Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110115 articles
Browse latest View live

Malima afanya ziara ya kushtukiza Kiwanja cha ndege cha Musoma

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Kigoma Malima (aliyenyoosha mkono), akielekeza jambo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma, Betha Bankwa leo alipotembelea kiwanjani hapo.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma, Betha Bankwa akitoa maelezo mbalimbali kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Kigoma Malima (wa pili kulia) leo Ijumaa alipofanya ziara kwenye kiwanja hicho.

DODOMA, SINGIDA KUTUMIA KILIMO CHA UMWAGILIAJI IFIKAPO 2019

$
0
0
Kiongozi wa msafara wa wawakilishi wa kampuni ya Henan Juren Crane Group kutoka Jimbo la Henan nchini China, Wang Yuheng (wa pili kulia) akisisitiza jambo wakati alipokutana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC), Bw. Henry Mwatwinza Mwimbe (kulia). Tukio hili lilifanyika jana, Alhamisi, Novemba 16, 2017 jijini Dar es Salaam.

Na Daniel Mbega

WANANCHI wa mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga na Simiyu wanaweza kujikwamua kiuchumi kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji ifikapo mwaka 2019 kutokana na kuwepo kwa mpango wa uwekezaji unaolenga kuchimbia visima virefu pamoja na mabwawa katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC Ltd), Bw. Henry Mwantwinza Mwimbe, amesema hayo jana baada ya kukutana na wawakilishi wa kampuni ya Henan Juren Group ya China, ambayo imeonyesha nia ya kuwekeza kwa ubia nchini kwa kutengeneza zana mbalimbali za kilimo ikiwa ni pamoja na kuchimba visima katika maeneo yaliyo kame.


Lengo la uwekezaji huo, kwa mujibu wa Mwimbe, ni kuwakwamua wakulima kiuchumi kwa kuwa na kilimo endelevu cha umwagiliaji badala ya kutegemea mvua, ambazo zimekuwa hazina uhakika kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi yanayotokana na uharibifu wa mazingira.


“Wanachama wetu karibu asilimia 80 wanajihusisha na kilimo, hivyo tunaona itakuwa ni vyema kama tutabadilisha namna ya uendeshaji wa kilimo hiki ili kilete tija kwao na kwa taifa kwa ujumla.


“Katika maeneo mengi mvua zinanyesha mara moja kwa mwaka na wakati mwingine siyo za kutosha, matokeo yake wananchi wanashindwa hata kupata mavuno yanayojidhi matumizi ya nyumbani, achilia mbali ziada ya kuuza sokoni, lakini kilimo cha umwagiliaji kina uhakika na kinaweza kuendeshwa wakati wote wa mwaka,” alieleza Mwimbe.


Alisema kwamba bado wapo katika hatua za awali kuhusu mchakato huo na akafafanua kwamba, mradi huo utawahusisha wanachama wote nchini walio kwenye ushirika ambao watashirikishwa.


Hata hivyo, alisema mradi mama ni kuunganisha (assembling) zana za kilimo kutoka China kama matrekta na mashine nyingine zinazoendana na kilimo watakazoziuza kwa wakulima wa ndani pamoja na nchi jirani, lakini wanaona kwamba hilo litafanikiwa ikiwa wakulima watajengewa uwezo hasa kwa kuwa na uhakika wa maji ili kuendesha kilimo cha umwagiliaji.

Mkalimani, Dkt. Chikira Ismail Msangi, akifasili kuhusu azma ya wawekezaji hao katika kuanzisha kampuni ya ubia itakayounganisha zana za kilimo kama matrekta na mitambo ya uchimbaji visima na umwagiliaji hapa nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC), Bw. Henry Mwimbe. Tukio hili lilifanyika jana, Alhamisi, Novemba 16, 2017 jijini Dar es Salaam.
Hii ni mitambo itakayounganishwa hapa nchini ambayo ni maalum kwa shughuli za ujenzi na uchimbaji wa mabwawa ya maji.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

VIDEO: SERIKALI KUIMARISHA MKAKATI WA KUPUNGUZA VIFO VYA WATOTO NCHINI

SERIKALI YA BURUNDI YANUIA KUWAREJESHA WANANCHI WAKE WALIOKIMBILIA TANZANIA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi wa Tanzania, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika mkutano na wakimbizi wa Burundi wanaoishi kambi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Katika ziara hiyo iliyokuwa pia na ujumbe kutoka Serikali ya Burundi, ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo, Pascal Barandagiye, lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Marco Gaguti, akizungumza katika mkutano na wakimbizi wa Burundi wanaoishi kambi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Katika ziara hiyo iliyokuwa pia na ujumbe kutoka Serikali ya Burundi, ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo, Pascal Barandagiye, lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea.
Mkimbizi wa Burundi anayeishi kambi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu, mkoani Kigoma Paul Ndalaizye., akitoa maoni kwa niaba ya wakimbizi wanaoishi katika kambi hiyo wakati wa Mkutano uliohutubiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo, Pascal Barandagiye (hawapo pichani), lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo nchini Burundi, Pascal Barandagiye (kulia), wakipiga ngoma baada ya kuwasili katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, iliyoko Wilayani Kasulu,mkoani Kigoma.
Wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) katika mkutano na wakimbizi hao, Katika ziara hiyo iliyokuwa pia na ujumbe kutoka Serikali ya Burundi, ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo, Pascal Barandagiye, lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea.

BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI

JAJI MKUU AWAASA WAHITIMU WA SHERIA KUJIENDELEZA KITAALUMA

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma amewataka wahitimu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kujiendeleza katika fani ya Sheria kwa kuwa na hitaji na hamu ya kujiendeleza zaidi toka kiwango kimoja cha elimu hadi cha juu zaidi. Prof. Juma ameyasema hayo mjini Lushoto katika mahafali ya 17 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama ambapo wahitimu 150 walitunukiwa Stashahada ya Sheria na wengine 142 walitunukiwa Astashahada ya Sheria.

Amesema kwamba wahitimu hao na wasomi wengine wa sheria nchini hawana budi kuzingatia kasi ya sasa ya maendeleo ya dunia na umuhimu wa elimu katika ulimwengu wa leo na kongeza kwa kutokana na hali hiyo ni lazima wajiendeleze zaidi katika fani hiyo. “ Ninawaasa popote pale mtakapokuwa someni na kujiendeeleza na jifunzeni mambo mapya kila siku, karne hii ya 21 ni karne ya teknolojia na habari , ni karne inayowategemea wahitimu wanaojiendeleza na kujifunza kila siku, jiendelezeni hadi kufikia viwango vya juu kulingana na kushindana na yeyote yule duniani , kumbukeni kuwa ajifunzae haachi kujua, naomba mtambue kuwa kujifunza ni kwekeza,” alisisitiza Jaji Mkuu

Mhe. Jaji Mkuu pia amewaasa wahitimu hao kuwa watakapopata kazi wahakikishe wanafanya kazi kwa bidii, uaminifu na kwa wakati ili kulinda maslahi ya Taifa na hivyo kuwa mabalozi wazuri wa Chuo. Awali akimkaribisha Jaji Mkuu katika mahafali hayo, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Mhe. John Mrosso amesema ndani ya miaka miwili chuo kimepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kujielekeza katika masuala ya utafiti na ushauri ambapo inao wanataaluma 22 ambao wamejikita katika eneo hilo na kuwezasha wahitimu wa chuo hicho kupata ajira serikalini na kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato ili kujiendesha.

Nae Mkuu wa Chuo hicha Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo alisema katika mwaka huu chuo kimefanikiwa kutoa wanafunzi 26 waliopata daraja la kwanza hali ambayo imetokana na kujitoa kwa wahadhiri na kujituma kawa wanachuo hao na hivyo kukiletea sifa chuo.

Amesema kama chuo wamepanga kuimarisha kitengo cha mafunzo, kuimarisha vyanzo vya mapato, kujenga uwezo wa watumishi ili kuhakikisha kinatekeleza kwa vitendo dhamira ya kuanzishwa kwa chuo ya kuboresha utendaji kazi wa Mahakama kupitia mafunzo kwa Maafisa wa Mahakama pamoja na wasaidizi wao na wadau wote wa sekta ya sheria nchini.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma akizungumza na wahatimu na wageni waalikwa katika mahafali ya 17 ya chuo cha uongozi wa Mahakama Lushoto ambapo wahitimu 292 walitunukiwa Stashahada na Astashahada za Sheria.
Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Jaji Dkt. Paul Kihwelo akizungumza kitu wakati wa mahafali ya 17 ya chuo hicho pembeni yake ni a na mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Juma
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Jaji Mst. wa Mahakama ya Rufaa Mhe. John Mrosso akizngumza wakati wa Mahafali ya 17 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto
Baadhi ya Wahitimu wa Stashahada ya Sheria wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania wakati wa mahafali ya 17 ya chuo hicho baada ya kutunukiwa Stashahada zao
Baadhi ya Wahitimu wa Astashahada ya Sheria wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania wakati wa mahafali ya 17 ya chuo hicho baada ya kutunukiwa Astashahada zao

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA NOVEMBA 17, 2017

SERIKALI YAKARABATI VYUO 10 KWA SH. BILIONI 12 - WAZIRI MKUU

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetumia sh. bilioni 11.9 kufanya ukarabati wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia pamoja na mabweni katika vyuo 10 vya ualimu nchini.

Amevitaja vyuo hivyo kuwa ni Morogoro, Mpwapwa, Butimba, Kasulu, Songea, Tukuyu, Marangu, Kleruu, Korogwe na Tabora. “Ukarabati huu umewezesha wanachuo 5,920 waliokuwa wanasoma Stashahada maalum ya Sayansi, Hisabati na TEHAMA katika Chuo Kikuu cha Dodoma kuhamishiwa katika vyuo hivyo,” ameongeza. 

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Novemba 17, 2017) bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa tisa wa Bunge la 11. Bunge limeahirishwa hadi Januari 30, mwakani.

Amesema ili kuongeza fursa za wanafunzi kusomea ualimu, Serikali imepanga kujenga na kukarabati vyuo vya ualimu vya Kitangali, Ndala, Mpuguso na Shinyanga kwa thamani ya sh. bilioni 36.47.  

Amesema mradi huo ambao utatekelezwa kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2016/2017 - 2018/2019, unalenga kuongeza fursa kwa wanafunzi wenye sifa kupata nafasi ya kujiunga na elimu ya ualimu. 

“Ujenzi na ukarabati huu utasaidia kuongeza udahili katika vyuo vya ualimu vya Serikali kutoka wanachuo 20,535 katika mwaka 2017 hadi kufikia wanachuo 23,835 katika mwaka 2019, ikiwa ni ongezeko la wanachuo 3,300,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali imeanza maandalizi ya awamu ya pili ya ukarabati wa vyuo saba vya ualimu vya Serikali. Amevitaja vyuo hivyo kuwa ni Tandala, Nachingwea, Tarime, Kinampanda, Mandaka, Patandi na Ilonga. 

Amesema vyuo vya ualimu vya Murutunguru, Kabanga na Mhonda vitalazimika kujengwa upya baada ya wahandisi kubaini kuwa vyuo hivyo havifai kukarabatiwa kutokana na uchakavu mkubwa wa majengo yake. 

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema ili kukabiliana na upungufu wa wahadhiri kwenye vyuo vya elimu ya juu, katika mwaka 2017/18, Serikali imepanga kusomesha wahadhiri 100 katika ngazi za shahada za umahiri na uzamivu.

Waziri Mkuu amesema kati ya mwaka 2016/17 na 2017/18, Serikali imeratibu upatikanaji wa wanafunzi wa Kitanzania wanaofadhiliwa kusoma nchi za nje ambapo China wapo wanafunzi 86, Uingereza (17), Misri (4), Korea (3), Urusi (13) na Thailand (2) huku baadhi ya wanufaika wakiwa ni wahadhiri wa vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu ya juu nchini.

Vilevile, kupitia kuimarika kwa mahusiano yetu ya kidiplomasia, Waziri Mkuu amesema, Septemba, mwaka huu, Serikali ilitia saini makubaliano na nchi ya Hungary ambapo itakuwa inatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 30 kwa kipindi cha miaka mitatu kuanza mwaka 2018/2019.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 18,2017


IGP SIRRO APOKEA MSAADA WA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA BILIONI MBILI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akimsikiliza mmoja kati ya madaktali wa hospitali ya Jeshi hilo iliyopo barabara ya Kilwa, wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba vilivyotolewa na serikali ya Marekani, vifaa vyenye thamani ya shilingi za Kitanzania bilioni mbili, kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa wateja wanaofika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.
Mkuu wa kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi (SACP) Paul Kasabago (kushoto), akitoa neno la shukurani wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba vilivyotolewa na serikali ya Marekani, kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa wateja wanaofika katika hospitalini ya Jeshi hilo iliyopo barabara ya kilwa kwa ajili ya matibabu.

Baadhi ya vifaa tiba vilivyotolewa na serikali ya Marekani na kukabidhiwa Jeshi la Polisi kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa wateja wanaofika katika hospitalini ya Jeshi hilo iliyopo barabara ya kilwa kwa ajili ya matibabu.

Picha na Jeshi la Polisi.

KAMPUNI YA BLUE COAST INVESTMENT YACHANGIA MADAWATI 200

$
0
0
Madawati mia mbili ambayo yametolewa na kampuni ya Blue coast Investment iliyopo Mkoani Geita kwa lengo la kusaidia mahitaji ya elimu.
Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akimshukuru mkurugenzi wa kampuni
ya Blue coast Investment ,Bw Athanas Inyasi ambaye yupo katika kwa kujitolea yeye na kampuni yake kutoa madawati kwenye halmashauri ya mji na wa kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola. 
mkurugenzi wa kampuni ya Blue coast Investment ,Bw Athanas Inyasi akimkabidhi mkuu wa Wilaya madawati mia mbili ambayo ameyatoa. 
Mkuu wa Wilaya ya Geita.,Mwl Herman Kapufi akipokea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita,wakati wa zoezi la kukabidhiwa madawati mia mbili.(PICHA NA JOEL MADUKA) .

MABORESHO YA MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI RUVU JUU

INTRODUCING "WANANGU" OFFICIAL AUDIO RELEASE BY NCHAMA THE BEST

Mdau Dr Baraka Noah Kadiva alamba nondozzz ya udaktari nchini malaysia

$
0
0
Kutoka kulia ni Baba Mzazi Mr. Noah Kadiva, mama mzazi Mrs. Florence Kadiva, Muhitimu Dr. Baraka Noah Kadiva, Mheshimiwa Balozi wa Tanzania Nchini Malaysia Dr. Ramadhan Dau, Mrs. Joyce Assenga na Mr. Deo Assenga.
  
Balozi wa Tanzania Nchimbi Malaysia Dr Ramadhani Dau Akiwa na Mdau Dr Baraka Noah Kadiva aliyelamba nondoz ya Udaktari leo Jumamosi katika chuo Kikuu cha MAHSA Kuala Lumpur.

TEKNOLOJIA YA MTANDAONI KUKUZA BIASHARA ZA WAJASIRIAMALI.

$
0
0
WAJASIRIAMALI wa nchi za Afrika ya Mashariki wametakiwa kuitumia ipasavyo fursa ya kuenea na kukua kwa matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ili kuendana na kasi ya mapinduzi ya biashara duniani kote.
Hayo yalisemwa kwenye semina kuhusu “Biashara za Mtandaoni” ikiwa na lengo la ‘kuongeza ufikiaji wa soko na kukuza mbinu za kibiashara kupitia mtandaoni,’ katika mkutano wa pili wa Maonyesho ya Afrika ya Mashariki ya Biashara na Ujasiriamali mwaka 2017 (EABECE) uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 14 mpaka Novemba 16.

Akizungumza kama mmojawapo wa jopo la wazungumzaji wakati wa semina hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Jumia Tanzania, kampuni ambayo inajihusisha na biashara ya manunuzi na uuzaji wa bidhaa mtandaoni, Bw. Albany James amesema kuwa changamoto kubwa wanayopambana nayo kwa sasa ni kuhakikisha kwamba inawashawishi wafanyabiashara wote kuhamia kwenye mfumo wa mtandaoni ili kuwafikia wateja wengi zaidi.
Baadhi y washiriki wa semina kuhusu “Biashara za Mtandaoni” ikiwa na lengo la ‘kuongeza ufikiaji wa soko na kukuza mbinu za kibiashara kupitia mtandaoni.

“Kikubwa tunachokifanya ni kuwakutanisha wauzaji wa bidhaa mbalimbali na wateja mtandaoni. Kupitia uwekezaji mkubwa wa teknolojia tulioufanya, tumedhamiria kuwapatia wauzaji na wanunuaji urahisi mkubwa sawasawa na kama wanavyokwenda madukani,” alisema na kuhitimisha Bw. James, “Tunafahamu kwamba kwenye biashara ili kufikia soko kwa urahisi ni lazima uwajue wateja wako na namna ya kuwafikia ambapo mara nyingi ni kwa njia ya matangazo. Lakini sio wafanyabiashara wote wanaweza kulimudu ukizingatia wengi ndio wanaanza na hawana mitaji au faida kubwa ya kuwekeza kwenye matangazo. Hivyo basi, Jumia tunachokifanya ni kuwapatia fursa ya kujitangaza kwa njia ya mtandao bila ya gharama yoyote kwani ndipo kwenye idadi kubwa ya watu kwa hivi sasa.”  
 Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wa wajasiliamali wa nchi za AfrikaMashariki ambao ulikuwa unahusu wajasiriamali hao kutumia Tehama katika ufanyaji wao wa kazi.

Naye kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Umma na Masoko wa Jumia Travel Tanzania, Bw. Kijanga Geofrey, kampuni dada ya Jumia Tanzania ambayo yenyewe inajihusisha na utoaji wa huduma za hoteli mtandaoni nchini na barani Afrika kwa ujumla, ameongezea kuwa fursa iliyopo kwa wafanyabiashara kuhamia mtandaoni ni kubwa na haina gharama kama wengi wanavyofikiri.
Katikati ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungan wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu akiwa katika mkutan uliowakutanisha wajasiliamali wa Afrika Mashariki. Kulia ni Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

“Wafanyabishara wengi bado ni waoga wa kutumia teknolojia kwenye kukuza na kurahisisha biashara zao. Ripoti zinaonyesha kwamba Tanzania ni mojawapo ya nchi 20 zenye uchumi unaokua kwa kasi duniani ambao kwa kiasi kikubwa unachangiwa na sekta za utalii, ujenzi, fedha na biashara ukiacha na nyinginezo. Lakini kikubwa zaidi ni ukuaji wa TEHAMA ambapo takwimu zinaonyesha 40% ya watanzania wamefikiwa na mtandao wa intaneti ambapo wameongezeka na kufikia milioni 19.86 mwaka 2016 kutoka milioni 17.26 mwaka 2015. Takwimu hiyo pia imechochea kuongezeka kwa watumiaji wa simu za mkononi na kufikia milioni 40.17 mwaka 2016,” alisema Bw, Geofrey.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungan wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu  akizungumza katika semina ya wajasiriamali.
 
“Hilo ni sawa na ongezeko la 0.9% kwa mwaka na ukuaji wa ueneaji kwa 83% kwenye nchi yenye idadi ya watu zaidi ya milioni 50. Hii ni dhahiri kwamba kuna mustakabali mkubwa kwa ukuaji wa biashara za mtandaoni kwenye sekta mbalimbali. Kwa sasa mawasiliano ya simu ni mojawapo ya sekta zinazokua kwa kasi nchini Tanzania na inatoa mchango mkubwa katika kuwaunganisha watanzania kwenye mfumo wa kifedha. Kwa kuongezea, idadi ya watumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya simu nayo imeongozeka na kufikia milioni 18.08 mwaka 2016 kutoka milioni 17.63 mwaka 2015. Hizi zote ni ishara kwamba watanzania wapo tayari kwa biashara za mtandaoni kitaalamu na kisaikolojia,” alihitimisha Meneja huyo wa Uhusiano wa Umma na Masoko wa Jumia Travel Tanzania.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungan wa Tanzania, Samia Hassan Suluhuakizungumza na baadhi ya wajasiliamali wa Afrika mashariki.

Akitoa maoni yake wakati wa semina hiyo mmoja wa washiriki, Bi. Isabella Mwampamba ambaye mbali na kuwa ni mjasiriamali lakini pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Upendo Friends iliyopo jijini Arusha, amesema kuwa wanawake wengi ni waoga wa kutumia teknolojia za mtandaoni zilizopo sasa kitu ambacho kinawaacha nyuma na kuwanyima fursa nyingi.

“Mimi kama mmojapo wa wanawake wajasiriamali nchini Tanzania ningependa kusema kuwa wengi miongoni mwetu ni waoga wa kutumia teknolojia za kisasa. Kwa mfano, wengi tunaogopa hata kutumia simu za kisasa ambazo ni rafiki na mifumo ya mtandaoni! Lakini kwa upande mwingine sio makosa yetu kwani tunakosa mafunzo ya kitaalamu ya namna ya kuzitumia,” alisema Bi. Mwampamba na kuhitimisha, “Hivyo basi ningependa kutoa wito kwa wanawake na wajasiriamali wenzangu kwamba tuanze kuzitumia teknolojia hizi zilizopo sasa kwani zitatufungua zaidi na kuongeza tija kwenye biashara zetu. Lakini pia natoa wito kwa makampuni ambayo yanajihusisha na sekta hii kuwakusanya na kutoa mafunzo ya mara kwa mara juu ya namna biashara za mtandaoni zinazofanya kazi.”
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia  Suluhu akiwa katika Picha ya pamoja.
 
Mkutano wa Maonyesho ya Afrika ya Mashariki ya Biashara na Ujasiriamali mwaka 2017 (EABECE) unalenga kutoa fursa kwa kuzikutanisha sekta za biashara na wenzao kwenye biashara pamoja na serikali na sekta za biashara. Ni jukwaa linalowakutanisha kwa pamoja wafadhili wa kifenda na wavumbuzi kwa lengo la kuimarisha ujasiriamali katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambapo mwaka jana ulifanyika Oktoba 10 mpaka 13 jijini Nairobi, Kenya.   

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMPA MRAJISI SIKU 7 ZA KWANINI MAGUNIA KUTOFIKA KWA WAKATI

$
0
0
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mara baada ya kushiriki mnada wa tano wa Korosho, Jana Novemba 17, 2017. Picha na Mathias Canal
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa akimuonyesha Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa jinsi magunia yalivyopangwa kwa ustadi ktika gala la kuhifadhia Korosho la Mtanda mara baada ya  Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mara baada ya kushiriki mnada wa tano wa Korosho, Jana Novemba 17, 2017.
Badhi ya wakulima wa zao la korosho wa Chama cha Ushirika cha Masasi-Mtwara Cooperative Union Ltd (MAMCU) wakifatilia mnada wa tano wa korosho katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara. Jana Novemba 17, 2017.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Wa Tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wazee maarufu wa kijiji cha Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa (Wa Kwanza Kushoto), na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini Mhe Hawa Ghasia (Wa Kwanza Kulia).
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza ushauri sambamba na pongezi kwa kushiriki Mnada wa tano wa Korosho Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara  wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Humo, Jana Novemba 17, 2017
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa wakikagua magunia ambayo tayari yamewasili katika Ofisi ya Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama Kikuu cha ushirika mara baada ya kumalizika kwa mnada wa tano wa Korosho Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.

Na Mathias Canal, Mtwara
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa leo Novemba 18, 2017 amemuagiza Mrajisi wa vyama vya ushirika kukamilisha haraka kazi ya uchunguzi kwenye Bodi za vyama vya ushirika vya Mkoa wa Mtwara ili kubaini sababu zilizopelekea kuuzwa kwa magunia kiholela.

Alisema kuwa kumalizika kwa uchunguzi huo kutarahisisha kuchukuliwa haraka hatua kali za kisheri kwa wale wote watakaobainika kukiuka sheria No 17 ya vyama vya ushirika.

Naibu waziri alitoa agizo hilo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mara baada ya kugundua kuwa kuna viashiria vya ukiukwaji wa taratibu katika upatikanaji wa magunia ya kuhifadhia korosho wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani humo.

Sambamba na hilo Naibu waziri Mhe Mwanjelwa wakati wote wa mkutano huo ameshuhudia malalamiko kutoka kwa wakulima wa zao la korosho wa Chama cha Ushirika cha Masasi-Mtwara Cooperative Union Ltd (MAMCU) kuhusu ucheleweshwaji wa upatikanaji wa maguni kutoka kwa mzabui, Mapungufu ya kilo kati ya PDA na WHRs ghala kuu, ikiwa ni pamoja na kuchelewa kwa malipo ya wakulima kwa njia ya benki kutoka kwa wanunuzi.

Katika ziara yake hiyo kilio cha wananchi wengi na wakulima walisiitiza zaidi kuhusu kukosekana kwa magunia hayo huku wakieleza kuwa wakati mwingine kuchelea kufika ama kutowafikia kabisa jambo ambalo linachangia kupunguza thamani ya zao la korosho.

“Nataka Mrajisi ufanye na ukamilishe kazi yako ya uchunguzi na baada ya kuipata taarifa hiyo hatua stahiki zitachukuliwa kwa wale wote watakaogundulika kukiuka sheria ya nchi” Amekaririwa Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa

Mbali na agizo hilo Naibu Waziri pamoja na wabunge wa Mkoa wa Mtwara walipata nafasi ya kujionea mnada wa tano wa ununuzi wa korosho unavyoendelea.

Hata hivyo Mnada wa tano ulishuhudiwa Kilogramu 7,524,104 za korosho zikiuzwa kwa thamani ya zaidi ya Bilioni 30.

Wakati huo huo Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa amesema Wizara itayafanyia kazi haraka mapendekezo ya tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa kufanya uchunguzi kuhusu mwenendo mzima wa magunia pamoja na upatikanaji wake.

ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA WATOTO NJITI DUNIANI.

$
0
0
 Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mh,Maudline Cyrus Castico akibeba Watoto Njiti katika Maadhimisho ya mtoto  Njiti Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.
  Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee , Vijana ,Wanawake na Watoto Maudline Castico akizinduwa Kitabu cha huduma muhimu kwa Watoto Wachanga wakati wa Maadhimisho ya watoto Njiti yaliyofanyika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni (kushoto) Naibu Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman na wapili (kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha Ali Abdalla.

Na Kijakazi Abdalla - Maelezo Zanzibar.  17/11/2017.
WAZIRI wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mh. Maudline Cyrus Castico amesema kuwa idadi ya watoto wanaozaliwa kabla ya kufika wakati (watoto njiti) Zanzibar imeongezeka kutoka 206  mwaka 2016 hadi kufikia 335 kwa mwaka 2017.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto njiti Duniani huko ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni, Waziri Castico alisema kuwa idadi hiyo ni ya kutisha hivyo jamii inapaswa kufanya juhudi kupunguza tatizo hilo .

Alisema ongezeko hilo la watoto njiti limekuwa likisababisha vifo vingi vya watoto wachanga hasa ndani ya siku saba za awali baada ya kuzaliwa.

Aliipongeza Wizara ya Afya kwa  kuchukuwa juhudi kubwa za kuboresha huduma za afya kwa mama na watoto ambapo hivi sasa huduma hizo  zinapatikana kila pahala mijini na vijijini.

Alizitaja huduma hizo kuwa ni pamoja na kuongeza wataalamu na vifaa muhimu za kuhudumia mama wajawazito  na wakati wa kujifunguwa pamoja na kusisitiza umuhimu wa kunyonyesha ziwa la mama pekee kwa muda wa miezi sita.

Hata hivyo alisema kuwa katika kuhakikisha huduma hizo zinaboreshwa kwa watoto njiti, Wizara imefanikiwa kutoa mafunzo mbalimbali kwa wafanyakazi wanaoshughulikia watoto hao na kwa wazazi.

Alisema jumla ya wafanyakazi 300 wamepatiwa huduma za watoto njiti Unguja na Pemba ili kuhakikisha watoto hao wanakuwa katika mazingira ya afya bora.

Mapema Naibu Waziri wa Afya Harusi Said  Suleiman amesema kuwa sababu kubwa zinazopelekea kuzaliwa  watoto njiti ni pamoja na  msongo wa mawazo wakati wa ujauzito, kujifungua katika umri mdogo chini ya miaka 20 na umri mkubwa zaidi ya miaka 40.

Aliwataka kinababa kuongeza mapenzi  kwa wake zao wakati wa ujauzito na kuacha kuwatelekeza ili kumpa nafasi kujifungua akiwa salama na mtoto mwenye afya nzuri.

“Kuna baadhi ya kinababa wanapogundua  wake zao  wanaujauzito  huona ndio fursa ya kutafuta mke mwengine na kumuongezea mke mkubwa matatizo zaidi,’’ alisema Naibu Waziri wa Afya.

Alisema kizazi cha mtoto njiti ni kizazi hai ambacho kinazaliwa kabla ya kutimia umri wa kuzaliwa hivyo ni muhimu kwa wazazi wote wawili kushirikiana katika malezi kuhakikisha kinakuwa vizuri.

Nao wazazi wenye watoto  Njiti wamewashukuru wafanyakazi wa Wizara ya Afya kwa huduma wanazozipata wakati wanapofika vituoni jambo ambalo linawapa faraja ya kuendelea kuwalea watoto wao katika misingi mizuri. 

Hata hivyo wamesema wapo baadhi ya watu wanaona kuzaa mtoto akiwana hali kama hiyo  ni mitihani jambo ambalo  linawatia huzuni  sana  hivyo  wameitaka  jamii kuondokana na dhana hiyo.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO   ZANZIBAR

UJENZI WA DARAJA LA JUU (FLYOVER) LA TAZARA JIJINI DAR ES SALAAM WAFIKIA ASILIMIA 63

wadau watakiwa kuwekeza katika vifaa vya kisasa vya kurekodia filamu

$
0
0
Na Genofeva Matemu – WHUSM
WADAU mbalimbali ndani na nje ya nchi wametakiwa kujitokeza na kuwekeza katika vifaa vya kisasa vya kurekodia filamu ili sekta ya filamu nchini Tanzania iweze kuendelea zaidi na kuvuka mipaka kwa kuwa na ubora wa kuweza kushindana na filamu za nchi nyingine.
Rai hiyo imetolewa na Rais Mstaafu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipokua akizindua chaneli mpya ya Jason’s Televisheni itakayokuwa ikionyesha filamu mpya za kitanzania inayopatikanakatika king’amuzi cha Star times chaneli namba 126 jana Jijini Dar es Salaam.
“Wadau wa tasnia ya filamu nchini hasa waandaaji wa filamu mnapaswa kuangalia namna ya kupata wadau watakaosaidia kuwekeza vifaa vya kisasa vya kurekodia na kwa upande wangu nitajaribu kuwakutanisha na wadau wenye uwezo wa kuwekeza ili muangalie namna ya kuzungumza nao na kuwekeza vifaa vitakavyowawezesha kuandaa filamu zenye ubora na kukidhi hadhi ya kushindana kimataifa” amesema Mhe. Kikwete.
Aidha Mhe. Kikwete amesema kuwa kuwepo kwa chaneli ya JTV itakayokua ikirusha filamu mpya za kitanzania ni jambo muhimu sana katika historia ya tasnia ya filamu hapa nchini hivyo uzinduzi wa chaneli ya JTV unafungua ukurasa mpya katika maendeleo ya tasnia ya filamu ambayo imekua ikikua kwa kasi.
Mhe. Kikwete amesema kuwa kufanikiwa kwa chaneli ya JTV  kutapunguza machungu mengi ya watayarishaji wa filamu kwa kutatua changamoto ya kutokuwa na soko la uhakika na kuleta nuru ya matumaini kwa wasanii  kwa kupata malipo yanayostahili kwa vipaji vyao, jasho lao pamoja na gharama wanayoingia katika kutengeneza filamu.
Kwa upande wake Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa uanzishwaji wa chaneli ya JTV ni moja ya mikakati kadhaa ya kuboresha usambazaji wenye tija wa filamu mpya za kitanzania hivyo kuwataka watayarishaji wa filamu kuthamini mandhari za filamu zetu kwani filamu iliyokosa hata dakika moja kuonyesha vivutio vya utalii tulivyonavyo inakosa sifa ya ubora.
Awali Mhe. Mwakyembe amesema kuwa Tanzania itabaki kuwa chimbuko la lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha ya 10 kuzungumzwa na watu wengi duniani kati ya lugha 6000 hivyo ni matarajio ya wizara baada ya muda mfupi mtu akisikia ala za nyimbo za Kiswahili katika filamu zetu kama vile Mdumange, Sindimba nk. ajue anaangalia filamu ya kitanzania.
Naye Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bw.  Benson Mkenda amesema kuwa bodi ya filamu ipo tayari kushirikiana na wadau wote katika tasnia ya filamu wenye nia ya kukuza na kuendeleza tasnia kama ilivyo kwa Jason’s TV ambao lengo lao mahususi limelenga kuendeleza sekta ya filamu hasa katika eneo la usambazaji ili kuweza kuitoa sekta hii mahali ilipo na kuifikisha katika viwango vya kimataifa.
  Rais Mstaafu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chaneli Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha Star Times chaneli namba 126 Ijumaa jijini Dar es Salaam. 
   Rais Mstaafu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akiwataka watendaji wa wa Star Times kusaidia katika kuleta vifaa vya kisasa vya kutengenezea filamu wakati wa uzinduzi wa Chaneli Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha Star Times chaneli namba 126 Ijumaa jijini Dar es Salaam. 
 Rais Mstaafu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na  wadau wa sekta ya filamu baada ya kuzindua  Chaneli ya Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126  Jijini Dar es Salaam. Wanne kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa  na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.
 Rais Mstaafu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na  wadau wa sekta ya filamu baada ya kuzindua  Chaneli ya Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126  Jijini Dar es Salaam. Wanne kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa  na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.
Rais Mstaafu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na  wadau wa sekta ya filamu baada ya kuzindua  Chaneli ya Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126  Jijini Dar es Salaam. Wanne kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa  na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.

TANESCO yafanya Zoezi la Kusafisha na Kuunga Bomba la Gesi-KINYEREZI 1

$
0
0
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linawataarifu Wateja wake kuwa leo Jumamosi Novemba 18 na kesho Jumapili Novemba 19, 2017 kuna usafishaji na kuunga bomba kubwa la Gesi katika Mitambo ya Kinyerezi I, sambamba na zoezi hilo pia yanafanyika maandalizi ya kukiunganisha Kituo cha Kinyerezi II, kuanzia Saa:02.00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni, kama tulivyowatangazia. 
  Kutokana na kazi hiyo kutakuwa na upungufu wa umeme katika Gridi ya Taifa, hivyo baadhi ya Wateja waliounganishwa katika Gridi ya Taifa wa maeneo mbalimbali Nchini watakosa huduma ya umeme.Zoezi hilo linaendelea kwa ufanisi mkubwa na uharaka ili kurejesha huduma ya umeme kwa wakati. 
TAHADHARI 
Kutokana na kazi hii Wananchi mnaombwa msipite karibu na eneo la Mitambo ya Kinyerezi, kutokuwasha moto, kutokufanya shughuli za uchomeleaji vyuma pamoja na shughuli nyingine yoyote yenye viashiria vya moto, ili kujikinga na madhara yanayoweza kutokea iwapo shughuli tajwa zinafanyika maeneo yaliyo karibu na Mitambo. Shirika limesha fanya taratibu zote za ki usalama katika eneo la Mitambo. 

WAGONJWA 33 WAFANYIWA UPASUAJI MOYO WA BILA KUFUNGUA KIFUA (CATHETERIZATION) KWA KUTUMIA MSHIPA WA DAMU WA MKONO KATIKA KAMBI MAALUM YA MATIBABU

$
0
0







Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya  Misaada (IIRO) ya nchini Saudi  Arabia wamefanya upasuajiwa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa wagonjwa 33. 
Kwa mara ya kwanza tangu Taasisi imeanza  kutoa huduma ya matibabu ya upasuaji wa Moyo bila ya kufungua kifua tumefanya  upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono. Upasuaji tuliokuwa tunaufanya kwa wagonjwa wetu ni wa kutumia mishipa ya paja.Upasuaji wa moyo unaofanyika katika kambi hii ambayo imeanza Jumatano tarehe 15/11/2017 hadi Jumamosi tarehe 18/11/2017 ni ya upasuaji wa bila kufungua kifua kwa watu wazima. Upasuaji uliofanyika  ni wa kuzibua mishipa ya moyo iliyoziba. 
Faida ya upasuaji uliofanyika ni  kumwezesha mgonjwa kutoka chumba cha upasuaji akiwa  anatembea na baada ya masaa manne kama hali yake inaendelea vizuri anaweza kuruhusiwa. Tofauti na upasuaji wa kutumia mshipa wa paja ambao tulikuwa tunaufanya, baada ya upasuaji mgonjwa ni lazima akae Hospitali kwa zaidi ya masaa 24 ili kuangalia maendeleo ya afya yake.Kambi hii imeenda  sambamba na utoaji wa elimu na kubadilishana ujuzi wa kazi  kati ya wafanyakazi wa Taasisi hizi mbili ikiwemo aina mpya ya upasuaji uliofanyika kitu ambacho kimewajengea uwezo zaidi wafanyakazi wetu.  
Aidha wageni nao wamepata muda wa kujifunza vitu vingi na kupata uzoefu mpya  wa baadhi ya magonjwa na mambo ya kiteknolojia ambayo katika nchi yao hakuna.Tunaendelea kuwasisitiza wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wana matatizo ya moyo au la na hivyo kupata tiba kwa wakati. Changamoto  kubwa tunayokabiliana  nayo katika matibabu ya wagonjwa wetu ni wagonjwa wengi tunaowapokea mioyo yao kutokuwa katika hali nzuri. 
Kama mnavyofahamu matibabu ya moyo ni ya gharama hivyo basi tunaendelea kuwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa taifa wa bima ya afya ambao utawasaidia kulipa gharama za matibabu pindi watakapougua na kuhitaji kupata matibabu. Kwa namna ya kipekee tunaishukuru sana  Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya  Misaada (IIRO) kwa kutuma wataalam wake wa magonjwa ya moyo kuja hapa nchini kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa wetu. 
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
18/11/2017
Viewing all 110115 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>