Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO LASHIKA KASI MANISPAA YA DODOMA

$
0
0
Ofisa mifugo wa Kata ya Chahanga katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma William Gervas akimpiga chapa Ng'ombe wakati wa zoezi la upigaji chapa mifugo linaloendelea katika Halmashauri hiyo. PICHA NA RAMADHANI JUMA.


Waziri Mwakyembe afanya ziara BASATA kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa maonyesho

$
0
0
Mtendaji Mkuu Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza (kushoto) akimuonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye kofia ya blue) eneo la jukwaa lilivyozingatia ubora wa maonyesho alipofanya ziara katika taasisi hiyo kujua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa maonyesho wa BASATA jana Jijini Dar es Salaam.
Mkandarasi wa ujenzi wa ukumbi wa BASATA Bw. Novart Ludovick (wapili kushoto) akimweleza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye kofia ya blue) maendeleo ya ujenzi ulipofikia alipofanya ziara katika taasisi hiyo kujua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa maonyesho wa BASATA jana Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza (katikati) akimuonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) picha inayoonyesha muonekano wa ukumbi wa BASATA utakavyokua baada ya kumalizika alipofanya ziara katika taasisi hiyo kujua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa maonyesho wa BASATA jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na watumishi wa BASATA (hawapo pichani) baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa BASATA jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu BASATA Bw. Godfrey Mngereza.
Mtendaji Mkuu BASATA Bw. Godfrey Mngereza (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha ya tingatinga Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa BASATA pamoja na kuzungumza na watumishi wa BASATA jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akisikiliza wimbo uliotungwa na kuimbwa na mwanamuziki kutoka Kongo unaosifia Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa BASATA pamoja na kuzungumza na watumishi wa BASATA jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu BASATA Bw. Godfrey Mngereza. Picha na Genofeva Matemu -WHUSM

NAIBU WAZIRI TAMISEMI AZIAGIZA HALMASHAURI KUTUMIA ‘MAFUNDI WAZAWA’ KATIKA MIRADI MIDOGO; AFURAHISHWA NA MIRADI YA WILAYANI MKALAMA

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Joseph Kakunda akipima kiasi cha saruji kilichowekwa kwenye mchanga katika ujenzi shule ya Sekondari Iguguni Wilayani Mkalama katika ziara yake ya Siku moja kufuatilia utoaji huduma mbalimbali kwa jamii.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Joseph Kakunda akisisitiza jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhandisi Jakson Masaka (kulia kwake) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhandisi Godfrey Sanga (kushoto kwake).
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Joseph Kakunda akisalimiana na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhandisi Jaksoni Masaka mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ajili ya Ziara ya ufuatiliaji wa miradi ya elimu na maji.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Joseph Kakunda akisalimiana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkalama Elizabeth Rwegasira mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ajili ya Ziara ya ufuatiliaji wa miradi ya elimu na maji.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Joseph Kakunda ameziagiza halmashauri zote nchini kutumia mafundi wa kawaida wazawa waliopo katika maeneo yao katika miradi yote midogo kupitia utaratibu unaojulika kama ‘force account’. Naibu Waziri Kakunda ametoa agizo hilo jana mara baada ya kufanya ziara Wilayani Mkalama kufuatilia utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii huku akijikita zaidi katika sekta ya Maji na Elimu, ambapo ametembelea mradi wa maji Iguguno na Shule ya Sekondari Iguguno.

“Matumizi ya Wakandarasi yabaki katika miradi mikubwa tu lakini miradi yote midogo tuwatumie mafundi waliopo katika maeneo yetu, mafundi hawa wazawa wanatekeleza kazi kwa ubora kama huu ambao nimeuona leo na kwa gharama ambazo ni nzuri,” amesisitiza mara baada ya kutoa agizo hilo. Ameeleza kuwa gharama na ubora wa mradi wa Shule ya Sekondari ya Iguguno ambao unajumuisha ujenzi na ukarabati wa madarasa 8, mabweni mawili, vyoo vyenye matundu 11, bwalo la chakula na maabara ambapo vyote hivyo vimegharimu milioni 416, unatosha kudhirihisha kuwa mafundi wa kawaida wazawa wanaweza kufanya kazi nzuri.

“Huu mradi endapo tungetumia utaratibu wa wakandarasi na wazabuni hiyo gharama ya milioni 416 ingekuwa kama robo ya gharama, nasisitiza wakandarasi na wazabuni watumike katika miradi mikubwa tu”, Naibu Waziri Kakunda amesisitiza.

Ameongeza kwa kuipongeza halmashauri hiyo kwa kutekeleza mradi mkubwa wa maji ambao umewezesha usambazaji wa maji katika kata yote ya Iguguno na kuwasaidia wananchi wasihangaike kupata maji. Aidha Naibu Waziri Kakunda ameonekana kutofurahishwa na taarifa kuhusu wanafunzi 12 waliokatishwa masomo tangu mwezi Januari Mwaka huu kutokana na sababu ya kupewa ujauzito, ambapo ametoa rai kwa wazazi na walezi wote nchini kuwa mstari wa mbele kukomesha tatizo hilo.

Ameeleza kuwa wazazi wengi wamekuwa wakifanya makubaliano ambapo mwanafunzi aliyepewa ujauzito anamkana mhalifu aliyempa ujauzito ili kumuepusha na kifungo cha miaka 30 jela, jambo linalofanya kesi nyingi kukosa ushahidi huku tatizo la mimba kwa wanafunzi likiendelea kuwepo.

Naibu Waziri Kakunda amesema ili kukomesha hilo serikali kupitia Wizara yake ina dhamira ya kupeleka hati ya dharula bungeni ili itungwe sheria itakayofuta dhamana ya mtuhumiwa atakayempa ujauzito mwanafunzi huku uchunguzi wa Vinasaba (DNA) utatakiwa kufanyika ili kuthibisha kama mtuhumiwa ndiye baba wa mtoto ama la.

Awali, Mbunge wa jimbo la Mkalama Mhe. Alan Kiula amewasilisha changamoto mbalimbali za Wilaya hiyo kwa Naibu Waziri Kakunda kwa kumueleza changamoto kubwa ni kutokuwa na hospitali ya Wilaya.

Mhe. Kiula ameongeza kuwa upungufu wa watumishi katika Wilaya hiyo hasa wa Sekta ya Elimu na Afya umekuwa ukikwamisha baadhi ya shughuli kufanyika kwa kasi inayotakiwa.

Aidha amemshukuru Naibu Waziri Kakunda kwa ahadi yake ya kuitazama Wilaya hiyo kwa jicho la pekee katika mgao ujao wa watumishi kwa Mwezi Disemba na Januari huku akimuhakikishia kuwa Halmashauri itafanya kwa haraka taratibu za awali za upatikanaji wa eneo kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya.

AGPAHI YAENDESHA WARSHA KWA WAVIU WASHAURI MKOA WA MWANZA

$
0
0

Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI limetoa warsha kwa Waviu Washauri kutoka mkoa wa Mwanza ili kuwajengea uwezo kwa ajili ya kuboresha huduma katika vituo vya tiba na matunzo (CTC).

Warsha hiyo ya siku tatu iliyoanza siku ya Jumanne Novemba 28,2017 katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza imekutanisha WAVIU washauri kutoka halmashauri za wilaya za Ilemela,Kwimba,Magu,Buchosa,Misungwi,Sengerema na Nyamagana.

Waviu washauri ni watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na wamejiweka wazi na huru kuwashauri watu wanaoishi na VVU katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufuasi mzuri wa dawa, kutoa ushauri nasaha kwa wenzao,kujitolea kufuatilia na kufundisha kwa njia ya ushuhuda wa maisha sambamba na kuhamasisha Waviu kujiunga katika vikundi ili kusaidiana na kupunguza unyanyapaa.
Mgeni rasmi, Mratibu wa watoa huduma ngazi ya jamii mkoa wa Mwanza, Bi. Esperance Makuza,aliyemwakilisha Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mwanza akifungua warsha ya siku tatu ya watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi mkoa wa Mwanza katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza Jumanne Novemba 28,2017. 
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona akielezea historia ya shirika la AGPAHI na shughuli zinazofanywa na shirika hilo nchini Tanzania. 
Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa. 
Mwezeshaji Gladness Olotu akiendelea kutoa mada ukumbini.

NAIBU WAZIRI MIFUGO NA UVUVI ULEGA AAHIDI KUTATUA MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI MKURANGA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema atahakikishia mgogoro wa wafugaji na wakulima katika Wilaya ya Mkuranga unamalizika kwa kufikia makubaliano yenye kuleta tija.

Alizungumza hayo wakati wa ziara yake katika vijiji vya Kiramba, Mkiu, Bigwa na Kilimahewa Kusini, Naibu Waziri ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Mkuranga amesema kuwa mgogoro baina ya wafugaji na wakulima upo siku nyingi ila kwa sasa anataka kuhakikisha analitatua kabla kufikia kuleta madhara kwa wananchi wa maeneo hayo.

Ulega amesema kuwa, tatizo la mgogoro wa Wafugaji na wakulima lipo siku nyingi hata kabla ya yeye kuteuliwa na amepita kwenye vijiji hivyo na ameendelea kuliona ila kwa ushirikiano baina yake na Halmashauri ya Manispaa ya Mkuranga watafanikiwa kutatua mgogoro huo ambao bado haujawa mkubwa sana.

"Tatizo hili lipo siku nyingi, na tunalifahamu na tumeshaliona ila wanakijiji leo wamenikumbusha tena, mimi pamoja na jopo langu la watu kutoka Halmashauri tumejipanga kuona tunalitatua kwani bado halijafikia kuwa donda ndugu," amesema Ulega.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kiramba kata ya Nyamato wakati wa ziara yake katika jimbo la Mkuranga na kuwaahidi kushugulikia mgogoro wa wafugaji na wakulima.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akisalimiana na wazee wa Kijiji cha Bigwa wakati wa ziara yake katika jimbo la Mkuranga jana Mkoani Pwani.

Katika Kijiji cha Kiramba na Mkiu, baadhi ya wananchi walitoa malalamiko yao kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega kuwa wafugaji waliokubaliwa na kijiji kwa ajili ya kuleta mifugo yao kwa sasa imekuwa kero wakiingia mpaka mashambani na kuharibu mazao yao.

Wanakijiji hao wamelalamika kuwa wafugaji walioidhinishwa katika mkutano wa kijiji wamekaribisha na ndugu zao ambapo kinasababisha mifugo kuwa mingi sana na mingine kuletwa mpaka kwenye mashamba yao kwa ajili ya malisho.

Mbali na hilo Naibu Waziri aliweza kukutana na changamoto ya barabara ya kimanzichana kulekea Kiramba, Tipo na Mkonoge na kumuagiza Mkandarasi kutoka Manispaa ya Mkuranga na Meneja wa TARURA kuhakikisha tatizo hilo linamalizika kabla ya kuanza kwa kipindi cha masika mwakani.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Ulega ametoa mifuko ya saruji kwa Kijiji cha Kiramba, Mkiu, Bigwa na Kilimahewa Kusini kwa ajili ya muendelezo wa maendeleo ya kijiji humo.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na wanakijiji wa Mkiu wakati wa ziara yake ya Jimbo la Mkuranga na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi akisalimiana na wanakijiji baada ya kuwasili kwenye ziara yake katika Jimbo la Mkuranga jana Mkoani Pwani.Picha na Emmanuel Massaka.

Mshindi wa Milioni 60 za Tatumzuka aamua kuwekeza ushindi wake kwenye elimu

$
0
0
Catherine Triphone wiki iliyopita alitimiza ndoto yake ya kusoma baada ya kushinda milioni 60 za jackpot ya Tatumzuka. Bi Catherine ambaye anaishi na wazazi wake, siku ya jumapili alikuwa nyumbani peke yake huku akisinzia alipopigiwa simu iliyobadilisha maisha yake.

Dada huyo mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akicheza Tatumzuka mara kwa mara kwa kutumia namba zinazoendana matukio mbalimbali yanayohusu maisha yake na ndugu zake ambapo ameshinda mara kadhaa katika droo za kila saa. "Namba zangu daima zimekuwa 842. Hizi namba zinawakilisha siku , mwezi na mwaka wangu wa kuzaliwa. Ninaishukuru Tatu Mzuka kwa kutoa fursa hii ambapo mtu yoyote anaweza kucheza na kushinda, " aliongeza Bi Catherine

Dhamira ya Tatu Mzuka kwa sasa ni zaidi ya kubadilisha maisha ya washindi wetu; tumejizatiti pia kuunga mkono mipango mbalimbali ya serikali katika jamii ili kuboresha maisha ya Watanzania wote. Mpango huu ni sehemu ya kauli mbiu yetu ya ‘Ukishinda, Tanzania inashinda’.

"Kwa ushirikiano na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori tumeamua kununua vitabu kwa baadhi ya shule Wilayani humo. Tunatarajia kukamilisha taratibu zote na kutoa vitabu hivyo hivi karibuni. “ Alisema Sebastian Maganga, Meneja wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka.

Kwa kuupendezesha msimu huu wa sikukuu, Tatu Mzuka imeahidi kufungua msimu huu wa furaha kwa kutoa shilingi milioni 500 kuanzia sasa mpaka Desemba 31, 2017. Utajisikiaje kama utamaliza mwaka kwa kupata ushindi mkubwa? Endelea kucheza, uendelee kushinda. Natumai Bi Catherine atafurahia sana sikukuu ambapo ni baada ya kucheza Tatumzuka kwa shilingi 500 tu.” Bwana Maganga alihitimisha

Bi Catherine anapanga kurudi shule kusoma kusoma shahada na kuwanunulia wazazi wake usafiri ili kuwaondolea adha ya usafiri wanayokumbana nayo.

 Meneja wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar,alipokuwa akimtangaza Mshindi wa milioni 60 za jackpot ya Tatumzuka. Bi Catherine Triphone (pichani kulia).
 Mshindi wa milioni 60 za jackpot ya Tatumzuka. Bi Catherine Triphone (pichani kulia).akitoa ufafanuzi namna alivyoshinda hizo milioni 60 na namna atakavyozitumia,ambapo Catherine amesema kuwa fedha hizo atazitumia kujielimisha .
 Meneja wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi,Mshindi wa milioni 60 za jackpot ya Tatumzuka. Bi Catherine Triphone (pichani kulia).

MADIWANI WA CCM WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI JIMBO LA HAI WAKABIDHIWA VYETI

$
0
0

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .

MSIMAMIZI wa uchaguzi katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro , Ndugu Yohana Sintoo amesema kuwa zoezi la uchaguzi katika kata tatu zilizokuwa hazina uwakilishi limekamilika salama na kuwapata viongozi watakaowawakilisha wananchi kwenye kata husika.


Ndg Sintoo ameyasema hayo wakati akikabidhi vyeti kwa madiwani wateule watatu walioshinda  kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Novemba 26 mwaka huu.


“Ndugu zangu mtakumbuka kuwa mwishoni mwa wiki kulikuwa na uchaguzi kwenye jimbo letu ambapo wananchi wa kata tatu walikuwa katika zoezi la upigaji kura kwa lengo la kuwapata viongozi wa ngazi ya udiwani baada ya madiwani wa kata husika kujiuzulu”


“Wananchi wa kata za Mnadani , Weruweru na Machame Magharibi walipiga kura ili kuwapata wawakilishi wao  ambapo zoezi hilo limekamilika bila uvunjifu wa amani kuanzia kipindi cha mikutano ya  kampeni hadi siku ya zoezi la upigaji kura na leo tunawapatia washindi vyeti vyao”

Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Weruweru Swalehe Msenges.kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu.
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Mnadani  Nassib Mdeme ,kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu.
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Machame Magharibi ,Martin Munisi .kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu.
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akiwa katika picha ya pamoja na Madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni .kutoka kushoto ni Diwani wa kata ya Mnadani ,Nasib Mdeme,Diwani wa kata ya Weruweru ,Swaleh Msenges na Diwani wa kata ya Machame Magharibi ,Martin Munisi ,Wengine katika picha ni kulia mwa msimamizi wa uchaguzi ni Msimaizi Msaidizi na Mkuu wa Idara ya Fedha Juma Massatu na kushoto ni Afisa Uchaguzi wilaya ya Hai,Edward Ntakiliho.
Madiwani waliochaguliwa hivi karibuni wakionesha vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Hai wakiwa na ndugu zao.


TIMU MBILI ZA MCHEZO WA BASEBALL ZANZIBAR ZAAGWA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Heshima na mfadhili mkuu wa Timu ya Baseball Zanzibar Nd. Shimaoka wanne kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na wachezaji wa Timu ya Baseball wakati walipofika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa ajili ya kuagwa kuelekea kwenyemashindano ya mchezo huo yatakayofanyika Tanzania Bara ili kumtafuta bingwa wa Tanzania ambapo Timu 12 zinatarajiwa kushiriki,Zanzibar ikitoa Timu mbili.Mwanakwerekwe C na Mwenge Magharibi A.
 Kapteni wa Timu ya Timu ya Baseball Zanzibar Omar Bakar Omar akizungumza na Mwandisahi wa Habari mara baada ya kuagwa kuelekea kwenyemashindano ya mchezo huo yatakayofanyika Tanzania Bara ili kumtafuta bingwa wa Tanzania ambapo Timu 12 zinatarajiwa kushiriki,Zanzibar ikitoa Timu mbili.Mwanakwerekwe C na Mwenge Magharibi A.
 Mwenyekiti wa Heshima na mfadhili mkuu wa Timu ya Baseball Zanzibar Nd,Shimaoka akizungumza na Mwandishi mara baada ya kuagwa kuelekea kwenyemashindano ya mchezo huo yatakayofanyika Tanzania Bara ili kumtafuta bingwa wa Tanzania ambapo Timu 12 zinatarajiwa kushiriki,Zanzibar ikitoa Timu mbili.Mwanakwerekwe C na Mwenge Magharibi A.
Mwenyekiti wa Chama cha Baseball(ZABSA)Othman Ali Msabah akizungumza na Mwandishi mara baada ya kuagwa kuelekea kwenyemashindano ya mchezo huo yatakayofanyika Tanzania Bara ili kumtafuta bingwa wa Tanzania ambapo Timu 12 zinatarajiwa kushiriki,Zanzibar ikitoa Timu mbili.Mwanakwerekwe C na Mwenge Magharibi A.

PICHA NA YUSSUF SIMAI /MAELEZO ZANZIBAR.

SERIKALI YASISITIZA DESEMBA 31 KUWA UKOMO WA UWEKAGI WA VIGINGI (BEACONS) VYA MPAKA HIFADHINI

$
0
0





Na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili
..........................................................................
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amesisitiza agizo la Serikali lililotolewa hivi karibuni na Waziri Mkuu kuhusu kukamilisha zoezi la uwekagi wa vigingi vya mpaka kwenye maeneo ya hifadhi nchini ifikapo Desemba 31 mwaka huu.

Amesema lengo la kukamilisha zoezi hilo ni kuiwezesha Serikali kufanya uamuzi wa mwisho wa kumaliza migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu baina ya vijiji na maeneo ya hifadhi nchini.


Mhe. Hasunga ametoa kauli hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi katika hifadhi ya msitu wa Isalalo Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe ambapo aliziagiza taasisi zilizo chini ya Wizara yake kukamilisha zoezi hilo kabla ya tarehe hiyo ili kuiwezesha Serikali kubaini maeneo yenye mapungufu na kuyatolea uamuzi.


“Ifikapo tarehe 31 tuwe tumemaliza kuweka hizo beacon (vigingi) za mipaka, baada ya hapo hatua itakayofuata, Serikali tutakaa na kuangaliza ni vijiji vingapi au maeneo gani yameingia ndani ya hifadhi, tuangalie je tuwaachie hayo maeneo wananchi au tuwahamishe tuwapeleke maeneo mengine, maamuzi hayo yatakuja baada ya kufanya tathmini na kubaini penye mapungufu.


“Sasa ikitokea kwamba imefika tarehe 31 hatujatekeleza hili mimi kama Naibu Waziri nitakuwa sina kazi, maana sijatekeleza agizo la Serikali, kwahiyo lazima tulisimamie, na mimi sasa kabla halijanipasukia nitakupasukia bwana Meneja (Meneja TFS Wilaya ya Mbozi), nitakuja kukagua mipaka, na kabla ya tarehe 31 nitakuja kukagua tena,”alisema Naibu Waziri Hasunga.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akioneshwa ramani ya Hifadhi ya Msitu wa Isalalo na Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Wilaya ya Mbozi, Fred Mgeni (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua hifadhi hiyo kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi mkoani Songwe jana.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, John Palingo wakati wa kukagua Hifadhi ya Msitu wa Isalalo Mkoani Songwe kwenye ziara yake ya kikazi ya kuimarisha uhifadhi mkoani humo jana.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA KWA OFISI YA RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA KIKWETE.

WAZIRI MWAKYEMBE AKIPONGEZA CHAMA CHA MCHEZO WA BASE BALL TANZANIA KWA KUPATA HATI YA KUTAMBULIWA NA SHIRIKISHO LA DUNIA LA MCHEZO HUO

$
0
0
 Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge (kulia) akiwatambulisha viongozi wa mchezo wa Base Ball na Soft Ball Tanzania kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) walipomtemtembelea kumkabidhi hati ya kutambuliwa na Shirikisho la dunia la mchezo huo jana Jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akipokea hati ya utambulisho wa mchezo wa Base Ball na Soft Ball kutambuliwa na Shirikisho la dunia la mchezo huo kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Mchezo wa Base Ball na Soft Ball Tanzania Dkt. Ahmed Makata (kushoto) jana Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akisoma hati ya utambulisho ya mchezo wa Base Ball na Soft Ball baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Mchezo wa Base Ball na Soft Ball Tanzania Dkt. Ahmed Makata (kushoto) jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Shirikisho la Mchezo wa Base Ball na Soft Ball Tanzania Dkt. Ahmed Makata (kushoto) baada ya kumkabidhi taarifa na hati ya utambulisho wa mchezo huo kutambuliwa na Shirikisho la dunia la mchezo huo jana Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM

WAZIRI MKUU MAJALIWA AIPONGEZA WCF KWA KUPIGA HATUA KUBWA NDANI YA KIPINDI KIFUPI.

$
0
0
 NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA.

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa mafanikio ambayo Mfuko umepayata katika kipindi cha muda mfupi tangu uanzishwe.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) jijini Arusha leo Novemba 29, 2017, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amesema, katika kipindi kifupi cha miaka miwili tangu WCF ianizshwe Mfuko umeweza kutekeleza wajibu wake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kusajili wanachama na kulipa Mafao ya Fidia.

“Mfuko umeanza kufikia wanyonge kwani umeonyesha jinsi ambavyo wafanyakazi wanyonge waliokuwa hawalipwa fidia wanapopata madhara kazini, sasa kutokana na kuwepo kwa Mfuko huu wanyonge wameanza kufaidi matunda kama ambavyo serikali ilidhamiria.

“Nitoe wito kwa viongozi wa Mfuko, endeleeni kutoa elimu kwa wananchi hususan waajiri ili waweze kujisajili na hivyo kuwapunguzia mzigo wa kuwalipa fidia wafanyakazi wao pindi wanapopata madhara wawapo kazini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Umlemavu, Mhe. Jenista Mhagama, akifungua mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kwenye ukumnbi wa Simba, Kituo cga Mikutano cha Kimataifa, AICC Arusha leo Novemba 29, 2017

  
Naibu Waziri wa Nchi Ofiosi ya Waziri Mkuu, Mhe. Anthony Mavunde, akitoa hotuba yake.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mashomba, akitoa hotuba yake.
 Mhe. Mhagama na viongozi wengine wakiimba wimbo wa Taifa.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

CAPACITY BUILDING TRAINING OF THE VITONGOJI MAMAS AND BABAS FOR THE UNESCO – GLOBAL LEARNING XPRIZE PROJECT

$
0
0
  Catherine Amri from UNESCO Dar es Salaam conducting a training in Korogwe 

 282 men and women from selected villages in Tanga region have participated in a three days training organized by UNESCODar es Salaam Office to build their capacities in supporting the implementation of the of Global Learning XPRIZE Project for the Promotion of Early Learning through Innovative Technologies in Tanzania. 

The group of participants comprised one selected community memberand a member of the village council from each participating village. The selected community members, also known as ‘Kitongoji (hamlet) mama and baba’ will perform the tasks related to the overall monitoring of the project at the community level and conduct the survey in terms of the Social Emotional Impact Study. 

Each kitongojimama/baba will be supporting a group of about 5 to 21 children, from the selected 141 remote and underprivileged hamlets in Mkinga, Muheza, Handeni, Korogwe, Lushoto, and Pangani districts in Tanga region. The Global Learning XPRIZE Project for the Promotion of Early Learning through Innovative Technologies in Tanzania aims to reach about 2,060 out of school children in Tanga region to promote the improvement of cognitive outcomes in terms of the 3R’s (reading, writing and arithmetic).Catherine Amri from UNESCO Dar es Salaam conducting a training in Korogwe 

 The training equipped vitongojimama and baba with the knowledge on the goals and objectives of the project, reporting procedures of technical issues, overall monitoring activities and basic skills to identify behavioural and social emotional changes occurring in the participating children and their families in the course of fifteen months of the field test, corresponding to the period which children will interact with the software.

The vitongoji mama and baba are key players for the success of the implementation of the project, and building their capacity in terms of the project knowledge, was one of the most relevant milestones regarding the preparation of the field testing and will contribute to empower members of rural, remote and underprivileged communities. 
 A training session in Pangani

NEWS ALERT:WAZIRI MKUU ABAINI SEMI TRELA 44 ZIKITAKA KUTOLEWA BANDARINI BILA YA KUFUATA UTARATIBU

$
0
0
Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa (mwenye Tai nyekundu) amefanya ziara ya kushitukiza katika Bandari ya Dar es salaam leo November 29, 2017 na kubaini Kampuni ya NAS ikitaka kutoa Semi Trela 44 bila ya kufuata utaratibu.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro kuwakamata, Bw. Bahman wa kampuni ya NAS na Wakala wa Kampuni ya Wallmark Bw. Samwel kwa kutaka kutoa bandarini magari makubwa aina ya semi tela 44 bila ya kulipa kodi kwa kutumia jina la Waziri Mkuu.

Pia Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kutowasikiliza wafanyabiashara wanaotaka kukwepa kodi kwa madai ya kupewa vibali vya msamaha wa kodi kutoka kwa viongozi wa juu Serikalini.

“Mtu asije hapa aseme amepewa kibali na Rais Dkt. John Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan au Waziri Mkuu cha kutaka kutoa mzigo wake bila ya kufuata taratibu. Akija mtu na taarifa hizo akamatwe mara moja na achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.”

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Novemba 29, 2017) alipofanya ziara ya ghafla bandarini baada ya kupata taarifa za mfanyabiashara huyo aliyetaka kuutapeli uongozi wa TPA kutaka kutoa magari hayo yaliyoingizwa nchini mwaka 2015 kutoka nchini Uturuki.

Hatua hiyo imekuja baada ya Bw. Bahman wa kampuni ya NAS kutaka kupata msamaha wa kodi kwa kuidanganya TPA kwa madai kwamba wamewasiliana na Waziri Mkuu na wasipotekeleza jambo hilo watapata matatizo.



HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

DJ Supreme la Rock headed for a 3-Day Dar es Salaam Extravaganza Party

$
0
0
US entertainer, Dj Supreme from Seattle, Washington, is set to rock Dar es Salaam this week. The 3 day event will be held in the company of Tanzania’s own DJ Vasley, DJ Sma and DJ FU. The 3 day events will be held at exclusive but divergent locations and hotels in Dar es Salaam.


Dj Supreme currently has over 50,000 records in his collection. While in Tanzania he will be looking sinto growing his number of records.

“I stopped counting (the records’ numbers) at 50,000 but there’s still so many (records) I don’t have that I need. In fact one of my main mission’s while in mama Africa is to acquire original African records on vinyl," says Dj Supreme.

He adds: "I'm looking for funk, soul, disco, boogie, high life, rock groups like Asiko, Geraldo Pino, Kelenkye, Marijata, Rob, Witch, and William Onyebor vinyl records.They are probably sitting somewhere in someone's house collecting dust. If anyone can help me out with getting records please do so.”

The events are organised by the new event company in Dar es Salaam, Xfinity Entertainment. Dj Supreme’s official 3 day events will be on 30th November (Thursday), 1st December (Friday) and 2nd December (Saturday). The 3 events are sponsored by Jameson and Red Bull and will have Clouds Media Group as the official media partner.

Xfinity is a fuse of jazz, funk, soul and lingala wrapped in bongo flava. The events and lifestyle company was founded this year, 2017, to meet the needs of the ever-changing social and entertainment industry in Tanzania and the rest of East Africa.


SERIKALI YA AWAMU YA TANO YA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI YAFANIKIWA KATIKA UKUSANYAJI MAPATO KIELEKTRONIKI

$
0
0
Tangu kuzinduliwa Dirisha la Ukusanyaji Kodi kidigitali June mosi 2017 (Electronic Revenue Collection System - eRCS) ambalo lilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Makamu wa Rais Mhe. Mama Samia Suluhu Hassani pamoja na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Mohamad Shein,  mawaziri kadhaa wa serikali za Muungano na serikali ya Mapinduzi; Kwa mara ya kwanza serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipatia bila bugudha Ushuru mkubwa wa bidhaa na kodi ya Ongezeko la Thamani zitokanazo na makampuni ya simu. 

Mfumo huu uliosukwa na vijana wa Kitanzania wazalendo, umefanikisha kuongeza mapato litokanalo na mtandao (Ciber Space) kwa Zanzibar kwa 51% kwa robo ya tatu ya mwaka 2017 ukilinganisha na miezi kama hiyo 2016.  Uchunguzi uliofanyika katika robo hiyo (tatu) ya mwaka 2017 (Julai,August na Septemba 2017), umebaini Zanzibar imelipwa kupitia mfumo wa eRCS Tsh Bil 7.2 ambayo imeongezeka kwa 51% ukilinganisha na miezi kama hiyo mwaka 2016 ambapo makusanyo ya jumla ya kodi yalikuwa  Tsh Bil 3.5 pekee.
Kwa mujibu wa vielelezo vya makusanyo wa TRA, miezi mitatu kabla ya mfumo huu kuzinduliwa rasmi (April,May na June); Makampuni ya simu yalilipa jumla ya kodi ya  Tsh Bil 101.7 lakini baada ya kuzinduliwa rasimi kwa mfumo huu wa eRCS na makampuni ya simu (TTCL, HALOTEL, AIRTEL, VODACOM, ZANTEL, SMART na TIGO) kuugwa ndani ya mfumo; Kwa kipindi cha miezi mitatu pekee ( Julai,Agost na Septemba 2017), yameweza kulipa kwa njia ya kielektroniki Tsh Bil 128.9 kukiwa na ongezeko la Sh Bil 27.2 sawa na 21% huku ongezeko la kodi ya thamani ikipanda kwa 9% yaani Tsh. Bil 4.7 sambamba na ongezeko la Ushuru wa Bidhaa 29% yaani Tsh. Bil 22.
Taarifa za kiuchunguzi zimebaini serikali inafuatilia kwa kina udanganyifu wowote utakao ama uliojitokeza kabla na baada ya mfumo hasa taarifa za makampuni ya simu katika matumizi yaoya kila mwezi.Mpaka sasa, benk kadhaa nchini zimekamilisha taratibu za kuungwa katika mfumo huu na kuanza kulipa kodi kielectroniki. 

 Huu ni ushindi mkubwa kwa mkakati wa Rais Magufuli katika kupata njia bora za kukusanya mapato nchini. Ikumbukwe wajenzi wa mfumo huu ni vijana wazalendo walioaminiwa na serikali ili kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo zingetumika katika ujenzi wa mfumo huo kutumia wataalamu na makampuni ya kigeni.Hivi ndivyo mapato yanavyoonekana katika Dashibodi ambazo viongozi wakuu wa nchi wanaona mapato yanavyokusanywa kielectroniki kwa kutumia mfumo  wa eRCS kila sekunde.

Mahakama yapokea maelezo ya onyo ya anayedaiwa kuwa malkia watembo.

$
0
0
Na Karama Kenyunko blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepokea maelezo ya onyo ya mshtakiwa Yang Feng Glan anayedaiwakuwa malikia wa tembo, ambayo yatatumika kama moja ya kielelezo katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Glan ambaye ni raia wa China na watanzania wawili.

Maelezo hayo yamepokelewa na hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi anayesikiliza kesi hio.Kabla ya kupokelewa,askari Polisi wa kikosi kazi cha taifa cha kupambana na ujangili, E.1180 Koplo Emmanuel alieleza kuwa alitumia masaa mawili kuchukua maelezo ya onyo ya mshtakiwa katika Kituo cha Polisi cha Osterbay.

Koplo Emmanuel alidai hayoleo alipokuwa akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu,Faraja Nchimbi kutoa ushahidi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.

Amedai,Septemba 27,2015 majira ya usiku alipigiwa simu na kaimu DCI akimtaka afike Polisi Osterbay ambapo alipofika hapo alimkuta mshtakiwa Yang Feng akituhumiwa kwa kujihusisha na tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo na kutakiwa amfanyie mahojiano.

Alidai katika mahojiano mshtakiwa alijitambulisha kwa jina la Yang, akamuuliza kama anatambua kosa lake na kwamba,Yang alimueleza kuwa anatuhumiwa na kujihusisha na nyara za Serikali ambazo ni meno ya tembo.

SHILINGI BILIONI 375.4 ZATOLEWA KUONDOA TATIZO LA MAJI MKOA WA SIMIYU

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe aliongoza kikao cha wadau kujadili mradi wa maji katika halmashauri za Mkoa wa Simiyu. Tayari tahmini ya mazingira imekamilika na kazi ya upembuzi yakinifu ipo katika hatua za mwisho na zabuni imepangwa kutangazwa mwezi Januari 2018 baada ya kukamilika kwa zabuni, Ujenzi wa Mradi unakadiriwa kuchukua miezi 24.

Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira iliwasilisha ombi la fedha kwa Mfuko wa Global Climate Fund (GCF) ili kutekeleza Mradi wa maji katika halmashauri zilizopo Mkoa wa Simiyu unaojulikana kama Simiyu Climate Resilience Water Supply Project. Kuibuliwa kwa Mradi huu kulitokana na uhitaji mkubwa wa maji katika Mkoa wa Simiyu kulikosababishwa na ukame wa muda mrefu.
Mradi huu, umepangwa kutekelezwa kwa awamu mbili katika Wilaya tano za Mkoa wa Simiyu. Wilaya hizo ni Busega, Bariadi, Itilima, Maswa na Meatu. Katika Awamu ya kwanza, Mradi utatekelezwa katika Wilaya za Busega, Itilima na Bariadi. Kiasi cha Euro milioni 140.7 sawa na takriban shilingi bilioni 375.4 zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha utekelezaji wa mradi huo.

Fedha za kutekeleza Awamu ya Kwanza ya Mradi zitachangiwa na Serikali ya Tanzania na Washirika wa Maendeleo ambao ni GCF na Serikali ya Ujerumani. GCF watachangia Euro Milioni 102, Serikali ya Ujerumani watachangia Euro Millioni 25.6 na Serikali itachangia Euro Millioni 13.1 na wananchi nao kupitia nguvu zao watachangia Euro Millioni 1.5. Matumizi ya Fedha za GCF na Serikali ya Ujerumani yatasimamiwa na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW).

Lengo kuu la Mradi ni kuboresha afya na kuongeza uzalishaji mali ili kuinua hali ya maisha ya wananchi walioathirika na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo husika ya Mradi.
Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha upatikanaji wa huduma ya maji ya uhakika kwa kujenga mfumo wa uzalishaji na usafirishaji maji na kuboresha mfumo wa usambazaji wa maji katika miji na vijiji husika.

Mradi pia utahusisha kujenga kwa mabwawa ya kilimo cha umwagiliaji endelevu (Smart Agriculture) ambayo pia yatatumika kunyweshea mifugo pamoja na kuimarisha huduma za usafi wa mazingira kwa kujenga mabwawa ya kukusanyia na kuchuja majitaka na vyoo vya mfano mashule na vituo vya afya.

MASAUNI AFUNGUA MKUTANO WA UCHAGUZI WA JUMUIYA YA UMOJA WA WAZAZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa chama hicho, mkoa wa Dar es Salaam, mkutano huo umefanyika leo, katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha Wetu
 Mwenyekiti anayemaliza muda wake   wa Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam, Angela Kizigha,   akizungumza wakati wa   Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa chama hicho, mkoa wa Dar es Salaam. Kushoto  aliyevaa kofia ni Mgeni Rasmi na Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni. Mkutano huo umefanyika leo, katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam. 
 Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi cheti cha Uongozi , Kiongozi anayemaliza muda wake katika Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam, Ibrahim Mpwapwa (kulia), wakati wa mkutano uliofanyika leo,ukumbi wa Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam. 
 atibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akipiga makofi baada ya kuwasili  katika Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa chama hicho,mkoa wa Dar es Salaam, Mkutano huo umefanyika leo Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi,mkoa wa Dar es Salaam, wakishangilia wakati Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), akizungumza katika mkutano huo uliofanyika leo, ukumbi wa Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam.

TPDC laendesha zoezi la Upimaji Afya kwa Wananchi wa Songo Songo

$
0
0
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuanzia tarehe 24/11/2017 hadi 25/11/2017 limeendesha zaoezi la upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi wa Songo Songo ambao wamekuwa wakilazimika kusafiri zaidi ya masaa mawili kufuata huduma ya vipimo hivyo katika Hospitali ya Kilwa kivinje.

Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni Tanzu ya TPDC inayosimamia uendesheshaji na utunzaji wa Miundombinu ya Uchakataji na Usafirishaji wa Gesi Asilia inayoitwa GAS COMPANY (GASCO) Mhandisi Baltazari Mrosso wakati wa ufungaji wa zoezi hilo ameeleza kuwa ni wajibu wao kama Shirika kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii zenye lengo la kuboresha maisha ya Wananchi wa Songo Songo ambao pia ni tegemeo kubwa katika shughuli zinazofanywa na Shirika kuanzia kwenye uzalishaji wa gesi visimani, uchakataji kiwandani na usafirishaji.
Diwani wa Kata ya Songo Songo Mh. Said Mwinyi akifungua rasmi zoezi la upimaji kwa kukipatiwa huduma ya upimaji wa Shinikizo la Damu kutoka kwa Daktari Octavian Modest.

“Sisi kama Shirika la Umma ambalo limewekeza katika Kisiwa hiki katika shughuli za uzalishaji na uchakataji wa gesi asilia tunao wajibu wa kushirikiana na wananchi pamoja na uongozi wa Songo Songo ili kuboresha maeneo mbalimbali ya huduma za kijamii kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi, kuboresha uhusiano na kuendelea vyema na shughuli za uzalishaji na uchakataji wa gesi asilia na hivyo leo hii tunahitimisha zoezi la upimaji wa afya kwa wananchi wa Songo Songo pamoja na kukabidhi vifaa tiba vya upimaji wa ugonjwa wa Kisukari ambavyo hapo awali havikuwepo.” Alieleza Kaimu Meneja Mkuu GASCO.
Daktari wa TPDC, Octavian Modest akimtibu moja ya Wazee wa Kijiji cha Songo Songo waliojitokeza katika zoezi la upimaji wa Afya liloratibiwa na kufadhiliwa na TPDC.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images