Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

RAIS WA SOS CHILDREN’S VILLAGE AAHIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA UTOAJI WA HUDUMA KWA WATOTO

$
0
0
Rais wa SOS Children’s Village, Siddhartha Kaul amesema taasisi hiyo itaendelea kuimarisha ushirikiano na serikali ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kuendelea kusaidia miradi mbalimbali inayohusu kuwalinda watoto hapa nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Ijumaa katika ziara yake ya siku nne nchini Tanzania, alisisitiza kwamba kupitia SOS Children Village ataendelea kufanya kazi na Serikali ya Tanzania ili kuangazia masuala mbalimbali yanayoathiri usalama wa watoto nchini Tanzania.

“Tutaendelea kufanya kazi na jamii pamoja na serikali katika kuweka mazingira mazuri ya baadaye kwa watoto ili kuhakikisha huko mbeleni wanatimiziwa mahitaji yao muhimu,” alisema.

Ziara ya Rais huyo ilianzia Zanzibar ambako alitumia fursa hiyo kutembelea watoto na kukagua baadhi ya miradi ambayo inatekelezwa na asasi hiyo.

Kwa Dar es Salaam Kaul atakutana na watoto na kukagua miradi michache ambayo inasimamiwa na asasi hiyo pamoja na kubadilishana mawazo na viongozi mbalimbali wa Serikalini.
Rais wa SOS Children’s Village, Siddhartha Kaul (kulia) akiwasili katika kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS Children’s village kilichopo Ubungo jana jijini Dar es salaam. Rais huyo yupo nchini kwa ziara ya siku 2 ambapo atakagua miradi ya shirika hilo na kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa SOS Village Tanzania, Dk. Mary Nagu.
Rais wa SOS Children’s Village, Siddhartha Kaul akisalimiana na wamama waliojitolea kuwalea watoto Shirika hilo baada ya kutembelea kituo cha watoto yatima cha SOS Children’s village kilichopo Ubungo jana jijini Dar es salaam. Rais huyo yupo nchini kwa ziara ya siku 2 ambapo atakagua miradi ya shirika hilo na kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali.
Kikundi cha watoto wanaolelewa katika makazi ya SOS children’s village Ubungo jijini Dar es salaam, kikitoa burudani ya aina yake wakati wa hafla ya kumpokea rais wa Shirika hilo ambaye aliwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku 4 mwishoni mwa juma. Raisi wa Shirika hilo ameweza kukagua miradi ya SOS Children’s village na kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali.
Rais wa SOS Children’s Village Siddhartha Kaul, akisalimiana na watoto wanaolelewa katika kituo cha SOS Children’s village kilichopo Ubungo hivi karibuni jijini Dar es salaam. Rais wa Shirika hilo alitua nchini kwa ziara ya siku 2 ambapo alikagua miradi ya shirika hilo na kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali.


MKUCHIKA ATEMBELEA WALENGWA WA TASAF KATIKA JIJI LA TANGA.

$
0
0
NA. Estom Sanga- Tanga

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Huruma Mkuchika amewaagiza viongozi wa halmashauri za wilaya nchini kote kusimamia kwa karibu utekelezwaji wa miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Akizungumza mwanzoni mwa ziara yake ya kukutana na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- katika jiji la Tanga Waziri Mkuchika amesema ufanisi wa Mpango huo umeanza kuonekana kutokana na idadi kubwa ya Walengwa kuanza kuboresha maisha yao hivyo kinachotakiwa ni kuweko na dhamira thabiti ya wataalamu hususani wa Maendeleo ya Jamii ambao wanaweza kutoa mchango muhimu zaidi kwa Walengwa.

Mheshimiwa Mkuchuka amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi hususani wanaokabiliwa na umaskini ili waweze kuondokana na kadhia hiyo kupitia mipango mbalimbali ukiwemo Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF.

Aidha Mhe. Mkuchika ameonya dhidi ya uwezekano wowote wa kuhudumia wananchi wenye uwezo katika Mpango huo na kuagiza Watendaji wa halimashauri za Wilaya kuhakiki mara kwa mara majina ya kaya zilizoko kwenye Mpango ili kujiridhisha na walengwa wa Mpango ambao ni kaya Maskini sana.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuchika ametembelea kaya za baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini katika jiji la Tanga na kujionea namna ruzuku wanaoipata ilivyoanza kuboresha maisha yao kwa kuboresha makazi ,kuanzisha miradi midogo midogo ya biashara, kusomesha watoto na kuimarisha huduma za kliniki kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Taarifa ya Mkoa wa Tanga imeonyesha kuwa tangu shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini zianza takribani miaka mitatu iliyopita Kaya zilizokuwa zinaishi katika umaskini mkubwa wa kipato zimeanza kuboresha maisha huku changamoto kubwa iliyobakia ikiwa ni idadi nyingine ya wananchi wanaoishi kwenye Umaskini mkubwa wa kipato kutojumuishwa kwenye mpango kutokana na uhaba wa fedha. 
 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora,Mhe. George Huruma Mkuchika (aliyevaa Kaunda suti )akiangalia ‘genge’ la bidhaa zinazouzwa na mmoja wa Walengwa wa TASAF katika mmoja wa mtaa wa jiji la Tanga.

 Waziri wa Nchi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Huruma Mkuchika akimpongeza mmoja wa Walengwa wa TASAF jijini Tanga baada ya kukagua nyumba aliyoijengwa kwa kutumia sehemu ya ruzuku ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini .
 Baadhi ya Viongozi walioambatana na Mhe. Mkuchika (wa nne kulia walioketi) wakisikiliza taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TASAF katika mmoja wa mitaa ya jiji la Tanga. Wa pili kulia waliosimama ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,bwana Ladislaus Mwamanga. 
 Waziri Mkuchika akiwa ameketi nje ya mgahawa wa mmoja wa Walengwa TASAF katika jiji la Tanga ,Mgahawa ambao ameuanzisha mlengwa huyo baada ya kupata ruzuku kutoka Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato. 
 Mhe. Mkuchika akiwa ndani ya nyumba ya mmoja wa Walengwa wa TASAF ,katika jiji la Tanga ,nyumba ya mlengwa huyo imeezekwa kwa mabati kwa kutumia sehemu ya ruzuku kutoka Serikalini kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Huruma Mkuchika akizungumza na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Tanga na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga kabla ya kuwatembelea walengwa wa TASAF kuona namna wanavyonufaika na huduma za Mfuko huo mkoani humo.

NEC yawajibu UKAWA

$
0
0
Na Mwandishi Maalum
MKURUGENZI wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani alisema chama cha siasa kutangaza kugomea kushiriki uchaguzi hakuwezi kuifanya tume ihahirishe uchaguzi kwani tume haiko kumshawishi mtu au chama kushiriki uchaguzi.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ramadhani alisema chama kushiriki uchaguzi ni jambo la hiyari na tume ya uchaguzi iko pale kwa ajili  ya kuweka na kutengeza mazingira yatakayofanya vyama vya siasa kushirki uchaguzi.

Alisema iwapo kuna chama kitaamua kutoshiriki uchaguzi, chama kitakachoshiriki hata kama ni mmoja mgombea wake atapita bila kupingwa.  Alisistiza kuwa hakuna sehemu yoyote ya katiba na sheria ya uchaguzi inayotamka kwamba chama kisiposhiriki uchaguzi basi uchaguzi unaahirishwa. 

“Ila ikitokea vyama vikasusa vyote kushiriki kwenye uchaguzi hapo ndipo unaweza kuahirishwa kwa kuwa hakutakuwa na mgombea,”alifafanua mkurugenzi wakati alipokuwa anazungumza na baadhi ya waandishi wa habari ambao walitaka kupata ufafanuzi wa tume kuhusu tamko lililotolewea na mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe.

Hivyo ameviasa vyama vya siasa vinavyotishia kutoshiriki kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo matatu na kata sita kufuata mifumo ya kisheria ya kushughulikia malalamiko ya uchaguzi.

Aliitaja mifumo hiyo kuwa ni kuwasilisha malalamiko kwenye kamati ya maadili wakati wa kampeni,  wakati wa kuanza kupiga kura wakala akiwa na malalamiko anajaza fomu namba 14 na fomu namba 16 wakati upigaji kura unapoeendelea  na kama mgombea hakuridhikai anaruhusiwa kwenda mahakamani.

Juzi Mbowe  alitishia kuwa vyama vinavyounda umoja wa katiba (UKAWA) havitashiriki uchaguzi iwapo changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 zisipofanyiwa kazi na NEC.

Akizungumzia hoja hiyo Ramadhani alisema kwamba katika orodha ya vyama vilivyopo NEC, Ukawa sio moja ya vyama vya siasa na akaongeza kuwa kushiriki kwenye uchaguzi ni hiyari ya chama cha siasa.

“Niwasihi vyama vya siasa watumie mifumo iliyopo ya kawaida ya kuwasilisha malalamiko yao, kwenye kamati za maadili, kujaza fomu namba 14 kabla ya kura kuanza kupigwa, fomu 16 wakati kura zinapigwa na kuwasilisha malalamiko mahakamani baada ya kura kuhesabiwa,”alisema Kailima.

Aliseima hiyo ndio mifumo iliyowekwa kisheria katika kushughulikia changamoto za  uchaguzi zinapojitokeza, “Je hiyo mifumo wanayotaka wao ni ipi?  Kama kama kuna mgombea hakuridhika mahakama zipo aende maana wamepewa siku 30 za kufungua kesi.”

Alisema NEC haiwezi kuahirisha uchaguzi kwani sheria inatamka kuwa uchaguzi unaweza kuahirishwa iwapo tu kuna mgombea amefariki, kutokuwepo mgombea, zikitokea ghasia na fujo au wagombea wakifungana kwa kura.

“Je kuna mgombea amefariki? Haya mambo yote manne hayajatokea, sasa tutaahirishaje uchaguzi? Alihoji Ramadhani na akavitaka vyama vya siasa kutumia mifumo iliyopo kuwasilisha malalamiko yao

Akizungumzia kuhusu jimbo la Longido ambalo Mbowe alidai kuwa shauri la uchaguzi bado liko mahakamani na kwamba wameiandikia NEC kuhusu suala hilo na hawajajibiwa barua yao, Ramadhani alisema madai hayo sio ya kweli kwani barua zote walizoandikiwa wamezijibu.

Alisema jimbo hilo liko wazi kwa kuwa mahakama ndio imeiandikia NEC kuitaarifu kumalizika kwa kesi iliyokuwepo mahakamani. Alisema kwamba NEC itasimamisha uchaguzi wa jimbo hilo iwapo tu wataambiwa na mahakama kusimamisha mchakato huo.

“Nimesikitishwa na kauli kwamba eti wametuandikia barua sisi tume ya kusimamisha uchaguzi wa Longido eti hatujawajibu, tulipata barua kutoka kwa ole Nangole (Onesmo) tukamjibu, tukapata barua kwa wakili wa Ole Nangole nikamjibu, tukapata barua kutoka kwa katibu wa Chadema tukamjibu na nikaongea naye kwenye simu, sasa aleo wanaposema kwamba hatujawajibu kwa kweli kauli hiyo imenisikitisha sana,”alisema Ramadhani.

RC MBEYA AMOS MAKALA AFUNGUA MAFUNZO YA MADAKTARI WA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI YANAYORATIBIWA NA WCF

$
0
0



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mbeya

TAKRIBAN madaktari na watoa huduma za afya 100 kutoka mikoa saba ya Kanada ya Nyanda za Juu Kusini, wameanza kupatiwa mafunzo jijini Mbeya yanayoratibiwa na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF).

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo ya siku tano yaliyofunguliwa rasmi Desemba 12, 2017 (jana) NA Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makala kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba, alisema, mafunzo hayo ni muendelezo wa mafunzo kwa madaktari na watoa huduma za afya ili kuwajengea uwezo wa kufanya tathmini ya ulemavu maradhi anayopata mfanyakazi wakati akitekeleza majukumu yake mahala pa kazi ili hatimaye madaktari hao waweze kutoa mapendekezo kuwezesha mfuko kutoa mafao ya fidia stahiki.

Kwa mujibu wa mratibu wa mafunzo hayo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, mafunzo hayo yamewaleta pamoja madaktari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya Mbeya, Songwe, Katavi, Rukwa, Iringa, Njombe na Ruvuma.

Katika hatua ya kuimarisha Hifadhi ya Jamii, Tanzania, Serikali ilianzisha Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi kwa mujibu wa kifungu namba 5 cha sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, kipengele cha 263 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2015 ili kuhakikisha kila mfanyakazi Tanzania Bara kutoka sekta ya umma na binafsi anapata fursa ya kuwekewa bima na mwajiri wake ili anapopata majeraha au magonjwa awapo kazini basi aweze kufidiwa kwa mujibu wa sheria, alisema Bw. Mshomba.

“Lengo kuu la kuanzishwa kwa Mfuko huu ni kutoa fidia stahiki kwa mfanyakazi aliyepatwa na majeraha, maradhi kutokana na kutekeleza wajibu wake awapo kazini, lakini pia kuwalipa fidia wategemezi wake anapofariki katika mazingira hayo.” Alifafanua Bw. Mshomba na kuongeza, WCF ilianza kutekeleza majukumu yake Julai Mosi, 2015 na mwaka uliofuata Mfuko ulianza rasmi kupokea madai ya fidia na kulipa mafao kwa waathirika.

Wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa WCF jijini Arusha mwishoni mwa mwezi uliopita, kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, aliitaka WCF kuendelea kutoa elimu kwa wadau, ili waweze kuelewa vema shughuli za Mfuko na nia njema ya serikali ya kuanzisha mfuko huo ili mfanyakazi wa Tanzania aweze kupata fidia stahiki anapopata madhara sehemu ya kazi.

Bw, Mshomba aliishukuru Serikali na Wizara zake kwa kuunga mkono na kusaidia juhudi za WCF katika kuimarisha mifumo yake ili kutoa huduma bora kwa wadau wake.“Pia napenda nizishukuru taasisi za Hospitali ya Taifa Muhimbili, MOI, Ocea Road Hospital, MUHAS, na OSHA kwa kuwaruhusu wataalamu wake ili tuwatumie katika kutoa mafunzo haya.” Alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Amos Makala ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo, alisema, juhudi za ushirikiano wa pamoja miongoni mwa wadau yaani Serikali, Wafanyakazi, Waajiri unahitajika sana kuhakikisha tathmini endelevu ili kuimarisha mfuko. 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makala, akihutubia wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku tano kwa madaktari wanaofikia 100 kutoka mikoa saba ya kanda ya nyanda za juu Kusini, kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa, jijini humo Desemba 12, 2017. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), yanalenga kuwajengea uwezo madaktari na watoa huduma za afya kufanya tahmini ya mfanyakazi aliyepata ulemavu au ugonjwa mahali pa kazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfukom wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba ya ukaribisho kweye ufunguzi rasmi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktari wanaofikia 100 kutoka mikoa saba ya kanda ya nyanda za juu Kusini, kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa, jijini humo Desemba 12, 2017. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na WCF, yanalenga kuwajengea uwezo madaktari na watoa huduma za afya kufanya tahmini ya mfanyakazi aliyepata ulemavu au ugonjwa mahali pa kazi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makala, na Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omar.
Washiriki wakifuatilia hotuba kwa umakini.
Washiriki wakifuatilia hotuba kwa umakini.
Washiriki wakifuatilia hotuba kwa umakini.
Mshiriki akizungumza kwenye mafunzo hayo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU MAJALIWA AHUDHURIA MKUTANO MKUU WA TISA WA UMOJA WA WAZAZI TANZANIA - MJINI DODOMA

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Phillip Mangula wakati alipohudhuria katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa Umoja wa Wazazi Tanzania kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma Desemba 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo wakati alipohudhuria katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa Umoja wa Wazazi Tanzania kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma Desemba 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati alipohudhuria katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa Umoja wa Wazazi Tanzania kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma Desemba 12, 2017. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

MKUU WA JESHI LA POLISI IGP SIRRO AAGANA NA MAAFISA NA ASKARI MKOANI TABORA BAADA YA KUMALIZA ZIARA YAKE.

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akiaga vingozi wa Jeshi la Polisi mkoani Tabora baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani humo.  Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati) kushoto kwake ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora SACP, Willprod Mtafugwa wakiwa katika  picha ya pamoja na kikosi cha kupambana wahalifu Mkoa wa Tabora.  Picha na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro katikati akiwa katika picha ya pamoja na Askari wa kike wa Jeshi la Polisi kikosi cha kupambana na uhalifu Mkoa  wa Tabora.  Picha na Jeshi la Polisi.

TANZIA

$
0
0
Marehemu Mama Badriya Kiondo

Familia za Bw. Kiondo wa Kwaminchi Tanga na Bw. Ramadhan Haji wa Betras, Zanzibar wanasikitika kutangaza kifo cha Mtoto wao mpendwa, Bi. Badriya Ramadhan Kiondo aliyekuwa Mkuu wa Utawala na Fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini India kilichotokea tarehe 11 Desemba, 2017 katika Hospitali ya Apollo mjini New Delhi, India. 

Mwili wa Marehemu Mama Kiondo unatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi tarehe 14 Desemba, 2017 saa 8.45 mchana kwa Ndege ya Shirika la Emirates. Aidha, mazishi yatafanyika katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam Ijumaa tarehe 15 Desemba, 2017 saa 10.00 jioni.

Msiba wa Marehemu Mama Kiondo upo nyumbani kwa mumewe Bw. Frank Mwamkai Kiondo maeneo ya Ada Estate, Na. 73, Kinondoni, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Ubalozi wa Ufaransa.

Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote wa familia hizi popote pale walipo.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina

KIKAO CHA KUJADILI HALI YA USALAMA BARABARANI NCHINI CHAFANA MJINI DODOMA

$
0
0
Na WAMJW - Dodoma .

Madereva nchini wamepongezwa kwa kuanza kubadilika na kutii sheria bila shuruti katika kukabiliana na ajali za barabarani na hivyo kupungua kwa ajali pamoja na vifo vitokanavyo na ajali kwa uendeshaji unaofuata taratibu na sheria za barabarani.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha Barabarani Tanzania  Fotunatus Mselemu –Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa kupokea maoni ya sheria kuhusu ajali za barabarani  unaojumlisha mashirika yasiyo ya Kiserikali .

Kamanda Mselemu alisema tatizo la ajali barabarani bado ni kubwa kwani watu wengi wanafariki na kujeruhiwa kutokana na ajali barabarani”sisi sote  ni wahanga wa usalama barabarani hivyo hatuna budi  wadau wote kushirikiana katika kukabiliana na suala hili  na kila mmoja anayo nafasi ya kuchangia ili usalama wa barabarani uimarike  na kuboreka zaidi”Alisema.

Alisema hivi sasa watu wengi wameanza kubadilika hususan madereva wengi ambapo kuna wakati inabidi jeshi la polisi kutumia nguvu nyingi ili kuweza kuepuka ajali zinazoweza kuepukika na nguvu hizi zimetumika kwa nia nzuri ili watanzania kuwa salama wanapotumia vyombo vya moto
Akitolea mfano kwa hali ya usalama barabarani kwa siku ya jana (juzi) nchi nzima kulikua na ajali nne ambazo zimesababisha vifi viwili na majeruhi nne,hivyo ni hatua nzuri.
 Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu aliyesimama akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani  hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
 Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bi. Mary Kessy akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani  hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
 ASP Deus Sokoni wa kwanza kulia akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani  hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Wizara ya Mambo ya Ndani  Bi. Marlin Komba  anayefuata ni Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu.
 Katibu Mkuu wa Shirikishi wa vyama vya Walemu nchini Bw. Felicina Mkude aliyesimama akiongea na baadhi ya wadau mbalimbali wa usalama barabarani  hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Mohammed Enterprises yashinda tuzo nne za ATE 2017

$
0
0
Kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group) imeshinda tuzo nne za Mwajiri Bora wa Mwaka 2017 (EYA) zinazotolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), katika hafla ya iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam. MeTL imeshinda tuzo hizo kupitia kampuni zake tanzu ambazo ni Mo Assurance Limited iliyoshinda kipengele cha Tuzo ya Kampuni Ndogo, 21st Century Holding Limited imeshinda nafasi ya pili ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Ndani na Star Oil Tanzania Limited imeshinda tuzo mbili, Tuzo ya Kampuni ya Kati na nafasi ya tatu ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Ndani. Ushindi huo wa tuzo nne, umeiwezesha MeTL Group kuwa moja ya kampuni nne ambazo zimeshinda tuzo nyingi za ATE 2017, na kuwa kampuni ya kizalendo ambayo imeshinda tuzo nyingi kuliko kampuni zingine ambazo zimeshiriki katika tuzo hizo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya Royal Soap, Jackline Mbaga, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya Star Oil Tanzania Limited , Ester Dotto, Meneja Mkuu wa Mo Assurance Limited, Kura Bonniface, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Mohammed Enterprises, Hassan Dewji, Meneja Mauzo na Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya 21st Century Holding Limited, David Mziray, Ofisa wa kitengo cha Rasilimali Watu wa Mohammed Enterprises, Jessica Julius, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya 21st Century Textiles, Godfrey Ndimbo na Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya 21st Century Food and Packaging, Anna Zongo wakiwa na tuzo nne ambazo wameshinda kwenye tuzo za ATE 2017.

Akizungumza kuhusu ushindi huo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MeTL Group, Hassan Dewji, alisema wamefurahishwa na ushindi huo, lakini pia unaonyesha jinsi gani kampuni inafanya vizuri katika soko la hapa nchini. "Tuna furaha kushiriki kwenye tuzo za ATE 2017 na tuna furaha kushinda tuzo nne, naamini tumekuwa moja ya kampuni tano ambazo zimeshinda tuzo nyingi. Nafikiri sisi ni moja ya kampuni kubwa nchini na tunaendelea kukua na kugusa maisha ya watu wengi kila siku, ushindi kama huu utuwezesha kuongeza juhudi zaidi," alisema Dewji.

ATE YATOA TUZO KWA MWAJIRI BORA WA MWAKA 2017

NAISINYAI YANYAKUA UBINGWA WA TAKUKURU SIMANJIRO

$
0
0
Na Woinde Shizza,Simanjiro.

Timu ya jamii ya wafugaji wa Naisinyai S. C ya Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imeshinda ngao ya maadili iliyoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kuifunga Mirerani SC kwa penalti 6-5.

Katika mchezo huo wa fainali uliochezwa juzi kwenye uwanja wa barafu mji mdogo wa Mirerani, mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Zuwena Omary. Hadi dakika 90 ya mchezo ulipomalizika timu hizo zilikuwa hazijafungana na walipopigiana penalti tano kwa tano hakukuwa na mshindi ndipo wakapigiana penalti moja kwa moja na Naisinyai ikashinda. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi ngao hiyo ya maadili kwa timu ya Naisinyai,Katibu Tawala Omary alisema jamii inapaswa kupiga vita matumizi ya vitendo vya rushwa kwa kila sehemu. Alisema jamii inapaswa kuzingatia hilo kupitia kauli mbiu ya wajibika, piga vita rushwa, zingatia maadili, haki za binadamu na utawala bora kuelekea uchumi wa kati. 

"Tupige vita rushwa kila mahali, kuanzia michezo ni, makazini, polisi, hospitalini, mahakamani na kila eneo ukiona rushwa inatumika toeni taarifa," alisema Omary. Mkuu wa Takukuru wilaya ya Simanjiro Mashauri Elisante alisema mashindano hayo yalishirikisha timu nne za Naisinyai SC, Mirerani SC, Veterani Mirerani za Simanjiro na Tanzanite FC ya wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. 

Alisema lengo la mashindano hayo ni maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu kitaifa na kupiga vita vitendo vya rushwa. Mwenyekiti wa Kijiji cha Naisinyai, Taiko Laizer alisema hii ni mara ya pili kwa mwaka huu timu hiyo kubeba ubingwa wa soka kwani awali walishinda kombe la mbunge wa jimbo la Simanjiro James Ole Millya. 
Laizer alisema siri ya ushindi mara mbili kwa mwaka mmoja kwenye timu hiyo ni kuzingatia mazoezi, nidhamu na ushirikiano wa uongozi na wananchi kwa ujumla. 
Mwenyekiti wa Kijiji cha Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Taiko Laizer akimbeba golikipa wa Naisinyai SC Joseph John baada ya kunyakua ngao ya Takukuru kwa kuifunga Mirerani SC kwa penalti 6-5
Mwenyekiti wa Kijiji cha Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Taiko Laizer akimbeba golikipa wa Naisinyai SC Joseph John baada ya kunyakua ngao ya Takukuru kwa kuifunga Mirerani SC kwa penalti 6-5

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT MAGUFUGULI AFUNGUA MKUTANO WA JUMUIYA YA WAZAZI MJINI DODOMA LEO

$
0
0

 Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017. 
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mhe. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mhe. Maalim Seif wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
 Wajumbe wakimshangilia Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Generali John Julius Mbungo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kaongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi aliyemaliza muda wake Alhaj Abdallah Majura Bulembo (kushoto) na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wengine baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Ndg. Kheri James baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
Wake wa viongozi kutoka kushoto Mama Janeth Magufuli, Mama Maria Nyerere, Mama Mary Majaliwa na Mama Bulembo wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmana Kinana akiwa na Mama Maria Nyerere muda mfupi kabla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia zawadi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi aliyemaliza muda wake Alhaj Abdallah Majura Bulembo wakati wa ufunguzi wa  Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.

PICHA NA IKULU

ONE STOP CENTRE YAWATAKA WADAU KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WATOTO

$
0
0
Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Edina Sanga (wa pili kushoto) akiwa na Afisa Polisi Kutoka dawati la Jinsia Christina Onyango na wadau mbalimbali wa masuala ya ukatili wa kijinsia.
 
Katika kusaidia kupinga ukatili wa kijinsia, kituo cha usuluhishi( Crisis Resolving Centre- CRC) kimejizatiti katika kutetea haki za binadamu kwa kulinda haki na ustawi wa watoto na wanawake.

Kituo hicho kilichoanzishwa 2007 kikiwa na mlengo wa utoaji huduma ya msaada wa kisheria  na ushauri nasaha kwa jamii.

Akizungumzia kazi zinazofanywa na CRC, Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi CRC Gladness Munuo amesema kuwa mnano Novemba 14 hafi 16 kimeweza kutoa ya huduma ya pamoja  kwa wahanga wa wa ukatili wa kijinsia  ijulikanayo kama One Stop Centre ikiwa inawalenga wakina mama na watoto ambao ndio waathirika wakubwa wa ukatili wa kijinsia.
Gladness amesema katika huduma ya pamoja na One Stop Centre  waliweza kutoa huduma kwa wateja 25 waliotembelea  kituo kwa kuhitaji msaada wakisheria na ushauri nasaha  ambapo wanawake walikuwa 22, wanaume 2 na mtoto mmoja.

Katika kesi hizo kesi mbili ziliweza kuhamishwa kutoka kituoni ambazo ni mgogoro wa ardhi na nyingine ilihusu kesi ya mauaji ambapo iliwezw kuhamishiwa polisi.

Ameelezea kuwa, katika usulihishi wa kifamilia uliweza kufanyika kwa wateja wanne na mashauri mawili ndio yaliyofanikiwa na nyingine ilikuwa ni matunzo ya mtoto.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KESI YA WEMA SEPETU KUENDELEA KUSIKILIZWA MWAKANI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006 na msanii maarufu wa Filamu nchini,  Wema Sepetu  itaendelea kusikilizwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka Januari mwaka kesho.

Kesi hiyo iliyoko katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo ilipaswa kuendelea kusikilizwa  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo Wakili wa Serikali, Costantine Kakula alieleza kuwa wapo tayari kwa ajili ya kuendelea na ushahidi na wana mashahidi wawili.

Hata hivyo wakili wa utetezi, Devotha Kianga aliyekuwa akimuwakilisha wakili Peter Kibatala aliomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine
kwa kuwa wakili Kibatala  ambaye anamtetea, wema na wenzake wawili, yuko Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kwenye kesi namba 85 ya mwaka 2016.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 10, 2018.

Washtakiwa wengine wanaoshtakiwa pamoja na Wema, ni Angelina Msigwa  na Matrida Seleman Abbas. Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Inadaiwa  kuwa  Februari 4, 2017 katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio  washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februani Mosi, 2017 katika  eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam,  alitumia dawa za kulevya  aina ya Bangi.

Wema ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda wakituhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa Februari 3, 2017, Wema alijipeleka mwenyewe katika Kituo cha Polisi Kati ambapo alikamatwa.

DK MGALULA ASHAURI WATANZANIA KUWA NA UZALENDO KWA NCHI YAO

$
0
0
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza vifaa Tiba cha Msagara, Dk.Ibrahim Mgalula akizungumza na Michuzi TV kuhusu jitihaza wanazofanya kutafuta ufumbuzi wa changamoto za uhaba wa vifaa tiba nchini huku akionesha baadhi ya aina za bidhaa wanazozalishwa kiwandani hapo kilichopo Mwananyamala kwa Kopa jijini Dar es Salaam.

Na Said Mwishehe wa Blogu ya Jamii
WATANZANIA wameshauriwa kuwa na uzalendo wa nchi yao kwa kutafuta suluhu ya ufumbuzi wa changamoto zilizopo nchini huku wakihimizwa pia kuunga mkono jitihada za Rais Rais, Dk. John Magufuli katika kufanikisha ujenzi wa viwanda nchini.

Hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza vifaa Tiba cha Msagara kilichopo Mwananyamala kwa Kopa jijini Dar es Salaam Dk.Ibrahim Mgalula wakati akielezea jitihaza za kiwanda chake kusaidia kutafuta ufumbuzi wa changamoto za uhaba wa vifaa tiba.

Amesema kuwa kitaaluma yeye ni daktari wa magonjwa ya binadamu lakini aliamua kutumia nafasi yake kufanya utafiti maeneo mbalimbali nchini hasa ya upatikanaji wa vifaa tiba na kubaini kuna tatizo la ukosefu wa vifaa hivyo, hivyo katika kutafuta ufumbuzi wake waliamua kuanzisha kiwanda hicho.

Dk. Mgalula amesema anatambua mchango wa viwanda vya ndani katika kuimarisha uchumi wa nchini  hivyo wamedhamiria kuunga mkono juhudi za Rais katika sekta ya viwanda kwani mpango wao ni kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza vifaa tiba Bagamoyo, mkoani Pwani.

"Nchi zote ambazo zimepiga hatua katika mambo mbalimbali zimefika hapo kwasababu tu ya kutanguliza uzalendo kwa nchi yao. Badala ya kuuliza nchi imefanya nini kwa ajili ya wananchi wake , ni wakati wa sisi wananchi kujiuliza tumeifanyia nini nchi yetu,"anasema.

Kuhusu vifaa tiba ambavyo wanadhalisha kwenye kwanda chao anasema wanafarajika kuona Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto na Serikali kwa ujumla kutambua uwepo wao na vifaa tiba na hasa magozi yanayotumika kwenye huduma za upasuaji.

Amesema vifaa vita ambavyo vinatengenezwa kwenye kampuni yao lengo lake zaidi ni kumsaidia Mtanzania ambaye anatumia gharama kubwa katika huduma za afya, hivyo wao wameamua kuuza vifaa tiba kwa gharama nafuu zaidi lakini katika ubora wa hali ya juu ambao umethibitisha Shirika la Viwango Tanzania(TBS) na Shirika la Afya Duniani(HWO).

Kuhusu utendaji kazi wa Rais Magufuli, Dk. Mgalula amesema kuwa Rais anafanya kazi wakati anaanza hakuwa anamuelewa lakini sasa  ameanza kumuelewa na anamuunga mkono kwa asilimia 100 na kuomba Watanzania wote nao kumuunga mkono ili afanikishe malengo yake ya kulitumikia Taifa.

Ametoa ombi kwa Serikali kuisaidia kiwanda hicho katika kufikia malengo yake na kubwa ambalo wanalihitaji ni kuondolewa kwa ukiritimba ambao upo kwenye baadhi ya taasisi za umma kiasi cha kukwamisha jitihada za kwanda hicho.Ameongeza tatizo si soko kwani lipo la uhakika kutokana na mahitaji ila tatizo ni ukiritimba lakini anaamini Serikali ya Rais Magufuli itatafuta ufumbuzi wake.

TANESCO kuimarisha Sekta ya Umeme Nchini

$
0
0
Shirika la Umeme Nchini TANESCO, limesema kuwa linaendelea kuimarisha Mifumo na Miundombinu ya Uzalishaji, Usafirishaji na Usambazaji umeme, lengo kuu kwa sasa likiwa ni Kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya umeme wa Uhakika na unaokidhi mahitaji ya kijamii na kimaendeleo kwa Wananchi ,wajasiriamali na wawekezaji mbalimbali wakiwemo wale wakubwa wa kati na hata wale wadogo

Hayo yamesemwa na Meneja mwandamizi Usambazaji Umeme wa TANESCO Mhandisi Raymond Sweya wakati wa Maonesho ya Pili ya ya bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Mw. J k. Nyerere Sabasaba Jijini Dar es salaam

''Tunaendelea kuimarisha na kupanua mifumo yetu ya usafirishaji na usambazji umeme pamoja na ile ya uzalishaji umeme ili kuhakikisha kuwa Sekta hii ndogo ya Nishati ya umeme inazidi kuimarika kwa kuwahudumia wateja wetu kwa huduma bora za umeme na zinazokidhi mahitaji'' alisema Mhandisi Sweya

Aliongeza kuwa mbali na utoaji wa huduma za umeme wa uhakika lakini TANESCO imedhamiria kutoa huduma hizo kwa bei nafuu itakayowezesha kupunguza gharama za uzalishaji na hivyo kuwezesha hata punguzo bei ya bidhaa husika na zitakazoweza kukidhi ushindani wa kibiashara katika soko la ndani na nje ya Nchi

Katika maonesho hayo yalishoshirikisha washiriki zaidi ya 500, TANESCO ilishiriki kama mdau Muhimu na wa karibu katika uendelezaji wa sekta nzima ya ujenzi na uendelezaji wa viwanda Nchini. 

Uwepo wa Umeme wa kutosha Nchini ni miongoni mwa vivutio vikubwa vinavyotarajiwa kuvutia uwekezaji mkubwa, mdogo na wa kati katika sekta nzima ya Viwanda Nchini na hvyo kuongeza ustawi wa maendeleo ya Kijamii  na kiuchumi kwa kutoa ajira, kukuza Soko la bidhaa za ndani, mauzo ya nje ya nchi pamoja na Kukuza uchumi wa Nchi nzima kwa ujumla.

Mchakato wa kura ya Maoni Jimbo la Singida Kaskazini wafutwa

IGP SIRRO AONGEA NA WANANCHI ALIPOKUWA NJIANI AKITOKEA MKOANI TABORA KWENDA KIGOMA KATIKA ZIARA YAKE

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP, Simon Sirro akiwagawia mahindi wananchi baada ya kumaliza kusalimiana nao wakati akitokea mkoani Tabora kwenda mkoa wa Kigoma katika ziara ya kikazi.  Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP, Simon Sirro akisalimiana na wananchi wakati akitokea mkoani Tabora kuelekea mkoani kigoma katika ziara yake ya kikazi.  Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP, Simon Sirro akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Polisi baada ya kuwasili mkoani Kigoma akitokea mkoani Tabora alipokuwa na ziara ya kikazi ya siku mbili.  Picha na Jeshi la Polisi.

MAKAMU WA CHUO CHA IJA ASHINDA KUKU LUSHOTO KATIKA BONANZA

$
0
0
Nazael Mkumbo Mshindi wa kuku

Makamu Mkuu wa Chuo cha uongozi wa mahakama IJA, Fahamu Mutlya mwishoni mwa wiki alionesha uhodari wa kukimbia baada ya kufanukiwa kumkamata kuku katika bonanza kuadhimisha siku ya uhuru na kufunga mwaka wa 2017lililofanyika katika uwanja wa chuoni hapo.

Mtulya aliweza kuwashinda wengine waliokuwa kwenye kundi la wahadhiri baada ya kuchomoka kwa haraka na kisha kumdaka kuku huyo wakati kundi la uhasibu mshindi alikuwa Noel Njau wakati Barnaba john alishinda kundi la utawala.Mpira wa kikapu watumishi waliweza kuwafunga wanafunzi wa chuoni hapo magoli 12 -8 na mpira wa wavu watumishi walifungwa seti 3-2.

Mwenyekiti wa kamati ya Bonanza hilo,Daudi Hemba alisema lilifanyika kwa lengo la kuwaeka pamoja watumishi na wanafunzi katika kujenga afya zao huku wakitafakari kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo uhuru wa nchi hii.“Bonanza hili limefanyika kwa lengo la kuwaweka pamoja watumishi na wanafunzi lakini pia kujenga afya zao huku wakitafakari kuhusu uhuru”alisema Hemba.

Mkuu wa Chuo cha IJA,Paul Kihwelo aliwataka watumishi kujenga tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kuimarisha afya zao.

“Bila shaka mnafahamu kwamba anayeshiriki michezo si rahisi
kushambuliwa na magonjwa mbalimbali,na ndiyo maana tumeanzisha IJA joging club ambayo watumishi na wanafunzi wanashiriki kila jumamosi”alisema Kihwelo.Katika bonanza hilo pia lilifanyika zoezi la upimaji wa afya ambapo watu 25 waliojitokeza kupima virusi vya ukimiwi walionekana kutokuwa na maambukizi wakati waliopima kisukari (Blood Suger) walikuwa 30 ambao walionekana kuwa ya kawaida.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
Mr. Fahamu Mtulya Mshindi wa kuku (Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma

Airtel Yaleta ‘SMATIKA Na Yatosha Intaneti’ SMATIKA NA 1GB Siku Tatu Kwa 2000 Tu

$
0
0
‘SMATIKA NA 1GB Yatosha Intaneti inayokupa muda mrefu kwa gharama nafuu zaidi. 

Airtel Tananzania Mtandao bora kwa Smartphone yako imewapatia wateja wake uhuru zaidi kwa kuwaletea bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ maalum kwa watumiaji wa huduma za intaneti. Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Isack Nchuna wakati wa hafla ya kuzindua ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti, alisema “Airtel itaendelea kuleta huduma zenye ubora na ubunifu wa hali ya juu ili kuendelea kuwa sambamba na mahitaji ya wateja katika huduma za intaneti ambapo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa Airtel imejiwekea mikakati endelevu mingi ili kukidhi uhitajika na wateja wote”

“Tuaendelea kudhihirisha dhamira yetu ya kutoa suluhisho la mawasiliano kupitia uzinduzi wa ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ kwa kutoa huduma nafuu ya Intaneti kwa watumiaji wote nchini huku tukiweka kipaumbele zaidi katika ubora wa mtandao pamoja na kuwapatia wateja uhuru zaidi” aliongeza Nchunda 

“SMATIKA na Yatosha Intaneti’ ni zawadi ya awali kabisa tunayowapatia watumiaji wa Airtel katika msimu huu wa sikukuu, tunaamini kuwa ndani ya msimu huu wa sikukuu wateja wanauhitaji mkubwa sana wa intaneti katika kukamilisha shamrasharna wakiwa wanawasiliana na ndugu, jamaa na marafiki wakati wote!”

Akifafanua zaidi Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi Beatrice Singano alisema Bando za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zinatoa uhuru kwa wateja wote wa airtel kujichagulia bando la intaneti KABAMBE wakati wowote.“Mteja wa Airtel ataweza kunufaika na SMATIKA na Yatosha Intaneti kwa gharama nafuu ya hadi shilingi 200 na kujipatia MB 40, vilevlie mteja ataweza KUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu” alieleza Bi Singano

“kujiunga na ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ unatakiwa kupiga *149*99# kisha chagua 5 Yatosha Intanet vilevile unaweza kujiunga kupitia Airtel Money kwa kupiga *150*60# kisha chagua Yatosha Intanet”.

Airtel Tanzania imekuwa katika programu ya uboreshaji wa miundombinu ya mawasiliano yake ili kukamilisha lengo lake la kutoa mawasiliano bora na yenye uhakika kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya U900. Tayari Airtel imezindua maboresho ya mtandao wake kwa kutumia teknolojia hiyo ya U-900 kwenye mikoa ya Arusha, Dar es salaam, Dodoma, Morogoro na Mwanza huku ikiendelea kuwahakikishia wateja wake mawasiliano bora hasa katika maeneo ya nje na ndani ya majengo marefu au yenye uhitaji zaidi.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano – kulia akiongea jana wakati wa uzinduzi wa bando za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ mpya ambapo mteja wa Airtel itamuwezesha mteja wa Airtel KUSMATIKA NA GB 1 ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda.
Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda – kushoto akiongea jana wakati wa uzinduzi wa bando za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ mpya ambapo mteja wa Airtel itamuwezesha mteja wa Airtel KUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili. Kushoto ni Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano.
Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda na Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano wakionyesha bango baada ya kuzindua bando za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ mpya ambapo mteja wa Airtel itamuwezesha mteja wa Airtel KUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images