Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WAPUNGUA HADI ASILIMIA 4.4

$
0
0
Na Emmanuel Ghula
Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Novemba, 2017 umepungua hadi kufikia asilimia 4.4 kutoka asilimia 5.1 mwezi Oktoba, 2017. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo amesema kupungua kwa mfumuko wa bei kumechangiwa na kupungua kwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma mbalimabli kwa mwezi Novemba, 2017.

“Mfumuko wa Bei wa mwezi Novemba, 2017 umepungua hadi kufikia asilimia 4.4 kutoka asilimia 5.1 kwa mwezi uliopita wa Octoba, 2017. Hii imechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula kama vile nyama ya ngombe ambayo imepungua kwa asilimia 5.4, samaki wabichi kwa asilimia 22.2, mbogamboga kwa asilimia 3.9, viazi mviringo kwa asilimia 14.0, mihogo mibichi kwa asilimia 24.8 na viazi vitamu kwa asilimia 13.4,” amesema Kwesigabo.

Amesema fahirisi za bei zimeongezeka hadi 108.94 mwezi Novemba, 2017 kutoka 108.41 mwezi Oktoba, 2017.

Kwesigabo amesema mfumuko wa bei nchini Tanzania una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo nchini Kenya Mfumuko wa Bei wa mwezi Novemba, 2017 umepungua hadi asilimia 4.73 kutoka asilimia 5.72 mwezi Oktoba, 2017 na nchini Uganda umepungua hadi asilimia 4.0 mwezi Novemba, 2017 kutoka asilimia 4.8 mwezi Oktoba, 2017. 

Amesema  bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na mafuta ya taa yaliyoongezeka kwa asilimia 4.6, mafuta ya dizeli kwa asilimia 2.0 na mafuta ya petrol kwa asilimia 2.8. 

Amesema uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Shilingi 91 na senti 79 mwezi Novemba, 2017 ikilinganishwa na Shilingi 92 na senti 25 ilivyokuwa mwezi Oktoba, 2017.
 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati akitangaza mfumuko wa bei wa Taifa wa mwezi Novemba, 2017.
Baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki katika mkutano wa kutangazwa kwa mfumuko wa bei wa Taifa leo jijini Dar es Salaam katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA)



DK SHEIN AWASILI MKOANI DODOMA KUHUDHURIA SHEREHE ZA UHURU WA TANZANIA BARA KESHO.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma na kusalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za Miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara zitakazofanyika katika uwanja wa Jamuhuri leo.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu wa UVCCM,  Shaka Hamdu Shaka alipowasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma kuhudhuria sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara zinazofanyika katika Uwanja wa Jamuhuri.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoani Dodoma alipowasili katika uwanja wa ndege kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara kesho katika viwanja vya Jamuhuri Dodoma.(Picha na Othman Maulid)  

SALAMU ZA MIAKA 56 YA UHURU KUTOKA KWA KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. A. P. Makakala ametoa salaam za Heri ya Sikukuu ya Uhuru wa Tanzania bara kwa Watanzania alipokuwa akiwaaga watumishi wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu akielekea Mkoani Dodoma kuhudhuria maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania bara.

Akizungumza Ofisini kwake Kamishna huyo amewataka Watanzania kudumisha uzalendo kwa kulinda Rasilimali, Ulinzi na Usalama wa nchi kwa faida ya kizazi kilichopo na kijacho. Hii ikiwa ndio njia pekee ya kuwaenzi waasisi wa Taifa letu.

“Uraia wetu una umuhimu wa kipekee kwani umebaki kuwa ndio msingi na utambulisho wetu unaotaunganisha wananchi wote bila ya ubaguzi ukilinganisha na utambulisho mwingine kama ukabila au dini na ndio utambulisho wetu kimataifa.Taifa lolote huru liwe kubwa au dogo haliwezi kukamilika bila ya kuwa na raia wake, ndiyo maana miaka 56 ya Uhuru wetu tunajitambua na kujivunia kuwa Watanzania” Alisema Kamishna Jenerali wa Uhamiaji.


Kwa msingi huo suala la kutambua nani ni raia na nani ni mgeni litabakia kuwa lengo kuu la Idara, kwakuwa raia ndiyo wanaotakiwa kunufaika na Rasilimali za nchi na Haki zinazotolewa na nchi kwa raia wake.

Pamoja na haki hizo za Kikatiba na za asili, lakini pia ni raia hao wenye wajibu wa kulinda Taifa lao dhidi ya uvamizi wowote na rasilimali za  Taifa kama zilivyopiganiwa na Mwasisi na Baba wa Taifa letu Hayati Mwl Julius K. Nyerere na kuongeza kuwa jukumu la ulinzi na usalama wa nchi ni la wananchi wote na hasa wazalendo.

Ni vyema kufahamu kuwa Uraia wetu ndio Utanzania wetu hivyo basi hatuna budi kuadhimisha siku hii adhimu tukiwa na ndoto na matarajio ya kuijenga Tanzania mpya ya Viwanda.

Madabida na wenzake wapelekwa rumande hadi Decemba 15

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imetupilia mbali hoja za mawakili  wa utetezi na kuuamuru upande wa jamhuri kuhakikisha tarehe ya kutajwa kwa shauri hilo wawe wameshawasilisha taarifa za kesi Mahakama Kuu ya Uhujumu Uchumi au wawasilishe kibali cha DPP kuipa mamlaka mahakama ya Kisutu kusikiliza kesi hiyo ili taratibu za dhamana zifanyike.

Kufuatia uamuzi huo aliyekuwa mwenyekiti wa  CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na wenzake watano wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, wamepelekwa gerezani kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Uamuzi huo uliotolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Victoria Nongwa umetokana na hoja zilizowasilishwa juzi na mawakili wa utetezi wakiongozwa na Dennis Msafiri kwamba mahakama hiyo  ina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi ambalo linahusisha shilingi milioni 148.

Hata hivyo, mawakili wa serikali Pius Hilla na Shadrack Kimaro walipinga hoja hiyo na kudai mahakama haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa kuwa linasikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi na DPP haijaipa kibali cha kuisikiliza.
Hakimu Victoria alisema shitaka la sita linalowakabili washtakiwa ni la uhujumu uchumi na tatizo lililoko ni wakati gani DPP anaweza kuwasilisha kibali cha kuipa mamlaka mahakama.
Alisema katika hilo sheria ipo kimya na kwamba washitakiwa hao walifikishwa mahakamani 2014  na kesi ilikuwa na kibali cha DPP na wameweza kuhudhuria kesi hadi Desemba 6, mwaka huu, ambapo DPP aliamua kuiondoa kesi ikiwa tayari mashahidi saba wa upande wa jamhuri wameshatoa ushahidi wao huku watatu wakiwemo mahakamani hapo kwa ajili ya kutoa ushahidi.
Hakimu Nongwa amesema siku hiyo, washitakiwa hao walifunguliwa kesi ya uhujumu uchumi hivyo kama kweli upande wa jamhuri una nia ya kutenda haki na haki ionekane imetendeka ni vema shauri hilo lianze kusikilizwa.
"Tunapokuja tarehe nyingine muwe mmefaili taarifa Mahakama Kuu ya Uhujumu Uchumi au mlete kibali cha DPP au muondoe mashtaka" alisisitiza Hakimu Nongwa.
Hakimu Victoria alitupilia mbali hoja za upande wa utetezi na kusema wanasubiri kibali cha DPP ili taratibu za dhamana ziendelee au wawasilishe taarifa Mahakama Kuu.
Kesi hiyo itatajwa tena, Desemba 15, mwaka huu, washtakiwa wamepelekwa mahabusu.
Madabida na wenzake waliposomewa mashitaka Desemba 6, mwaka huu , mbele ya Hakimu Victoria, muda mfupi baada ya kufutiwa kesi ya awali hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi.
Washtakiwa wote wanakabiliwa na mashitaka sita ya kula njama,  kusambaza dawa bandia za kufubaza virusi vya ukimwi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuisababishia MSD hasara ya milioni 148.
Mbali na Madabida wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Seif Shamte ambaye ni mkurugenzi  wa uendeshaji,  Simon Msoffe (meneja masoko) na  Fatma Shango (mhasibu msaidizi) wa Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd.

Pia wamo ni Sadick Materu na Evans Mwemezi ambao ni maofisa wa Bohari Kuu ya Dawa. 

HATUA YA AWALI YA MABORESHO YA RELI YA KUROKA KOROGWE MPAKA ARUSHA YAENDELEA

$
0
0
Mafundi wakiendelea na Maboresho ya Reli ya kutoka Korogwe, Mombo, Moshi mpaka Arusha katika eneo la Stesheni ya Mombo ikiwa ni kazi ya awali ya kumalizia maeneo yaliyokuwa wazi kutokana na mataluma ya reli hiyo na viungashio kupotea baada ya kung'olewa na watu wasiojulikana.
 Kazi ikiendelea kwa umoja.

Naibu Waziri Nditiye atoa siku 14 kwa Tipper kuunganisha bomba kwa TPA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Ashasta Nditye, ametoa siku 14 kuhakikisha bomba la mafuta la Kimataifa linalosambaza mafuta (TIPPER), liwe limeunganishwa kwenye mfumo unaodhibitiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili serikali iweze kupata mapato sahihi.

Kutokana na bomba la tipper kuunganishwa katika bandari kumesababisha serikali kupata mapato kwa kampuni hiyo kujisimamia yenyewe.

Akizungumza katika ziara ya kikazi aliyoifanya bandarini hapo jana,  Nditye amesema, TPA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na EWURA wafanye uchunguzi wa haraka kufahamu upotevu wa mapato ya serikali yaliyotokana na Tipper kujiunganishia mafuta kutoka kwenye meli bila kupitia katika kituo cha Kurasini Oil Jet (KOJ).

Amesema Tipper  wamekiuka maagizo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaaliwa yaliyolewa Februari mwaka jana  ya kutaka waunganishe bomba lao katika mfumo wa TPA ili kufahamu kiwango cha mafuta wanayoyachukua.

" Wizi wa waziwazi  tangu Februari mwaka jana alipoagiza Waziri  Mkuu  hadi leo TIPPER mmeshindwa kuunganisha bomba lenu hali inayochangia mapato ya Serikali kuzidi kupotea," alisema Nditye.

Amesema TIPPER waliagizwa na waziri ndani ya mwezi.mmoja wawe wamejiunga katika.mfumo huo lakini cha ajabu maaagizo yamekiukwa hali inayoashiria bado kuna ujanja unaendelea.

Amesema haiwezekani TIPPER wakajiunganisha wenyewe halafu wakajisimamia wao.kufahamu kiwango cha mafuta ya dizeli na ya kula wanayotumia.

Aliagiza pia TPA iimarishe ulinzi kwa mtoa taarifa za upotevu wa mafuta hayo na endapo atapata madhara Serikali.itachukua hatua.
 Naibu  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Ashasta Nditye akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) katika ziara yake alipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini  (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko  akitoa taarifa za utendaji wa mamlaka hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Ashasta Nditiye (Kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea mamlaka ya Bandari jijini Dar es Salaam.
 Naibu  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Ashasta Nditiye akizungumza katika ujenzi wa scanner ya ukaguzi katika bandari ya Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TANZIA: ROSE FANUEL MARO AFARIKI DUNIA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Familia ya Dkt. Fanuel Maro na  Bibi Violet Maro ya Upanga Mashariki jijini Dar es salaam  inasikitika kutangaza kifo cha binti yao mpendwa Rose Fanuel Maro kilichotokea jana Alhamisi Desemba 7, 2017 katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam.

Habari ziwafikie ndugu, jamaa, majirani na marafiki popote pale walipo.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwao Mtaa wa Longido, Upanga Mashariki, jijini Dar es salaam.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa
Jina lake na lihimidiwe - AMINA

HUDUMA YA USAFIRI WA APP YA TAXIFY YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Taxify, App ya huduma ya usafiri inayokuwa kwa kasi barani Ulaya na Afrika, leo imezinduliwa jijini Dar es Salaaam, huku mamia ya madereva wakiwa wamejiorodhesha ili kutoa huduma katika sehemu mbalimbali za jiji.

Katika kusherehekea uzinduzi wa huduma hiyo mpya, Taxify imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja watakaotumia huduma yao kuanzia tarehe 08 Desemba saa tatu asubuhi. Gharama kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo kwa fedha ya Shilingi ya Kitanzania; Sh 600, Sh300 kwa kila kilometa moja. Sh 50 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 3000.

“Dar es Salaam ni jiji lenye soko kubwa na lenye faida kwa usafiri wa watu binafsi mijini na sehemu muhimu ya shughuli za kibiashara ambapo shida kubwa ya kutumia usafiri binafsi maeneo ya mjini hutokea.

Tunayofuraha kubwa kuzindua huduma hii hapa na tuna uhakika Taxify itasaidia kwa kiasi kikubwa kuchangia kwa ufanisi katika ushindani wenye afya na kuboresha ubora wa huduma huku tukitoa kutoa fursa kwa madereva kujipatia kipato kizuri,” alisema Shivachi Muleji, Meneja Maendeleo wa Kanda, Taxify.

Taxify inachukua asilimia 15 pekee ya mapato kutoka kwa madereva wake, ikiwa ni gharama ndogo zaidi ukilinganisha na washindani wetu wa kibiashara wanaochokua asilimia 25. Kamisheni ndogo ambayo inachukuliwa na Taxify inatufanya tuweze kupunguza gharama ya huduma kwa wateja wetu na kuhakikisha madereva wanapata kipato cha kukidhi mahitaji ya familia.
 Shivachi Muleji, Meneja Maendeleo wa Taxify Kanda ya Afrika Mashariki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa App hiyo leo jijini Dar es salaam. Taxify ni App inayotoa huduma ya Usafiri ambayo inakuwa kwa kasi barani Ulaya na Afrika. App hiyo mpya imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja watakaotumia huduma yao kuanzia tarehe 08 Desemba saa tatu asubuhi. Gharama kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo TZS; Sh 600, TZS 300 kwa kila kilometa moja. TZS 50 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 3000. Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Taxify Tanzania, Remmy Eseka.
 Shivachi Muleji, Meneja Maendeleo wa Taxify Afrika Mashariki (kulia) na Remmy Eseka, Meneja Uendeshaji wa Taxify Tanzania wakibonyeza vitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma ya Taxify leo jijini Dar es salaam. App hiyo mpya imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja watakaotumia huduma yao kuanzia tarehe 08 Desemba saa tatu asubuhi. Gharama kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo TZS; Sh 600, TZS 300 kwa kila kilometa moja. TZS 50 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 3000.
 Nyota wa filamu za bongo, Wema Sepetu (katikati) akijumuika pamoja na Meneja Masoko wa Taxify Afrika Mashariki, Lorreen Ajiambo (kulia) na Meneja Uendeshaji wa Taxify nchini Tanzania, Remmy Eseka kuzindua App mpya ya Taxify inayotoa huduma ya usafiri leo jijini Dar es salaam. App hiyo mpya imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja watakaotumia huduma yao kuanzia tarehe 08 Desemba saa tatu asubuhi. Gharama kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo TZS; Sh 600, TZS 300 kwa kila kilometa moja. TZS 50 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 3000.
(Kutokea kushoto) Maafisa wa Taxify, Shivachi Muleji Meneja Maendeleo wa Taxify Kanda ya Afrika Mashariki, Remmy Eseka Meneja Uendeshaji wa Taxify nchini Tanzania na Meneja Masoko wa Taxify Afrika Mashariki, Lorreen Ajiambo kwa pamoja wakimuonyesha Nyota wa filamu za kibongo Wema Sepetu jinsi App hiyo inavyofanya kazi katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. App hiyo mpya imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja watakaotumia huduma yao kuanzia tarehe 08 Desemba saa tatu asubuhi. Gharama kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo TZS; Sh 600, TZS 300 kwa kila kilometa moja. TZS 50 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 3000.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAONGOZA NDEGE WAASWA KUTUMIA TAALUMA KWA MAENDELEO YA KUKUZA UCHUMI WA NCHI

$
0
0
Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamkala ya Usafiri wa Anga (TCAA), Valley Chamuluyu amesema kuwa waongoza ndege wameaswa  kutumia taaluma zao katika maendeleo ya taifa.

Chamuluyu ameyasema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa Chama cha Waongoza Ndege uliofanyika katika ukumbi wa mamlaka wa TCAA leo jijini Dar es Salaam, amesema TCAA itaendelea kutoa ushirikiano kwa chama cha waongoza ndege katika usimamizi wa usafiri wa anga.

Amesema kuwa waongoza ndege ni watu muhimu katika maendeleo ya taifa ambapo kazi hiyo ndiyo wanafanya usalama wa usafiri wa ndege na taifa kupata uchumi.

Nae Rais wa Chama cha Waongoza Ndege nchini (TATCA), John Msagga amesema kuwa mkutano huo watajadili mada mbalimbali ikiwemo maadili ya taaluma hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamkala ya Usafiri wa Anga (TCAA), Valley Chamuluyu akizungumza jambo wakati akifungua mkutano wa chama cha waongoza Ndege uliofanyika ukumbi wa Mamlaka ya TCAA jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Chama cha Wongoza Ndege nchini (TATCA), John Msagga akitoa taarifa za utekelezaji wa majukumu ya chama kwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Chama cha Waongoza Ndege Nchini Kenya (KATCA), Peter Oduer akizungumza juu ya ushirikiano wa chama cha waongoza Ndege Tanzania, leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Waongoza Ndege wakiwa katika mkutano.

WAZIRI JAFO AMSIMAMISHA KAZI MKURUNGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NKASI

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma juu ya kumsimamisha kazi Mkurungenzi wa Halmashauri ya wilya ya Nkasi bw. Julius Kaondo,picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii Dodoma. 




WAGONJWA 80 WENYE MATATIZO YA MOYO KUFANYIWA UPASUAJI WA KUFUNGUA NA BILA KUFUNGUA KIFUA KATIKA KAMBI YA MATIBABU YA MOYO INAYOTARAJIA KUANZA TAREHE 10/12/2017

$
0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Little Hearts ambao wanafadhiliwa na Taasisi ya Al- Murtada ya nchini Saudi Arabia wanatarajia kufanya matibabu ya moyo kwa wagonjwa 80 katika kambi maalum inayotarajia kuanza tarehe 10 – 14/12/2017.

Matibabu yatakayofanyika katika kambi hiyo ni ya upasuaji wa kufungua kifua na upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa watoto na watu wazima.

Leo tarehe 08/12/2017 madaktari bingwa wa Moyo wameanza kufanya uchunguzi kwa wagonjwa wote watakaofanyiwa upasuaji. Katika kambi hii ya siku tano tumepanga kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa 30 na upasuaji wa bila kufungua kifua kwa wagonjwa 50. Upasuaji wa kufungua kifua utafanyika zaidi kwa watoto na watu wazima watafanyiwa zaidi upasuaji wa bila kufungua kifua.

Kwa nama ya kipekee tunaishukuru sana Serikali kupitia Balozi wetu wa nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza kwa kutoa kibali cha kuingia nchini (Visa) bila malipo kwa wataalamu wetu hawa ambao wamekuja nchini kutoa matibabu ya moyo bure kwa wagonjwa wetu.

Kama mnavyofahamu matibabu ya moyo ni ya gharama hivyo basi tunaendelea kuwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa taifa wa bima ya afya ambao utawasaidia kulipa gharama za matibabu pindi watakapougua na kuhitaji kupata matibabu.

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza ( wa pili kushoto) pamoja na Madaktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto wa JKCI na Taasisi ya Little Hearts ya nchini Saudi Arabia. Mhe. Balozi Mgaza alitembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi ya upasuaji wa Moyo kwa watoto na watu wazima inayotarajia kuanza siku ya jumapili tarehe 10/12/2017.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani na Ali Al-Akhfash wa Taasisi ya Little Hearts ya nchini Saudi Arabia mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea JKCI kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi ya upasuaji wa Moyo kwa watoto na watu wazima inayotarajia kuanza siku ya jumapili tarehe 10/12/2017. Jumla ya wagonjwa 80 wanatarajia kufanyiwa upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua katika kambi hiyo.Picha na JKCI

MAKAMU WA RAIS MH.SAMIA SULUHU ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI KATIKA KILELE CHA SIKU YA MAADILI DESEMBA 10

$
0
0

 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,George Mkuchika akizungumza na waandishi wa habari juu ya Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasimi katika kilele cha siku ya maadili na haki za binadamu Desemba 10 mwaka huu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere mkoani Dodoma.kulia ni Kamishna wa Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold R.Nsekela. Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,George Mkuchika Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,George Mkuchika akitembelea mabanda mbalimbli katika viwanja vya Mwalimu Nyerere mkoani Dodoma.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii Dodoma.

MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO DECEMBA 9,2017

Wasanii wakiwa katika sherehe za Uhuru uwanja Jamhuri, mjini Dodoma

$
0
0
 Baadhi ya Wasanii wa kizazi kipya wanaounda kundi la Tanzania All Stars wakiwa katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara, yanayoendelea kufanyika hivi sasa kwenye uwanja Jamhuri, mjini Dodoma

KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA MSAADA WA KISHERIA

$
0
0
Mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria, Jaji Mkuu wa Tanzania , Mhe. Prof. Ibrahim Juma akiongea na wananchi kabla ya kufunga maadhimisho hayo katika viwanja vya shule ya sekondari ya Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria katika viwanja vya shule ya sekondari ya Dodoma leo .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akimshukuru Mgeni rasmi baada ya hotuba yake ya kufunga Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria.
Sehemu ya wahudhuriaji wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria kilichofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Dodoma tarehe 8/12/2017.

MAKAMU WA RAIS AFANYA UZINDUZI WA KAMPENI YA UZALENDO NA UTAIFA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Uzalendo na Utaifa uliofanyika jana usiku kwenye ukumbi wa mikutano Chimwaga mkoani Dodoma (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akitoa nasaha zake wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Uzalendo na Utaifa kwenye ukumbi wa mikutano Chimwaga, mkoani Dodoma.
 Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Kampeni ya Uzalendo na Utaifa Kwanza katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha Uzalendo na Utaifa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha muonekano wa kitabu cha Uzalendo na Utaifa mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya Uzalendo na Utaifa uliofanyika jana usiku kwenye ukumbi wa mikutano Chimwaga mkoani Dodoma.

BREAKING NYUZZZ: RAIS MAGUFULI ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 8157, BABU SEYA NA PAPII KOCHA PIA WAPITIWA NA MSAMAHA HUO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli leo ametoa msamaha kwa wafungwa 8157 ambapo wafungwa 1828 wataachiwa huru leo na 6329 watapunguziwa muda wao wa kifungo,  Pia ametoa msamaha kwa wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa na kuziagiza idara husika kuwatoa leo au kesho.

Kabla ya kutoa hukumu hiyo, Rais Dkt. Magufuli alisema kuwa Tanzania tuna wafungwa 39,000 mpaka jana, kati ya hao 37,000 ni wanaume na 2,000 ni wanawake huku Wanaosubiri kunyongwa wakiwa ni 522, wanaume 503, wanawake 19 tu.
Wakati huo huo Rais Dkt. Magufuli ametoa msamaha kwa Familia ya Nguza Viking (Babu Seya) na Johnson Nguza (Papii Kocha), ambao walihukumiwa kifungo cha maisha miaka kadhaa iliyopita, hivyo kuanzia leo familia hiyo iko huru.

Rais Dkt. Magufuli ametoa misamaha hiyo leo katika Sherehe za Maadhimishi ya Miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara, yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

TANESCO yakabidhiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu Kwa Mwaka 2016/2017

$
0
0
Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limekabidhiwa tuzo ya Utunzaji bora wa Mahesabu na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA), baada ya kufanya Vizuri kwenye kada hiyo katika Mwaka wa fedha 2016/2017.

Akipokea tuzo hiyo Afisa mkuu wa Masuala ya fedha wa TANESCO, Bi RENATA NDEGE ameishukuru Bodi ya Wahasibu na wakaguzi (NBAA), kwa kutambua Utendaji Kazi wa Shirika hilo la Ugavi wa umeme hapa Nchini.

" Napenda kuishukuru Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi kwa kuonesha imani katika Utendaji kazi wetu hususani kwenye Kada hii ya Masuala ya Utunzaji wa fedha, Sisi kama Idara tunaahidi Kuimarisha Utendaji Kazi wa TANESCO kwa Kushirikiana na NBAA" alisema Bi RENATA.

Baadhi ya Watumishi wa Idara ya Fedha katika Shirika la Umeme (TANESCO), wakionekana kufurahia tuzo waliyokabidhiwa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu, wameuambia Mtandao wa www.habari360.co.tz kwamba Wataendelea Kuchapa kazi Kwa weledi ili Kulisaidia Shirika Kutimiza Majukumu yake kwa Umma wa Watanzania.

Tuzo hiyo iliyokabidhiwa kwa Idara ya Fedha ya Shirika la Umeme (TANESCO), imeakisi Ubora wa Shirika hilo la Umma katika Utunzaji wa Mahesabu ya Fedha.

Afisa mkuu wa Masuala ya fedha wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Bi RENATA NDEGE akizungumza na Waandishi wa habari (Hawapo pichani), mara baada ya Kupokea tuzo ya utunzaji Bora wa Mahesabu kutoka Bodi ya wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA) katika mwaka wa fedha 2016/2017, Sherehe hizo Zimefanyika Jijini Dar es Saalam.
Afisa mkuu wa Masuala ya fedha wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Bi RENATA NDEGE, akionesha tuzo ya utunzaji Bora wa Mahesabu aliyokabidhiwa na Bodi ya wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA) kwa niaba ya Shirika la umeme, Baada kufanya vizuri kwenye kada ya utunzaji Mahesabu ya fedha kwa Mwaka 2016/2017.
Afisa mkuu wa Masuala ya fedha wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Bi RENATA NDEGE, akiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya watumishi katika Idara ya Uhasibu Mara baada ya Kukabidhiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu katika Mwaka wa fedha 2016/2017.
Watumishi katika Idara ya Uhasibu Kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), wakifurahia tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu BAada ya Kukabidhiwa na Bodi ya Wahasibu na wakaguzi wa Mahesabu (NBAA), Sherehe hizo zimefanyika Jijini Dar es Salaam.

Article 1

MICHUZI TV LIVE: SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 56 YA UHURU WA TANZANIA BARA, MJINI DODOMA LEO

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images