Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live

TAARIFA KUHUSU UINGIZWAJI WA MIFUGO TANZANIA

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

Simu:255-26-2323201-7
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Nukushi: 255-26-2116600

              

               Jengo la LAPF Ghorofa ya 6,
                          Barabara ya Makole S.L.P. 2933,
                 DODOMA ,  
                                   Tanzania.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa katika baadhi ya vyombo vya habari na kutoka kwa baadhi ya wanasiasa kuishutumu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia hatua ya kukamata na kupiga mnada mifugo iliyoingizwa nchini bila kufuata sheria. Aidha, taarifa hizo zinajenga sintofahamu kuhusiana na suala la vifaranga vya kuku vilivyoteketezwa kufuatia kuingizwa nchini bila kufuata sheria. Baadhi ya taarifa hizo zimeenda mbali zaidi na kudai kuwa hatua hizi zinaweza kudhoofisha mahusiano yetu na nchi jirani.  

Kadhalika, kufuatia suala hilo la kupigwa mnada kwa ng’ombe walioingia nchini kinyume cha sheria, na wenye ng’ombe hao kukaidi kuondoa mifugo yao hata baada ya kupewa muda kufanya hivyo, na kufuatia kuteketezwa kwa vifaranga vilivyoingia nchini kinyume cha sheria na kanuni, Serikali ya Kenya ilimwita Balozi wetu aliyeko Nairobi kutaka maelezo. Balozi wetu alisikiliza maelezo ya Serikali ya Kenya na akatumia fursa hiyo kuelezea masuala haya kwa Serikali ya Kenya. Vile vile Serikali imepokea barua kutoka Serikali ya Kenya kuhusu masuala haya, na Serikali itaijibu barua hiyo kutoa ufafanuzi.

Serikali inapenda kuufahamisha umma kwa ujumla kuwa uingizwaji wa mifugo na bidhaa zake nchini Tanzania huongozwa na sheria za nchi, makubaliano ya kikanda na kimataifa.


Sheria na taratibu hizi ni pamoja na:
  1. Sheria ya Magonjwa ya Wanyama (Animal Disease Act) Na. 17 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2007 na 2010, ambazo zinatumika kudhibiti na kukagua uingizaji wa mifugo na mazao yake katika maeneo ya mpakani, bandarini na viwanja vya ndege;
  2. Sheria ya Nyanda za Malisho na Rasilimali ya Vyakula vya Wanyama (Grazing-land and Animal Feed Resources Act) Na. 13 ya mwaka 2010 ambayo inasimamia nyanda za malisho na ubora wa malighafi za kusindika vyakula vya mifugo;
  3. Zuio (quarantine)  la uingizaji ndege na mazao yake nchini la mwaka 2006, kutokana na uwepo wa ugonjwa hatari wa Homa ya Mafua Makali ya Ndege katika nchi mbalimbali duniani. Ugonjwa huo umejitokeza kwenye nchi jirani ya Uganda mwanzoni mwa mwaka 2017 na hivyo kuiweka nchi yetu katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huu iwapo zuio hili litakiukwa. Zuio hilo halijaondolewa hadi leo.
  4. Ukweli kwamba katika Jumuiya ya Afrika Mashariki mifugo na bidhaa za mifugo zinavuka mipaka kwa utaratibu maalum kupitia kwenye vituo vya mipakani ambapo maofisa mifugo kutoka pande zote za mipaka hufanya shughuli ya udhibiti.
Utekelezaji wa sheria na makubaliano haya hufanyika bila ubaguzi wa uraia wa mwingizaji wa mifugo au nchi inakotoka mifugo hiyo. Nchi zote duniani, zikiwemo nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, zinadhibiti uingizwaji wa mifugo na mimea katika nchi zao. Udhibiti huu hufanyika katika viwanja vya ndege, bandari na vituo vya mipakani. Kwa mfano, katika Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani cha Namanga, wapo maofisa wa mifugo na kilimo kutoka Kenya na Tanzania wanaodhibiti uingizwaji wa mifugo na mimea kwenye nchi zao.

Katika utekelezaji na usimamizi wa sheria hii, ilibainika kuwa idadi kubwa ya mifugo kutoka nchi za jirani imeingizwa nchini pasipo kufuata sheria na taratibu zilizopo. Serikali iliagiza mifugo hiyo irudishwe kwenye nchi ilikotoka kwani ilikuwa inahatarisha mazingira na kuongeza uwezekano wa kusambaa magonjwa ya mifugo. Serikali ilitoa muda wa kutosha kwa wamiliki wa mifugo hiyo kuiondoa nchini. Tahadhari ilitolewa kwamba muda uliotengwa ukifikia ukomo, mifugo hiyo itakamatwa na kushugulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Pamoja na agizo hilo, Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilituma Waraka wa Kidiplomasia  kwa Serikali za Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda, ikizihimiza kuwataka raia wao walioingiza mifugo nchini isivyo halali waiondoe. Wamiliki wengi walitii agizo hilo la Serikali ya Tanzania na kuondoa mifugo yao nchini.

Hata hivyo, wapo wamiliki wachache kutoka nchi za jirani waliokaidi agizo hilo na hivyo ng’ombe wapatao 1113 walikamatwa katika Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro na kupigwa mnada baada ya wamiliki wake kushindwa kujitokeza. Katika mkoa huo wa Kilimanjaro wapo ng’ombe 74 ambao wamiliki wake walijitokeza, wakalipa faini kwa amri ya mahakama na kuondoka na ng’ombe wao. Katika Mkoa wa Kigoma ng’ombe 324 ambao wamiliki wake hawajajitokezawamekamatwa na hatua stahiki zinachukuliwa. Aidha, katika mkoa huo wa Kigoma ng’ombe 728 walikamatwa na wamiliki wao walijitokeza na kulipa faini kutokana na maamuzi ya Mahakama. Katika mkoa wa Kagera jumla ng’ombe 1,536 ambao wamiliki wake bado hawajulikani wanashikiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama na sheria itachukua mkondo wake.

Kwa takwimu hizi ni wazi kwamba zoezi hili halijalenga nchi yeyote, kwa sababu sio nchi moja tu imeathirika. Zoezi hili limelenga kutekeleza sheria na kanuni za nchi yetu ili kulinda mazingira na kupunguza uwezekano wa kusambaa kwa magonjwa ya mifugo. Hili suala halipaswi kusababisha mgogoro wa kidiplomasia na nchi yeyote, labda tu mtu aamue kwa makusudi yasiyo mema kupotosha na kuchochea mgogoro.

Aidha, tarehe 24 Oktoba, 2017 jumla ya vifaranga vya kuku wa mayai 6,400vilikamatwa katika Mkoa wa Arusha kwa kuingizwa nchini bila kufuata sheria na kanuni. Vifaranga hivyo vilikuwa kwenye maboksi 60 vikiwa kwenye gari lenye namba za usajili T 285 BAY. Mmiliki wa vifaranga hivi alidai kwamba ameviingiza nchini kutokea Kenya. Vifaranga hivi viliteketezwa kutokana na msafirishaji wa vifaranga hivi kutokuwa na kibali cha aina yoyote kutoka mamlaka husika ya udhibiti wa magonjwa ya mifugo hapa nchini ambayo ni Idara ya Huduma za Afya Mifugo katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Pia, mmiliki huyu alishindwa hata kuonesha kibali cha Serikali ya Kenya kumruhusu kusafirisha vifaranga hivyo kutoka Kenya kuvileta Tanzania pamoja na kwamba mmiliki huyu alidai kwamba vifaranga hivyo amevitoa Kenya. Ni muhimu ikafahamika kwamba nchi zote duniani, ikiwemo Kenya, hufuata miongozo ya WTO na Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (OIE) kwa kutoa vibali (export permit) kwa mtu yeyote anayetaka kusafirisha mifugo nje ya nchi.Kosa jingine kubwa ni kwamba vifaranga hivi havikupitishiwa kwenye vituo rasmi vya Ukaguzi wa Mifugo na Mazao yake mipakani (zoosanitary border posts) kwa mujibu wa sheria na kanuni husika.

Pamoja na yote haya, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Tanzania alimpigia simu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo (Director of Veterinary Services) wa Kenya kutaka kujua kama Mamlaka za Kenya zina habari kuhusu vifaranga waliokamatwa na kama Kenya itakubali kuruhusu vifaranga hivyo virudishwe Kenya. Mkurugenzi huyu wa Kenya alisema hana taarifa kuhusu vifaranga hivyo na kwamba Kenya haiko tayari kuruhusu vifaranga hivyo kurudishwa nchini mwao kwa sababu havina nyaraka kulingana na miongozo ya kimataifa.

Ni vizuri umma ukajua kwamba hii si mara ya kwanza kwa Serikali kuteketeza vifaranga vilivyoingizwa nchini bila kufuata sheria kanuni na taratibu. Vipo vifaranga vingi tu vimeteketezwa kwa namna hiyo hiyo baada ya kukamatwa kwenye viwanja vyetu vya ndege na sehemu nyingine. Kadhalika vifaranga ambavyo vimekuwa vikiteketezwa havitokei nchi moja tu. Vifaranga vyote vinavyoingizwa nchini bila kufuata sheria na kanuni zinazotulinda dhidi ya uwezekano wa magonjwa vinateketezwa mara moja bila kujali vinatoka nchi gani. Hatua hizi tumekuwa tukizitekeleza tangu tuweke zuio mwaka 2006, na hazijaathiri kwa namna yeyote ile mahusiano yetu na nchi yeyote. Hatua yeyote ya kujaribu kufanya jambo hili kuwa ni la mgogoro wa kidiplomasia dhidi ya nchi yeyote ile ni hatua isiyo sahihi.

Serikali inawaasa wananchi na raia wa kigeni wazingatie sheria, kanuni na taratibu pale wanapotaka kuingiza nchini  au kusafirisha nje ya nchi mifugo na mazao yake. Serikali ya Tanzania itaendelea kusimamia sheria, kanuni na taratibu za nchi, kikanda na kimataifa zinazohusu utoaji na uingizaji wa mifugo na mazao yake nchini. Tunapenda kuuhakikishia umma kwamba, usimamizi wa sheria hizi hauwezi na hautakiwi kwa namna yoyote ile kuathiri mahusiano yetu na nchi nyingine kwa sababu nchi zote duniani zinasimamia sheria kama hizi.
Mojawapo ya misingi ya Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania ni kujenga na kuimarisha mahusiano na nchi nyingine pamoja na kudumisha ujirani mwema. Hivyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuhakikisha kuwa inalinda mahusiano mazuri yaliyojengwa kwa muda mrefu kati yake na nchi nyingine duniani. Kadhalika, Serikali itaendelea kutumia fursa mbali mbali, kama vile vikao vya Jumuiya ya Afrika Mashariki na vikao vya pande mbili kati yetu na jirani zetu, na pia vikao vya ujirani mwema mipakani, kutatua changamoto zozote za kimahusiano zitakazo jitokeza kwa nia ya kuendelea kuimarisha ujirani mwema.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

19 Novemba, 2017


MELI YA CHINA YATUA JIJINI DAR KUTOA HUDUMA ZA MATIBABU KUANZIA JUMATATU HADI IJUMAA

MAGAZETI YA JUMATATU LEO NOVEMBA 20,2017

MAKONDA ATOA MILIONI 10 KWA KAMPUNI YA MSAMA AUCTION MART KUSAIDIA KUTOKOMEZA UHARAMIA WA KAZI SANAA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa Shilingi Milioni 10 za Kitanzania kwa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart inayosimamia zoezi la kutokomeza kazi feki za sanaa nchini.

Kiasi hicho cha Pesa kimetolewa katika Kampuni hiyo ya Msama ili kuendesha vizuri mapambano dhidi ya wanaodurufu kazi hizo sehemu zote za jiji la Dar.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake, Mkurugenzi wa Msama Auction Mart, Alex Msama amesema kuwa Kampuni hiyo inamshukuru Mkuu huyo wa Mkoa kwa kufanya jambo kubwa na la mfano ambalo hakulitegemea.

"Sikutegemea kuona kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam anawapenda Wasanii, baada ya kuniita na kuniambia kuwa kazi ninayoifanya ya kupigania haki za Wasanii ni nzuri", amesema Msama."Ameniita amenimbia kazi inaenda vizuri, kwani amejaribu kupita maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar wala haoni Kompyuta, CD Feki na ameona kila CD anayoishika ina Stika ya TRA", ameongeza Msama

Aidha, Msama ameendelea kusisitiza kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanafanya biashara yakuuza Kazi Feki za Sanaa waache kwa kutafuta kazi zakufanya.Pia amewaasa Wananchi kununua Filamu zenye Stika ya TRA inayong'aa vizuri, kwani watapofanya hivyo Wasanii hao watanufaika na kazi zao pamoja na kulipa Kodi kwa manufaa ya Taifa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart, Bw. Alex Msama akizungumza na Wanahabari mapema jana jijini Dar,akieleza taarifa ya Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam,Mh Paul Makonda kuongeza nguvu katika suala zima la kupambana na uharamia wa kazi sanaa hapa nchini,ambapo Mh Makonda amechangia milioni 10 kwa kampuni ya Msama Auction Mart ambayo inasimamia shughuli hizo za kupambana na Maharamia hao.

VIRTUAL ADVOCATE - A SOLUTION SET TO REVOLUTIONIZE OFFICE PRODUCTIVITY

$
0
0
‘Virtual Advocate’is a revolutionary document solution platform that allows users to transform their frequently used documents and forms into intelligent templates, enabling super-fast production of tailor-made documents, increasing efficiency and productivity.


Departments such as legal, credit, human resources, sales and the like, whether in bank, real estate, insurance companies or education providers, can leverage from the myriad of benefits of the new platform.


By streamlining the documentation process, Virtual Advocate guarantees improved productivity by cutting down document processing time and operational costs by over 90 percent. The system reduces the need for multiple editing and dependency on lawyers and thus reduces costs and time spent.


Speaking to journalists, the CEO of Virtual Advocate, Mr Nzaro Kachenje, said that they found the existing traditional processes of drafting, monitoring and managing documents to be unnecessarily time consuming, costly, stressful and prone to errors. To counter this, they endeavored and succeeded to integrate modern technologies into the day-to-day documentation process to produce a robust, one stop center for most documentation needs, which they branded ‘Virtual Advocate’.


Pointing out a few key features of the system, Mr Kachenje said that the system has a dynamic dashboard, enabling quick real-time view of all activities in the system; a bulk document generation feature for the generation of similar documents to multiple addressees at once; a simplified user management module to control accesses of different users; a customer management module where all customer records are stored and easily accessible; and also security alerts to ensure no duplication of information in the system, which is best suited for Banks, as it would prompt the user if the Customer and/or the property pledged as security already exists in the system.


Virtual Advocate also offers complimentary support services such as round-the-clock customer service, training and consultancy to its clients.


Speaking on the novelty of the system, Mr Kachenje said that the system is first of its kind in East and Central Africa; and noted that they intend to export their revolutionary system to international markets, as their research has revealed a need for the product in all neighboring countries. He expressed jubilation to have pioneered such a technology that would put Tanzania in the limelight of innovation.

Virtual Advocate Chief Executive Officer, Nzaro Kachenje (centre), addresses participants during the official launch of Virtual Advocate online document solutions application in Dar es Salaam yesterday. With him are, Virtual account manager, Asha Bura (right) and application’s administrator, Francis Lusinde. Application is said to cut down document processing time and operational costs by over 90 percent. 


KABURI LAFUKULIWA MOSHI KUONDOA UTATA WA MWILI WA MTU ALIYEZIKWA BAADA YA KUOKOTWA MTONI

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu 
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

 UTATA umeighubika familia ya Jackson Makundi ambayo kijana wake aliyetambulika kwa jina la Humphrey Makundi, Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo kupotea katika mazingira tatanishi.
 Utata wa kupotea kwa mwanafunzi huyo unatiliwa shaka zaidi na familia hiyo baada ya kufukuliwa kwa kaburi ulimozikwa mwili uliookotwa mto Ghona mita 300 ,jirani na shule hiyo ukidaiwa kushabihiana na wa mwanafunzi huyo.
  Humphrey Makundi, mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Scolastica anatajwa kupotea tangu Novemba 7 mwaka huu akiwa shuleni hapo huku wanafunzi wenzake wakiendelea na mitihani ya kidato cha Pili ya upimaji ya kitaifa .
Kaburi likifukuliwa.
Baba mzazi wa Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Scolastica aliyepotea,Jackson Makundi (katikati) akijadili jambo na wanandugu wakati zoezi la kufukua kaburi likiendelea.
Baba mzazi wa Mwanafunzi Humphrey ,Jackson Makundi (Mwenye suti nyeupe) akitizama mwili baada ya kaburi kufukuliwa.
.
Mwili uliofukuliwa katika makaburi hayo ukiwekwa katika gari la Polisi kwa ajili ya kwenda kuhifadhiwa katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC.





KUMBUKUMBU YA KIFO CHA BARKHE MWINYI UBAYA

$
0
0
Picha ya Henry Kapinga

Familia ya Mwinyi Ubaya inakumbuka kifo cha Barkhe M. Ubaya kilichotokea miaka minne iliyopita.
Unakumbukwa na Mumeo Ndg. Mwinyi Ubaya, watoto wako Salama na Rahma, Dada yako, Kaka yako, Mama yako, wifi zako, familia ya Magoha na Ubaya kwa ujumla pamoja na Ndugu, marafiki na jamaa. 
Tunazidi kukuombea kwa Allah azidi kukupa kauli thabiti na makazi mema Akhera. 
INNA LILLAH WAINNA LILLAH RAJIUN

Barabara ya Mbezi kwa Msuguli kuelekea Bwaloni-Masaki mpaka Malamba Mawili ni utelezi tu

$
0
0
 Kutokana na mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia leo katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaam, kumepelekea Barabara ya Mbezi kwa Msuguli kuelekea Bwaloni-Masaki mpaka Malamba Mawili kupitika kwa shida kutokana na utelezi wa tope. hali iliyoleta adha kubwa kwa watumiaji wa njia hiyo, kwani si gari wala pikipiki zinazoweza kupita kwa sasa.
 Mmoja wa waendesha bodaboda akijaribu kumuelekeza dereva wa gari iliyokuwa mbele yake kutembea katika sehemu yenye unafuu kidogo wa kupitika.
 Ni nadra sana kuona waendesha bodaboda wakiwa kwenye msururu namna hii, lakini kutokana na hali ya barabara hiyo imewalazimu na wao kufuata utaratibu na kukubali matokeo.
 Baadhi ya watembea kwa miguu.
Moja ya gari ikiwa imekwama katika barabara hiyo.

WAKAZI WA DAR WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA MATIBABU BURE KWENYE MELI YA CHINA

$
0
0
Wakazi wa kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye eneo la Kituo cha Kati cha Polisi ili kupata utaratibu wa kuelekea kwenye Meli kubwa ya Madaktari bingwa kutoka nchini China iliyotia nanga Bandarini, ambapo madaktari hao watatoa huduma mbalimbali za matibabu bure kwa wakazi hao. Ujio wa Meli hiyo ni kutokana na jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani akagua mitambo ya kuzalisha Umeme ya kituo cha Umeme KIDATU

$
0
0
 Waziri wa Nishati  Dkt.Medard Kalemani akagua mitambo ya kuzalisha Umeme ya kituo cha Umeme KIDATU, sambamba na ukaguzi huo Dkt.Kalemani alipokea taarifa ya hali ya mitambo ya uzalishaji umeme pamoja na kukagua maendeleo ya ukarabati wa Mtambo namba 1, ulioanza kufanyiwa ukarabati  tarehe 19 Oktoba 2017 na kampuni ya Koncar yenye makao yake nchini Croatia.
Waziri wa Nishati  Dkt.Medard Kalemani akikagua mitambo ya kuzalisha Umeme ya kituo cha Umeme KIDATU, sambamba na ukaguzi huo Dkt.Kalemani alipokea taarifa ya hali ya mitambo ya uzalishaji umeme pamoja na kukagua maendeleo ya ukarabati wa Mtambo namba 1, ulioanza kufanyiwa ukarabati  tarehe 19 Oktoba 2017 na kampuni ya Koncar yenye makao yake nchini Croatia.

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa kaongozana
 na Katibu Mkuu wake Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM  jijini 
Dar es salaam  leo Jumatatu Novemba 20, 2017
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa kaongozana na Katibu Mkuu wa chama hicho  Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM  jijini Dar es salaam  leo Jumatatu Novemba 20, 2017

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka sawa makabrasha kabla ya kuanza kwa  kikao cha Kamati Kuu ya CCM  jijini Dar es salaam  leo Jumatatu Novemba 20, 2017

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka sawa makabrasha kabla ya kuanza kwa  kikao cha Kamati Kuu ya CCM  jijini Dar es salaam  leo Jumatatu Novemba 20, 2017










  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  Ndugu Abdulrahman Kinana akithibitisha kutimia kwa akidi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es salaam kinachoongozwa na Mwenyekiti wa
chama hicho Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumatatu Novemba 20, 2017

U.S. Government Hands Over Medical Equipment and Supplies to the Tanzania Police Force

$
0
0
 The United States Agency for International Development (USAID) in collaboration with John Snow Inc. and Project C.U.R.E handed over TZS 2 billion worth of medical goods and equipment to the Tanzania Police Force today at Dar es Salaam’s Kilwa Road Police Hospital Grounds. Donations include modern hospital beds, operating tables, ultrasound machines and surgical instruments, all of which will be distributed among 26 police health facilities supported by the USAID AIDSFree Strengthening Police and Prison Comprehensive HIV Services Project.

The AIDSFree Project is currently servicing over 10,000 HIV-positive individuals on sustained antiretroviral therapy, in addition to providing medical services to police staff, their families, and surrounding communities. Through this support, the United States Government continues to show its commitment to a comprehensive approach to strengthening health systems in Tanzania. The AIDSFree Project, which has been working in Tanzania since 2015, aims to improve the quality of comprehensive HIV and TB prevention, treatment, care, and support services delivered at police and prison health care facilities in mainland Tanzania and Zanzibar. This support contributes to the objectives of the Tanzania National Multi-Sectoral Strategic Framework for HIV and AIDS (2013/14–2017/18).

To date, AIDSFree has built capacity of approximately 1,000 health care providers on various aspects of HIV provision through on-the- job trainings and clinical attachments. In partnership with the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children and local government authorities, the project has implemented policies, guidelines, standard operating procedures, and various tools to further improve service provision within police health facilities.
These efforts have also provided infrastructural support through the procurement and installation of air conditioning units in medicine storage facilities to ensure the quality and efficacy of medicines and medical supplies. The quality and availability of data has also been improved through the provision of computers for data entry and analysis. Due to these improvements, the health facilities have witnessed an increase of patient flows and improved access to quality health services of police officers, their families, and surrounding communities.

AIDSFree is a five-year cooperative agreement funded through the U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) by the U.S. Agency for International Development. AIDSFree is implemented by JSI Research and Training Institute, Inc., with support from partners including Abt Associates Inc., Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation, EnCompass LLC, IMA World Health, the International HIV/AIDS Alliance, Jhpiego Corporation, and PATH.

AIDSFree supports and advances the implementation of the U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief in 12 countries by providing capacity development and technical support to USAID missions, host-country governments, and HIV implementers at the local, regional, and national level.

TAARIFA KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

$
0
0
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakanusha taarifa inayosambaa katika Mitandao ya Kijamii kuhusu Taasisi ya Kiraia ijulikanayo kama Samia Habari Suluhu. 

Taasisi hiyo inajitambulisha  kuwa inatoa mikopo ya fedha taslim, pikipiki na bajaji kwa wanawake wajasiriamali kwa masharti ya kuweka dhamana ya fedha taslimu shilingi laki mbili. Ofisi inapenda kuujulisha umma kuwa taarifa hizo ni za uongo na uzushi na zina lengo la kuupotosha umma wa Watanzania.

Makamu wa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, hamiliki taasisi yoyote ya aina hiyo na hahusiki kwa namna yoyote na kazi za taasisi hiyo na wala haitambui taasisi hiyo.

Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka Wananchi kuzipuuza taarifa hizo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwani zinalenga kuleta taharuki na kupotosha Umma wa Watanzania.

Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ikulu- Dar es Salaam.

CHAMA CHA MBIO ZA MAGARI TANZANIA (AAT) CHAWAKUMBUKA WAATHIRIKA WA AJALI NA KUJADILIANA NA WADAU NAMNA YA KUZIPUNGUZA

$
0
0
Mgeni Rasmi Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Afande Deus Sokoni akifungua mjadala katika Siku ya Kukumbuka waathirika wa Ajali Duniani (The World Day Of Remembrance For Road Traffic Victims 19 November 2017) iliyoandaliwa na kufanyika kwenye ofisi za Chama Cha Mbio za Magari Tanzania AAT Upanga jijini Dar es salaam ikishirikisha wadau kutoka taasisi mbalimbali nchini Tanzania.

Wadau mbalimbali wamekutana na kujadiliana namna ya kupunguza ajali hasa katika kuzipitia sheria za usalama barabarani na kuzifanyia marekebisho pamoja na kuwakumbusha watumiaji wa Barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani, Taasisi zilizoshiriki katika mjadala huo ni WHO, KIkosi Cha Usalama Barabarani, SUMATRA, Chama Cha Mbizo za Magari Tanzania AAT, Chama cha Kutetea Abiria Tanzania CHAKUA, TIRA na wawakilishi Idara ya Habari Maelezo.
Mratibu wa Semina hiyo Bw. Alferio Nchimbi akizungumza katika semina hiyo na kukaribisha wadau mbalimbai ili kuchangia michango yao katika mada mbalimbali zilizowasilishwa.
Mgeni Rasmi Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Afande Deus Sokoni akisisitiza jambo wakati akijibu maswali katika semina hiyo kulia ni Mratibu wa Semina hiyo Bw. Alferio Nchimbi.
Bw. Monday Likwepa Katibu Mkuu wa Chama cha Kutetea Abiria akichangia mada katika semina hiyo.

BREAKING NYUZZZZ.....: WAKILI MAARUFU WA KUJITEGEMEA DKT. RINGO TENDA NA ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU WA TIB, PETER NONI WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0
Wakili marufu wa kujitegemea Dkt. Ringo Tenga (aliye mbele), akifuatiwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), Peter Noni na wenzao wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, walipofikishwa kusomewa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili. Kesi hiyo inatarajiwa kisikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa.
Wakili marufu wa kujitegemea Dkt. Ringo Tenga, aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), Peter Noni na wenzao wakiwa katika Ukumbi Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakisubiri kusomewa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili. Kesi hiyo inatarajiwa kisikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa.

MAHAFALI YA KWANZA YA CHUO CHA MANJANO BEAUTY ACADEMY YAFANYIKA JIJINI DAR

$
0
0
Chuo cha Manjano Beauty Academy  kimetunuku Astashahada (Certificates) na Stashahada (Diploma) kwa wahitimu 120 wa kwanza wa chuo hicho katika nyanja ya urembo na utengenezaji wa nywele.Urembo na mitindo ni moja kati ya sekta zinazoajiri mamilioni ya wanawake kwa sasa, lakini bado sekta hiyo imeendelea kuwa isiyo rasmi.
Wanawake wengi wanaofanya kazi kwenye saluni hawana utaalamu, lakini ndiyo wanaofuatwa na wanaume na wanawake kwa ajili ya kutengenezwa mionekano inayovutia, wanaishi kwa kufanya kazi kubahatisha.

Akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya  Manjano Beauty Academy iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwanzilishi wa Manjano Beauty Academy, Shekha Nasser alisema kuwa maono hayo ndiyo yaliyosababisha yeye kuanzisha Manjano Beauty Academy.Manjano Beauty Academy ni shule kwa ajili ya afya na urembo ambayo ina lengo la kuwawezesha wasichana wa Kitanzania.
“Tunashauri, tunatoa mafunzo na kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya soko kwa kuwapatia ujuzi unaohitajika. Serikali haiwezi kuwaajiri wahitimu wote, hata sekta binafsi haiwezi kwa hivi sasa, kwa hiyo mafunzo haya yanawasaidia wasichana wadogo kuweza kujitengenezea soko kwenye sekta ya urembo,” alisema Shekha.

Kwa mujibu wa Shekha, wasichana hao wamekuwa wakipewa mafunzo na wakufunzi bora wanaopatikana katika sekta ya urembo  ambayo yatawatasaidia wao kutimiza malengo yao binafsi pamoja na malengo ya kitaasisi. 
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama  Sophia Mjema Akizungumza Machache wakati wa Mahafali  ya kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy .Ambapo amewataka Wanawake Kuchangamkia Fursa ya Urembo kwa kuwa ukuaji wake kwa sasa ni kubwa na inakabiliwa na Upungufu wa Wataalamu hivyo akiwashauri wanawake wengi Kujiunga na Kuiga Mambo Mazuri Yanayofanywa na Chuo cha Manjano Beauty Academy.Akieleza zaidi Alisema Sekta ya Urembo ina Fursa kubwa kwa Ajira kwa sasa,Katika Mahafali hayo  Wahitimu 120 Wametunukiwa vyeti katika  katika nyanja ya urembo.
Mwanzilishi wa Chuo cha  Manjano Beauty Academy Mama Shekha Nasser Akitoa Hotuba yake wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliofanyika Kwenye Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam.Mama Shekha Nasser Amewashukuru wazazi na walezi kwa kuwapeleka Watoto wao kwenye chuo hicho kwa LengoKupata Ujuzi wa Maswala ya Urembo,Aidha Ametaja Changamoto kubwa Alizokabiliana nazo wakati anaanzishi Chuo hicho Ikiwemo ukosefu wa Wataalamu wazawa wa Maswala ya Urembo.
 Baadhi ya  Wahitimu waliotunukiwa kwenye Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy yaliofanyika Kwenye Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam
 Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama  Sophia Mjema  Akitoa Cheti kwa Mmoja wa Wahitimu Kwenye  Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy..


 Mgeni Rasmi,Uongozi wa Chuo cha Manjano Bauty Academy ,Wageni waalikwa na Wahitimu Wakiwa katika Picha ya Pamoja.

WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE

$
0
0
Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipokea moja ya vifaa vya uchunguzi wa saratani ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran kushoto wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya kizazi leo jijini Dar es salaam.

WAZIRI Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewaelekeza waganga wakuu wa mikoa wote nchini kuanzisha zoezi la wazi la uchunguzi wa saratani ya kizazi angalau mara moja katika mwezi ili kusaidia kutokomeza tatizo kwa wanawake hilo nchini.

Hayo amesema wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratan vyenye thamani ya shilingi milioni 98  ambavyo vimetolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya JHPIEGO kwa kushirikiana na USAID ili kusaidia kupambana na tatizo hilo nchini.

“Angalau ifikapo Desemba 2018 nataka  vituo vya Afya vya Serikali  524  viwe vinatoa huduma ya matibabu ya awali ya Saratani ya mlango wa kizazi na kufikia  wanawake milioni 3 watakaopata huduma hii ili kuokoa wanawake wa vijijini  kwani mpaka sasa hivi tunavyo vituo vya afya  265 vinavyotoa huduma hii ” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa uchunguzi na kutoa chanjo ya Saratani ya mlango wa kikazi  kwa wasichana kuanzia miaka 9 mpaka 14 ili kuweza kupunguza vifo vitokanavyo na tatizo hilo kwani katika kila wanawake 100 vifo vinavyotokana na ugonjwa huo ni 32.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa katika kuongeza jitihada za  kupambana na ugonjwa huo Serikali imeongeza vituo vya afya 100 kutoka 343  hadi kufikia 443 mwaka huu ili kutokomeza tatizo hilo nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran amesema kuwa walianzisha mpango wa kupambana na tatizo hilo na kufanikiwa kuwafikia wanawake elfu 75 kwa mikoa 4 tangu mwaka 2009.

“Mbali na mikoa hiyo 4 bado tunalengo la kuongeza mikoa mingine 7 ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa ajili ya kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi ili kuweza kuokoa wanawake wengi zaidi nchini” alisema Bw. Zoungran.
Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipokea moja ya nyenzo za kufundishia juu ya uchunguzi wa saratani ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran kushoto wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya kizazi leo jijini Dar es salaam katikati ni Afisa Afya kutoka USAID Bi. Ananth Thambinygan .
Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini Dar es salaam .
Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara ya afya,Jpiego na USAID wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini Dar es salaam, wa tatu kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran na aliyevaa nguo ya pundamilia ni Afisa Afya kutoka USAID Bi. Ananth Thambinygan .picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

SIKUKUU ZA KITAIFA ZENYE MAPUMZIKO KWA MWAKA 2018

Balozi wa Tanzania nchini Shelisheli awasilisha Hati za Utambulisho

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Shelisheli mwenye makazi yake nchini Kenya, Mhe. Dkt. Pindi Chana akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Shelisheli, Mhe. Danny Faure. Makabidhiano hayo yalifanyika tarehe 14 Novemba 2017, katika Ikulu ya nchi hiyo. 
Mhe. Balozi Chana akizungumza na Mhe. Rais Faure ambapo Serikali ya Jamhuri ya Shelisheli imemuhakikishia kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake. 
Mhe. Balozi Chana akiwasili katika Ikulu ya Jamhuri ya Shelisheli. 

BENKI YA KILIMO YATEMBELEA MIRADI YA JKT KITEULE CHA BULAMBA, BUNDA

$
0
0
Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetembelea mradi wa ufugaji wa vifaranga vya samaki unaotekelezwa na kikosi cha 822 Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Rwamkoma wilaya ya Butiama kupitia Kiteule chake cha Bulamba, wilayani Bunda.

Akizungumza lengo la ziara hiyo, mkuu wa msafara huo ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila amesema lengo kubwa la kutembelea Mradi huo ni kujionea juhudi za serikali za kuchagiza mapinduzi ya kilimo hasa katika tasnia ya ufugaji na uvuvi wa samaki nchini.

Bibi Kurwijila aliongeza kuwa tasnia ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ni mojawapo ya minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa ufugaji wa samaki nchini.

Aliongeza kuwa Benki ya Kilimo imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Samaki na uvuvi nchini ili ziweze kuchangia ukuaji wa uchumi nchini.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (kulia) akizungumza wakati walipotembelea Mradi wa Ufugaji wa Samaki kwa Vizimba Kiteule cha Bulamba uliopo wilaya ya Bunda, Mkoani Mara. Kushoto ni Afisa Uvuvi wa wilaya ya Bunda, Bw. Steven Ochieng’.
 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Bw. Dome Malosha (kulia) akizungumza wakati walipotembelea Mradi wa Ufugaji wa Samaki kwa Vizimba Kiteule cha Bulamba uliopo wilaya ya Bunda, Mkoani Mara. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Bw. Joseph Mutashubilwa (katikati).
Msimamizi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki wa JKT Kiteule cha Bulamba, Luteni Kelvin Gondo akitoa maelezo juu ya maendeleo ya ufugaji wa samaki katika hatua mbalimbali.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>