Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live

MWANAFUNZI WA CHUO CHA UHAZILI TABORA AKUTWA AMEJINYONGA KWA KUTUMIA TAI

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT - RS TABORA

MWANACHUO mmoja Chuo cha Utumishi wa Umma –Tawi la Tabora kinachojulikana kama Uhazili  Raphael Kadesha (22)  amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia tai ya kuvaa shingoni.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Graifton Mushi tukio hilo limetokea jana saa 4 asubuhi ambapo marehemu alifunga tai juu ya kitanda chake.

Alisema kuwa marehemu alikuwa akisoma kozi cha Cheti cha Awali cha Utawala katika Chuo hicho.

Mushi aliongeza kuwa chanzo cha kifo hicho hakijulikani na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kujua nini kilimfanya mwanachuo huyo kuchukua maamuzi hayo yaliyoacha simanzi katika jamii yake na Chuo kwa ujumla.

Alitoa wito kwa wanachuoni kuomba ushauri kwa viongozi wao Chuo au wa kiroho pindi wanapokuwa na matatizo binafisi kwani kujiua sio suluhisho la matatizo bali ni kuwaongezea walezi wao shida na majonzi zaidi.
Mushi alisema kuwa mwili wa marehemu umehifahiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete.

Naye Mkurugenzi wa  Chuo hicho Dkt. Ramadhani Marijani alitoa wito kwa wanachuo kuwa watulivu wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa sababu zilizopelekea mwanachuo huyo kuchukua maamuzi yaliyoacha simamazi sio tu kwa familia yake bali hata kwa Jumuiya nzima ya Uhazili.

Alisema kuwa ni vema kama kuna mwanachuo yoyote anakuwa na tatizo au msongo wa mawazo kuwaeleza viongozi wake wawe wa Serikali ya Wanafunzi, Mama Mlenzi, Mshauri wa Wanachuo au Mkurugenzi mwenye ili waweze kusaidia katika ushauri utakaowapa ufumbuzi kuliko kuchukua maamuzi ya haraka.

TANZANIA YAPIGWA MSASA NA ISRAEL WA KUTANGAZA UTALII KIDIGITALI

$
0
0
Ziara ya kutembelea nchi ya Israel iliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania na kuhususisha viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii imeanza kuzaa matunda ambapo mtaalamu wa mfumo wa mawasiliano kutoka Israel, Dkt Norma Kortiat amewasili nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo yanayohusiana na jinsi ya kutangaza utalii wa Tanzania kwa njia ya kidigitali “Digital Marketing”. 

Mafunzo hayo yanategemewa kuwawezesha watumishi kuongeza ufanisi kwa wa kutumia teknologia mpya katika kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania. Mafunzo haya ya siku mbili yameanza leo tarehe 21-22 yanafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam ambayo yanahudhuriwa na watumishi Kutoka Idara ya Utalii , Bodi ya Utalii, Mamlaka ya Wanyama Pori,Mamlaka ya Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro, Wakala wa Huduma za Misitu na kamisheni ya Utalii Zanzibar.
Dkt. Noam Koriat akitoa mafunzo kwa watumishi wa Wizara ya Utalii na Taasisi zake katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Watumishi wakimsikiliza Dkt. Noam Koriat wakati wa mafunzo.

AWESO AWATAKA WAKANDARASI KUWA WAZALENDO

$
0
0
Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Jumaa Aweso amewataka wakandarasi nchini kuwa wazalendo katika kuhakikisha fedha zinazopelekwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji zinafanya kazi iliyokusudiwa.

Aweso ametoa rai hiyo akiwa katika kijiji cha Bubutelo wilayani Chemba akiwa katika ziara yake ya kutembelea na kuzumgumza na wananchi wa vijiji vya Mombose na Bubutelo ambavyo vipo katika eneo linalotarajiwa kujengwa bwawa la Farkwa.

Aweso amesema serikali inajitahidi kutenga fedha ili kukamilisha miradi hiyo na hatimaye ifikie azma ya kumtua ndoo ya maji kichwani kama ilivyokusudiwa hivyo ni wajibu wao kuwa wazalendo.

"Mkandarasi anayepewa kazi ajione kabisa yeye ni Mtanzania avae uzalendo kwa Taifa lake,serikali inatenga fedha nyingi za miradi lakini wapo wakandarasi ambao sio waaminifu jambo ambalo linakwamisha nia nzuri ya serikali iliyonayo,"amesema Aweso.Katika ziara hiyo Aweso amesikiliza vilio vya wananchi ambao wengi waliomba kujua hatma ya fidia zao ili wapishe mradi huo suala ambalo amesema linashughulikiwa na likikamilika kila anayestahili kulipwa atalipwa.

Kwa upande wake mbunge wa Chemba Juma Nkamia amesema wananchi wameupokea mradi huo vizuri na wanachosubiri ni fidia zao na kuwasisitiza wananchi kuwapuuza baadhi ya watu wanaopita na kusema mradi huo haufai.Naye kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Jofrey Pima amesema hali ya upatikanaji wa maji ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya watu waliokuwepo ambapo mijini wananchi 4490 ndio wanapata maji na kijijini ni asilimia 44.

"Bwawa la Farkwa likikamilika litasaidia kuongeza idadi ya wanaopata maji na hivyo kukidhi dhamira ya serikali,kwa sasa upembuzi yakinifu umeshafanyika,tunasubiri suala la kuwalipa fidia wananchi,"amesema kaimu mkurugenzi huyo.Wilaya ya Chemba ilianzishwa mwaka 2012 na mwaka 2013 iliundwa halmashauri ambapo ina jumla ya tarafa 4,kata 26 na vijiji 114 ikiwa na jumla ya wakazi laki 256,623 kwa sasa.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bubutelo wilayani Chemba.


Mbunge wa Chemba Juma Nkamia akizungumza na wananchi wa Bubutelo katika ziara ya Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso.

Wananchi wa Bubutelo wilayani Chemba wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso.

WAZIRI JENISTA ATEMBELEA VITUO VYA HALI YA HEWA ARUMERU

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa mkutano na baadhi ya Watendaji wa Serikali alipofanya ziara Wilayani Arumeru kujionea Vituo vya Hali ya Hewa vinavyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mfumo wa Tahadhari Novemba 21, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa mkutano na baadhi ya Watendaji wa Serikali alipofanya ziara Wilayani Arumeru kujionea Vituo vya Hali ya Hewa vinavyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mfumo wa Tahadhari Novemba 21, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika ziara na Baadhi ya Watendaji wa Serikali walioongozana naye kutembelea Vituo vya Hali ya Hewa vilivyofungwa na Mradi waKuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mfumo wa Tahadhari Arumeru.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Mwikolojia Bi.Clara Manase alipokuwa akieleza faida ya kituo cha Utoaji wa Taarifa za Hali ya Hewa kilichojengwa katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha mkoani Arusha.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

STANDARD CHARTERED BANK MWENYEJI WA ‘ONE BELT- ONE ROAD’ (OBOR) AFRICA-CHINA ROADSHOW

$
0
0
   Mgeni Rasmi Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, Mh. Charles Mwijage akihutubia waalikwa mbalimbali kuhusu fursa zinazopatikana katika uwekezaji. (OBOR Initiative) katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Stanchart bank jana,
    Sanjay Rughani akizungumza na wageni waalikwa katika hafla fupi ya chakula cha jioni ambayo Standard Chartered Bank iliwaandalia wateja wake ambao ni wenyeji kutoka China.
   Bw. Sun Chengfeng, Mkuu wa kitengo cha uchumi na biashara ambaye ni mwakilishi wa China nchini Tanzania akizungumza na waalikwa katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam
   Mgeni rasmi Mh. Charles Mwijage Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji akibadilishana mawazo na Bw, Chengfeng , Mkuu wa kitengo cha uchumi na biashara ambaye ni mwakilishi wa China nchini Tanzania katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na standard charterd bank
     Wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi,Bw Sanjay Rughani, Bw.Sun Chengfeng na wawakilishi mbalimbali katika kitengo cha uchumi na biashara wanaoiwakilisha China nchini Tanzania.

BALOZI WA JAPAN ATEMBELEA WIZARA YA MADINI

$
0
0
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida,  Novemba 21, 2017 alitembelea Ofisi za Wizara ya Madini za jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki na Naibu wake, Stanslaus Nyongo ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ikiwemo fursa za uwekezaji kwenye Sekta ya Madini nchini. 

 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (Kushoto) akizungumza jambo wakati wa mkutano na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida (hayupo pichani) alipotembelea Ofisi za Wizara ya Madini za Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (katikati) akijadiliana jambo na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida (kushoto). Kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida (kushoto). Kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.

RC MAKONDA ATINGA OFISI ZA CLOUDS MEDIA GROUP KUWAPA POLE.

$
0
0

 Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar,ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda wamefika mjengoni Clouds Media Group kutoa pole  na kujionea athari zilizosababishwa na moto uliozuka jana asubuhi katika ofisi hizo zilizopo Mikocheni jijini Dar.Pichani wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bwa.Joseph Kusaga.
  Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar,ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda wakipata maelezo mafupi mara baada ya kufika katika jengo la Clouds Media Group kutoa pole  na kujionea athari zilizosababishwa na moto uliozuka jana asubuhi katika ofisi hizo zilizopo Mikocheni jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh Paul Makonda akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni  ya Clouds Media Group Bwa.Joseph Kusaga mara baada ya kuwasili katika ofisi hizo kutoa pole  na kujionea athari zilizosababishwa na moto uliozuka jana asubuhi katika ofisi hizo zilizopo Mikocheni jijini Dar.Pichani kati ni Mmoja wa Maafisa Uhusiano wa Kampuni hiyo Simon  Simalenga

VIONGOZI WILAYANI HANDENI WASHIRIKI UJENZI KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI NGUVU KAZI

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe na viongozi wengine wakishiriki kujaza zege kwenye ndoo kwaajili ya kumwaga kwenye jamvi la matundu ya vyoo.
 Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe akishiriki kujaza zege kwa ajili ya kumwaga kwenye jamvi la matundu ya vyoo na viongozi wengine.
 Mkuu wa Wilaya na Viongozi wengine wakikagua moja ya darasa Shule ya Sekondari Kiva.
 fundi mkuu wa ujenzi wa madarasa na vyoo akitoa maelezo kwa viongozi juu ya ujenzi wa matundu ya vyoo​
Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea kushiriki ujenzi wa matundu ya vyoo.


NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. JAPHET HASUNGA AAGIZA KUUNDWA KWA CHOMBO CHA KUDHIBITI UBORA WA MAZAO YA MISITU NCHINI

$
0
0


Na Hamza Temba – WMU

..........................................................
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kubuni utaratibu mpya ikiwemo kuanzishwa kwa chombo kitakachosimamia upangaji wa madaraja ya ubora wa mbao zinazozalishwa hapa nchini ziweze kukidhi viwango vya mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

Ametoa agizo hilo jana kwenye kikao cha majumuisho na watumishi wa Shamba la Miti la Serikali la Kiwira ambalo linasimamiwa na wakala huyo wakati anahitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

“Kuna changamoto kubwa kwenye soko la mbao, kwa kiwango kikubwa mbao zetu nyingi tunaziuza hapa nchini, Lazima tufike mahali hizi mbao tuwe tunaziexport (uza nje) kwa kiwango kikubwa. Lakini ili tufikie malengo hayo mbao zetu lazima ziwe kwenye kiwango kinachokubaliwa.

“Mbao zinazokuwepo kwenye soko letu la ndani huwezi kuzitenganisha kwamba hizi ni za TFS au za mwananchi wa kawaida, nyingine zina ubora nyingine hazina, agizo langu kwenu kaeni chini kama watendaji tuje na utaratibu utakaotuwezesha kuzipanga kwenye madaraja, daraja la kwanza, la pili, la tatu au la nne ili mnunuzi ajue ananunua mbao ya ubora wa aina gani,” alisema Hasunga.

Alisema amepata taarifa kuwa baadhi ya wananchi wanavuna miti ambayo haijakomaa jambo ambalo linaathiri ubora wa mbao kwenye soko kwa kutokidhi mahitaji ya wateja, hivyo akaagiza Wakala huyo kubuni mbinu mpya za kuwalinda wateja ikiwemo kuanzishwa kwa chombo maalum cha udhibiti wa ubora wake.

"Kwa maeneo mengine tuna TBS, kwenye chakuka tuna TFDA, kwenye mbao je? Nani anaregulate?(dhibiti), ni lazima tufike mahali tuwe na mdhibiti atakayetusaidia kuhakikisha kwamba ubora unakuwepo,” alisema Hasunga.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja (wa pili kushoto) alipofika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo akiongozana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza (wa pili kulia) kwa ajili ya kujitambulisha wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani humo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akimsikiliza Meneja wa Shamba la Miti Kiwira, William Dafa wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi katika shamba hilo jana katika Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YATOA MKOPO WA SHILINGI MILIONI 102 KWA VIKUNDI 49 VYA WAJASIRIAMALI

$
0
0

NA VICTOR MASANGU, KISARAWE

HALMASHAURI YA wilaya ya Kisarawe iliyopo Mkoani Pwani katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kuwa na uchumi wa viwanda imetoa kiasi cha shilingi milioni 102 kwa vikundi vya wajasiriamali vipatavyo 49 vya wakinamama,vijana pamoja na walemavu kwa lengo la kuweza kuwasaidia kuendesha shughuli zao mbali mbali za biashara mbali mbali ikiwemo na kuwawezeha ili waweze kujikita zaidi katika kujenga viwanda vidogo vidogo.

Akizungumza katika halfa fupi ya kukabidhi hundi ya fedha hizo iliyohuduriwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na viongozi wa vikundi hivyo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama alisema kwamba fedha hizo za mikopo zimetolewa kwa vikundi hivyo kutokea kata zote 17 ambapo zimetokana na makusanyo ya mapato ya ndani.

Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa kutaweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo na kuweza kukuza uchumi wa nchi kutokana na kuweza kuwapa fursa wajarisiamali hao kupania wigo wa kibiashara pamoja na kuanzissha viwanda vingine vidogo vidogo ambayo vitaweza kuongeza upatikanaji wa ajira mpya na kupunguza wimbi la umasikini.

“Kwa kweli sisi kama halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe tumejipanga kuweka mipango madhubuti katika kuviwezesha vikundi vyetu vya ujasiriamali kwa kutumia fedha zetu ambazo zinatokana na makusanyo ya mapato ya nadani, hivyo vikundi hiivi ni moja ya mipango yetu katika kuhakikisha ile asilimia 10 iliyotengwa inawafikia walengwa na kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo,”alisema Mkurugenzi huyo.
Baadhi ya vikundi vya wajasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe wakati wa sherehe za kukabidhiwa hundi ya kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili ya mikopo ambayo iatawasaidia katika kuendeshea shughuli zao za biashara pamoja na ujenzi wa viwanda vidogo vidogo.
Mkuu wa Wilaya Kisarawe Happiness Seneda aliyesimama akizungumza na vikundi vya wajasiriamali kutoka kata mbali mbali katika halfa fupi ya kukabidhiwa hundi ya kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili mkopo wa kuwawezesha kiuchimi.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashari ya Kisarawe Mussa Gama akizungumza na vikundi vya wajasiriamari hao hawapo pichani kabla ya kukabidhiwa hundi hiyo ya kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili ya kuwawezesha mikopo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU.


Applying Nuclear Medicine in Tanzania to Tackle Serious Diseases

$
0
0
According to estimates of Dar es Salaam’s Ocean Road Cancer Institute (ORCI), Tanzania registers about 50,000 new cancer patients every year. However, ORCI, which is the largest cancer referral institution in the country, is only able to attend to 5,000 or 10% of the patients.

In Tanzania, there are few cancer treatment centers to serve the entire population of 55 million people. Unfortunately, not many can afford to cover long distances from all over the country to receive treatment, which can take weeks or months. And it’s not always easy to get cancer patients to keep coming back following initial on-the-scene diagnosis of oncology. Many don’t have the money to get to the hospital or stay for treatment.

With few medical facilities patients need to wait long time to clear out their diagnosis and receive timely treatment.For many of the patients who manage to receive treatment, their cancers have already metastasized to the point that administering palliative care becomes the only remaining option.

Such a tragic state of affairs can be considerably leveled down by increasing services of nuclear medicine and development of special centers of isotope production for local hospitals. Isotopes, nuclear particles, are used in scanning and treatment as they are able to detect and cure tumors at early stage. Globally more than 40 million procedures with nuclear isotopes are performed annually. Nuclear medicine proved to be very efficient in treating oncology and other serious diseases.

FOR MORE NEWS CLICK HERE

MAMA MCHUNGAJI GEITA AIBUKA MSHINDI WA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 15/=TUSUA MAPENE YA VODACOM

$
0
0
 Bi.Adivella Muhimba,Mkazi wa Mkoa wa Geita  akikabidhiwa kitita cha  shilingi Miliono 15/- fedha taslimu na Meneja wa kanda ya ziwa  wa Vodacom Tanzania PLC, Undule Mwamkamba ambazo amejishindia kupitia promosheni ya  Tusua mapene inayoendeshwa na kampuni hiyo. 
 Mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 15/kupitia promosheni ya Tusua Mapene Bi.Adivella Muhimba ambaye ni Mkazi wa Mkoa wa Geita,akifurahia  baada ya kukabidhiwa rasmi kitita chake na Meneja wa kanda ya ziwa  wa Vodacom Tanzania PLC, Undule Mwamkamba hapo jana.
Bi.Adivella Muhimba ambaye aliibuka mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 15/- kupitia promosheni ya Tusua Mapene  akifurahia jambo pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania  Mkoani Geita baada ya kupokea fedha rasmi.

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO NA VYAMA VYA SIASA WATAKIWA KUSHIRIKIANA ILI KUFANIKISHA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI.

$
0
0
Na Clarence Nanyaro – NEC

Mwenyekeiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage amewataka wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi nchini Kuwashirikisha Viongozi wa Vyama vya siasa katika maamuzi mbalimbali wanayofanya yenye maslahi kwa pande zote ili kuendeleza amani na utulivu ulipo nchini.

Akizungumza na Wasimamizi wa uchaguzi katika Manispaa ya Moshi, Jaji Kaijage alisema kuwa katika kipindi hiki ambapo vyama vinashiriki katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakafanyika Novemba 26,2017 ni muhimu kwa Wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha kuwa Maadili ya Uchaguzi wakati wa kampeni yanazingatiwa ili kuepusha uvunjifu wa amani miongoni mwa wananchi.

Jaji Kaijage ambaye yuko katika ziara ya kutembelea Mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Arusha kushuhudia utekelezaji wa maadili ya Uchaguzi katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Udiwani, amewataka Wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha kuwa Vifaa vyote ambavyo vinahitajika ili uchaguzi uweze kufanyika vimepatikana na vile ambavyo havijapatika wawasiliane na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kasoro zinazobainika ziweze kupatiwa ufumbuzi mapema kabla ya siku ya Uchaguzi.

Wakati katika mkoa wa Tanga Uchaguzi utafanyika Katika Kata ya Majengo iliyoko katika Halmshauri ya Mji Korogwe,Mkoani Kilimanjaro,Uchaguzi mdogo wa Udiwani utafanyika katika Kata ya Bomambuzi katika Manispaa ya Moshi na Katika Kata za Machame Magharibi ,WeruWeru na Mnadani katika Halmashauri ya Hai.

Aidha,Jaji Kaijage alitoa wito kwa Wasimamizi wa Uchaguzi kuhakikisha Kuwa siku ya Upigaji Kura ulinzi unaimarishwa katika Vituo vya Kupigia kura lakini usiwe ulinzi wa kuwatia wananchi hofu wakashindwa kufika katika vituo vya kupigia kura viongozi wanaowataka ili washirikiane nao katika kujiletea Maendeleo.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage (Kulia) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidi wa Uchaguzi Katika Manispaa ya Moshi 20.11.2017. Kushoto ni Mwanasheria Mwandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mtibora Selemani.

MENEJA WA NYANZA CORMERCIAL FARM APIGWA FAINI YA SH MILIONI 534 AU KIFUNGO CHA MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA KUCHA 17 ZA SIMBA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu meneja wa Nyanza Commercial Farm, Dilipkumar Pater, kulipa faini ya Sh milioni 534 ama kutumikia kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na kucha 17 za simba kinyume na sheria.

Hukumu hiyo imetolewa leo Novemba 22 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha,

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkeha alisema ameridhika na ushahidi wa mashahidi wanne uliotolewa upande wa mashtaka na vielelezo vitatu kuwa mshtakiwa kweli alitenda kosa hilo Katika kesi hiyo, mshtakiwa Pater alijitetea mwenyewe.

Hakimu Mkeha amesema mahakama imemuona mshtakiwa Pater ana hatia baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kesi yao pasipo kuacha shaka.

Katika ushahidi, upande wa utetezi waliwasilisha, vielelezo vitatu ambavyo ni kucha za simba, hati ya ukamataji na cheti cha kutathmini kucha hizo.
Kabla ya kusomwa hukumu hiyo, Hakimu Mkeha alimuuliza Wakili wa serikali kama alikuwa na lolote la kusema ndipo, wakili Elia Atanas kwa kushirikiana na wakili Batlida Mushi aliiomba mahakama Kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Akijitetea kabla ya kusomewa hukumu hiyo Pater alidai a yeye ni mgonjwa na anategemewa na familia. "Kutokana na ushahidi uliotolewa unaonyesha mshtakiwa alibeba kucha hizo huku akijua ni kosa na akajaribu kuzisafirisha kwenda nchini India kupitia Dubai" amesema Mkeha.

Katika kesi hiyo mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa Novemba 19, mwaka 2016, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Pater alikutwa na kucha 17 za Simba zenye thamani ya Sh 53,483,500 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

WADAIWA SUGU WA KAMPUNI YA TTCL KUPELEKWE MAHAKAMANI- NAIBU WAZIRI MHANDISI NDITIYE

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. 

NAIBU Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amefanya ziara makao makuu ya kampuni ya simu Tanzania (TTCL) na kuwataka kuwachukulia hatua wadaiwa sugu ikibidi kuwapelekea mahakamani kwa mujibu wa sheria. 

Akizungumza mbele ya menejinenti ya TTCL, Mhandisi Nditiye amesema kuwa wale wanaodaiwa na hawafuati taratibu za kulipa madeni wanatakiwa wapelekwe mahakamani na zaidi wadaiwa hao bado wanaendelea kutumia huduma za TTCL. 

Mbali na hilo, Mhandisi Nditiye amesifia huduma ya Conference Video Call kwani itasaidia kupunguza gharama kwa serikali na itaruhusu watu kufanya mikutano kupitia njia ya mawasiliano na sio kukutana kama ilivyokuwa zamani. 

"Huduma hii ya Conference Video Call itasaidia kupunguza gharama kwa serikali ambapo awali ilikuwa unatakiwa kuwakusanya viongozi wote .Kuja katika mkutano ila kwa huduma hii unaweza kuzungumza nao wakiwa huko huko waliko," amesema Mhandisi Nditiye. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na Menejimenti ya kampuni ya simu Tanzania (TTCL) wakati alipotembelea makao makuu ikiwa ni mara ya kwanza na kuwataka kuwachukulia hatua wale wote wanaodaiwa madeni sugu. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt Mary Sassabi. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba akielezea namna kampuni yao ilivyowez akukusanya deni la bilioni 6.8 kwa kipindi cha miezi mitatu kutoka kwa wadaiwa sugu huku akimuelezea Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye namna Conference Video Call inavyoiweza kufanya kazi. 

Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba amesema kuwa kwa sasa TTCL inatekeleza mpango mkakati wa mageuzi ya kibishara na ni mahsusi kwa mabadiliko ya kuwa kiongozi wa huduma za mawasiliano na TEHAMA katika soko la Tanzania. 

Kindamba amesema wanamatumaini kuwa mchakato wa kupata sheria mpya ya kampuni ya TTCL kuja kuwa Shirika la Mawasiliano iliyopitishwa na bungeni wiki iliyopita unaweza kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Magufuli. Kampuni ya TTCL imeweza kukusanya takribani bilioni 6.8 za madeni ndani ya miezi mitatu ambapo awali deni lilikuwa ni Bilioni 10.7. 

Kwa sasa, TTCL imeweza kuboresha huduma zake kwa takribani mikoa 18 ikiwemo Unguja na Pemba pamoja na kutumia teknolojia za kisasa za 2G, 3G, 4G na FMC pia kuwa na huduma za TTCL PESA.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiwa anaongea na wafanyakazi wa kampuni ya simu (TTCL) kutoka Dodoma kwa njia ya Conference Video Call. 

WAZIRI MWAKYEMBE ATUMA SALAMU ZA POLE KWA KITUO CHA RADIO NA TELEVISHENI CHA CLOUDS MEDIA

KUMBUKUMBU YA SABINUS KWEKA

$
0
0
30/12/1935                                                                                         
 22/11/2004

SABINUS        PETER    KWEKA

Baba yetu mpendwa, leo umetimiza mwaka wa 13 tangu ulipotwaliwa gafla na Bwana Picha yako uliyoipiga siku ya mwisho inatukumbusha uwepo wako tulipokuwa sote hapa duniani, na hasa upendo wako na wingi wa busara.


Ni vigumu kukubali kwamba haupo nasi lakini hatuna budi kuamini kwamba uko nasi kiroho kwa vile tunaye Mungu ambaye  anaendelea kututia nguvu kila iitwapo leo. Busara zako zinazidi kutuimarisha kila siku na tunaendelea kuzingatia maneno yako uliyokuwa ukihimiza juu ya kuwa na umoja katika familia na upendo kwa watu wote huku tukiendelea kumtumainia Mungu wetu ambaye amekuita kwake.



Unakumbukwa sana na sisi wanao tuliobaki, JANE,FESTO,EUGENIA,ELIZABETH,CECILIA NA THADEI, Dadako SR. DEVOTHA KWEKA  CDNK, WA – Narumu wote, ndugu, jamaa na marafiki kokote pale walipo.



Misa ya kumbukumbu imefanyika leo – Parokia ya Mkolani – Mwanza.

Tumaini letu linajengwa na neno lisemalo “Umevipiga vita vilivyo vizuri, Mwendo umeumaliza na imani umeilinda (2 Tim-4-7)”


Tunaomba  Eee Bwana Uendelee  kuipumzisha roho yake mahali pema peponi.

NAIBU WAZIRI MASAUNI, KAMISHNA JENERALI WAKAGUA MPAKA WA TANZANIA KENYA ULIOPO WILAYANI TARIME

$
0
0
 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk, Anna Makakala, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (katikati)  wakiangalia jiwe la mpaka unaotenganisha  nchi ya Tanzania na Kenya uliopo katika kijiji cha Nyamhunda, wilayani Tarime ambapo upande wa pili ni Kaunti ya Migori nchini Kenya. Naibu Waziri yupo katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua mipaka na kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu kupitia vipenyo katika mipaka hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea alama ya Mpaka unaotenganisha nchi za Tanzania na Kenya uliopo katika kijiji cha Nyamhunda wilayani Tarime.Wengine ni   Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk, Anna Makakala, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorius Luoga. Naibu Waziri yupo katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua mipaka na kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu kupitia vipenyo katika mipaka hiyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorius Luoga, akitoa maelezo kwaNaibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk, Anna Makakala, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima(katikati), walipotembelea jiwe la mpaka unaotenganisha nchi za Tanzania na Kenya uliopo katika kijiji cha Nyamhunda wilayani Tarime. Naibu Waziri yupo katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua mipaka na kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu kupitia vipenyo katika mipaka hiyo.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk, Anna Makakala(watatu kulia),akizungmza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wakielekea kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya uliopo katika kijiji cha Nyamhunda,Wilayani Tarime.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima. Naibu Waziri yupo katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua mipaka na kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu kupitia vipenyo katika mipaka hiyo.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KESHO KUWASILI MKOANI RUVUMA KWA ZIARA YA SIKU TATU

$
0
0
Waziri mkuu Mh.KASSIM MJALIWA kesho anatarajia kuwasili mkoa RUVUMA majira ya saa saba mchna kwa ziara ya siku tatu ambapo ataanzia katika wilaya ya NAMTUMBO pamoja na TUNDURU hayo yamesemawa na mkuu wa mkoa wa RUVUMA CHRISTINE MNDEME wakati akizungumza na waandishi wa habari habari kamili hii hapa video yake.

WAZIRI MWIJAGE AWATAHADHARISHA WATENDAJI WA SERIKALI WANAOWAKWAMISHA WAWEKEZAJI

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Jengo la usambazaji wa Vifaa vya ujenzi na Saruji linalojengwa na umoja wa Wafanyabiashara wa Kichina Barani Afrika CNBM kwa thamani ya Dola za kimarekani Bilioni 56  Katika Mtaa wa Buguruni Mivinjeni Jijini Dar es Salaam

 Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji, Charles Mwijage akiongoza zoezi la uwekaji wa mchanga katika sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi katika Uzinduzi wa ujenzi wa eneo la Uuzaji wa Vifaa vya Ujenzi katika kutoka kwa umoja wa Wafnyabiashara wa kichina Afrika CNBM
 Balozi wa Serikali ya China ya China nchini Tanzania , Ke Wang akihutubia  wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi kwa jengo la uuuzaji wa bidhaa za ujenzi kutoka kwa umoja wa Wafanyabiashara wa kichina nchini CNBM
 Mwenyekiti wa bodi ya Umoja wa Wafanyabiashara wa kichina , CNBM GROUP COLTD, Dr Zhiping Song  akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuweka jiwe la Msingi
 Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote ,Hemendra Raithatha  akitoa salam za Kiwanda chake juu ya jengo hilo la usamabazji wa Vifaa vya Ujenzi .

 Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji, Charles Mwijage akisaini katika ubao wa wageni .

Viewing all 110016 articles
Browse latest View live




Latest Images