Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

KAMISHNA MKUU WA TRA AZINDUA MRADI WA TRA NA JICA WA KUWAJENGEA UWEZO WAFANYAKAZI WA TRA


Wafanyakazi wa Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel wamtembelea mtoto Julius Kaijage

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel ambao walifika katika mkoa huo kwa ajili ya kumjulia hali na kufuatilia maendeleo ya elimu ya mtoto Julius Kaijage ambaye mwaka 2013 alifanyiwa upasuaji wa Moyo nchini humo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiwa katika kikao na wafanyakazi wa Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel ambao walifika katika mkoa huo kwa ajili ya kumjulia hali na kufuatilia maendeleo ya elimu ya mtoto Julius Kaijage ambaye mwaka 2013 alifanyiwa upasuaji wa Moyo nchini humo.
Mama Judy Shore kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel ambaye anaishi nchini Marekani wakizungumza jambo na mtoto Julius Kaijage ambaye mwaka 2013 alifanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel. Mama Shore aliamua kuja nchini kumjulia hali mtoto Julius baada ya kupata taarifa za kupona kwake ugonjwa wa moyo.
Mama Judy Shore na Tamar Shapira kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel wakizungumza jambo na mtoto Julius Kaijage ambaye mwaka 2013 alifanyiwa upasuaji wa moyo nchini humo. Wafanyakazi wa SACH walitembelea mkoa wa Kagera kwa ajili ya kumjulia hali mtoto huyo.
Tamar Shapira kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel akipokea zawadi ya kitenge kutoka kwa mtoto Julius Kaijage ambaye mwaka 2013 alifanyiwa upasuaji wa moyo nchini humo. Wafanyakazi wa SACH walitembelea mkoa wa Kagera kwa ajili ya kumjulia hali mtoto huyo.Picha na JKCI

Chuo cha Ustawi wa Jamii chafanya kongamano la kitaaluma na kujadili mada;"Skills Development for Industrial Transformation in Tanzania".

$
0
0

Mkuu wa chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt. Abu Mvungi(wa
pili toka kulia) akizindua Jarida la kitaaluma liloandaliwa na idara ya
taaluma ya chuo cha Ustawi wa jamii,wa tatu kulia ni Makamu Mkuu wa chuo utawala Dkt.Zena Mabeyo akifuatiwa na mtoa Mada mkuu kwenye kongamano hilo Bw. Kabeho Solo.
Toka kushoto Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt.Abu Mvungi,Mtoa mada mkuu Mr. Kabeho solo na Makamu Mkuu wa chuo Utawala Dkt.Zena Mabeyo wakimkabidhi cheti Agneta Ishengoma mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi kwenye masomo kati ya wahitimu wa mwaka huu 2017 kwenye
kongamano la kitaaluma chuoni hapo.
Mtoa mada Mkuu Bw Kabeho solo akiongoza mjadala kwenye kongamano hilo lililo hudhuriwa na wahadhiri na alumni wa chuo cha Ustawi
wa Jamii.

MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO NOVEMBA 25,2017

MAJALIWA: TANESCO KAWAHUDUMIENI WANANCHI VIJIJINI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liwafuate wananchi walioko katika vijiji vinavyotarajiwa kuunganishiwa umeme kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kuwahudumia.

Amesema Serikali imetenga shilingi trilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijaunganishiwa nicety hiyo nchini, hivyo ni vema wakawatembelea wananchi katika maeneo yao na kuwahudumiahuko huko.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana jioni (Ijumaa, Novemba 24, 2017) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa michezo Tunduru, ambapo aliwasisitiza watumishi wa TANESCO kutokaa maofisini na badala yake wakawahudumie wananchi katika vijiji vyao.

Alisema katika kipindi hiki ambacho Serikali inatekeleza miradi ya kusambaza umeme vijini kupia REA, TANESCO wanatakiwa kwenda vijijini na kuwaandikisha wananchi wanaohitaji huduma hiyo pamoja na kufungua vituo vya muda vya malipo.

Waziri Mkuu alisema hatua hiyo itawapunguzia wananchi gharama za kusafiri hadi kwenye makao makuu ya wilaya kufuata huduma mbalimbali ikiwemo ya kulipia gharama za kuunganishiwa umeme katika nyumba zao.

Alisema Serikali imedhamiria kusambaza huduma ya nishati ya umeme katika vijiji vyote nchini vikiwemo vya wilaya ya Tunduru ambapo wananchi hao wataunganishiwa umeme huo kwa gharama ya sh. 27,000 tu.

Pia Waziri Mkuu aliesema wananchi hawatowajibika tena katika kulipia gharama za nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.

Waziri Mkuu aliongeza kwamba lengo la Serikali ya awamu ta tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli ni kufikisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania na kwa vile ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi vitafungiwa sola, jambo ambalo litafungua fursa za ajira na kukuza uchumi kwa wananchi na Taifa.

Waziri Mkuu alisema huduma hiyo ni muhimu kwani mbali ya kutumika katika matumizi ya majumbani, pia kwa kusogezwa karibu na maeneo ya pembezoni itawezesha zahanati, shule ,viwanda na vituo vya afya kuwa na umeme.

Awali Waziri Mkuu alitembea na kukagua shughuli za ujenzi wa mradi wa kituo cha afya kinachojengwa katika eneo la Nakayaya wilayani Tunduru pamoja na kukagua ghala la kuhijfadhia korosho na kisha kupokea taarifa ya kiwanda cha kubangulia korosho cha Korosho Afrocan Limited.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMAMOSIni, NOVEMBA 25, 2017.

Serikali kutoa leseni kwa hospitali na vituo vya afya vya Umma vitakavyokidhi vigezo vya ubora

$
0
0
Na.WAMJW,Mtwara

Serikali inatarajia kutoa leseni kwa hospitali na vituo vya afya vya Umma vitakavyokidhi vigezo vya ubora wa kutoa huduma za afya ili mwananchi wajue kituo atakachoenda kina ubora gani wa huduma hivyo nchini

Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati akiongea na Viongozi na Watendaji wa afya wa Mkoa na Wilaya zake kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara wakati wa zoezi la kutoa ngao kwa wilaya iliyofanya vizuri na vituo vya afya vilivyofanya vizuri wakati wa zoezi la tathimini ya kutoa nyota kwa vituo vya kutolea huduma za afya.

Dkt.Ndugulile alisema hivi sasa serikali inasisitiza kuweka ubora wa huduma za afya katika vituo vyote vya afya vya umma ili kukidhi ubora unaotakiwa wa kutoa huduma kwa wananchi”tunakwenda mbali zaidi usipokuwa na vigezo hospitali yako na kituo chako hutopewa leseni”

Hata hivyo amewataka wale wote waliopewa maelekezo ya nini wafanye basi viongozi wawajibike kwa kurekebisha changamoto zilizopo na wasingoje idara ya uhakiki ubora kutoka wizarani waje kukagua kwani Lengo liliowekwa na wizara ni kila kituo cha afya kupata nyota tatu hadi kufikia mwezi juni mwakani.

“Nyinyi wengine wote hamkustahili kupata cheti hata kimoja hapa,Mkoa wa Mtwara asilimia 3 za vituo vyenu vina nyota mbili na asilimia 51 vina nyota moja na zaidi ya nusu mna nyota 1 na asilimia 46 mna nyota sifuri hali ya utoa huduma bado”Nimetoka hapo zahanati ya Ziwani,kwakweli hapana,ubora wa kutoa huduma pale hapana wakati mpo mjini.
Naibu Waziri akimpongeza Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu baada ya kuibuka mshindi.Dkt.Ndugulile aliipongeza Wilaya hiyo kwa mpangilio mzuri wa utoaji huduma pamoja na utunzaji wa kumbukumbu kwenye stoo ya dawa katika kituo cha afya cha Mtambaswala ambacho kimeanza miezi miwili iliyopita lakini kimeonyesha ufanisi wa hali ya juu.
Picha ya pamoja mara baada ya Naibu Waziri kutoa ngao na vyeti kwa washindi kwa Mkoa wa Mtwara
Dkt.Ndugulile akisoma taarifa ya dawa katika Zahanati ya Ziwani iliyopo Manispaa ya Mtwara,ambapo Naibu Waziri huyo alichukizwa hali ya miundombinu na uwajibikaji wa Zahanati hiyo na kuwapa miezi miwili wawe wamefanya marekebisho kama walivyoelekezwa.
Mkuu wa Zahanati ya Shangani akipokea cheti kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya.


CHUO KIKUU MZUMBE CHAZINDUA RIPOTI YA UTAFITI JUU YA KILIMO CHA MKATABA KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Juu ya Fursa na Changamoto za Kilimo cha Mkataba uliofanyika chuoni hapo mkoani Morogoro Novemba 24, 2017. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka.
aibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, akionyesha nakala ya kitabu cha ripoti ya utafiti juu ya fursa na changamoto za kilimo cha mkataba. Kulia ni Mratibu wa Mradi Prof. Joseph Kuzilwa na Katikati ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dk. Hawa Tundui.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka (kushoto), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, nakala ya kitabu cha ripoti ya utafiti juu ya fursa na changamoto za kilimo cha mkataba wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripo hiyo. 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija (wa pili kulia), Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka (wa pili kushoto), Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dk. Hawa Tundui (kulia) na kushoto ni Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha, Dk. Nsubiri Isaga. 
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo pamoja na watafiti.


WAZIRI ATAKA UTEKELEZAJI UPANUZI WA VIWANDA VYA SUKARI NCHINI UFANYIKE KWA HARAKA.

$
0
0
Na John Nditi, Kilimbero

WAZIRI wa Kilimo, Dk Charles Tizeba amesema kuwa suala ya kupanua viwanda vya sukari nchini halina mbadala ni jambo la lazima ili kukidhi uchakataji mkubwa wa miwa inayolimwa kuongeza kiwango cha upatikanaji wa sukari na ya bei nafuu.

Waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na Menejimenti ya Kiwanda cha Sukari Kilombero kiwandani hapo pamoja na kwa baadhi ya wakulima na viongozi wa vyama vya zao la miwa wa pande mbili za wilaya ya Kilosa na Kilombero kwenye ukumbi wa Chuo cha Sukari Kilombero.

Alisema ,Serikali ilipoamua kuuza sehemu ya hisa zake kwa kampuni binafsi , lengo lake lilikuwa ni moja kwamba wanauowezo wa kifedha unaoendana na ufanisi na upanuzi wa viwanda kuweza kukidhi mahitaji ya zao la miwa na utengeenzaji wa sukari.

Dk Tizeba alisema , kutokana na dhana hiyo, maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuona viwanda vya sukari vinapanuliwa kwa ajili ya kukidhi usagaji wa miwa nayolimwa na mashamba ya viwanda nay a wakulima wan je na kutengeneza sukari nyingi za kujitoshereza.

Alisema ,uamuzi hyo unatokana na kubaini kuwa viwanda uwezo vya sukari ni mdogo kuchakata tani nyingi za miwa kwa msimu wa kilimo ikiwemo miwa ya wakulima wa n je na badala yake kusalia shambani na kuharibika.

“ Kinachohitajika ni utosherezaji wa sukari nchini na ya bei nafuu ,kama uwezo wa viwanda ni mdogo kuchakata miwa na kuzalisha sukari kinachohitajika ni upanuzi wa kiwanda ” alisema Dk Tizeba.Dk Tizeba alisema, kinachofanyika kwa sasa ni kuweka programu ya wizara na wenye viwanda kutakiwa kuwasilisha mpango kazi wao unaoinesha hatua za utekelezaji wa upanuzi wa viwanda vyao kikiwemo cha Kilombero .

Naye Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe, alimwomba Waziri kuuangalia kwa karibu zaidi mkoa huo kwani utafiti wake umeonesha ni kitovu cha kuzalisha sukari nchini na maziwa makuu kwa kufikisha zaidi ya tani milioni moja za sukari .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sukari Kilombero, Guy Willium akitoa maelezo ya uendeshaji na uzalishaji wa sukari katika kikao na Waziri , licha ya kueleza faida na changamoto zinazokikabili alisema ,zinahitajika zaidi ya Sh bilioni 500 kwa ajili ya mpango endelevu wa upanuzi kiwanda .Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema , mpango huo utatekelezwa kwa awamu nay a kwanza ya miaka minne kulingana na upatikanaji wa fedha ikamilika kufikia June 2021 na kukamilishwa hadi ifikapo mwaka 2025.

Alisema ,kutokana na mpango wa upanuzi wa kiwanda na mashamba ya miwa , uzalishaji wa sukari utaongezeka kutoka wastani wa tani 125,000 kwa mwaka zinazozalishwa hadi kufikia wastani tani za sukari 260,000 kwa mwaka.
Waziri wa Kilimo Dk Charles Tizeba ( kati kati) akijadiliana na Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule ( kushoto) alipofanya ziara ya kikazi katika Kiwanda kilichopo sehemu ya wilaya mbili ya Kilombero na Kilosa, mkoani Morogoro kwa ajili ya kuona shughuli za uzalishaji wa sukari na kilimo cha zao la miwa kwa kiwanda na wakulima wa nje
Waziri wa Kilimo Dk Charles Tizeba akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sukari Kilombero, Guy Willium , wakati alipofanya ziara katika Kiwanda kilichopo sehemu ya wilaya mbili ya Kilombero na Kilosa, mkoani Morogoro kwa ajili ya kuona shughuli za uzalishaji wa sukari na kilimo cha zao la miwa kwa kiwanda na wakulima wa nje.

Waziri wa Kilimo Dk Charles Tizeba akiteremka kutoka katika ndege ndogo baada ya yeye na viongozi wengine wa mkoa , wilaya za Kilombero na Kilosa , Bodi ya Sukari na wataalamu wa Kilimo kukagua eneo la mashamba makubwa ya miwa waliyolimwa na kupanuliwa na Kiwanda cha Sukari Kilombero waiiwa angani mara baada ya kupatiwa taarifa ya Kiwanda hicho na Mkurugenzi Mtendaji Guy Willium , wakati alipofanya ziara kwa ajili ya kuona shughuli za uzalishaji wa sukari na kilimo cha zao la miwa kwa kiwanda na wakulima wan je. ( Picha na John Nditi).

Dk. Kigwangalla, Naibu Katibu Mkuu CCM Mpogolo kumnadi Mabonde Udiwani Nata leo

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Bara), Rodrick Mpogolo, Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla leo Novemba 25,2017, wanatarajia kumnadi mgombea nafasi ya Udiwani katika uchaguzi mdogo wa marudio Bwana John Cheyo Mabonde anayewania kiti cha Udiwani Kata ya Nata iliyopo Nzega Vijijini.

Kampeni hizo za kishindo zinatarajia kufikia tamati leo hii katika Kata hiyo ya Nata ambapo tayari Mgombea huyo ameweza kuninadi katika maeneo mbalimbali ya Kata hiyo.Awali Dk.Kigwangalla ambaye ni Mbunge wa jimbo hilo, aliwataka wananchi kuhakikisha wanaendelea kulinda Kata yao ambayo walishashinda tokea 2015.

“Ushindi tulishamaliza. Tulishinda Kata hii 2015. Kura za kesho ni kuhitimisha tu ushindi wetu hivyo tujitokeze kwa wingi kupiga kura za ndio kwa CCM kwa kumchagua Mabonde.” Alieleza Dk.Kigwangalla wakati wa kumandi mgombea huyo katika kampeni zilizofanyika jana Novemba 24 kwenye tawi la Mwamalulu.

Kwa upande wake, Mgombea udiwani huyo Bwana Mabonde aliendelea kuwashukuru wananchi wa Kata hiyo kwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni zake huku akiwataka kuhakikisha wanaendelea kujitokeza katika kupiga kura siku ya Novemba 26 katika kupiga kura za ndio.

“Kura zenu ni mtaji wetu. Nawaombeni sana ndugu zangu, wana Nata kujitokeza kwa wingi kupiga kura. Ushindi huu ni wetu ili kuendelea kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika vita yake ya kiuchumi na kupambanana mafisadi.

Aidha, katika mkutano huo wa jana jioni, ambao pia ulikuwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho waliweza kuwashukuru wananchi kwa kuendelea kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi (CCM).
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla wakicheza ngoma wakati wa shamrashamra za kampeni hizo
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora,Ndugu Hassani Wakasubi akimadi Mgombea nafasi ya Udiwani Kata ya Nata, Bwana John Cheyo Mabonde kwenye viwanja vya kampeni katika tawi la Mwamalulu katika Kijiji cha Mwamalulu Kata hiyo ya Nata, Katika jimbo la Nzega Vijijini, jana jioni Novemba 24,2017.
Mgombea nafasi ya Udiwani Kata ya Nata, Bwana John Cheyo Mabonde akiwa amebebwa juu wakati wa kampeni hizo kwenye viwanja vya kampeni katika tawi la Mwamalulu katika Kijiji cha Mwamalulu Kata hiyo ya Nata, Katika jimbo la Nzega Vijijini, jana jioni Novemba 24,2017.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa pamoja na Mgombea nafasi ya Udiwani Kata ya Nata, Bwana John Cheyo Mabonde wakifanya matembezi wakati wa kuelekea kwenye viwanja vya kampeni katika tawi la Mwamalulu katika Kijiji cha Mwamalulu Kata hiyo ya Nata, Katika jimbo la Nzega Vijijini, jana jioni Novemba 24,2017.

KUMBILAMOTO; VIJANA MUUNGENI MKONO RAIS MAGUFULI AMEFANYA MAKUBWA

$
0
0
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na umoja wa Vikundi vya Jogging Vingunguti mara baada ya kumaliza uasafi wa mwezi katika juhudi za kumuunga mkona Rais John Pombe Magufuli kuifanya Tanzania iwe safi.

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, akiongoza zoezi la Usafi katika mtaa wa Miembeni kata ya Vingunguti kama agzio la Rais lilivyotaka kila Jumamosi ya Mwisho wa mwezi watu kufanya usafi
Afisa Ugavi wa Manispaa ya Ilala,Vicent Odero akitoa shukrani kwa umoja wa Vikundi vya Jogging Vingunguti kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usafi wa Mwisho wa Mwezi
Afisa usafishaji wa Manispaa ya ilala Cosmas Mwaitete akihahidi kuwaongezea vifaa zaidi vya kufanyia usafii umoja wa wakimbiaji mbio za pole Vingunguti
Mtangazaji wa kituo cha Radio cha east Afrika Zembwela akionyesha kwa vitendo namna ya kufanya usafi katika mitaa ya vingunguti mara baada ya kualikwa na Naibu Meya.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, akitoa uchafu kwenye mitaro ya mitaa ya Vingunguti
Sehemu ya wana kikundi wakikimbia kabla ya kuanza kwa usafi wa mazingira kata ya VINGUNGUTI

NEC YASISITIZA AMANI NA UTULIVU UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATA 43

DKT. MWAKYEMBE AIPONGEZA PSPF KWA KUTWAA TUZO YA KIMATAIFA YA ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017

MAALIM SEIF ABAMU

BAMIZA CHART 25TH NOVEMBER 2017

WAZIRI MWAKYEMBE KUZINDUA LIGI YA WANAWAKE ARUSHA

$
0
0
Ligi ya wanawake inatarajia kuanza Jumapili Novemba 26, 2017 kwenye vituo viwili vya Dar Es Salaam na Arusha ambapo kundi A litakuwa Dar es Salaam likitumia Uwanja wa Karume wakati kundi B litakuwa Arusha likitumia Uwanja wa General Tyre.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dk. Harrison Mwakyembe kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi  katika mchezo wa uzinduzi wa Ligi Kuu soka ya Wanawake jijini Arusha.
Mbali ya Dk. Mwakyembe, wageni wengine wanaotarajiwa kuwa katika uzinduzi huo ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo; Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred pamoja na viongozi wengine wakiwamo Wakuu wa Wilaya mbalimbali za Arusha na mikoa ya jirani.

Kundi A lina timu za Mlandizi Queens ya Pwani, JKT Queens ya Dar es Salaam, Fair Play ya Tanga, Simba Queens ya Dar es Salaam, Ever Green Queens ya Dar es Salaam na Mburahati Queens ya Dar Es Salaam.
Kundi B lenyewe linajumuisha timu za Marsh FC ya Mwanza, Kigoma Sisters ya Kigoma, Panama FC ya Iringa, Baobab Queens ya Dodoma, Alliance Queens ya Mwanza na Majengo Queens ya Singida.

Ufunguzi rasmi wa ligi hiyo utafanyika mkoani Arusha Jumapili Novemba 26, 2017 na mchezo wa ufunguzi utakuwa kati ya Panama FC itakayocheza na Alliance Queens mchezo utakaotanguliwa na hafla ya ufunguzi.
Katika siku hiyo kituo cha Dar Es Salaam kinachotumia Uwanja wa Karume nako kutakuwa na mchezo mmoja utakaowakutanisha Mlandizi Queens dhidi ya JKT Queens.

Makatibu wakuu nchini wafanya Mkutano wa Kuvutia Uwekezaji nchini China

$
0
0
Katibu Mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja na Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Prof Adolf Mkenda wakutana na wawekezaji kutoka makampuni mbalimbali kwenye Mkutano wa Kuvutia Uwekezaji uliofanyika Ubalozi wa Tanzania  nchini China. 
Mkutano huu umehudhuriwa na wawakilishi wa makampuni 100 yenye nia ya kuwekeza Tanzania. Aidha wamekutana na Uongozi wa Benki ya AIIB iliyoanzishwa kutoa mikopo kwa miradi ya miundombinu kwa nchi wanachama wa Belt&Road. Benki hiyo imeikaribisha Tanzania kujiunga nayo ili iweze kufaidika na fursa za mikopo nafuu. 
Vilevile, wamekutana na Uongozi wa Kampuni ya Hainan Group (H&A Group) inayomiliki mashirika mbalimbali ya ndege na mahoteli. China imeeleza kwamba katika miaka mitano ijayo itanunua bidhaa kutoka Nje ya nchi zenye thamani ya Dola za Kimarekani Trilioni 24 hivyo nchi za Afrika zina fursa ya kunufaika na soko lake endapo zitajipanga. 
Kwenye mkutano huo China imeahidi kuendeleza ushirikiano na Tanzania katika nyanja za uchumi hususan kwenye ujenzi wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa Bagamoyo SEZ. 
Pia China imeeleza kwamba inaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kutekeleza miradi mingine ya ujenzi wa miundombinu.
 Katibu Mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja akiongea  na wawekezaji kutoka makampuni mbalimbali kwenye Mkutano wa Kuvutia Uwekezaji uliofanyika Ubalozi wa Tanzania  nchini China. 
 wawakilishi wa makampuni 100 yenye nia ya kuwekeza Tanzania. 
 Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Prof Adolf Mkenda akiongea na wawekezaji kutoka makampuni mbalimbali kwenye Mkutano wa Kuvutia Uwekezaji uliofanyika Ubalozi wa Tanzania  nchini China. 
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akiwa na maafisa wa ubalozi pamoja na wawakilishi wa makampuni 100 yenye nia ya kuwekeza Tanzania. 

WAHITIMU CHUO CHA MIPANGO WATAKIWA KUWA SEHEMU YA SULUHISHO YA CHANGAMOTO ZA JAMII

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amewataka  Wahitimu 3108 wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP)   waliotunukiwa  tuzo zao  katika  Fani mbalimbali kwa mwaka 2016/2017 kuwa sehemu ya suluhisho katika changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi nchini pindi  watakapoanza kuwatumikia wananchi hao na siyo kuwa sehemu ya matatizo katika jamii.

Akizungumza katika mahafali hayo ya 31 ya Chuo hicho yaliyojumuisha Kampasi ya Dodoma na Mwanza yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Chuoni hapo Maeneo ya Miyuji mjini Dodoma Dkt. Kijaji amesema kuwa elimu waliyoipata wakaifanyie kazi kwa uhalisia wa maisha ya Wananchi waliopo maeneo mbalimbali ili kuliwezesha Taifa kufikia uchumi wa kati hata kabla ya 2025 kama Dira ya Taifa linavyotuelekeza.

‘Wahitimu wetu wana deni, deni hilo ni utumishi uliotukuka. Nendeni mkawatumikie Watanzania nendeni mkairejeshe imani ya Watanzania  iliyoanza kupotea kwa Wataalam wa fani ya Mipango ya Maendeleo Vijijini’. alisema Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji aliongeza kwa kuwataka Wahitimu hao kwenda kuwafundisha Watanzania kwa vitendo mipango na mbinu thabiti ili waweze kuzalisha kwa tija kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu na ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja. Aidha alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haitokuwa tayari kuwavumilia Wataalamu wazembe makazini na kuwataka wakafanye kazi kwa weledi mkubwa kwa manufaa ya Taifa. 
Dkt. Kijaji amefafanua kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu bora itakayowaongezea maarifa ili kuwa chachu katika Maendeleo ya Taifa.

‘Serikali inatekeleza majukumu yake kwa vitendo, ndiyo maana mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu inapewa kipaumbele cha kwanza (first charge). Alisema Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji ametoa wito kwa Taasisi za Elimu ya Juu zote Nchini kutoa mafunzo yatakayowawezesha Wahitimu mbalimbali kuweza kujiajiri pindi wamalizapo masomo yao ili kuongeza kasi ya uchumi nchini.

Katika hatua nyingine Dkt. Kijaji amekipongeza Chuo hicho kwa utoaji wa elimu bora katika fani mbalimbali kwa kuwa idadi ya wanachuo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka na kwamba huo ni mfano tosha kuwa taaluma inayopatikana katika Chuo hicho ni nzuri na kutoa rai kwa wananchi wengine kuleta watoto wao kupata taaluma mbalimbali.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Prof. Hozen Mayaya amesema kuwa wameendeleza, kuboresha na kudumisha mahusiano bora kati ya Chuo na wadau mbalimbali.

Prof. Mayaya aliongeza kuwa ushirikiano mzuri wa wadau wao umekuwa kichocheo kikubwa katika kutekeleza majukumu yao makuu ya kufundisha, kufanya utafiti na kutoa huduma za ushauri na uelekezi kwa wadau mbalimbali.

‘Chuo kinajivunia kuongeza udahili wa Wanafunzi 6,129 kwa mwaka 2016/17 kutoka wanafunzi 4,916 kwa mwaka 2015/16 ikiwa ni ongezeko la asilimia 24’. aliongeza Prof. Mayaya.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo hicho Prof. Razack Lokina katika hotuba yake ya kumkaribisha Mgeni Rasmi amesema kuwa Uongozi wa Chuo umeendelea kutekeleza wajibu wake wa kuandaa wataalamu wa mipango ya maendeleo hasa vijijini ambako watanzania wengi wanaishi.

‘Utekelezaji wa wajibu huu umeendana sambamba na kuongeza uwezo wa Chuo katika kutoa mafunzo yanayozingatia umahiri, kufanya tafiti na kutoa huduma za uelekezi katika Nyanja zote za mipango ya maendeleo’. aliongeza Prof. Lokina.

Katika mahafali hayo ya 31 ya Chuo hicho jumla ya wahitimu 3,108, wanawake 1,631 wanaume 1,477 wamehitimu ngazi ya Astashahada, Stashahada, na Shahada za Uzamili.

Imetolewa na:
Benny Mwaipaja
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akihutubia wahitimu na wageni waalikwa  katika mahafali ya 31 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwashudia  wahitimu wakiwa wanavaa  kofia (hawapo pichani) baada ya kuwatunuku tuzo  za fani mbalimbali kwenye mahafali ya 31 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) mjini Dodoma.

 Wahitimu wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) wakivaa kofia zao mara baada ya kutunukiwa tuzo mbalimbali katika mahafali ya 31 ya Chuo hicho mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akimtunuku mhitimu Felista Mayunga Shahada ya Uzamili katika  Uchumi wa Maendeleo katika mahafali ya 31 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati) akiwa na  viongozi wa Chuo na  wageni waalikwa katika picha ya  pamoja na wahitimu wa  Stashahada za Uzamili  na Shahada za Uzamili katika  mahafali ya 31 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) mjini Dodoma. 

Picha na Kitengo cha Mawasiliano 
Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango

mbio za 'Aids Trust Fund Marathon' zafana

$
0
0
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde,  akimkabidhi Cheti mwakilishi wa Mkapa Foundation, Deogratius Rimoy, kutambua mchango wa kufanikisha mbio za 'Aids Trust Fund Marathon' za Kilometa 5, 9 na 21  zilizofanyika leo asubuhi jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, kuelekea wiki ya Siku ya Ukimwi Duniani. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde,  akimkabidhi Cheti Mkurugenzi wa kampuni ya Montage, Teddy Mapunda, kutambua mchango wa kufanikisha mbio za 'Aids Trust Fund Marathon' za Kilometa 5, 9 na 21  zilizofanyika leo asubuhi kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, kuelekea wiki ya Siku ya Ukimwi Duniani.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde,  akiongoza matembezi ya Kilometa tano.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde (wa pili kuli)  akiongoza mazoezi ya viungo baada ya kumalizika mbio hizo.

The State University of Zanzibar (SUZA) and Zhejiang University of Media and Communication (ZUMC) forge academic partnership

$
0
0
Related image

The State University of Zanzibar (SUZA) and Zhejiang University of Media and Communication (ZUMC) signed a five year extendable Memorandum of Understanding  (MoU) on promotion of cooperation and the advancement of academic, research and educational disciplines. This agreement was reached on Friday 24th November, 2017 at Tunguu Main Campus of the State University of Zanzibar.
D:\MoU-ZUMC-SUZA\ZUMC - ii.jpgD:\MoU-ZUMC-SUZA\ZUMC - iv.jpg
Memorandum of Understanding signing event. Prof. Zhaowu Tang, the ZUMC Vice Chairman who led a mission of four members signed on behalf of his institution in the presence of Dr. Haji Mwevura, the Acting Vice Chancellor and Deputy Vice Chancellor for Academics, Research and Consultancy.

The areas of cooperation to be covered in this cooperation are staff and student exchange, joint research activities and publications, visits for studying teaching principles and methods, development of cooperation projects and of joint degrees, also participation in seminars, congresses and meetings.

Under this cooperation the State University of Zanzibar will be responsible for initiating staff exchange programmes, facilitating the provision of Kiswahili language experts to Zhejiang University of Media and Communication in addition to facilitating and cooperating with academicians of ZUMC in conducting research in Zanzibar in related field areas of cooperation.
The responsibilities of Zhejiang University of Media and Communication in this cooperation will be to support media and communication programmes for SUZA staff and students by granting them scholarships to study in China. ZUMC will also provide opportunities for SUZA staff in developing their knowledge, skill and attitude in order to engage with and contribute effectively to tackling global challenges. The University will provide professional teachers in relevant specialties and advance the labs for media and communication researches and it will facilitate exchange students programme.
The State University of Zanzibar envisages introducing the School of Computing, Communication and Media in the near future and through this School media studies will be taught. Currently SUZA owns the Centre for Digital Learning (CDL) which runs digital television studio for educational purposes.  ZUMC delegation paid a brief visit to this studio.
D:\MoU-ZUMC-SUZA\ZUMC - i.jpgD:\MoU-ZUMC-SUZA\ZUMC - viii.jpg
SUZA and ZUMC officials in discussion (right) and a visit at CDL TV Studio (left).

Earlier before signing the MoU, Prof. Zhaowu Tang informed that ZUMC is ready to influence its expertise to SUZA as it has extensive experience in operating media industry saying that they are sincerely ready to work with SUZA.
Dr. Mwevura said that ZUMC has many Zanzibari students pursuing their undergraduate media studies, he appealed to Prof. Tang to think of granting Masters Degree scholarships to some of them who come out with very good performance so as to serve at the State University of Zanzibar on completion of their studies.
During their one day visit in Zanzibar the delegation was expected to meet with Hon. Riziki Pembe Juma, the Minister of Education and Vocational Training at the Ministry quarters.
Zhejiang University of Media and Communication (ZUMC) is one of China’s major hubs that cultivate specialized talents for the broadcast industry and other industries in media and communications. For more than thirty years, ZUMC has provided central and local broadcast and media industries with a myriad of specialized talents. Almost 14,000 full-time students are currently studying in over fifty programmes at the thirteen Colleges and Schools of ZUMC.

Ajali ya gari aina ya Toyota Noah Kilombero- Mikumi mkoani Morogoro

$
0
0
 Wasamaria wema akiwemo Mwandishi wa habari na mpiga picha wa Kituo cha ITV , Mkoa wa Morogoro, Hussein Nuha wakitoa msaada wa kusaidia mmoja wa majeruhi ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ambaye ni dereva wa gari Toyota Noah namba ya usajili T 782 DKV  inayofanya safari zake mji wa Ruaha   Kilosa - Mikumi baada ya gari hiyo kupinduka  eneo la Kijiji cha Lumango, katika  kona kali ya barabara ya Kilombero- Mikumi  katika ajali hiyo hapakutokea kifo chochote na majeruhi wote takribani 10 walikimbizwa katika Hospitali ya St Kizito   iliyopo Mikumi,  wilayani  Kilosa.
……………………………….
  Mmoja wa majeruhi wa ajali akimsaidia  kumbeba mwezake mama wa makamo  wote majina yao hayakuweza kufahamika mara moja  ambao walipata ajali baada ya gari Toyota Noah yenye namba ya usajili T 782 DKV  inayofanya safari zake mji wa Ruaha   Kilosa - Mikumi  kupinduka eneo la Kijiji cha Lumango, katika  kona kali barabara ya Kilombero- Mikumi , katika eneo la ajali hiyo hapa kuwa na  kifo chochote na majeruhi takribani 10 walikimbizwa katika Hospitali ya St Kizito  iliyopo Mikumi , wilayani Kilosa.( Picha na John Nditi).
Gari  aina ya Toyota Noah yenye namba ya usajili T 782 DKV  inayofanya safari zake mji wa Ruaha   Kilosa - Mikumi  baada ya kupinduka eneo la Kijiji cha Lumango, katika  kona kali barabara ya Kilombero- Mikumi

Wasamaria wema akiwemo Mwandishi wa habari na mpiga picha wa Kituo cha ITV , Mkoa wa Morogoro, Hussein Nuha wakitoa msaada. Picha na John Nditi
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images