Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live

RC RUVUMA ATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA NCHINI.

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa RUVUMA CHRISTINA MNDEME amewataka wafanya biashara wote nchini kuja mkoani ruvuma kununua mahindi,tamko la kutaka wafanya biashara kuja mkoani Ruvuma linakuja baada ya serikali ya awamu ya tano kufungua mipaka kwa ajili ya wafanyabiashara waweze kupeleka mahindi nje ya nchi

WANANCHI WA KIGAMBONI GEZAULOLE WAIOMBA SERIKALI KUWALIPA FIDIA YAO KUPISHA UJENZI SHIRIKI WA MPANGO MJI.

$
0
0
 Na David John

BAADHI ya wananchi wa Kigamboni Gezaulole Kata ya Somangila mtaa wa Mwela jijini Dar es Salaam, wameiomba serikali kulipa fidia kwa wananchi hao ambao walitakiwa kupisha ujenzi shiriki wa mpango Mji.

Wamesema kuwa ni muda mrefu sasa umepita hawajuwi mstakabali wa fidia hiyo nakudai ni vema serikali ikafanya haraka kuwafidia ili waondokane na hali ngumu wanazokutana nazo.

Akizungumza kwaniaba ya wezake mmoja wa waathirika na mchakato huo Marando Nyanda alisema wakati wanaambiwa wapishe tayari wao walikuwa na mazao mbalimbali ambapo Serikali walisema watafidia.

"Sisi kwa kutambua umuhimu wa mradi huu tulikubaliana na Serikali kwamba wangetufidia lakini cha ajabu hadi kufikia leo sisi baadhi ya wakazi wa maeneo haya hatujalipwa. "amesema Marando

Ameongeza kuwa mchakato huo ulikuwa shirikishi lakini hadi kufikia leo watu zaidi ya 160 hawajuwi mstakabali wa malipo yap na kudai nimiaka mitano imepita sasa.

Wananchi hao amesema hakuna asijuwa juu ya jambo hilo kuazia mkuu wa mkoa hadi mawaziri wenye dhamana wanajuwa huku wakimtaka Rais Magufuli kuingilia kati suala hilo ili wao wapate haki zao.

Akizungumzia jambo hilo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula alisema kuhusu jambo hilo wananchi hao wanatakiwa waende katika ofisi za halmashauri ya kigamboni.

Alisema kuwa kuhusu uboreshaji wa mpango mji katika halmashauri hiyo upo chini ya halmashauri hiyo ya kigamboni hivyo nivema wakafika huko au kuonana na Mkuu wa wilaya hiyo ili kupata ufumbuzi wa jambo hilo.
 
Marando nyanda mmoja wa wakazi wa Kigamboni Gazaulole ambaye anasotea fidia ya kupisha ujenzi shirikishi wa mpango mji katika eneo hilo picha na David John.  

NAIBU SPIKA DKT. TULIA ACKSON AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KAMATI YA MAMBO YA NJE KUTOKA BUNGE LA CHINA

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akizungumza na ugeni kutoka kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China ulioongozwa na Naibu Mkurugenzi wa kamati hiyo, Mheshimiwa CAO Weizhou (wa pili kulia) wengine ni wajumbe wa kamati hiyo, pale ugeni huo ulipomtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akimsikiliza Naibu Mkurugenzi wa kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China, Mheshimiwa CAO Weizhou (kulia) pale ugeni kutoka kamati hiyo ulipomtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimpatia zawadi Naibu Mkurugenzi wa kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China, Mheshimiwa CAO Weizhou (kushoto) pale ugeni kutoka kamati hiyo ulipomtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya Mambo ya Nje kutoka Bunge la China wakiongozwa na Mheshimiwa CAO Weizhou (kushoto waliokaa) pale ugeni kutoka kamati hiyo ulipomtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Uamuzi kesi ya Madabida kutolewa Kesho

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

Uamuzi kama Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inayo mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi Ama la, dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano  kutolewa kesho.

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa baada ya kumaliza kusikiliza hoja za upande wa jamhuri kufuatia mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa utetezi.

Wakili wa Serikali Shadrack Kimaro alidai kuwa hoja ya Mawakili wa utetezi kuwa mahakama ya Kisutu inamamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo kwa sababu ipo chini ya Sh 1 bilioni  siyo sahihi.

Amedai, ni dhahili kuwa makosa wanayoshtakiwa nayo washtakiwa ni ya uhujumu uchumi na mahakama pekee yenye mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo ni Mahakama Kuu Kitengo cha Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu mahakama ya Mafisadi.

Ameongeza, mahakama za chini kama Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo labda kuwepo na kibali kutoka kwa DPP kitakachoipa mahakama ya chini cha kulipa mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo.

Kufuatia hoja hiyo, Hakimu Kimaro aliiomba mahakama kutupilia mbali hoja za upande wa utetezi na kwamba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Wakili wa utetezi, Denis Msafiri akijibu hoja hiyo alidai, marekebisho ya sheria ya uhujumu uchumi ya 2016 yanaipa mahakama ya Kisutu mamlaka ya  moja kwa moja kuisikiliza kesi hiyo.

"Kosa lolote lililopo chini ya Sh 1 bilioni haliwezi kusikilizwa na Mahakama Kuu Kitengo cha Rushwa na Uhujumu Uchumi ni Mahakama za chini ikiwamo Mahakama ya Kisutu". Amedai msafiri.

Aidha amedai, kibali cha DPP cha kuipa mamlaka mahakama kusikiliza kesi kilipaswa kupelekwe mahakamani hapo pamoja na hati ya mashtaka.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Kesho kwa mahakama kutoa maamuzi, pia ameamuru washtakiwa wapelekwe polisi.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Pius Hilla aliomba washtakiwa wapelekwe magereza kwa sababu kuendelea kuwa mikononi mwa polisi kuna suala la gharama na polisi hawana fungu hilo pia watuhumiwa ambao wameishasomewa mashtaka hawaruhusiwi kukaa polisi zaidi ya siku Tatu.

 Wakili Nehemia NNkoko aliomba mahakama kusimamia amri yake kama ilivyoitoa na kuomba mahakama iendelee na oda yake ilivyoitoa jana.

Hakimu Nongwa alisema suala la gharama haliwezi kukwepeka pale Haki inapotafutwa na kuamuru washtakiwa wapelekwe polisi hadi Leo atakapotoa uamuzi kama mahakama hiyo ina mamlaka ama la.

Madabida na wenzake wanakabiliwa na mashtaka sita  ya uhujumu uchumi ikiwamo kusambaza dawa bandia za kufubaza virusi vya Ukimwi ' ARV’s ' na kusababisha hasara ya Sh 148 milioni.

Rais Dkt Magufuli Kuzindua Kampeni ya Utamaduni na Utaifa

VIDEO:NAIBU WAZIRI WA MAJI AWESO ASITISHA MALIPO YA MKANDARASI SONGEA

$
0
0
Naibu waziri wa maji na umwagiliaji JUMAA AWESO ameitaka mamlaka ya maji safi na taka wilaya ya songea kusitisha malipo ya mkandarasi anayejenge maradi wa maji wa LIULA MATIMIRA kusitisha malipo yake na kama amelipwa basi pesa zirudishwe mara moja.

UNGANA NA MCHUNGAJI DKT. HURUMA NKONE NA MWINJILISTI JOHANNES KATIKA SEMINA YA SIKU 3 ZA MATUMAINI

CTI WAZINDUA TUZO ZA VIWANDA KWA MWAKA 2017 LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Loedigar Tenga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa tuzo za The President's Manufacturer of the Year Awards 2017 kwa wanachama na wasio wanachama wa CTI na kuvitaka washiriki kujitokeza kuchukua fomu za ushiriki.



Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) limezindua tuzo za President's Manufacturer of the year awards 2017 (PMAYA) ikiwa ni mara ya 12 toka kuanzisha kwake mwaka 2005.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tuzo hizo za PMAYA kwa mwaka 2017, Mkurugenzi Mtendaji wa CTI Leodigar Tenga amesema kuwa tuzo hizi zinaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika kuelekea uchumi wa viwanda.

Tenga amesema kuwa tuzo hizi kwa mwaka huu zimezinduliwa mapema zaidi ili kuwapa fursa wenye viwanda kushiriki kwa wingi, kwani kuanzia mwaka 2016 tuzo za PMAYA zinajumuisha kwa wanachama na wasio wanachama wa CTI.


Akielezea tuzo zilizopita ambapo ziliweza kuleta hamasa kwa wamiliki mbalimbali wa Viwanda, Mkurugenzi Mtendaji Tenga amesema kwa mwaka 2017 anatarajia kuona namba ya washiriki ikizidi kuwa kubwa kutokana na kuruhusu pia wasio wanachama kuja kushiriki na kwa mara nyingine tena kutakuwa na tuzo ya ufanisi wa nishati.

"Kuanzia mwaka jana tumeamua kushirikisha wasio wanachama wa CTI ili kuweza kushiriki nasi katika tuzo hizi za PMAYA na hili ni jambo kubwa sana kwani tunaamini washiriki watakuwa wengi na kwa mwaka huu kutakuwa tena na tuzo ya ufanisi wa nishati, "amesema Tenga.

Kwa upande wa mdhamini mkuu wa tuzo hizo, Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa wateja kutoka benki ya CRDB Tully Mwambapa amesema mwaka huu watadhamini tuzo hizo kwa kiasi cha fedha dola za kimarekani 35,000 sawa na milioni 70 za kitanzania.

Tully amesema kuwa, benki yao imeweza kushirikiana na viwanda mbalimbali kwani benki yao inatoa mikopo kwa viwanda vidogo na vikubwa na ukiangalia kwa mwaka jana walitumia takribani bilioni 160.

Mkurugenzi Mkuu wa ISHARA Consultant Olive Mosha amesema kuwa viwanda vyote vikubwa na vidogo vinaruhusiwa kuja kushiriki katika tuzo hizo ambapo kampuni yao itasimamia kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa mashindano hayo.

Tuzo hizo zinazoratibiwa na CTI zimekuwa zinatoa mchango mkubwa sana kwa wamiliki wa viwanda kuweza kujitathmini kila mwaka kwa kuangalia wanapotakiwa kuboresha kuanzia kwenye uendeshaji wa kiwanda.
Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa wateja kutoka benki ya CRDB Tully Mwambapa akizungumza na waaandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa tuzo za The President's Manufacturer of the Year Awards 2017 wakiwa kama wadhamini wakuu wa tuzo hizo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania Leodigar Tenga.
Mkurugenzi Mkuu wa ISHARA Consultant Olive Mosha akielezea namna watakavyoweza kupata mshindi wa tuzo za The President's Manufacturer of the Year Awards 2017 na wakisisitiza washiriki kuchukua fomu mapema leo Jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wakisikiliza kwa makini.

MATUKIO KATIKA PICHA MASHINDANO YA MABUNGE YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI MECHI KATI YA BUNGE LA TANZANIA NA UGANDA UWANJA WA UHURU, JIJINI DAR

$
0
0
Wachezaji wa Timu ya Bunge la Tanzania katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mechi yao na Timu ya Uganda Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam Jioni ya leo.
Mchezaji wa Timu ya Bunge la Tanzania, Prof. Norman Sigalla akimtoka ,Mchezaji wa Timu ya Bunge la Uganda wakati wa mechi yao iliyochezwa Jioni Leo Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya Mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki yanaoendelea Jijini Dar es Salaam ambapo Uganda waliibuka kwa ushindi wa Magoli 2-1.
Mchezaji wa Timu ya Bunge la Tanzania Ridhiwan Kikwete (kushoto) akijiandaa kuwatoka Mabeki wa Timu ya Bunge la Uganda wakati wa mechi yao iliyochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam Jioni Leo ikiwa ni sehemu ya Mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki yanaoendelea Jijini Dar es Salaam ambapo Uganda waliibuka kwa ushindi wa Magoli 2-1.
Mchezaji wa Timu ya Bunge la Tanzania Omary Mgumba (katikati) akijiandaa kupiga Mpira mbele ya wachezaji wa Timu ya Bunge la Uganda wakati wa mechi yao iliyochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam Jioni Leo ikiwa ni sehemu ya Mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki yanaoendelea Jijini Dar es Salaam ambapo Uganda waliibuka kwa ushindi wa Magoli 2-1.
Mchezaji wa Timu ya Bunge la Tanzania Ally King (katikati) akimiliki Mpira mbele ya Wachezaji wa Timu ya Bunge la Uganda wakati wa mechi yao iliyochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam Jioni Leo ikiwa ni sehemu ya Mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki yanaoendelea Jijini Dar es Salaam ambapo Uganda waliibuka kwa ushindi wa Magoli 2-1.

KAMISHNA SURURU, AKAMILISHA ZIARA YAKE MKOA WA KASKAZINI UNGUJA KWA MAFANIKIO

$
0
0
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kulia), kipokea Salamu ya Heshima kutoka kwa Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Muhsin A. Muhsin akimkaribisha rasmi Kamishna, kutembelea Kituo cha Uhamiaji kilichopo Bandari ya Mkokotoni, Wilaya ya Kaskazini “A” jana tarehe 06 Disemba, 2017 wakati akiendelea na ziara ya kikazi Mkoani Humo.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, akiwaasa watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, kuzingatia Maadili ya kazi, Heshima na Uadilifu kuwa ndio nguzo kwa Utumishi uliotukuka. Pia alikemea vitendo vya Rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wasio waadilifu. Alitoa nasha hizo leo tarehe 07 Disemba, 2017 wakati akihitimisha ziara ya siku tatu Mkoani Humo. Kulia kwake ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Muhsin A. Muhsin na kushoto ni Afisa Utumishi, Mrakibu wa Uhamiaji, Ali J. Abdulkadir.
Sheha wa Shehia ya Mnarani Bwana Mdungi Sharifu Makemi (picha ya juu) na Sheha wa Shehia ya Nungwi – Banda Kuu Bwana Mohamed Khamis Haji, akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu na Maafisa alioambatana nao, eneo lenye changamoto kubwa wanazokabiliana nazo za Uingiaji wa watu wasiofata sheria katika Ukanda huo. Alipofanya ziara ya kikazi kwenye maeneo ya utendajikazi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja jana tarehe 06 Disemba, 2017.
Mkuu wa Bandari ya Mkokotoni, Bwana Ahmed Salim Said, akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zaznibar, Johari Masoud Sururu na Maafisa aliombatana nao, eneo linalotumiwa na baadhi ya Manahodha kushusha abiria kinyume na utaratibu wa Bandari hiyo, wakati alipofanya ziara ya kikazi kwenye maeneo ya utendaji kazi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja jana tarehe 06 Disemba, 2017.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kulia), akimsikiliza kwa makini Sheha wa Shehia ya Kilindi Bwana Omar Ali Mussa (wa pili kushoto), akitoa shukran zake kwa Uongozi wa Idara kwa ushirikiano mkubwa anaoupata toka kwa Askari wa Uhamiaji. Akisisitiza kauli hiyo Sheha alisema “Ziara yako Kamishna imethibitisha kauli yangu na umeonesha kwa vitendo jinsi ulivyojipanga kushirikiana na wananchi wa eneo letu kutatua changamoto za baadhi wageni wanaoishi hapa bila ya kufata utaratibu” aliyasema hayo jana wakati Kamishna akiendelea na ziara ya kikazi Mkoa wa Kaskazini Unguja

KILIMANJARO WACHEZEA KICHAPO TOKA KWA NDUGU ZAO ZANZIBAR HEROES

$
0
0
Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars Eliuas Maguli (jezi nyeupe) akiwania mpira na mchezaji wa Zanzibar Heroes katika mchezo wa pili wa michuano ya CECAFA Senior Challenge leo Jijini Nairobi na kumalizika kwa Zanzibar Heroes kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

Timu ya Tanzania Bara "Kilimanjaro Stars" kupoteza mchezo wao dhidi ya Zanzibar Heroes kwenye michuano ya Cecafa Senior Challenge inayoendelea nchini Kenya Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Ammy Ninje amesema kikosi chake bado kina nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi mbili zilizobaki.

Kilimanjaro Stars iliyopo katika kundi A imebaki na michezo dhidi ya Rwanda na wenyeji Kenya ambayo Kocha Ninje anaamini watashinda na kusogea hatua ya nusu fainali.

Akizungumzia Kilimanjaro kupoteza mchezo dhidi ya Zanzibar, Kocha Ninje amesema kipindi cha kwanza timu ilicheza vizuri kiasi cha kupata goli lililofungwa na nahodha Himid Mao, lakini kipindi cha pili wakaanza taratibu na kuwaruhusu Zanzibar kurudi mchezoni hali iliyopelekea ushindi wao.

Amesema makosa mawili yaliyofanyika ndio yamewaghalimu kupoteza lakini kimpira timu imecheza mchezo mzuri.
Beki wa Kilimanjaro Stars Boniface Maganga akiwa anapambana na beki wa Zanzibar Heroes Haji Mwinyi katika mchezo wa pili wa michuano ya CECAFA Senior Challenge leo Jijini Nairobi na kumalizika kwa Zanzibar Heroes kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

"kuangalia makosa ya mchezaji mmoja mmoja Nimewaambia Wachezaji wangu wasikate tamaa bado tuna nafasi ya kufanya vizuri katika mechi zetu mbili zilizobaki,” amesema Ninje.

Kwa matokeo hayo Kilimanjaro Stars inabakiwa na pointi 1 baada ya kucheza michezo miwili katika kundi hilo la A ikisaliwa na michezo dhidi ya Rwanda “Amavubi” na wenyeji Kenya ‘Harambee Stars’.
Beki wa Zanzibar Heroes akiwa anawania mpira na mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars Elius Maguli katika mchezo wa pili wa michuano ya CECAFA Senior Challenge leo Jijini Nairobi na kumalizika kwa Zanzibar Heroes kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA, WAZUNGUMZIA UJENZI WA MAHAKAMA KUU DODOMA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu ya Chamwino kuhusu ujenzi wa Mahakama Kuu mjini Dodoma leo Desemba 7, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo katika Ikulu ya Chamwino kuhusu ujenzi wa Mahakama Kuu mjini Dodoma leo Desemba 7, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu ya Chamwino kuhusu ujenzi wa Mahakama Kuu mjini Dodoma leo Desemba 7, 2017.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA TAIFA YA USAFI WA MAZINGIRA AWAMU YA PILI MKOANI DODOMA

$
0
0


​Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameagiza utekelezaji wa Kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira uwe ni ajenda ya kudumu ya kila ngazi ya Uongozi.

Makamu wa Rais ameyasema hay oleo wakati wa Uzinduzi wa Kamapeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira awamu ya Pili ukiofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe,mkoani Dodoma.

Makamu wa Rais alisema Serikali imejiwekea mikakati mbali mbali ya kupambana na maradhi ya kuambukiza ambapo usafi wa mazingira ni njia mojawapo ambapo katika awamu ya kwanza ya kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira ambapo jumla ya kaya 1,662,550 zilijengwa vyoo na shule 2,133 vilijengwa vyoo bora.

Katika awamu ya Pili iliyozinduliwa leo kaya 5,600,000 zinatarajiwa kuongeza idadi ya vyoo bora na shule za msingi 3,500 na sekondari 700 zitapata huduma ya vyoo bora na sehemu maalum ya kunawa mikono baada ya kutoka chooni.

“Wahenga walisema Samaki mkunje angali mbichi, methali hii inatukumbusha jukumu la kuwafundisha watoto wetu umuhimu wa usafi wa mazingira tangia wadogo wakiwa mashuleni”alisisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais alitoa Wito kwa Wanawake wote nchini kujifunga Kibwebwe na kujenga vyoo, alisema Wanawake wamekuwa na vikundi mbali mbali vya kusaidiana na kuwezeshana hivyo kwa kupitia vikundi hivyo wanaweza kufanikisha ujenzi wa vyoo bora majumbani.

Makamu wa Rais aliwapongeza Washindi wote wa Afya na Usafi wa Mazingira kwa mwaka 2016/17. Pia aliwashukuru wadau mbali mbali ambao wamechangia kwa namna moja au nyingine kufanikisha uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mbele ya mfano wa Choo bora mara baada ya kuzindua kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira awamu ya pili, iliyozinduliwa rasmi kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Chang'ombe mkoani Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipokea mfano wa funguo kwa ajili ya kumkabidhi Mgeni rasmi Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya ishara ya kuzinduliwa mfano wa Choo bora ndani ya uzinduzi wa kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira awamu ya pili, iliyozinduliwa rasmi kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Chang'ombe mkoani Dodoma. 

Mgeni Rasmi,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwenye moja ya banda lililokuwa likionesha baadhi ya vifaa vinavyotumika katika suala zima la usafi wa mazingira,alipopita kukagua mabanda mbalimbali yaliyokuwepo uwanjani hapo kabla ya uzinduzi wa kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira awamu ya pili, iliyozinduliwa rasmi kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Chang'ombe mkoani Dodoma.

Sehemu ya Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika uzinduzi huo mapema leo mkoani Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira awamu ya pili, iliyozinduliwa rasmi kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Chang'ombe mkoani Dodoma.
Sehemu ya zawadi mbalimbali walizokabidhiwa watu,taasisi na vikundi mbalimbali vilivyofanya vizuri katika suala zima usafi wa mazingira sambamba na vyoo bora,zawaidi hizo kama vile vyeti,piki piki pamoja na matrekta

Kikundi cha ngoma kikitumbuiza kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo.

UTT AMIS YATOA ELIMU YA MIFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA KWA WASHIRIKI WA SEMINA JIJINI MOROGORO

$
0
0
Maafisa wa UTT AMIS wakitoa elimu ya jinsi mifuko ya Uwekezaji wa pamoja inayosimamiwa na kampuni hiyo na kwamba ni suluhisho kubwa la maisha baada ya kustafu katika semina iliyoandaliwa na National Institute of Productivity (NIP) jijini Morogoro.

RAIS DKT. MAGUFULI KUZINDUA KAMPENI YA UTAMADUNI NA UTAIFA

$
0
0


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa kampeni ya Utamaduni na Utaifa yenye kaulimbiu ya "NCHI YANGU KWANZA" uzinduzi huo utafanywa na Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ijumaa Desemba 08, 2017 katika ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuanzia saa 9 mchana. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa kampeni ya Utamaduni na Utaifa yenye kaulimbiu ya "NCHI YANGU KWANZA" ambapo alisema dhumuni ya kampeni hii ni kuendelea kutengeneza Taifa ambalo linajali utamaduni, mila na desturi zake.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa kampeni ya Utamaduni na Utaifa yenye kaulimbiu ya "NCHI YANGU KWANZA" ambapo alisema kampeni hiyo itakuwa inafanyika kila mwaka na itakuwa ni sehemu ya kumbukumbu ya maadhimisho ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Nicholous William

PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO

JAFO ATANGAZA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2018

$
0
0
Angela Msimbira – OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amesema kati ya wanafunzi 662,035 waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi wanafunzi 650,862 sawa na asilimia 98.31 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza mwaka 2018

Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 Tanzania Bara kwenye kikao na waandishi wa habari leo katika ofisi za Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Jafo amesema kuwa idadi wa wanafunzi mwaka huu imeongezeka kwa wanafunzi 124,209 ambapo ni sawa na asilimia 23.58 ikilinganishwa na wanafunzi 526,653 waliochaguliwa awamu ya kwanza kuingia kidato cha kwanza mwaka 2016.

Amesema kuwa wanafunzi 1912 wenye uhitaji maalum (pupils with special needs) waliofaulu mitihani ya darasa la saba wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2018 kwenye shule za sekondari za Serikali.

Mhe. Jafo amefafanua kuwa wanafunzi 11,173 sawa na asilimia 1.69 ya waliofaulu hawakupata nafasi ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza ya uchaguzi kutokana na uhaba wa miundombinu ya elimu hususani vyumba vya madarasa kwenye baadhi ya Halmashauri ya Mikoa ya Lindi (170), Mbeya (3,092), Rukwa (4,091), Manyara (1,268), Katavi (976) na Simiyu (1,576).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na Waaandishi wa habari kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 katika ukumbi wa Mikutano wa Tamisemi Mjini Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo kwenye mkutano i kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 katika ukumbi wa Mikutano wa Tamisemi Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akifafanua jambo wakati akiongea na Waaandishi wa habari kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 katika ukumbi wa Mikutano wa Tamisemi Mjini Dodoma.


Waziri Prof. Mbarawa Awapa Hadi Feb 1, 2018 Wadaiwa JNIA

$
0
0
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa amewataka wadau wanaofanya shughuli mbalimbali zinazohusisha na kodi ya pango kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Julius Nyerere (JNIA), kuhakikisha ifikapo Februari 1, 2018 wawe wameshalipa madeni yao.

Prof. Mbarawa alisema leo wakati alipoongea na wadau hao kwenye ukumbi wa watu Mashuhuri wa JNIA-TBII, wakati walipozungumza nao kujadili masuala mbalimbali.

Alisema baadhi ya wadau wameshalipa madeni yao kati ya bil 10 zilizokuwa zinadaiwa na sasa zimesalia bil. 3.7 ambapo amewataka baada ya kumalizika kwa sherehe za Krismas na Mwaka Mpya wahakikishe wanakamilisja madeni yao.

“Hatutasita kumuondoa mtu yeyote atakayekuwa akiendelea kudaiwa kwani atakuwa hana sifa za kupangisha katika majengo haya ya viwanja vya ndege kwa kuanzia TBI na hapa TBII,” alisema Prof. Mbarawa.

Hatahivyo, aliyapongeza mashirika na ofisi ambazo zimekuwa zikilipa kwa wakati fedha za pango, ambapo uaminifu huo utawasaidia kupata nafasi katika jengo jipya la la tatu la abiria, ambalo litakuwa linauwezo wa kuhudumia abiria milioni sita (6) kwa mwaka.
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati mbele) akiwa katika chumba cha mikutano cha Kampuni ya ujenzi ya Kimataifa ya Uholanzi (BAM) linalojenga Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII) alipofanya ziara. (Wa kwanza kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela na (wa kulia) ni Balozi wa Uholanzi nchini, Jeroen Verheul.
Mkandarasi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Bw. Wolfgang Marschick (katikati kushoto) akitoa maelezo ya ujenzi huo leo. Wa pili kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanza nia (TAA), Bw. Richard Mayongela.
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akifurahia jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela wakati walipokuwa wakitembelea ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII). Nyuma ni Kaimu Mkurugenzi wa JNIA, Bw. Johannes Munanka.
Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), Bw. Wolfgang Marschick (Kulia) akimuonesha waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) leo alipotembelea jengo hilo. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (katikati).

Balozi Maiga katika Maadhimisho Siku ya Mshikamano na Wapalestina Dar

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mheshimiwa Balozi Maiga akizungumza kwenye sherehe ya Siku ya Mshikamano na Watu wa Palestine, kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Towers,5 Desemba 2017.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (kulia) akizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mshikamano na Watu wa Palestina, iliyofanyika tarehe 5 Desemba 2017 jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wajumbe wa Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina. Kutoka kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na
Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour wakiwa katika hafla hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (kushoto) akitembelea picha za maonesho kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mshikamano na Watu wa Palestina, iliyofanyika tarehe 5 Desemba 2017 jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliandaliwa na ubalozi wa Parestina nchini Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).
Hafla ya kuadhimisha Siku ya Mshikamano na Watu wa Palestina, iliyoandaliwa na ubalozi wa Parestina nchini Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) ikiendelea.
Wajumbe wa Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina wakipata picha ya kumbukumbu katika hafla hiyo.

SHULE YA MSINGI TABATA YANUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA MISS UBUNGO 2014 DIANA KATO

$
0
0
Mkurugenzi msaidizi Sera na Mipango kutoka wizara ya maji na Umwagiliaji  Paul Suley aliyekuwa anamwakilisha Katibu mkuu wa Wizara ya maji na Umwagiliaji amesema kuwa amezipokea changamoto ya shule hiyo na atawasilisha wizarani kwa ajili ya kufanyiwa kazi.


Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa Shule ya Msingi Tabata ulioratibiwa na aliyekuwa Miss Ubungo 2014, Diana Kato uliogharimu takribani shilingi 613,000 za kitanzania.

Sulley alisema kuwa, amezipokea changamoto zao ikiwemo ya kutokuwa na tanki la kuhifadhia maji ataliwasilisha wizarani na pia amefurahi sana kuona wadau mbalimbali wanajitoa kwa ajili ya kusaidia jamii.

Diana Kato amesema kuwa ameweza kutoa msaada huo kwa shule ya msingi Tabata ikiwa ni katika moja ya mradi ambapo alitumia takribani kiasi cha shilingi 613,000 kwa ajili ya kulipia gharama za kuwekwa maji na kununua vifaa vya ujenzi ili kukamilisha mradi huo.


 Mgeni Rasmi Mkurugenzi msaidizi Sera na Mipango kutoka wizara ya Maji na Umwagiliaji, Paul Sulley  aliyekuwa anamwakilisha Katibu mkuu wa Wizara hiyo akizungumza na wanafunzi, walimu na wazazi walioudhulia uzinduzi wa bomba la maji safi katika shule ya Msingi Tabata iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni alifadhiri mradi huo Miss Ubungo 2014, Diana Joachimu Kato na kulia ni Mkuu wa Shule ya msingi Tabata, Hamisi Ngoda
Miss Ubungo 2014, Diana Joachimu Kato akisoma risala kuhusu historia fupi kuhusu alivyoanza kutekeleza mradi wa bomba la maji safi uliokamilika na kukabidhiwa leo katika shule ya Msingi Tabata.
Mkuu wa Shule ya msingi Tabata, Hamisi Ngoda akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi wakati wa uzinduzi wa bomba la maji kwenye shule hiyo lililofadhiliwa na aliyekuwa Miss Ubungo Diana Kato leo shuleni hapo.
Wanafunzi wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa bomba la maji safi lililofadhiliwa na aliekuwa Miss Ubungo 2014.

Baadhi ya wazazi na wanafunzi wakufuatilia tukio la kukabidhi Bomba la maji kwenye shule ya Msingi ya Tabata, Ilaa jijini Dar es Salaam leo
Mkurugenzi msaidizi Sera na Mipango kutoka wizara ya Maji na Umwagiliaji, Paul Sulley akikata utepe kuashiria uzinduzi wa bomba la maji kwa ajili ya matuminzi mbalimbali katika shule ya Msingi Tabata leo jijini Dar es Salaam.
Picha pamoja mara baada ya kuzindua bomba la maji safi kwa ajili ya matumizi mbalimbali shuleni  hapo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAGAZETI YA IJUMAA LEO DECEMBER 8,2017

Viewing all 110016 articles
Browse latest View live




Latest Images