Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

REPOA YAZINDUA MATOKEO YA NA FAIDA ZA UTUMAJI WA FEDHA KWA MTANDAO KATIKA KUMUWEZESHA MWANAMKE KIUCHUMI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la uwezeshaji wa kiuchumi nchini(NEEC),Bengi Issa akizungumza wakati alipokuwa akifungua Warsha ya Faida za kumuwezesha Mwanamke kiuchumi kupitia mpango wa matumizi ya fedha kwa njia ya mitandao ya simu iliyofanyika katika ukumbi wa Tasisi ya utafiti nchini REPOA Jijini Dar es Salaam leo kwa kushirikiana na IDRC na TASAF.
Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya utafiti ya REPOA ,DK .Donald Mmari akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ili aweze kufungua Warsha ya Faida za kumuwezesha Mwanamke kiuchumi kupitia mpango wa matumizi ya fedha kwa njia ya mitandao ya simu
Muwakilishi wa tasisi ya IDRC Kutoka nchini Canada ,Dr Arjan De Haan akizungumza na na wadau waliofika katika warsha hiyo namna taasisi yake ilivyohusika katika tafiti za kumuwezesha mwanamke kiuchumi kupitia mtandao wa simu.
Mtafiti kutoka Tasisi ya Utafiti ya REPOA , Dr.Abel Kinyondo akizungumza na wadau walioshiriki Warsha ya Faida za kumuwezesha Mwanamke kiuchumi kupitia mpango wa matumizi ya fedha kwa njia ya mitandao ya simu ambapo alipata fursa ya kuwaeleza wadau faida na changamoto ya huduma hiyo katika mradi wa TASAF.


Kampuni ya Chai Bora yainunua kampuni ya Dabaga

$
0
0
Katika kutekeleza sera ya uwekezaji nchini ili kuendana na kasi ya serikali ya kuwa na Tanzania ya Viwanda ifikapo mwaka 2025, kampuni ya Chai Bora imeinunua kampuni ya Dabaga iliyokuwa ikitamba na bidhaa za kuongeza ladha za vyakula kama vile Dabaga tomato sauce , Pilipili Mbuzi, Mango pickle na bidha nyinginezo.

Kampuni ya Chai Bora imekuwa ikifanya shughuli zake hapa nchini tangia mwaka 1990, Chai Bora inaogoza kama chata ya kuzalisha majani ya chai, Ikijikita zaidi katika uzalishaji wa bidhaa kama vile majani kama vile Black Tea, Green Tea pia Kahawa aina ya Café Bora. Kwa kuwa imeanza kazi tangia mwaka 1990 hadi sasa ni takribani miaka 27 inaashiria ukuaji katika sekta husika ya bidhaa za Chai . Katika hiyo miaka 27 Chai Bora imeinunua kampuni ya Dabaga, imeongeza uzalishaji wa bidhaa tofauti na imeboresha kiwanda cha Dabaga Iringa na teknolojia za kisasa.
Uwekezaji huo ambao umehusisha teknolojia za kisasa na mitambo ya kisasa zaidi ni wazi kuwa itaongeza ufanisi kwenye uzalishaji wa bidhaa husika na kusukuma ongezeko la ajira nchini. Kupitia uzalishaji huo kwa sasa kiwanda hicho kimetoa ajira ya moja kwa moja na ajira isiyokuwa ya moja kwa moja kwa wakazi wa kijiji cha Ikokoto cha wilayani Ilula, Iringa. Wakulima ambao wanaojihusisha na shughuli za malighafi za viwanda kama hicho hasa wakulima, wasambazaji wa bidhaa za kilimo pamoja na watoa huduma wengine kama vile kampuni za ulinzi, usafi na hata watoa huduma za vyakula nao watanufaika na uwekezaji huo.

Mkurugenzi wa Chaibora, Mr.Kapila Mr.Kapila Ariyatilakakaalisema wakulima watanufaika kwa kuuza mazao yao hasa nyanya kwa kuwa kwa sasa kiwanda hicho kinahitaji nyanya tani 300 hadi 400 kwa mwezi. "Hii inaashiria kuwa wakulima wa nyanya wa ndani na nje ya Iringa watanufaika na uwepo wa kiwanda hicho hasa kwa kuuza bidhaa zao humo" anasema Mr.Kapila Ariyatilaka. Anasema wasambazaji wanaojihusisha na bidhaa za kilimo nao wamepata mwanya wa kuuza bidhaa zao na hasa wanaweza kununua kwa wakulima na kisha kuuza kwenye kampuni hiyo na hivyo kuongeza wigo wa ajira.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI SINGIDA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenuyekiti wa CCM wa Mkoa wa Singida, Martha Mlata baada ya kuwasili Ikulu Ndogo ya Singida Novemba 29, 2017. Kesho Mheshimiwa Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya Chuo Kikuu Huria chaTanzania yatakayofanyika mjini Singida. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kuila) wakimsikiliza mwimbaji wa Kwaya ya Africa Inland Church Tanzania, Loice Jonathan (kushoto) baada ya kuwasili kwenye Ikulu ndogo ya Singida Novemba 29, 2017. Kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yatakayofaanyika mini Dodoma. Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Dkt. Ndugulile kushiriki mbio za Kigamboni Marathoni, Disemba 2 Mwaka huu.

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza wakati akiwahamasisha wakazi wa Dar es Salaam kufika katika mbio za Kigamboni Marathon.

Na Agness Francis, Globu ya Jamii

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile, awataka wakazi wa wilaya ya Kigamboni pamoja na wananchi wengine kutoka maeneo mbali mbali kujitokeza kwa wingi katika kushiriki tamasha la Mbio la Kigamboni Marathon, ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika kwa Kigamboni.

Dkt. Ndugulile amesema hayo leo katika Ofisi zake Jijini Dar Es Salaam kuwa mbio hizo ambazo huleta manufaa kwa mwanadamu ambazo hujenga afya na mwili pamoja na kukutana na watu mbali mbali wapya na kubadilisha mawazo ili kuleta mafanikio katika Wilaya hiyo mpya. amesema mbio hizo za Kigamboni Marathoni zitafanyika siku ya jumamosi Disemba 2 mwaka huu kuanzia saa 12 asubuhi katika Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Mbio hizo zenye kilomita 21,10 hadi 5 zitakazoanzia darajani,feri kuelekea kibuguni hadi kumalizikia katika ofisi za afisa wilaya ya kigamboni .

Pia amemalizia kwa kusema kuwa wanachi waendelee kujitokeza katika zoezi zima la kujaza fomu ambazo zinapatikana katika ofisi za Mkuu wa wilaya wa Kigamboni ili kushiriki mbio hizo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  na Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile akipokea fulana kw ajili ya kushiriki Mbio za Kigamboni Marathoni 

Mwanza mko tayari? Her initiative inakuletea PANDA msimu wa nne

$
0
0
Mwanza mko tayari? Her initiative inakuletea PANDA msimu wa nne "Innovation in everything", (tamasha la ujasiriamali , uvumbuzi na ajira kwa wanafunzi wa kike vyuo  vya Sauti, Cbe, Btc, Feta, Bugando)  litakalofanyika katika ukumbi wa  M 12 Chuo kikuu cha St Agustine Sauti Mwanza.Tarehe 2 December 2017 kutakua na waongeaji , muziki zawadi na selfies zakutosha Mtag rafiki  aliye ndani ya Rock city Mwambie hii si ya kukosa @her_initiative @her_initiative @Kent_reen  Kwa mahitaji ya meza za maonyesho ya bidhaa na Tshirt piga simu (0756540156/0654359701)
Ukija na mwenzako hakika itapendeza
#hercash
#herinnovation
#pandanauvumbuzi

Democratised and Rebranded Slavery!

Maonesho ya Utalii wa Tanzania Saudi Arabia yalivyofana

$
0
0

Maonyesho ya Utalii wa Tanzania yalivyofanyika mjini Riyadh nchini Saudi Arabia kwa watu mbalimbali kutembelea kwenye maonyesho hayo yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia. Aidha Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza yupo nchini Tanzania kwa ajili ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Maonyesho yakiendelea kwa wageni mbalimbali kuelezewa namna ya vivutio vya utalii wa Tanzania.Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza kushoto akiwa na mke wake, Maimuna Mgaza, wakiwa kwenye maonyesho hayo ya Utalii.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza mwenye suti nyeusi mkono wa kushoto akijadiliana jambo na wageni wake waliotembelea katika maonyesho ya utalii yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini hapa. 

Hapa maonyesho ya chakula yakiendelea mjini Riyadh, nchini Saudi Arabia.


Wananchi Jijini Mwanza wapatiwa Tiba ya Viungo na Ushauri Bure


MHE MWANJELWA AWATAKA WAJUMBE WA JUMUIYA ZA CCM KUCHAGUA VIONGOZI WAADILIFU NA WACHAPA KAZI

$
0
0
Wajumbe wa Jumuiya mbalimbali za Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kuchagua viongozi waadilifu, weledi na wenye maono ya kuziongoza Jumuiya hizo ila kuendana na kasi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Mbeya uliokuwa na Ajenda ya uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya hiyo Mkoa na Taifa, Mhe Mwanjelwa ambaye ni mjumbe Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa aliwasisitiza wajumbe hao kutochagua viongozi kwa matakwa ya urafiki na kujuana Bali kuchagua viongozi wa kazi watakaoisaidia jumuiya kuendana na mtazamo mpya wa CCM Mpya na Tanzania Mpya.
Mbali na kuwashukuru makada hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya jambo lililopelekea Mhe Rais John Pombe Magufuli kumteua kuhudumu nafasi muhimu ya Kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mwanjelwa alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ni ya kazi hivyo uchaguzi huo ni vyema kumalizika kwa kuwapata viongozi wachapakazi.
"Tunaelekea kwenye Mbeya Mpya, CCM Mpya, UWT Mpya na Tanzania Mpya hivyo msichague viongozi kutokana na makundi au watakaoendeleza makundi baada ya uchaguzi Bali chagueni viongozi shupavu na wachapakazi" Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Mhe Mwanjelwa (MNEC), alisema kuwa atafanya ziara katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya ili kuangalia jinsi utekelezaji wa ilani ya CCM inavyotekelezwa.
Mkutano huo Maalumu ulimalizika kwa salama hapo Jana Novemba 28, 2017 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mbeya ambapo viongozi mbalimbali walichaguliwa katika ngazi ya Mkoa na Taifa.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Kutwa ya Mbeya, Jana Novemba 28, 2017.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Akisakata rumba kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Kutwa ya Mbeya, Jana Novemba 28, 2017.
Makada wa CCM Mkoani Mbeya wakimlaki Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Wakati akiondoka kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Kutwa ya Mbeya, Jana Novemba 28, 2017.
Makada wa CCM Mkoani Mbeya wakimlaki Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Wakati akiondoka kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Kutwa ya Mbeya, Jana Novemba 28, 2017.

MBUNGE WA ILEJE JANET MBENE AZINDUA NAMBENE CUP

$
0
0
 Mbunge wa Wilaya ya Ileje, Janet Mbeneakizungumza wakati wa Uzinduzi wa Nambene Cup inayoshirikisha timu za Wilaya nzima kutoka kila Kata ambapo Mbunge huyo ametoa ufadhili wa Jezi na Zawadi ya Mshindi wa kwanza mpaka wa tatu wafungaji bora.

Mbunge wa Ileje  akisalimia timu zilizojitokeza kushiriki Nambene Cup aliyoiandaa katika Wilaya yake kama hatua za kukuza michezo na kuleta Umoja kwa Jamii
 Wachezaji wa Timu Mbalimbali zinazoshiriki Nambene Cup wakiwa uwanjani wakijandaa kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi
 Wacheaji wa timu zilizoshiriki uzinduzi wa Nambene Cup wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo wa ufunguzi.
Mbunge wa Ileje Janet Mbene akifurahi wa na Watoto waliofika katika uzinduzi wa Nambene Cup

KILIMANJARO STARS YAONGEZA WATATU, KULIFUATA KOMBE LA CHALENJI KESHO

$
0
0

LIFUATA KOMBE LA CHALENJI KESHO

Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania Bara, ‘Kilimanjaro Stars’, Ammy Conrad Ninje, ameongeza nyota watatu katika kikosi chake mara baada ya Baraza la Soka la Afrika Mashariki (CECAFA), kuridhia kuongezwa wachezaji watatu kwa kila timu.
Awali, CECAFA ilihitaji wachezaji 20 tu, lakini sasa wameongeza watatu na kufanya idadi mpya ya wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo ya Chalenji kwa mwaka huu kuwa 23.
Wachezaji walioongezwa na Kipa Ramadhani Kabwili kutoka Young Africans ya Dar es Salaam, Amani Kiata  wa Nakuru All Stars ya Kenya na Yahya Zayd kutoka Azam FC ya Dar es Salaam.
Kikosi cha wachezaji 20 wa awali wa Ninje - Kocha wa Daraja ‘A’ la Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA), ni makipa Aishi Manula (Simba SC) na Peter Manyika (Singida United).
Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphace Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Young Africans), Kennedy Juma (Singida United), Erasto Nyoni (Simba SC) na Mohammed Hussein (Simba SC).
Viungo wa kati ni Himid Mao ambaye ni Nahodha (Azam FC), Jonas Mkude (Simba SC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Raphael Daud (Young Africans), Shizza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya) na Ibrahim Ajib (Young Africans).
Washambuliaji ni Mbaraka Yussuph (Azam FC), Elias Maguri (Dhofar/Mascat, Oman), Daniel Lyanga (Fanja FC/Mascat) na Yohana Mkomola (Ngorongoro Heroes). 
Benchi la Ufundi linaundwa na yeye Ninje ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa). 
Katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Desemba 3, mwaka huu, Kilimanjaro Stars imepangwa Kundi ‘A’ pamoja wenyeji Kenya, Rwanda na Libya ambayo ni timu mwalikwa kutoka Kaskazini mwa Afrika.
Kilimanjaro Stars ambayo imewahi kutwaa mara tatu taji hilo la Chalenji tangu kuanzishwa kwake, itaaza kampeni za kurudisha heshima yake dhidi ya Libya katika kundi hilo la A utaofanyika Desemba 3, mwaka huu. 

DAWA ZA SARATANI ZAPATIKANA KWA ASILIMIA 80 % KUTOKA ASILIMIA 4%

$
0
0
Na Dotto Mwaibale
TAASISI ya Saratani ya Ocean Road wameipongeza Bohari ya Dawa (MSD), kwa usambazaji wa dawa katika taasisi hiyo na maeneo mengine nchini.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dk. Julius Mwaiselage wakati akizungumza na watendaji wa MSD ambao walifanya ziara ya kikazi ya kujua changamoto mbalimbali za usambazaji dawa katika taasisi hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu.
Katika hatua nyingine  upatikanaji wa dawa za saratani,vifaa tiba na vitendanishi  vya maabara katika taasisi hiyo ni asilimia 80  kutoka asilimia nne mwaka 2015.
Kutokana na hatua hiyo taasisi hiyo imesema ipo haja jamii kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Bohari ya Dawa MSD katika kupunguza changamoto za huduma za saratani ambapo ilikuwa kero miaka miwili iliyopita.
 Mwaiselage alisema hapo awali  upatikanaji wa dawa vifaa tiba na vitendanishi ilikuwa ni changamoto kubwa katika utendaji.
"2015 taasisi hiyo ilikuwa ikipata dawa,vifaa tiba na vitendanishi asilimia nne sasa ni asilimia 80 haya ni matokeo mazuri ya utendaji wa kazi
  Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Laurean Bwanakunu (kulia), akizungumza na maofisa wa Hospitali ya Rufaa ya Amana wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja Dar es Salaam leo ya kujua changamoto za upatikanaji wa dawa katika hospitali hiyo na kuzitafutia ufumbuzi. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Meshack Shimwela.
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Meshack Shimwela, akisisitiza jambo katika mkutano huo.
.
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Laurean Bwanakunu (wa sita kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Hospitali ya Rufaa ya Amana. 

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA HUDUMA MPYA YA WCF YA WAAJIRI KUJISAJILI KWENYE MTANDAO WA INTERNET

$
0
0
 NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID. ARUSHA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, amezindua huduma mpya itakayowawezesha waajiri kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa kutumia mtandao wa Internet.
Mhe. Mhagama amezindua huduma hiyo leo Novemba 29, 2017, wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC, Arusha.
“Huduma hii itawawezesha waajiri kujisajili na Mfuko kupitia mtandao wa internet na hawalazimiki kujaza fomu na kuja ofisini kwetu au kwa maafuisa kazi” Mkuu wa kitengo cha Tehama cha WCF, Bw. Stephen Goyayi, alisema wakati akitambulisha huduma hiyo kwa Mhe. Waziri.
Katika hatua nyingine, Benki ya NMB Bank plc  imenyakua tuzo baada ya kuwa mwajiri bora katika uwasilishaji michngo miongoni mwa waajiri wenye wafanyakazi wengi.
Kampuni zingine zilizonyakua tuzo kundi la waajiri ni Steel Master Ltd kwa kuwa mwajiri bora katika uwasilishaji nyaraka za madai ya fidia kwa wafanyakazi na kampuni nyingine ni KPMG  Advisory Ltd kwa kuwa mwajiri bora katika uwasilishaji michango miongoni mwa kundi la waajiri wenye wafanyakazi wengi.
WCF iliwatunukia tuzo wadau wa Mfuko huo ambapo Waziri Jenista kwa niaba ya Serikali alipokea tuzo hiyo, kwa kutambua mchango wa Serikali katika kuanzisha na kufanikisha utendaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
Wadau wengine ni Shirika la Vyama vya Wafanyakazi, (ATE), Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, (TUCTA), Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), kwa kutambua ushiriki wake katika uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF)
Mkuu wa kitengo cha Tehama cha WCF, Bw. Stephen Goyayi, akielezea jinsi huduma hiyo iyakavyofanya kazi.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, (wapili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshjomba, wakishuhudia Mwenyekiyti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilinhi milioni 15, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, ikiwa ni mchango wa Mfuko kusaidia mpango wa elimu mkoani humo. Makabidhiano haya yamekwenda sambamba na ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wadau wa WCF jijini Arusha
 Waziri Mhagama (watatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi, (wakwanza kushoro), wakipokea hundi yenye thamani ya shilingi milioini 33.8 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, (wapili kushoto). Fedhab hizo ni kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa komputa nundu (perkins Braille Machines) kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa kuona katika shule za umma.
  
 Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya WCF,. Wakwanza kushoto ni katibu wa Waziri Jenista Mhagama.
 Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama, akimkabidhi tuzo Bw. Richard L.Makungwa kutoka NMB Bank Plc tuzo ya mwajiri mwajiri bora katika uwasilishaji michngo miongoni mwa waajiri wenye wafanyakazi wengi. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba.
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

KUMBUKUMBU

$
0
0
                             C:\Users\emakaya\Desktop\gk makaya0001.jpg  
    The  Late Col. Godfrey K. Makaya   
Leo tarehe 30/11/2017, baba yetu mpendwa umetimiza miaka 10 tangu ututoke, unakumbukwa sana na familia yako, ndugu, jamaa na marafiki. Pumzika kwa amani G.K - Amen.   

MAGAZETI YA ALHAMIS LEO NOVEMBA 30,2017


TANESCO: HITILAFU KWENYE GRIDI YA TAIFA ASUBUHI HII

$
0
0
MAJIRA ya saa 7:20 leo hii Alhamisi Novemba 30, imetokea hitilafu kwenye Gridi ya Taifa na hivyo kusababisha umeme kukatika takriban kwenye mikoa yote iliyounganishwa kwenye Gridi hiyo.


Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, mafundi na wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO wameanza kufuatilia kujua chanzo chake hasa ni nini na taarifa Zaidi zitatolewa kila baada ya muda ili kuufahamisha umma na watuamiaji wa umeme.

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI NOVEMBA 29, 2017

MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI

$
0
0
Na Mathias Canal, Mbeya

Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Jana Novemba 29, 2017 amemuagiza Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kumsimamisha kazi Afisa Kilimo Wilaya ya Mbeya anayesimamia zao la Pareto Ndg Emmanuel Halinga ili kupisha uchunguzi.

Mhe Naibu Waziri ametoa agizo hilo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini mwa Tanzania mara baada ya Mhe Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Oran Njeza na Wananchi wote waliokuwepo kwenye mkutano huo wa hadhara kumrushia shutuma nzito na kumkataa mtaalamu huyo wa kilimo mbele ya Naibu Waziri.

Alisema kuwa pamoja na zao hilo la Pareto kuwa la kwanza kwa uzalishaji katika nchi za Afrika huku likiwa zao la pili kwa uzalishaji Duniani lakini bado halijamkomboa Mkulima nchini jambo ambalo linaonyesha namna ambavyo baadhi ya wataalamu Wa Kilimo wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Alisema kuwa wataalamu wa kilimo walipaswa kusimamia kwa kiasi kikubwa zao hilo kwani Pato lake ni wastani wa tani 2000 kwa mwaka sawa na Bilioni 12 mpaka 14 ambapo katika kipindi hili bei ya kuanzia Mkulima analipwa shilingi 2300 kwa kilo lakini inapanda mpaka shilingi 3300 kulingana na ubora wa zao hilo ambalo mkulima amelima.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa  akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017. Picha zote Na Mathias Canal
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa  akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa  akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.
 Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Mhe Oran Njeza akizungumza katika mkutano huo kufikisha kilio cha wananchi mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwwa kuhusu zao la Pareto na matatizo la wafanyabiashara kujaza Lumbesa kwenye uuzaji wa mazao mbalimbali likiwemo zao la viazi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kijijini Jojo Kata ya Santilya, Jana Novemba 29, 2017.



Machinjio ya kisasa ya Ruvu lazima yakamilike ifikapo 2018 - Mpina

$
0
0
Waziri  wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga  J. Mpina ameagiza machinjio ya kisasa ya Ruvu yaliyotelekezwa kwa muda mrefu kujengwa na  kukamillika  ifikapo Desemba, 2018.
Maagizo hayo ameyatoa jana katika ranchi ya Ruvu, alipokuwa katika ziara ya kutembelea baadhi ranchi za mifugo nchini, ambapo amesema ni muhimu machinjio hayo ya ya kisasa yakamilike ili Tanzania ianze kuuza mazao yatokanayo na mifugo katika masoko ya kimataifa.

Ametoa siku tatu kwa Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kumpelekea mpango kazi unaoainisha  namna ya kukamilisha ujenzi wa machinjio hiyo ya kisasa ambayo  baada ya kukamilika itakuwa machinjio kubwa kuliko zote nchini.

Amesema kuwa Tanzania ni nchi ya tatu katika bara la Afrika kwa kuwa na uwingi wa mifugo hivyo hakuna sababu ya kushindwa kuongoza katika  soko la mazao ya mifugo katika masoko ya duniani.

Aidha, Waziri Mpina  amesema  kukamilika kwa machinjio hayo kutasaidia kupunguza  usumbufu kwa wafanyabiashara wa mifugo ambao wote nawapeleka mifugo yao Dar es Salaam   hali ambayo inaongeza uharibifu wa mazingira  kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Waziri Mpina amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Ranchi  za taifa kuhakikisha kuwa  kunatafutwa fedha kwa ajili ya kuzalisha  mbegu bora za mifugo na kuongeza idadi ya mifugo kulingana na uwezo wa eneo la ranchi ya Ruvu lenye ukubwa wa hekta 44,000 ambapo hivi sasa eneo hilo la ranchi ya Ruvu lina mifugo ipatayo 1530 wakati uwezo wa ni kuwa na mifugo kuanzia 12000 hadi 22000.

Alisisitiza kwamba maboresho hayo lazima yafanyike ifikapo Desemba , 2018  ambapo ifikapo Juni 2018 tathimini ya awali itafanyika kuona ni kwa namna gani agizo hilo limetekelezwa.

 Jengo la machinjio ya kisasa lililopo katika eneo la ranchi ya Ruvu ambalo Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina amewaagiza Watendaji kuhakikisha linakamilika ifikapo Desemba 2018.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akijaribu kukata nyama kwa kutumia mashine ya kisasa alipotembelea ranchi ya Ruvu hivi karibuni.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akihakiki taarifa za ununuzi wa dawa za mifugo alipotembelea ranchi ya mifugo ya Ruvu hivi karibuni.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye miwani katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ranchi ya Ruvu na watumishi wa Wizara  ya Mifugo na Uvuvi alipotembelea ranchi hiyo jana.
Waziri wa Mifugo na  Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akiwa na  viongozi wa ranchi ya mifugo nchini akionyeshwa mbuzi wanaofugwa katika ranchi ya Ruvu alipotembelea ranchi hiyo hivi karibuni.

Machinjio Ya kisasa Ya Ruvu Lazima Yakamilike Ifikapo 2018 – Mpina

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga J. Mpina ameagiza machinjio ya kisasa ya Ruvu yaliyotelekezwa kwa muda mrefu kujengwa na kukamillika ifikapo Desemba, 2018.

Maagizo hayo ameyatoa jana katika ranchi ya Ruvu, alipokuwa katika ziara ya kutembelea baadhi ranchi za mifugo nchini, ambapo amesema ni muhimu machinjio hayo ya ya kisasa yakamilike ili Tanzania ianze kuuza mazao yatokanayo na mifugo katika masoko ya kimataifa.

Ametoa siku tatu kwa Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kumpelekea mpango kazi unaoainisha namna ya kukamilisha ujenzi wa machinjio hiyo ya kisasa ambayo baada ya kukamilika itakuwa machinjio kubwa kuliko zote nchini.

Amesema kuwa Tanzania ni nchi ya tatu katika bara la Afrika kwa kuwa na uwingi wa mifugo hivyo hakuna sababu ya kushindwa kuongoza katika soko la mazao ya mifugo katika masoko ya duniani.Aidha, Waziri Mpina amesema kukamilika kwa machinjio hayo kutasaidia kupunguza usumbufu kwa wafanyabiashara wa mifugo ambao wote nawapeleka mifugo yao Dar es Salaam hali ambayo inaongeza uharibifu wa mazingira kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Waziri Mpina amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Ranchi za taifa kuhakikisha kuwa kunatafutwa fedha kwa ajili ya kuzalisha mbegu bora za mifugo na kuongeza idadi ya mifugo kulingana na uwezo wa eneo la ranchi ya Ruvu lenye ukubwa wa hekta 44,000 ambapo hivi sasa eneo hilo la ranchi ya Ruvu lina mifugo ipatayo 1530 wakati uwezo wa ni kuwa na mifugo kuanzia 12000 hadi 22000.

Alisisitiza kwamba maboresho hayo lazima yafanyike ifikapo Desemba , 2018 ambapo ifikapo Juni 2018 tathimini ya awali itafanyika kuona ni kwa namna gani agizo hilo limetekelezwa.“Tunataka wananchi wapate sehemu ya kujifunza,ranchi ya Ruvu iwe sehemu ya kupata mbegu bora. Siwezi kuwa Waziri wa Mifugo wakati shamba langu halina mifugo” alisisitiza Mpina.

Waziri aliongeza kuwa na mfumo wa kisasa wa kufuga mifugo kitaalamu badala ya mfumo wa sasa ambapo mifugo inafugwa kwa muda mrefu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akijaribu kukata nyama kwa kutumia mashine ya kisasa alipotembelea ranchi ya Ruvu hivi karibuni.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akiwa na viongozi wa ranchi ya mifugo nchini akionyeshwa mbuzi wanaofugwa katika ranchi ya Ruvu alipotembelea ranchi hiyo hivi karibuni.
Jengo la machinjio ya kisasa lililopo katika eneo la ranchi ya Ruvu ambalo Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina amewaagiza Watendaji kuhakikisha linakamilika ifikapo Desemba 2018.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akihakiki taarifa za ununuzi wa dawa za mifugo alipotembelea ranchi ya mifugo ya Ruvu hivi karibuni.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye miwani katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ranchi ya Ruvu na watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi alipotembelea ranchi hiyo jana.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images