Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

NBC KUPITIA HUDUMA YA ISAMIC BANKING YAANDAA FUTARI KWA WATEJA WAKE

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha, Bi. Saada Mkuya Salum (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bi. Mizinga Melu (kushoto kwake) wakichukua mlo wa futari pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Fedha, Bi. Saada Mkuya Salum (kushoto) akizungumza na Mjumbe wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk Kassim Hussein (kulia) wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bi. Mizinga Melu na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Bi. Mwinda Kiula Mfugale.
Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata kanuni za Kiislamu wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (wa pili kushoto) pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo, wakichukua mlo wa futari katika hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Bi. Mizinga Melu (kulia) akimsilikiliza Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Bi. Mwinda Kiula Mfugale (kushoto) katika wakati wa hafla hiyo. 
Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata kanuni za Kiislamu wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (katikati) akiteta jambo na Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Eddie Mhina wakati wa hafla ya futari waliyoiandaa kwa wateja wao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein.
Baadhi ya wateja wa benki ya NBC, wakila futari waliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

MAMBO YA CARNIVAL 2013 NDANI YA MJI WA MARYLAND,MAREKANI

$
0
0
13248_10200413822683623_340761968_nMdau Charles Kaiza akiwakilisha kwenye Carnival 2013 huko Baltimore Maryland. 400749_10200413813003381_332493024_nMaandamano yakiwa yamechanganya kama mdundiko. 1069172_10200413810843327_358761529_n178998_10200413820243562_2037111565_n988632_10200413824043657_1824575750_nKwa picha zaidi bofya Sundayshomari.com

Kamanda Kova ziarani nchini Marekani

$
0
0
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishna wa Polisi,Suleiman Kova (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania waishio jijini Houston,Marekani mara baada ya kupata futari ya pamoja.Kamanda Kova yupo nchini Marekani kwa ziara ya kikazi.Kushoto ni Ankal Khamsini.Kamanda Kova amewahamasisha Watanzania hao na kuwapa changamoto kubwa sana na kuwataka kuwa karibu na nyumbani wakati wowote wata pojiskia.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishna wa Polisi,Suleiman Kova akipata futari ya pamoja na wenyeji wake,Ankal Khamsin pamoja na Bw Ali Mjungu 

SERIKALI KUSHUGHULIKIA MAPENDEKEZO TOZO KODI ZA SIMU

$
0
0
Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa akisisitiza jambo juu ya tozo la kodi katika laini za simu wakati alipokutana na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Frank Shija – Maelezo)

Na. Eliphace Marwa (MAELEZO) 

Serikali yawataka wananchi kutokuwa na wasiwasi kuhusiana na mpango wa ukusanyaji wa kodi ya laini za simu.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

Mgimwa amesema kuwa Serikali inaendelea kukutana na wadau mbalimbali ili kujadili na kupokea mapendekezo kuhusiana na dhamira ya Serikali kutoza kodi kutoka katika laini za simu.

Aliongeza kuwa Serikali ina nia njema ya kuongeza mapato yake ili kuongeza kasi ya kutoa huduma za msingi kwa wananchi wake hususani wa vijijini.

“Lengo hasa la kodi hii ni kuboresha huduma za msingi vijijini kama umeme, maji na barabara ambazo ni duni sana vijijini, hata hivyo tunafanyia kazi mapendekezo mbalimbali ya wananchi na wadau wenye mitazamo mbalimbali” alisema Dk. Mgimwa.

Aidha Dk. Mgimwa amesema kuwa hivi karibuni amekutana na chombo cha watoa huduma za mawasiliano (MoAT) nakujadiliana nao na kuwaahidi kuwa mapendekezo yao yatafanyiwa kazi.

Mkutano huo umekuja baada ya wadau mbalimbali kutoa malalamiko juu ya uwepo wa tozo ya kodi ya laini za simu ambapo mmiliki wa laini ya simu atatakiwa kulipia shilimgi 1000 kila mwezi mara kodi hiyo itakapo anza kutozwa.

Waziri Mkuu aendelea na ziara yake Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiendesha pikipiki wakati alipozindua Mradi wa Pikipiki wa Kikundi cha SACCOS ya vijana wa Mbinga kwenye uwanja wa CCM mjini Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa CCM mjini Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakizungumza na Mzee Andrea Mapunda (84) wakati alipotembelea shamaba la kahawa la mzee huyo katika kijiji cha Masumuni wilayani Mbinga wakiwa katika ziar ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua mradi wa kupeleka umeme Mbambabay katika wilaya mpya ya Nyasa kutoka kwenye kituo cha kuzalisha umeme cha Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013. Kulia ni Mkewe Tunu na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Thabiti Mwambungu. Watatu Kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapongeza baadhi ya waendesha pikipiki wa Mbinga baada ya kuzindua mradi wa pikipiki za kikundi cha SACCOS ya vijana wa Mbinga kwenye uwanja wa Mpira wa CCM mjini Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

International African Festival Tubingen 2013,Kuanza tarehe 8 hadi 11 .08.2013 Mjini Tubingen,Ujerumani

$
0
0
Onyesho kubwa la kimataifa "International African Festival Tubingen 2013,linatalajiwa kuanza tarehe 8 hadi 11.Augost 2013,mjini Tübingen, jirani na Stuttgart huko Ujerumani. Maonyesho hayo ya aina yake yanatarajiwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 100,000 kutoka sehemu mbali mbali duniani.

wanasanii zaidi 600 zikiwemo bendi za muziki za kiafrika zitatumbuiza katika maonyesho hayo makubwa ya kiafrika barani ulaya.

Bidhaa na sanaa kutoka nchi mbali mbali za kiafrika ndizo zitakaonyeshwa katika maonyesho hayo,kutakuwa na mikutano katika ya wafanyibiashara wa kiafrika na wa Ujerumani kwa lengo la kukuza uhusiano wa kibiashara.

Onyesho hilo pia litaudhuriwa na mabalozi na wawakilishi wa nchi za kiafrika nchini Ujerumani,pamoja na viongozi wa jumuiya za kiafrika nchi ujerumani.

Maonyesho ya "International African Festival Tubingen " yanayo andaliwa na shirika lisilo la kiserekali Afrikaktiv e.V, chini ya mkurugenzi wake Madam Susan Enih Tatah,maonyesho hayo yanakuwa kwa kasi kubwa na kuwa na mvuto wa maelfu ya watazamaji.

Kwa wale wanao shiriki au kuhudhuria maonyesho hayo wanaweza kuwasiliana at Susan Enih Tatah – Founder & CEO
AFRIKAKTIV e.V
Call:+49(0)15210910374

kontakt@afrikafestival.net

ankal alipotembelea hospitali alikolazwa mandela jijini Pretoria Jumapili ilopita

Wanahabari watembelea Nyumba 3 za Airtel Yatosha Kigamboni

$
0
0
Meneja Mawasiliano wa shirika la nyumba la Taifa Bw, Yahaya Charahani akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati ambapo waandishi hao walitembelea eneo la kibada wilaya ya Temeke kujionea Nyumba 3 zinazoshindaniwa katika promosheni ya Airtel Yatosha. Nyumba hizi zimenunuliwa na Airtel toka shirika la nyumba la taifa kwaajili ya promosheni ya AIRTEL shinda Nyumba.kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando
Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati ambapo waandishi hao walitembelea eneo la kibada wilaya ya Temeke kujionea Nyumba 3 zinazoshindaniwa katika promosheni ya Airtel Yatosha. Nyumba hizi zimenunuliwa na Airtel toka shirika la nyumba la taifa kwaajili ya promosheni ya AIRTEL shinda Nyumba 3.


Mwishoni mwa wiki hii Shirika la nyumba la taifa limewathibitishia watanzania kwamba tayari nyumba tatu zinazoshindaniwa katika promosheni ya airtel yatosha zimekamilika na tayari mafundi wanafanya matengenezo ya mwisho tayari kwa kukabidhiwa kwa washindi hao.

Afisa Uhusiano wa NHC YAHAYA CHARAHANI amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati ambapo wanahabari toka vyombo mbali mbali walitembelea nyumba hizo kujionea jinsi mradi unavyokwenda “nyumba hizi tatu zenye thaman ya shilingi milioni 194 zimekamilika na pindi washindi watakapotangazwa wataweza kuhamia katika nyumba hizi mara moja tu.

Amesema nyumba hizo ambazo ni za kisasa zitakidhi mahitaji ya wengi kwani ujenzi wake umezingatia mahitaji ya familia kubwa. Nyumba hizi zina vyumba vitatu vya kulala, jiko, sebule nzuri pamoja na sehemu ya nje iliyonakishiwa kwa umakini ili kuipa nyumba mvuto wa hali ya juu. Aliongeza bw, CHARAHANI Pia alibainisha kuwa wateja wa kampuni ya airtel wanaweza kuzitembelea nyumba hizo na kujionea wenyewe kiwango cha ubora wa nyumba hizo.

“Hizi nyumba ziko wilaya ya Temeke eneo la kibada karibu kabisa na Tuangoma ambapo hadi kufika katika nyumba hizi ni umbali wa kilomita 2 tu kutoka kituo cha basi kilipo, eneo ambalo linafikika na linamakazi mzuri sana” alimalizia kwa kusema Bw, CHARAHANI.

Nae Meneja Uhusiano wa Airtel JACKSON MMBANDO amewataka watanzania kuendelea kutumia mtandao wa airtel hususani huduma ya yatosha kwa kupiga *149*99# na kuchagua vifurushi vinavyowatosha ili kujihakikishia nafasi ya kushinda nyumba hizo.

Amesema airtel imedhamilia kutatua matatizo ya wateja wake kwa kutoa huduma nafuu na bora kuliko mtandao wowote lakini pia promosheni hiyo ya YATOSHA inalenga kubadilisha maisha ya watanzania hasa wale wanaotumia mtandao wa airtel Amesema katika promosheni hiyo jumla ya shilling million 284 zitatumika kuwazadia wateja wa kampuni hiyo ambapo milioni 194 zitanunua nymba hizo 3 toka shirika la nyumba na kiasi kinachobaki kwa siku 90 Airtel itatoa milioni moja kwa mshindi mmoja kila siku.

RUBADA yawataka vijana Makambako kuchangamkia kilimo

$
0
0
 Mmoja wa vijana wanaojishughulisha na kilimo cha mboga mboga katika Bonde la Mlowa katika Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe, Saimon Mdee (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (Rubada), Bw. Aloyce Masanja alipowatembelea vijana hao katika shamba la maparachichi na mbogamboga, ikiwa ni katika kuhamasisha kilimo kupitia Mpango wa Ukuaji wa Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).

Mkulima wa mboga mboga katika Bonde la Mlowa katika Halmashauri ya mji Makambako Mkoani Njombe, Bw. Joseph Chengula (Kulia) akimwonyesha ukubwa wa bonde la Mlowa, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (RUBADA) Bw. Aloyce Masanja( katikati)  alipofanya ziara ya kutembelea kambi za vijana wanaojishughulisha na kilimo katika mji huo jana.  Mkurugenzi huyo alikua katika ziara ya kuhamasisha kilimo kupitia Mpango wa Ukuaji wa Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).  Kulia ni mkulima mwingine wa mbogamboga, Bw. Silas Martin.

Article 13

TANGA SOBER HOUSE: Rehab inayowanusuru vijana na matumizi ya dawa za kulevya, yapunguza mateja Tanga

$
0
0
Idadi kubwa ya vijana wanaojiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya inaweza kupungua ama kuisha kabisa endapo waathirika wa utumiaji wa dawa hizo watatumika kutoa elimu kwa vijana wenzao ambao bado hawajaingia katika janga hilo ambalo ni hatari sana kwa nguvu kazi ya taifa.
Vijana wa walioacha kutumia dawa za kulevya wakiomba dua kabla ya kuzungumza na mwandishi wa habari hizi Dotto Kahindi wa kwanza kulia
 
Tone Media kupitia TANGA YETU imefika katika kituo cha watumiaji wa dawa za kulevya (Rehab, SOBER HOUSE) jijini Tanga ambao wanatoa mbinu na elimu ya kutorudia kutumia dawa hizo ambazo zinaathiri na kugharimu maisha ya vijana wengi.

 Mwenyekiti wa SOBER HOUSE, Ibrahim Daga akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari (hayupo pichani)

Vijana wadogo ambao pengine sasa wangekuwa wakilitumikia taifa katika mambo mbalimbali walijikuta katika janga hili la dawa za kulevya kutokana na sababu mbalimbali wengine wakirubuniwa na marafiki, tamaa, kwenda na wakati, unywaji pombe na uvutaji bangi ambao uliwapeleka moja kwa moja katika matumizi ya dawa hizo.
Ibrahimu Daga ambaye ni Mwenyekiti wa Rehab SOBER HOUSE jijini Tanga anasema kituo hicho hulea watu 35 na kuwapatia elimu ya namna ya kuishi bila kurudia matumiazi ya dawa hizo, mafunzo ambayo hudumu kwa miezi minne.
Anasema kuwa kituo hicho hakijapata msaada wowote kutoka serikalini hasa mamlaka zinazohusika na dawa za kulevya na kwamba kinajiendesha kwa michango ya wazazi wa waathirika.
“Tunahitaji sana kuungwa mkono na serikali hasa katika upande wa kupata chakula kwa hawa vijana tulionao, lakini katika mipango ya muda mrefu tunahitaji eneo kubwa kwajili ya kujenga Rehab itakayochukua watu wengi zaidi” anaeleza Ibrahim


Meneja wa Rehab hiyo Salum Amour anasema mahitaji makubwa katika rehab hiyo ni kupata elimu ya ujasiliamali, biashara, kilimo na ufugaji kwa waathirika hao ili baada ya kumaliza muda wa Rehab wawe na uwezo wa kuendesha maisha yao hata baada ya kurejea katika hali zao za kawaida.


Miongoni mwa shughuli wanazojifunza ni usafi na kupika

 Vijana hawa wanatoa ujumbe mzito kwa vijana wenzao, wakisema USIJARIBU KUFIKIRIA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA NI HATARI.
Meneja wa Rehab hiyo Salum Amour (mwenye t-sheirt nyekundu) akizungumza na mwandishi wa habari

Nyumba inayotumika kuhifadhia vijana hao
Viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na Kitaifa ni jukumu lenu sasa kuhakikisha kuwa mnaunga mkono jitihada za Rehab hii kwa kusaidia kuboresha hudumu ikiwemo chakula ili malengo ya kumaliza tatizo la mateja mitaani yafanikiwe, PESA ZA DAWA ZA KULEVYA NA UKWIMWI ZINAKWENDA WAPI??? Walengwa ndio hawa hamuwaoni?
Picha Zote na Tanga Yetu


wanataaluma wanogesha mahafali ya kwanza ya chuo cha ulinzi cha taifa

$
0
0
 Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali akiagana na wanataaluma waliotoa mada kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Kunduchi, jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki.

 Wanataaluma waliotoa mada kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Kunduchi, jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya wahitimu na wanataaluma waliotoa mada kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Kunduchi, jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki.
Viongozi wa kitaifa wakiwa na wahitimu kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Kunduchi, jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki.
iongozi wa kitaifa wakiwa na wanataaluma waliotoa mada kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Kunduchi, jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki.

SHEREHE ZA UZINDUZI WA UPANUZI WA ZAHANATI YA POLISI ZANZIBAR

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akipokea zawadi ya mfano wa mashua kutoka kwa mwakilishi wa kikundi cha ulinzi shirikishi cha shehia ya Stone Town, Saidi Mkweche wakati wa sherehe za uzinduzi wa upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar  jana. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
 Wanafunzi wa kikundi cha sanaa cha Shule ya Msingi Matopeni Unguja, wakiimba nyimbo ya kuhimiza vijana kuacha dawa za kulevya, baada ya IGP Saidi Mwema kufanya uzinduzi wa  upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani, Visiwani Zanzibar  jana. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
Hapsa Omar wa kikundi cha Kung Fu cha Shehia ya Nyerere akifanya onyesho la kung fu dhidi ya mpinzani wake Nassir Hassan jana Visiwani Zanzibar baada ya IGP Saidi Mwema kufanya  uzinduzi wa upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar  jana. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi

Bei ya Madafu leo

RAIS KIKWETE AWAONGOZA WANANCHI KUAGA NA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MIILI YA ASKARI 7 WALIOFARIKI HUKO DARFUR,SUDANI

$
0
0
 Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Rais na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Makamu na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


TAARIFA YA MSIBA

Bongo kweli Tambarareeeee

$
0
0
Cheki wasauzi wanavyomiminika kwa wingi ndani ya Pipa kuja bongo. Hapo ni Oliver Tambo international airport kama walivyonaswa na Kamera ya Globu ya Jamii leo.

WAZIRI MEMBE AZUNGUMZA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NEW ZEALAND

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza masuala mbalimbali katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na New Zealand alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Murray McCully tarehe 22 Julai 2013. Mhe. McCully na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili tarehe 21  na 22 Julai, 2013.
Mhe. McCully nae akimweleza Mhe. Membe masuala ya msisitizo katika kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili ikiwemo ushirikiano katika masuala ya biashara na kilimo.

Mhe. Membe na wajumbe kutoka Tanzania na New Zealand wakimsikiliza Mhe. McCully.
Mhe. Membe  akimkabidhi Mhe. McCully zawadi ya kinyago mara baada ya mazungumzo yao.

kumbukumbu

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD WAZEE WA KAZI SIMPLY THE BEST!

$
0
0
WE PROMISED, WE DID IT AND WE ARE MAKING IT EVEN BETTER!
GOOD NEWS TO ALL!
REACHING THE COMMUNITY!, WE NOW HAVE AGENTS ALL OVER UK
NORTHAMPTON AGENT,
MOSES MBAA,  TEL 07904773779
SUITE 15 NOTHAMPTON BUSINESS CENTRE, NOTHAMTON NN1 2JL
READING AGENT
GERALD LUSINGU,  TEL  07405571187
MILTON KEYNES AGENT
CHOLLO , BUZZ INN TEL 0751408834
6 THE SQUARE, MILTON KEYNES, MK12 5DG

TUNAWAOMBA WATEJA MKACHUKUE MIZIGO YENU 
MPIGIE AGENT WETU DAR; TORNADO LUKOSI TEL; 0713607116
MZIGO UNANDOKA KILA IJUMAA UNACHUKUA JUMATANO
FROM NOW ALL OUR CARGO GOES  WITH KENYA AIRWAYS! 
THIS MEANS A DIRECT FLIGHT TO NAIROBI/DAR EVERY WEEK 
THIS MEANS NO MORE DELAYS OR EXCUSES!
THIS MEANS BETTER SERVICE THAN BEFORE!
AIR CARGO TO DAR  
£3.50 per KILO! INCLUSIVE CLEARANCE
ONCE YOU PAY HERE IN UK YOU DONT PAY ANYTHING IN TANZANIA
UKIISHA LIPA UK UNAKWENDA KUCHUKUA ILALA DAR BILA KULIPA TENA
FLIGHTS EVERY WEEK
KWA WALE WANAOTAKA KUNUNUA VITU UK TUTUMIE EMAIL AU TUPIGIE
MINIMUM WEIGHT IS 40K HANDLING/ADMIN FEE £20
40' CONTAINER TO DAR/MOMBASA NOW £1,800
CHRIS LUKOSI +44 07903828119  & 07404279633 
SIMON LOUIS (MOHSIN) +44 07950689243
OUR AGENT IN DAR; TORNADO TEL; +255 713607116

HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>