Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110090 articles
Browse latest View live

WANANCHI WA BOLISA KUPATA SHULE MPYA YA SEKONDARI

$
0
0
Wananchi wa kata ya Bolisa wanatarajia kujengewa shule mpya ya sekondari ya kata ili kuondokana na  tatizo la umbali kwa wanafunzi  wa kata hiyo, amebainisha na Mkurugenzi wa Mji Kondoa Bw. Khalifa Kondo alipokuwa akijibu swali wakati wa mkutano wa wananchi  wa kata ya Bolisa na Mkuu wa Mkoa  alipofanya ziara ya kujitambulisha wilayani humo hivi karibuni.  
"Shule ya Gubali imeshughulikiwa na wananchi wa kata ya Gulisa kabla ya kugawanywa kuwa kata mbili lakini kwasasa kata ipo kata ya Kolo tunaomba kujua mipaka ya kata hizi mbili ili shule ya Gubali ibaki Bolisa".aliuliza bwana Abubakari Mussa.
Akifafanua Bwana Kondo alisema kuwa ni kweli shule hiyo ipo lakini kutokana na mazingira ya shule hiyo wameanza kupata fedha za kujenga mabweni  katika shule ya  Sekondari Gubali  kwa ajili ya wanafunzi  kutoka nchi nzima na si Kolo tu. 
Kondo aliendelea kufafanua kuwa kutokana na mipango hiyo wilaya imejipanga kujenga shule mpya ya Sekondari  kwa ajili ya wananchi wa kata ya Bolisa kwa ajili ya kuwasogezea huduma wananchi kwa ukaribu kwani ndio lengo la serikali ya awamu ya tano.
Aidha aliongeza kuwa  Rais amemwagiza Waziri wa ujenzi  kuiachia wilaya  majengo yaliyokuwa yanatumiwa na kampuni ya ujenzi wa barabara eneo la Kolo ili yatumike kwa ajili ya kuanzisha shule ya sekondari kwa wanafunzi wenye vipaji maalum toka nchi nzima.
Baada ya ufafanuzi huo Mkuu wa Mkoa Dkt. Binilith Mahenge alipongeza mpango huo na kuwataka kuutekeleza kwa ushirikiano ili wananchi wapate huduma inayostahili.
Shule ya Sekondari Gubali ni shule ya Sekondari iliyopo katika kata ya Kolo ikihudumia wananchi wa kata hiyo na kata ya Bolisa ambapo imejengwa juu ya mlima hali inayowapa shida wanafunzi kufika shule.
 Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Nobility Mahenge kushoto akimuonyesha kitu Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mh. Sezaria Makota wakati wa ziara yake wilayani humo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Mwalimu Kibasa akijibu swali kwenye mkutano wa wananchi na mkuu wa Mkoa katika kata ya Bolisa.
 Mkurugenzi wa Mji Kondoa Khalifa Kondo akifafanua jambo kwenye mkutano wa wananchi na Mkuu wa mkoa
 Wanafunzi wa shule ya msingi Bolisa wakicheza ngoma ya Kirangi kwenye mkutano wa wananchi na mkuu wa wilaya


Courtesy visit by Bank of Africa in Zanzibar

$
0
0
The Minister of Trade, Industry and Marketing of the Revolutionary Government of  Zanzibar, Hon. Amb. Amina Salum Ali with the Managing Director and CEO of Bank Of Africa Tanzania Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah. The visit was a courtesy with intentions of supporting various Government initiatives in Zanzibar.

Alpha Abdul ashinda kinyang'anyiro cha Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 Mtwara

$
0
0
Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota toka mkoa Mtwara, Alpha Abdul akionesha umahiri wake wa kufokafoka kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka mshindi wa shindano hilo la kusaka vipaji kama sehemu ya shamrashamra za msimu wa Tigo Fiesta 2017.
Tano bora walioingia kwenye mchujo wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 mkoani Mtwara.
Tatu bora walioingia kwenye mchujo wa Tigo Fiesta Supa Nyota Mtwara.
Majaji wakiongozwa na Nickson George (katikati) wakijadili jambo katika shindano la kusaka vipaji la Tigo Fiesta 2017 Super Nyota lililofanyika mjini Mtwara.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA WABUNGE WANAOTOKA MIKOA INAYOLIMA PAMBA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Kilimo ifanye utafiti wa kina ili kupata aina bora ya mbegu za pamba zitakazowanufaisha wakulima. Amesema ni lazima utafiti huo ufanyike kwa kuzingatia aina ya udongo unaopatikana katika kila mkoa unaolima pamba. Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Novemba 14, 2017) alipozungumza na wabunge wanaotoka katika mikoa inayolima pamba, Bungeni mjini Dodoma.

“Mbegu za pamba ziko nyingi na zina migogoro. Mbegu nyingine zina manyoya, nyingine zina vipara hivyo lazima utafiti wa kina ufanyike ili kupata aina bora.”

Alisema Wizara ya Kilimo itumie taasisi zake vikiwemo vyuo kufanya uchunguzi na kubaini ni aina gani za mbegu zinafaa kutumika kulingana na eneo husika. Alisema utafiti huo ambao utabainisha aina ya mbegu inayofaa kulingana na aina ya udongo katika kila eneo ili kumuwezesha mkulima kupata mazao ya kutosha. Pia aliwataka Maofisa Kilimo katika mikoa inayolima mazao makuu ya biashara waweke kipaumbele katika kuyasimia mazao hayo.

Waziri Mkuu alisema Maofisa hao lazima wahakikishe wanayasimamia vizuri mazao hayo ambayo ni korosho, chai, pamba, kahawa na tumbaku ili yawe na tija. Alisema Serikali imeweka mkakati wa kuimarisha mazao makuu ya biashara ambayo uzalishaji wake umeanza kupungua likiwemo na zao la pamba. Waziri Mkuu alisema Serikali inataka kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa zao la pamba kuanzia hatua za maandalizi ya shamba, pembejeo hadi masoko.

“Tunataka kulifanya zao hilo ambalo lilikuwa likijulikana kama dhahabu nyeupe lifikie kiwango cha juu cha uzalishaji, hivyo kuongeza tija kwa wakulima.”

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa kwenye ukumbi wa Msekwa, bungeni Mjini Dodoma kabla ya kikao kati ya Waziri Mkuu na Wabunge wanaotoka mikoa inayolima pamba Novemba 14, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokutana na wabunge wanaotoka mikoa inayolima pamba kwenye ukumbi wa Msekwa, bungeni mjini Dodoma Novemba 14, 2017. Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa.
Baadhi ya wabunge wanaotoka mikoa inayolima pamba wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Msekwa, bungeni mjini Dodoma Novemba 14, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 14, 2017. Kutoka kushoto ni John Heche wa Tarime Vijijini, Marwa Ryoba wa Serengeti na Esther Matiko wa Tarime Mjini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MUME WA IRENE UWOYA AFARIKI DUNIA

$
0
0
Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii kutoka nchini Rwanda, inaeleza kuwa mume wa zamani wa Muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya, Ndikumana Hamad Katauti amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo, Ndikumana ambaye alikuwa kocha msaidizi wa timu ya soka ya Rayon Sports ambayo inaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi nchini Rwanda, amefikwa na mauti hayo akiwa nyumbani kwake mjini Kigali. 

kwa mujibu wa Uongozi wa timu hiyo umesema kuwa jana Ndikumana ambaye alionekana kuwa bado yuko fiti na haonyeshi dalili zozote za kuumwa alifanya mazoezi na wachezaji wake na baadaye kuagana na kurudi nyumbane kwake, ambapo wamepatwa na mshtuko baada ya kusikia amefariki Dunia. Haijajulikana kifo chake kimesababishwa na nini kwani hakuwa mgonjwa na wala hajapata ajali. 

Mwili wake umepelekwa monchwari ya kiislamu ya dispensari ya Rwampala kwa maombi ya familia yake kwani miili ya waislamu haihifadhiwi katika monchwari za kawaida kwa mujibu wa imani zao. Uwoya na Ndikumana walifunga ndoa mwaka 2009 na kujaaliwa kupata mtoto mmoja aitwaye Krish kisha wakaja kutengana mwaka 2013. 

 Mungu ampe malazi mema peponi - Amin

MASHINDANO YA KUMUENZI MTAKATIFU GASPARI ITIGI

$
0
0
MASHINDANO ya michezo ya maadhimisho ya siku kuu ya kumbukumbu ya kumuenzi Mtakatifu Gaspari Del Buffalo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya michezo vya kanisa, hatimaye yamefikia tamati,ambapo timu ya Wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari na chuo cha uuguzi iliyopo katika Mji mdogo wa Itigi,wilayani Manyoni imatawazwa kuwa mabingwa wa mpira wa miguu wa mashindano hayo mwaka huu.

Katika mashindano hayo yalizishirikisha jumla ya timu nane za wanaume za mpira wa miguu na mpira wa pete huku kukiwa na malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya viongozi na wachezaji wa timu zilizoshiriki katika mashindano hayo.

Mmoja wa viongozi wa timu ya mpira wa pete kwa wanawake,Hayfat Hassani aliwashauri waandaaji wa mashindano hayo kwamba kwa kuwa timu nyingi zilizoshiriki hazikuwa na jezi,hivyo aliwataka kuangalia uwezekano wa kuzipatia jezi timu zitakazoshiriki katka mashindano ya mwaka ujao.

Aidha akizungumzia kuondokana na malalamiko ya upendeleo unaofanywa na waamuzi,Hayfat alishauri pia kwamba katika mashindano kama hayo kwa mwaka ujao ni vyema waamuzzi wa michezo hiyo wakatafutwa kutoka nje ya maeneo ya Halmashauri ya Itigi.

“Kwa sababu kulikuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wachezaji kuhusu kocha wa timu yetu ambaye naye alikuwa akichezesha kwenye mashindano hayo kuwa alikuwa hazitendei haki timu zingine pinzani na timu yake wakati zilipokuwa zikichuana huku yeye akiwa mwamuzzi wa mchezo huo”alifafanua Hayfat. 
Ni baadhi ya washiriki wa mchezo wa kuvuta kamba kwenye mashindano ya maadhimisho ya kumuenzi Mtakatifu Gaspari,Itigi,wilayani Manyoni.(Picha Na Jumbe Ismailly).

KUFUATIA KESI YA MTANDANO,MAHAKAMA YA KISUTU YAMUHUKUMU BOB CHACHA WANGWE MWAKA MMOJA NA NUSU JELA AMA FAINI YA MILIONI 5

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mtoto wa marehemu Chacha Wangwe, Bob Chacha Wangwe kwenda jela mwaka mmoja na nusu au kulipa faini ya shilingi milioni tano baada ya kupatikana na hatia kuchapisha habari za uongo mtandaoni, katika akaunti yake ya Facebook

hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma shahidi ambaye amesema ameridhika na ushahidi ulioletwa mahakamani na mashahidi sita wa upande wa mashtaka na vielelezo vitano, walioweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo.

Bob ambaye ni mwanafunzi wa sheria chuo kikuu na mtoto wa aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime, mkoani Mara na Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara amepatikana na hatia chini ya kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015. 

Akisoma hukumu hiyo, Shaidi amesema, Mei 7, 2016 polisi walipata taarifa ya chapisho la Bob ambapo walianza kumfatilia na kumkamata kisha walichukua simu na kuipeleka maabara ya Polisi ili kuikagua.

"Kimsingi Bob hukupinga kuandika maneno hayo lakini umedai kuwa hukuyachapisha katika jamii bali yalikuwa ni siri kwenye akaunti yako,".amesema Shahidi.

Hakimu Shaidi amesema, wakati wa ushahidi imeelezwa kuwa simu yake ilipokaguliwa ilionekana ilitumika kuchapisha ujumbe huo kwa jamii na watu waliujibu, kuashiria ujumbe uliwafikia.

Hiyo inaonyesha dhahiri alikuwa na nia ya kuchapisha taarifa hiyo, kueleza kile ambacho alikiona sahihi kama ingekuwa ni ujumbe wake binafsi basi polisi wasingeweza kumtafuta, na watu wasingejibu-respond,".

Akijitetea asipewe adhabu kali, Bob aliomba apunguziwe adhabu kwa sababu ni mwanafunzi wa masomo ya sheria, pia ni kijana mdogo na ni mara yake ya kwanza kutenda kosa.Hakimu Shaidi alikubaliana na hoja za Bob, kwa kuwa mahakama inamuona kweli bado ni mdogo na anapaswa kufanya mambo mengi mazuri katika jamii.

Pia amesema kama yeye ni mwanafunzi wa masomo ya sheria anapaswa kufanya mambo mema katika jamii vitu ambavyo wengine watamuiga." Mahakama imezingatia utetezi wako ba ule ushahidi wa upande wa mashtaka na inakuhukumu kulipa faini ya Sh. milioni 5 ama uende jela mwaka mmoja na nusu, dhamana iko wazi," Alisema Shaidi

Bob Wangwe alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 12,2016.

Katika kesi hiyo, mshitakiwa hiyo anadaiwa kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake wa Facebook, kosa alilotenda Machi 15,2016 ambapo kupitia ukurasa wake wa Facebook aliandika ujumbe usemao: “Tanzania ni ambayo….inajaza chuki wananchi … matokeo ya kubaka Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania bara kwa sababu za kijinga.”

REDESO YATOA MAFUNZO K WA WAZAILISHAJI NA WASINDIKAJI WA ZAO LA MKONGE MKOANI SIMIYU

$
0
0

Na Robert Hokororo, Kishapu DC.


Shirika la Msaada na Mandeleo ya Jamii (REDESO) katika Halmashauri ya wilaya ya Kishapu limewapa mafunzo wazalishaji na wasindikaji wa zao la mkonge kutoka Kishapu na Meatu mkoani Simiyu.


Mafunzo hayo yaliyofanyika ukumbi wa Halmashauri Kishapu yanalenga kuwajengea washiriki hao uwezo wa utumiaji rasilimali kwa tija katika kuzalisha na kukidhi mahitaji ya soko la bidhaa wanazozalisha katika maeneo yao.


Mafunzo hayo yalitolewa kwa pamoja na Mshauri wa kujitegemea, Steven Tilubuza kutoka Mwanza na Afisa Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephano Shadrack.Yanatarajiwa kuwapatia washiriki hao kutoka vikundi vya ujasiriamali elimu na ujuzi wa namna ya uanzishaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali kwenye maeneo hayo.

Meneja wa REDESO Kishapu, Charles Buregeya alisema washiriki hao kutoka vikundi vya ujasiriamali watanufaika na mafunzo hayo ambayo yatawajengea uwezo wa kutambua fursa mbalimbali waliko.“Kupitia mafunzo hayo washiriki wataweza kujikwamua kutoka umaskini na kuwa na fursa nzuri za kujipatia kipato kwani wataweza kuibua na kuanzisha miradi ya maendeleo,” alisema Buregeya.

Pia aliongeza kwa kusema kuwa mafunzo hayo yatasaidia washiriki kupata elimu ya kubaini na kutafuta masoko ya bidhaa zao wanazozalisha hivyo kupata wigo mkubwa wa wateja.Utaalamu mwingine washiriki wanaopata kupitia mafunzo hayo ni pamoja na namna ya ufungashaji mzuri wa bidhaa zilizozalishwa pia kuzitangaza kupitia njia mbalimbali ili ziwafikie wateja.
 Mshauri wa kujitegemea, Steven Tilubuza kutoka Mwanza akitoa mada katika mafunzo hayo yaliyofanyika ukumbi wa Halmashauri Kishapu.

 Meneja wa Shirika la Msaada na Mandeleo ya Jamii (REDESO) Kishapu, Charles Buregeya akitoa ufafanuzi kuhusu mafunzo hayo kwa waashiriki.
Afisa Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephano Shadrack akitoa mada kuhusu ushirika katika mafunzo hayo.

MAGAZETI YA JUMATANO LEO NOVEMBA 15,2017

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yatoa zawadi kwa wafanyakazi bora wa mwezi wa tisa na wa kumi

$
0
0
 Daktari Bingwa wa Magojwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akimkabidhi zawadi ya mfanyakazi bora wa mwezi wa tisa  Adilla  Musa ambaye ni mtunza kumbukumbu katika kikao cha asubuhi cha kujadili mabadiliko na maendeleo katika tasnia ya  magonjwa ya moyo kinachofanyika kila jumatano  katika Taasisi hiyo. Kulia ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo Tulizo Shemu na kushoto ni Meneja wa kampuni ya uuzaji wa dawa za binadamu na vifaa tiba ya Samiro,  Masilamani Guru 
 Daktari Bingwa wa Magojwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akimkabidhi zawadi ya Daktari bora wa mwezi wa  kumi Siza Ngomero  katika kikao cha asubuhi cha kujadili mabadiliko na maendeleo katika tasnia ya  magonjwa ya moyo kinachofanyika kila jumatano  katika Taasisi hiyo. Kulia ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo Tulizo Shemu na kushoto ni Meneja wa kampuni ya uuzaji wa dawa za binadamu na vifaa tiba ya Samiro, Masilamani Guru .
 Daktari Bingwa wa Magojwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akimkabidhi zawadi ya Mfanyakazi  bora wa mwezi wa  kumi Flora Kasembe ambaye ni Msimamizi wa Majengo   kwenye kikao cha asubuhi cha kujadili mabadiliko na maendeleo katika tasnia ya  magonjwa ya moyo kinachofanyika kila jumatano  katika Taasisi hiyo. Kulia ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo Tulizo Shemu na kushoto ni Meneja wa kampuni ya uuzaji wa dawa za binadamu na vifaa tiba ya Samiro,  Masilamani Guru .
 Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia utoaji wa zawadi kwa wafanyakazi bora wa mwezi wa tisa na kumi kwenye kikao cha asubuhi cha kujadili mabadiliko na maendeleo katika tasnia ya magonjwa ya moyo kinachofanyika kila jumatano  katika Taasisi hiyo.Picha na JKCI

JUMUIYA YA WATANZANIA NCHINI CANADA WAFANYA IBADA MAALUM YA KUIMBEA TANZANIA AMANI

$
0
0
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Christ Chapel la nchini Canada, Jacob Afolabi akiongoza ibada maalum ya kiswahili ya kuombea Amani kwa Tanzania pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Uchumi na Uwekezaji Makini, iliyofanyika katika kanisa hilo, Novemba 5, 2017 Ottawa nchini Canada . Ibada hiyo pia ilihudhuliwa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Balozi Jack Mugendi Zoka aliyeambatana na Mkewe pamoja na Watanzania wengine waishio nchini humo. Ibada hiyo iliangaliwa na Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Canada.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Good News for All, Charles Gadi alikuwa ni mmoja wa Maaskofu walioongoza Ibada hiyo, iliyofanyika katika kanisa la Christ Chapel lililopo, Ottawa nchini Canada
Balozi wa Tanzania nchini Canada, Balozi Jack Mugendi Zoka aliyeambatana na Mkewe wakishiriki Ibada hiyo.
Balozi wa Tanzania nchini Canada, Balozi Jack Mugendi Zoka akiwa katika picha ya pamoja na Waumini wa Ibada hiyo ambao ni Wanajumuiya ya Watanzania waishio nchini humo, wakiwa wameshika picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Balozi wa Tanzania nchini Canada, Balozi Jack Mugendi Zoka akibadilishana mawazo na Bw. John Kalonga ambaye ni Mmoja wa Watanzania waishio nchini humo, baada ya kumalizika kwa ibada hiyo. Wengine pichani ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Good News for All, Charles Gadi (wa pili kulia), Mke wa Balozi (katikati) pamoja na Afisa wa Ubalozi. 

Rais Dkt Magufuli awasili jijini Dar akitokea kijijini kwake Chato,mkoani Geita

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasili jijni Dar es salaam muda huu akitokea kijjini kwake Chato, mkoa wa Geita, na kupokelewa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine

Maafisa AAKIA wafurahishwa ulinzi JNIA

$
0
0
MAAFISA kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar (AAKIA), wamefurahishwa na namna ulinzi na usalama wa abiria na mali zao unavyofanywa kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), imeelezwa.

Maafisa hao kutoka Idara mbalimbali walitoa kauli hiyo jana katika ziara ya siku moja ya mafunzo JNIA, ambapo walitembelea maeneo mbalimbali na kupata maelezo ya kina kutoka kwa maafisa husika.

Mkuu wa msafara wa maafisa hao, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama cha AAKIA, Bw. Shaaban Kombo alisema JNIA inaulinzi madhubuti kwa abiria na mizigo hukaguliwa kwa kutumia mitambo maalum kabla ya kupanda ndege au kuingia ndani ya jengo kwa kazi mbalimbali, ambapo wameahidi kufuata nyayo hizo ili kuzuia uhalifu unaofanywa na baadhi ya watu wasiowaaminifu.

Bw. Kombo alisema pamoja na kupata mambo mengi ya msingi ya uendeshaji wa viwanja vya ndege, JNIA imekuwa darasa tosha, ambapo pia katika upande wa utoaji wa vitambulisho wamejifunza namna utoaji wa vitambulisho unavyofanyika, ukiwa ni tofauti na AAKIA ambao hutoa vitambulisho vya kudumu mara baada ya taratibu kukakamilika, wakati JNIA hutoa vitambulisho vya muda kwa muombaji ili aweze kuendelea na kazi, wakati akisubiri cha kudumu kikamilike kutengenezwa.

“Tumefaidika na mambo mengi ukiangalia sisi kwetu hii ya vitambulisho ni tofauti kabisa, ila kwetu kwa kipindi chote mteja anasubiri kitambulisho cha kudumu anakuwa hawezi kuendelea na kazi zake eneo la kiwanja hadi atakapopata cha kudumu, lakini hapa anakuwa na cha muda kinachomfanya aendelee na shughuli zake huku cha kudumu kikiwa katika matengenezo,” alisema Bw. Kombo.
 Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Lugano Mwansasu (kulia), akitoa maelezo kwa Maafisa wa Idara mbalimbali kutoka kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar (AAKIA) waliofanya ziara ya mafunzo. Kushoto ni Msaidizi wa Mkuu wa kitengo cha Ulinzi na usalama JNIA, Bw. Hamis Mashaka.
 Maafisa wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar (AAKIA), Bw. Shaaban Kombo (kuanzia wa pili kulia), Bi. Zakhia Mohamed, Bw. Salehe Said na Bi. Fatma Yussuf wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Lugano Mwansasu (kulia) akiwaelekeza jambo wakati wa ziara yao ya mafunzo iliyofanyika jana.
  Msaidizi wa Mkuu wa kitengo cha Ulinzi na usalama wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Hamis Mashaka (kushoto), akitoa maelezo mbalimbali yanayohusiana na ulinzi na usalama kwa maafisa kutoka idara mbalimbali za Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume (AAKIA) cha Zanzibar jana walipofanya ziara ya mafunzo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAVUNDE AFUNGUA KONGAMANO LA VIONGOZI VIJANA BARANI AFRIKA, JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera , Bunge , Kazi, Vijana , ajira na Walemavu, Anthony Mavunde  akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Viongozi Vijana Barani Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, ambao umehudhuriwa na Vijana zaidi ya 100 kutoka Mataifa mbalimbali ,Kongamano hilo lilikuwa likijadili namna ya fursa zilizopo kwa Vijana katika kutumia rasilimali za nchi zao kama Viongozi katika kujiletea maendeleo
 Mratibu wa kongamano hilo kutoka Taasisi ya The Open Society Initiative for Eastern Africa,Adam Anthony akizungumza kabl ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua kongamano hilo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera , Bunge , Kazi, Vijana , ajira na Walemavu, Anthony Mavunde akiwa meza kuu pamoja na Mratibu wa kongamano hilo kutoka Tasisi ya The Open Society Initiative for Eastern Africa,Adam Anthony na Balozi wa Uholanzi nchini Lianne Houben
 Balozi wa Uholanzi nchini Lianne Houben, akitoa neno kwa vijana kama mfadhili wa kongamano hilo lililowaleta Viongozi Vijana zaidi ya 100 kutoka bara la Afrika.

SHIRIKA LA PELUM TANZANIA NA HALMASHAURI YA MUFINDI KUTOA HATI MILIKI ZA KIMILA 795

$
0
0
SHIRIKA la PELUM Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa kupitia linatarajia kutoa hati miliki za kimila 795 kwa wananchi wa Vijiji vya  Ugesa, Isaula, Magunguli na Usokami na Mukungu waliopimiwa ardhi zao kupitia Mpango wa Matumizi bora ya ardhi.

Hayo yamesemwa jana (juzi) Wilayani Mufindi na Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Leonard Jaka  wakati wa zoezi la upitishaji wa mpango wa matumizi bora ya ardhi uliofanywa katika kijiji hicho na Shirika la PELUM Tanzania kupitia mradi wa Ushiriki wa wananchi katika Sekta ya Kilimo (CEGO).

Jaka alisema Wananchi wa kijiji cha Makungu pamoja na vijiji jirani katika Halmashauri hiyo kuchangamkia fursa hiyo ya kupima ardhi zao ili kuweza kuepekana na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikiathiri shughuli za maendeleo ya wananchi Wilayani humo.

Jaka alisema mpango huo ni muhimu kwa kuwa unatoa kipaumbele kwa wajane, wagane, walemavu, wazee na watu wenye kipato cha chini kupata hati miliki ya ardhi na hivyo aliwataka wananchi ambao hawajapimiwa ardhi zao wahakikishe wanajipanga ili waweze kufikiwa na mpango huo.

“Kupimwa kwa ardhi zenu kutasaidia kuepukana na migogoro ya ardhi, kujihakikishia ulinzi wa ardhi,kuwa na umiliki halali wa kisheria wa ardhi, kuongezeka kwa thamani ya ardhi pamoja na kurahisisha upatakanaji wa mikopo kwa kuweka ardhi yako kama dhamana,” alisema Jaka.
 Mmoja wa wajumbe toka Kamati ya Usimamizi wa Mpango wa Matumizi ya Ardhi (VLUMC) ya Kijiji cha Makungu akiwasilisha Mpango pendekezwa wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji hicho wakati wa Mkutano wa pamoja uliojadili na kupitisha Mpango wa Matumizi bora ya ardhi katika Kijiji hicho. Mafunzo hayo yaliyofanyika juzi Kijijini hapo yalifadhiliwa na Shirika la PELUM Tanzania. 
Mwanasheria kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa Mufundi, Method Msokeve akiwasomea wananchi wa Kijiji cha Mukungu Wilayani humo sheria ndogondogo zitakatumika wakati wa mipango mbalimbali ya matumizi ya ardhi Wilayani humo. Mafunzo hayo yaliyofanyika juzi Kijijini hapo yalifadhiliwa na Shirika la PELUM Tanzania. 
 Timu ya wataalamu toka Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, na Wafanyakazi wa Shirika la PELUM Tanzania, pamoja na Viongozi wa Serikali za Vijiji vya Kiyowela, Idete na Makungu alama ya Mipaka inayotenganisha vijijiji hivyo kabla ya kufanyika kwa Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji cha Makungu. Mafunzo hayo yaliyofanyika juzi Kijijini hapo yalifadhiliwa na Shirika la PELUM Tanzania.

Baadhi ya vibao vilivyowekwa katika baadhi ya maeneo ya kijiji cha Mukungu yakionesha mgawanyo wa matumizi ya ardhi katika kila eneo husika. Mafunzo hayo yaliyofanyika juzi Kijijini hapo yalifadhiliwa na Shirika la PELUM Tanzania.


Serikali yalifungia shirika lisilo la kiserikali la TSSF

Rais Dkt Magufuli aagiza jengo la Makao makuu ya tanesco na Wizara ya Maji yawekwe x ili yabomolewa kupisha mradi wa ujenzi

$
0
0
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan walipokuwa wakitembelea na kukagua ujenzi wa barabara ya Flyover ya TAZARA mapema leo,kulia ni Mkuu wa mkoa Dar Mh Paul Makonda.Wakati huo huo  pia Rais Dkt Magufuli ametembelea mradi wa ujenzi wa barabara za juu za Ubungo ‘Ubungo Interchange’, katika ukaguzi wa Ubungo Rais Dkt Magufuli ameagiza jengo la makao makuu ya TANESCO lililopo eneo hilo pamoja na jengo la wizara ya maji ambalo liko mkabala na jengo la TANESCO, yawekwe alama ya ‘X’ ili yabomolewe kupisha ujenzi wa mradi huo.
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akizungumza mapema leo mbele ya baadhi ya Wananchi (hawapo pichani) walikuwepo katika eneno hilo, mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Flyover ya Tazara,kushoto ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda walipokuwa wakiwasili maeneo ya Ubungo na kuanza kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara za juu za Ubungo ‘Ubungo Interchange’, ambapo katika ukaguzi huo Rais Dkt Magufuli ameagiza jengo la makao makuu ya TANESCO lililopo eneo hilo pamoja na jengo la wizara ya maji ambalo liko mkabala na jengo la TANESCO, yawekwe alama ya ‘X’ ili yabomolewe kupisha ujenzi wa mradi huo.
  Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakimsikiliza mmoja wa Wakandarasi wa mradi huo wa ujenzi wa barabara za juu ‘Ubungo Interchange’,mapema leo 
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi mbalimbali waliokuwa wamejitokeza mapema leo,wakati Rais Dkt John Pombe Magufuli (pichani kulia),alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za juu za Ubungo ‘Ubungo Interchange’,mapema leo jijini Dar.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa mradi huo wakishangilia wakati Rais Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza nao 
 Maendeleo ya Ujenzi wa Flyover ya Tazara jijini Dar Es Salaam kama unavyoonekana pichani mapema leo mchama,ambapo Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassani walitembelea na kujionea maendeleo yake,ambapo Mkandarasi wa mradi huo amesema kuwa asilimia 63 ya ujenzi umekamilia na kwamba Flyover hiyo inatarajiwa kufunguliwa Agosti 8,2018 badala ya Desemba 2018.


UPDATES KESI YA MTANDANO MAHAKAMA YA KISUTU;BOB WANGWE ALIPA FAINI YA MILIONI TANO BADALA YA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA NA NUSU

$
0
0

Mtoto wa marehemu Chacha Wangwe, Bob Wangwe, Wa kwanza kulia  na Wakili wake Benedict Ishabakaki, mwenye suti ya bluu, wakitoka katika viunga vya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kufanikiwa kuruka kiunzi cha kwenda jela mwaka mmoja na nusu kwa kulipa faini ya sh. Milioni tano.

Pamoja na kulipa faini hiyo na kuwa huru wangwe amesema anatarajia kukata rufaa hivi karibuni kwani hajaridhika na uamuzi uliotolewa mahakamani hapo kwa sababu nyingi, Mojawapo ikiwa Hakimu hakusema kama ujumbe wake ule alioposti ulikuwa wa uchochezi au la.

Amesema, suala lolote la kutoa maoni siyo suala la mjadala, lipo kikatiba na ni haki ya watu wote ya msingi.

Mapema leo Novemba 15/2017 Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alimuhukumu Wangwe kulipa faini ya Sh.Milioni 5 ama kwenda jela mwaka mmoja na nusu baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuchapisha taarifa ya uongo kwenye mtandao wa Facebook.

Katika kesi hiyo namba 167, Chacha Wange anatuhumiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.


Inadaiwa Machi 15/2016 alichapisha taarifa iliyosema,

) “….Tanzania ni ambayo inajaza chuki wananchi.… matokeo ya kubaka Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya Muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania Bara kwasababu za kijinga.”
 Picha ya juu, Prof. Samwel Mwita Wangwe akishuka ngazi za mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kumaliza kulipa faini ya mtoto wake,Bob Wange aliyepatikana na hatia ya kuchapisha taarifa ya uongo kwenye mtandao kupitia ukurasa wake wa facebook.PICHA/HABARI NA KARAMA KINYUNKO

ZAINA FOUNDATION HELP WOMEN TO ICREASE KNOWLEDGE IN CYBER SECURITY

$
0
0
Recently Zaina Foundation hosted two days training about Digital Security for Women’s in Arusha Tanzania with great support from Internews,Defend Defenders from Kampala Uganda and trainers Mr. Paschal Masalu Founder us Elimika Wikiendi and Badru Juma from YUNA Tanzania. 

The objective of workshop where to empower women’s and girls to be aware and get knowledge about digital security skills 

In that training twenty (20) participants and Zaituni safe sister fellow in East Africa was a facilitator, stay together and learn several topic about digital security skills and practiced all skills acquired by using their devices also participant learn and practiced new tools like Signal Mobile app in their phone. 
Zaituni explained about password manager and how it can helps to secure  password, and reuse one password for many accounts and how to create strong password.
Zaituni facilitated about Mobile Safety:  She explained mobile rules and advantages and disadvantages of using smart phone and dump phone.
Some of Participants during reflection about day one before we started day 2 agenda.

Group photo with some participants with banners of different agenda of our workshop.


TMF YAIPATIA REDIO HABARI NJEMA YA MBULU, FEDHA ZA RUZUKU YA SHILINGI MILIONI 112

$
0
0
Tanzania Media Foundation (TMF) imeipatia ruzuku ya shilingi milioni 112 Radio Habari Njema ya Mbulu Mkoani Manyara, kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi ili waibue kero, changamoto, mafanikio na kuandika kwa wingi habari za wananchi hasa waliopo Vijijini. 

Mkurugenzi wa TMF Ernest Sungura, akizungumza mjini Babati wakati wa zoezi hilo, alisema vyombo vya habari ni mhimili usio rasmi ambao umekuwa ukiibua changamoto mbalimbali za wananchi ikiwemo za maji, elimu, afya na mengineyo ambayo yakipatiwa ufumbuzi jamii inapata furaha. 

Sungura alisema kupitia ruzuku hiyo, hii ni mara ya nne kupatiwa ruzuku na TMF na mara zote wamekuwa wakiomba fedha kwa ajili ya kuandaa vipindi vyenye maslahi ya wananchi. Alisema kupitia vipindi vilivyoandaliwa na redio hiyo haki za watoto na wanawake zimepatikana kwa ufadhili wa TMF. 

Alisema kwa kuandika habari za jamii ikiwemo mafanikio, kero, ukosefu wa maji, vyoo, shule na mambo hayo yakapatiwa ufumbuzi wananchi hupata furaha baada ya mafanikio hayo. Mkuu wa wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga ameipongeza TMF kwa kuiwezesha Redio Habari Njema, ambayo imekuwa inashirikiana na serikali katika kuchochea maendeleo ya jamii kupitia habari wanazozitangaza. 
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Mofuga (kulia) akishuhudia utiwaji sahihi wa kupatiwa shilingi milioni 112 ambazo ni fedha za ruzuku kwa Redio Habari Njema ya Mbulu zilizotolewa na Tanzania Media Foundation (TMF) mjini Babati, (katikati) ni Mkurugenzi wa TMF Ernest Sungura na Mhasibu mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbulu, Padri Anthony Lagwen
 Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF) Ernest Sungura akizungumza mjini Babati wakati wa zoezi la kupatiwa fedha za ruzuku ya shilingi milioni 112 kwa Radio Habari Njema ya Wilayani Mbulu. 
 Mwandishi wa habari mwandamizi wa Mkoa wa Manyara, Joseph Lyimo akizungumza kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa namna ya kuomba fedha za ruzuku Tanzania Media Foundation (TMF) Mjini Babati. 
 Waandishi wa habari wa Mikoa ya Manyara na Arusha, wakiwa kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa namna ya kuomba fedha za ruzuku kupitia Tanzania Media Foundation (TMF) mjini Babati. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110090 articles
Browse latest View live




Latest Images