Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live

WAZIRI MWAKYEMBE KUHUDHURIA UZINDUZI WA BARAZANI ENTERTAINENT

$
0
0
Na Agness Francis Blog ya jamii
Waziri wa habari utamaduni na michezo Harson Mwakyembe, amehudhuria uzinduzi  wa mradi wa  Barazani Entertaiment  ambapo mradi huo ulianza kutengenezwa miaka minne iliyopita mpaka kufikia hapa ulipo.
Uzinduzi huo umefanyika jana katika ofisi za Barazani Entertaiment Jijini Dar es Salaam. Waziri Mwakyembe amewapongeza vijana hao wa bongo muvi walioungana kukamilisha zoezi la mradi huo  ambao unajishughulisha na usambazaji wa filamu ikiwa lengo ni kutaka kukomesha unyonyaji wa wasanii wa bongo muvi hapa nchini.
Aidha Waziri huyo ameongelea changamoto zinazowakabili wasanii hao ni kukandamizwa kimaslai  kutokana  na miundo mbinu za usambazaji wa kazi zao,na kuwata wasanii wote kuunga mkono mradi huu ambao utakuwa ni mkombozi  kwao.
Hata hivyo Meneja masoko na uzalishaji Barazani Entertaiment  Jacob Stiven  amesema kuwa wamejipanga vema katika kuhakikisha wanakabiliana na changamoto hizo kwa kila msanii wa filamu anapata haki yake kupitia mradi huo
Nae Msanii wa filamu Jacklen Wolper amewataka wasanii wenzake kuunga mkono mradi huu ili uwe endelevu na pamoja  kuwa na imani na mikakati iliyowekwa ili kuleta mafanikio na mapinduzi ya filamu hapa nchini 
Makamu mwenyekiti wa chama cha waigizaji Tanzania Jimy Mafufu amemalizia kwa kutoa shukrani kwa ujio wa Barazani Entertaiment na kuitaka pia serikali ya awamu ya 5 kuinga mkono tasnia hiyo na kuiwekea ulinzi ili kukomesha unyonywaji na ukandamizwaji   katika mauzo ya filamu
 Waziri wa habari utamaduni na michezo Harson Mwakyembe akizungumza na waandishi wa wageni waalikwa  kuhusu kazi nzuri inayofanywa  Barazani Entertaiment na kuwapongeza wasanii  hao walioanzisha mradi huo ili kukomesha uuzwaji wa kazi feki za filamu jana katika ofisi za Barazani Entertaiment Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa habari utamaduni na michezo Harson Mwakyembe akikata utepe akionyesha kuwa ni ishara ya kufungua rasmi mradi huo jana katika ofisi za Barazani Entertaiment Jijini Dar es Salaam.
 Afisa utumishi rasilimali watu Barazani Entertaiment Silvana Joseph akitoa risala fupi kuhusu mradi huo  unaohusisha  wasanii mbalimbali wa filamu hapa nchini ikiwa lengo ni kutokomeza ukandamizwaji wa kazi zao, jana katika ofisi za Barazani Entertaiment Jijini Dar es Salaam.
 Wageni waalikwa  waliojitokeza katika hudhuria uzinduzi huo kutoka sehemumu mbalimbali jana katika ofisi za Barazani Entertaiment Jijini Dar es Salaam.
 Msanii wa filamu Jacklen Wolper akizungumza na waandishi wa habari huku akiwataka wasanii wenzake kuwa na imani katika mradi huo jana katika ofisi za Barazani Entertaiment Jijini Dar es Salaam.
Meneja masoko na uzalishaji Barazani Entertaiment  Jacob Stiven  akizungumza na waandishi  wa habari juu wa muamko wa wa wasanii katika kuleta maendeleo na kuwataka wale wenye viwanda feki majumbani vya kutengeneza dvd waende kukunua bidhaa kwao ili kuleta usawa katika kipato jana katika ofisi za Barazani Entertaiment Jijini Dar es Salaam.

IGP SIRRO AONGOZA HARAMBEE YA KUCHANGIA UKARABATI WA MAKAZI YA ASKARI MKOANI MOROGORO

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwasili kwa ajili ya kushiriki harambee ya kuchangia ukarabati wa nyumba za askari wa Jeshi hilo, ambapo harambee hiyo iliwashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wanasiasa na wafanyabiashara mbalimbali wa mkoa wa Morogoro.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akisalimiana na maofisa wa Jeshi hilo alipowasili mkoani Morogoro, kwa ajili ya kushiriki harambee ya kuchangia ukarabati wa nyumba za askari wa Jeshi hilo, ambapo harambee hiyo iliwashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wanasiasa na wafanyabiashara mbalimbali wa mkoa wa Morogoro.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe stephen Kebwe (wa pili Kulia), akifuatiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, wakimsikiliza kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Ulrich Matei (aliyesimama), akitoa neno wakati wa harambee ya kuchangia ukarabati wa nyumba za askari wa Jeshi hilo mkoani humo, harambee ambayo iliwashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wanasiasa na wafanyabiashara mbalimbali wa mkoa wa Morogoro

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe stephen Kebwe (aliyesimama), akitoa neno mbele ya wanasiasa na wafanyabiashara mbalimbali pamoja na wadau wa maendeleo (hawapo pichani) wakati wa harambee ya kuchangia ukarabati wa nyumba za askari wa Jeshi hilo mkoani humo ilikutoa makazi salama kwa askari. Picha na Jeshi la Polisi.

THE 8TH INTERNATIONAL TÜBINGEN AFRICA FESTIVAL 2018 IN GERMANY IT IS NOW OFFICIALLY OPEN FOR REGISTRATION & PARTICIPATION.

$
0
0
The 1 year break is over, its time to get back to business as usual and this time on a big note. The festival is now called GAIEXPO as it has included African Small and Medium enterprises worldwide. This sector shall promote the continent Africa not just as tourist but  business destination with endless opportunities in sectors such as Agriculture, Agri-business -food,Tourism, Arts and Culture etc. 
We are calling on all small businesses and enterprises, Africa and Diaspora Entrepreneurs, Traders, workshops givers, trainers, Artist, panelist... in Africa, Germany, Europe & USA to register and participate. GAIEXPO is an African market and meeting place open to countries, companys, Ngo´s with interest in sub-Sahara Africa to share contacts, information, network and do deals.  
We look forward to meeting you in Tübingen, Germany 2018 contact:

Susan Tatah
Managing Director 

TradeMark East Africa Kuwasaidia Wafanyabiashara Wanawake wa Tanzania, Kufanya Biashara za Kimataifa.

$
0
0
 Taasisi ya TradeMark, East Afrika itawasaidia wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, kuweza kufanya biashara ya kimataifa kwa kuyafikia masoko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, hata nje ya Afrika. 
Ahadi hiyo, imetolewa na Mkurugenzi wa TradeMark  Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga (pichani), wakati akizungumzia mpango kamambe wa kuwasaidia wafanyabiashara wanawake wan chi 6 za Afrika Mashariki, uliozinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Nairobi nchini Kenya. 
Ulanga amesema, TradeMark East Africa, kupitia mradi wake wa “Women in Trade”  uliolenga kuwajengea uwezo wa wafanyabiashara wanawake kuhimili ushindani wa kibiashara na kukabiliana na vikwazo vya kibiashara kwa wafanyabiasha wanawake Tanzania kuwawezesha kufanya biashara ya kimataifa ikiwemo kuwezesha bidhaa zao kuyafikia masoko ya nchi za Afrika Mashariki na soko la kimataifa kwa kuanzia na wafanyabiashara wanawake wanaovuka mipaka ya nchi xa Afrika Mashariki. 

Bwana Ulanga amesema, TradeMark East Africa ni taasisi inayoongoza katika kuleta usawa wa kijinsia katika biashara, kwa sababu utafiti umeonyesha kuwa asilimia 70% ya wanaofanya biashara za mipakani ni wanawake na wanakabiliwa na vikwazo vingi vya kibiashara vikiwemo vikwazo vya kijiografia, vikwazo vya kijinsia, vikwazo vya kisheria, vikwazo vya kimtazamo, hivyo TradeMark imeandaa mpango kamambe wa miaka sita wa kuwajengea uwezo, atakaogharimu shilingi bilioni 12. 
TradeMark East Africa (TMEA) ni shirika lisilo la kiserikali, la maendeleo kwa lengo la kuongezeka ustawi wa kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa njia ya biashara. TMEA inafanya kazi kwa karibu na taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), serikali za kitaifa, sekta binafsi na asasi za kiraia.
 TMEA inachangia ukuaji wa biashara Afrika Mashariki kwa kufungua fursa za kiuchumi kwa kuongeza fursa za upatikanaji  wa  masoko, kuboresha mazingira ya biashara, biashara ya ushindani na kuongeza mchango wa biashara kuchangia ukuaji wa uchumi, kupunguza umaskini kwa kuleta maendeleo na ustawi wa jamii.

TMEA ina makao yake makuu mjini Nairobi nchini Kenya, na ina  matawi katika miji ya Arusha, Bujumbura, Dar es Salaam, Juba, Kampala na Kigali.

Ili kujua zaidi kuhusu TMEA, tafadhali tembelea tovuti TMEA katika www. www.trademarkea.com

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AFUNGUA MKUTANO MKUU WA CCM MKOA WA KUSINI UNGUJA

$
0
0
 WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika ukumbi wa mkutano katika hoteli ya coconut marumbi wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akifungua mkutano huo 
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Nyenzo za utendaji Kazi za CCM Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Chwaka Mwalimu Mussa Jecha, wakati wa mkutano huo, kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhani Abdallah Ali na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM pia ni Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeri rasmin Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kufungua Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa coconut marumbi Unguja.
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Coconut Marumbi Wilaya ya Kusini Unguja. 
 MSIMAMIZI Mkuu wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi Mkoa wa Kusini Unguja Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati wa zoezi la kupiga kura likiaza katika ukumbi wa hoteli ya Coconut Marumbi Unguja.
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipiga kura yake kuwachagua Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Marumbi Wilaya ya Kusini Unguja. 
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM pia ni Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga kura yake kuwachagua Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa Mkutano Mkuu uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya coconut marumbi Wilaya ya Kusini Unguja. Picha na Ikulu

KONGAMANO LA PETROLI AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA KENYA 2019

$
0
0
Na Veronica Simba - Kampala
Kongamano na Maonesho ya Tisa ya masuala ya Petroli kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, yanatarajiwa kufanyika nchini Kenya, Machi 2019. Azimio hilo limepata baraka za Mkutano Ngazi ya Makatibu Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, uliofanyika Kampala, Desemba 1, mwaka huu.
Mkutano huo wa Makatibu Wakuu ni maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wenye lengo la kupitia nyaraka na taarifa za Maandalizi ya Mkutano wa Kazi wa Wakuu wa Nchi kabla ya kuziwasilisha kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliopangwa kufanyika mwezi Januari, 2018.
Kuteuliwa kwa Kenya kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo kubwa, kunatokana na mzunguko wa kawaida wa ratiba yake, ambapo makongamano yaliyotangulia yalifanyika katika nchi za Jumuiya husika kwa mlolongo wa Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi.
Hivyo basi, kutokana na mzunguko huo, Makatibu Wakuu wamebariki, Kongamano lijalo lifanyike Kenya kuanzia tarehe 6 hadi 8 Machi, 2019.
Aidha, Mkutano huo pia uliazimia kuwa, maandalizi ya Kongamano husika yaanze mapema ili kuwepo muda wa kutosha wa kujitangaza na kuvutia ushiriki wa mataifa mbalimbali duniani.
Masuala mengine yahusuyo nishati, yaliyojadiliwa katika Mkutano huo ni pamoja na maendeleo ya upembuzi yakinifu kwa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Kigali hadi Bujumbura, Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Mbarara – Mwanza - Isaka hadi Dar es Salaam, pamoja na kuoanisha mfumo wa kisheria na udhibiti wa masuala ya nishati.
Vilevile, Mkutano huo pia ulijadili maendeleo endelevu ya Kituo cha Ubora (Centre of Excellence) cha masuala ya Nishati Jadidifu na Matumizi Bora ya Nishati katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichopo kwenye Kitivo cha Uhandisi cha Chuo Kikuu cha Makerere, nchini Uganda.
Mbali na masuala ya nishati, sekta nyingine zilizojadiliwa katika Mkutano huo ni elimu ya juu, miundombinu, uchukuzi, fedha pamoja na afya.
Tanzania, kama ilivyokuwa kwa nchi nyingine wanachama, iliwakilishwa na wataalam mbalimbali kutoka sekta husika pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara hizo akiwamo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto), akishiriki katika Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ngazi ya Makatibu Wakuu na Wataalam, uliofanyika Kampala hivi karibuni. Pamoja naye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati) na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gerson Mdemu.
 Mwakilishi kutoka Tanzania, ambaye ni Ofisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Steven Mbundi (kushoto), akisaini makubaliano ya masuala mbalimbali yaliyojadiliwa katika Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ngazi ya Makatibu Wakuu na Wataalam, uliofanyika Novemba 30 hadi Desemba 1, mwaka huu Kampala, sambamba na wenzake kutoka nchi nyingine za Jumuiya hiyo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto), akijadiliana jambo na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Maendeleo ya Petroli, James Andilile (katikati) na Mhandisi Nishati, Samuel Mgweno, muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ngazi ya Makatibu Wakuu na Wataalam, uliofanyika Kampala Novemba 30 hadi Desemba 1, mwaka huu.
 Sehemu ya Ujumbe wa Wataalam kutoka Tanzania, wakiwa katika Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, uliofanyika Kampala, Novemba 30 hadi Desemba 1, mwaka huu.
 Meza Kuu – Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ngazi ya Makatibu Wakuu na Wataalam, uliofanyika Kampala, Novemba 30 hadi Desemba 1, mwaka huu.

Wajumbe wa Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ngazi ya Makatibu Wakuu na Wataalam, uliofanyika Kampala, Novemba 30 hadi Desemba 1, mwaka huu, wakiendelea na Mkutano.

Azam TV - CECAFA: TANZANIA VS LIBYA (0-0) FULL HIGHLIGHTS (3/11/ 2017)

Azam TV - Mohammed Dewji ashinda zabuni Simba, awekeza Tshs 20 bilioni


Introducing New Song from Uingereza..."Machungu Ya Kuachwa" by Bidder

KUMSOMESHA MTOTO NI IBADA KUBWA SANA KATIKA MAISHA YETU YA KILA SIKU - WAZIRI JAFO

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akizungumza wakati Mahafali ya Shule Mikocheni Islamic ambapo aliwaasa wazazi kuwataka kuwekeza katika kuwapatia wtoto elimu ya Duniani na dini hili waweze kuja kuwa watumishi waadilifu baadae pindi wanapokuja kuwa viongozi wa Umma.
 Katibu wa Shule ya Mikocheni Islamic akizungumza kablaya kumakaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo katika mahafali ya shule ya Msingi ya Mikocheni Islamic Jijini Dar es Salaam

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akikagua Maonesho ya kisayansi ya shule ya Msingi ya Mikocheni Islamic wakati wa mahafali ya Darasa la Saba ya shule hiyo yaliyofanyika jana.
 Wanafunzi wa Kike wa Shule ya Msingi ya Mikocheni Islamic wakionyesha Umahiri wao wa kuimba Kaswida mbele ya Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa kitengo cha Sayansi na walimu wao wa shule ya Msingi Mikocheni Islamic.
Picha na Humphrey Shayo wa Globu ya Jamii

WAZAZI WEKEZENI KWENYE ELIMU YA WATOTO - MAMA MARY MAJALIWA

$
0
0
MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewaomba wazazi wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi wahakikishe wanatumia sehemu ya kipato chao katika kuwekeza kwenye elimu ya watoto wao. Amesema elimu ndiyo jambo pekee linaoweza kumsaidia mtoto katika kutimiza ndoto zake za maisha pamoja na kumtoa katika kundi la wategemezi. 
Mama Mary aliyasema hayo jana (Jumamosi, Desemba 2, 2017), katika maafali ya shule ya awali na msingi ya Wonder Kids, iliyopo wilayani Ruangwa, Lindi. Mke wa Waziri Mkuu alialikwa katika maafali hayo kama mdau wa elimu. Maafali hayo yaliyohusisha watoto wa awali ambao wanaingia darasa la kwanza. 
 “Walimu wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunzi hao wanajua kusoma vizuri, hivyo wazazi watumie kipato chao kuwekeza katika elimu kwani faida watakuja kuiona baadaye.” Alisema kitaaluma yeye ni mwalimu hivyo anatambua kuwa walimu wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunzi hao wanajua kusoma vizuri na wanakuwa na tabia nzuri, hivyo wazazi hawana budi kushirikiana nao. Pia Mama Mary alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi wawatie moyo walimu kwa sababu kazi wanayoifanya ni kubwa. 
“Wote ni mashahidi watoto wetu tulivyowaleta na sasa ni tofauti.” Alisema ni vizuri wazazi wakashiriki kikamilifu katika suala la elimu kwa watoto wao ikiwa ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya masomo yao badala ya kuwaachia walimu peke yao. 
 Kwa upande wake ,mgeni rasmi katika maafali hayo ambaye ni Muwakilishi Mkazi wa Children in Crossifire Bw Craig Ferla aliwapongeza wanafunzi hao kwa kutimiza moja ya hatua katika safari yao ya elimu na aliwasihi waendele kupenda kwenda shule na kusoma kwa bidii. Pia aliwapongeza wazazi kwa kutambua umuhimu wa elimu ya awali na kuwapeleka watoto wao kwenye shule hiyo ya Wonder Kids. 
“Wonder Kids ni mahali sahihi ambapo mtoto anapata elimu na malezi bora. Alisema elimu ya awali ninzuri kwa mtoto kwa kuwa inawawezesha kujua kusoma, kuandika na kuhesabu, hivyo aliwaeleza Wanaruangwa kutumia vizuri fursa ya uwepo wa shule hiyo katika wilaya yao. 
 Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bibi Nancy Tausi alisema Wonder Kid ilianzishwa Januari, 2017 ikiwa na wanafunzi 117 ambao ni wa kuanzia darasa la awali hadi darasa la tatu. Alisema lengo la kuanzisha shule hiyo ni kuhakikisha watoto wanapata kujua kusoma vizuri na kwamba wanatarajia kuanzisha darasa la kompyuta kwa ajili ya watoto kujifunza TEHAMA pamoja na kuanza kufundisha lugha ya Kifaransa.

 Watoto wa Shule ya Msingi na Awali ya Wonder Kids wakiimba wimbo wa Shule yao katika Mahafali ya Kwanza ya Shule hiyo iliyopo Ruangwa Mjini

 Wahitimu wa  darasa la Awali wa Shule ya Wonder Kids  wakiimba  katika Mahafali ya Kwanza ya Shulel hiyo iliyopo Ruangwa Mjini Desemba 2, 2017.
 Wahitimu wa  wa Shule ya Msingi na Awali ya Wonder Kids wakicheza ngoma ya asili  katika Mahafali ya Kwanza ya Shulel hiyo iliyopo Ruangwa Mjini 
 Mgeni Rasmi katika Mahafali ya kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya mjini Ruangwa , Bw. Craig Ferla ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Children in Crossfire akimkabidhi cheti  kwa mhitimu wa Mafunzo ya Awali katika shule hiyo, Jasmine Madamba, Desemba 2, 2017.Wapili kuil ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa.
Sehemu ya wazazi na waalikwa wa Mahafali ya Kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya Mjini Ruangwa wakimsikiliza Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa wakati alipozungumza katika Mahafali hayo

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza katika mahafali ya kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya Mini Ruangwa

ZIARA YA NAIBU WAZIRI MHANDISI MASAUNI NA WAZIRI BARANDAGIYE WA BURUNDI KATIKA KAMBI ZA WAKIMBIZI NDUTA NA MTENDELI MKOANI KIGOMA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma, ikiwa ni ziara ya kikazi kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao. Katika ziara hiyo Naibu Waziri aliongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo kutoka serikali ya Burundi, Pascal Barandagiye (hayupo pichani).
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo kutoka serikali ya Burundi, Pascal Barandagiye, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma, ikiwa ni ziara ya kikazi kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao.
wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma wakinyoosha mikono juu baada ya kuulizwa wangapi wanataka kurudi nchini kwao na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), katika mkutano wa hadhara ikiwa ni ziara ya kikazi ya naibu waziri kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo kutoka serikali ya Burundi, Pascal Barandagiye (kulia), wakipiga ngoma baada ya kuwasili katika uwanja ulipofanyika mkutano wa hadhara uliowahusisha wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma. Ziara hiyo lengo lake ni kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo kutoka serikali ya Burundi, Pascal Barandagiye (kulia), wakiagana baada ya kumaliza kuzungumza na wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma. Ziara hiyo lengo lake ni kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma, baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara ikiwa ni ziara ya kikazi kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JAPHET HASUNGA ATOA MIEZI MITATU WANANCHI WALIPWE FIDIA WAPISHE ENEO LA HIFADHI

$
0
0
Na Hamza Temba, Mbarali - Mbeya
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ametoa miezi mitatu kwa uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kukamilisha malipo ya fidia ya shilingi milioni 771.6 kwa kaya 308 za Kitongoji cha Machimbo ili ziweze kupisha eneo la hifadhi katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengele.
Naibu Waziri Hasunga ametoa agizo hilo jana katika mkutano wa hadhara baada kutembelea kitongoji hicho katika Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutatua migogoro kwenye maeneo ya hifadhi mkoani humo.
“Kaimu Mkurugenzi (TAWA) kama unavyoona wananchi hawa wapo tayari kupisha eneo hili la hifadhi, wanachosubiri ni malipo yao ya fidia, naagiza mpaka ifikapo mwezi Februari mwakani (2018) wawe wameshalipwa fidia zao, na ikiwezekana hata ndani ya mwezi Januari wawe wameshalipwa,”alisema Hasunga.
Awali akiwasilisha taarifa ya pori hilo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, David Kenyata alisema wakati pori hilo linaanzishwa mwaka 2002 kwa Tangazo la Serikali Na. 483 wananchi wa kitongoji hicho na vitongoji vingine walikuwa ndani ya eneo hilo la hifadhi.
Alisema mazungumzo yalishafanywa kupitia vikao halali vya uongozi wa viijiji na halmashauri ambapo wananchi hao waliridhia kulipwa fidia ili kuachia maeneo hayo ya hifadhi.
Alisema sababu kubwa ya kuanzishwa kwa pori hilo ni pamoja na kuhifadhi vyanzo vya maji yanayotiririka kwenda mto Ruaha na kwenye mabwawa ya kidatu na mtera yanayotumika kuzalisha umeme nchini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (waliokaa mbele katikati) akizungumza na watumishi wa Pori la Akiba Mpanga Kipengele alipotembelea makao makuu ya pori hilo jana katika Wilaya ya Wangin'ombe mkoani Njombe.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akisalimiana na Kaimu Meneja wa Pori la Akiba la Mpanga Kipengele, Stanslaus Odhiambo muda mfupi baada ya kuwasili makao makuu ya pori hilo jana katika Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Machimbo wapatao kaya 308 katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya jana ambapo aliiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania kuwalipa fidia ya shilingi milioni 771.6  kabla ya Februari, 2018 ili wapishe eneo la Hifadhi katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengele.
Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Machimbo wapatao kaya 308 katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ambaye aliwatembelea jana na kuagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania iwalipe fidia ya shilingi milioni 771.6 kabla ya Februari, 2018 ili wapishe eneo la Hifadhi katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengele alipowatembelea.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na wananchi wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji katika Skimu ya Igomelo, wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya ambao waligomea zoezi la uwekwaji wa vigingi vya mpaka kwenye eneo lao na Pori la Akiba la Mpanga Kipengele kwa hofu ya kupoteza maeneo hayo. Baada ya kuwaelimisha wananchi hao walikubali kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika ili kukamilisha zoezi hilo. Taarifa kamili BOFYA HAPA

WAJASIRIAMALI JIJI LA ARUSHA WAPATIWA MKOPO WA MILIONI 605

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha
Jumla ya Shilingi milioni 605 zimetolewa kama mkopo wa kuwanufaisha wajasiriamali walioko kwenye vikundi vya kinamama na vijana pamoja na walemavu waliopo  katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Akizungumzia mikopo hiyo inayotolewa na Halmashauri Afisa Ustawi wa Jamii Jiji la Arusha Hanifa Ramadhani amesema kuwa mikopo hiyo inatolewa ili kuwawezesha kinamama na vijana kuondokana na hali ngumu za kiuchumi zinazowakabili ili kuinua uchumi .
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amewataka Vijana ambao ni wasomi kujiunga katika vikundi hivyo na kupata mikopo ili kujiendeleza kiuchumi badala ya kusubiri ajira serikalini ile hali nafasi ni chache na wahitimu wa vyuo ni wengi.
Kwa upande wao Wanufaika wa Mikopo hiyo kwaniaba ya Walemavu Mwajuma Juma  na Patrick Petro  wameishukuru serikali kwa kutoa mikopo hiyo yenye masharti nafuu ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Mkuu wa Wilayaya Arusha  Gabriel Daqarro akabidhi hundi ya shilingi milioni 500 ya mkopo wa kinamama iliyotolewa na Halmashauriya Jiji la Arusha 

 Kinamama na vijana waliokusanyika katika ukumbiwa Arusha School kupewa mafunzo kabla y akupatiwa mikopo ya halmashauri ya jiji la Arusha.

WAZIRI KIJAJU AWATAKA WAHITIMU CHUO CHA UHASIBU ARUSHA KUJIEPUSHA NA RUSHWA

$
0
0
Na Pamela Mollel,ARUSHA 
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaju ametoa onyo kali kwa  wahitimu wa Uhasibu nchini kujiepusha na rushwa kwa kutaka utajiri wa haraka kuacha tabia hiyo kwani hawatabaki salama katika utawala huu. 


Akizungumza juzi  katika mahafali ya 19 katika Chuo cha Uhasibu Njiro Arusha, wakati akitunuku vyeti vya ngazi mbalimbali viiwemo vya Uhasibu kwa wahitimu 1324, Dk.Ashatu alisema baadhi ya wataalamu wa Uhasibu wanachangia kurudisha nyuma Maendeleo kwa tamaa zao.


Alisema ni vema watumie elimu waliopata kubuni ajira na pale watakaotoa ajira wafanye kwa weledi na uadilifu.Alisema endapo wataalamu hao watabadilika na kuwa na uadilifu itawezesha Taifa kufanikisha ndoto yake ya kufikisha uchumi wa Viwanda kabla ya mwaka 2025.

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaju ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza juzi katika mahafali ya Chuo cha Uhasibu Njiro Arusha ambapo pamoja na mambo mengine amewaonya wahitimu nchini kujiepusha na rushwa kwa kutaka utajiri wa haraka kuacha tabia hiyo kwani hawatabaki salama katika utawala huu. (Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
 Mwenyekiti wa Bodi ya chuo cha uhasibu Arusha Bi.Rukia Adam akisoma maelezo ya chuo cha Uhasibu Arusha katika mahafali chuoni hapo juzi

Mkuu wa kitivo cha uhandisi,mazingira na Computer Paul David Greening kutoka Uingereza akizungumza katika mahafali yao juzi katika Chuo cha Uhasibu NjiroArusha

 Wahitimu wakifatilia mahafali hayo kwa ukaribu zaidi

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Simba SC kwenda na kasi ya Rais Magufuli kwa kuzalisha ajira - MO

$
0
0
Mwekezaji mpya katika klabu ya Simba, Mohammed Dewji MO amesema amejipanga kushirikiana na wanahisa wenzake wa klabu hiyo kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kupitia kampuni ya Simba Sports Club Limited. 
  Dewji aliyasema hayo wakati akitoa salamu kwa wanachama na mashabiki wa Simba kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo, baada ya kutangazwa na kamati maalum ya kusimamia mchakato wa kumpata mwekezaji katika klabu ya Simba, kuwa mshindi wa tenda ya kuwekeza katika klabu hiyo. 
  Alisema klabu ya Simba inampongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuongoza serikali ya awamu ya tano, na wao wamedhamiria kuhakikisha wanakwenda sambamba na kasi yake kupitia mchezo wa mpira kwa kutoa ajira kwa Watanzania kwenye kampuni mpya itakayosimamia timu hiyo katika mfumo wa hisa. 
"Tamati yangu nielekeze kwa sisi sote kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayofanya ya kuongoza taifa hili. Wote tumtakie kila la kheri, baraka na fanaka tele katika utumishi wake uliotukuka.
"Pamoja na kupongeza sera yake ya ujenzi wa viwanda nchini, ambapo sisi kwa upande wetu, klabu ya Simba inamuunga mkono kwa ujenzi wa kiwanda kikubwa kabisa cha soka yaani Simba Sports Club Limited, ambacho licha ya kuongeza ajira lakini pia tutaendelea kulipa kodi kwa mujibu wa sheria za nchi," alisema Dewji. 
Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mohammed Entreprises, alitumia mkutano huo kuelezea mipango ambayo wameipanga ili kuiwezesha Simba kuwa klabu kubwa zaidi barani Afrika kuliko ilivyo sasa, huku malengo ikiwa ni kuwania mataji makubwa barani Afrika.

"Katika mwaka wa kwanza, nawaahidi kwa kushirikiana na ninyi tutakuwa na kiwanja cha nyasi asilia, na kiwanja cha nyasi za bandia ambapo viwanja hivi tutavitumia kwa mazoezi kwa kadri ya mahitaji ya mechi tunayokwenda kucheza, "Pia tutajenga hosteli ambayo itakuwa na vyumba 35 ambavyo wataishi wachezaji 30 na support staff, kila chumba kitakuwa na ukubwa wa 35 square- meter... ili kufanya eneo hilo kuwa bora kwa wachezaji wetu," alisema Dewji na kuongeza. 
"Wote tunaopenda mpira, tunajua kama ukitaka kuwa na wachezaji bora lazima utumie pesa. Nia yetu kwa mwaka wa kwanza, tunatarajia kiwango cha chini cha pesa ya usajili iwe bilioni moja. Pia tumetenga milioni 500 kuboresha benchi la ufundi, kwa kushirikiana na benchi liliopo sasa." 
Hata hivyo Dewji, alisema klabu ya Simba itajenga kituo cha kukuzia vipaji ambacho kitakuwa na wachezaji vijana. Jambo ambalo litaisaidia Simba kuwa na wachezaji bora vijana ambao wamefundishwa kucheza soka katika kituo cha timu hiyo. "Ili kuwa na wachezaji bora kwa miaka ijayo tunahitaji kuwa na kituo cha kukuzia vipaji kwa wachezaji wa umri chini ya miaka 14, 16, 18. Na mipango yetu ya baadae ni kushirikiana na timu kubwa za ulaya kutuongoza na kutuelemsha jinsi gani ya kujenga kituo chenye hadhi ya kimataifa na mungu akipenda tutakuwa na kituo bora barani Afrika." alisema Dewji.
Mwekezaji mpya katika klabu ya Simba, Mohammed Dewji MO akizungumza kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere. 
Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah akimkabidhi cheti cha ushindi wa tenda ya kuwekeza katika klabu ya Simba mfanyabiashara na mwanachama wa muda mrefu wa klabu hiyo, Mohammed Dewji MO kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere.

Wanachama wa klabu ya Simba wakishangilia baada ya kamati maalum ya kusimamia mchakato wa kumpata mwekezaji katika klabu ya Simba kumtangaza Mohammed Dewji MO kuwa mshindi wa tenda ya kuwekeza katika klabu hiyo.

Mchango wa Sekta Binafsi Kwenye Elimu Wapongezwa, 288 Wahitimu Udaktari Chuo cha Kairuki

$
0
0
Mchango wa Sekta Binafsi kwenye utoaji wa Elimu ya Juu nchini Tanzania, umepongezwa na kuelezewa  kuwa unalisaidia Taifa kukidhi mahitaji ya wataalamu wa fani mbalimbali, hivyo kusaidia kwenye maendeleo ya taifa.

Pongezi  hizo, zimetolewa jana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Dr. Salim Ahmed Salim, wakati wa mahafali ya 15 ya Chuo hicho, yaliyofanyika jana chuoni hapo ambapo jumla ya wanafunzi  288 Walihitimu kozi mbalimbali za astashahada, shahada na shahada za uzamili katika fani ya uuguzi na udakitari wa binadamu, wakiwemo wanafunzi  136 waliohitimu udakitari wa binadamu wakiongozwa na  mhitimu, Dr. Delilah Mwindadi aliyeibuka mwanafunzi bora wa udakitari.
Dr. Salim amesema, tangu chuo hicho kimeanzishwa, kimetoa madaktari wengi wanaolisaidia taifa hili, hii ikiwa ni ishara ya kutimizwa kwa azma ya muasisi wa chuo hicho, Marehemu Prof. Hubert Kairuki, la kuhakikisha chuo hicho kinatoa mchango kwa maendeleo ya taifa.
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Chuo hicho, Mama Kokushubira Kairuki, aliwataka wahitimu hao, kwenda kuyatumia mafunzo waliyoyapata kwa bidii, weledi  na uadilifu, ili kuendelea kulinda sifa na heshima za wahitimu wa chuo, waliojinjengea kwa miaka mingi.
Makamo Mkuu wa Chuo, Prof. Charles Mgone, amesema wahitimu wa Chuo hicho, wamefunzwa kuweza kufanya kazi popote nchini Tanzania, na mrejesho wa wahitimu hao huko makazini ni mzuri kwa sababu ni wachapa kazi kwa kujituma kwa bidii, weledi na waadilifu sana. 
Kwa upande wa chuo hicho, kinaongeza kampasi nyingine, na kutanua wigo wa mafunzo na huduma za kusafisha figo, dialysis, na huduma za kupandikiza uzazi, IVF kwa wanandoa wenye matatizo ya kutopata watoto.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, John Ulanga, amesema, mahafali haya ya 15, ni kielelezo cha mchango wa sekta binafsi katika kusaidia maendeleo ya taifa, kwa upande wa sekta ya afya na tiba ya binadamu, hivyo akatoa wito kwa serikali na sekta ya umma, kuendelea kujenga mazingira wezeshi kuwezesha sekta binafsi, kukua na kutoa mchango wake kuisaidia serikali na sekta ya umma kuleta maendeleo ya taifa letu, kwa sababu maendeleo ya kweli, yatapatikana kwa ushirikiano wa sekta binafsi na sekta ya umma, pamoja, tutaweza.
Jumla ya wahitimu 288 walihitimu, kati yao wauguzi ni 49, shahada za uuguzi ni 22, shahada za udaktari 136, na shahada za uzamili kwenye udakitari, ni 21. Mwisho
 Mhitimu shahada ya Uzamili akipongezwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Dr. Salim Ahmed Salim, wakati wa mahafali ya 15 ya Chuo hicho, yaliyofanyika jana chuoni hapo
 Mhitimu shahada ya Uzamili akitunukiwa  na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Dr. Salim Ahmed Salim, wakati wa mahafali ya 15 ya Chuo hicho, yaliyofanyika jana chuoni hapo
 Mwanafunzi Bora wa Udaktari, Dr. Delillah Mwindadi
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Bw. John Ulanga  akimpongeza mwanafunzi bora
 Mhitimu shahada ya Uzamili akitunukiwa  na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Dr. Salim Ahmed Salim, wakati wa mahafali ya 15 ya Chuo hicho, yaliyofanyika jana chuoni hapo

TANZIA NA HARAMBEE YA MSIBA WA MRS ALICE MWANYALALA HUKO READING, UK

$
0
0

Tanzania Reading  Association tunasikitika Kutangaza Kifo cha Mtanzania Mwenzetu, Mrs. Alice Mwanyalala (pichani)  Kilichotokea Royal Berkshire Hospital. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda nyumbani  Tanzania tarehe 15.12.2017.Gharama zote  ni £12,000.


Tafadhali Tunaomba Tuwachangie na kufika  Kuwafariji Familia Ya Pastor Zephania Mwanyalala Katika Kipindi Hiki Kigumu.

08 CARSDARE CLOSE
COLEY PARK
READING
RG1 6D

Kwa michango ya rambirambi ielekezwe 
kwa account ya mmoja wa wana familia, 


*Ref. Jina lako*👇🏿👇🏿👇🏿


*Miss G Mwanyalala*
*LLOYDS BANK*
*A/C 415 72 860*
*S/CODE 30-67-99*

https://www.gofundme.com/help-Mwanyalalafamily

TICTS FAMILY DAY BONANZA ILIVYOFANYA JIJINI DAR

$
0
0
 Kamati ya Maandalizi ya Bonanza la Familia za Wafanyakazi wa Kampuni ya kuhudumia makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS), ikiwa katika picha ya pamoja wanati wa sherehe hiyo, iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es salaam.

Katika Bonanza hilo, wafanyakazi wa kampuni hiyo pamoja na familia zao walishindana katika michezo mbali mbali, ikiwemo ya mpira wa miguu, kivuta kamba, kuogelea, kukimbia na magunia na mingineyo huku watoto walitoana jasho katika kulisakata dansi na kuogelea huku wengine wakiondoka na zawadi kemkem.

Akizunguma katika Bonanza hilo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Jared Zerbe alisema lengo kubwa la Siku hiyo ilikuwa ni kuwakutanisha wafanyakazi na familia zao ziweze kufurahi kwa pamoja na pia kusherehekea kuuaga mwaka na kujiandaa kuukaribisha mwaka mpya katika kazi zao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya kuhudumia makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS), Jared Zebre (wa nne kulia) akikabidhi kikombe kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo waliounda timu ya Mameneja baada ya kuibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya wakanyakazi wa ngazi y chini, katika mchezo wa Bonanza la Familia za Wafanyakazi hao, lililofanyika kwenye ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi, jijini Dar es salaam. wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa na kushoto ni, Meneja Utekelezaji wa Kampuni hiyo, Patrick Kusiga.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya kuhudumia makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS), Jared Zebre (pili kushoto) akipikea tuzo maalum kutoka kwa viongozi wa Kamati ya Maandalizi ya Bonanza la Familia za Wafanyakazi wa Kampuni hiyo, lililofanyika kwenye ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi, jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Kampuni ya kuhudumia makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS), Erik Sazs akijaribu kuuzuia mpira bila mafanikio katika mchezo wa Bonanza la Familia za Wafanyakazi wa Kampuni hiyo, lililofanyika kwenye ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi, jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Mkali wao akiondoka na mpira .
Mkuu wa Kitengo cha Uhandishi wa Kampuni ya kuhudumia makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS), Cornelis Kwadjik akijaribu kumkoka mmoja wa wachezaji wa timu ya Wafanyakazi wa Kampuni hiyo, katika bonanza la familia za wafanyakazi hao, lililofanyika kwenye ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi, jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki.
Mpira wa Wavu
Kuvuta kamba.

MAGAZETI YA JUMATATU LEO DECEMBER 4,2017

Viewing all 110129 articles
Browse latest View live




Latest Images