Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amefanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la 3 la abiria la kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) ambao unatarajia kukamilika ifikapo mwakani .
Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya ndege Juliuas Nyerere (JNIA) profesa Mbarawa amesema kuwa ujenzi huo ambao umefikia asilimia 67 kukamilika umegharimu takribani shilingi bilioni 560 katika ujenzi wake hadi sasa.
Aidha waziri huyo ametanabaisha kuwa jengo hilo la 3 la abiria litakuwa na uwezo wa kuhifadhi ndege kubwa 11 ambapo huchukua abiria mia 300 hadi 400 na ikiwa kwa ndege ndogo daraja c ni 21 nazo huchukua abiria 120-160 kwa kila moja.
Hata hivyo profesa Mbarawa amesema kuwa abiria wataondokana na changamoto ya kuchukua muda mrefu katika kitengo cha uhamiaji pale wanapolazimika kufanyiwa ukaguzi kutakuwa na mabadiliko ya kisasa ya wahudumu 24 watakaokuwa wanahudumia abiria hao kwa muda usiopungua dakia 20 ili kuondokana na usumbufu pamoja na kuboresha huduma hizo .
Vile vile Mkurugenzi wa viwanja vya ndege vya mikoa Richard Mayongela ( DRA) amesema kuwa abiria watapata huduma za viwango vya kimataifa ikiwa pia na kufungwa mitambo ya kisasa ili kudhibiti uhalifua utakojitokeza ikiwemo kusafirisha nyaraka za serikali bila kibali maalumu.
Mkurugenzi mayongela amemalizia kwa kusema kuwa kutakuwa na fursa za wafanya biashara mara baada ya jengo hilo kumalizika na kuwataka wawekezaji kuchangamkia fursa hiyo ikiwa ni mojawapo ya kuiingizia kipato mradi huo .
aziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la 3 la abiria Jijini Dar es Salaam katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Mkurugenzi wa viwanja vya ndege vya mikoa Richard Mayongela ( DRA) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wa hapa nchini kuhusu uwanja huo utakavyokuwa wa kisasa na huduma bora leo Jijini Dar es Salaam katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Wadau mbalimbali hapa nchini waliohudhuria mkutano huo wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la 3 la abiria Jijini Dar es Salaam katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua ujenzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la 3 la abiria Jijini Dar es Salaam katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiteta jambo na Mkurugenzi wa viwanja vya ndege vya mikoa Richard Mayongela ( DRA) Jijini Dar es Salaam katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).