Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA IJUMAA LEO NOVEMBA 24,2017


TANZIA:MBUNGE WA SONGEA MJINI LEONIDAS GAMA AFARIKI DUNIA

$
0
0
Mbunge wa Songea mjini na Diwani wa Songea mjini, mkoa wa Ruvuma, Mhe. Leonidas Gama Enzi za uhai wake akiwa kwenye kikao cha madiwani. Mhe. Gama amefariki usiku wa kuamkia leo Novemba 24, 2017, wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya Peramiho mkoani humo. Itakumbukwa ya kwamba Mhe. Gama alikuwa nchini India ambako nako alikuwa akitibiwa. 

Mheshimiwa Gama kabla ya kuwa mbunge amewahi kushika nyadhifa nyingine za kiserikali ikiwemo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro wakati wa utawala wa awamu ya Nne. Bunge limethibitisha ,kutokea kwa kigfo hicho na kwamba taarifa Zaidi zoitatolewa baadaye. 

Taarifa za kifo chake zimeanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo marafiki zake wa karibu na marehemu, akiwemo diwani wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam, Mhe. Songoro Mnyonge ameandika katika ukurasa wake wa Facebook, akieleza kusikitishwa kwake na kwamba taarifa za kifo cha mbunge huyo amezipokea majira ya saa 7 usiku wa kuamkia leo Novemba 24, 2017.

Katika maandishi yake Mhe. Mnyonge alieleza masikitiko yake kwani ni wiki tatu tu Mhe. Gama alimpigia simu Mhe. Songoro Mnyonge na walijadiliana kuhusu matibabu ya nduguye, Dominic Gama ambaye anapatiwa matibabu nchini Afrika Kusini.
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Leonidas Gama akipimwa afya na Muuguzi Asha Shao bungeni Dodoma.
Katika picha hii ya maktaba, Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akimuapisha Mhe. Leonidas Gama kuwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
Katika picha hii ya maktaba Mhe. Waziri Mkuu, akizungum,za jambo na Mhe. Leonidas Gama, mbunge wa Songea mjini, kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Katika picha hii ya maktaba, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe.Leonidas Gama akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Rombo mara baada ya kuwasili katika shule ya sekondari Olele kwa ziara ya kikazi.
Mhe. Gama (mwenye jaketi jeupe), akiwa na viongozi wengine wa mkoa wa Kilimanjaro, akitekeleza majukumu yake Enzi za uhai wake.
Mhe. Leonidas Gama akiwa na wabunge wenzake, Mhe. Hamisi Kigwangalla, (mbunge wa Nzega), na Mhe. Sixtus Mapunda, Mbunge wa Mbinga mjini.

WAZIRI MKUU AMPA OFISA ARDHI WA NAMTUMBO MWEZI MMOJA KUFIDIA WANANCHI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempa mwezi mmoja Ofisa Ardhi wa wilaya ya Namtumbo Bw. Maurus Yera awe ametafuta ardhi ya kuwafidia wakazi wa kijiji cha Lwinga wilayani Namtumbo. Wakazi hao 21 mwaka 2008 eneo lao lenye ukubwa wa ekari 101 lilitwaliwa na Serikali kupitia halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili ya kupisha ujenzi wa shule ya sekondari ya mkoa wa Ruvuma na waliahidiwa kulipwa fidia.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Alhamisi, Novemba 23, 2017) alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Lwinga akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma. Alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao kupitia mabango, ambapo walimuomba awatatulie kero hiyo ya madai ya fidia ya ardhi iliyodumu kwa miaka 10 bila kupatiwa ufumbuzi.

Waziri Mkuu alisema haoni sababu ya Halmashauri hiyo kushindwa kuwafidia wananchi hao sehemu ya ardhi kwa muda wote huo ukizingatia wilaya hiyo ina hifadhi ya ardhi. 
“Nataka wananchi hawa wawe wamelipwa fidia yao ya ardhi kabla ya siku kuu ya Krismasi ya mwaka huu. Serikali haiko tayari kuona wananchi wake waliotoa ardhi kupisha maendeleo wakisumbuliwa," alisema Waziri Mkuu na kuongezea kwamba Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli inataka kila mtumishi ahakikishe anatumia taaluma yake vizuri kwa kuwahudumia wananchi ikiwa ni pamoja na kutatua kero zinazowakabili kwa wakati.

Pia Waziri Mkuu alitoa wito kwa wananchi hao kuhakikisha hawakubali kutoa rushwa pale wanapohitaji kupata huduma mbalimbali kutoka kwa watumishi kwa kuwa ni haki yao kuhudumiwa.Aliwataka wananchi kuwa na imani na Serikali yao na kuiunga mkono katika mapambano dhidi ya rushwa kwani vitendo hivyo vinakwamisha shughuli za maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

VIKUNDI 40 VYA VIJANA NA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KATIKA HALMASHAURI YA CHALINZE WILAYANI BAGAMOYO VYAPATIWA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 120

$
0
0
NA VICTOR MASANGU, LUGOBA BAGAMOYO

KATIKA kukabiliana na wimbi la umasikini na ukosefu wa ajira kwa vijana pamoja na wanawake hatimaye halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani imeamua kuvipatia mikopo wa kiasi cha shilingi milioni 120 Vikundi 40 vya wajasiriamali kutoka kata 15 kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi.

Akizungumza katika halfa ya makabidhiano ya hundi kwa ajili ya fedha hizo iliyofanyika katika kata ya Lugoba Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema lengo la serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufui ni kuhakikisha inawawezesha kiuchumi wananchi wake pamoja na kuwapatia mikopo ya fedha kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za ujasiriamali.

Aidha Mwanga aliwaagiza watendaji na viongozi kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu vikundi vyote ambavyo vimeshakopeshwa kufanya ukaguzi wa kina kujua fedha amabzo zimetolewa zinatumika katika matumizi sahihi kwani amebaini kuna baadhi yao wanakwenda kinyume na taratibu zilizowekwa hivyo kurudisha nyuma kasi ya maendeleo.

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze Mohamed Sume akisoma taarifa yake amebainisha kuwa fedha hizo zote zimetokana na makusanyo yatokanayo na mapato ya ndani kwa lengo la kuweza kuviwezesha vikundi hivyo ikiwa ni kutekeleza Agizo la ya Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli ya kutenga asilimia kumi kwa ajili ya kuwawezesha vijana pamoja na wanawake.

Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Said Zikatimu amesema kuwa fedha ambazo zimetolewa katika vikundi vya wajasiriamali hao ni katika kota ya kwanza ambapo pia wametenga milioni 300 kwa lengo la kuweza kuvipatia vikundi vingine ili kuweza kuongeza pato la Taifa kupitia biashara wanazozifanya.

Alisema kwamba mipango ya halmashauri hiyo ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2020 vikundi vyote vya ujasiriamali vinawezeshwa kwa kupatiwa mikopo ya kufanyia biashara zao mbali mbali sambamba na kuwapatiua wataalamu ambao watakuwa wakiwafundisha namna na kuweza kujifunza masuala mbali mbali yanayohusina na namna na kuweza kutafuta masoko katika bidhaa wanazozizalisha.

Baadhi ya wajasiriamali ambao wamenufaika na fedha hizo akiwemo Zawadi Rashid pamoja na Mwajuma Shaban walieleza malengo na matarajio yao ni kuhakikisha wanakuza mitaji yao kwa kuendeleza biashara walizonazo, ikiwemo ufugaji, kilimo, ufyatuaji wa matofali pamoja na ujenzi wa viwanda vidogo vidogo ili kuweza kujikwamua kimaisha na kukuza uchumi.
 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza na vikundi mbali mbali vya wajasiriamali  havipo pichani  kutoka halmashauri ya Chalinze katika halfa fupi ya  makabidhiano ya hundi yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 120 ambayo itaweza kuwasaidia katika kufanya biashara zao.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Said Zikatimu akizungumza jambo na vikundi vya wajasiriamali ambao walifika katika sherehe hiyo ya makabidhiano ambayo ilifanyika katika viwanja vya sokoni Lugoba.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga kulia akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 120  mmoja wa wanakikundi wajasiriamali katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya soko la Lugoba(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

WATU SABA WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA UVAMIZI WA MELI BANDARI YA DAR ES SALAAM

Mtandao wa Muziki Tanzania waipongeza Msama Auction Mart KWA KAZI NZURI YA KUPAMBANA NA UHARAMIA WA KAZI ZA SANAA

$
0
0
kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiendelea nayo muda mrefu ya kukamata wezi wa kazi za muziki na hivyo kutoa mchango mkubwa katika kupunguza uharamia na kuhamasisha uchangiaji wa pato la Taifa kupitia kazi za sanaa. 

Katika pongezi hizo Mwenye kiti wa Tanzania Musicians Network , John Kitime amesema, 'Kwa niaba ya wanachama wa chama chetu Tanzania Musicians Network, naomba nitoe shukrani kwa mchango wako mkubwa ambao kampuni yako inaufanya katika jitihada za kupunguza uharamia wa kazi za sanaa Dar es Salaam.

 Tuko tayari kushirikiana nawe kila wakati kwa lengo la kuboresha mazingira yanayohusu uboreshwaji wa stahiki za wanamuziki wakati wowote.Tunarudia tena kushukuru kwa hili'

Msama amekuwa akifanya kazi hii ya kukamata kazi zisizo halali kwa miaka mingi, na Kitime amekuwa mwanaharakati wa swala la Hakimiliki kwa miaka mingi pia.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali,Msama Auction Mart Alex Msama akizungumza na Waandishi wa Habari mapema jana jijini Dar,kuhusiana na hatua aliyofikia ya kuwakamata maharamia wa kazi zaWasanii na Wakwepa kodi kupitia tasnia hiyo,ampao pia amewashukuru wadau wa Muziki mbalimbali wakiwemo Mtandao wa Muziki Tanzania kumpongeza na kumuunga mkono katika mapambano hayo ya kazi za Wasanii hapa nchini


Mwenye kiti wa Tanzania Musicians Network , John Kitime .
NSAMA3

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kifo cha Mbunge wa Songea Mjini Leonidas Gama

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afungua wa maadhimisho ya miaka 10 ya chuo cha Ardhi Dar es Salaam

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) Tabitha Siwale wakifunua kitambaa kuashiria ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 10 ya chuo hicho Dar es Salaam jana. Kutoka (kwa waziri Mkuu) ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Prof Joyce Nadlichako, Mkuu wa ARU, Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya, Makamu Mkuu wa ARU, Prof Evaristo Riwa na Rais wa Jumuiya ya ARU, Haruna Masebu. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa pili kushoto), Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Prof Joyce Nadlichako (wa nne kushoto), Mkuu wa ARU, Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya (kushoto) na mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi wakionesha kitabu kilichozunduliwa wakati ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 10 ya chuo hicho Dar es Salaam jana. Pamoja nao (wa tatu kushoto) ni Mwenyekiti wa ARU, Tabitha Siwale,  Makamu Mkuu wa ARU, Prof Evaristo Riwa (kulia) na Rais wa Jumuiya ya ARU, Haruna Masebu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 10 ya chuo hicho Dar es Salaam jana. Pamoja naye ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Prof Joyce Ndalichako (wa tatu kushoto), Mkuu wa ARU, Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya (wa nne kushoto), mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa ARU, Tabitha Siwale (kushoto), Makamu Mkuu wa ARU, Prof Evaristo Riwa (kulia) na Rais wa Jumuiya ya ARU, Haruna Masebu. Picha na Robert Okanda Blogs

Introducing Beka Flavor's "Sarafina" Produced By Awesome

maandalizi ya michezo ya Mabunge ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza Desemba Mosi Jijini Dar

$
0
0
  Wabunge wakiwa wakijiandaa na mazoezi ya Bunge Sports Club yakiendelea kwenye Viwanja vya Chuo cha Biashara Dodoma (CBE: tayari tayari kwa michezo ya Mabunge ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza Desemba Mosi Jijini Dar es salaam.
 Mhe Omary Mgumba kushoto na Mhe Musa Sima wakinyoosha viungo
Mhe Ridhiwani Kikwete na Sixtus Mapunda wakimsikiliza Mwalimu wao

MBUNGE LEONIDAS GAMA KUZIKWA JUMATATU KIJIJINI KWAO LIKUYUFUSI RUVUMA, RAIS MAGUFULI ATUMA RAMBIRAMBI

$
0
0
Aliyekuwa mbunge wa Songea Mjini (CCM), Leonidas Gama anatarajiwa kuzikwa Jumatatu katika makaburi ya familia yaliyopo Kijiji cha Likuyufusi mkoani Ruvuma.
Gama aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa Novemba 24,2017 atazikwa Jumatatu Novemba 27,2017 katika makaburi hayo yaliyopo umbali wa kilomita 25 kutoka Songea mjini.
Bw. Issa Fussi ambaye ni msemaji wa familia na mdogo wa Gama amesema amefariki usiku wa kuamkia leo akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni ya Peramiho. Amesema Gama alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na alipelekwa hospitalini hapo Jumatano Novemba 22,2017 usiku na kulazwa hospitalini hapo.
Fussi amesema msiba huo ni pigo kwa familia kwa kuwa Gama alikuwa nguzo akitegemewa katika masuala mbalimbali ya maendeleo na kifamilia.
Amesema mwili wa marehemu Gama umehifadhiwa katika Hospitali ya Peramiho na utaratibu wa mazishi unaendelea.

TANZIA; MSIBA WA MHESHIMWA LEONIDAS GAMA

Article 5

HAYA NDIYO MAAJABU YA KIMONDO CHA MBOZI KILICHOPO MKOANI SONGWE

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kulia) akiwa ameshikilia kivutio cha utalii cha Kimondo leo wakati wa ziara yake ya kikazi katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.

Kimondo hicho kinachokadiriwa kuwa na tani 12 kiligunduliwa wilayani Mbozi mwaka 1930 na kimeundwa kwa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11.


Aidha, kimondo hiki ni cha pili kwa ukubwa kati ya 35 vilivyopo barani Afrika na cha nane kati ya 578 vilivyopo duniani kote ambavyo vimeundwa kwa chuma. Sifa kuu ya kimondo hiki ni kuwa na ubaridi wakati wote hata mchana wa jua kali.


Pamoja na mambo mengine katika ziara hiyo, amekagua ujenzi unaoendelea wa jengo la kituo cha taarifa (Information Centre) katika kivutio hicho ambalo linagharimu Shilingi milioni 400. 


Alisema Serikali kupitia wizara yake ina mpango thabiti wa kuendeleza kivutio hicho pamoja na vivutio vya ukanda wa kusini ambapo kupitia Benki ya Dunia imepata mkopo nafuu wa Dola za Kimarekani milioni 150 sawa na shilingi bilioni 340 kwa ajili ya kuendeleza vivutio vya ukanda wa kusini ikiwemo kuimarisha miundombinu.



Vivutio vingine vya utalii vinavyopatikana Mkoani Songwe ni pamoja na chemchem ya maji moto, vitalu vya uwindaji vyenye wanyamapori mbalimbali, mifupa ya shingopana songwensis, unyayo wa mtu wa kale, mapango ya popo, maporomoko ya maji, mbega weupe, kituo cha kwanza cha polisi Tanzania, mabaki ya nyumba za kufua chuma,  na ziwa Rukwa
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Muhifadhi wa Mambo ya Kale, Winnie Msacky kuhusu kivutio cha utalii cha Kimondo wakati wa ziara yake ya kikazi katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi Mkoani wa Songwe jana. 
Jengo la kituo cha taarifa katika eneo la kivutio hicho (Information Center) ambacho ujenzi wake unaendelea. Ujenzi wa kituo hiki unagharimu Shilingi Milioni 400.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KONGAMANO LA WASOMI WANATAALUMA KUFANYIKA KESHO HOTELI YA LANDMARK UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Na Dotto Mwaibale

WANAFUNZI waliohitimu vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini kesho wanatarajia kufanya kongamono kubwa la kihistoria kujadili namna watakavyoweza kutumia taaluma zao kusaidia jamii, kanisa na taifa kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mratibu wa Kongamamo hilo, Ephrahim Mwambapa alisema kongamanao hilo linaundwa na muungano wa wasomi wa kristo uitwao Tanzania for Jesus Prayer Movement ambao mlezi wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus.

Alisema licha ya muungano huo kuundwa na vijana wa kikristo lakini vijana wote wasomi kutoka katika vyuo na shule za sekondari na madhehebu mbalimbali wanaalikwa ili kuchangia mada zitakazo jadiliwa na mgeni rasmi atakuwa ni Kiongzi Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Center nchini, Askofu Flaston Ndabila.

Mwambapa alisema kuwa katika kongamano hilo kutakuwepo na mada mbalimbali na kuona ni jinsi gani kila mmoja na taaluma yake ataweza kusaidia jamii badala ya taaluma hiyo kuachwa bila ya kuifanyia kazi.

"Tunapokuwa vyuoni tunakuwa na mipango mingi ya maendeleo lakini baada ya kumaliza masomo kila mtu anakuwa kivyake wakati tunapaswa kushirikiana na jamii na ndio maana tumeona ni vizurio kuazisha muungano huu lengo likiwa kujumuika na jamii katika shughuli za maendeleo ya nchi na dini" alisema Mwambapa.

Alisema wazo la kuanzisha muungano huo nimatunda ya mkutano ya mkutano mkuu wa kitaifa wa kuliombea taifa ulioratibiwa na Askofu Flaston Ndabila na kuhudhuriwa na watu mbalimbali na vijana kutoka vyuo vikuu uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mwambapa alisema kongamano hilo litahudhuriwa na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali,sekondari baadhi wa viongozi.
Mratibu wa Kongamamo la Wasomi Wanataaluma wa Kikristo liitwalo Tanzania for Jesus Prayer Movement ambalo mlezi wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus, Ephrahim Mwambapa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Kanisa la Abundant Bressing Center (ABC), Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam, kuhusu kongamano hilo litakalofanyika Hoteli ya Landmark siku ya Jumamosi. Kulia ni Katibu Mkuu  wa Kongamano hilo, Lendian Bigoli.
Mratibu wa Kongamano hilo, Ephrahim Mwambapa akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni Kiongzi Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Center nchini, Askofu Flaston Ndabila.


WAZIRI AAGIZA UPATIKANAJI WA MAJI KWENYE HALMASHAURI KUFIKIA ASILIMIA 75 MWAKANI

$
0
0

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinafikisha huduma ya maji kwenye maeneo yao kwa wastani wa asilimia 75 hadi kufikia mwakani.

Akihutubia wadau wa Sekta ya Maji jijini hapa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Usambazaji Maji nchini, Mhandisi Kamwelwe alisema Halmashauri zinatakiwa kufikia asilimia hizo, ili kutekeleza Ilani ya chama tawala ya kuwapatia wakazi wa mijini wastani wa asilimia 95 na vijijini asilimia 85 ifikapo 2020.

“Nitumie fursa hii kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinafikisha asilimia 75 mwakani, na zile Halmashauri ambazo wanahisi hawatafika waje tuzungumze tuone namna gani ya kuweza kufika hapo” aliagiza Waziri Kamwelwe.

Mkutano wa wadau wa usambazaji maji hufanyika kila mwaka kwa lengo la kubadilishana uzoefu miongoni mwa wadau wa sekta hiyo, ambapo mada mbali mbali hutolewa na wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi, na kwa mwaka huu jumla ya mada 20 zitatolewa kwa washiriki wa mkutano huo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo, amewashukuru Jumuiya ya Wasambazaji Maji (ATAWAS) kwa jitihada zao za dhati za kuhakikisha Sekta ya Maji inapiga hatua kimaendeleo.

Pia, amewahakikishia kuwa wizara itatoa ushirikiano wa kutosha, kuhakikisha lengo la kuwapatia wananchi wa Tanzania huduma bora na endelevu ya majisafi na usafi wa mazingira linafikiwa. “Wizara yote leo ipo hapa, Waziri na Katibu Mkuu wote tupo, sasa ni nguvu gani mnayoitaka tena? Tuwahakikishie kuwa tupo pamoja na nyie ili kutimiza lengo la Serikali yetu,’’ alisema Prof. Mkumbo.

Mkutano wa mwaka wa ATAWAS umeanza tarehe 23 na kukamilika tarehe 25 mwezi Novemba na hufanyika kila mwaka kwa lengo la kubadilishana uzoefu na utaalamu katika Sekta ya Maji.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi. Isack Kamwelwe akihutubia washiriki wa mkutano katika Ukumbi wa Tanga Beach Resort.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo wakati alipokuwa akitoa neno.
Mwenyekiti wa ATAWAS, Mhandisi Mkama Bwire wakati alipokuwa akitoa maelezo.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe.

SERIKALI KUTOA MUONGOZO WA UTOAJI TIBA KWA HOSPITALI ZOTE

$
0
0
Na.WAMJW,Ruangwa.

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto inatarajia kutoa mwongozo wa utoaji tiba kwenye hospitali zote nchini ili kuwe na mfumo mzuri wa dawa muhimu ili kuepusha madaktari kuagiza dawa ambazo zipo nje ya mfumo wa dawa muhimu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa ziara yake ya kuangalia hali ya upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali .

“Kabla ya mwisho wa mwaka tunataka kutoa muongozo huo(Standard Treatment Guidline) kwa sababu imekua changamoto kwani wale wauzaji wakubwa wa dawa wamekua wakizitembelea hospitali kubwa na kuwarubuni wanunue dawa zao ambazo zipo nje ya dawa zetu muhimu”

Kwahiyo muongozo huo itakua kila ugonjwa dawa ya kwanza itakua ipi na kama itashindika dawa itakayofuata dawa ipo na hizo dawa zitaagizwa na kutunzwa na Bohari ya Dawa(MSD).

Hata hivyo Dkt.Ndugulile amewataka watendaji wa hospitali hiyo kuweka utaratibu na mpangilio mzuri na unaohitajikwa wa utunzaji wa dawa kwenye stoo ya madawa iliyopo hospitalini hapo,baada ya kukuta hakuna upangaji mzuri wa dawa na vifaa tiba “mmenithibitishia kwamba dawa zote mnazipata kwa asilimia 90 hivyo ni vyema Mfamasia wa Wilaya kuzipanga dawa hizo vizuri na kuweka kiyoyozi ambacho kitasaidia kutunza dawa kwa muda bila kuharibika”

Alisema hivi sasa nchi haina tatizo la upatikanaji wa dawa kwani bajeti ya dawa hivi sasa imeongezeka kutoka shilingi bilioni 30 mpaka zaidi ya bilioni 260 kwa mwaka huu wa fedha “bajeti hii imekua ikitolewa na Mhe.Rais amekua akizitoa fedha zote,hivyo hatuna shida ya fedha hivyo nasi hatutarajii kuwa na shida ya dawa na dawa tunazokuwa tunazipata zitunzwe vizuri”.

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE ZIARANI CHINA KUSHIRIKI MKUTANO WA FOCAC

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akifungua Mkutano wa kuvutia wawekezaji uliofanyika Ubalozi wa Tanzania nchini China na kuhudhuriwa na wawakilishi wa Makampuni 100 yenye nia ya kuwekeza Barani Afrika. Prof. Mkenda yupo nchini China kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 12 wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC unaofanyika kwa ngazi ya Watendaji. 
Prof. Mkenda akizungumza na Kiongozi wa Benki ya AIIB iliyoanzishwa kwa lengo la kutoa mikopo kwa miradi ya miundombinu kwa nchi wanachama wa Belt and Road. Benki hiyo imeikaribisha Tanzania kujiunga nayo ili iweze kufaidika na fursa za mikopo nafuu. Vilevile, Prof. Mkendaamekutana na uongozi wa Kampuni ya Hainan Group inayomiliki mashirika mbalimbali ya ndege na Hoteli zaidi ya 1000 ulimwenguni. Katika mazungumzo hayo Prof. Mkenda amewashawishi wawekeze kwenye ujenzi wa Hoteli katika maeneo ya Utalii Zanzibar na Tanzania Bara. 
Ujumbe ukifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Kiongozi wa Benki ya AIIB (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Prof. Elisante Ole Gabriel, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Lu Yongqing, aliyekuwa Balozi wa China nchini Tanzania na Mhe. Mbelwa Kairuki, Balozi wa Tanzania nchini China. 
Ujumbe kutoka Benki ya AIIB 
Prof. Mkenda akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufungua Mkutano wa Kuvutia Wawekezaji uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini China. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. Chen Xiaodong akifungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika unaofanyika tarehe 24 Novemba, 2017 Beijing, China. Baada ya ufunguzi kiongozi huyo amefanya mazungumzo ya kukuza ushirikiano na nchi nne Tanzania ikiwa ya kwanza kukutana nayo. Katika mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Mhe. Xiaodong, China imeahidi kuendeleza ushirikiano katika nyanja za uchumi hususan kwenye ujenzi wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa Eneo Maalum la Uwekezaji Bagamoyo. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. CHEN Xiaodong mara baada ya kukamilisha mazungumzo ya ushirikiano kati ya Tanzania na China. 

WAZIRI MKUU AMPA OFISA ARDHI MWEZI MMOJA KUFIDIA WANANCHI

$
0
0


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempa mwezi mmoja Ofisa Ardhi wa wilaya ya Namtumbo Bw. Maurus Yera awe ametafuta ardhi ya kuwafidia wakazi wa kijiji cha Lwinga wilayani Namtumbo.

Wakazi hao 21 mwaka 2008 eneo lao lenye ukubwa wa ekari 101 lilitwaliwa na Serikali kupitia halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili ya kupisha ujenzi wa shule ya sekondari ya mkoa wa Ruvuma na waliahidiwa kulipwa fidia.Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Alhamisi, Novemba 23, 2017) alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Lwinga akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma.

Alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao kupitia mabango, ambapo walimuomba awatatulie kero hiyo ya madai ya fidia ya ardhi iliyodumu kwa miaka 10 bila kupatiwa ufumbuzi.Waziri Mkuu alisema haoni sababu ya Halmashauri hiyo kushindwa kuwafidia wananchi hao sehemu ya ardhi kwa muda wote huo ukizingatia wilaya hiyo ina hifadhi ya ardhi.“Nataka wananchi hawa wawe wamelipwa fidia yao ya ardhi kabla ya siku kuu ya Krismasi ya mwaka huu. Serikali haiko tayari kuona wananchi wake waliotoa ardhi kupisha maendeleo wakisumbuliwa.”

Waziri Kairuki afanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini leo

$
0
0
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Jasem Al Najem leo tarehe 24 Novemba, 2017.
Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam ambapo wamezungumza masula mbalimbali kuhusu uendelezaji wa Sekta ya Madini nchini.

Waziri Kairuki amesema kuwa mazungumzo yake na Balozi wa Kuwait yamelenga katika suala la uwekezaji kwenye Sekta ya Madini ambapo ameikaribisha nchi hiyo kuja kuwekeza nchini ili kuendeleza Sekta husika.
Aidha, ameongeza kuwa, katika kikao hicho wamezungumzia suala la kuwajengea uwezo Wataalam wa Madini nchini ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Vilevile wamejadiliana suala la kubadilisha uzoefu kati ya Kuwait na Tanzania lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inachangia ipasavyo katika uchumi wa nchi husika.
 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) akiwa na Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al-Najem (kushoto),  katika ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) akipokea zawadi ya Ngao kutoka kwa Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al-Najem (kulia),  katika ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam. 
Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al-Najem (kulia) akimweleza Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) kuhusu alama mbalimbali zilizo katika Ngao kutoka nchini Kuwait, mara alipomtembelea katika ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images