Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

Dkt. Mwakyembe aipongeza TAMWA kwa kuwa na wanachama wanaokidhi vigezo vya Sheria ya Habari

$
0
0
Na  Shamimu Nyaki –WHUSM.
Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa pongezi kwa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kwa kuwa na wanachama ambao wanakidhi vigezo vilivyopo katika Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 ambapo moja ya vigezo hivyo ni kuwa na Wanataaluma ya Habari wenye elimu ya kuanzia Stashahada.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo Jana Jijini Dar es Salaam katika sherehe za maadhimisho ya miaka 30 ya Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) ambapo amewataka wanachama hao kuendelea na juhudi zao za kukemea ukatili wa kijinsia, ndoa za utotoni, na mauaji ya vikongwe yaliyotoa sifa kubwa kwa  chama hicho.
“Nimefurahi sana kusikia kuwa wanachama wa chama hiki wanaanzia ngazi ya Stashahada kama ambavyo Sheria yetu ya Habari inavyosema kuwa ni lazima kwa mwanataaluma ya Habari kuwa na kiwango cha Elimu kinachoanzia hapo,lakini pia Serikali inatambua sana mchango wenu wa kuilemisha jamii masuala mbalimbali ikiwemo ukatili wa kijinsia endeleeni kufanya hivyo ili jamii yetu iwe jamii bora”.Alisema Mhe. Mwakyembe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Bibi Alack Mayombo ameishukuru Serikali kwa mchango mkubwa inaotoa kwa Chama hicho pindi inapohitaji msaada na kuahidi kushirikiana na Serikali katika kuelimisha jamii hasa masuala ya Ukatili wa Kijinsia.
“Tunashukuru sana Serikali kwa jinsi inavyotuunga mkono katika juhudi zetu za kutatua changamoto zinazoikumba jamii yetu hasa mauaji ya Vikongwe,watu wenye ulemavu wa ngozi,ndoa za utotoni  pamoja na ukatili wa kijinsia mara zote tulizotoa taarifa kwa Serikali imekuwa ikichukua hatua zinazostahili”. Aliongeza Bibi  Alack.
Naye Mkurugenzi wa Chama hicho Bi Edda Sanga ameeleza kuwa kwa kipindi cha miaka 30 tangu kilipoundwa chama hicho kimefanikiwa kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo kiwango cha Ukeketaji, Mimba za utotoni, madawa ya kulevya na athari zake katika jamii na kutoa taarifa ambayo imesaidia kupunguza matatizo hayo.
Chama hicho kilianzishwa tarehe 17 Novemba 1987 na wanahabari wanawake lengo ikiwa ni kupinga ukatili wa aina yoyote katika jamii na tayari kimeefanikiwa kwa kiasi kikubwa,Aidha chama hicho kimezindua luninga ya Mtandaoni itakayotoa taarifa mbalimbali za Ukatili wa kijinsia pamoja na mambo mengine ya kijamii.
 . Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na viongozi na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya chama hicho.
 . Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) Bibi Alack Mayombo akieleza mafanikio ya chama chao ikiwa ni pamoja na kupambana na ukatili wa kijinsia  jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya chama hicho.
 Mkurugenzi  wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) Bibi Edda Sanga akieleza majukumu ya chama chao jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya chama hicho.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe  akikata utepe kuashiria  uzinduzi wa kitabu cha mafanikio tangu kuanzishwa kwa   Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya kutimiza  miaka  30 ya chama hicho.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe  akibonyeza kitufe  kuashiria  uzinduzi wa  luninga ya mtandaoni ya Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya kutimiza miaka 30 ya chama hicho. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali  Dkt. Hassan Abbas.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe akimkabidhi Tuzo ya Heshima Bibi Fatma Alloo kwa mchango wake katika  Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya kutimiza  miaka 30 ya chama hicho.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe (katikati)  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya wanachama wa  Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya kutimiza  miaka 30 ya chama hicho. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali  Dkt. Hassan Abbas.

DKT. SHIKA: NIKISHINDWA KUNUNUA NYUMBA KWA LUGUMI, NITANUNUA NYUMBA NYINGINE

$
0
0

Tazama video ya Dk. Luis Shika alipofika katika ofisi za Posta.

MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI YAZINDULIWA LEO MKOA WA SHINYANGA, 2017.

$
0
0
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amefunga wiki ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga yaliyoanza siku ya Jumatatu Novemba 13,2017 katika viwanja vya jeshi la Zimamoto mjini
Shinyanga.

Akizungumza leo Jumamosi Novemba 18,2017 wakati wa kufunga maadhimisho hayo, yenye kauli mbiu "Zuia ajali,Tii sheria,Okoa
Maisha",Kamanda Haule aliwataka watumiaji wa barabara kuzingatia alama na michoro ya barabarani na watembea kwa miguu kuhakikisha wanapokuwa barabarani wanavuka katika maeneo yanayostahili ili kupunguza ajali zisizo za lazima.

Katika hatua nyingine aliwataka wananchi kulinda miundombinu ya barabara kwa kushirikiana na serikali na kuhakikisha wanawakata baadhi ya watu wasio waaminifu wanaoiba miundombinu ya barabara.
“Naomba tushirikiane kuwafichua na kuwakamata watu wanaoiba miundombinu ya barabara,na tukiwakamata tuwafikishe katika vyombo vya sheria”,aliongeza Haule.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwakumbusha akina mama kukaa mkao wa kiume wanapopanda pikipiki ama baiskeli badala ya kukaa upande upande ili kupunguza ajali za barabarani.
Naye Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga,Anthony Masanzu alisema katika wiki hiyo ya nenda kwa usalama,wamefanikiwa kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha bodaboda 184.
Alisema mbali na kutoa elimu kwa waendesha bodaboda na wananchi waliotembelea mabanda ya usalama barabarani pia walitembelea shule mbalimbali mjini Shinyanga ambazo zipo karibu na barabara.
“Tumetumia wiki hii kutoa elimu ya usalama barabarani kwa makundi mbalimbali ya watumiaji wa barabara ili kuhakikisha kuwa tunazuia ajali na kuokoa maisha yao”,aliongeza Masanzu.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga,Anthony Masanzu akizungumza wakati wa kufunga wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Shinyanga,Wilson Majiji akizungumza wakati wa kufunga wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga.Burudani ya ngoma ya kucheza na nyoka ikiendelea
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akitoa vyeti kwa mmoja wa waendesha bodaboda (kati ya 184) waliopata mafunzo/elimu ya usalama barabarani wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga mwaka 2017.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

NZUNDA: MARUFUKU KUINGIA MAKUBALIANO NA NGO's BILA KUPITA TAMISEMI.

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT, RS-TABORA
SERIKALI imepiga marufuku Halmashauri zote nchini kuingia makubaliano na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali(NGO’S) bila kupitia na kiuhidhinishwa na Ofisi ya Rais , Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa( TAMISEMI ) kwa kuwa baadhi ya mambo yamekuwa hayaendebi na vipaumbule vya Serikali ambayo nakusudia kuwasaidia kuwasaidia wananchi.
Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais , Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa( TAMISEMI ) Tixon Nzunda wakati akizungumza na Watendaji  na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Manispaa ya Tabora , Halmashauri za Wilaya ya Sikonge, Uyui , Kaliua na Urambo.
Alisema kuwa  kabla ya kuanza utekelezaji wa shughuli za NGO ni vema Halmashauri zikapeleka maombi ya mashirika ambayo yameomba kufanyakazi katika maeneo yao ili Serikali inone kama kweli inaendana na vipaumbele ambavyo imepanga katika kuboresha maisha ya watanzana ambao maisha yao yako chini.
Nzunda alisema mashirika hayo yamekuwa yakidai pesa ya kusaidia Watanzania kutoka kwa wafadhili lakini matokeo yake fedha hizo zimekuwa zikiishi kuwanufaisha watu wachache na wanapoaandika taarifa kwa watu waliowapa fedha wadai kuwa wamewasaidia Watanzania katika miradi ya maendeleo ya mabilioni ya fedha kumbe sio kweli imeshia mifukoni kwa wachache.
Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inelenga kuhakikisha kuwa kama fedha zinatolewa kwa ajili ya walemgwa ziende kusaidia eneo husika ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana kwa jami husika , kwa Serikali na wafadhili na wafadhili husika.
Nzunda alisema kuwa kumekuwepo na mashirika ambapo yamekuwa yakutumia mbinu ya kuwasaidia wananchi kumbe fedha hizo zimekuwa zikiwanufaisha watu wachache kwa kulipwa posho na mambo mengine ambayo hayana tija kwa wananchi wa kawaida.
Alisema Mashirika amabayo yana nia ya kweli ya kusaididia watanzania lazima yakubaliane na viapumbe vya Serikali ili yaweze kufanya kufanya kazi nchini vingine ni vema yakatafute nchini nyingine ya kufanya mambo yake bila kufuata utaratibu wa nchi hisika.
Nzunda alitoa wito kwa Halmashauri ya kuhakikisha kuwa kabla ya kuyaruhusu Mashirika hayo yamepata kibali cha TAMISEMI ili kuepuka kisingizio cha kuwageuza wananchi mtaji wa wache kujipatia fedha kwa maslahi binafisi.
Alisema mashirika yamekuwa yakianda taarifa nzuri kwa wanawapa fedha kuwa wamesaidia jamii husika kumbe hakuna kinachoonekana Zaidi ya wao kunufaika
Nzunda alisema  kuwa Halmashauri itakayoingia makubaliano ya NGO bila kupitia TAMISEMI watendaji wake itabika wawajibishwe kwa kusimamia maslahi ya umma.
Naibu Katibu Mkuu yupo katika ziara ya kikazi katika Mikoa ya Kigoma, Tabora na Singida kwa lengo ya kuhimiza usimamizi bora wa sekta ya elimu , kilimo, mifugo , utawala bora na mengine mengi.

WAZIRI MKUU AONGOZA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA KATIBU MKUU WA CWT

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo,alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Katibu Mkuu. Wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Marehemu, Alhaji Yahya Msulwa .leo Novemba,18. 2017. Nyumbani kwa marehemu Toangoma jijini Dar es salaam.Aliye simama kwa kwa Waziri Mkuu ni Mke wake Mama Mary Majaliwa.
 Mke wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo,alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Katibu Mkuu. Wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Marehemu, Alhaji Yahya Msulwa .aliye simama kushoto kwake ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa  pamoja na Mke wake  leo Novemba,18. 2017. Nyumbani kwa marehemu Toangoma Jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa Pole, Bi. Sharifa Msulwa. kufuatia kifo cha Mume wake aliye kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Marehemu Alhaji Yahya Msulwa  ,Waziri Mkuu alifika nyumbani kwa Marehmu Toangoma  jijini Dar es salam leo November 18, 2017
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

KAIMU MKURUGENZI MKUU NIDA AWASILI MARA TAYARI KWA UZINDUZI WA ZOEZI LA USAJILI; AKIWA AMEAMBATANA NA KAMISHNA GENERALI WA IDARA YA UHAMIAJI NCHINI

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu (NIDA), Ndg Andrew W. Massawe amewasili mkoani Mara akiwa ameambatana na Kamishna Generali wa Idara ya Uhamiaji nchini Dkt. Anna Peter Makakala tayari kwa uzinduzi rasmi wa kuanza kwa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Mkoa huo utakaofanywa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mhandisi Hamad Masauni.
Mara baada ya kuwasili viongozi hao walipokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Malima ambaye aliwatambulisha kwa wananchi wa Bunda kabla ya kukutana na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe.  Annarose Nyamubi  ambaye pamoja na kuwapa ripoti ya maandalizi ya Usajili kwenye Wiilaya yake, walipata fursa kutembelea Kambi ya JKT Butiama kukagua mafunzo kwa vijana ambao wataendesha zoezi hilo ndani ya siku 60.
Akizungumza na vijana katika Kambi hiyo, ndg. Masssawe amewataka kuwa wazalendo na makini katika zoezi wanalokwenda kulisimamia kwa kuhakikisha wanalifanya kwa uangalifu na nidhamu ya hali ya juu kwa faida ya Taifa lao.
“ tunafarijika sana tunapoona zoezi hili likiendeshwa na vijana wa JKT kwani mara zote wamekuwa wakijitoa kufanya kazi nzuri yenye uzalendo wa kweli kwa Taifa lao; ndiyo maana nawapongeza kwa dhati uongozi wa Mkoa na Wilaya kwa kuamua kusimamia zoezi hili na kuweka malengo ya utekelezaji, na sisi tunaahidi kwenu hatutawaangusha” alisisitiza.
Uzinduzi wa zoezi la Usajili kwa mkoa wa Mara utafanyika Jumapili 19/11/2017 na unategemewa kuhudhuriwa na viongozi wote wa Mkoa wakiwemo wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Madiwani, watendaji na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji, watumishi wa umma, Viongozi wa Dini na Wananchi. 
 Kamishna Generali wa Idara ya Uhamiaji nchini Dkt. Anna Peter Makakala, akizungumza jambo wakati alipowasili ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe. Annarose Nyamubi  (Aliyeketi Katikati). 
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu (NIDA) Ndg. Andrew W. Massawe akiweka saini kitabu cha wageni alipotembelea Kambi ya JKT Butiama kukagua mafunzo kwa vijana watakaoshiriki kuendesha zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu akipokea maelezo ya namna mafunzo yanavyotolewa kwa vijana wa JKT. Katikati ni Afisa wa Nida mtaalamu wa mifumo ya komputa Bw Godfrey Surera ambaye amekuwa akiendesha mafunzo hayo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida akisisitiza jambo mbele ya vijana wa JKT (Hawapo pichani) wakati alipotembelea kambi ya Butiama kukagua mafunzo ya namna ya kutumia mashine yanayoteolewa kwa vijana wa JKT. Kulia ni  Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe. Mhe.  Annarose Nyamubi 

TAASISI ZA SERIKALI ZATAKIWA KUTUMIA SHIRIKA LA POSTA KUTUMA NA KUPOKEA MIZIGO

UPDATES ZA DKT LOUIS SHIKA NA UNUNUZI WA NYUMBA ZA LUGUMI


Azam TV - FULL HIGHLIGHTS: TZ PRISONS 0-1 SIMBA SC

DKT. KAYANDABILA: SERIKALI KUENDELEA KUKIJENGEA UWEZO CHUO CHA KODI

$
0
0
SERIKALI kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imesema itaendelea kukijengea uwezo Chuo cha Usimamizi wa Kodi Nchini (ITA) ili kuhakikisha kuwa Chuo hicho kinazalisha Wataalamu  bora wenye kukithi  mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Yamungu Kayandabila wakati wa mahafali ya kumi cha Chuo cha Kodi Nchini (ITA) na kuongeza kuwa malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa Chuo hicho kinazalisha wataalamu wenye umahiri katika masuala ya forodha na kodi.
Dkt. Kayandabila alisema Serikali inatambua umuhimu wa Chuo hicho kwa ustawi wa kiuchumi na kijamii, hivyo kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itaendelea kukipangia Chuo hicho bajeti ya maendeleo ili kukithi matumizi yake ya kimaendeleo ikiwemo kufanya tafiti kwa kiwango kinachohitajika.
“Serikali itaendelea kushirikiana na Chuo cha Kodi kupitia Mamlaka ya Mapato kwa kuhakikisha kuwa mipango yenu hususani Mpango Mkakati wa Nne unaoanza kutekelezwa mwaka 2017/18 unatekelezwa kikamilifu kwa kuwapatia hosteli mpya za wanafunzi, upanuzi wa majengo ya ofisi za wakufunzi na ujenzi wa kampasi mpya ya Misugusugu Kibaha Mkoani Pwani” alisema Dkt. Kayandabila.
Dkt. Yamungu aliwataka wahitimu hao kutambua kuwa Serikali inatambua umuhimu na mahitaji ya Wataalamu wa kodi, hivyo Chuo hicho hakina budi kuzalisha wataalamu watakaosaidia juhudi za Serikali za kukuza mapato ya ndani na kupunguza utegemezi kwa wafadhili.
Aliongeza kuwa pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Chuo hicho, Dkt. Kayandabuila aliutaka Uongozi wa Chuo hicho kuendelea kujiimarisha katika utafiti na kutoa mafunzo katika masuala ya kodi hususani sekta ya uchimbaji madini, mafuta na gesi na sekta ya fedha ili kusaidia kuongeza makusanyo ya mapato katika sekta hizo. 
Akifafanua zaidi Kayandabila alisema utafiti katika sekta za madini, mafuta na gesi utasaidia kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kwa kukuza mapato ya ndani na kuongeza uwezo wa Serikali kutoa huduma za kijamii na kusimamia viwanda.
Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kicheere alisema Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa Chuo hicho kinazalisha Wataalamu bora wa forodha na kodi pamoja na kupanua wigo wa ushirikiano na mataifa ya nje ikiwemo Botswana, Kenya, Burundi na Sudan Kusini.
Alisema kupitia Chuo hicho mamlaka yake imejipanga kuhakikisha kuwa Tanzania inaweza kuzalisha wataalamu wake wa ndani na kupunguza gharama ya kuchukua wataalamu wa nje ya nchi kwa ajili ya kufanya tafiti mbalimbali za masuala ya forodha na kodi.
“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa ITA kinazalisha wataalamu bora sambamba na kuendelea kuwa  kuwa na Chuo cha Umahiri kama tulivyopendekezwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki” alisema Kicheere.   
Naye Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Isaya Jairo alisema tangu Chuo kilipopata usajili kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wameweza kutoa kudahili wanafunzi 6000, ambapo ili kupanua wigo wa masomo ya forodha na kodi, Chuo hicho kimepanga kushirikiana na vyuo mbalimbali vya nje ya nchi.
Aliongeza kuwa pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana hadi sasa, Chuo hicho kinaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo wanafunzi wengi wa masomo ya shahada kushindwa kuhitimu masomo yao kutokana na ukosefu wa ada.
 Baadhi ya Wanafunzi  wa Chuo cha Usimamizi wa Kodi  (ITA) pichani wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na wageni mbalimbali waliohudhuria mahafahali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Novemba 11, 2017. 
 Baadhi ya ndugu na jamaa za wanafunzi waliohitimu katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Novemba 18, 2017.
 Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Huduma kwa Walipa Kodi wa Malamka ya Kodi Tanzania (TRA), (katikati) Richard Kayombo akijadiliana jambo na Maafisa Waandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) wakati wa  mahafali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Novemba 18, 2017.
 Viongozi na Wahadhiri wa Chuo cha Usimamizi wa Kodi wakiongozwa na kikosi cha bendi cha Jeshi la Polisi kuingia katika ukumbi wa Multipurpose katika Chuo hicho wakiwa tayari kuanza mahafali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Novemba 18, 2017.

Viongozi na Wahadhiri wa Chuo cha Usimamizi wa Kodi wakiongozwa na kikosi cha bendi cha Jeshi la Polisi kuingia katika ukumbi wa Multipurpose katika Chuo hicho wakiwa tayari kuanza mahafali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Novemba 18, 2017.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 10 ya Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA), Dkt. Yamungu Kayandabila (kushoto) akiongozwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kicheere kuingia ukumbini kwa ajili ya kuanza kwa hafla ya mahafali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Novemba 18, 2017.

CLOUDS TV yapewa tuzo ya Kituo Bora cha Televisheni 2017

$
0
0
Umoja wa Mataifa kupitia Umoja wa Vijana (YUNA) umetoa tuzo kwa Taasisi na watu binafsi wenye mchango mkubwa katika maisha ya watu barani Afrika.Kupitia tuzo hizo zinazotambulika kama PAHA, kituo cha Televisheni cha Clouds kimetambuliwa kama kituo bora cha Runinga kwa mwaka 2017.
Hiyo ni kutokana na kurusha maudhui yanayomulika maisha ya watu na kutoa tumaini kwao kupitia vipindi na kampeni mbalimbali kama vile...
(#IshiNaMimi #Kipepeo #MalkiaWaNguvu #RudishaTabasamuMiaMoyo na nyinginezo).

Baada ya kupokea tuzo hiyo ya heshima Kampuni ya Clouds Media Group imeishukuru YUNA pamoja na umoja na umoja wa mataifa kutokana na Utambuzi huo.

Sambamba na hilo Clouds Tv imewashukuru Watanzania Kwa kuendelea Kuwaamini na Kuwachagua." Tunaahidi kuendelea kuwatumikia kwa moyo na nguvu zaidi kwani tulishakula kiapo cha kuwa Taasisi ya watu" sehemu ya taarifa hiyo ilieleza.
(#RedioYaWatu #ThePeoplesStation).
#TunakufunguliaDuniaKuwaUnachotaka

BODI YA CHAKUA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR YAANGAMIZA TANI 11.6 YA MAZIWA NA BIDHAA MCHANGANYIKO ZILIZOHARIBIKA

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo

Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa nchini kutoka nje wameshauriwa kutoogopa gharama wakati wa kusafirisha bidhaa zao na wahakikishe wanatumia njia bora za usafirisha ili mizigo yao ifike ikiwa salama.

Mkuu wa Idara ya Udhibiti na usalama wa chakula wa Bodi ya Chakula na Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Khamis Ali Omar ametoa ushauri huo wakati wa kuangamiza tani 11.6 za maziwa katika dampo la Kibele yaliyoingizwa nchini baadhi yakiwa yameharibika kutokana na usafirishaji mbaya.

Alieleza kuwa sehemu ya maboksi ya maziwa yalipasuka na kuharibu mengine na baada ya kuyafanyia uchunguzi walijiridhisha kuwa yalikuwa hayafai kwa matumizi ya binaadamu.Alisema waliishauri Kampuni iliyoiingiza maziwa hayo Farid Supply kuyarejesha yanakotoka ama kuyaangamiza baada ya kuona yako katika hali hatarishi ya afya za wananchi na walikubali yaangamizwe ili kupunguza gharama ya kuyarejesha.

Dkt. Khamis aliwataka wafanyabiashara kuelewa kuwa kunatafauti kubwa ya kusafirisha vyakula vya maji maji na bidhaa nyengine za kawaidi na vyakula vya maji maji vinahitaji tahadhari kubwa zaidi wakati wa kusafirishwa.Alisema lilijitokeza katika kusafirisha maziwa hayo ni kukosekana umakini na kusababisha kontena lililobeba maziwa kuserereka wakati wa safari na baadhi ya maboksi yalianguka na kuapasuka nadani ya kontena hilo.

Meneja wa Kampuni ya Farid Supply Mansour Said ambae alishiriki katika zoezi hilo Kibele, alikubali kuwa kulitokea tatizo katika kontena hilo na baadhi ya maboksi ya maziwa yalipasuka lakini sehemu kubwa ya maziwa hayo yalikuwa hayajaharibika na yalikuwa yanafaa kutumika.

Alisema maziwa hayo yaliyokuwa na thamani ya zaidi ya sh. 52 milioni huenda yalianza kuharibika baada ya kuzuiliwa kwa kwa kipindi cha miezi nane katika bandari ya Zanzibar .
Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakishusha maziwa tani 11.6 na bidhaa mchanganyiko zilizo haribika kwa ajili ya kuangamizwa katika dampo la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.
Gari la Kijiko likiangamizwa maziwa yaliyoharibika pamoja na bidhaa mchanganyiko katika dampo la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkuu wa Idara ya Udhibiti na Usalama wa chakula Dkt. Khamis Ali Omar (wambele) akisimamia ungamizwaji wa bidha zilizoharibika katika dampo la Kibele.
Meneja wa Kampuni ya Farid Supply iliyoingiza maziwa hayo Mansour Said akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sababu ya sehemu ya maziwa hayo kuharibika.Picha na Makame Mshenga.

SHIRIKA LA POSTA LAFADHILI SHINDANO LA 'NATIONAL SPELLING BEE' TANZANIA

$
0
0
SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Coconut Foundtion lenye Makao yake Makuu Kijitonyama Manispaa ya Kinondoni jijini Dar-es-Salaam, leo hii limewatangaza washindi kumi baada ya kumalizika kwa shindano la kutaja herufi sahihi ya sentensi za kiingereza, lililoanza Novemba 11.

Wahusika wa shindano hilo, walikuwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari (English Medium School). Shindano hilo lilikuwa na lengo la kuwajengea uwezo na kujiamini katika matumizi ya lugha ya Kiingereza.

Washindi hao wanatarajia kwenda kwenye mashindano hayo nchini Uganda mnamo mwezi Desemba mwaka huu, ambako mashindano hayo yatazijumuisha nchi za Afrika Mashariki.

Shirika la Posta Tanzania lilikuwa miongoni mwa wafadhili wa shindano hilo.
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Philip Kowero akimkabidhi cheti Mwalimu wa kutoka Shule ya Feza baada ya shule yao, kufanya vizuri katika shindano hilo. 
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Philip Kowero akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi baada ya shule yake, kuwa moja ya shule zilizoshiriki na kufanya vizuri katika shindano hilo.  
Washindi wakiwa wamekaa na zawadi zao walizotunukiwa. 
Baadhi ya washindi wa shindano la Nationa Spelling Bee wakiwa katika picha ya pamoja wa katikati ni mshindi kutoka Shule ya Feza, Bw. Adnan Abdallah. Kulia kwake ni Prokrith Ghandi kutoka Shule ya Aga Khan na kushoto ni Bi. Jackline, jijini Dar-es-Salaam. 
Walimu kutoka Shule mbalimbali na wazazi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi wa shindano la National Spelling Bee, lililofanyika katika ukumbi wa jumba la Makumbusho jijini Dar-es-Salaam. 

SIKU YA TAKWIMU AFRIKA KUADHIMISHWA KESHO

$
0
0

Na: Veronica Kazimoto,Dar es Salaam,

Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yatafanyika kesho tarehe 20 Novemba, 2017 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya alisema maadhimisho hayo yanayoratibiwa na ofisi hiyo kwa niaba ya Serikali, yana lengo la kuongeza ufahamu kuhusu nafasi na mchango wa Tasnia ya Takwimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii Barani Afrika. 

Ruyobya alisema kuwa kaulimbiu ya Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka huu ni “Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora" 

"Kaulimbiu hii inalenga kuweka mkazo katika matumizi ya Takwimu za Uchumi kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wote nchini na Afrika kwa ujumla", amebainisha Ruyobya.

Ruyobya alifafanua kuwa matumizi sahihi ya Takwimu za Uchumi yanaiwezesha Serikali kutunga sera na kutathmini programu mbalimbali kama vile Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP-II), Agenda ya Dunia ya Mwaka 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na Agenda ya Afrika ya Mwaka 2063. 

"Progaramu zote hizi, zina lengo la kuboresha maisha ya wananchi kwa kuhakikisha kuwa, kuna upatikanaji wa Huduma za afya, Elimu, Miundombinu ya umeme na barabara, Mawasiliano, Utunzaji wa mazingira pamoja na Utawala bora", amesema Ruyobya.

Jumla ya washiriki 200 kutoka katika Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Wadau wa Maendeleo, Vyuo vya Elimu ya Juu, Wanafunzi wa Shule za Sekondari pamoja na Wadau mbalimbali wa takwimu nchini wanatarajiwa kuhudhuria kwenye maadhimisho hayo. 

Siku ya Takwimu Afrika huadhimishwa kila mwaka tarehe 18 Novemba ambapo kwa mwaka huu, Tanzania itaadhimisha siku hiyo kesho tarehe 20 Novemba, 2017.
Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) hivi karibuni kuhusu maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yatakayofanyika kesho tarehe 20 Novemba, 2017 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

Dkt Mahiga, (MB) akamilisha Ziara ya Marekani

$
0
0
Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, MB, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki akamilisha ziara ya Marekani alipokuwa kwa Mwaliko wa Mhe. Rex Wayne Tellerson, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Washington, D.C. tarehe 17 Novemba, 2017.

UTAFITI MAPATO NA MATUMIZI KAYA BINAFSI WAANZA TANZANIA BARA

$
0
0
Benny Mwaipaja

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amezindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, utakaogharimu shilingi bilioni 10 zilizotolewa na Benki ya Dunia.

Lengo la utafiti huo utakaofanywa na Ofisi Kuu ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni kupata takwimu zinazohusu shughuli za kijamii na kiuchumi, mapato na matumizi, hali ya makazi na umiliki wa rasilimali katika ngazi ya kaya.

Dkt. Mpango alisema kuwa Utafiti huo utaiwezesha Serikali kupima kiwango cha hali ya umaskini wa kipato, chakula na pengo baina ya matajiri  na maskini kuanzia kipindi cha mwaka 2013 hadi sasa.

“Takwimu zilizopo hivi sasa zinaonesha kwamba kiwango cha umasikini wa kipato ulipungua kutoka asilimia 34 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 28.2 mwaka 2012” Alisema Dkt. Mpango.

Alisema pamoja na takwimu hizo, bado kiwango cha umasikini ni kikubwa na kwamba Serikali kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali inahakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma za msingi za kijamii kwa kadri uchumi unavyokua hivyo kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo la umasikini.

“Nimefurahi kuelezwa kuwa utafiti huu utakusanya takwimu katika kaya binafsi 10,460 kwa Tanzania Bara kuanzia Novemba 2017 hadi Novemba 2018 na kwamba kupitia zoezi hili, Serikali ya Awamu ya Tano imetoa ajira kwa vijana wapata 620 katika maeneo ya vijijini na mijini” alieleza Dkt. Mpango.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza jambo wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi na kuzindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za Utafiti wa Mapato na Matumizi wa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, mjini Dodoma, utakaohusisha kaya binafsi 10,460.

 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu  (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo kuhusu namna utafiti  wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi utakavyotekelezwa wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi na uzinduzi wa wa zoezi la ukusanyaji takwimu za utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi, Mjini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akimkaribisha  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kufunga mafunzo ya Wadadisi, na kuzindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za Utafiti wa Mapato na Matumizi wa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, Mjini Dodoma.
 Wadadisi wa Takwimu za Utafiti  wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/2018, wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanywa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), Mjini Dodoma.

MAGAZETI YA JUMAPILI LEO NOVEMBA 19,2017

RC MAKONDA KUWAKARIBISHA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA KIZALENDO.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA ameandaa tamasha la kuwakaribisha Wanafunzi wa Mwaka wa kwanza kwa Vyuo Vikuu vya Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo, kuwaepusha kuingia kwenye makundi hatarishi. 

Tamasha hilo linalotaraji kufanyika eneo la Maegesho Mliman City litatawaliwa pia na Burudani kutoka kwa Wasanii Mbalimbali ambapo vyombo vya Habari vya TBC, CHANNEL TEN NA E FM wamejitolea kulibeba tukio hilo la kipekee. RC MAKONDA amesema hayo wakati wa Mkutano na hafla ya kupata Chai na Maraisi wa Vyuo Vikuu vya Mkoa wa Dar es salaam pamoja na Viongozi wa Asasi za Kiraia. 

Katika Mkutano huo Vyuo vikuu vimeunga Mkono kampeni ya ujenzi wa Ofisi za Walimu kwa kuchangia Mifuko 25 ya Saruji na kuahidi kuendelea kuunga mkono kampeni hiyo. Aidha RC MAKONDA ametoa nafasi kwa Vyuo vikuu kumuweka kikaangoni kwa kufanya mdahalo wa kubadilishana mawazo na kuelezana changamoto.

RC MAKONDA pia amesema anao mpango wa kuandaa Shindano la Uongozi Wanafunzi wa Vyuo vikuu kwa lengo la kuwajengea Wanafunzi uwezo wa uongozi bora na namna ya kupatia majibu changamoto ambapo Mshindi atapata ofa ya kusoma Bure Chuo cha Diplomasia. 

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam LAZARO MAMBOSASA amewaomba Wanafunzi wa vyuo vikuu kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi pale wanapobaini uwepo wa Wahalifu.

Kampeni ya Uzalendo na Utaifa kuzinduliwa Disemba nane Mjini Dodoma

$
0
0
Na Shamimu Nyaki –WHUSM.

Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo imeandaa Kampeni ya “Uzalendo na Utaifa” inayotarajiwa kuzinduliwa Disemba nane mwaka huu Mjini Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli lengo ikiwa ni kurejesha hali ya Uzalendo na Utaifa katika kutatua changamoto zilizojitokeza na zitakazojitokeza katika Taifa letu.

Akizungumza na Wakuu wa Taasisi za Serikali jana Jijini Dar es Salaam Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Kampeni hiyo inadhamiria kuwakumbusha watanzania Utamaduni wetu na Uzalendo uliokuepo miongoni mwa Watanzania ambao ulileta heshima kubwa ndani na nje ya nchi.

“Kampeni hii ina lengo la kurudisha Uzalendo tuliokuwa nao Watanzania katika kuheshimu mali za Umma, kuogopa rushwa,ubaguzi wa kidini,kikabila,kiitikadi na kikanda ambavyo vilianza kupotea,lakini Serikali ya awamu ya Tano imeanza kurudisha hivyo sisi kama watanzania tunapaswa kuunga mkono jitihada hizi”Alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa Kampeni hiyo inatarajiwa kuleta matokeo chanya ikiwemo kurejesha na kuimarisha moyo wa Uzalendo na Utaifa kwa Watanzania hususan vijana na watoto umuhimu wa kuipenda na kuithamini nchi yao pamoja na kuimarisha umoja upendo na mshikamano wa kitaifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wakuu wa Taasisi za Serikali kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geofrey Mwambe amesema Taasisi za Serikali zinaunga mkono Kampeni hiyo kwani itasaidia watanzania wengi kuelewa historia na Utamaduni ya nchi yao na kuitilia maanani popote watakapokuwa.

Kampeni hiyo yenye kauli mbiu “Nchi Yangu Kwanza” itakuwa ni endelevu na inatarajiwa kufanyika kila mwezi Oktoba kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza jana Jijini Dar es Salaam na Wakuu wa Taasisi za Serikali kuhusu Kampeni ya Uzalendo na Utaifa inayotarajiwa kuzindiliwa mwezi ujao Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Wakuu wa Taasisi za Serikali Bw. Geofrey Mwambe kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) (aliyesimama )akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na Wakuu hao kuhusu Kampeni ya Uzalendo na Utaifa inayotarajiwa kuzindiliwa mwezi ujao Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akiwaonyesha Wakuu wa Taasisi za Serikali Jarida la Nchi Yetu linaloelezea mafanikio ya miaka miwili ya Serikali ya awamu ya Tano lililondaliwa na Idara yake kwa kushirikiana na Taasisi hizo jana Jijini Dar es Salaam.

WATUMISHI WA AFYA BADO WANAHITAJIKA NCHINI.

$
0
0
WATUMISHI wa kada mbalimbali katika sekta ya afya bado wanahitajika nchini ili kuboresha huduma ya afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania ili kuifikisha nchi katika uchumi wa viwanda mpaka kufikia 2020.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa mahafali ya pili ya chuo cha Afya na tiba cha KAM yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

“Tuna malengo ya kuwa na watumishi wa kada mbalimbali za sekta ya afya wapatao laki 1.849 na kati ya hao tumefanikiwa kuajiri watumishi 89842 na bado tunahitaji watumishi 95800 ili kuweza kuwa na rasilimali watu” alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa wanakishukuru chuo hiko kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwa kutoa rasilimali watu katika sekta ya afya kwani wametoa wataalamu wa afya wapatao 1600 mpaka hivi sasa.

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kupunguza vifo vya mama na mtoto Serikali kupitia Wizara ya afya imetoa shilingi milioni 700 kwa vituo vya afya ili kuweza kuboresha huduma za afya nchini.

“Tumetoa milioni 700 kwa kwa vituo vya afya vipatavyo 100 hapa nchini ikiwa milioni 400 kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya upasuaji na vyumba vya kujifungulia na milioni 300 ni kwa ajli ya kununua vifaa tiba” alisema dkt. Ndugulile.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akigawa vyeti kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Afya na Tiba KAM waliofanya vizuri kwenye masomo ya fani mbalimbali ya afya wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akigawa vyeti kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Afya na Tiba KAM waliofanya vizuri kwenye masomo ya fani mbalimbali ya afya wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akipokea na zawadio kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba wa Chuo cha Afya na Tiba KAM dkt. Aloyce Musika kulia wakati wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi Wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha KAM wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha KAM wakimsikiliza wakati wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.Picha Na Ally Daud- Wizara ya Afya (WAMJW).


Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images