Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

VIJANA MUUNGENI MKONO RAIS MAGUFULI AMEFANYA MAKUBWA - KUMBILAMOTO

0
0
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na umoja wa Vikundi vya Jogging Vingunguti mara baada ya kumaliza uasafi wa mwezi katika juhudi za kumuunga mkona Rais John Pombe Magufuli kuifanya Tanzania iwe s
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, akiongoza zoezi la Usafi katika mtaa wa Miembeni kata ya Vingunguti kama agzio la Rais lilivyotaka kila Jumamosi ya Mwisho wa mwezi watu kufanya usafi
 Afisa Ugavi wa Manispaa ya Ilala,Vicent Odero akitoa shukrani kwa umoja wa Vikundi vya Jogging Vingunguti kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usafi wa Mwisho wa Mwezi
 Afisa usafishaji wa Manispaa ya ilala Cosmas Mwaitete akihahidi kuwaongezea vifaa zaidi vya kufanyia usafii umoja wa wakimbiaji mbio za pole Vingunguti
 Mtangazaji wa kituo cha Radio cha east Afrika  Zembwela akionyesha kwa vitendo namna ya kufanya usafi katika mitaa ya vingunguti mara baada ya kualikwa na Naibu Meya.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, akitoa uchafu kwenye mitaro ya mitaa ya Vingunguti
Sehemu ya wana kikundi wakikimbia kabla ya kuanza kwa usafi wa mazingira kata ya Vingunguti

MAADHIMISHO YA UFUNGUZI WA KAMPENI YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

POP UP SWAHILI FASHION WEEK YAWAVUTIA WANA MITINDO NA WADAU WAKE

0
0
 Mwanamitindo wa kampuni ya African Doll akimuonesha nguo ndugu John Ulanga katika Swahili Fashion week Pop Up iliyofanyika Nyumbani kwa Balozi wa Italy jijini Dar es Salaam
 Mwanamitindo,Diane Kapela kutoka Naled Fashion Tanzania akiweka sawa bidhaa zake katika Pop Up ya Swahili Fashion Week iliyofanyika Nyumbani kwa Balozi wa Italy
 Mwanamitindo Maarufu nchini Martin Kadinda, akichagua nguo za Mwanamitindo Kulwa Mkwandule katika Pop Up ya Swahili Fshion Weeek iliyofanyika nyumbani kwa balozi wa Italy
 Mwanamitindo Manca Mushi akiuza bidhaa zake za mikoba na nguo kutoka kwa moja ya wateja waliofika katika Pop Up ya Swahili Fashion Week
Mwanamitindo Rebecca Mwaipopo  akiwaonyesha wateja wake  nguo wakati wa Pop Up ya Swahili Fashion Week iliyofanyika nyumbani kwa balozi wa Italy jijini Dar es Salaam
--

Wanawake watakiwa kushiriki katika michezo.

0
0
Na Shamimu Nyaki-WHUSM
Wanawake nchini wametakiwa kushiriki katika Michezo mbalimbali kwani ni fursa nzuri ambayo inasaidia kupata ajira na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja pamoja na kuitangaza nchi kama ambavyo wanafanya wanamichezo wakiume.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa akizindua Mashindano ya Riadha kwa wanawake kuelekea Olimpiki ya mwaka 2020 yatakayofanyika Tokyo nchini Japan ambapo amewataka wanawake waliopata fusa ya kushiriki katika mashindano hayo kujituma zaidi na kujiamini ili wapate nafasi ya kushiriki katika Olimpiki hiyo na kuiletea heshima Nchi yetu. 
“Leo vitaibuka vipaji vingi vitakavyosaidia nchi yetu kupiga hatua katika mchezo wa Riadha,nawaasa mjitume zaidi muwe na nidhamu pamoja na kujiamini ili mfanye vizuri katika mashindano haya hatimaye mpate nafasi ya kushiriki Olimpki ya  mwaka 2020 kule nchini Japan”.Alisema Mhe. Mwakyembe.
Aidha amewataka waamuzi wa mchezo huo kutumia vizuri taaluma yao kwa kufuata Sheria,taratibu na kanuni walizofundishwa na kutii kiapo walichoapa katika kuchezesha mchezo huo kwa kutoa matokeo sahihi na kwa wakati ili kuepusha manung’uniko.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Juliana Shonza amesema Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano kwa wanamichezo wote ambao wapo tayari na wanashiriki katika michezo mbalimbali kwani nia ya Serikali ni kukuza na kuendeleza Michezo hapa nchini.
“Ni fursa ya pekee kwenu vijana na wanawake kwa ujumla kutumia nafasi hii kuonyesha uwezo wenu katika michezo hii ili mpate nafasi ya kushiriki mashindano malimbali duniani na hatimaye mpate ajira itakayowezesha kutengeneza maisha yenu ya baadae.”Alisisitiza Mhe.Shonza.
Naye mwanariadha wa mbio za mita mia Bi. Winifrida Makenji kutoka Shule ya Sekondari Makongo ya Jijini Dar es Salaam ambaye ameingia katika fainali itakayochezwa hapo kesho amesema sifa kubwa ya yeye kufikia hatua hiyo ni kujiamini,kufanya mazoezi pamoja na kufuata maelekezo ya mwalimu.
Mashindano hayo yaliyofadhiliwa na Kampuni ya Ushirikiano ya Japan (jicA) yamehusisha michezo ya Riadha,kurusha mikuki pamoja na Kisahani ambapo yatamalizika kesho katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akifyatua bastola juu leo Jijini Dar es Salaam kuashiria Ufunguzi wa Mashindano ya Riadha kwa Wanawake kuelekea Olimpiki ya mwaka 2020 yatakayofanyika Tokyo nchini Japan.
 Naibu Waziri wa Habari Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza leo Jijini Dar es Salaam katika Ufunguzi  wa Mashindano ya Riadha kwa Wanawake kuelekea Olimpiki ya mwaka 2020 yatakayofanyika Tokyo nchini Japan.Kulia ni Waziri wa Wizara hiyo  Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.
 Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimpongeza mshindi wa kurusha kisahani Bi. Mwanjala Abdala kutoka Dodoma wakati wa Mashindano ya Riadha kwa Wanawake kuelekea Olimpiki ya mwaka 2020 yatakayofanyika Tokyo nchini Japan yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
 . Naibu Waziri wa Habari Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akimvalisha Medali ya ushindi mshindi namba mbili wa kurusha kisahani leo Jijini Dar es Salaam katika Mashindano ya Riadha kwa Wanawake kuelekea Olimpiki ya mwaka 2020 yatakayofanyika Tokyo nchini Japan.Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja.
 Waziri Mhe.Dkt Mwakyembe na Naibu Waziri Mhe.Juliana Shonza wa Wizara ya Habari Sanaa na Michezo wakimvalisha medali ya ushindi mshindi namba moja wa kurusha kisahani Bi.Joyce Barnabas kutoka Dodoma leo Jijini Dar es Salaam katika Ufunguzi wa Mashindano ya Riadha kwa Wanawake kuelekea Olimpiki ya mwaka 2020 yatakayofanyika Tokyo nchini Japan.
Waziri Mhe.Dkt Mwakyembe na Naibu Waziri Mhe.Juliana Shonza wa Wizara ya Habari Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wanamichezo pamoja na wafadhili kutoka kampuni ya jiCA ya nchini Japan wanaoshiriki Mashindano ya Riadha kwa Wanawake kuelekea Olimpiki ya mwaka 2020 yatakayofanyika Tokyo Nchini Japan yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.Wa pili kushoto waliokaa ni Balozi wa Japan hapa nchini Mhe.Masahran Yoshida.

DC SHINYANGA AIBUKIA KWENYE SHAMBA DARASA LA PAMBA KUANZA RASMI MSIMU WA KILIMO CHA PAMBA

0
0
Shamba darasa hilo litatumika kama darasa la kilimo cha pamba kwa njia za kitaalamu kwa wakulima wa pamba katika wilaya hiyo katika msimu hu wa kilimo cha pamba ili waweze kuvuna mazao mengi na kujiongezea kipato pia kuondokana na uhaba wa chakula.   
DC Matiro ambaye alikuwa ameambatana na wataalamu pamoja na viongozi wa kata ya Solwa ,mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bakari Mohamed Novemba 24,2017,amepanda zao la pamba kwenye shamba darasa la kata hiyo.  
Akizungumza wakati wa kupanda pamba katika shamba hilo Matiro aliwataka wakulima wa halmashauri hiyo kuiga mfano wa kilimo cha kitaalamu kinachofanywa kwenye mashamba darasa kwa kutumia kamba. “Lengo la mimi kuingia shambani na kuanza kupanda zao la pamba pamoja na viongozi wa kata hii ni kuhamasisha wakulima kulima kitaalamu ili waweze kupata mavuno mengi kwani wakizembea hakuna wa kuwaletea chakula na serikali haina shamba hivyo wajitahidi kufuata maelekezo ya wataalamu ili kujiinua kiuchumi kupitia zao hili la biashara”,alisema Matiro.  
Hata hivyo alisema katika msimu huu wa kilimo cha pamba serikali imejitahidi kuleta mbegu bora za aina zote kwa wakulima. Matiro alisisitiza kila kata iwe na shamba darasa litumike kama mfano kwa wakulima na kila shule kupanda zao la mtama kwa wingi. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameshiriki katika kilimo cha pamba katika shamba darasa lililoanzishwa katika kijiji cha Solwa kata ya Solwa katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kwa habari kamili BOFYA HAPA

MJEA YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI WAISLAMU NCHINI

0
0

 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amana Bank, Bw. Bakari Kisuda  akizungumza na Waandishi wa Habari Waislamu jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akifungua mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Mtandao wa Waandishi wa Habari wa Kiislamu wa  Afrika ya Mashariki (MJEA) kwa kushirikiana na kampuni ya KO Innovates zimeendesha  mafunzo kwa waandishi wa habari wanaofanya kazi kwenye vyombo vya habari vya Kiislamu hapa nchini.
Mwenyekiti wa MJEA, ABUOBAKARI FAMAU,amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa waandishi wa habari wanaotoka kwenye vyombo hivyo vya habari ili waweze kuendana na mazingira ya sasa ya tasnia ya habari.
FAMAU  ameongeza kuwa vyombo vya Kiislamu vina wajibu kubwa sana kwa jamii na hivyo kuna haja ya kukumbushana juu ya wajibu huo.
nae  Khadijah Omar amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwakutanisha waandishi wa habari wa vyombo vya Kiislamu na kubadilishana uzoefu.
Zaidi ya washiriki 25 wamepatiwa mafunzo hayo ambayo yatafanyika Novemba 25 mwaka huu katika ukumbi wa Tangaza House jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amana Bank,Bakari Kisuda  akizungumza na Waandishi wa Habari Waislamu jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akifungua mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Mtandao wa Waandishi wa Habari wa Kiislamu wa  Afrika ya Mashariki (MJEA)
Waandishi wa Habari wa Mashirika ya Kislamu nchini wakifatilia hotuba ya mgeni Rasmi kwa makini

Introducing "NARINGA" official audio by Genevive

TUPAMBANE KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA: WAZIRI KAIRUKI.

0
0


Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Watanzania wametakiwa kutumia nguvu zao katika kupambana na ukatili wa kijinsia katika maeneo yao ili kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki alipokuwa akimwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.

Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa kimsingi kiwango cha ukatili wa kijinsia nchini na dunia bado ni kubwa na kwa mujibu wa Taarifa ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2015/2016 inaonesha kuwa wanawake 4 kati ya 10 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15.

Ameongeza kuwa takwimu zinonesha kuwa asilimia 42 ya wanawake waliowahi kuolewa wamekumbana na ukatili wa wenza wao ama wa kimwili,au ukatili unaohusisha ngono.“Nawaomba watanzania wenzangu katika maeneo yenu pazeni sauti na kufanya kwa vitendo kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia unaowakumba sana wanawake na watoto” alisema Mhe. Angellah.

Aidha kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa athari za ukatili wa kijinsia ni kubwa sana katika Nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki akinyajua bango juu lenye ujumbe unaosema “Ukatili wa Kijinsia Unachelewesha Tanzania ya Viwanda” wakati akipokea Maandamano maalum ya ufunguzi wa Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Kinondoni Dar es Salaam Novemba 25, 2017.
Baadhi ya wananchi na wadau wa maendeleo wakiwa katika maandamano maalum ya ufunguzi wa Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Kinondoni Dar es Salaam Novemba 25, 2017.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki akiwaasa wadau na watanzania kujikita katika kupambana na ukatili wa kijinsia wakati akimwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba 25,2017.
Niabu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akieleza namna Wizara inavyoshikiana na wadau na wananchi kupambana kuondoa ukatili wa kijinsia katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba 25,2017.
Mkurugenzi wa Shirika la WILDAF Tanzania Dkt Judith Odunga akitoa salamu kwa niaba ya wadau katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leade’s Club Dar es Salaam Novemba 25,2017.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KAMISHNA MKUU WA TRA AZINDUA MRADI WA TRA NA JICA WA KUWAJENGEA UWEZO WAFANYAKAZI WA TRA

NEWS ALERT: Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) afuzu majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya Sweden

0
0
Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) amefanikiwa kufuzu kwenye majaribio yake ya kucheza Soka la kulipwa barani Ulaya. Mchezaji huyo, aliyekuwa nchini Sweden kwa majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya hukoanatarajiwa kurejea nchini siku ya Jumatatu inayokuja. 

Na mara baada ya kurejea klabu za Simba na Eskilstuna zitaanza mazungumzo ya kimkataba ili kumwezesha kiungo huyo kwenda Sweden kwa ajili ya kucheza Soka huko. Kiufupi klabu imefurahishwa na azma ya Ndemla ya kutaka kusonga mbele zaidi, na kama ilivyo desturi na utamaduni wa Simba, klabu haitasita kumruhusu mchezaji yoyote anayepata fursa adhimu kama hiyo itakayomsaidia mchezaji binafsi.klabu na Taifa kwa ujumla. 
Wakati huo huo kesho klabu ya Simba itakutana na viongozi wote wa matawi. Mkutano huo ni maandalizi ya mkutano mkuu maalum wa klabu wa tarehe 3-12-2017. na mkutano huo wa kesho utafanyika makao makuu ya klabu kuanzia saa Nne kamili asubuhi ya jumapili ya tarehe 26-11-2017.

Uongozi wenu unawaomba Wanachama na washabiki wa klabu yetu kujitokeza kwa wingi kesho uwanja wa Uhuru kuishangilia timu yao, itakapocheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Timu ya Lipuli ya Iringa. 

Imetolewa na..... 
HAJI S. MANARA
Mkuu wa Habari  na mawasiliano, Simba  Sports Club. 

WANAFUNZI ZAIDI YA 700 WAHITIMU MAFUNZO YAO CHUO KIKUU CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE MNMA

0
0

 Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 12 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mkurugenzi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  ZanzibarMashavu Ahmad Fakir akihutubia wakati wa kutunuku vyeti kwa wahitimu wa Ngazi ya Shahada na Astashahada wa chuo hicho kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Prof . Shadrack Mwakalila  akizungumza juu ya mipango ya chuo hicho wakati wa mahafali ya 12 yaliyofanyika katika jengo la utamaduni la MNMA Kigamboni jijini Dar es Salaam.


 Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 12 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mkurugenzi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  ZanzibarMashavu Ahmad Fakir akikabidhi zawadi kwa Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika mwaka wa masomo 2017
 Baadhi ya wahitmu wa Shahada ya Maendeleo ya Jinsia ya MNMA Wakiwa wanasubiri kutunukiwa shahada zao wakati wa mahafali ya 12 ya Chuo hicho yaliyofanyika jijini Dare s Salaam
  Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 12 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mkurugenzi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  Zanzibar Mashavu Ahmad Fakir  akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi waliofanya Vizuri

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AFUNGA KWA KISHINDO KAMPENI KATA YA MURIET JIJINI ARUSHA, APOKEA WANA CHADEMA 91. Katibu wa CCM,Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Kata ya Muriet jijini Arusha wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za udiwani wa Kata hiyo leo, awataka wananchi kuwachagua wagombea wa CCM kwenye Kata 43.

0
0

Aliyekua Kada ya Chadema akiwa ameshika kadi  na bendera za chama hicho baada ya wanachama 91 kurejea CCM katika mkutano wa kufunga kampeni kata ya Muriet jijini Arusha leo

Wafuasi wa CCM wakifurahia hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana katika mkutano wa kufunga kampeni kata ya Muriet jijini Arusha leo

Wakili msomi Albert Msando akiunguruma kwenye mkutano huo katika mkutano wa kufunga kampeni kata ya Muriet jijini Arusha leo

Katibu wa CCM,Abdulrahman Kinana akipokea kadi za Chadema baada ya kupokea wanachama wapya 91 waliojiunga na CCM leo katika mkutano wa kufunga kampeni kata ya Muriet jijini Arusha leo

WAZIRI MKUU AUNGANA NA WANASONGEA KUOMBOLEZA KIFO CHA MAREHEMU LEONIDAS GAMA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na wanafamilia, wananchi wa Songea katika kuomboleza kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo la Songea, Bw. Leonidas Gama, nyumbani kwa marehemu Likuyu wilayani Songea. 
Marehemu Gama amefariki dunia jana Ijumaa, Novemba 24, 2017 katika Hospitali ya Peramiho mkoani Ruvuma alikokuwa akipatiwa matibabu. Marehemu anatarajiwa kuzikwa Jumatatu, Novemba 27, 2017 katika kijiji cha Likuyu wilayani Songea.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali kwa sababu marehemu alishirikiana nayo vizuri tangu akiwa mtumishi wa umma na hata baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Songea. 
 Waziri Mkuu amesema msiba huo umeleta mtikisiko mkubwa kwa sababu baada ya kurudi nchini kutoka India alikokuwa akipatiwa matibabu aliwaeleza kuwa hali yake kwa sasa ni nzuri. ”Ametuachia pengo kubwa ambalo hatuna namna ya kuliziba.” 
 Ameongeza kuwa alipokea taarifa za msiba huo kwa huzuni na mshtuko mkubwa kwa sababu siku mbili kabla ya Waziri Mkuu kuanza ziara yake mkoani Ruvuma, Bw. Gama alimpigia simu na kumjulisha kwamba yeye anatangulia Songea kumpokea. 
 “Kifo ni mipango ya Mwenyezi Mungu na kwamba Bw. Gama ametangulia nasi tutafuata, hivyo wajibu wetu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema. Gama alikuwa kiongozi na mwanga wa maendeleo.” 
 Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaomba wanafamilia, mke wa marehemu na watoto na wananchi wa jimbo la Songea waendelee kuwa watulivu na wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.” 
 Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bibi Christine Mndeme alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake na kwenda kuwafariji wafiwa licha ya majukumu mengi na makubwa aliyonayo. 
 Awali msemaji wa familia Bw. Issa Fusi alimshukuru Waziri Mkuu pamoja na viomgozi mbalimbali waliojitokeza na kuwafariji baada ya kutokea kwa msiba huo.”Kaka yetu tulimpenda sana kazi ya Mungu haina makosa.”
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Songea  Marehemu Leonidas Gama. Waziri Mkuu aliungana na wanafamilia pamoja na wananchi wa Songea katika kijiji cha Lukuyi Wilayani Songea leo Novemba 25/2017 katika kuomboleza msiba huo.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiongea machache  nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Songea  Marehemu Leonidas Gamaambako aliungana na wanafamilia pamoja na wananchi wa Songea katika kijiji cha Lukuyi Wilayani Songea leo Novemba 25, 2017  kuomboleza msiba huo.
Picha na habari na Ofisi ya Waziri Mkuu

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA HOSPITALI YA TAALUMA NA TIBA YA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI KAMPASI YA MLOGANZILA

0
0




Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa akielezea ujenzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Kampasi ya Mloganzila wakati wa ufunguzi wa hospitali hiyo leo Novemba 25, 2017

 Muonekano wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila wakati wa  sherehe za ufunguzi leo Novemba 25, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa pole OCS wa Kibamba Mrakibu wa Polisi (SSP)  Pius  Lutumo akipata matibabu wakati akitembelea  Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa ameongozana na Balozi wa Korea Kusini Nchini Tanzania Bwana Song Geum Yong wakifuatiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia suluhu Hassan, makamu wa Rais Mstaafu Mstaafu Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Peter Serukamba wakielekea sehemu ya ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila
leo Novemba 25, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akifunua kitambaa kuashiria kufungua rasmi Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akisaidiwa na viongozi wengine na wadau wa afya akikata  utepe kuashiria kufungua rasmi  Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017.


MAGAZETI YA JUMAPILI LEO NOVEMBA 26,2017


Ibrahim Class awapa Watanzania kile walichotarajia.

0
0

Na Shamimu Nyaki-WHUSM.

Mwanamasumbwi Ibrahim Class amewapa raha watanzania jana Jijini Dar es Salaam baada ya kumpiga Bondia Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini katika mtanange wa kimataifa baina yao uliokuwa na mizunguko kumi na mbili.

Katika pambano hilo lililohuzuriwa na Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, Ibrahim Class alishinda katika mzunguko wa kumi na mbili ambapo ameandika historia ya muda mrefu hapa nchini kwa mabondia kutofanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa.

Akizungumza baada ya mchezo huo kumalizika Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema amefurahiswa sana na ushindi aliopata Ibrahim Class na kuahidi kumpa ushirirkiano zaidi ili aendelee kufanya vizuri katika mashindano mengine

“Siri ya mafanikio katika Michezo ni kufanya mazoezi,kujiamini kusikiiza mafundisho ya mwalimu pamoja na nidhamu,Ibrahim Class ni mwanamasumbwi anaepaswa kuigwa na mabondia na wanamichezo wengine wote kutokana na uwezo wake wa kujituma hivyo wanamichezo wanapaswa kuiga kutoka kwake ili wafanikiwe na kuitangaza nchi yetu kimichezo.” Alisema Dkt. Mwakyembe.

Naye bondia Ibrahim Class ameishukuru Serikali kwa ushirikiano iliyompa wakati wa mazoezi mpaka leo amefanikiwa kupeperusha vyema Bendera ya Tanzania na ameahidi kuendelea kufanya vizuri zaidi kila atakapokuwa ulingoni na kushinda mataji na mikanda mingi zaidi.
Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimpongeza Bondia Ibrahim Class baada ya kuibuka mshindi katika pambano la ngumi la kimataifa lenye mizunguko kumi na mbili dhidi ya Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo.
Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wananchi waliojitokeza katika pambano la ngumi la kimataifa kati ya mtanzania Ibrahim Class pamoja na Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja.
Bondia Mtanzania Ibrahim Class (kushoto) akipambana na na Mwenzie kutoka Afrika Kusini Koos Sibiya katika pambano la kimataifa la ngumi lenye mizunguko kumi na mbil lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam ambalo mtanzania huyo alishinda.
Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo (katikati) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja wakifurahia pambano la ngumi kati ya mtanzania Ibrahim Class dhidi ya Koos Sibiya wa Afrika Kusini lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Mabondia wanawake Felicha Mashauri (mwenye kaptula nyekundu) dhidi ya Happy Daudi wakizipiga jana Jijini Dar es Salaam wakati wa pambano la kimataifa kati ya Ibrahim Class wa hapa nchini dhidi ya Koos Sibiya wa Afrika kusini ambapo mtanzania aliibuka kidedea.
Bondia Haidari Mchanjo akifurahia ushindi wa mizunguko sita alioupata dhidi ya Bondia Bakari Magona lililochezwa jana Jijini Dar es Salaam wakati wa pambano la kimataifa kati ya Ibrahim Class wa hapa nchini dhidi ya Koos Sibiya wa Afrika kusini ambapo mtanzania aliibuka kidedea.

MDAU BEATRICE SINGANO MALLYA ALA NONDOZZ YAKE YA UTAWALA KWENYE BIASHARA A.K.A MASTERS IN BUSINESS ADMINISTRATION (MBA)

0
0
 Tabasamu Mubashara toka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania dada yetu Beatrice Singano Mallya baada ya kuhitimu na kutunukiwa nondoz yake ya Masters in Business Administration (MBA) kutoka chuo cha kimataifa cha ESAMI (The Eastern and Southern African Management Institute) ambao makao makuu yake yapo jijini Arusha Tanzania

Waziri Mhagama aitaka Halmashauri ya Bahi kukamilisha ujenzi wa Soko la Kigwe

0
0

Na. MWANDISHI WETU – DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kuhakikisha inamaliza ujenzi wa soko la Kigwe kwa kuhakikisha wanajenga vyoo na vibanda vidogo vitakavyo saidia soko hilo lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

Ameyasema hayo alipofanya ziara yake Wilayani Bahi Novemba 21, 2017 kwa lengo la kujionea namna uboreshaji wa soko hilo ambalo tayari limekamilika kwa asilimia 90 na kukabiliwa na changamoto za vibanda na vyoo vya kudumu.

“Ninaiagiza Halmashauri hii kuhakikisha inaleta timu ya wataalamu kupima viwanja na kuvigawa kwa wananchi pamoja na kumalizia ujenzi wa Vyoo vya soko ili lianzae utekelezaji wake haraka na kuhakikisha umeme unafungwa ndani ya soko hili”.

Kwa upande wake Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel alieleza ujenzi wa soko ni jambo ja muhimu linalogusa wanakigwe wote kwani tangu enzi za mkoloni kumekuwa na changamoto ya soko na kuwataka wananchi kulitunza na kuhakikisha linakuwa msaada kwao wote.

“Soko hili toka utawala wa mkoloni kulikuwa na soko bovu hivyo hatua ya kulikamilisha litavutia wengi na kukuza uchumi wa wana Kigwe wote.”Alisisistiza Badwel
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa wananchi wa Kigwe alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa soko la Kidwe Wilayani Bahi Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel alipowalisi kukagua ujenzi wa Soko la mazao la Kigwe Lililopo Bahi Dodoma.
Afisa Mtendaji Kata Bw. John Mchiwa akikabidhi taarifa ya Ujenzi wa Soko Kigwe kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara Bahi kuona maendeleo ya ujenzi huo.
Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa soko la Kigwe lililofadhiliwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) kwa kushirikiana na Halmashauri wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama Wilayani Bahi Dodoma.

MAONI YA MDAU: UCHUMI WA VIWANDA

0
0
Naunga mkono harakati za kuwa na Uchumi wa Viwanda.

Wakati wa Ukoloni, mataifa ya Afrika yalikuwa ni wazalishaji wa mali-ghafi wa viwanda vya watawala wao. Baada ya Afrika kujikomboa, Afrika ilianza harakati za kujikomboa ki uchumi. Na mataifa mengi yalijenga viwanda vya kila bidhaa muhimu.
 Kuanzia miaka ya tisini, mataifa mengi ya Afrika yaliingia katika Uchumi huria ulioambatana na vyama vingi vya kisiasa. Uchumi huru ulileta changamoto nyingi hasa kwa viwanda vingi vya ndani. Uchumi guru ulikuja na bidhaa bora, nzuri na za aina tofauti tofauti.

Viwanda vya ndani vilishindwa kuhilimili mikikimiki ya ushindani, ukichanganya na utawala na usimamizi mbovu, ufisadi, na hujuma viwanda vingi vilikufa. Kuanzia miaka hiyo ya tisini mwishoni na miaka ya elfu mbili na kuendelea, Afrika imekuwa ikipokea kila aina ya bidhaa kutoka nje ya bara hili, ziwe bidhaa mpya au mitumba.

Kilichonisukuma kuandika ni baada ya kuhudhuria mhadhara kuhusu kupiga marufuku mitumba kwa mantiki ya kutengeneza chachu ya kufufua viwanda vyetu hasa hasa viwanda vya nguo na viatu, ikizingatiwa Tanzania tunazalisha pamba na ngozi. Hapo awali, mitumba ilikuwa ni ya nguo na viatu tu. Leo hii kuna mitumba ya kila aina. Mitumba ya nguo, viatu, magari, bidhaa za majumbani, ndege, meli,baisikeli,vifaa vya maosipitalini,mashuleni nakadhalika. Tuna mitumba hadi ya Wataalamu.
Nia yangu sio kuongelea aina za mitumba inayoingia Afrika na Tanzania ikiwepo. Nia yangu ni kujaribu kuona ni namna gani hii mitumba inaweza kuisadia Afrika hasa hasa Tanzania katika hii Sera ya Uchumi wa viwanda. Kwa muda mrefu, Afrikaimelalamika kuwa jalala la bidhaa chakavu na kukuuu kutoka nje. Mbinu nyingi zimefanyika kuzuia uingizwaji wa bidhaa chakavu,kukuu na zilizo chini ya kiwango, aidha kwa kuzitoza kodi kubwa au kwa kuzipiga marufuku.

Pia viongozi wa Kisiasa wamejeribu Mara nyingi kukataa uingizwaji wa mitumba katika mataifa yao ya Afrika. Hivi karibuni tulishuhudia jumuiya ya Afrika Mashariki ikiazimia hadi ifikapo mwaka 2019 iwe mwisho wa kuingiza mitumba katika jumuiya.

Dalili za kushindikana kwa azma hii zishaanza kuonekana kwa majirani zetu Kenya kushinikizwa hadi kujitoa katika mpango huo. Hivyo basi mbinu pekee inayobaki ni Afrika kuwa na viwanda vyake vitakavyozalisha bidhaa kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao ya ndani. Tatizo litabaki kwenye ushindani.

Mimi siungi mkono hoja ya kupiga marufuku MITUMBA na siungi mkono hoja ya kuwekeza katika viwanda vitakavyodhalisha bidhaa kama za nje halafu tuhimizane kuwa na UZALENDO katika kutumia bidhaa zetu.

Nashauri tujenge VIWANDA vitakavyo RECYCLE MITUMBA ya kila aina, iwe nguo, viatu,magari,vifaa vya kielektroniki na kadhalika. so called conflict of interest 

Baada ya KU RECYCLE, tuwauzie tena wazungu malighafi.  Hapa na maanisha kwamba TU SI RECYCLE hadi kuzalisha bidhaa, bali tuichakate MITUMBA iwe tena malighafi.

Kwa sisi kuwa na viwanda vya aina hii tutaepusha the so called conflict of interest na tutakuwa unique katika aina ya viwanda tulivyonavyo.

Theophani C. Ishika
Assistant Lecturer
CFR.

BALOZI WA KUWAIT ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA DODOMA

0
0
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem akimkabidhi vitabu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma UDOM, Profesa Frowin Nyoni (kulia) na kukutana na baadhi ya viongozi na wahadhiri wa Chuo hicho. kushoto ni Mkuu wa Chuo Cha Sayansi ya Kijamii na Masomo ya Kibinadamu Profesa, Albino Tenge.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem katika picha y pamoja akisalimiana na Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma UDOM, Profesa Frowin Nyoni (wa nne kushoto).
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem akimkabidhi kitabu Mkuu wa Chuo Cha Sayansi ya Kijamii na Masomo ya Kibinadamu Profesa, Albino Tenge kushoto na kulia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma UDOM, Profesa Frowin Nyoni.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem akielekeza jambo mara baada ya kukabidhi vitabu kwa uongozi wa Chuo hicho.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili katika Chuo Kikuu cha UDOM
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live




Latest Images