwa ardhi yenye ukubwa wa ekari 1756 aliyepewa mwekezaji Davidi Mazoya Poli ( aliyesimama kushoto) kinyume cha taratibu miaka 10 iliyopita.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Membe wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  alipofanya ziara katika Kata hiyo jana.

Washindi wa Promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde wakabidhiwa mkwanja wao

$
0
0
Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa Mary Rutta (aliyekaa kushoto) pamoja na Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (aliyekaa kulia) wakiwa pamoja na baadhi ya washindi wa zawadi za shilingi milioni moja na laki tano katika promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde'. Jumla ya wateja 55 wa Tigo wamejishindia donge nono katika promosehni hiyo inayoendelea ambapo wateja wa Tigo wanaofanya miamala kupitia Tigo Pesa wana fursa ya kujishindia zawadi za kila siku za shilingi milioni moja na shilingi laki tano. Pia kuna zawadi kubwa ya shilingi milioni 15, milioni 10 na shilingi milioni 5 zinazoshindaniwa.
Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta akizungumza na baadhi ya washindi wa promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde' ambapo wateja 11 wamejishindia zawadi za kila siku za shilingi milioni moja kila mmoja, huku wengine 44 wakijishindia zawadi za kila siku za shilingi 500,000 kila mmoja. Pamoja na zawadi hizo za kila siku, zawadi kubwa katika promosheni hiyo inayoendelea ni shilingi milioni 15, milioni 10 na shilingi milioni 5.

MWANASHERIA MKUU AWATAKA MAWAKILI WAPYA KUJIARI

$
0
0
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Mawakili wapya muda mfupi baada ya kukubaliwa na kusajiliwa. Pichani pia yupo Jaji Mkuu Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma na Majaji.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akizungumza na Mawakili wapya waliokubaliwa na kusajiliwa ambapo katika nasaha zake kwao alisema atawashangaa sana mawakili hao kama watakuwa wazururaji mitaani wakisubiri ajira badala ya kuitumia taaluma yao kujiajiri wenyewe. Hafla ya kuwakubali na kuwasajili Mawakili hao imefanyika leo katika Viwanja vya Karimjee
Sehemu ya Mawakili wapya 296 ambao wamekubaliwa na kusajiliwa kuwa Mawakili wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wakashindwa kujizuia kushangilia pale alipowapa changamoto ya kuzitumia fursa zilizopo kujiajiri wenyewe kwa kwenda Mikoani na Wilayani badala ya kung'ang'ania kukaa Dar es Salaam.
Mhe. George Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akibadilishana mawazo na Mkurugezi wa Mashtaka ( DPP) Bw. Biswalo Maganga muda mfupi kabla ya hafla ya kuwakubali na kuwasajili Mawakili 296 wapya katika hafla iliyofanyika leo Ijumaa katika Viwanja vya Karimjee.

Na Mwandhishi maalum.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju, amewataka Mawakili wapya kuzitumia fursa nilizopo kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa. Ametoa ushauri huo leo ( Ijumaa) wakati wa hafla ya kuwakubali na kuwasajili Mawakili wapya 296. Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Karimjee.

“Niwashauri Mawakili wapya, anzeni kufanya kazi. Itashangaza sana, na nitawashangaa sana kama na nyie mtakaa mtaani mkisubiri kuajiriwa badala ya kutumia taaluma na ujuzi milioupata kujiajiri wenyewe” Mhe. Masaju amewataka mawakili hao wa kike na wakiume, na ambao wengi wao ni vijana wa umri wa kati ya miaka 30 na 40, kwenda mikoani na wilayani ambako amesema, kuna fursa nyingi za kujiajiri na pia kuna wateja wengi wenyeuhitaji mkubwa wa kupata huduma ya za kisheria.

“Nendeni mikoani na wilayani badala ya kung’ang’nia kukaa hapa Dar es Salaam na katika majiji na miji mingine mikubwa hapa nchini. Huko mtapata soko kubwa la wananchi wanaohitaji huduma zenu na wenye uwezo wa kulipia huduma hizo kutokana na shughuli zao mbalimbali zikiwamo za kilimo” amesisitiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kwa wale Mawakili ambao wataajiriwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na katika Utumishi wa Umma. Mwanasheria Mkuu amesema watatakiwa kuzingatia ipasavyo Maadili ya Msingi yanayosimamia utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live


Latest Images