Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

MADABA YAWA MFANO BORA KATIKA KUTATUA KERO YA MAJI KATIKA WILAYA YAO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akikagua mabomba yatakayotumika kusambazia maji kwa mradi wa Maweso akiwa na Mbunge wa Jimbo la Madaba, Joseph Mhagama katika Wilaya ya Madaba, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akikagua ujenzi wa tenki la maji la mradi wa Lolindo na Mbunge wa Jimbo la Madaba, Joseph Mhagama ambao utekelezaji wake unaendelea katika Wilaya ya Madaba, mkoani Ruvuma.
Mhandisi wa Mkoa wa Ruvuma, Jones Kimaro (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso katika kitekeo cha maji ikiwa ni sehemu ya mradi wa Lilondo katika Wilaya ya Madaba, mkoani Ruvuma.
Mradi wa mfano uliotekelezwa na wakazi wa Lilondo, ambao wametumia teknolojia ya kienyeji ya kukusanya maji kwa mabomba kutoka milimani na kuyahifadhi kwenye bwawa walilochimba na kuyasambaza kwa wananchi kupitia mitaro waliyochimba kwa gharama zao wenyewe ili kukabiliana na changamoto ya maji katika kijiji chao.

ZARA TOURS YA MOSHI YARATIBU SAFARI YA MABALOZI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
Kampuni ya zara tours ya mkoani Kilimanjaro imeratibu mabalozi 13 wa Tanzania wanaowakilisha nchi tofauti tofauti kupanda mlima kilimanjaro kupitia Marangu . Idadi yao wakiwa. Wageni hawa wamepokelewa na Mkurugenzi wa East Point hotel ya Moshi tanzania, Bw. Rashid Adam akimuwakilissha Mama Zainab Anslem maarufu kama Mama Zara ambaye ni CEO wa Zara Tours ya mjini Moshi.
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghilwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi Mhe. Kippi Walioba wakikaribisha mabalozi 13 wa Tanzania wanaowakilisha nchi tofauti tofauti kupanda mlima kilimanjaro kupitia Marangu  chini ya uratibu wa Zara Tours
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghilwa na Mkuu akimkabidhi kiongozi wa mssafara bendera ya Taifa kabla mabalozi 13 hao wa Tanzania wanaowakilisha nchi tofauti tofauti kupanda mlima kilimanjaro kupitia Marangu  chini ya uratibu wa Zara Tours
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghilwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi Mhe. Kippi Walioba wakiagana na mabalozi 13 wa Tanzania wanaowakilisha nchi tofauti tofauti kupanda mlima kilimanjaro kupitia Marangu  chini ya uratibu wa Zara Tours
 Mkurugenzi wa East Point hotel ya Moshi Tanzania, Bw. Rashid Adam akiwa na Balozi Dkt. Aziz Mlima kabla ya kuanza safari hiyo
Mkurugenzi wa East Point hotel ya Moshi Tanzania, Bw. Rashid Adam akiwa na kiongozi wa msafara  kabla ya kuanza safari hiyo

WAFUGAJI NA WAKULIMA BADO CHANGAMOTO, NAIBU WAZIRI ULEGA AAGIZA WAFUGAJI KUFUATA SHERIA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Ili kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (mb) Abdalah Ulega amewataka wafugaji wote waliongia vijijini kinyume cha sheria kufuata sheria vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa zidi yao. 

Hayo ameyasema Mkuranga mkoani pwani wakati alipofanya ziara ya kutembelea vijiji vya jimboni kwake kuangalia changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo ambapo moja ya changamoto hizo ni tatizo la wakulima na wavugaji. 

Aidha ulega amesema moja ya sababu ya migogoro ya wakulima na wafugaji ni kutokuwa na matumizi bora ya ardhi hivyo ameitaka jamii kuwa na matumizi bora ya ardhi ilikuweza kuepuka migogoro inayoweza kutokea. "tatizo hakuna matumizi bora ya ardhi na ni lazima kuwe na matumizi bora ya ardhi pamoja na kupima maeneo ili maeneo ya wafugaji yaweze kujulikana",alisema 

Amesema yeye kama Waziri atazungumza na watalaamu kutoka wizarani ili waweze kushirikiana na wataalamu wa halmashauri ya mkuranga kwa pamoja waweze kwenda katika kijiji cha Matanzi kutafuta ufumbuzi wa kudumu juu ya tatizo la wakulima na wafugaji.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb) Abdalaah Ulega akimsikiliza moja ya wafugaji wa Kijiji cha Matanzi Kata ya Beta wakati wa ziara yake katika Jimbo la Mkuranga akisikiliza changamoto za wananchi wake. 
Hata hivyo amemuagiza Afisa Mifugo wa kata ya Beta kuhakikisha ng'ombe wote wanapigwa chapa ili kuweza kujua idadi kamili ya ng'ombe na ametoa wito kwa wakulima na wafugaji kuhakikisha  anashirikiana,wanapenda,wavumiliane na waishi kwa amani. 

Awali wanachi wa kijiji cha Matanzi wakitoa malalamiko yao mbele ya Naibu Waziri huyo wamesema kijiji chao kilipokea kaya nne za wafugaji ambazo zina tambulika wakiwa na mifugo isiyozidi 300 lakini mpaka sasa kaya hizo zimeongezeka kinyume na utaratibu na idadi ya ng'ombe kuwa zaidi ya 900 hali inayopelekea mifugo kuwa mingi na kusambaa kwenye mashamba ya wakulima na kuharibu mazao yao. 

Mbali na changamoto hiyo, katika ziara ya Naibu Waziri amekutana na ukosefu wa walimu katika kata ya Mkwechembe na Matanzi na kumuagiza Afisa Elimu wa Wilaya kuhakikisha walimu wanaongezwa kwenye shule hizo, pia ameshukuru Bruda Marcos kwa hatua kubwa aliyoifanya ya kujenga madarasa manne ya Shule ya Msingi Mkwechembe. 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb) Abdallah Ulega akikagua shule ya Mkwechembe iliyojengwa na mfadhili Bruda Marcos katika Kijiji cha Mkwechembe. 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb) Abdallah Ulaga akipokea zawadi kutoka kwa wanakijiji cha Mkwechembe wakati wa ziara yake kwenye Jimbo lake la Mkuranga jana Mkoani Pwani. 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb) Abdallah Ulega akisalimiana na wanakijii wakati wa ziara ya Jimbo la Mkuranga jana Mkoani Pwani.

UJERUMANI YATOA MSAADA MUHIMU KWA WAKIMBIZI NCHINI TANZANIA NA RWANDA

$
0
0
DAR ES SALAAM – Serikali ya Jamhuri ya Kifederali ya Ujerumani imetoa mchango wa Euro milioni 2 kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani  (WFP) ili taasisi hiyo imudu kuendelea kutoa msaada wa chakula kwa takribani nusu milioni ya wakimbizi na watu wanao omba hifadhi waishio katika nchi za Tanzania na Rwanda. Mchango huu wa fedha ni muhimu sana kwa kazi za kuhudumia wakimbizi zinazofanywa na WFP katika ukanda huu ambapo shirika hilo linakabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha. Kutoka katika mchango huo, kazi za WFP katika nchi za Tanzania na Rwanda kila moja itapokea Euro milioni 1. Balozi wa Ujerumani Detlef  Wächter alisisitiza  umuhimu wa kuwepo kwa msaada wa haraka kutoka jumuiya za kimataifa ili kupunguza makali ya changamoto za wakimbizi nchini Tanzania. 

“Tukiwa miongoni mwa wahisani wakubwa kabisa wa kimataifa, ni wajibu wa nchi yetu kusaidia na kuunga mkono juhudi za nchi wenyeji na mashirika ya kimataifa katika mgogoro huu wa kiutu. Tuna imani kwamba msaada huu wa fedha utaisaidia WFP kukabiliana na upungufu wa fedha uliopo hivi sasa.” Nchini Tanzania, mchango wa Ujerumani ulitumika kununua mahindi ambayo ni sehemu ya mgao wa kila mwezi wa chakula unaojumuisha pia kunde, chumvi, mafuta ya kupika na unga wa uji ulioongezwa virutubisho. Nchini Rwanda, mchango huo ulitumika hasa kununua mahindi na maharage kwa migao ya chakula cha kila mwezi. Vilevile, WFP Rwanda ilinunua unga wa uji ulioongezwa virutubisho, sukari na maziwa ya unga yenye viturubisho ili kuwasaidia watu walio katika hali mbaya zaidi wanaohitaji mlo maalumu.  
 Katika nchi zote mbili, WFP inatoa chakula cha nyongeza kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha, watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, wagonjwa waliolazwa hospitalini na watu walio katika tiba ya VVU/UKIMWI na kifua kikuu. Programu hizi maalumu zinazolenga makundi ya watu hutoa lishe inayohitajika sana kupitia chakula cha ziada kama vile uji ulioongezewa virutubisho na maziwa ya unga yenye virutubisho. Vyakula hivi ni muhimu katika kukabiliana na tatizo la kudumaa na ukosefu wa lishe kwa watoto, na vinaongeza kinga ya mwili kwa watu walio na hali mbaya. Vilevile, WFP hutoa milo ya chakuala kilicho pikwa kwa wakimbizi walio katika vituo vya mpakani wakisubiri utaratibu wa kupokelewa.

“WFP inatoa shukrani za dhati kwa Ujerumani, ambayo katika miaka mitano iliyopita imekuwa miongoni mwa wahisani wetu wakubwa kabisa na imeimarisha zaidi utayari wake katika kutatua migogoro ya kiutu nchini Tanzania, ukanda na kote duniani,” alisema Mwakilishi wa WFP Tanzania Michael Dunford. “Mwendelezo wa msaada huu kutoka Ujerumani ni muhimu katika kukidhi mahitaji ya chakula kwa wanaume, wanawake na watoto waliokimbia makwao.” Tangu kuibuka kwa mgogoro nchini Burundi mwaka 2015, zaidi ya wakimbizi 258,000 kutoka Burundi waliingia nchini Tanzania, jambo lililoifanya Tanzania kuwa na idadi kubwa zaidi ya wakimbizi kutoka Burundi katika ukanda wa Afrika Mashariki. 

Hivi sasa, Tanzania inawahifadhi takribani wakimbizi 317,000 katika kambi tatu, idadi ambayo ni takribani mara tano ya ile iliyokuwepo miaka miwili iliyopita. Kwa upande wake, Rwanda hivi sasa inawahifadhi wakimbizi 172,000 katika kambi sita. Katika hao, wakimbizi 87,000 wanatoka Burundi, ambapo 55,000 wanaishi katika Kambi ya Mahama na ambao wanategemea kwa asilimia zote msaada ili wajikimu katika mahitaji ya chakula. “WFP inaweza kuendelea kutoa chakula kwa watoto na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha katika kambi za wakimbizi, na hii ni kwa sababu ya msaada kutoka Ujerumani,” alisema Jean-Pierre de Margerie, Mkurugenzi na Mwakilishi wa WFP Rwanda. 
“Kwa kuwa wakimbizi wana nafasi ndogo ya kujiingizia kipato nchini Rwanda, msaada wa chakula unabaki kuwa wa muhimu sana.” Kufuatia mmiminiko mkubwa wa watu katika nchi zote hizi mbili, WFP linahitaji rasilimali zaidi ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi hasa yale ya msingi ya chakula. Tangu Februari, kutokana na kupungua kwa upatikanaji wa fedha, WFP nchini Tanzania ililazimika kupunguza mgao wa chakula hadi kufikia asilima 72 ya kiwango cha chini cha kalori 2,100 zinazohitajika. 
Ili kurejesha mgao katika kiwango kinachostahili cha mahitaji ya chakula ya wakimbizi katika nchi zote mbili, WFP inahitaji nyongeza ya Dola za Marekani milioni 29 katika kazi zake nchini Tanzania na Dola za Marekani milioni 10 huko Rwanda kati ya sasa na mwezi Aprili, 2018. Endapo fedha za nyongeza hazitapatikana, huenda WFP ikalazimika kupunguza zaidi mgao wa chakula .

WFP ni shirika kubwa zaidi duniani la misaada ya kiutu linalopambana na njaa kote duniani, kutoa msaada wa chakula katika nyakati za dharura na linaloshirikiana na jamii ili kuinua viwango vya lishe na kujenga uwezo wa kujinusuru na majanga. Kila mwaka, WFP inawasaida takribani watu milioni 80 katika nchi 80 kote duniani.

Wateja wa Tigo Kushinda Mamilioni ya Fedha Katika Promosheni ya Msimu wa Sikukuu

$
0
0
Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Kampuni ya Tigo, Hussein Sayed (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa promosheni ya 'Fanya Muamala na Ushinde na Tigo Pesa' jijini Dar es salaam leo, ambapo wateja wa Tigo pesa wana nafasi ya kujishindia hadi shilingi 15 milioni kwa kufanya miamala na Tigo Pesa. Kushoto ni Meneja wa Wateja Maalum, Mary Rutta na kulia ni Mkuu wa Huduma ya Tigo Pesa, James Sumari.
Meneja wa Wateja Maalum, Mary Rutta akieleza jambo kwa waandishi wa habari katika uzinduzi wa promosheni ya 'Fanya Muamala na Ushinde na Tigo Pesa' jijini Dar es salaam leo, ambapo wateja wa Tigo pesa wana nafasi ya kujishindia hadi shilingi 15 milioni kwa kufanya miamala na Tigo Pesa. Katikati ni Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Kampuni ya Tigo, Hussein Sayed na kulia ni Mkuu wa Huduma ya Tigo Pesa, James Sumari.

Dar es Salaam - Huduma ya fedha ya simu za mkononi inayoongoza nchini, Tigo Pesa leo imetangaza zawadi kemkem kwa wateja wake ambao watajishindia mamilioni ya pesa kupitia promosheni ya ‘Fanya muamala na ushinde na Tigo Pesa’ inayoendeshwa katika msimu huu wa Krismasi na Mwaka Mpya .

Promosheni hiyo itakayodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja itashuhudia washindi watatu wa jumla wakijinyakulia vitita vya TZS 15 millioni, TZS 10 millioni na TZS 5 millioni kila mmoja. Pamoja na hayo, kutakuwa na washindi wa kila siku ambapo mmoja atalamba donge nono la TZS 1millioni, huku wengine wanne wakijinyakulia TZS 500,000 kila mmoja, kila siku.

‘Tunatarajia kupata jumla ya washindi 153 katika kipindi cha mwezi mmoja wa promosheni hii,’ Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed alisema akizindua promosheni hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Wateja watapata nafasi ya kushinda kwa kufanya miamala yoyote kutoka kwa simu zao kupitia Tigo Pesa. ‘Kadri ya unavyofanya miamala mingi zaidi ndivyo unavyojiongezea nafasi ya kushinda ,’ Sayed alifafanua. Hakuna masharti.

“Tunajivunia mchango wetu katika kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za kifedha nchini kupitia Tigo Pesa. Tigo Pesa ni zaidi ya huduma ya kutuma na kupokea pesa. Ni sehemu ya maisha. Kwa hiyo tuna furaha kubwa kuwapa fursa ya kujishindia zawadi hizi nono ambazo zitawawezesha kufurahia msimu hu wa sikukuu huku wakiendelea kufaidika na huduma zetu bora za kidigitali,’ aliongeza.

Zawadi hizi murwa zinakuja kwa nguvu ya mtandao mpana na ulioboreshwa wa Tigo, huku lengo kuu la Tigo likiwa ni kuwasikiliza wateja wake na kuwapa huduma za kisasa zinazoendana na mahitaji yao. Tigo Pesa ni huduma ya fedha ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini yenye mtandao mpana wa mawakala zaidi ya 70,000 waliosambaa kote nchini. Miamala ya takriban TZS 1.7bn inafanyika kupitia Tigo Pesa kila mwezi.

MADABA YAWA MFANO BORA KATIKA KUTATUA KERO YA MAJI KATIKA WILAYA YAO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akikagua mabomba yatakayotumika kusambazia maji kwa mradi wa Maweso akiwa na Mbunge wa Jimbo la Madaba, Joseph Mhagama katika Wilaya ya Madaba, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akikagua ujenzi wa tenki la maji la mradi wa Lolindo na Mbunge wa Jimbo la Madaba, Joseph Mhagama ambao utekelezaji wake unaendelea katika Wilaya ya Madaba, mkoani Ruvuma.
Mhandisi wa Mkoa wa Ruvuma, Jones Kimaro (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso katika kitekeo cha maji ikiwa ni sehemu ya mradi wa Lilondo katika Wilaya ya Madaba, mkoani Ruvuma.
Mradi wa mfano uliotekelezwa na wakazi wa Lilondo, ambao wametumia teknolojia ya kienyeji ya kukusanya maji kwa mabomba kutoka milimani na kuyahifadhi kwenye bwawa walilochimba na kuyasambaza kwa wananchi kupitia mitaro waliyochimba kwa gharama zao wenyewe ili kukabiliana na changamoto ya maji katika kijiji chao.

Airtel yaimarisha mawasiliano kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

$
0
0
Kamishna Generali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kupokea msaada wa simu za mkononi kutoka kampuni ya Airtel Tanzania zitakazotumika kuimarisha mawasiliano ndani ya jeshi hilo kupitia namba ya dharura 114. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano.
Kamishna Generali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akipokea baadhi ya simu za mkononi ambazo zimetolewa na Airtel Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano kupitia namba ya dharura 114 ndani ya jeshi hilo. Simu hizo zitasaidia wananchi wote kutoka mitandao yote watakapopiga katika namba ya dharura 114 na kuhudumiwa kwa haraka wakiwa miko yote.

Kampuni ya Airtel Tanzania imetoa msaada wa simu kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambazo zitatumika kwa ajili ya kurahisisha na kuimarisha mawasiliano ya namba ya dharura 114 wakati wa kuripoti dharura za moto na majanga mbalimbali nchini. Simu hizo zimetolewa kwa mikoa maalumu ya Jeshi la Zimamoto ambapo wateja wa Airtel watapiga bure ili kupata huduma za jeshi hilo.

Akikabidhi simu hizo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya alisema wao kama Airtel wanatambua umuhimu wa Jeshi hilo na wanaamini kuwa wananchi sasa wataweza kupata huduma za Jeshi hilo kwa urahisi kupitia namba hiyo ya dharura.

“Airtel tunatambua umuhimu wa jeshi la zimamoto na uokoaji katika jamii,hivyo tunaamini utoaji wa taarifa za majanga kwa wakati muafaka unarahisisha shughuli za uokoaji na kuzuia kwa kiwango kikubwa hasara ambayo inaweza kusababishwa na majanga hayo katika jamii.

 Alisema kupitia namba hii ya dharura ya 114 na kwau wezeshaji wa kuitumia kwa urahisi na uhakika, Jeshi la Zimamoto litaweza kuwahudumia wananchi kwa haraka wakati wa moto na majanga yanapotokea. Alisema Airtel itaendelea kushirikiana na Jeshi hilo ili kuhakikisha mawasiliano yanafanyika kwa urahisi na haraka ili kulisaidia jeshi la zima moto kuweza kuwafikia wananchi wengi Zaidi kote nchini na kuepusha hasara zinazoweza kutokea wakati wa majanga ya moto na kadhalika.

“Tunataka kuwahakikishia wateja wetu wote kuwa mtandao wa Airtel uko imara kwa kuwa hivi karibuni tumeboresha zaidi mtandao kwa kutumia teknolojia mpya ya U900 katika baadhi ya mikoa ikiwemo hii inayofaidika na huduma ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, hivyo basi tunawaomba muitumie namba hiyo ya dharura vizuri huku pia mkifaidi huduma zetu bora za Airtel ,” alisema. 

Mikoa iliyopokea simu hizo ni pamoja na Ilala, Kinondoni, Temeke, Pwani, Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe, Mwanza, Mara, Shinyanga, Tabora, Simiyu, Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Rukwa, Ruvuma, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Tanga, Mtwara, Lindi, Singida na Bagamoyo.

kwa Upande wake Kamishna Generali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,  Thobias Andengenye aliishukuru Airtel kwa msaada huo wa simu na kusema utaimarisha tendaji wa Jeshi hilo kwani wateja wa Airtel sasa wataweza kupata hudma kwa haraka baada ya kupiga simu.

“Tunashukuru mno na tuna imani kuwa wateja wa Airtel sasa watakuwa na urahisi wa kutufikia kupitia namba 114, tofauti na hapo nyuma,” vilevile Simu hizi zitasaidia wananchi wote wanaotumia mtandao wowote  watakapopiga katika namba ya dharura 114 ili tuwahudumie wa haraka pindi kunapokuwa na dharura au majanga. alisema.

TANZANIA NA CHINA KUSHIRIKIANA KUUKABILI UHALIFU WA KIMATAIFA

$
0
0
Tanzania na China wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika maeneo mbalimbali kama njia mojawapo ya kupambana na uhalifu wa kimataifa ambao umekuwa ukiisumbua dunia. Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya kufanyika mazungumzo kati ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na mgeni wake Naibu Waziri wa China mhe. Zhao Dacheng ambae yuko nchini kwa ziara ya siku nne nchini.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo, Prof.Kabudi ameyataja makosa ya kimataifa ambayo wamekubaliana kuwa ni makosa ya kimtandao,utakatishaji fedha, usafirishaji binadamu na mengineyo ambayo yamekuwa yakiikabili dunia kwa wakati huu.

Prof.Kabudi pia amesema kwamba wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kayika eneo la msaada wa kisheria kwa watu wenye uhitaji ambapo China pia watajifunza kutoka kwa Tanzania katika eneo hilo ambalo Inataka kuwa na sheria yake kama ilivyofanya Tanzania.

Viongozi hao pia wamekubaliana kushirikiana katika eneo la mafunzo ili kuwaongea ujuzi na uwezo watendaji wao kupitia semina za kimataifa au mafunzo maalum ili kubadilidhsna uwezo na uzoefu katika eneo la usimamizi wa sheria nchini. Tanzania na China pia wamekubaliana kushirikiana katika eneo la Mahakama ikiwa ni pamoja na usimamizi na uendeshaji wa Magereza nchini.

Awali akizungumza katika kikao hicho Naibu Waziri wa China Mhe. Dacheng alisema Tanzania ni moja ya nchi marafiki wa dhati wa China urafiki ambao uliasisiwa na viongozi waandamizi wa nchi hizo. Alisema ziara yao nchini inafungua milango mipya ya ushirikiano baina ya China na Tanzania na kuongeza kuwa itazidi kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo.

Amesema anaamini kuwa Wizara yake imedhamiria kuisaidia Tanzania katika sekta ya Sheria ili isonge mbele kama ilivyofanikiwa China na kuongeza kuwa wao pia wataitumia nafasi hiyo kujifunzakatima maeneo ambayo Tanzania imepiga hatua kama eneo la msaada wa sheria kwa watu wake.

Naibu Waziri huyo wa Sheria wa China yuko nchini kwa mwaliko wa Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania Prof. Kabudi, anatarajiwa kutembelea Shule Kuu ya Sheria ya Chio Kikuu chabDar es salaam na Chama cha Wanasheria Tanganyika na Desemba Mosi ataelekea visiwani Zanzibar ambako atakutana na Jaji Mkuu wa Tanzania na viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof.Palamagamba Kabudi wa pili kushoto akizungumza na ugeni wa Naibu Waziri wa Sheria wa China mhe. Zhao Dacheng katika ukumbi wa mikutano jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Sheria wa China mhe. Zhao Dacheng watatu toka kulia na ujumbe wake wakiwa katika ukumbi wa mikutano jijini Dar es salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Kabudi aliekaa katikati akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Sheria wa China mhe. Zhao Dacheng wa pili kushoto wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mazungumzo yao jijini Dar es salaam.

Mkazi wa Iringa ashinda milioni 161 ya M-bet

$
0
0

Mkazi wa Iringa, Alex Kalinga (26) amejishindia kitita cha sh milioni 161 kwa kubashiri kwa usahihi mchezo maarufu kwa ‘Perfect 12’ unaondeshwa na kampuni ya mchezo wa kubahatisha ya M-Bet.

Kalinga alikabidhiwa kitita chake jana na Afisa Habari wa Kampuni ya M-Bet, David Malley kwa kushirikiana na Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Catherine Lamwai.

Malley alisema kuwa Kalinga alifanikiwa kubashiri sahihi jumla ya mechi 12 kati ya 17 na kuwa mshindi wao wa droo ya 17 tokea kuanzishwa kwa mchezo wa Perfect 12.Alisema kuwa serikali imejipatia jumla ya Sh milioni 29 kutoka kiasi hicho cha fedha ambacho ni asilimia 18 kwa mujibu wa sheria.

“Ni faraja kubwa kuona kijana mwenye umri wa miaka 26 akishinda mamilioni ya fedha kwa kutumia kiasi cha She elfu moja tu, hii imedhihirisha kuwa M-Bet ni nyumba ya mabingwa, tunawaomba mashabiki wa soka kuendelea kucheza mchezo wetu ili kujishindia fedha,” alisema Malley.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Kalinga alisema kuwa hakuamini taarifa ya kushinda mchezo huo mara baada ya kupokea simu ya kujulishwa kushinda.

“Nina furaha sana, mimi ni fundi wa kuchomelea mageti ya chuma, sikuwa na kipato kikubwa pale Iringia Mjini, nitaanza kujenga nyumba na kufungua kiwanda cha kuchomelea na nyingine kusaidia familia yangu,” alisema Kalinga.

Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Catherine Lamwai aliwashukuru M-Bet kwa kuendelea vyema na shughuli zake mbali ya kuwazawadia washindi mara kwa mara.
 Afisa Habari wa Kampuni ya M-Bet, David Malley (katikati) akimkabidhi hundi mshindi wa mchezo wa Perfect 12 Alex Kalinga (kulia) ambaye amejishindia kitita cha sh milioni 161. Kuliakushoto ni Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Catherine Lamwai.
Mshindi wa mchezo wa Perfect 12 Alex Kalinga 'akipozi' na mfano wa hundi mara baada ya kukabiziwa jana. Kalinga alijishindia kitita cha sh milioni 161.

AZAM TV KUONYESHA MASHINDANO YA CECAFA

$
0
0
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Azam Media akizungumza na waandishi akiwaeleza waandishi wa Habari , namna watanzania watakavyopata nafasi ya kuangalia mashindano ya Cecafa moja moja, baada ya kuingia mkataba na Cecafa kufanya hivyo. Kulia kwake ni Mkuu wa uzalishaji wa vipindi Charles Hillar, na kushoto ni meneja Mauzo na Masoko John Mbele.

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii. 

Shirikisho la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati, (Cecafa), limeingia mkataba na kampuni ya Azam Media kuonyesha mechi zote za Kombe la Challenge mwaka huu zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi mapema mwezi ujao. Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa Azam, Tido Mhando amesema mkataba Huu utawezesha watanzania kupata uwezo mkubwa wa kandanda na pia tunataka kupata uwezo mkubwa zaidi na kusaidia kifanikisha soka ya Tanzania.

"Bado tunadhamira kubwa ya kuhakikisha ari hii inasambaa hadi katika nchi za jirani, mara nyingi tunakuwa tunajilaumu kuwa hatujapiga hatua, tunataka kuhakikisha tunakuwa chachu ya mafanikio" amesema Mhando. Amesema, watatoa matangazo yao katika mashindano hayo ambayo ni kongwe zaidi nchini kuliko mengine yotote kwa lugha ya kiswahili na kiingereza na hata kwa lugha mbali mbali hasa hasa Rwanda na Uganda.

"Watanzania wajiandae kupata burudani ya kutosha na inayowastahili kwa kuhakikisha tunawafikishia matangazo yetu ya Cecafa Challenge kwa ubora wa hali ya juu. Aidha amesema wanamatumaini makubwa kuwa timu za Tanzania na Zanzibar Zitafanya vema na hatimae kufudhu katika hatua za fainali na mshindi atabaki nchini..

Ameongeza kuwa hawataishia kwenye mashindano ya Cecafa tu, watafanya maonyesho makubwa katika mashindano ya Kagame cup." Naomba tushirikiane ili kuhakikisha mashindano haya yanapata hadhi yake inayostahili. Mashindano ya Cecafa yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi nchini Kenya kuanzia Desemba 3 katika viwanja vya Machakos na Kakamega huku timu tisa zikitarajiwa kushiriki baada ya timu ya Zimbabwe kujitoa.

Timu zitakazoshiriki ni Kenya, Rwanda Libya, Tanzania, Zanzibar, Uganda, Burundi, Ethiopia na S.Sudan

MAWAZIRI WA UGANDA WATEMBELEA MIGODI YA WACHIMBAJI WADOGO GEITA

$
0
0
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kushoto) na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Madini wa Uganda, Lokeris Peter (kushoto) wakitembelea mgodi wa Dhahabu wa Blue Reef uliopo Rwamgasa. Wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Lughumbi na kulia ni mmiliki wa mgodi huo, Christopher Kadeo.

Mawaziri Wanne kutoka Uganda wakiongozwa na mwenyeji wao Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo Agosti 29, 2017 walitembelea migodi ya dhahabu ya Mkoani Geita inayomilikiwa na Watanzania. Miongoni mwa migodi iliyotembelewa ni Mgodi wa Dhahabu wa Blue Reef uliopo Rwamgasa, Mgodi wa Dhahabu wa Busolwa Gold Mine Project uliopo Nyarugusu na Kituo cha Mfano cha Uchimbaji Madini ya Dhahabu cha Tan Discovery kilichopo Rwamgasa.

Mawaziri hao waliwasili nchini Tanzania Agosti 27, 2017 kwa ajili ya zira ya siku mbili ya kujifunza juu ya Usimamizi wa Sekta ya Madini hususan suala la Uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo wa Madini. Kwa mujibu wa Naibu Waziri Nyongo, Mawaziri hao wametembelea migodi hiyo ili kuona namna gani migodi hiyo inaendesha shughuli zake na namna ambavyo serikali imekuwa ikiwasaidia kuhakikisha wanakuwa na uchimbaji madini wenye tija. “Wamekuja kujifunza, kuangalia Sera zetu, Sheria zetu na mchango wa Serikali katika kuwasaidia wachimbaji wadogo,” alisema.

Alisema walipendekeza kutembelea migodi inayomilikiwa na Watanzania ili kujionea namna ambavyo wazawa wanavyoendesha shughuli za uchimbaji madini ikiwa na pamoja na kuzungumza nao ili kupata uzoefu wa uendeshaji wa shughuli husika na kubaini ushirikiano uliopo baina yao na Serikali.

Akizungumza kwa niaba ya Mawaziri wa Uganda, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Madini wa Uganda, Lokeris Peter alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi Barani Afrika zilizopiga hatua kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini hususan eneo la Uchimbaji Mdogo wa Madini ikilinganishwa na nchi zingine walizotembelea.

"Uamuzi wa kufanya ziara nchini humu unafuatia uzoefu wa muda mrefu wa Tanzania kwenye masuala ya uchimbaji wa madini hususan namna ambavyo Tanzania imeweza kurasimisha suala la uchimbaji mdogo," alisema Waziri Peter.

Awali kabla ya kuwasili Mkoani Geita, ujumbe huo wa Mawaziri kutoka Uganda; Agosti 28, 2017 ulikutana na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ambapo ulielezwa masuala mbalimbali yanayohusu sekta husika ikiwemo Sera, Sheria na Kanuni za Madini pamoja na masuala yanayohusu Wachimbaji Wadogo wa madini.

Mawaziri kutoka Uganda waliofanya ziara hiyo ni Waziri wa Nchi- Madini, Lokeris Peter, Waziri wa Nchi- Mambo ya Ndani, Obiga Kania, Waziri wa Nchi- Mamlaka ya Mji Mkuu wa Kampala,  Namugwanya Bugembe na Waziri wa Nchi- Masuala ya Uchumi, Dkt. Kasirivu Atwooki.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) akiongozana na Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Madini nchini Uganda, Lokeris Peter (kulia kwake) mara baada ya kuwasili kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Busolwa Gold Mine Project uliopo Nyarugusu.
Mawaziri kutoka Uganda wakiwa pamoja na mwenyeji wao, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo walipotembelea mgodi wa Dhahabu wa Blue Reef uliopo Rwamgasa ili kujionea shughuli zinavyoendeshwa mgodini hapo.
Mawaziri kutoka Uganda wakimsikiliza mmiliki wa Mgodi wa Dhahabu wa Blue Reef, Christopher Kadeo (hayupo pichani) baada ya kutembelea eneo (shimo) linalochimbwa Dhahabu. Kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi- Mambo ya Ndani, Obiga Kania, Waziri wa Nchi- Masuala ya Uchumi, Dkt. Kasirivu Atwooki, Waziri wa Nchi- Madini, Lokeris Peter na Waziri wa Nchi- Mamlaka ya Mji Mkuu wa Kampala, Namugwanya Bugembe.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri kutoka Uganda mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.

waliokutwa na madini ya milioni 500, wahukumiwa kulipa faini ya milioni 3 au jela miaka miwili

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu watanzania  watatu wanaofanya biashara ya madini kulipa faini ya sh. Milioni tatu ama kwenda jela miaka miwili baada ya kupatikana na hatia kwa makosa ya kusafirisha dhahabu ya zaidi ya milioni 507. Aidha mahakama imetaifisha madini hayo ya dhahabu yenye uzito wa kilo 6.242 yenye thamani ya Sh 507,347,241.11 kuwa mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wafanyabiashara wa madini, wakitoka mahakamani baada ya kupatikana na hatia na kuhukumiwa kulipa faini ya sh. Milioni Tatu au kwenda jela miaka miwil
Hatua hiyo imekuja baada ya washtakiwa hao Mashaka Lucas, Jafarri Hussein na mwenzao, Akifu Mohamed waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kusafirisha madini hayo bila ya kuwa na vibali kukubali makosa hayo na kutiwa hatiani.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu,Huruma Shaidi.  Akisoma hukumu hiyo  Hakimu Shaidi amesema, mahakama imezingatia taarifa kutoka upande wa mashtaka kuwa washtakiwa ni wakosaji kwa mara ya kwanza na wamekubali makosa ingawa mshtakiwa Mashaka na Jafarri wanaleseni za kuendesha biashara hizo lakini suala ni kukutwa na madini hayo na kuyasafirisha bila ya kuwa na vibali.

 “Lengo la mahakama siyo kumfanya mtu aondoke katika kile alichokifanya bali ajutie" Amesema Hakimu Shaidi.

Kufuatia hayo, mahakama imemuamuru kila mshtakiwa kulipa faini ya Sh milioni 1.5 katika kila kosa hivyo kila mshtakiwa atapaswa kulipa Sh milioni 3 na iwapo watashindwa watatumikia kifungo cha miaka miwili gerezani. Kuhusu gari aina ya Noah walilokamatwa nalo washtakiwa hao siku ya tukio  Bandarini eneo la Azam, Hakimu Shaidi alisema mahakama inashindwa kutoka amri kwa sababu upande wa  mashtaka haukupeleka kadi ya gari hilo wala gari lenyewe mahakamani hapo kama kielelezo.

Kabla ya hukumu kusomwa, Wakili wa Serikali Jehovaness Zacharias aliiambia mahakama kuwa hawana kumbukumbu za makosa ya nyuma za washtakiwa Ila aliomba wapewe adhabu Kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Pia aliomba mahakama itoe oda ya kutaifishwa kwa madini pamoja na gari aina ya Noah walilokamatwa nalo washtakiwa hao Bandarini eneo la Azam. Hatua hivyo Mawakili wa washtakiwa hao,Hadson Ndusyepo na Evodius Mtawala waliiomba mahakama iwatazame kwa jicho la huruma washtakiwa hao.

Alidai kuwa washtakiwa hao wanajihusisha na shughuli za madini katika maisha yao , kujipatia kipato na wana leseni halali. Kwa kutokuelewa utaratibu wa madini ndio wamejikuta katika tatizo hilo, ndio maana hawakupenda kuisumbua mahakama wakakubali ili waweze kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa Taifa.

Katika kesi ya msingi,washtakiwa Jafarri na Akifu  wanakabiliwa na shtaka la kukutwa na vipande vitano vya madini ya dhahabu vyenye uzito wa kilo 6.242 vyenye thamani ya Sh 507,347,241.11bila ya kuwa na kibali.

Pia washtakiwa Mashaka, Jafarri na Akifu wakiwa Bandarini eneo la Azam wanadaiwa kuyasafirisha madini hayo bila ya kuwa na vibali.

VIDEO: KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI IDARA KUU MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

WAFANYABIASHARA UFARANSA WATUA TANZANIA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA

$
0
0
Chemba ya viwanda, biashara na kilimo nchini (TCCIA ) imepokea ugeni wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa wenye lengo la kujadili na kupanua mianya ya biashara kati ya Tanzania na Ufaransa Ugeni huo kutoka nchini ufaransa umeambatana na wafanyabiashara pamoja na wamiliki wa makampuni makubwa ambapo lengo kuu la mkutano ni kutaka kutengeneza urafiki wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili na kubadilishana uzoefu wa kibiashara pamoja kupanua fursa za uwekezaji baina ya Tanzania na Ufaransa
Makamu wa Rais wa TCCIA Ndg. Octavian Mshiu (katikati), kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TCCIA Ndg. Gotfid Muganda,pamoja na wafanyabiashara kutoka ufaransa wakati wa mkutano
Makamu wa Rais wa TCCIA Bwana Octavian Mshiu amesema Tanzania imekuwa nchi yenye bahati ya kutembelewa na wafanyabiashara wakubwa kutoka nchi mbalimbali na hii ni kutokana na Tanzania kuwa na sifa kubwa kimataifa kama nchi yenye malighafi nyingi za kibiashara 
Makamu wa Rais wa TCCIA Ndg. Octavian Mshiu akisisitiza jambo wakati wa Mkutano na wafanyabishara kutoka ufaransa.Aidha Mshiu amesema kuwa ziara hii inatoa fursa nyingi kwa wafanya biashara nchini kutanua biashara zao kwenda kimataifa zaidi.Mshiu amewataka wafanyabiashara wakubwa na wadogo kutumia ujumbe huu wa wafanyabiashara kutoka Ufaransa kama njia ya kukuza biashara zao kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla. 

WCF YAPATA HATI SAFI KATIKA UKAGUZI WA TAARIFA YA FEDHA ULIOFANYWA NA CAG

$
0
0

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) umepata hati safi katika taarifa ya hesabu zake za fedha katika kipinmdi cha mwaka 2015-2016 ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu kuanzishwa kwake.

Katika taarifa hiyo mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2016 (mwaka wa kwanza tangu kuaza kufanya kazi zake), thamani ya Mfuko ilifikia shilingi bilioni 65.68 na mfanikio haya yaliweza kufikiwa kutokana na ubunifu na ushirikiano mkubwa kati ya Mtendaji Mkuu wa Mfuko na Bodi ya Udhamini, Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Mfuko huo, Bw.Bezil Kwala, aliwaambia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wadau wa Mfuko huo unaoingia siku yake ya pili nay a mwisho kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha, wakati akiwasilisha taarifa hiyo ya fedha leo Novemba 30, 2017.
Amesema Mfuko umekuwa ukiaandaa hesabu zake kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya uaandaji wa hesabu za fedha na kwa mujibu wa sheria CAG ndiye mwenye mamlaka ya kufanya ukaguzi na Hati Safi ni uthibitisho wa taarifa ya fedha za Mfuko kuonyesha hali halisi na kutokuwa na dosari ya aina yoyote.
Amesema katika ukaguzi huo, CAG alishirikiana na kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PwC). Mwakilishi wa kutoka Ofisi ya CAG, Bw…….. amethibitishia wajumbe usahihi wa taarifa hiyo ya fedha ya WCF.
Mkutanmo huo ambao umeanza Novemba 29, 2017 na kubeba kauli mbiu isemayo, "Mafao ya Fidia: Haki ya Mfanyakazi na chachu katika kukuza uchumi wa viwanda”, pia ulipokea taarifa ya mipango ya uwekezaji ambapo Bw. Kwala aliwaambia wajumbe kuwa, katika kipindi kati ya mwaka 2017/18 – 2021/22, Mfuko umepanga kuwekeza kwenye miradi mbalimbali itakayoleta faida kwa mujibu wa tathmimi za kitaalamu zitakazofanyika.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akifafanua baadhi ya mambo wakati viongozi wa Mfuko walipokuwa wakiwasilisha taarifa za utendaji wake kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadu kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC, jijini Arusha leo Novemba 30, 2017.

 Baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Idara wa WCF wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, akizungumza
 Mkurugenzi wa Fedha WA WCF, Bw.Bezil Kwala, akiwasilisha ripoti ya fedha ya Mfuko kwa mwaka wa 2015-2016.
 Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa Ofisi ya Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Johanes Joel Kisiri, akisikiliza uwasilishaji wa taarifa hiyo ya fedha.
 Mkuu wa Kitengo cha Sheria cha WCF, Bw.Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu Sheria juu ya kuanzishwa kwa Mfuko na jinsi unavyofanya kazi zake. Pamoja na mambo mengine Bw. Siyovelwa aliwaambia wajumbe kuwa,   Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoazishwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura Na. 263 (Marejeo ya 2015) na kuanza kazi rasmi tarehe 1 Julai 2015. Lengo la kuazishwa kwa Mfuko ni kushughulikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi waliopo katika sekta rasmi (Binafsi na Umma) Tanzania bara ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DKT SHIKA KUTAMBULISHWA RASMI USIKU WA 900 ITAPENDEZA DAR LIVE MBAGALA

$
0
0
Dokta Louis Shika akiwa na meneja wake Catherine Kahabi wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna tamasha hilo la usiku wa 900 itapendeza zaidi litakavyokuwa siku hiyo na kuwataka watu kuhudhuria na kumsikiliza bilionea huyo atazungumza nii juu ya maisha yake kiujumla pale Dar live,leo katika ukumbi wa habari maelezo Jijini Dar es Salaam.

Na Agness Francis Blogu ya Jami.
Dokta Louis Shika ambaye ni mshindi wa mnada wa uuzaji wa Nyumba za Lugumi awakaribisha wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kushiriki tamasha la usiku wa 900 itapendeza ambapo atazungumzia maisha yake kiujumla toka alipoanzia hadi mpaka sasa alipofikia.

Meneja wa Dkt Shika Catherine Kahabi amesema hayo leo Jijini Dar es salaam katika ukumbi wa habari maelezo ambapo Tamasha hilo limeandaliwa na udhamini wa Global tv ambapo mgeni rasmi atakuwa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Rawrence Kego Masha.

Aidha amesema kuwa lengo ni kutaka kumtambulisha rasmi Dkt Shika ili kumuweka katika muonekano wa kibilionea na akiwa kama miongoni mwa watu walioshika umaarufu mkubwa kwa muda mfupi hapa nchini

Hata hivyo bilionea huyo amemalizia kwa kuwataka wakazi wa Dar es Salaam kuhudhuria Tamasha hilo ambalo litasindikizwa na Burudani mbalimbali ikiwemo wanamuziki na vikundi vya vichekesho hapa nchin.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MENEJA WA COCA COLA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Coca Cola Afrika Mashariki Bw. Ahmed Rady (kushoto) ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Coca Cola Afrika Mashariki Bw. Ahmed Rady (kushoto),Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola nchini Bw. Basil Godzios na viongozi wengine wa kampuni hiyo mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

FINLAND YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA BILIONI 75 KUENDELEZA MISITU, MAFUNZO YA UONGOZI NA UBUNIFU

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

Serikali ya Tanzania na Finland zimetiliana saini mikataba mitatu yenye thamani ya Euro milioni 28.8 sawa na Shilingi bilioni 75 kwa ajili ya kuendeleza misitu, ubunifu na masuala ya uongozi.

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa mikataba hiyo, Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James amesema, msaada huo kutoka Finland umetolewa ili kuendeleza  uwezo wa viongozi na kufanya maamuzi sahihi yenye tija kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa, mradi ambao unasimamiwa na Taasisi ya Uongozi, ambapo kiasi cha Euro milioni 9.90 zimetolewa kuendeleza mradi huo.

Aidha Serikali ya Finland imetoa kiasi cha Euro milioni 8.95 kwa mradi wa  kuiimarisha mfumo wa ubunifu nchini kwa kutengeneza mazingira rafiki kwa wabunifu ili kuweza kubuni na kuendeleza ubunifu wao na kuchochea ukuaji wa viwanda. Bw. James alisema fedha hizo zitatumika kuwasaidia wabunifu kwa kuwapatia vifaa na msaada wa kitaalamu ili kuyaendeleza mawazo yao na kuyafanya yawe ya kibiashara na kuweza kusaidia kubadili mawazo hayo kuwa viwanda. 

“Fedha hizi zitasaidia kutatua changamoto katika viwanda vilivyopo nchini ili vifanye kazi kwa ufanisi kwa kuwaunganisha wanataaluma mbalimbali nchini, ikiwa ni pamoja na wabunifu wachanga, wataalamu kutoka vyuoni, wataalamu kutoka Serikalini na Sekta binafsi” Alisema Bw. Doto JamesEneo lingine lililonufaika na msaada huo ni programu ya misitu, ambayo imepatiwa Euro milioni 9.95 kwa lengo la utuzaji wa misitu na uongezaji thamani ya mazao yatokanayo na misitu ili kuongeza kipato kwa Wananchi, kupunguza umasikini na kulinda mazingira.

Katibu Mkuu amemshukuru balozi wa Finland Nchini, Mhe. Pekka Hukka kwa msaada walioutoa na kwa kuunga mkono shughuli za maendeleo za Serikali, na kuongeza kuwa Finland wamekuwa wakifadhili miradi mbalimbali nchini, ukiwemo mradi wa kilimo biashara Mkoani Lindi na Mtwara (LIMAS), uliogharimu Euro milioni 9, Mradi wa kuimarisha usambazaji na upatikanaji wa umeme wa uhakika Jijini Dar es Salaam, uliogharimu Euro milioni 25, na Programu ya maboresho ya Serikali za Mitaa, Euro milioni 10.5

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja aliiishukuru Serikali ya Finland kwa kuendelea kuisaidia Taasisi hiyo.
‘Hii ni mara ya tatu Finland wamekuwa wakitusaidia kuendeleza jitihada zilizoanzishwa na Serikali yetu ambapo awamu ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2012 ambapo walitupatia Euro milioni 7, mwaka 2014 Euro milioni 12 na sasa wametupatia Euro milioni 9.90 huu ni msaada mkubwa’ alisema Profesa Semboja.

Aidha kwa upande wake Balozi wa Finland Bw. Pekka Hukka, aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendeleza ushirikiano na Serikali yake, na kuongeza kuwa msaada huo ni muhimu sana katika kutimiza malengo ya maendeleo ya nchi.Amesema msaada huo ukitumika ipasavyo hasa katika kuendeleza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu utasadia kuongeza ajira na kuongeza pato la Taifa.

Ameitaka Serikali kupitia Wizara ya nishati,  kushirikiana na sekta binafsi na kuitumia fursa hiyo ya kuboresha misitu ili kuiongezea nchi mapato zaidi yatakayotokana na makusanyo ya kodi.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) akionesha kalamu aliyozawadiwa na Balozi wa Finland Bw. Pekka Hukka (kushoto) ambayo imetengenezwa kwa mbao, akionesha uzalendo wa matumizi ya misitu. Kutoka kulia ni Kamishna wa Bajeti Wizara ya Fedha na Mipango Bibi. Mary Maganga na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. John Rubuga.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James (kulia) akitia saini moja kati ya mikataba mitatu yenye jumla ya shilingi bilioni 75 kama msaada kwa Tanzania, Kushoto ni Balozi wa Finland Bw. Pekka Hukka kwa pamoja wakisaini mikataba hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) akibadilishana mkataba na Balozi wa Finland Bw.Pekka Hukka. Mkataba wa kwanza wa Euro milioni 9.9 ni kwa ajili ya kusaidia Taasisi ya Uongozi, wa pili wa Euro milioni 8.9 kwa ajili ya kuimarisha mfumo wa ubunifu na watatu wa Euro milioni 9.5 ni kwa ajili ya program ya misitu.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) pamoja na Balozi wa Finland Bw. Pekka Hukka (kushoto) wakionesha moja ya mikataba mara baada ya kumaliza kutia saini mikataba hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS Nchini akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana(wa pili kulia) alipowasili kwenye katika Ukumbi wa  Chuo cha Mipango Dodoma tayari kwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. Mkutano huo unafanyika kwa siku moja leo 30 Novemba, 2017 hapa mjini Dodoma. 

Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara (TPS SACCOS) kimefanya Mkutano wake Mkuu wa Tano wa Mwaka 2017 kwa ufanisi Mkoani Dodoma.
Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini,  Miyuji Dodoma leo Novemba 30,  2017.

Akiongea katika Mkutano huo Kaimu Naibu  Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw.  Charles Malunde kwa niaba ya Naibu Mrajisi ametoa angalizo kwa Vyama vya ushirika nchini kutokufanya biashara za Kibenki nje ya lengo la kuanzishwa kwa SACCOS.

Amesema kuwa katika  vyama vingi vya ushirika uzoefu umeonesha kuwa wakishakuwa na mtaji mkubwa huwa na wazo la kuanzisha Benki, ametoa angalizo kuwa masharti ya uendeshaji wa Benki ni tofauti kabisa na masharti ya uendeshaji wa vyama vya ushirika hivyo ameziasa Saccos zote nchini kutafakari vyema kabla ya kubadili vyama hivyo na kuwa Benki.
“ Ukianzisha Benki huduma za Saccos zitafifia, kumbukeni wateja wa Saccos ni pamoja na wale wa hali ya chini kabisa ikiwa benki hawa huenda mkawaacha” alisisitiza  Kaimu Mrajis Malunde.

Aidha,  amewaasa Magereza SACCOS pamoja na Saccos zote nchini kufanya shughuli zake kwa kufuata sheria  lakini pia kuheshimu na kusikiliza sana wenye mali ambao ni wanachama wa vyama hivyo vya ushirika.
Aliongeza kuwa kwakuwa Mkutano huu utahusisha uchaguzi wa wajumbe wa Bodi Bw. Charles Malunde pia amewaasa Wajumbe wa Mkutano Mkuu kuwa makini katika uchaguzi huo kwa kuchagua watu wenye weledi na wenye mapenzi ya dhati na ushiriki wao ili waweze kutimiza majukumu yanayokusudiwa.

Pia amewataka wagombea wote wanaowania nafasi mbalimbali za chama hicho kujiuliza mambo manne kama ifuatavyo;- Je, watumishi wa Jeshi la Magereza wote ni wanachama? na mnaweka Mkakati gani?, Je wanachama wanaweka akiba za kila mwezi?, Mnajiendesha kisayansi? Mtu akitaka mkopo anapata baada ya muda gani? na swali la mwisho uhusiano na vyama vingine vya ushiriki, SCULT, nje ya nchi ukoje?.

Awali akitoa taarifa ya Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara (TPS SACCOS), Mwenyeki wa Bodi ya Magereza Saccos, DCP. Gideon Nkana amesema kuwa Idadi ya wanachama imeongezeka hadi kufikia wanachama zaidi ya 13,000 ikiwa na mtaji wa zaidi ya bilioni 18.
Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana(katikati) akimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS kuingia Ukumbini tayari kwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara(kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara ulifanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WCF YAPATA HATI SAFI KATIKA UKAGUZI WA TAARIFA YA FEDHA ULIOFANYWA NA CAG

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akifafanua baadhi ya mambo wakati viongozi wa Mfuko walipokuwa wakiwasilisha taarifa za utendaji wake kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadu kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC, jijini Arusha leo Novemba 30, 2017.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) umepata hati safi katika taarifa ya hesabu zake za fedha katika kipinmdi cha mwaka 2015-2016 ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu kuanzishwa kwake.
Katika taarifa hiyo mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2016 (mwaka wa kwanza tangu kuaza kufanya kazi zake), thamani ya Mfuko ilifikia shilingi bilioni 65.68 na mfanikio haya yaliweza kufikiwa kutokana na ubunifu na ushirikiano mkubwa kati ya Mtendaji Mkuu wa Mfuko na Bodi ya Udhamini, Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Mfuko huo, Bw.Bezil Kwala, aliwaambia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wadau wa Mfuko huo unaoingia siku yake ya pili nay a mwisho kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha, wakati akiwasilisha taarifa hiyo ya fedha leo Novemba 30, 2017.
Amesema Mfuko umekuwa ukiaandaa hesabu zake kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya uaandaji wa hesabu za fedha na kwa mujibu wa sheria CAG ndiye mwenye mamlaka ya kufanya ukaguzi na Hati Safi ni uthibitisho wa taarifa ya fedha za Mfuko kuonyesha hali halisi na kutokuwa na dosari ya aina yoyote.
Amesema katika ukaguzi huo, CAG alishirikiana na kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PwC). Mwakilishi wa kutoka Ofisi ya CAG, Bw…….. amethibitishia wajumbe usahihi wa taarifa hiyo ya fedha ya WCF.
Mkutanmo huo ambao umeanza Novemba 29, 2017 na kubeba kauli mbiu isemayo, "Mafao ya Fidia: Haki ya Mfanyakazi na chachu katika kukuza uchumi wa viwanda”, pia ulipokea taarifa ya mipango ya uwekezaji ambapo Bw. Kwala aliwaambia wajumbe kuwa, katika kipindi kati ya mwaka 2017/18 – 2021/22, Mfuko umepanga kuwekeza kwenye miradi mbalimbali itakayoleta faida kwa mujibu wa tathmimi za kitaalamu zitakazofanyika.
“Maeneo tuliyoyaanisha katika uwekezaji kwenye sekta ya viwanda ni pamoja na kiwanda cha Grape Processing Factory kwa ushirikiano kati ya  GEPF na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, kiwanda cha Madawa mkoani Simiyu kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Kiwanda cha Morogoro Canvas Mills kwa kushirikiana na mifuko ya WCF, NSSF, PSPF, GEPF, na LAPF”. Alifafanua.
Akifafanua zaidi kuhusu umuhimu wa Mfuko kuwekeza, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba alisema, fedha zitokanazo na michango ya Wanachama ni kidogo ukilinganisha na mahitaji halisi ya ulipaji Mafao ya fidia na kwa hali hiyo, ni muhimu Mfuko kuwekeza ili kupanua wigo wa kuongeza mapato na hivyo kuendelea kutoa Mafao ya Fidia bila ya shaka yoyote.
 Baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Idara wa WCF wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, akizungumza.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images