Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

SERIKALI YA OMAN YAVUTIWA NA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI TANZANIA

$
0
0
Na Eliphace Marwa
BALOZI wa Oman Ali Al Mahruqi amesema Wafanyabiashara wa nchi hiyo wamevutiwa na na hatua mbalimbali znazochuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kujenga mazingira bora kwa wawekezaji na wengi wao wapo mbioni kuja kuwekeza katika miradi mikubwa ya maendeleo nchini.

Balozi Al Mahruqi aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wa mazungumzo baina yake na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Kakunda na kuongeza kuwa suala la usalama wa mitaji yao ni jambo ambalo Wafanyabiashara hao wanapenda kuhakikishiwa na Serikali ya Tanzania.
Balozi Mahruqi alisema miongoni mwa fursa zinazowavutia Wafanyabiashara wa Oman kuja kuwekeza nchini ni pamoja na ubora wa miundombinu katika sekta za elimu na mifugo ikiwemo upatikanaji wa tasnia ya nyama.
“Serikali ya Oman ina mpango wa kuja kuwekeza katika ukanda wa Afrika Mashariki na kipaumbele kikubwa kitakuwa ni nchi ya Tanzania kutokana na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo Tanzania,” alisema   Balozi Mahruqi.
Aidha Balozi Mahruqi aliitaka Serikali kuharakisha makubaliano ya mikataba baina ya Mataifa hay ili kuwezesha wawekezaji kutoka Oman kupata fursa ya kuwekeza nchini na kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji kutoka Oman.
Kwa upande wake Naye Naibu  Waziri Kakunda alimuahidi Balozi Mahruqi kufanyia kazi changamoto zilizopo ili kuhakikisha wawekezaji kutoka Oman wanakuja kwa wingi kuwekeza nchini bila ya kuwa na hofu ya usalama wa mitaji yao.
“Nitafuatilia kwa kina kwa wataalamu weu wanaohusika na uwekezaji kwenye kiwanda cha nyama ambapo wawekezaji kutoka Oman watawekeza takribani dola milioni tatu ambazo zitasaidia wafugaji wa Watanzania kupata soko la mifugo yao” alisema Naibu Waziri Kakunda.
Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. AL Mahruqi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ofisi ya Naibu Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Naibu Waziri huyo Bi. Debora Mkemwa.
Naibu Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (katikati) akizungumza jambo alipotembelewa na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Ali A. AL Mahruqi leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Afya Bibi. Zainabu Chaula.
 Naibu Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda akizungumza jambo na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Ali A. AL Mahruqi walipokutana leo Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. AL Mahruqi akizungumza jambo na Naibu Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda alipomtembelea Ofisi kwake leo Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UMEME USIKATIKE BILA SABABU MAALUM- SUBIRA MGALU

$
0
0
Na Teresia Mhagama.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewaagiza watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa hawakati Umeme bila sababu maalum na hivyo kuwaondolea wananchi adha ya kukosa nishati hiyo.

Naibu Waziri aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa TEDAP unaohusu upanuzi na ujenzi wa vituo vya kupozea Umeme na njia za Umeme ambapo vituo vya kupozea Umeme alivyovitembelea ni Mbagala, Gongo la Mboto, Kipawa na City Centre.

“Umeme ukatike pale inapostahili tu, na endapo tatizo linatokea mfano kwenye mifumo ya Umeme ni muhimu mkatoa taarifa mapema kwa wananchi,” alisema Subira Mgalu.

Aliongeza kuwa ukatikaji wa Umeme unasababisha malalamiko kutoka kwa Wananchi kwani kukosekana kwa nishati hiyo kunaathiri shughuli nyingi hasa za kimaendeleo na kiuchumi zinazowaingizia kipato.

Aidha Naibu Waziri aliwaagiza watendaji wa TANESCO wanaosimamia mradi huo wa TEDAP jijini Dar es Salaam, kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakamilika tarehe 15 Desemba, 2017.

Vilevile alieleza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unaendelea vizuri na kwamba kukamilika kwake kutaboresha hali ya upatikanaji wa Umeme katika jiji la Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa kwanza kushoto) akiwa katika eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Meneja Mradi wa Usafirishaji na Usambazaji Umeme kutoka TANESCO, Mhandisi Emmanuel  Manirabona.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa pili  kushoto) akikagua mitambo ya Umeme katika kituo cha City Centre jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha ni watendaji kutoka TANESCO.
 Baadhi ya mitambo ya Umeme katika kituo cha Mbagala  jijini Dar es Salaam iliyojengwa chini ya mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar es Salaam.
 Miundombinu ya kusafirisha Umeme  wenye Msongo wa kV 132 iliyojengwa katika eneo la Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar es Salaam.

HABARI  ZAIDI BOFYA HAPA

Jamii yatakiwa kuweka mikakati ya kuhakikisha kila mama anajifungulia katika vituo vya afya

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

KATIKA kuhakikisha Vifo vinavyotokana na uzazi kwa kina Mama vinapungua,Jamii imehimizwa kumpeleka mzazi kwenda kwenye vituo vya Afya ambavyo vina wataalamu ,kwani hatua hiyo ndio njia ya kusaidia kuondokana vifo hivyo.

Hayo yamebainishwa na Mratibu Taifa wa Muungano wa UtepeMweupe na Uzazi Salama, Rose Mlay wakati wa mkutano wa wadau wakati wa Mkutano wa Wadau wa Afya na Mama na Mtoto uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kupoteza mtoto na mama ni ajali ambayo inatokana na kukosekana kwa huduma sahihi wakati wa kujifungua.

Amesema kuwa mkutano wadau ni pamoja na kujadili takwimu za Afya ya Mama na Mtoto pamoja na kuweka mikakati ya kupunguza vifo vya uzazi.

Mlay amesema kwa sasa vifo vya wakina Mama vimeongezeka kutoka kwa vifo 24 vya wakinamama kwa siku hadi kufikia vifo 30 kwa siku huku akisema ongezeko hilo limechangiwa na wakina Mama kujifungulia sehemu zisizo salama,
Profesa Innocent Ngalinda Mtaalam Mshauri wa takwimu akitoa mada katika warsha ya kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi iliyoandaliwa na Taasisi ya Utepe Mweupe White Ribbon Alliance for Safe Motherhood Tanzania (WRATZ)ambapo mambo mbalimbali yanajadiliwa na wadau kutoka taasisi mbalimbali hapa nchini ili kutatua changamoto zinazokabili huduma ya Mama na mtoto, Warsha hiyo inafanyika kwenye hoteli ya Regency Park Mikocheni jijini Dar es salaam
 
Bi. Rose Mlay Mratibu wa Taifa wa Utepe Mweupe White Ribbon Alliance for Safe Motherhood Tanzania (WRATZ) akifafanua jambo wakati alipokuwa akitoa mada katika Warsha hiyo iliyojadili mambo mbalimbali yanayohusu kupunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua na salama kwa mama na mtoto nchini.
 
Kutoka kushoto ni Tausi Sued kutoka Taasisi ya Childbirth Survivas International ya Marekani, Angelina Ballat kutoka Taasisi ya Childbirth Survivas International, Julieth MawallaKutoka Halmashauri ya Wilaya Ubungo na Sara Luaimay kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni wakifuatilia mjadala huo.
Anna Sawaki Ofisa Mawasiliano na Habari Taasisi ya Utepe Mweupe White Ribbon Alliance for Safe Motherhood Tanzania (WRATZ) akifafanua jambo katika warsha hiyo.

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO ATASHASTA NDITIYE ATEMBELEA TUME YA TAIIFA YA TEHAMA NA TCRA-CCC

$
0
0
Naibu Waziri, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), akizungumza na wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya TEHAMA katika ziara hiyo. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya TEHAMA, Mhandisi Samson Mwela akitoa maelezo kwa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia niNaibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye. 
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prisca Ulomi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) katika ziara yake ya kutembelea Tume ya Taifa ya TEHAMA, jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Tumeya Taifa ya TEHAMA, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani), alipowasili katika tume hiyo, jijini Dar es Salaam.   
Katibu Mtendaji wa Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC), Mary Shao Msuya, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani),  wakati wa ziara hiyo. CCC), katika ziara hiyo.  

DIAMOND ALIVYOTIKISA JIJI LA DUBAI

MICHUZI TV: WATUMIAJI WA AIRTEL MONEY SASA KUNUFAIKA NA GAWIO

Rais Magufuli amteua Bw. Edwin Rutageruka kuwa Mkurugenzi Mkuu TANTRADE

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara 
Tanzania (TANTRADE) Bw. Edwin Rutageruka

BREAKING NEWZZZZ: Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amejiuzulu

$
0
0
Spika wa bunge la Zimbabwe ametangaza leo kuwa Rais wa nchi hiyo  Robert Mugabe amejiuzulu.Spika  Jacob Mudenda alisema kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko ya amani ya mamlaka kulingana na chombo cha habari cha reuters.
Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake.Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Reuters, Spika wa bunge amesema kuwa kiongozi mpya atawekwa madarakani siku ya Jumatano.
Awali bwana Mugabe alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka mamlakani wiki hii. Amekuwa mamlakani tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake 1980.Bwana Mugabe ameshinda uchaguzi wa urais mara kadhaa lakini katika kipindi cha miaka 15 iliopita shughuli hiyo imekumbwa na ghasia dhidi ya wapinzani wake. 
Kusoma zaidi na kupata chanzo BOFYA HAPA

NAIBU WAZIRI WA NISHATI ATEMBELEA BAADHI YA MIRADI YA TANESCO JIJINI DAR ES SALAAM

USHIRIKA WA WACHINJA KUKU KISUTU WENYE MALENGO MAKUBWA YA UWEKEZAJI

$
0
0
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini.

SAUTI za kuku zinasikika hata ukiwa nje ya jengo dogo ndani ya Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam, lakini ghafla zinakoma na zinasikika nyingine.

Siyo kwamba kuku hao wanahitaji chakula ama wanacheza, bali hapa ni machinjio, na sauti zinapokoma ujue tayari zimekwishapigwa kisu na zinaandaliwa kwa ajili ya kitoweo.

Nje ya jengo hilo unaweza kuwa umekuta akinamama wengi wakiwa wamelundikana huku wakiwa wamekalia ndoo zao.Hawa nao wanasubiri huduma, wanataka kununua utumbo, miguu pamoja na vipapatio vya kuku hao wanaochinjwa ili wakafanye biashara.

Akinamama hawa wanatoka katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na hapa Kisutu ndiko mahali pekee ambako wanaweza kupata bidhaa hiyo wanayokwenda kuuza mitaani.Bila shaka baadhi yetu tumekutana ama tumewakuta akinamama wakiuza firigisi na utumbo mitaani, basi amini kwamba asilimia kubwa wanapata bidhaa hiyo katika eneo hili la Kisutu.

Ukiingia ndani ya jengo hilo usishangae ukasalimia usiitikiwe na watu wengi, japokuwa waliomo ni wengi.Kabla hujajua usimame wapi, utasikia sauti ya mtu akikutaka radhi kwamba anaomba kupita ama anataka kuweka mzigo.Naam. Kila mtu hapa yuko ‘busy’ na kazi inakwenda mtindo mmoja, na hata kutokukuitikia si kwamba wanafanya kiburi ama hawajakuona, la hasha. Kwa sababu wanataka kuhakikisha kazi wanayoifanya inakuwa katika hali bora hasa ikizingatiwa kwamba hicho ni chakula kwa afya ya binadamu.
Kuku wakiendelea kuandaliwa ndani ya Soko la Kisutu. Picha zote na MaendeleoVijijini.
Mazingira ya ndani yanaridhisha kutokana na usafi ambao unazingatiwa sana na wahusika licha ya changamoto za hapa na pale.
Hawa ni wanaushirika wa Kisutu Poultry Farm Cooperative Society (KIPOCOSO), ambao wamekuwepo katika soko hilo kwa zaidi ya miaka 28 na ndio waanzilishi wa kuchinja kuku jijini Dar es Salaam.

BALOZI WA OMAN NCHINI AMTEMBELEA NAIBU WAZIRI WA OFISI YA RAIS TAMISEMI MHE. JOSEPH KAKUNDA

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AMJULIA HALI MZEE SIMAI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo alimtembelea na kumjulia hali Mzee Abdulrazack Mussa Simai 'Kwacha' ambaye amelazwa MOI.

Mzee Abdulrazack Mussa Simai 'Kwacha' ni Mzee wa Chama Cha Mapinduzi lakini pia alishawahi shika nafasi mbali mbali za Uongozi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wapigwa msasa jinsi ya kumpima mgonjwa umeme wa moyo (ECG)

$
0
0
 Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pal Bhadreshwara akionyesha namna  ya kumpima mgonjwa umeme wa moyo (Electrocardiogram - ECG) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayotolewa na maafisa uuguzi kutoka Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia.
 Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakijadili namna  ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (Electrocardiogram - ECG) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayotolewa na maafisa uuguzi kutoka Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia.
  Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akiwaonyesha wauguzi jinsi   ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (Electrocardiogram-ECG) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayotolewa na maafisa uuguzi kutoka Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia.
 Afisa Uuguzi kutoka  Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia Kiasha Munnis akifundisha jinsia   ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (ECG) kwa wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayotolewa na wauguzi hao.

Menejimenti ya TAA yakutana na Wajumbe wa TUGHE

$
0
0

  1. Kaimu Mwanasheria wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Joachim Maambo akijitambulisha kwenye mkutano wa Menejimenti na Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) wa kuihusha mkataba wa zamani.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Gaudence Kadyango (wa kwanza kushoto) akiandika masuala mbalimbali kwenye mkutano wa wajumbe wa TUGHE na Menejimenti ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) wa kuihusha mkataba wa zamani.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) aliyekuwa Mwenyekiti wa mkutano wa Menejimenti na Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE), akiandika masuala mbalimbali wakati wa kuihusha mkataba wa zamani.Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) na Menejimenti ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kuihusha mkataba wa zamani.

   

SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WAFANYABIASHARA WA MBOLEA WANAOKWEPA BEI ELEKEZI

$
0
0

Na EmanuelMadafa,Mbeya

SERIKALI imewataka wafanyabiashara wa mbolea nchini kuhakikisha wanafuata bei elekezi ya uuzaji wa mbolea iliyowekwa na serikali ili kumsaidia mfanyabiashara mdogo aweze kuuza kwa rejareja.

Kauli hiyo imetolewa jijini Mbeya na Naibu waziri wa Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa wakati akifungua mkutano wamakatibu Tawala na washauri wa kilimo wa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini .Amesema kuwa endapo itagundulika kwamba kuna mfanyabiashara wa jumla anamuuzia mfanyabiashara wa rejareja kwa bei itakayomfanya ashindwe kuuza kwa bei elekezi wizara itamchukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungia biashara yake

Mwanjelwa amesema ofisi yake inaushahidi kwamba wapo baadhi ya wafanyabiashara wa jumla wamekuwa wakiwauzia mawakala wanaouza kwa bei elekezi ya serikali hivyo kuleta mkanganyiko na kuwafanya wauze mbolea hiyo kwa bei zaidi ya elekezi .

Amesema katika Mikoa ya Ruvuma,Lindi ,Mtwara ,Mwanza na Geita wapo wafanyabiashara ambao sio waaminifu wamekuwa wakifungua mifuko na kuuza mbolea ya kupandia (DAP) kwa Shilingi 2,000 kwa kilo kwa lengo la kujipatia kiasi cha shilingi laki moja (100,000) kwa mfuko wa kilo 50 badala ya bei elekezi ya shilingi elfu hamisini na moja.

Aidha Naibu Waziri huyo amesema pamoja na kuwauzia wakulima mbolea iliyopoteza ubora wake kwa kufunguliwa kwa kuachwa wazi wafanyabiashara hao wanawaingizia hasara kubwa wakulima hasa katika kipindi cha mavuno.Kutokana hali hiyo Naibu waziri huyo ametoa wito kwa wafanyabiashara kote nchini kuacha tabia hiyo mara moja ili kumpa fursa Wakala aweze kuuza kwa bei ya rejareja na kwa bei elekezi bila kuathiri biashara zao .

Mkutano huo unalenga kuongeza uelewa wa pamoja kuhusu mifumo mipya iliyoanzishwa ya uagizwaji wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement system-BPS )na usimamizi wa mbolea kwa lengo la kumuwezesha mkulima kupata mbolea bora kwa bei nafuu sanjali na kuongeza usalishaji wenye tija.
Naibu Waziri wa Kilimo Mh.Dkt Mary Mwanjelwa akizungumza katika Mkutano wa Makatibu Tawala na Washauri wa kilimo wa Mkoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Katika KUKUMBI WA kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya Nov 21 ,2017. 
Washiriki wa Mkutano wa Makatibu Tawala Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini unaolenga kuongeza uwezo uelewa wa pamoja kuhusu mifumo mipya iliyoanzishwa ya uagizwaji wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System -BPS) na Usimamizi wa bei ya mbolea ,katika ukumbu wa mikutano Mkapa jijini Mbeya Nov 21 mwaka huu. 
Mshiriki akichangia katika Mkutano huo.
Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa katika Piha ya Pamoja na washiriki wa semina hiyo. 

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MAGAZETI YA JUMATANO LEO NOVEMBA 22,2017

SHAMBA LA MIFUGO LA JK KUTUMIWA NA SUA SHAMBA DARASA KWA WANAFUNZI WAO , WATAALAMU NA WAFUGAJI.

$
0
0
Na John Nditi, Morogoro

UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) umeingia makubaliano ya pamoja na Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne , Dk Jakaya Kikwete ili kulitumia shamba lake la mifugo lililipo kijijini kwake Msoga , liwe shamba darasa la kutolea elimu ya vitendo kwa wanafunzi wao , wataalamu wa mifugo na wafugaji.

Makamu Mkuu wa SUA , Profesa Raphael Chibunda alisema hayo Nov 20, 2017 wakati Rais Mstaafu Kikwete alipofanya ziara ya siku moja na wataalamu wake wa Mifugo walipofika Chuoni hapo kwa ajili ya kujifunza kuhusu ufugaji bora wa Ng’ombe wa maziwa.

Rais Mstaafu Kikwete kwa sasa amejikita zaidi kwenye suala la ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa maziwa , kilimo cha mazao ya chakula na matunda hasa mananasi kijijiji Msoga, Chalinze , wilayani Bagamoyo , mkoa wa Pwani.

“ Tumemwomba Rais Mstaafu Kikwete lile shamba lake la mifugo tulitumie kuwa ni shamba darasa kwa wanafunzi wetu wa Sanyansi ya wanyama , ukuzaji viumbe majini na Nyanda za Malisho pamoja na wataalamu wa mifugo na wananchi hasa wafugaji” alisema Profesa Chibunda na kuongeza .

“ Katika ombi letu naye ameridhia shamba hilo litumike kuwa shamba darasa” alisema Profesa Chibunda.Makamu mkuu wa Chuo hicho alisema , kwa kuridhia kwake , SUA inaweza kusongeza elimu bora ya ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa maziwa na nyama na matumizi ya malisho bora kwa wafugaji kutoka maeneo mbalimbali ya karibu na nje badala ya mtu mmoja mmoja kufika Chuoni hapo.

Kwa upande Rais Mstaafu alisema “ Nimefuata kujifunza na nimelizika na nilichokifuata na nimekipata na ahadi yangu kwenu SUA nitaendeela kushirikiana nayi , lengo ni kuleta mabadiliko ya kisayansi ya sekta ya ufugaji iweze kumletea tija mfugaji” alisema Rais Mstaafu Kikwete.

Naye Naibu makamu mkuu wa chuo hicho , Profesa Peter Gilla alisema, Sua itaendelea kufanya tafiti mbalimbali kwenye sekta ya Kilimo na Mifugo na kupanua wigo wa uzalishaji mkubwa wa mbegu za aina mbalimbali zikiwemo za matunda kwa nia ya kimaabara ya uhandisijeni ili kuwezesha mahitaji katika soko la Dunia. 
 Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Sayansi ya wanyama ,ukuzaji viumbe maji na nyanda za malisho , Dk Nazael Madalla  ( mwenye kuvaa miguuni  mabuti ya mvua ) kuhusu mashine ya kusaga majani ya malisho  ya mifugo hasa  ng’ombe wa maziwa ,wakati alipofanya ziara ya siku moja  ya kujifunza  ufugaji wa kisasa  katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Novemba 20, 2017  na ( watano kutoka kulia  ) ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Raphael Chibunda . 
 Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete, akiangalia  aina ya majani ya malisho yaliyosagwa na mashine kwa ajili ya kulisha   ng’ombe wa maziwa ,wakati alipofanya ziara ya siku moja  ya kujifunza  ufugaji wa kisasa  na malisho katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Novemba 20, 2017  na ( kushoto kwake ) ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Raphael Chibunda .

 Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete, akiwapatia ng’ ombe wa maziwa majani ya malisho yaliyosagwa na mashine  wakati alipofanya ziara ya siku moja ya kujifunza  ufugaji wa kisasa  katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Novemba 20, 2017 na ( kushoto  ) ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Raphael Chibunda .( Habari na Picha na John Nditi).

KONGAMANO LA WASOMI WANATAALUMA KUFANYIKA JUMAMOSI HOTELI YA LANDMARK UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

WANAFUNZI waliohitimu vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini Jumamosi ya Wiki hii wanatarajia kufanya kongamono kubwa la kihistoria kujadili namna watakavyoweza kutumia taaluma zao kusaidia jamii, kanisa na taifa kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mratibu wa Kongamamo hilo, Ephrahim Mwambapa alisema kongamanao hilo linaundwa na muungano wa wasomi wa kristo uitwao Tanzania for Jesus Prayer Movement ambao mlezi wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus.

Alisema licha ya muungano huo kuundwa na vijana wa kikristo lakini vijana wote wasomi kutoka katika vyuo na shule za sekondari na madhehebu mbalimbali wanaalikwa ili kuchangia mada zitakazo jadiliwa na mgeni rasmi atakuwa ni Kiongzi Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Center nchini, Askofu Flaston Ndabila.

Mwambapa alisema kuwa katika kongamano hilo kutakuwepo na mada mbalimbali na kuona ni jinsi gani kila mmoja na taaluma yake ataweza kusaidia jamii badala ya taaluma hiyo kuachwa bila ya kuifanyia kazi.

"Tunapokuwa vyuoni tunakuwa na mipango mingi ya maendeleo lakini baada ya kumaliza masomo kila mtu anakuwa kivyake wakati tunapaswa kushirikiana na jamii na ndio maana tumeona ni vizurio kuazisha muungano huu lengo likiwa kujumuika na jamii katika shughuli za maendeleo ya nchi na dini" alisema Mwambapa.

Alisema wazo la kuanzisha muungano huo nimatunda ya mkutano ya mkutano mkuu wa kitaifa wa kuliombea taifa ulioratibiwa na Askofu Flaston Ndabila na kuhudhuriwa na watu mbalimbali na vijana kutoka vyuo vikuu uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mwambapa alisema kongamano hilo litafanyika Hoteli ya Landmark Ubungo jijini Dar es Salaam na litahudhuriwa na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali,sekondari baadhi wa viongozi.

 Mratibu wa Kongamamo la Wasomi Wanataaluma wa Kikristo liitwalo Tanzania for Jesus Prayer Movement ambalo mlezi wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus,  Ephrahim Mwambapa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Kanisa la Abundant Bressing Center (ABC), Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam, kuhusu kongamano hilo litakalofanyika Hoteli ya Landmark siku ya Jumamosi. Kulia ni Mjumbe wa Kongamano hilo, Lendian Bigoli.

Mratibu wa Kongamano hilo, Ephrahim Mwambapa akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni Kiongzi Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Center nchini, Askofu Flaston Ndabila.

NCC Yatakiwa Kuzingatia Ubora wa Miundombinu Nchini

$
0
0

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) limetakiwa kuzingatia ubora katika kutekeleza kazi zake ili kuokoa fedha zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa alipokuwa akijitambulisha na kuongea kwa mara ya kwanza na Wafanyakazi wa Baraza hilo jana jijini Dar es Salaam.Kwandikwa amesema kuwa Taasisi hiyo ni muhimu na ina manufaa kwa nchi ingawa kuna maeneo ambayo yanahitaji kusukumwa zaidi ili kazi zinazofanywa zizidi kuleta tija zaidi kwa Taifa.

“Baraza hili ni kama jicho katika Wizara kwa sababu majukumu yake yamejikita katika kusimamia Sera, hivyo Wafanyakazi tunatakiwa tujikite zaidi katika kufanya kazi zinazoonyesha ubora wa hali ya juu”, alisema Kwandika. 

Akizungumzia juu ya upunguzaji wa gharama za ujenzi, Naibu Waziri amesema kuwa gharama za ujenzi zinabadilika mara kwa mara, hivyo ni lazima zichunguzwe ili ujenzi ufanyike kwa bei ndogo lakini uwe katika kiwango bora zaidi na fedha zinazobaki zitumike kwa shughuli nyingine.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa NCC, Matiko Mturi amesema ili kutekeleza majukumu yake kikamilifu, kwa mwaka huu wa fedha Baraza limejiwekea malengo mbalimbali yakiwemo kukusanya maoni ya Wadau na kuandaa kuhusu utendaji wake ili kufanya maboresho ya utoaji wa huduma na shughuli zinazotekelezwa na Baraza.

Malengo mengine ni kuandaa na kukamilisha Kanuni za utekelezaji washeria, kuratibu na kutoa mafunzo kwa Wadau, kutoa ushauri wa kiufundi na kutatua migogoro, kufanya ukaguzi wa miradi ya ujenzi inayotumia fedha za Umma pamoja na jitihada za kutunisha Mfuko wa Maendeleo ya Ujenzi.

“Katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Oktoba mwaka huu, tumetoa ushauri mbalimbali ikiwa ni jukumu letu la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba za kuishi za magomeni, tulitathmini usahihi wa idadi ya nondo katika ujenzi wa jengo la maabara iliyopo katika eneo la Mabibo, pia tulifanya tathmini ya thamani ya pesa katika jengo la dharura lililopo Makumbusho pamoja na tathmini ya kiufundi ya miradi inayotekelezwa kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara”, alisema Mturi

Baraza la Taifa la Ujenzi lilianza kazi rasmi mwaka 1981 likiwa na lengo kuu la kuboresha shughuli zinazofanywa na Sekta ya ujenzi ambapo jukumu lake kubwa ni kutoa uongozi wa kimkakati wa kuendeleza Sekta ya ujenzi kwa nia ya kuboresha uwezo wa Wataalam na Taasisi za ndani zinazotoa huduma katika Sekta ya ujenzi.
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Matiko Mturi (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa mara baada ya kuripoti ofisini hapo jana Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha na kuongea na wafanyakazi wa Baraza hilo.
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Matiko Mturi (kulia) akitoa taarifa fupi mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa pamoja na wafanyakazi wa baraza hilo alipofika kwa mara ya kwanza ofisini hapo jana Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha na kuongea na wafanyakazi wa Baraza hilo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa akiongea na wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) jana Jijini Dar es Salaam katika kikao kilichofanyika kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kujitambulisha na kuongea na wafanyakazi hao.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images