Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 200 | 201 | (Page 202) | 203 | 204 | .... | 3283 | newer

  0 0
 • 07/20/13--13:56: URA YAIFUNGA SIMBA 2-1
 •  Mshambuliaji wa Simba, Marcel Boniventure akichuana na beki wa URA ya Uganda, Walulya Derrick  katika mchezo wa kimatifa wa kirafiki uliofanyika le okwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. URA imeshinda 2-1. (Picha na Habari Mseto Blog)
  Mshambuliaji wa Simba, Marcel Boniventure akitafuta mbinu za kumtoka beki wa URA ya Uganda, Walulya Derrick.
  Mshambuliaji wa Simba, Betram Mombeki akishangilia bao pekee aliloifungia timu yake katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya URA ya Uganda. 
   Heka heka katika lango la URA. 

   Beki wa URA, Mugabi Jonathan akitoka nje baada ya kuumia.
  Waamuzi wa mchezo huo.

  0 0


  0 0

  IMG_9312 
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa ( wa nne kulia)akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa mihogo katika soko la Ilala alipofanya ziara rasmi katika masoko ya Buguruni na Ilala kuangalia utofauti wa bei za bidhaa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
  Mstahiki Meya aliwaasa wafanyabiashara kutokupandisha bei ya bidhaa mbalimbali wakati mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuwawezesha Waislamu wa mkoa wa Dar kuwa na mfungo mwema na wao pia kupata Thawabu kwa Mwenyezi Mungu kwani watawezesha hata wale wenye kipato cha chini kumudu bei ya bidhaa zinazotengeneza futari. Mh. Silaa amewatembelea wafanyabiashara katika masoko kuangalia uwiano wa bei katika masoko hayo.
  IMG_9295
  IMG_9315
  IMG_9286
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akiendelea na ziara yake kwenye masoko katika halmashauri yake ya Ilala akiwa ameambatana maafisa wa mbalimbali wa Manispaa ya Ilala.

  0 0

  Hii ni game ya soccer kati ya viongozi wa dini ya Kiislam (Imams) na kikstrotu (Mapadre) iliyofanyoka huko Yorkshire, UK. Viongozi hawa hawakuishia kuvaa majoho yao na kuhubiri  bali waliamua kujumuika na kucheza game kwa ajili ya Charity na waliweza kuc kiashangisha i cha Paundi elfu 5 za kiingereza
  Imagine tungekuwa nao viongozi wetu wa dini  kwenye jogging clubs na wakaonyesha wao wanavyoshirikiana na jamii katika nyanja mbalimbali. Hii ni changamoto sana kwetu.

  Tafadhalini toeni maoni yenu kuhusu hili.
  MDAU UK

  0 0


  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Madagascar kuchezesha mechi kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) itakayochezwa Jumamosi (Julai 27 mwaka huu) Uwanja wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala.

  Waamuzi wataongozwa na Kanoso Abdoul Ohabee wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Andirvoavonjy Pierre Jean Eric. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Jinoro Velomanana Ferdinand huku Andriamiharisoa Hubert Marie Bruno akiwa mwamuzi wa mezani (fourth official).

  Kamishna wa mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya mwisho kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) ni Ismail Kamal kutoka Ethiopia.

  Mechi hiyo namba 38 itachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Taifa Stars ilipoteza mechi ya kwanza iliyochezwa Julai 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa bao 1-0.

  Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza ikijiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali za CHAN mwakani nchini Afrika Kusini.

  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0

  Na. Tamimu Adam- Jeshi la Polisi

  Vikundi vya ulinzi shirikishi kote nchini vimetakiwa kuwa makini na kuzingatia madili katika kutekeleza majukumu yao ya kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao ili kupunguza uhalifu hapa nchini.

  Hayo yalisemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema wakati akijibu swali kuhusu mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa program ya Polisi jamii na Ulinzi shirikishi ambapo alibainisha kuwa mpaka hivi sasa vikundi hivyo vimefikia zaidi ya 4500 nchi nzima

  IGP Mwema alijibu swali hilo wakati alipokutana na waandishi wa habari wa Jeshi la Polisi ofisini kwake Makao makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salam na kuongeza kuwa, kuongezeka vikundi hivyo ni mafanikio makubwa sana kwa Jeshi hilo kwani inaonesha jinsi gani jamii imeelewa na kutekeleza kwa vitendo dhana nzima ya ulinzi shirikishi/ Polisi jamii kwa lengo la kupunguza uhalifu katika makazi yao kwa lengo la kujiletea maendeleo bila bugudha ya uhalifu na wahalifu.

  Alisema kuwa ili taifa na jamii iweze kuendelea kiuchumi ,kiutamaduni na kijamii wananchi wote kwa ujumla hatuna budi kuwekeza katika suala la ulinzi na usalama kama mtaji wetu wa maendeleo. Vikundi hivyo vimekuwa vikisaidia katika suala la ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo wengine wamekuwa wakifanikisha kukamata na kudhibiti uhalifu na wahalifu kwa kutoa taarifa katika vituo vya Polisi na kufanya ukamataji salama.

  Alisema kuwa lengo la Program hiyo ni kupunguza uhalifu na wahalifu kwenye jamii kila mtaa, kijiji, kitongoji hadi ngazi ya familia na kuwa daraja la kuunganisha kila familia katika kutambua viashiria vya uhalifu na uvunjifu wa amani pamoja na stadi za utatuzi wa migogoro ndani ya jamii.

  IGP Mwema aliongeza kuwa, hatua hiyo imesaidia sana katika kuwajengea uelewa wananchi juu ya kutambua na kubaini viashiria vya uhalifu na wahalifu na kuweza kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi za kuwepo kwa viashiria vyovyote vyenye lengo la kuhatarisha amani ama kuharibu amani iliyopo hapa nchini.

  Moja ya kazi kubwa inayofanywa na Jeshi la Polisi nchini ni utekelezaji wa program ya maboresho ambayo inalenga kuwa na Jeshi dogo la kisasa, lenye weledi na linaloshirikisha jamii katika masuala ya ulinzi, Ushirikiano huo wa wananchi lengo lake kubwa ni kudhibiti vitendo vya uhalifu na kutekeleza dira ya taifa ya maendeleo 2025 inayoelekeza kuwepo kwa utawala bora na uwajibikaji.

  Pia alitoa mwito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa uhalifu na uvunjifu wa amani mapema katika vituo vya Polisi ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahalifu kwani hiyo pia ni moja ya mbinu ya kudhibiti wahalifu katika jamii.

  Mbali na mwito huo pia aliwataka watendaji wa Serikali za vijiji, mtaa wakuu wa tarafa na wilaya, viongozi wa dini na kisiasa pamoja na kamati zote za ulinzi na usalama katika ngazi zote kuanzia kitongoji, kijiji, mtaa hadi mkoa kutumia fursa hiyo itakayosaidia kubaini migogoro, matatizo/kero za jamii mapema na kuzipatia ufumbuzi kwa wakati kabla ya madhara kutokea.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya uhamiaji wakati alipowasili kwenye jengo la Idara hiyo mjini Songea kuweka jiwe la msingi akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 20, 2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mabwawa ya kufugia samaki wakati alipotembelea Kituo cha Maendeleo ya Ufugaji Samaki cha Ruhila kilichopo mjini Songea. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 20, 2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama chakula cha samaki wakati alipotembelea Kituo cha Maendeleo ya Ufugaji wa Samaki cha Ruhila kilichopo Songea Mjini akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 20, 2013. Wapili kulia ni mkewe, Mama Tunu Pinda na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Thabit Mwambungu.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarest Ndikilo akishirikiana na Mfanyakazi wa Vodacom Mwanza Jumao Khamis kukabidhi kitoweo cha mbuzi kwa wanafunzi wa moja ya madrasa za jijini humo zilizonufaika na sadaka ya vyakula kutoka Vodacom Foundation kupitia kampeni ya Pamoja na Vodacom ya kufuturisha na kusaidia madarasa na Makundi mengine ya wasiojiweza wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.Hafla hiyo ilihusisha pia futari kwa wanafunzi wa madrasa na jumuiya za kiislamu za jijini Mwanza.Kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Sheikh Salum Fereji.
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarest Ndikilo akiandaa vipande vya keki kuwalisha watoto wa madrasa kama ishara ya kufungua swaumu wakati wa hafla ya kufuturisha wanafunzi wa madrasa na jumuiya ya waislamu wa Mwanza iliyoandaliwa na Vodacom Foundation. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim ambapo kampeni yake ilitoa pia sadaka ya vyakula kwa madrasa 10 za jijini humo ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Pamoja na Vodacom ya kufuturisha na kusaidia madarasa na Makundi mengine ya wasiojiweza wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarest Ndikillo akimlisha kipande cha keki mtoto wa Madrasa kama ishara ya kufungua swaumu wakati wa halfa ya kufuturisha wanafunzi wa madrasa na jumuiya ya waislamu wa Mwanza iliyoandaliwa na Vodacom Foundation. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim ambapo kampuni yake pia ilikabidhi sadaka ya vyakula kwa madrasa 10 za jijini humo kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom.
  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Sheikh Salum Fereji akiongoza zoezi la kupakua futari wakati wa hafla ya kufuturisha wanafunzi wa madrasa na jumuiya ya waislamu wa Mwanza iliyoandaliwa na Vodacom Foundation. Wanaomfuatia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarest Ndikilo, Katibu wa Bwakata Mkoa Sheikh Salum Balla na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Futari hiyo ilijumuisha watu zaidi ya 500.
  Mfanyakazi wa Vodacom Mwanza Juma Khamis akiwahudumia futari wanafunzi wa madrasa mbalimbali za jijini humo wakati wa hafla ya Vodacom ya kufuturisha wanafunzi wa madrasa na jumuiya ya waislamu wa Mwanza kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom yake ya kufuturisha wanafunzi wa madrasa na kusaidia Makundi yenye uhitaji wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani. Mbali na futarti Vodacom Foundation ilitoa pia sadaka ya vyakula kwa madrasa 10 za jijini humo.

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, leo amefanya ziara ya kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kusini Unguja.

  Katika ziara hiyo Maalim Seif amewaombea wagonjwa hao ambao ni watu wazima wapone haraka, pamoja na kuwataka wafiwa kuwa na subra katika kipindi hiki cha misiba inayowakabili.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wagonjwa hao wamemshukuru Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kuandaa ziara hiyo ya kuwafariji, ambayo wamesema inathibitisha kuwepo na upendo na ukaribu baina ya viongozi na wananchi.

  Jumla ya wagonjwa na wafiwa 14 wametembelewa katika maeneo mbali mbali ya Wilaya za Kusini na Kati Unguja, yakiwemo Kizimkazi Mkunguni, Kijini Makunduchi, Jambiani na Ndijani.

  Maalim Seif anatarajiwa kuendelea na ziara hizo za kuwatembelea wagonjwa na wafiwa katika mikoa yote ya Unguja na Pemba ndani ya kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimjulia hali na kumfariji Bi. Mkasi Jihadi wa Kijini Makunduchi wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Mkoa wa Kusini Unguja.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na wananchi wa Makunduchi wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Mkoa wa Kusini Unguja.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali na kumfariji mzee Muombwa Rashid wa Kajengwa Makunduchi, wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Mkoa wa Kusini Unguja.
  Wananchi mbali mbali wakijumuika katika futari iliyoandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake Mbweni Zanzibar. (picha na Salmin Said, OMKR).

  0 0

  Na Israel saria
  WIKI hii ulimwengu wa soka umempoteza mmoja wa wataalam wa soka waliobobea, Mjerumani Bert Trautmann (pichani) aliyefariki dunia Ijumaa ya Julai 19, 2013 jijini Valencia nchiniHispania alikoamua kuweka makao yake baada ya kustaafu shughuli za soka. Amefariki akiwa na umri wa miaka 89 akikaribia miaka 90 kwani alizaliwa jijini Bremen, Ujerumani Oktoba 22, 1923. Msiba huu unatugusa Watanzania kwa sababu mtaalam huyo alikuwepo nchini mwetu mwaka 1975 katika kutimiza mpango maalum wa FIFA wa kutuma wataalam wake kuinua soka kwenye nchi zilizokuwa chini kisoka.Alianzia kutekeleza mpango huo Burma (1972-1974), akawa kwetu (1975), kisha akaendaLiberia (1978-1980) na kumalizia mpango huo Pakistan (1980-1983). Inaelezwa kuwa kutokukaa sana hapa kwetu kulisababishwa na ugunduzi wake kwamba kisoka hatukuwa chini kihiiivyo kabisa kwa hiyo alishauri aende maeneo hasa yaliyokuwa hoi kabisa kisoka. Usishangae kuona Liberia alikaa kwa muda zaidi ya hapa. Walikuwa chini yetu hao na ukweli ni kwamba hata sasa hawatuwezi.
  Bert Trautmann, ambaye jina lake halisi ni Bemhard Carl Trautmann, alikuwa mchezaji maarufu wa Manchester City kati ya mwaka 1949 na 1964 akicheza mechi 508 katika nafasi ya ukipa aliyokuwa akichezea. Cha kusisimu, akiwa hapa kwetu alitengeneza timu ya makipa hodari tupu, Athumani Mambosasa na Omar Mahadhi wote kutoka Simba ambao kwa sasa ni marehemu. Aidha, alimuibua kijana mdogo wa wakati huo, Juma Nassor Pondamali na kumfanya kuwemo kwenye timu ya taifa kukamilisha orodha ya makipa watatu hodari tupu-Mambosasa, Mahadhi na Pondamali. Hii isitafsiriwe kwamba utaalam wake hapa ulikuwa zaidi kwa makipa, hapana, Trautmann, kama mtaalam wa soka, alifundisha mbinu za mpira kwa nafasi zote akitupia macho umuhimu wa vipaji vya vijana na kutoa elimu kwa makocha wetu wa wakati huo hasa Joel Bendera aliyekuwa msaidizi wake na wengine kama kina Mohammed Msomali. Joel bendera kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
  Kwenye kuwaamini vijana, mbali ya Pondamali, aliwainua kina Mohammed Salim wa Coastal Union ya Tanga, Omari Hussein, Aluu Ali na Hussein Ngulungu wa Mseto ya Morogoro na vijana wengine waliochipuka tu mwaka huo 1975 na mwaka mmoja kabla. Ni kocha huyo ndiye aliyeona kuwa Mohammed Kajole wa Simba (marehemu) ndiye aliyestahili kuziba pengo la beki ya kushoto lililoachwa wazi na Mohahammed Chuma wa Nyota ya Mtwara aliyestaafu kuchezea timu ya taifa mwaka huo baada ya kuichezea mfululizo tangu mwaka 1964. Kama tulivyoeleza majuzi, Kajole aliitwa kujiunga na wenzake Zambia kwenye mashindano ya Challenge ya mwaka huo.
  Tuna kila sababu za kumkumbuka kocha wetu Bert Trautmann kwa sababu msingi wa soka aliouweka uliimarishwa vizuri na waliompokea jukumu la kuifundisha timu yetu ya taifa kwani miaka minne baadaye, 1979, tulifanikiwa kukata tiketi ya fainali ya mashindano ya mataifa (huru) ya Afrika nchini Nigeria, tuliyoshiriki mwaka 1980.
  Katika historia ya maendeleo ya soka yetu, Watanzania hatupaswi kumsahau Trautmann kwani alichangia kwa kiasi kikubwa kutuinua kisoka. Mungu amlaze pema peponi mtaalam wetu wa soka Bemhard Carl Trautmann, maarufu kama Bert Trautmann.

  0 0

  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Mathias Chikawe (kulia)akikata utepe kuzindua rasmi kitabu hicho(katikati) Mtunzi wa kitabu cha (Mabadiko ya Katiba na Hatima na Tanzania) Luten Kanali Lindwino Simon Mgumba(kushoto) Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mhe Emmanuel Nchimbi.
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Mthias Chikawe (kulia)akionesha kitabu hicho mara baada ya kukizindua(katikati) Mtunzi wa kitabu cha (Mabadiko ya Katiba na Hatima na Tanzania) Luten Kanali Lindwino Simon Mgumba(kushoto) Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mhe Emmanuel Nchimbi.
  Waandishi wa habari wakisikiza kwa umakini hotuba ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe:Mathias Chikawe. wakati wa uzinduzi wa kitabu kiitwacho (Mabadiliko ya Katiba na Hatima ya Tanzania)kilichoandikwa na Naibu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Tanzania, Luten Kanali Lindwino Simon Mgumba.
  Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.

  0 0

  THE 2012 OLYMPIC CHAMPION IN THE MARATHON SAYS IT ALL..! Stephen Kiprotich is a Ugandan long-distance runner, born in Kapchorwa District. He is the 2012 Olympic champion in the marathon, with a winning time of 2:08:01 in hot, sunny, and humid conditions. 
  MORE ON www.sporah.com

  0 0

  Mfanyabiashara mmoja ameuwawa na majambazi walokuwa wakitumia usafiri wa pikipiki maarufu kama Boda Boda huko Magomeni Mapipa jijini Dar es salaam, karibu na makutano ya mtaa wa Jaribu na Tosheka milango ya saa 4 asubuhi tarehe 19 July, 2013 siku ya ijumaa na kumpora pesa taslim millioni 8 na laki 3. 
  Tukio hilo limetokea nyumbani kwake barazani akiwa ametoka bank kuchukua pesa hizo na kuvamiwa na majambazi hayo. Mfanya biashara huyo mwenye asili ya kiarabu anaitwa Abdul Hakim Salmin na alikuwa maarufu sana katiko maeneo hayo. 
   Marehemu amezikwa katika makaburi ya Kisutu na ameacha mke na watoto watano, sasa tunajiuliza je jeshi la polisi liko wapi? Tunaomba serikali ifuatilie na kupanga mkakati jinsi ya kuwalinda wananchi wake. Jee wana usalama wako wapi kwani kila mara matukio ya kuporwa wafanyabiashara na wengine kupoteza maisha na hizo boda boda. 
  Jeshi la polisi au askari polisi wengi wanaoutumia pikipiki , maarufu kama 'TIGO FASTA', utawakuta kibao maeneo ya jangwani wakifatilia magari (pick up) zinazoleta mizigo inayosafirishwa mikoani kutaka risiti na kama hamna basi huwa wanadai kitu kidogo ili upite. 
  Kwa kweli ukiwaona hao mapolisi wanaotumia pikipiki wanavyolizunguka jangwa ni vituko vikubwa, sisi kama wananchi tunajiuliza je wamepewa hayo mapikipiki kwa kazi hiyo au kulinda raia na mali zao? Wadau wa Magomeni Mapipa.

  0 0

  BAADA YA KUONA SUALA LA KUSAFIRISHA VIFURUSHI KWENDA NAIROBI NA DAR LIMEKUWA GUMU KWA WATANZANIA NA WAKENYA WAISHIO UK, WAZEE WA KAZI WALIAMUA KULITAFUTIA UFUMBUZI AMBAPO MZEE WA KAZI CHRIS LUKOSI ALISAFIRI KWENDA NAIROBI  NA DAR ES SALAAM  MWISHO MWA MWEZI WA SITA KUHAKIKISHA KUWA SHUGHULIA ZA MIZIGO ZINABORESHWA NA KUHAKIKISHA WANASHIRIKIANA NA MAWAKALA AMBAO WAKO KIKAZI ZAIDI.
  KUANZIA SASA MIZIGO YOTE YA SERENGETI ITAKUWA INASAFIRISHWA NA KENYA AIRWAYS ILI ISICHELEWE NJIANI
  PICHANI MZEE WA KAZI ALIPEWA NAFASI YA KUSAFIRI NA  MZIGO KUTOKA LONDON MPAKA DAR ES SALAAM ILI KUJIONEA MWENYEWE JINSI HUDUMA ZA MZIGO ZINAVYOKWENDA MSWANO NA BILA KWIKWI

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijibu maswali toka kwa wanahabari wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation) katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini, Jumamosi usiku. Kutoka kulia ni Rais wa Afrika Kusini Mhe Jacob Zuma, Rais wa Msumbiji ambaye pia ni mwenyekiti wa SADC Mhe Armando Guebuza, Katibu Mtendajji wa SADC Dkt Tomaz Augusto Salomão na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah.
  Ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation) katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini, Jumamosi usiku.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation), Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Rais Armando Guebuza baada ya mkutano wa kamati ya Troika katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini, Jumamosi usiku.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa Jumuiya za Watanzania waishio Afrika ya Kusini leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation).

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal amempongeza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kwa kushirikiana vyema na watendaji wa eneo la Mbagala na maeneo mengine katika kuhakikisha wanatekeleza maagizo aliyo yatoa ya kuweka jiji katika hali ya usafi.

  Aidha Dkt. Bilal aliwataka wale wote ambao wamekuwa na tabia ya kuchajafua mazingira waache mara moja kwani kwa kufanya hivyo wanakuwa wanaendeleza kudidimiza pato la Taifa na kudhorotesha ukuwaji wa uchumi.

   Dkt. Bilal alimeyasema hayo mapema leo asubuhi alipokuwa akikagua kituo kipya cha mabasi katika kata ya Mbagala na kujionea hali ya usafi inayozunguka maeneo husika ya kituo hicho.

  Makanu wa Rais aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick pamoja na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Mh. Joyce Mjema.

  Manispaa ya Temeke tayari imetunga sheria ndogo ya uchafuzi wa mazingira ambayo itaanza kutumika hivi karibuni,sheria hiyo itamuhusu kila mwananchi atakaye chafua mazingira husika ndani ya Manispaa ya Temeke na kupata tozo la papo kwa papo lisilo pungua kiasi cha TSH 50,000 za kitanzania.
  Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke,Bwana Ngimbo wakati alipotembele standi mpya ya mabasi,iliopo Mbagala rangi tatu leo asubuhi.
  Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisalimia na Mkuu wa idara ya Usafi na taka,Bw. Ally Hatibu katika standi mpya ya mabasi mbagala rangi tatu.
  Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisikiliza maelezo kutoka kwa kina dada wajasiliamali katika kituo hicho cha mabasi mbagala rangi tatu.
  kikosi maalumu cha usafi na ulinzi shirikishi katika manispaa ya temeke.

  0 0

  Kikosi kazi cha Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni kinatarajiwa kutingisha jukwaa la Jambo Seeheim usiku wa jumapili 28.Julai 2013 kuanzia saa 2.00 usiku katika ukumbi wa Sport & Kulturhalle uliopo Berg Strasse,mjini Seeheim-Jugenheim,huko Ujerumani. Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya itavaana tena jino kwa jino na washabiki wa muziki katika International African Festival tubingen 2013 siku ya ijumaa ya 9 na 10 .08.2013 mjini Tubingen,South Germany. Wadau kaeni tayari tayari kwa gwaride la FFU wa Ngoma Africa band. msikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com


  0 0


    Mdau Pastor Uwezo Mwakitalima ambaye pia ni mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya Ualimu, akiwa na mai waifu wake Lillian baada ya kumeremeta hivi karibuni katika kanisa la Azania Front jijini Dar es salaam na baadaye kukamilisha mambo kwa mnuso wa nguvu katika ukumbi wa Msimbazi center. Picha na  Michael Angulile


  0 0

  LIGI KUU YA VODACOM 2013/2014 KUANZA AGOSTI 24
  Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2013/2014 inaanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu kwa timu zote 14 kuwa viwanjani katika miji saba tofauti.

  Hata hivyo, kabla ya ligi hiyo kuanza kutakuwa na mechi ya kufungua msimu (Ngao ya Jamii- Community Shield) kati ya bingwa mtetezi Yanga na Makamu bingwa Azam itakayochezwa Agosti 17 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Mechi za VPL za Agosti 14 mwaka huu zitakuwa kati ya Yanga na Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Mtibwa Sugar na Azam (Uwanja wa Manungu, Morogoro), na JKT Oljoro na Coastal Union (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).

  Nyingine ni Mgambo Shooting na JKT Ruvu (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers na Simba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Kagera Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Ruvu Shooting na Tanzania Prisons (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani).

  Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Novemba 3 mwaka huu wakati wa pili utamalizika Aprili 27 mwakani. (Ratiba ya mzunguko wa kwanza na wa pili imeambatanishwa- attached).

  TAIFA STARS KWENDA KAMPALA J5
  Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inaondoka Mwanza keshokutwa (Julai 24 mwaka huu) kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la CHAN itakayochezwa Jumamosi (Julai 27 mwaka huu) Uwanja wa Mandela kuanzia saa 10 kamili jioni.

  Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza chini ya Kocha Kim Poulsen tangu Julai 14 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

  Timu hiyo itaondoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza saa 7.25 mchana kwa ndege ya PrecisionAir, na inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 10.15 jioni.

  Wakati huo huo, Kocha Kim Poulsen kesho (Julai 23 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya kikosi chake. Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye hoteli ya La Kairo jijini Mwanza.

  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

older | 1 | .... | 200 | 201 | (Page 202) | 203 | 204 | .... | 3283 | newer