Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109583 articles
Browse latest View live

VISIMA VYA MAJI VILIVYOCHIMBWA NA UNHCR WILAYANI KAKONKO KUWANUFAISHA WATANZANIA NA WAKIMBIZI WALIOPO KAMBINI MTENDELI

0
0
Kisima Cha Maji Kilichochimbwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR)katika Kijiji cha Kasanda ambacho kitawanufaisha Wananchi wa Maeneo hayo na Wakimbizi waishio katika Kambi ya Mtendeli Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.
Moja wapo ya bomba la maji yaliyosambazwa ndani ya Kambi ya Wakimbizi Mtendeli kutoka katika mojawapo ya Visima Vilivyochimbwa katika Vijiji Jirani na eneo la Kambi.
Wahandisi wa Maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) na Shirika la TCRS wakikagua chumba chenye mashine ya kuchuja na kusafisha maji yanayotoka katika kisima kilichochimbwa kwa ajili ya matumizi ya Wakimbizi waishio katika Kambi ya Mtendeli Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma.

Mhandisi wa Maji kutoka shirika la TCRS Linalofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),Emmanuel Busanga akitoa maelezo juu ya mahitaji ya maji katika kambi ya Mtendeli iliyopo Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma
Muhandisi wa Maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),Mukiza Florinus akitoa maelezo kwa Mwandishi wa habari wa Gazeti la The Guardian ,Getrude Mbago ambaye ni sehemu ya ujumbe wa waandishi watano waliotembelea kambi za wakimbizi 

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA AFYA MKOANI ARUSHA.

0
0
 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile aliyevaa shati la drafti la mikono mirefu akikagua baadhi ya majengo ya kituo cha afya cha Nduruma  ambayo yapo kwenye ujenzi wakati wa ziara yake Jijini Arusha leo.
 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa kwanza kulia akiangalia kwa makini dawa zilizopo kwenye hifadhi ya dawa ya kituo cha afya cha Nduruma wakati alipotembelea kituo hiko kwenye ziara yake jijini Arusha.
 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katikati akiangia mojawapo ya  nyenzo za kuhifadhia dawa za maji (syrup) katika kiwanda cha kuzalisha dawa nchini TPI  wakati alipotembelea kiwanda hiko kwenye ziara yake jijini Arusha, kushoto ni Naibu Mkurugenzi  Mtendaji wa TPI Bi. Zarina Madaba.



Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile  wa pili kulia akipata maelekezo namna kiwanda cha TPI kinavyofanya kazi ya kuzalisha dawa muhimu nchini kutoka kwa Naibu Mkurugenzi  Mtendaji wa TPI Bi. Zarina Madaba.

MAGAZETI YA IJUMAA LEO DECEMBER 15,2017

NAIBU WAZIRI AWESO ATEMBELEA MAMLAKA YA MAJI TANGA UWASA

0
0
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akisalimiana na Afisa Rasilimali watu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa),Haika Ndalama mara baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya kuitembelea mamlaka hiyo.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Phares Aram wakiingia kwenye ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo kwa ajili ya kumpatia taarifa wakati wa ziara yake.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi anayefuatia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Phares Aram.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akichimba mtaro katika eneo la Mikanjuni Jijini Tanga wakati alipotembelea mradi wa mfumo wa uboreshaji wa Maji 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MBUNGE BALOZI DKT. KAMALA AKABITHI VIFAA VYA MICHEZO KWA SHULE ZOTE WILAYANI MISSENYI NA TIMU 13 ZA KATA JIMBONI NKENGE

0
0
Mbunge wa Jimbo la Nkenge leo amekabidhi vifaa vya michozo vyenye thamani ya shilingi milioni 36,080,000 za kitanzania kwa shule zote za sekondari zilizo ndani ya Wilaya ya Missenyi na timu za mpira za kata 13 zilizomo jimboni Nkenge
Vifaa hivyo vimekabidhiwa katika mkutano mkubwa wa kila mwaka wa Wadau wa maendeleo wa Jimbo la Nkenge uliofanyika jana Alhamisi Dec 14,2017 katika ukumbi wa Halmashauri ya Missenyi-Bunazi
Akiongea na wadau Balozi Dk. Kamala amesema; 'anaomba vifaa hivyo vitunzwe kama ilivyokusudiwa pia ametumia fursa hiyo kutoa shukrani kwa Ubalozi wa Ubeligiji Tanzania,Chama cha Mpira cha Ubeligiji kwa kusaidia kupata Vifaa hivyo pia amekishukuru kiwanda cha Kagera Sugar kwa kusaidia kusafirisha vifaa hivi kutoka Dar es Salaam mpaka Missenyi jimboni mwake.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

SHIRIKA LA NDEGE LA ATCL LAFUNGUA OFISI MPYA ZANZIBAR

0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe,Mohammed Abdalla Salum katikati akikata Utepe kuashiria Ufunguzi wa Ofisi mpya ya Shirika la Ndege la ATCL Kijangwani Posta mjini Unguja.kushoto yake ni Naibu Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe,Chumu Kombo Khamis na Kulia ni -Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ndege la ACTL Ar Tanzania Eng Emanuel Koroso.
Katibu Mtendaji Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dk,Lila Vuai Lila kushoto na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la ATCL, Albinus Manumbu wakitiliana saini mkataba wa utumiaji wa ndege kwa watalii watakaofika Zanzibar katika Ufunguzi wa Ofisi yao Mpya Kijangwani Posta mjini Unguja.
Katibu Mtendaji Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dk,Lila Vuai Lila kushoto na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la ATCL, Albinus Manumbu wakibadilishana hati ya mkataba wa utumiaji wa ndege kwa watalii watakaofika Zanzibar katika Ufunguzi wa Ofisi yao Mpya Kijangwani Posta mjini Unguja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ndege la ATCL,  Eng Emanuel Koroso akitoa hotuba ya makaribisho kwa Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Ofisi yao Mpya Kijangwani Posta mjini Unguja.
Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe,Mohammed Abdalla Salum akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Ofisi Mpya ya Shirika la Ndege la ATCL, Kijangwani Posta mjini Unguja.

WALIODANGANYA RUZUKU YA UCHIMBAJI WATAKIWA KUREJESHA

0
0
Serikali imewataka wanufaika wa ruzuku ambao hawakuitumia kama ilivyokusudiwa warejeshe fedha walizopatiwa mara moja na vyombo vya ulinzi na usalama vihakikishe waliohusika kuidhinisha wanawajibishwa. Agizo hilo limetolewa Desemba, 12, 2017 na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo Mkoani Singida wakati wa ziara yake ya kutembelea Migodi ya Dhahabu kwa ajili ya kujionea shughuli zinazoendelea na kuzungumza na wachimbaji.

“Aliyenufaika na ruzuku na hakufanya lolote, arejeshe mara moja fedha hiyo na aliyehusika kuwapatia ruzuku watu hawa hali yakuwa anaelewa hawakuwa na dhamira ya kuendeleza uchimbaji nae achukuliwe hatua,” aliagiza Nyongo.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto aliyenyoosha mkono) akielekeza jambo alipotembelea Mgodi wa Dhahabu wa Mwandami Small Scale Mine uliopo katika Kijiji cha Sambaru, Kata ya Mang’onyi Wilayani Ikungi. 

Agizo hilo linafuatia malalamiko ya wachimbaji wadogo ambao hawakunufaika na mpango huo wa ruzuku ambapo walimueleza kwamba wapo baadhi ya watu wasiostahili lakini walipatiwa ruzuku. Naibu Waziri Nyongo alisema anampongeza Rais John Magufuli kwa uamuzi wake wa kusimamisha utoaji wa ruzuku kwani imeshindwa kufikia matarajio yaliyokusudiwa. Alisema Serikali ilisimamisha utoaji wa ruzuku kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini baada ya kubaini kwamba imeshindwa kuleta mafanikio yaliyokusudiwa.

Nyongo alisema dhamira ya Serikali ya kutoa ruzuku ilikuwa ni kuhakikisha wachimbaji wadogo wa madini nchini wanaweza kuendeleza machimbo yao kwa kufanya shughuli zenye tija kwao na Taifa kwa ujumla. Hata hivyo alisema dhamira hiyo haikuzaa matunda yaliyokuwa yamekusudiwa kwani imedhihirika kwamba ruzuku iliyotolewa haikuwanufaisha walengwa kama ilivyotarajiwa badala yake ilinufaisha watu wachache tofauti na ulivyokuwa mpango mzima wa utoaji wake.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akitazama mtambo wa kusaga mawe yenye Madini ya Dhahabu uliopo kwenye Mgodi wa Mzaki na Wenzake uliopo katika Kijiji cha Mwau, Wilayani Ikungi. Kulia ni Mmoja wa Wamiliki wa mgodi huo, Kasirate Mzaki. 

“Wapo wachimbaji wachache ambao walifanikiwa kupata ruzuku na waliweza kuendeleza migodi; japo hawa ni wachache tofauti na malengo ya Serikali,” alisema Naibu Waziri Nyongo. Mbali na hilo, alisema baadhi ya wachimbaji wadogo walipewa ruzuku na walichimba lakini hawakufanikiwa kwani walichimba kwa kubahatisha bila kuwa na elimu ya kutosha ya kutambua uwepo wa mashapo katika maeneo yao.

Exim Benki Tanzania yashinda tunzo za Mwajiri Bora 2017 (EYA)

0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha ushiriki Tuzo za Mwajiri Bora 2017 (EYA), Mkuu wa Rasilimali watu wa Exim Bank Tanzania, Mr Fredrick Kanga kwenye hafla ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana usiku. Exim Bank Tanzania imeshinda tuzo ya ushindi wa jumla wa mwajiri bora wa ndani ya nchi.
 Mkuu wa Rasilimali watu wa Exim Bank Tanzania, Mr Fredrick Kanga akipokea tuzo ya ushindi wa jumla wa mwajiri bora wa ndani ya nchi jana usiku katika halfa ya utoaji tuzo hizo kutoka chama cha waajiri Tanzania (ATE) Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Rasilimali watu wa Exim Bank Tanzania, Mr Fredrick Kanga pamoja na Mr Stanely Kafu, Mkuu wa idara ya masoko wa benki hiyo wakipiga picha na baadhi ya wafanyakazi katika halfa ya utoaji tuzo hizo kutoka chama cha waajiri Tanzania (ATE) Dar es Salaam jana ambapo Exim Bank Tanzania imeshinda tuzo ya ushindi wa jumla wa mwajiri bora wa ndani ya nchi.

Prof Lipumba ashangaa kuzushiwa ugonjwa

0
0
Na Baba Feilsal.

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi(CUF) Ibrahimu Lipumba amesema afya yake iko imara na hana tatizo lolote kiafya.

Ametoa kauli hiyo  muda huu wakati akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu ambapo amesema anashangazwa na taarifa ambazo zipo kwenye baadhi ya mitandao kuwa anaumwa na amelazwa Hospitali ya Agha Khan.

"Nimeshangaa sana kusikia eti kuna taarifa zinadai nimepatwa na nshtuko, taarifa hizo si za kweli na ndio hizo hizo zinaitwa feck news.Nipo imara na najiandaa kwenda msikiti na baada ya hapo nitakwenda makao makuu ya chama kwa ajili ya kusimamia kikao," amesema Prof Lipumba.

Amefafanua hakuwa anajua kinachoendelea mtandaoni kuhusu yeye kwani anapoingia kwenye mtandao ni kwa ajili ya kuangalia tafiti mbalimbali na si taarifa za kuzusha.

Amesema alishangaa kuona anapigiwa simu na watu mbalimbali wakimpa pole ya ugonjwa ndipo aliposhangaa na kuanza kufuatilia chanzo cha hiyo taarifa.

Nimepata fursa ya kuzungunza kwa kirefu na prof lipumba yupo bukheri wa afya njema  na ameshangazwa na uzushi kuwa ameptwa na mshutuko.

TADB PAYS A FAREWELL TO MIVARF’S RAVI MALIK

0
0
The sole agricultural bank in in the country, Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) has paid a farewell to the Technical Adviser (Rural Finance) to Marketing Infrastructure, Value Addition and Rural Finance (MIVARF) Support Programme.

MIVARF is a project under the Prime Minister’s Office. The program aims to reduce rural poverty and accelerate economic growth on a sustainable basis. The Programme Development Objective is to enhance incomes and food security of the target group on a sustainable basis.

Speaking during the farewell meeting at TADB’s premises, the Acting Managing Director of the Bank, Mr. Francis Assenga said the Bank will remember Mr. Malik’s contribution toward establishment of Smallholder Credit Guarantee Scheme (SCGS) and Management of Rural Innovation Fund (RIF) under custodian of TADB.

“Your contribution toward establishment of Credit Guarantee Scheme and Rural Innovation Fund is remarkable, we will forever remember you for making these two prestigious projects under TADB to happen,” he said.

An Indian born, Mr. Malik has been in Tanzania since 15 February 2014 where he was assisting MIVARF to meet its twin objectives. Firstly, to collaborate with and support Bank of Tanzania, Ministry of Finance and the Ministry of Agriculture, Food Security & Cooperatives and the Networks, with a view to facilitating formulation of a suitable policy/institutional framework (including enactment of a legislation) for the orderly growth and regulation & supervision of rural finance sector in Tanzania, including the Micro Finance (MF) sector.

Secondly, to help a few partner institutions, (the Community/Cooperative Banks and MF Institutions (MFIs), to extend their outreach in rural areas, so as to bring five hundred thousand additional rural households under the ambit of the formal financial system by 2017.

According to the recently issued statement by African Development Bank MIVARF has successfully achieved its development objectives in increasing the percentage of all-year passable rural roads and decrease in the number of households located more than 10kms from passable roads; increased volume of goods moved within and out of the focal areas and access of farmers’ produce to markets; and increased price of farmers produce and districts’ revenue collection.
TADB’s Acting Managing Director, Mr. Francis Assenga (left) talks during the  farewell ceremony for Mr. Ravi Malik (not in picture), the outgoing Technical Adviser (Rural Finance) to Marketing Infrastructure, Value Addition and Rural Finance (MIVARF). Others in picture are some the senior management of the Bank
TADB’s Acting Managing Director, Mr. Francis Assenga (right) gives souvenirs to the outgoing Technical Adviser (Rural Finance) to Marketing Infrastructure, Value Addition and Rural Finance (MIVARF), Mr. Ravi Malik (left). Mr. Malik has been in Tanzania since 15 February 2014.

The outgoing Technical Adviser (Rural Finance) to Marketing Infrastructure, Value Addition and Rural Finance (MIVARF), Mr. Ravi Malik (left) chats with TADB’s Acting Managing Director, Mr. Francis Assenga (right) after a farewell ceremony held at TADB’s premises.

UNHCR: YAELEZA NAMNA INAVYOFANYA SHUGHULI ZAKE KWA WANA HABARI WALIOTEMBELEA KAMBI ZA NDUTA NA MTENDELI

0
0
 Ofisa wa Masuala ya Maji na Usafi wa Mazingira  kutoka Shirika la  Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR), Nosakhare Boadi akizungumza wakati  wa Mkutano wa kutoa maelezo kwa ufupi kwa Ujumbe wa Waandishi wa Habari watano kutoka Vyombo mbalimbali nchini Tanzania.
 Mtaalamu wa Masuala ya Ukatili wa Kijinsia na Ustawi wa Jamii Kutoka Shirika la kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),Rehema Katyega akizungumza na ujumbe wa Waandishi wa Habari waliotembelea Kambi za Nduta na Mtendeli Mkoani Kigoma.
 Sehemu ya Ujumbe wa Waandishi wa habari waliotembelea Kambi za Wakimbizi za Mtendeli na Nduta Mkoani Kigoma kujionea shughuli zinazotekelezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la  Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) pamoja na Wadau mbalimbali .
 Wafanyakazi wa  Ofisi ndogo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la  Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) Kibondo mkoani Kigoma  wakifatilia kwa karibu mkutano wa maelezo  mafupi juu utekelezaji wa shughuli  mbalimbali za shirika hilo katika kambi za Wakimbizi  za Nduta na Mtendeli
Sehemu ya  Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la  Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) wakiwa katika mkutano huo

IGP SIRRO, AZINDUA ZAHANATI NA KUSHIRIKI MAZOEZI YA UTAYARI MKOA WA KATAVI

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa pili kulia akiwa na maafisa wa Jeshi la Polisi wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Mkoa wa Katavi leo katika ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani humo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati) kulia kwake ni Meja Jenerali Mstafu Rafael Muhuga, wakiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Katavi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wanne kutoka kulia akiwa katika mazoezi ya utayari na Askari waliokuwa wakifanya maonyesho ya utayari Mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake.Picha na Jeshi la Polisi.

RAIS DKT. MAGUFULI ATEKELEZA AHADI YAKE YA SH. MILIONI 60 KWA WAJUMBE WA CHAMA CHA WALIMU PAMOJA NA WANAFUNZI WA UDOM WALIOHUDHURIA MKUTANO HUO CWT

0
0
Katibu wa Rais Ngusa Samike akikabidhi kiasi cha Shilingi milioni 60 kwa Kaimu Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Leah Ulaya kutekeleza ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa hapo jana mara baada ya kuendesha harambee ya papo kwa papo ambapo kiasi hicho cha fedha kilipatikana.
Katibu wa Rais Ngusa Samike akizungumza mara baada ya kukabidhi kiasi hicho cha Shilingi milioni 60 kwa Kaimu rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Leah Ulaya. Katika fedha hizo, kiasi cha Shilingi milioni 50 zitagawiwa kwa wajumbe wote wa CWT waliopo mkutanoni na kiasi cha Shilingi milioni 10 ni kwa ajili ya wanafunzi Tarajali wa UDOM waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo.
Fedha hizo kiasi cha Shilingi milioni 60 zilizo kabidhiwa kwa CWT ambazo Rais Dkt. John Pombe Magufuli alizichangisha kwa viongozi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano wa CWT siku ya jana. Katika fedha hizo Rais Dkt. Magufuli alitoa kiasi cha Tsh. Milioni 10 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa kiasi cha Sh. Milioni 10 pia na zilizobaki zilichangwa na viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo.

PICHA NA IKULU

HOTUBA YA RAIS DKT.JOHN MAGUFULI KWENYE UFUNGUZI WA NYUMBA ZA NHC IYUMBU ,DODOMA

POLISI TAZARA WATOA ONYO KWA WAHALIFU

0
0

Na. Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi nchini limewaonya badhi ya watumishi wasio waaminifu wanaofanya kazi katika Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya wizi wa mafuta na miundombinu mbalimbali ya shirika hilo kuacha mara moja.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi, Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi Mwandamizi PATRICK BYATAO wakati wa hafla fupi ya kuwatunukia zawadi baadhi ya Askari waliofanya vizuri katika kuhakikisha usalama wa miundombinu ya shirika hilo ambapo baadhi yao walifanikiwa kuwakamata watumishi wa shirika hilo wakiiba mafuta.

Amesema katika siku za karibuni kumekuwa na matukio kadhaa ya watumishi wa shirika hilo wasio waaminifu ambapo wamekuwa wakilitia hasara shirika hilo jambo ambalo amesema wanaendelea kuimarisha usalama ili kuhakikisha kuwa wanawadhibiti.

BYATAO amesema Kikosi hicho kitaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara ili kuhakikisha wanakomesha tabia hiyo ambayo imekuwa ikidhoofisha utendaji wa TAZARA pamoja na kuitia hasara Serikali.

Akizungumzia utoaji wa Zawadi hizo BYATAO amesema askari hao kumi wamefanya vizuri kwa kujituma katika kipindi cha mwaka 2017 hivyo kwa mujibu wa taratibu za Jeshi la Polisi ni vyema kuwazawadia ili kuongeza morali yao ya kazi na kuwafanya wengine kuendelea kujituma zaidi.

Kwa upande wake mmoja wa Askari waliopata zawadi baada ya kufanya vizuri WP NINA DACHI amewaasa askari wenzanke kuendelea kufanya kazi kwa umakini ili kuhakikisha kuwa miundominu ya shirika hilo inakuwa salama wakati wote.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akimkabidhi cheti cha utendaji bora WP Nina Dachi wa kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akimkabidhi cheti cha utendaji bora mmoja wa askari wa kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akimkabidhi zawadi ya jiko la gesi mmoja wa askari wa  kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akikagua gwaride wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku askari waliofanya vizuri kwa mwaka 2017 katika kikosi hicho ambapo kwa kiasi kikubwa wamezuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA.Picha na Jeshi la Polisi


WAZIRI LUKUVI AMALIZA MGOGORO WA ARDHI ULIODUMU MIAKA 10 CHAMWINO DODOMA

0
0
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi amefuta uamuzi wa viongozi wa Vijiji vya Membe na Mlimwa vilivyopo Kata ya Membe Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma wa kumpatia ardhi yenye ukubwa wa ekari 1756 mwekezaji David Mazoya Poli takribani miaka 10 iliyopita hali iliyosababisha mgogoro wa ardhi na kuhatarisha amani katika Kata hiyo.

Hali ya sintofahamu iliwagubika wakazi wa Kata hiyo kwani licha ya kukataa kutoa ardhi yao kwa mwekezaji huyo kupitia mikutano mikuu ya Vijiji, viongozi wao walimmilikisha Mwekezaji huyo ardhi hiyo ikiwemo ekari 100 alizopewa na Kijiji cha Membe kwa makubaliano kuwa atawajengea Ofisi ya Serikali ya Kijiji ahadi ambayo hata hivyo hajaitekeleza.

Akizungumza na wakazi wa Kata hiyo kwenye mkutano wa hadhara jana, Waziri Lukuvi alisema kuwa amefuta maamuzi yote yaliyofanywa na Serikali za Vijiji hivyo kwani yalikiuka Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 1999 inayotoa mamlaka kwa Vijiji kumilikisha ardhi isiyozidi ekari 50 tu na sio vinginevyo.

“Kuanzia leo nimefuta maamuzi yote yaliyofanywa na viongozi wa Vijiji hivi kumpa mwekezaji huyu ardhi yenye ukubwa wa ekari 1756 kwani ni kinyume cha Sheria ya Vijiji…hata kama Vijiji vitakubali kutoa ardhi kupitia mikutano mikuu ya Vijiji bado maamuzi hayo hayatakuwa halali endapo ardhi inayotolewa itazidi ukubwa wa ekari 50” alifafanua Waziri Lukuvi.

Alimtaka Mwekezaji huyo ambaye alifika katika mkutano huo, kufuata taratibu za kumilikishwa ardhi inayozidi ukubwa wa ekari 50 endapo ana nia ya kuendelea kuwekeza katika Kata hiyo, ikiwa ni kuomba ardhi katika Vijiji hivyo na endapo vitaridhia, vitapendekeza kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye mwenye Mamlaka ya kumilikisha ardhi inayozidi ekari 50 baada ya ardhi hiyo kuhama kutoka katika Mamlaka ya Vijiji.

Wakazi wa Kata hiyo walimshukuru Waziri Lukuvi kwa uamuzi huo wa Serikali kwa madai kwamba wameteseka kwa kipindi kirefu ikiwa ni pampoja na kukosa maeneo ya kulima na malisho kwa ajili ya mifugo yao.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza wakati wa Mkutano wa Hadhara katika Kata ya Membe Wilayani Chamwino jana ambapo alitoa uamuzi wa kuirudisha kwa Wananchi wa Vijiji vya Membe na Mlimwa ardhi yenye ukubwa wa ekari 1756 aliyepewa mwekezaji Davidi Mazoya Poli ( aliyesimama kushoto) kinyume cha taratibu miaka 10 iliyopita.


Baadhi ya wakazi wa Kata ya Membe wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipofanya ziara katika Kata hiyo jana.


Baadhi ya wakazi wa Kata ya Membe wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipofanya ziara katika Kata hiyo jana.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Membe wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipofanya ziara katika Kata hiyo jana.

KINANA AWAASA WANA CCM KUMUUNGA MKONO MWENYEKITI WAO,RAIS DKT MAGUFULI KATIKA KUPAMBANA NA VITA YA RUSHWA NA UFISADI

0
0
 Katibu MKuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mapema jana kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya Wilaya uliokuwa ukifanyika jana katika kata ya Ilongero,Singida vijijini katika jimbo la Singida Kaskazini,ambapo Wajumbe wa CCM walikuwa wakipiga kura kutafuta Mbunge atakaekiwakilisha chama hicho katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni,kufuatia jimbo hilo kuachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Mh.Lazaro Nyalandu aliyehamia CHADEMA.Ndugu Kinana aliwaasa Wajumbe hao kumchagua mtu anaefaa na atakawasaidia na kuwasemea matatizo yao,na atakae kuwa tayari kuwaletea maendeleo.

Kina pia aliwaasa Wana CCM kumuunga mkono Mwenyekiti wao,Rais Dkt John Pombe Magufuli katika suala zima la kupambana na vita ya rushwa,ufisadi,ubadhirifu wa mali za umma na kuhakikisha nidhamu ndani ya chama na watumishi wa umma inaimarika kwa kiwango kikubwa.
Wajumbe wakimsikiliza Ndugu Kinana kwa umakini kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wananchi waliovutiwa na hotuba ya Katibu Mkuu Ndugu Kinana,ilibidi wasogee zaidi na kuendelea kusikiliza
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida Ndugu Juma Kilimba akimkaribisha Mgeni rasmi,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyepita kuwasalimia na kuona wamejiandaaje na uchaguzi wao wa kura za maoni kwa ajili ya kumchagu Mtu atakaewawakilisha katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni,kufuatia jimbo hilo kuachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Mh.Lazaro Nyalandu aliyehamia CHADEMA.Ndugu Kinana aliwaasa Wajumbe hao kumchagua mtua anaefaa na atakawasaidia na kuwasemea matatizo yao,na atakae kuwa tayari kuwaletea maendeleo.
 Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Singida Vijijini wakishangilia jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahamani Kinana alipokuwa akizungumza nao kabla ya kupiga kura ya kumchagua atakaewawakilisha katika nafasi ya Ubunge,na hatimaye kugombea katika uchaguzi mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika jimboni humo hivi karibuni.
Mjumbe wa kamati kuu ya siasa ya Mkoa,Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt Rehema Nchimbi akizungumza mapema jana kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya Wilaya uliokuwa ukifanyika jana katika kata ya Ilongero,Singida vijijini katika jimbo la Singida la Kaskazini,ambapo Chama cha Mapinduzi kinamtafuta Mbunge atakaekiwakilisha chama hicho katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni,kufuatia jimbo hilo kuachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Mh.Lazaro Nyalandu aliyehamia CHADEMA. 


 Katibu MKuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mjumbe wa kamati kuu ya siasa ya Mkoa,Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt Rehema Nchimbi jana mara baada ya kuwasili katika Kata ya Ilongero,Singida vijijini katika jimbo la Singida la Kaskazini,ambapo Chama cha Mapinduzi jana kilikuwa kinapiga kura za maoni kumchagu Mbunge atakaekiwakilisha chama hicho katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni,kufuatia jimbo hilo kuachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Mh.Lazaro Nyalandu aliyehamia CHADEMA.

MKUTANO MKUU WA YANGA KUTOA MAAMUZI YA MFUMO WA UENDESHAJI KLABU

0
0
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa  akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

Klabu ya Yanga inatarajia kuwa ya pili kuingia katika mfumo wa hisa kutoka ule wa umiliki wa wanachama kama walivyofanya watani wao wa jadi Simba wiki mbili zilizopita.

Simba iliweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza Tanzania na Afrika Mashariki na kati kuingia mfumo huo ambapo Yanga wanatarajiwa kuwa wapili.

Katibu mkuu wa timu ya Yanga, Boniface Mkwasa amesema kikako cha kamati ya Utendaji kilichoketi Disemba 13 kimefikia maamuzi hayo ambapo watasubiri mkutano mkuu wa wanachama utakaofanyika ndani ya miezi mitatu ili kukamilisha jambo hilo.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa alisema wataunda kamati itakayosimamia mchakato wa zabuni ambao kwa mujibu wa katiba yao wanachama wanatakiwa kubaki na asilimia 51 na wawekezaji asilimia 49.

"Kamati ya utendaji imekutana juzi na kupitisha kubadili mfumo wa uendashaji wa klabu kutoka mfumo wa umiliki wa wanachama hadi hisa ambapo mchakato tayari umeanza siku chache zijazo tutatangaza kamati ya kusimama jambo hilo," alisema Mkwasa.

Simba iliingia rasmi kwenye mfumo wa hisa Disemba 3 mwaka huu ambapo mfanyabiashara Mohammed Dewji 'MO' alifanikiwa kushinda zabuni na atawekeza kiasi cha sh bilioni 20 kwa Wekundu hao.

WAZIRI MWIJAGE :HAKUNA CHANGAMOTO ZA KIBIASHARA

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema hakuna changamoto za biashara nchini bali kinachotokea ni kukosa elimu na taratibu za kufanya biashara.

Mwijage ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Tanzania Growth Trust ambayo awali ilifahamika Gatsby Growth , amesema soko la bidhaa liko la kutosha na hakuna sababu ya kuangalia masoko ya nje wakati ndani  soko bado halijatosholeza mahitaji ya wananchi kupata bidhaa.

Amesema kuwa changamoto  zinazotajwa na wajasiriamali ni zile zinazohusu Shirika la Viwango Tanzania( TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA ) ambapo kazi ya vyombo hivyo ni kuhakikisha vitu vinavyozalisha vinakuwa na ubora wa kuhimili soko la ndani na nje ya nchi.

Mwijage amesema kukutana katika uzinduzi huo ni pamoja na kueleza namna Serikali inavyoangalia masuala ya viwanda  na wajisiriamali  katika kuzalisha bidhaa ambazo zitahimiri soko la ndani.

 Naye Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la  Tanzania Grouth Trust(TGT) Oliva Lwena amesema anaishukuru Serikali kwa kutatua changamoto zinazowakabili wajasiriamali nchini.

Pia amesema wao wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wajasiriamali wanafanikiwa katika shughuli zao za kimaendeleo na kuongeza ni wakati wa Watanzania kujikita kufanya maendeleo yao.

Ameshauri vijana kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii huku akionesha kutofurahishwa na tabia ya baadhi ya wananchi wanaotumia muda mwingi kucheza mchezo wa kubeti wapate fedha za haraka.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charle’s Mwijage akizungumza katika uzinduzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya  Tanzania Growth (Trust TGT) jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Growth Trust (TGT), Oliver Lwena akizungumza juu ya mikakati ya kuwasaidia wajasirimali ili waweze kukua na kuchangia uchumi wananchi jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa  Bodi wa Tanzania Growth Trust (TGT),  Mhandisi Zebadiah Moshi akizungumza juu ya taasisi ya TGT inavyofanya kazi karibu na serikali.
  Sehemu ya wajasiriamali katika uzinduzi wa  TGT.
Bidhaa za wajasiriamali ambao wako katika mwamvuli wa TGT

MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU HASSAN AHAMIA RASMI MKOANI DODOMA

0
0
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na baadhi ya watendaji wa Ofisi yake muda mfupi baada ya kuhamia rasmi Makao Makuu ya Nchi, Dodoma. Amefikia Ikulu ndogo iliyopo eneo la Kilimani Mchana wa leo.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye makazi yake Mjini Dodoma leo.

Viewing all 109583 articles
Browse latest View live




Latest Images